Dhulma dhidi ya wanafunzi wa kiislamu. - Msamaa.
Headlines News :
Home » » Dhulma dhidi ya wanafunzi wa kiislamu.

Dhulma dhidi ya wanafunzi wa kiislamu.

Written By Unknown on Friday, March 15, 2013 | 1:43 PM

Dhulma dhidi ya wanafunzi wa kiislamu.

Wanapenda kusema kuwa waislamu ni watu wa kulalamika tuu, lakini wanasahau kuwa sisi tunalalamika tukiwa na evidence (ushahidi).


Hizi hapa ni baadhi ya dhulma wanazotendewa wanafunzi wa kiislamu mashuleni;


SHULE YA SEKONDARI KIZUNGUZI WILAYANI KILOSA –MOROGORO
Mwanafunzi wa kidato cha nne, Frank Thobias Cosmas, aliandika waraka ulioukashifu uislamu, Qurani tukufu na Mtume Muhammad Sallalahu alaihi wasallam.Wakati wanafunzi wakristo wakiwa wanaubandika katika mbao za matangazo shuleni hapo na kusambaziana waraka huo Tarehe 13/05/2011 mwanafunzi muislamu Saidi Suleiman aliupata na kuufikisha kwa viongozi wa wanafunzi waislamu na hatimaye malalamiko hayo yalifika kwa mkuu wa shule.

Mkuu wa shule alimpa Adhabu Yule mwanafunzi aliye peleka taarifa na
viongozi wa wanafunzi waislamu walisimamaishwa shule kwa muda wa siku 21, na Yule aliyendika waraka huo alibakishwa kufanya kazi za shule.

Tukio hili liliripotiwa kwa Mkuu wa polisi Morogoro, Afisa Elimu Mkoa Morogoro na ofisi ya mkuu wa wilaya ambao walipuuza. Hatua hiyo ilisababisha waislamu wa Mkoa wa Morogoro kuandamana kwa amani siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2011.

PIA SHULE YA SEKONDARI ULONGONI – DAR ES SALAAM
Siku ya Alhamisi,tarehe 27/01/2011Mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha wanafunzi wa kike wa shule hiyo kuvua Hijabu wakati wa zoezi la kupiga picha kwa ajili ya Mtihani wa kidato cha nne.Alifanya hivyo kwa chuki za udini kwa sababu waraka wa baraza la mitihani unaotoa maelekezo ya namna na utaratibu wa kupiga picha kila mkuu wa shule amepatiwa na haukuagiza hivyo.

SHULE YA SEKONDARI ENGUSERO KIBAYA –KITETO
Mkuu wa shule hiyo kwa kushirikiana na Kaimu katibu Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa barua yake ya Kumb.Na.FA.58/347/01/27 aliwaamrisha wanafunzi wavunje msikiti uliopo hapo shuleni kwa madai ya kwamba katika shule za serikali hairuhusiwi kujengwa nyumba ya ibaada. Lakini sikweli kwa kuwa zipo shule nyingi za serikali zilizo na nyumba za ibada makanisa tena makubwa sana. Mfano Shule ya sekondari Ndanda,Shule ya sekondari Umbwe, Lyamungo Sekondari, Pugu Sekondari Dar es salam na karibu shule zote kubwa za Serikali nchini. Huu ndio udini na mfumo kristo unaolalamikiwa na unaoliyumbisha taifa.

SHULE YA SEKONDARI ALDERSGATE BABATI MANYARA
Mkuu wa shule hiyo aliwanyima wanafunzi waislamu darasa kwa ajili ya kusomea somo la maarifa ya uislamu na kuwaambia kama wanataka kusoma somo la dini wachanganyike na wakristo ambao wamepewa chumba cha kusomea shuleni hapo, Jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za nchi.aidha alipiga marufuku uvaaji wa hijabu shuleni hapo kwa taarifa tuliyo letewa ya 17/03/2011.

