Jinsi uwongo wa serikali ulivyogeuka ukweli. - Msamaa.
Headlines News :
Home » » Jinsi uwongo wa serikali ulivyogeuka ukweli.

Jinsi uwongo wa serikali ulivyogeuka ukweli.

Written By Unknown on Saturday, March 16, 2013 | 11:43 AM

Jinsi uwongo wa serikali ulivyogeuka ukweli.
 
Na Paul Craig Roberts
Septemba 30, 2012 - “Mtandao wa Kupashana Habari” Katika safu iliyopita , “Utamaduni wa Kujidanganya,” niliandika kuwa “Wamerikani wanaishi katika mkabala wa uwongo. Uwongo unatawala kila mjadala wa sera, kila uamuzi wa kisiasa.” Safu hii itatumia habari mbili muhimu: makombora ya nuklia ya Iran na Julian Asaange, kudhihirisha jinsi uwongo ulivyogeuka kuwa “ukweli,” Mitandao ya kidola ya nchi za Magharibi inatumia kila uwongo kuinua hofu kuhusu serikali ya Iran. Hapo Septemba 28, katika ukurupukaji wenye kudhihirisha kutojali linachoongea, gazeti hafidhina la Uingereza, toleo la mtandao la Mail Online lilimwita Rais wa Iran kuwa ni “dikteta.” Nafasi ya urais nchini Iran hujazwa kwa kupigiwa kura katika uchaguzi shindanishi, na uwezo wa rais uko chini ya uangalizi wa wakuu wa kidini.

Asaange anaandamwa kwa upande mmoja kwa madai ya ukabaji, halafu ujasusi. Vyombo vya habari vya Magharibi na Bunge la Marekani vinaunda makusanyiko ya waongo zaidi katika historia ya dunia. Moja ya maeneo ya uwongo wanayoyapenda sana ni kuwa Rais wa Iran, Ahmadinejad, anataka kuwaua Wayahudi wote. Angalia mkanda wa dakika sita na sekunde 42 wa video ya mkutano wa Ahmadinejad na viongozi wa kidini wa Kiyahudi. Usikinaishwe na jina la video hiyo. Washington Blog inafanya dhihaka.

Wiki iliyopita habari zilitawaliwa na mpango usiokuwepo lakini upo katika mitanda wa silaha za nuklia za Iran. Waziri Mkuu wa Israel, Netanyahu, kaingilia kwa kishindo kampeni ya uchaguzi Marekani, akitaka Obama afafanue ‘mstari mwekundu’ wa kuishambulia Iran. Netanyahu anaamini kuwa ana nguvu zaidi kwa Obama, Rais wa ‘taifa lenye nguvu zaidi pekee diniani,’ wakati uchaguzi unapokaribia. Israel haiwezi kuishambulia Iran peke yake bila kuhofia kuteketezwa kwa Israel. Lakini Netanyahu anafikia tamati kuwa akiishambulia Iran wiki kabla ya uchaguzi mkuu nchini Marekani, Obama itabidi ajiunge au apoteze kura za Wayahudi kwa kutokuiunga mkono Israel katika majimbo kama Florida, ambalo lina Wayahudi wengi na viti vingi vya kumpigia kura mgombea wa chama kimojawapo. Kama uchaguzi unatoa hali ya nguvu sawa kwa wagombea, Netanyahu, mtu anayetawaliwa na kujigamba na maonyesho, anaweza kufanya kweli katika vitisho vyake na kuishambulia Iran, licha ya kupingwa na wakuu wa zamani wa ujasusi na jeshi, chama cha upinzani, na wengi zaidi kati ya wananchi wa Israel.

Kwa maana nyingine, matokeo ya uchaguzi mkuu katika nchi ‘yenye nguvu zaidi duniani’ itategemea kama rais aliyeko madarakani katika nchi hiyo ‘yenye nguvu zaidi’ ni mnyenyekevu kiasi cha kutosha kwa waziri mkuu kichaa wa Israel. Kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Marekani unaweza kutegemea agenda ya Waziri Mkuu wa nchi ndogo ambayo ipo kwa sababu tu ya msaada wa kifedha, kijeshi na kidiplomasia wa Marekani, hasa kura ya turufu katika
Umoja wa Mataifa, ni sababu ya kuwasumbua Wamarekani ambao wanadhani kuwa wao ni “raia wa nchi isiyokwepeka.” Ni vipi hamkwepeki kama inabidi
mfanye kama atakavyo Waziri Mkuu wa Israel? Vyombo vya habari vya Marekani vinahakikisha kuwa swali hili haliingii katika vichwa vya Wamarekani. Wamarekani wameambiwa kuwa kama Iran haina silaha za nuklia ina mpango wa kutengeneza silaha hizo. Ndicho ambacho wanasiasa wa vyama vote viwili, vyombo vya habari, na wahamasishaji kuunga mkono Israel wanavyowaambia.

