Mapungufu ya Katiba-I. - Msamaa.
Headlines News :
Home » » Mapungufu ya Katiba-I.

Mapungufu ya Katiba-I.

Written By Unknown on Saturday, March 16, 2013 | 9:45 PM


Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu

 

 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

 

Utangulizi

 

Sifa zote njema anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Rehema na Amani zimshukie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) na Radhi za Mola ziwafikie Maswahaba zake wote Kiramu na kila mwenye kufuata nyayo zao mpaka siku ya Qiyaamah.

 

Kitabu ”MAKOSA YA MSINGI YALIYOMO NDANI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MTAZAMO WA UISLAMU” ni mkusanyiko wa Maudhui mbali mbali zilizotolewa na wahadhiri na wasemaji mbali mbali katika  semina maalumu juu ya maudhui hiyo hapo juu iliyokusanya wanachuoni, wanasheria, walinganiaji na wasomi mbali mbali waliojikusanya katika Ukumbi wa Chuo cha Wasichana cha UMMU SALAMAH, mnamo tarehe 25 Swafar 1432 H sawa na 30 Januari 2011 M, lengo la semina hiyo lilikuwa ni kutafakari maneno ya Mheshimiwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwataka wananchi wa Tanzania wakiwemo wanadini kuchangia maoni  katika mchakato mzima wa kutungwa upya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Semina hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti Shaykh ‘Alliy Adamu ‘Alliy kutoka Msumbiji ilitoa mapendekezo kwamba katika hatua ya awali iko haja ya kueneza yaliyopatikana katika semina hiyo kwa njia ya makongamano mengine katika kiwango cha wilaya, mikoa na Kitaifa, pia kwa njia ya mihadhara mbali mbali, khutba za ijumaa na kwa kutumia vyombo vya habari, Magazeti, Redio, Televisheni, na Makala mbali mbali.

 

Juhudi hii ni katika kutekeleza agizo hilo ambalo tunaamini litaleta mwamko mpya hasa kwa Waislam kuijua hali waliyo nayo kwa sasa na wanatakiwa wafanye nini.

Na kuwasaidia wale watakaoshiriki katika kutoa maoni kwenye kamati ya kuratibu maoni ya uandishi wa katiba mpya.

 

 

Shukrani

 

Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliochangia mada hii hadi kupatikana kwa maandiko haya katika umbo la kitabu. Mola Ajaalie Juhudi zao hizi ziwe katika Mizani ya Matendo yao mema siku ya Qiyaamah.

 

Mkusanyaji:

Shaykh Salim ‘Abdur-Rahiym Barahiyan, (L.L.B. Shari’ah, L.L.M. Shari’ah and Law)

P. O.BOX 1542,

TANGA

 

 

 

 

 

Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu.

 

 

 

SURA YA KWANZA

 

 

Kwa nini Mada hii?

Tuna sababu zifuatazo zinazotufanya tuzungumzie mada hii:

 

1. Ni katika kulingania dini yetu kwa Jihadi ya hoja na kuzuia Munkari (Maovu).

 

 ﴿فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُمْ بِهِ جِهَادًا كَبِيرًا﴾(الفرقان:٥٢ قال تعالى:

 

Amesema Allaah:

“Na wala usiwatii Makafiri na pigana nao Jihadi ya hoja ya (Quraan) Jihadi kubwa”. (Surat AlFurqaan: 52).

 

وقال تعالى:﴿ قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴾(يوسف:١٠٨).

 

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“Sema hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah kwa ujuzi mimi na yule aliyenifuata na Ametakasika Allaah na kila upungufu nami si katika washirikina”

(Surat Yuusuf: 108).

 

وقال صلى الله عليه وسلم:(من رأى منكم منكرا فليغيره بيده فإن لم يستطع فبلسانه فإن لم يستطع فبقلبه وذلك أضعف الإيمان)رواه مسلم.

 

Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):

“Atakaeona miongoni mwenu ovu lolote aliondoe kwa mkono yake, na kama hataweza basi na kwa ulimi wake na kama hataweza basi na aliondoe  kwa moyo wake (alichukie) na hali hii (kulichukia kwa moyo) ni udhaifu mkubwa wa imani” (Imepokewa na Imaam Muslim).