SHULE YA SEKONDARI LUGOBA
Mwalimu aliwataka wanafunzi waislamu washerehekee Krismas walipokataa akawaambia tutaweka Taarabu maana waislamu mnapenda sana taarabu.Siku ya 21/01/2011 kwa makusudi Makamu Mkuu wa shule hiyo aliingia na viatu katika eneo la chumba wanachotumia waislamu kuswalia na kuwaamuru watoke katika chumba hicho wakati wa swala.Makamu Mkuu huyo alikwenda tena siku ya tarehe 31/01/2011 kwa hasira na kundi kubwa lililo sheheni wanfunzi wakristo kwa ajili ya kuwafanyia fujo waislamu waliokuwa wakiswali. jambo ambalo lileta tafrani kubwa shuleni hapo cha kusikitisha ni kuwa ukweli ulipotoshwa na hatimaye wanafunzi waislamu walionekana ndio chanzo cha tatizo.

SHULE YA SEKONDARI ILBORU ARUSHA
Mwanafunzi Juma Hassan alifukuzwa shule 13/01/ 2006 ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita. Sababu ya kufukuzwa shule ilidaiwa alimsukuma Mama Mkwizu mwalimu sheleni hapo alipotaka kuingia msikitini.

SHULE YA UFUNDI TANGA JIJINI TANGA
Mwaka 2006 Mkuu wa shule hiyo bwana T. Z. Kinala amekuwa na tabia ya Kutoa salamu ya HALELUYAH mstarini wakati wa PAREDI huku akijua kwamba wanafunzi walio mbele yake ni mchanganyiko wa waislamu,wakristo na watu wa dini nyingine.Lakini si hivyo tu, Tarehe 24/7/2006 mkuu wa shule alileta kikundi cha kwaya cha kanisa wakati PAREDI na kuimba nyimbo za ibada ya kikristo.

Wakati alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa, katika hafla fupi ya kuwakaribisha kidato cha tano mnamo tarehe 28/4/2006 Pia alitamka wazi wazi kuwaambia wanafunzi waislamu kuwa hapa shuleni hakuna kuswali swala tano kwani hii siyo seminari.Mnamo tarehe 18/06/2006 aliwaambia wanafunzi wa kiislamu wanaovaa mavazi yanayotambulisha uislamu wao, kama Kofia, Kanzu na Kilemba lau kama angeliwajua asingewachagua kujiunga na shule yake.Mnamo tarehe 02/08/2006 aliwaita waislamu wanaovaa mavazi ya kiislamu kama kanzu kuwa ni Mashoga

CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Madhila haya na manyanyaso hayawasibu wanafunzi wa kiislam waliopo mashule tu lakini hata wale waliopo vyuo na vyuo vikuu pia hawajasalimika hapa tutatoa mfano wa chuo kimoja tu cha Dodoma (UDOM) ambako wanafunzi wa kiislam chuoni hapo wamekuwa wakidhalilishwa, kwa kutukaniwa dini yao na mtume wao mfano wa haya ni mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo yalibandikwa matangazo yenye ujumbe unaowatukana na kukejeri uislam na waislam kuwa ni watu wasioweza na wasiostahiki kuongoza,jambo ambalo liliwafanya wanafunzi wakiislam chuoni hapo kuripoti katika uongozi wa chuo na vyombo vya usalama bila ya kupewa msada, hatimae waislam waliamua kujitowa katika mchakato huo wa kampeni na uchaguzi wakiwa na nia njema ya kujiepusha na uadui na uhasma baina yao na wanafunzi wa dini zingine, lakini hata hivyo baada ya uchaguzi walitukanwa na kukashifiwa wazi wazi na wakirsto wakishangilia kwa kusema Yesu ameshinda na Mohammad ameshindwa katika kona zote za chuo, bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika za chuo na serikali.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/1/taarifa-ya-jumuiya-ya-wanafunzi-na-vijana-wa-kiislamu-tanzania.html#ixzz1ng58uqv1
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template