Wamarekani wanaambiwa hivi licha ya kuwa Shirika la Ujasusi la CIA na Makisio Rasmi ya Kijasusi yamebakia katika tamati kuwa Iran iliacha kutafuta kutengeneza silaha za nuklia mwaka 2003 na wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki waliofika nchini Iran hawajatoa ushahidi mpya wa kuwepo mpango wa silaha za nuklia na pia hakuna ushahidi wakuelekezwa kwa urani iliyoshindiliwa (nguvu za uvutano, uwezo wa kuchanganyika) kwenda kwenye mpango wa kutengeza silaha za nuklia. Isitoshe, Iran ingeweza kufanya nini na silaha ya nuklia, kuacha tu kwa kuitumia dhidi ya nchi inayoishambulia Iran? Kuitumia kwa kushambulia nchi nyingine kungefikia kuteketezwa kabisa kwa Iran.

Kwanini Wamarekani wanaamini kuwa Iran ina silaha za nuklia au inatengeneza silaha hizo wakati CIA inasema kuwa haifanyi hivyo? Jibu ni kuwa Netanyahu anasema hivyo, na waliochanguliwa katika serikali, Bunge na Ikulu ya Marekani wanaogopa kupingana na Waziri Mkuu wa Israel, kama ilivyo kwa vyombo vya utangazaji na uchapishaji habari nchini humo. Ni taifa ‘lenye nguvu kuliko yote, ’Marekani! Watu wasiokwepeka inabidi wajikunyate katika vumbi mbele ya Netanyahu. Wamarekani hata hawafahamu aibu yao. Iran, tofauti na Israel, ilitia saini mkataba wa kimataifa wa kutokueneza silaha za nuklia. Nguvu za nuklia zinahitaji ushindiliaji mdogo, kiasi cha asilimia 5 au pungufu. Dakika ambako Iran itatangaza mpango wa nguvu za nuklia, serikali ya Israeli na mahawara wake mjini Washington walisema uwongo kuwa Iran inatengeneza bomu.

Kwa kutumia haki zake za kisheria chini ya mikataba (ya kimataifa), Iran imeonekana kuwa ni dola ya kihuni na kihalifu na kuchukuliwa kama tishio kwa dunia.

Silaha ya nuklia, tofauti nahapo, inahitaji ushindiliaji asilimia 95 (yaani, ya uzito au uwezo wake wa awali wa kukamata au kutoa nguvu smakujoto), hivyo kupata asilimia tano kutoka mwanzo na halafu kufikia asilimia 95 ni kazi ngumu na ndefu. Nadhani nilianza kusikia madai ya serikali ya Israel kuwa Iran inatafuta silaha za nuklia kuanzia miaka ya 1990, karne iliyopita.

Wakati Iran ilipotangaza kuwa, kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani, vikwazo ambavyo vinaathiri upatikanaji wa dawa hospitalini, Iran ilikuwa inataka kushindia urani kwa kiwango cha asilimia 20 ili kuweza kujipatia ‘isotopes’ (atom zinazohitaji elektroni za ziada, zinazoyumba) za kitiba, madai ya serikali ya Israel kuwa hii itafikia kutengeneza bomu yalifikia Iran kusema kuwa serikali ya Iran inaridhika kwa Ufaransa au nchi nyingine kuipatia ‘isitope’ za tiba inazohitaji na isingefuatilia ushindiaji zaidi ya mahitaji ya uzalishaji wa umeme. Marekani na Russia pia zilitajwa kama watoaji tarajiwa wa mahitaji hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times la Septemba 29, 2011, “ Rais wa Iran aliliambia (gazeti la) Washington Post, na baadaye, kwa maneno hayo hayo kimsingi, New York Times: “kama ninyi (Marekani na Ulaya) mtatupatia urani gredi 20 (iliyosindiliwa kwa kiwango hicho) tutaacha uzalishaji.”