 

عن النعمان بن بشير رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:(مثل القائم في حدود الله والواقع فيها كمثل قوم استهموا على السفينة فصار بعضهم أعلاها وبعضهم أسفلها وكان الذين في أسفلها إذا استقوا الماء مروا على من فوقهم فقالوا لو أنا خرقنا في نصيبنا خرقا ولم نأذي من فوقنا،فإن تركوهم وما أرادواهلكوا جميعا وإن أخذوا على أيديهم نجوا ونجوا جميعا).رواه البخاري.

 

Toka kwa Nu”umaan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ‘anhu) amepokea toka kwa Nabii (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) akisema:

“Mfano wa yule aliesimama katika mipaka ya Allaah na yule alievuka mipaka yake ni mfano wa watu walioingia kwenye Safina kwa kupiga kura na wakawa miongoni mwao juu ya ile Safina na wengine chini (inaashiria ukubwa wa hiyo Safina) ikawa wale waliokuwa chini wakitaka maji huyafuata kwa kupitia kwa wale wa juu, wakasema (kwa kushauriana): kama tungetoboa hukuhuku chini tungeyapata maji bila ya kuwaudhi wenzetu walio juu, kama wataachwa na matakwa yao hayo wataangamia wote na kama wakizuiwa wataokoka wote).”

(Imepokewa na  Imaam Al-Bukhaariy).

 

قال الله تعالى:﴿ كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ)( آل عمران:١١٠)

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“Mmekuwa Umma bora utokanao na watu mnaamrishana mema na mnakatazana mabaya na mnamwamini Allaah” (Surat Al-‘Imraan: 110).

 

 

2. Ni haki ya Kikatiba kwa kila Raia:

 

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania 18(1):

“Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa”

 

 

3. Ni wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa Raia wa nchi hii kuchangia maoni katika mchakato wa kuandikwa upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:

 

Katika Gazeti la MWANANCHI la Jumamosi tarehe 1 Januari 2011:

“Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mchakato wa kuandikwa katiba Mpya.Katika salamu zake za mwaka mpya kwa Taifa jana, Rais Kikwete alisema: “Nimeamua kuunda Tume Maalumu ya Katiba yaani Constitutional Review  Commision. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbali mbali kutoka jamii yetu kutoka pande mbili za Muungano, alisema jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbali mbali ya watu wote, katika kutoa maoni wayatakayo kuhusu katiba ya nchi yao.”

 

 

4. Ni wajibu wetu kutoa Nasaha:

 

قال تعالى:﴿ وَإِنْ أَحَدٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّهِ (التوبة:٦).

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“Kama mmoja yeyote katika washirikina atakuomba awe karibu nawe basi kuwa karibu nae ili apate kusikia maneno ya Allaah”

(Surat At-Tawbah: 6).

 

عن التميم الداري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:(الدين النصيحة.قلنا لمن يارسول الله.قال:لله ولكتابه ولرسوله ولأئمة المسلمين وعامتهم).رواه مسلم.

Imepokewa na Tamiym Ad-Daariy (Radhiya Allaahu ‘anhu),

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):

“(Dini ni nasaha) tukasema kwa ajili ya nani ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? akasema:kwa ajili ya Allaah na Kitabu Chake na Mtume Wake na kwa viongozi wa Waislamu na watu wote)”

(Imepokewa na Imaam Muslim).

 

وقال صلى الله عليه وسلم:(إذا استشار أحدكم أخاه فليشر عليه).رواه ابن ماجه.

Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):

“Atakapotaka ushauri mmoja wenu kwa ndugu yake basi amshauri”.

(Imepokewa na  Ibn Maajah).

 

 

5. Kuwatanabaisha baadhi ya masheikh ambao mara baada ya Rais kutangaza mchakato wa Katiba mpya wakakurupuka na kutoa maoni kwamba wanataka mahakama ya Qaadhi (Kadhi) na nchi kujiunga na OIC na Ijumaa iwe ni siku ya mapumziko, na wameghafilika kwamba Katiba imewanyima haki zao za msingi na kubwa kuliko mahakama ya Qaadhi na OIC na siku ya Ijumaa. Na wengine kuona bado wakati wa kutoa maoni wamewausia WaIslamu wasiseme kitu wasubiri kamati ya kukusanya maoni itakayoundwa na Mheshimiwa Rais.
 
Chanzo: Alhidaaya.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template