- Msamaa.
Headlines News :
Home » »

Written By Unknown on Saturday, March 16, 2013 | 10:07 PM


JINSI YA KUMFURAHISHA MKEO

Namna ya kumfurahisha Mkeo (How to make your wife happy) na Sheikh

Muhammad Abdul Haliym Haamid.

 

1.  Mapokezi Mazuri. Baada ya kurudi kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale alipowatenganisheni:

     ·        Anza kwa maamkizi mazuri

     ·        Anza kwa Assalaamu 'Alaykum na tabasamu.

     Salaam ni Sunnah na ni duaa kwake (mkeo) pia.

     ·        Mpe mkono na ziache habari mbaya mpaka baadae

 

 2.  Maneno mazuri na makaribisho ya kufurahisha

     ·        Chagua maneno mema na jiepushe na maneno mabaya.

     ·        Shughulika nae unaposema au anaposema yeye

     ·        Sema kwa ufasaha na rejea maneno inapohitajika mpaka afahamu/aelewe.

     ·        Mwite kwa majina mazuri anayoyapenda, mfano, Mpenzi wangu, honey (asali,

              tamtam),  (habibty), swaaliha (mwanamke mwema), n.k

 

3.  Urafiki na maliwazo

     ·        Tumia muda kuzungumza nae

     ·        Mfikishie habari njema

     ·        Kumbuka kumbukumbu  zenu  nzuri za kuwa pamoja

 

 4.  Michezo na burudani

     ·        Mfanyie mzaha na jiweke katika hali ya furaha

     ·        Chezeni na mshindane katika michezo na mambo mengine

     ·        Mchukue kuangalia aina za burudani zilizo halali.

     ·        Jiepushe na mambo ya haram katika kuchagua aina ya burudani.

 

5.  Msaada katika kazi za nyumbani

     ·        Fanya kile ambayo wewe mwenyewe unaweza/unapenda kukifanya ili kumsaidia, hasa

 anapokuwa mgonjwa au amechoka.

     ·        La muhimu kuliko yote ni kumuonyesha wazi kuwa unathamini unashukuru    jitihada

 zake katika kazi.

 

6.  Kushauriana (Shuura)

     ·        Hususan katika masuala ya familia

     ·        Kumpa hisia kuwa maoni yake ni muhimu kwako.

     ·        Kuyazingatia maoni yake kwa makini

     ·        Kuwa tayari kubadilisha maoni yako kwa yake yeye iwapo yatakuwa ni bora zaidi.

     ·        Mpe shukurani kwa msaada wake wa maoni.

 

7. Kutembelea wengine

     ·        Chagua watu wenye malezi mema wa kufanya mahusiano nao. Kuna

malipo makubwa katika kuwatembelea jamaa na watu wacha Mungu. (Sio

kuwatembelea kwa kupoteza wakati)

     ·        Kuwa muangalifu kuhakikisha tabia za Kiislamu wakati

mnapowatembelea watu.

     ·        Usimlazimishe kuwatembelea wale ambao yeye hajisikii raha

kuwa nao.

 

8. Muongozo wakati wa kusafiri

     ·        Muage vizuri na kumpa ushauri mwema

     ·        Mtake akuombee dua

     ·        Watake jamaa wacha Mungu na marafiki kuiangalia familia

 wakati wa kutokuwepo kwako.

     ·        Mpe pesa za kutosha kwa mahitaji anayoweza kuhitajia

     ·        Jaribu kuwa na mawasiliano nae ama kwa simu, e-mail (barua

 pepe), barua, n.k.

     ·        Rejea haraka iwezekanavyo.

     ·        Mchukulie zawadi

     ·        Jiepushe na kurejea nyakati zisizotarajiwa au nyakati za

 usiku.

     ·        Mchukue (safarini) ikiwezekana.

 

9.  Msaada wa Kifedha

     ·        Unatakiwa kuwa mtumizi kwa mujibu wa uwezo wake wa kifedha.

 Usiwe bahili na pesa zake (wala usiwe mfujaji).

     ·        Unapata malipo kwa matumizi yote unayotumia kwa ajili ya

 kumkimu (mkeo) hata kwa kipande kidogo cha mkate ambacho unamlisha kwa mkono   wako (hadiyth).

     ·        Unahimizwa sana kumpa kabla yeye hajakuomba.

