CHADEMA NA MBIO ZA URAISI KUPITIA KANISA. - Kitoloho
Headlines News :
Home » » CHADEMA NA MBIO ZA URAISI KUPITIA KANISA.

CHADEMA NA MBIO ZA URAISI KUPITIA KANISA.

Written By Msamaa on Friday, March 29, 2013 | 12:27 PM

"Someni na hii mjue kwamba Chadema ni Chama kinachofukuzia uraisi nyuma ya pazia la Kanisa"
 
Wa Denmark wamsaidia Slaa kuing’oa CCM
RaiaMwema. Hafidh Kido
Toleo la 287
27 Mar 2013
Dr. Slaa na Rolf Aagaard-Svendsen wakitia saini mkataba
  • Yamwaga milioni 400 kunoa vijana kisiasa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kupata bahati ya kusaidiwa mamilioni ya fedha na safari hii mbali na msaada uliokuwa ukitolewa na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jaffer Sabodo, chama hicho kimepewa Sh milioni 400 kutoka chama rafiki cha Conservative cha Denmark.
Malengo ya msaada huo yanatajwa kuwa ni pamoja na kusaidia kuwanoa kisiasa vijana na wanawake wa chama hicho, kupitia mabaraza yao, Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) na Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA).
Hata hivyo, ingawa haijawekwa bayana ni dhahiri kwamba matokeo ya msaada huo ni pamoja na ama kupunguza makali ya CCM kuendelea kubaki madarakani au kuking’oa kabisa chama hicho, ambacho hakijawahi kuonja ladha ya siasa za kambi ya upinzani tangu kuundwa kwake, mwaka 1977.

Akizungumza kwenye hafla ya kutiliana saini makabidhiano hayo ya msaada Makao Makuu ya CHADEMA jijini Dar es Salaam Jumanne, wiki hii, Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willbrod Slaa alisema msaada huo unalenga kusaidia vijana 9,000 kutoka BAVICHA na wanawake 9,000 kutoka BAWACHA.

“Tunao mpango wa kuwajengea uwezo kisiasa wanawake na vijana katika chama chetu, hivyo tumelenga pesa hizi tutazielekeza kwenye mpango huo ambao utaanza hivi karibuni kuanzia ngazi ya taifa mpaka jimbo, na awamu ya pili itaanza mwakani.
“Miaka ya nyuma tuliwahi kuomba msaada kutoka Umoja wa Vyama vya Demokrasia duniani (IDU), lakini wakati huo Conservative cha Denmark hakikuwa katika umoja huo, ila baadaye serikali yao ikaona haja ya kuruhusu chama hicho kujiunga na IDU, ndipo wakaaanza kutafuta vyama rafiki kutoka Afrika, wakachagua CHADEMA na leo kama unavyoona matunda ya urafiki wetu ni huu msaada wa pesa za Kidenish Krone milioni 1.3, ambazo ni sawa na milioni 400 za Tanzania,” alisema Slaa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Chama cha Conservative – Denmark, Rolf Aagaard-Svendsen, ambaye ndiye aliyetia saini mikataba hiyo alisema chama chake kilikuwa kikitafuta chama muafaka cha kidemokrasia barani Afrika, lakini kutokana na uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Denmark, wameona Tanzania wanaweza kuwa marafiki bora.
“Kabla ya kukubali urafiki huu tulifanya uchunguzi wa muda mrefu kuhusu CHADEMA, wapo vizuri sana katika masuala ya kukuza uwezo wa vijana na wanawake kisiasa, hata nchini kwetu wanawake na vijana wanapewa kipaumbele sana katika masuala ya siasa.

“Nina imani kutokana na urafiki huu Chama cha Conservative kinaweza kufanya kitu kuboresha mfumo wa vyama vingi Tanzania, huu ni mwanzo tu nina hakika mustakabali wa uhusiano huu utaleta mambo mengi kwa CHADEMA na Tanzania kwa ujumla,” alisema Rolf.
Aidha, Mwenyekiti wa BAVICHA ambaye pia ndiye aliyewakilisha BAWACHA, John Heche alisema “Msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa vijana kujitambua, hasa vijijini, maana vijana na wanawake wengi Tanzania hawajui haki zao wala hawajui Katiba ya nchi inawalinda vipi. Hivyo kupitia mafunzo haya naamini wanawake na vijana wa CHADEMA watakuwa mabalozi wazuri kwa vijana wengine Tanzania.”
CHADEMA imewahi kupewa misaada mbalimbali na fedha na kada wa CCM, Sabodo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo hasa katika majimbo yanayoongozwa na chama hicho.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template