Kwa amri ya Israel Washington ilikataa pendekezo la Iran. Kutatua tatizo siyo ilichokuwa inataka serikali ya Israel. Tatizo liko katika kuendeleza mzozo huo ili uweze kutumika kutayarisha shambulio dhidi ya Iran. Silaha za nuklia za Iran ni moja ya habari kubwa danganyifu za kusukwa, uwongo wenye nia ya kuficha agenda halisi. Agenda halisi ni nini? Agenda halisi inayojificha nyuma ya wasiwasi kichaa kuhusu silaha za nuklia za Iran, ni mpango wa kihafidhina wa serikali ya Israel kuhusu raslimali maji ya kusini ya Lenanon. Mara mbili serikali ya Israel imepeleka jeshi la Israel kuingia Lebanon Kusini na kutwaa eneo hilo na baadaye kulichukua liwe sehemu yake. Na mara mbili Hizhbollah wameshinda na kulifukuza eneo hilo jeshi linaloaminika sana la Israel.

Wapiganaji elfu kadhaa wa Hizbollah waliweza kulishinda jeshi la Israel, ambalo linapewa silaha na mahitaji mengine kwa dola za walipa kodi wa Marekani wakati watu wa Marekani wanafungiwa nje ya nyumba zao za mikopo na kuachwa hawana ajira huku Washington ikifurahia kuhamishiwa kwa kazi zao ng’ambo, kwa sababu Syria na Iran zinawapa Hizbollah misaada ya kifedha na silaha ambazo zinateketeza vifaru vya Israel.

Syria, kwa uhakika, inajihami na maangamizi yanayoendeshwa na Israel na serikali yake kibaraka ya Marekani. Kuangushwa kwa Syria hakujaenda vizuri, kwa sababu Warusi na Wachina hawakuridhia, kama walivyofanya kipumbavu Libya.

Lakini serikali ya uhafidhina mkali ya Israel imefikia tamati kuwa kwa vile sifa ya Marekani ipo katika kuangushwa kwa serikali ya Assad nchini Syria, hilo litafanyika. Hiyo inaiacha Iran. Serikali ya Israel inafahamu kuwa haiwezi kusema ukweli na kutaka Marekani iingie vitani na Iran ili Israel iweze kuiiba Lenanon ya Kusini. Ila kama hofu kuhusu silaha za nuklia za kubuni inaweza kutanda katika hisia za watu wa Magharibi kuunga mkono shambulio la Israel dhidi ya Iran, Iran inaweza kuondolewa kama mfadhili wa Hizbollah na Israel itaweza kuyaiba maji kutoka Lebanon. Hakuna mjadala wowote kuhusu agenda halisi kokote pale katika vyombo vya utangazaji na magazeti nchini Marekani. Nina mashaka kama kuna mjadala kama huo kokote Ulaya, ambayo ni mkusanyiko wa nchi vibaraka wa Marekani.

Hivi tutakuwa na Vita Kuu ya Tatu ya dunia kwa Krismasi? Inawezekana, kama uchaguzi Marekani utakuwa ni patashika wakati unakaribia. Ikiwa matokeo ya uchaguzi yatakuwa hayatabiriki, Netanyahu anaweza akatupa karata na kumtegemea Obama kufuata watangulizi wake. Iran itashambuliwa, na matokeo yake hayawezi kufahamika. Tugeukie kwa Julian Asaange na Wikileaks. Kama Iran, Assange ameshutumiwa, siyo kwa msingi wa vitu dhahiri, bali kwa msingi wa uwongo. Washington, ambayo inajianika kama msambazaji wa haki za binadamu, imekuwa ikimtaabisha kama si kumtesa Bradley Manning tangu Mei 2010 bila kumfikisha mahakamani katika jaribio la kumfanya Manning aseme kuwa yeye na Assange ni kundi la ujasusi linalofanya kazi dhidi ya Marekani.

Assange amepata sifa duniani kote, kwa sababu Wikileaks ilichapisha habari zilizovujishwa kwenye mtandao huo ambazo vyombo-dola vya habari vinazizuia. Akiwa Sweden, Assange alikumbwa na wanawake wawili wanaotaka sifa ambao walimchukua nyumbani kwao kwenye vitanda vyao. Wanawake hao baadaye walijigamba ushindi wao katika mitandao ya kijamii, ila walipogundua kuwa wanashindana, wakamgeukia ‘mla kuwili’ Assange na kumfungulia mashitaka. Mmoja akadai hakutumia kondomu kama alivyomtaka, na mwingine akadai kuwa alimruhusu ajisikiemara moja akafanya mbili.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template