 

10. Kunukia vizuri na Kujipamba mwili

     ·        Kufuata Sunnah ya kunyoa nywele za  utupuni na kwapani.

     ·        Daima uwe msafi na nadhifu.

     ·        Jitie manukato kwa ajili yake (mkeo)

 

11. Jimai (Tendo la ndoa)

     ·        Unawajibika kulifanya mara kwa mara iwapo huna dharura (ugonjwa, n.k)

     ·        Uanze kwa "Bismillah" na dua zilizo sahihi.

     ·        Umuingilie katika sehemu iliyo sahihi tu (sio sehemu ya nyuma)

     ·        Uanze kwa vitangulizi (vya jimai) ikiwa ni pamoja na maneno ya mapenzi.

     ·        Uendelee mpaka umtosheleze hamu yake.

     ·        Mpumzike na mfanyiane mzaha mnapomaliza

     ·        Epukana na jimai wakati wa damu ya mwezi kwa sababu kufanya hivyo ni haram

     ·        Fanya chochote unachoweza kuepuka kuharibu kiwango chake cha haya alicho

 nacho (haya na staha) mfano kuvua nguo pamoja badili ya kumtaka avue yeye mwanzo   huku ukiwa unamuangalia.

·      Epuka wakati wa jimai mkao ambao unaweza kumuumiza mfano kumgandamiza katika  kifua inayopelekea kumzuilia pumzi, hususan iwapo wewe ni mzito.

·      Chagua muda muwafaka kwa jimai na uwe unamjali kwani wakati mwengine anaweza kuwa ni mgonjwa au amechoka.

 

12. Kudhibiti Siri

·      Jiepushe na kutoa habari za siri mfano wa siri za chumbani, matatizo yake binafsi na masuala mengine ya kibinafsi.

 

13. Kumuongoza katika Kumtii Allaah

     ·        Muamshe katika sehemu ya tatu ya mwisho ya usiku kusali "Qiyaam-ul-Layl" (sala

              za ziada za usiku zenye sujuud na ruku'u za muda mrefu).

     ·        Mfundishe kile unachokijua katika Qur'an na tafsiri zake.

     ·        Mfundishe "Dhikr" (njia za kumtaja Allaah kama alivyofundisha Mtume) za

              asubuhi na jioni.

     ·        Muhimize kutumia pesa kwa ajili ya Allah (S.W.T.) kama vile kutoa sadaka.

     ·        Mchukue katika safari ya Hijja na Umrah wakati unapokuwa na uwezo.

 

 

 

     14. Kuonyesha Heshima kwa familia yake na marafiki zake

 

     ·        Mchukue katika matembezi kwa familia na jamaa,hususan wazazi wake

     ·        Waalike kumtembelea na wakaribishe.

     ·        Wapatie zawadi kunapokuwa na jambo maalum (kama sikukuu).

     ·       Wasaidie wanapokuwa na haja kwa msaada wa fedha, nguvu, n.k.

    ·       Endeleza uhusiano mzuri na familia yake baada ya kifo chake iwapo atakufa mwanzo. Pia kwa hali kama hii mume anahimizwa kufuata Sunnah na kutoa kile ambacho yeye (mke) alizoea kutoa wakati wa uhai wake kuwapa rafiki ya jamaa zake.

 

15. Mafunzo ya Kiislam na Kumshauri kwa kumrekebisha

     ·        Misingi ya Uislam

     ·        Haki na wajibu wake

     ·        Kusoma na kuandika

     ·        Kumhimiza kuhudhuria darsa na halaqah (darsa duara za msikitini na majumbani)

     ·        Hukumu za Kiislam zinazowahusu wanawake

     ·        Kumnunulia vitabu vya Kiislam na kaseti kwa ajili ya maktaba ya nyumbani.

 

16. Wivu unaokubalika

     ·        Hakikisha kuwa anavaa hijaab kamili anapotoka nyumbani.

     ·        Usimruhusu kuchanganyika ovyo na wanaume wasio- mahram

     ·        Jiepushe na wivu uliozidi mno. Mfano wake ni kama:

1. Kulichambua kila neno na sentensi asemayo na kuyajaza maneno yake kwa maana ambazo hakuzikusudia.

             2. Kumzuia kutoka nje ya nyumba hata kama kuna sababu zinazokubalika.

             3. Kumzuilia kujibu simu, n.k.

 

17. Subira na Upole

·      Matatizo yanatarajiwa katika kila ndoa kwa hivyo hili ni jambo la kawaida, Lililo kosa ni majibizano ya kupindukia na kuyakuza matatizo mpaka yakapelekea kuvunjika kwa ndoa.

·      Hasira lazima zionyeshwe pale anapochupa mipaka ya Allaah (S.W.T.), kwa kuchelewesha Sala, kusengenya, kuangalia yasiyofaa katika TV, n.k.

     ·        Kumsamehe makosa anayokukosea wewe (Angalia sehemu ya 18).

     ·        Ni namna gani unaweza kumrekebisha makosa yake?

              1-   Kwanza, mpe ushauri kwa njia ya mzunguko na ya moja kwa moja mara kwa mara.

 2-   Kisha kwa kumpa mgongo katika kitanda (kumuonyesha hisia zako).Tanabahi kuwa hii haihusishi kuhamia chumba kingine, kuhamia nyumba nyingine, au kutomsemesha.

 3-   Utatuzi  wa mwisho ni kumpiga kidogo (kwa namna ilivyoruhusiwa) Katika hali hii, mume ni lazima aangalie yafuatayo:

-     Ni lazima ujue kuwa Sunnah ni kuepuka kumpiga kwani Mtume (S.A.W.) hakuwahi

            kumpiga mwanamke wala mtumwa.

 -     Ni lazima ufanye hivyo katika hali ya juu kabisa ya kutotii, mfano mara kwa mara kukataa tendo la jimai bila ya sababu, mara kwa mara kutosali kwa wakati wake, kuondoka nyumbani kwa muda mrefu bila ya ruhusa na kukataa kusema pahala

alipokuwepo, n.k

-     Usifanye hivyo mpaka awe umeshampa mgomo na kulijadili hilo suala pamoja nae ama ilivyoelezwa katika Qur'an.

-     Usimpige pigo la nguvu la kumuumiza, au kumpiga usoni au katika sehemu zilizo nyepesi kuathirika katika mwili wake.

-     Jiepushe na kumdhalilisha kama kumpiga kwa kiatu, n.k.

 

18. Kusamehe na makaripio yanayofaa

     ·      Mhukumu kwa makosa makubwa tu.

     ·      Msamehe makosa aliyokukosea wewe bali mhukumu kwa makosa ya haki za Allaah, mfano kuchelewesha Sala, n.k

     ·      Kumbuka mazuri yote anayomfanyia kila wakati anapofanya makosa.

     ·      Kumbuka kuwa kila mwanaadamu hukosea na umuwazie dharura mfano huenda

amechoka, ana huzuni, yumo katika siku zake za mwezi au imani/mafungamano yake

katika Uislam bado yamo katika kukua.

     ·      Jiepushe na kumgombeza  kwa mapishi mabaya kwani Mtume (S.A.W.) hakuwahi

kumlaumu yeyote katika wake zake kwa jambo hili. Iwapo amekipenda

chakula, hula na iwapo hakukupenda hukiwacha na hatoi maoni yoyote.

·       Kabla ya kumuwekea wazi kuwa amefanya makosa, jaribu njia nyingine za mzunguko ambazo ni za hekima kuliko kumlaumu wazi wazi.

·       Epukana na kutumia jeuri au maneno yanayoumiza hisia zake.

·       Inapokuwa kuna ulazima wa kujadili tatizo subiri mpaka mnapokuwa

faragha.

    ·       Subiri mpaka hasira zipungue kidogo, hii inasaidia kuweza kudhibiti maneno yako.

 

NYONGEZA YA AL HIDAAYA:

Mwisho, tafadhali mumuombee du'aa aliyeandaa haya, Sheikh Muhammad Abdul Haliym Haamid, mfasiri wa kwa kiingereza Al Akh Abu Talhah na mfasiri wa makala haya kwa kiswahili Ukht Ummu Ummu Ayman, bila kuwasahau walioyatafuta na kuyachagua AL HIDAAYA www.alhidaaya.com
 

 

 

     Mwinyi I. Msellem

     (Health Laboratory Scientific Officer)

     Zanzibar Malaria Control Programme

     P.O.Box 503

     Zanzibar - Tanzania

     Tel             +255 24 223 64 51 (Res)

     Cell Phone +255 747 43 29 11  (Mob)

     Fax             +255 24 223 95 40

    E:mail- mmwinyi@hotmail.com
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template