- Msamaa.
Headlines News :
Home » »

Written By Unknown on Thursday, May 2, 2013 | 7:34 AM

Kanisa mshiriki wa ukandamizaji.

Wakati wa kipindi kijulikanacho kama "Dark Ages" yaani zama za Giza (400-900 A.D.) Kanisa likiwa na nguvu za dola lilishiriki moja kwa moja kuwanyonya na kuwakandamiza watu kwa njia mbalimbali. Ukristo ulifanywa dini rasmi ya utawala wa Kirumi (Roman Empire) baada ya Mfalme Constantine kurithi kiti cha Kaizari mnamo mwaka 305 A.D.
 
Kipindi hiki Ukristo ukiwa ni zao la mchanganyiko wa mafundisho ya Paulo na itikadi za kipagani (za mfalme wa Kirumi), ulikuwa na nguvu kubwa sana. Wakuu wa Makanisa pamoja na taasisi zake walijimilikisha ardhi kama ilivyokuwa chini ya mfumo wa kikabaila (wachache kuhodhi ardhi na kuwatumia wengine kuzalisha au kuwakodisha kwa kulipa mazao, nguvu na fedha wakati wa baadaye).
 
Kipindi hiki na kilichofuatia maneno kama "tithe" yalianza kutumika yakimaanisha sehemu ya kumi (1/10) ya mazao kwa ajili ya Kanisa au watumishi wake kutoka kwa waumini.
Ilivyokuwa hii ni dini ya wanaadamu, Waasisi na Wataalamu wa Kanisa walilazimika kukaa na kuandika nadharia zao ambazo zilichukuliwa kuwa ni sehemu ya mafunzo na sheria ya Kanisa, Mt. Ambrose (340-397), Mt. Augustine (354-430) na Papa Gregory the great (540-604) walishikilia kuwa milki ya utawala wa kiroho na ule wa kupita (wa dunia) vyote vinatoka kwa Mungu.
 
Papa Gelasius I (492-496) alipokuwa akifafanua nadharia ya panga mbili nguvu za kanisa na dola-alisema kuwa nguvu hizi zote ni muhimu kwani dola kuweka njia ya kwendea peponi kwa kuhakikisha usalama na kanuni wakati kanisa lina dhamana ya maendeleo ya kiroho (Kaizari mpe haki yake na Mungu mpe haki yake). Papa Gelasius I alitaka upanga wa kiroho uwe juu ya Papa asiwe na wa kumkalia juu.
 
Nadharia ya haki za kiungu kwa wafalme "divine right of Kings" iliasisiwa ili kuikanusha ile ya mgawanyo wa dola na kanisa. Kwa kuwa kipindi cha zama za kati (middle Ages) kilikuwa na mivutano ya utawala - na mfalme awe mas-uli kwa watu wake au mwenye amri na nguvu za mwisho (absolute monarch).
 
Akina Martin Luther (1483-1586) na John Calvin (1509-1564) ambao wanaitakidiwa kuwa wahuishaji wa kanisa (reformers) na waasisi wa madhehebu ya Kiprotestanti walianzisha nadharia zao za utii wa kibubusa (passive obedience). Leon P. Baradat akifafanua nadharia hii anasema:
"The Reformation and absolutist factions agreed that political power came from God and that those who were chosen to exercise it were higher on the social scale than ordinary people. Consequently people were duty bound to obey the prince, even if he was a tyrant, because he was God’s magistrate on earth*.
Tafsiri:
 
Wahuishaji na wapendao mfalme aliye mas-uli walikubali kuwa nguvu za utawala (dola) zimetoka kwa Mungu na wale waliochaguliwa kutawala ni wabora katika daraja ya kijamii kuliko watu wa kawaida. Hivyo watu wanawajibika kumtii mtawala hata akiwa muovu (jeuri) kwani yeye ni hakimu wa Mungu duniani.
 
Nadharia hizi zilitumika kuwanyonyea watu kwa jina la dini. nchini Uingereza na Ufaransa hasa wakati wa utawala wa akina Stuart (Uingereza) na Louis XIV (Ufaransa). Hali hii ilikuwako Spain, Ureno, Italia na sehemu nyinginezo ambazo Kanisa lilishamiri. Ni kutokana na hali hiyo iliyoshamiri kwa karne nyingi na mauaji ya maelfu ya watu ndipo akina Karl Marx na waliowatangulia wakaandika kuwa dini ni KASUMBA na inapingana na sayansi.
 
"All religions however are nothing but fantastic reflection in men’s minds of those external forces which control their daily life, a reflection in which terrestrial forces assume the form of supernatural forces."
Tafsiri:
Kwa ujumla dini zote si chochote ila ni matokeo ya fikra ya mwanaadamu juu ya nguvu za maumbile zinazomiliki maisha yake ya kila siku, mtazamo ambao huzipa nguvu za kawaida umbile la nguvu za kiungu".
 
Aidha ni hali hiyo hiyo iliyochangia mapinduzi ya Ufaransa ya 1789 na kusababisha mali nyingi ya kanisa kutaifishwa na kuibuka nadharia za Secularism (kutenganishwa dini na dunia).
Kwa mfano korti ya Papa (Inquisition) kwa kipindi cha miaka 1481 iliwaadhibu watu 340,000 ambao kati yao 32,000 walichomwa wakiwa hai akiwemo mwanasayansi Bruno.
Hali ya baadhi ya watu kuchukia dini ni matunda ya ukandamizaji na mauaji yaliyofanywa na kanisa kwa karne nyingi. Ni hali iliyopelekea baadhi ya Wanafalsafa wa kikomunisti kuandika kwa mlinganisho wa kamajeruhi pasi na uitafiti kwamba:
like other religions, Islam for the Marxists is opium of people, a reactionary and antiscientific Ideology....... It indicates the spirit of resignation and humility and distracts him from revolutionary action".
 
Masalia ya unyonyaji na ukandamizaji kwa kisingizio cha dini yangali yanaonekana hadi leo.
Tofauti na Tanzania ambapo serikali hudai haina dini, nchi nyingi za Ulaya bado hadi leo zina dini za serikali (state or official religion). Spain, Italia, n.k., zinaitambua dini ya Kikatoliki kama "State religion", wakati Uingereza inaitambua dini inayosimamiwa na kanisa la Uingereza (Church of England) kuwa ni kanisa rasmi la serikali. Nchini Uingereza hadi leo Mfalme (Malkia) ndiye mkuu wa kanisa la Uingereza ambaye humchagua Askofu-Mkuu wa kanisa hilo kama ni mwakilishi wake.
Hali kadhalika baadhi ya sheria za kanisa hilo hupitishwa na bunge la nchi hiyo na baadhi ya viongozi wa kanisa huwa wana nafasi maalumu katika sehemu moja ya bunge lao (House of Lords).
 
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template