Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) jana iliwasilisha bajeti yake ya Sh708.8 bilioni kwa mwaka 2014/2015 ambazo ni pungufu mara 28 ya Bajeti ya Jamhuri ya Muungano ya Sh19.7 trilioni inayotarajiwa kuwasilishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) jana iliwasilisha bajeti yake ya Sh708.8 bilioni kwa mwaka 2014/2015 ambazo ni pungufu mara 28 ya Bajeti ya Jamhuri ya Muungano ya Sh19.7 trilioni inayotarajiwa kuwasilishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu.
Sambamba na bajeti hiyo, SMZ imetangaza mikakati
ya kukusanya fedha hizo kwa kupandisha kodi za leseni za udereva na ada
ya usafiri wa anga kwa wasafiri wa ndani.
Waziri wa Fedha wa SMZ, Omar Yussuf Mzee
alitangaza mpango huo jana alipowasilisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Serikali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi
kinachoendelea Chukwani, Unguja.
Waziri Mzee alisema ili kuimarisha uwezo wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na kutoa huduma bora, wasafiri wa
ndani watalazimika kulipa Sh3,000 badala ya 1,000 na mabadiliko hayo
hayatawahusu wasafiri wa nje ya nchi ili kutoathiri sekta ya utalii
visiwani.
Pia ada za leseni ya udereva kwa miaka miwili italipwa kwa Sh35,000, miaka mitatu Sh45,000 na kwa miaka mitano kwa Sh60,000.
Alisema SMZ imeamua kufuta utaratibu wa kila mwaka
kwa madereva kulipia leseni ili kuwaondolea usumbufu na sasa kuweka
utaratibu wa kukata leseni za muda mrefu na utekelezaji wake utaanza
mwaka huu wa fedha.
EFD zaingia Zanzibar
Pia Waziri Omar alisema ili kudhibiti ukwepaji
kodi, SMZ inatarajia kuanzisha utaratibu wa stakabadhi kutolewa kwa
mashine maalumu za (EFD) na wafanyabiashara wote watalazimika kuwa na
mashine hizo kwenye maduka yao ambazo zitasaidia biashara kufanyika
kisasa na kudhibiti mapato ya Serikali.
Hata hivyo, alisema bajeti ya mwaka huu ina nakisi
ya Sh36 bilioni na kwamba Serikali itaziba pengo hilo kupitia mapato
yatakayokusanywa kutokana na Kodi ya Wafanyakazi (Paye) wa Muungano
walioko Zanzibar na Sh21 bilioni zitakusanywa kutoka vyanzo hivyo na
Sh15 bilioni zitatokana na mikopo ili kuleta uwiano wa bajeti, mapato na
matumizi yake.
Pia alisema Pato la Taifa limekua kutoka Sh1,342.6
bilioni mwaka 2012 hadi kufikia Sh1, 442.8 bilioni wakati pato la mtu
binafsi limekua kwa asilimia 4.6 kutoka Dola za Marekani 656 hadi Dola
667 mwaka 2013.
Kuhusu deni la Taifa, Waziri Mzee aliwaeleza
wajumbe wa Baraza hilo kwamba limeongezeka na kufikia Sh294.90 bilioni
sawa na ongezeko la asilimia 17.0 ikilinganishwa na deni la Sh252.3
bilioni lilikuwapo hadi Machi mwaka jana.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !