Sura ya Tatu na Nne. - Kitoloho
Headlines News :
Home » » Sura ya Tatu na Nne.

Sura ya Tatu na Nne.

Written By Msamaa on Saturday, March 16, 2013 | 9:48 PM


Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu

 
SURA YA PILI

 

Nini Maana Ya Katiba Ya Nchi? Kwa Mtazamo Usio Wa Kidini.

 

Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea  Katiba. Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi (watawaliwa). Ni makubalianao ya wananchi husika juu ya ni jinsi gani taratibu za kanuni za uendeshaji wa mambo mbali mbali katika nchi yao unapaswa kuwa.

(Angalia kitabu HAKI Tolea la 5 Namba 4 Dec. 2002 Uk. 6).

 

Ni muafaka wa Kitaifa juu ya misingi mikuu ya kuendesha nchi.

(Maneno ya Pro.Shivji katika kongamano tarehe 15/1/2011Dar es Salaam.)

 

 

Maana ya katiba ya nchi kwa mtazamo wa Kiislamu

 

Sheria kuu na Sheria Mama katika nchi kwa mujibu wa Uislamu ni Qur-aan na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa sallam).

 

قال تعالى:﴿ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ﴾.(النساء:٥٩).

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

”Ikiwa mkikindana (kukhitalifiana) katika jambo lolote basi lilerejesheni (jambo hilo) kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake”

(Surat An-Nisaa: 59).

 

قال تعالى:﴿ وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا ﴾(الأحزاب:٣٦).

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

”Na haifai kwa muumini mwanamme au mwanamke pale atakapolitolea hukumu jambo lolote Mwenyezi Mungu na Mtume wake wawe na hiari katika kulitekeleza Jambo hilo, na anae muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotevu wa wazi)”

(Surat  Al-Ahzaab: 36).

 

 

 

Historia Ya Katiba Katika Nchi Zilizotawaliwa Na Makafiri

 

“Kwa ujumla nchi nyingi hasa zile zinazoendelea zina katiba zilizoandikwa.nyingi kati ya katiba hizo zilitungwa na kurekebishwa na watawala wa kikoloni, na nyingine zilitungwa baada ya makubaliano na tawala za kikoloni kabla ya kuondoka.Katiba hizo ni maridhiano ambayo yalilinda maslahi ya pande zote mbili:

(1)Tawala za kikoloni zilizokuwa zikiandika.

(2)Nchi iliyokuwa ikipata uhuru(Angalia Jarida la HAKI Toleo la 5 uk.7), (Angalia pia Shetani wa mwalimu uk.6):

"Katiba nyingi katika nchi zilizoendelea zina uhusiano na Katiba na Tawala za kikoloni.

Historia ya katiba hapa Tanzania pia ina uhusiano na tawala za kikoloni zilizokuwa zinatawala kabla ya uhuru".Angalia HAKI toleo la 5 uk.7(Kamati ya Msaada ya Kisheria).

 

 

Historia Ya Mabadiliko Ya Katiba Tanzania

 

1961Katiba ya kwanza ya uhuru iliyowekwa na waingereza (Independence Constitution).

1962Katiba ya Jamhuri (The Republic Constitution) iliitambua Tanganyika kama Jamhuri na ilipunguza madaraka ya Bunge(Imewekwa na Waingereza).

1965Iliwekwa katiba ya muda (The Interim Constitution)

1977Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitungwa na bunge maalum (Constitutional Assembly), (wananchi hawakuhusishwa).Angalia HAKI toleo la 5 uk.10).

Pr.Issa Shirji anabainisha haya pia katika kongamano la Katiba lililoandaliwa na wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Jumamosi tarehe 15/1/2011 angalia Gazeti la MWANANCHI uk.4 tarehe 16/1/2011.

 

 

Mabadiliko Makubwa Yaliyotokea Katika Katiba

 

1961Katiba iliruhusu mfumo wa vyama vingi,

Vyama vifuatavyo vilisajiliwa:TANU, United Tanganyika Party(UTP), African National Congress(ANC), The Peoples Democratic Party(PDP), Peoples Convertion Party(PNP), National Enterprise Party(NEP), All Muslim Nationalist Union of Tanganyika(AMNUT), African Independence Movement(AIM).

1963Halmashauri kuu ya TANU ilipitisha maamuzi kufanya Tanganyika kuwa nchi ya chama kimoja.

1965Sheria ya chama kimoja iliingizwa kwenye Katiba.

1977Haki za binaadamu ziliingizwa rasmi katika Dibaji.

1984Katika katiba ya Jamhuri haki za binaadamu ziliingizwa rasmi katika katiba.

1992Katiba iliruhusu tena mfumo wa vyama vingi kwa shinikizo la nchi za kibeberu (kikafiri).

Katika kitabu: Elimu ya Demokrasia shirikishi (Kitabu kilichotolewa na CTP Dom uk.7) chasema hivi:

"Wanasayansi wa mambo ya siasa wanaelekea kukubali kwamba demokrasia ya vyama vingi imeingizwa toka nje kwa kutokana na masharti ya kupata misaada ya fedha".

 

 

Katiba Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Haibadiliki

 

قال تعالى:﴿ وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنْ كِتَابِ رَبِّكَ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ﴾(الكهف:٢٧).

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):”Nawasomee kilichoteremshwa kwako kwa wahyi (Ufunuo) katika kitabu cha Mola wako ambacho hayabadiliki maneno yake)” (Surat  Al Kahfi: 27).

قال تعالى:﴿ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ. لَا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنْزِيلٌ مِنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴾

(فصلت:٤١-٤٢)

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“Na hakika hiyo (Qur-aan) ni Kitabu kitukufu, hakiingiliwi na batili yoyote mbele yake wala nyuma yake imeteremka kutoka kwa Mwenye hekima ya hali ya juu na Mwenye kushukuriwa sana)”

(Surat Fusswilat: 41- 42).

 

 

 

 

 

 

SURA YA TATU

 

Mambo Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Yanayokwenda Kinyume Na Uislam

 

1.    Mfumo Wa Demokrasia

 

Nini maana ya Democracy?

Ni neno lenye asili ya kigiriki (Demo – crates) yaani utawala wa watu.

"Ni mfumo wa kuendesha serikali ya watu iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu, madaraka na mamlaka, ya mwisho ya serikali hiyo yako mikononi mwa watu"

(Angalia Jifunze Uraia kwa shule za msingi kitabu cha nne na S. A. Numisi uk. 10).

 

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, sehemu ya pili, Serikali na watu, sheria ya 1984 na.15, 16.6,

“Jamhuri ya muungano wa tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki za kijamii na kwa hiyo:

a) Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii.

b) Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi serikali itawajibika kwa wananchi”

 

 

2.    Mamlaka Ya Kutunga Sheria Yako Mikononi Mwa Watu Badala Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)

 

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kifungu 64 (1):

“Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo yote yahusuyo Tanzania bara yatakuwa mikononi mwa bunge”

 

Kifungu 106 (3):

Madaraka yote ya kutunga sheria katika zanzibar katika mambo yote yasiyo mambo ya muungano yatakuwa mikononi mwa baraza la wawakilishi wa Zanzibar.

 

 

3.    Mfumo Wa Kutenganisha Dini Na Mamlaka Ya Nchi (Siasa)

 

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kifungu 19 (2):

“Bila kuathiri sheria zinazohusika za jamhuri ya muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi”.

 

Katika katiba toleo la 2005 ibara ya 3:

3 (1) “Jamhuri ya muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”.

 

 

4.    Mfumo Wa Kufuata  Siasa Ya Ujamaa Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano

 

Kifungu cha 9:

“Lengo la katiba hii ni kuendesha ujenzi wa jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu wa amani kutokana na kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika jamhuri ya muungano”.

 

 

5.    Mfumo Wa Kukataza Kuanzishwa Chama Cha Siasa Chenye Lengo La Kukuza Dini

 

Kwa mujibu wa katiba kifungu 20 (2):

“Kwa kujali masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake:

A) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya:

I) “imani au kundi lolote la dini”.

 

 

6.    Sera Ya Kulazimisha Kila Raia Kufuata Na Kutii Katiba Ya Jamhuri Na Sheria Zake Hata Kama Zinakhalifu Shari”ah Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)

 

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 26 (1):

“Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii katiba hii na sheria za jamhuri ya muungano”.

 

 

7.    Kiongozi Wa Nchi (Rais) Kupewa Madaraka Ya Kuchupa Mipaka (Udikteta)

 

Ka mujibu wa katiba ya jamhuri kifungu 45 (1):

“Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:

A) kutoa msamaha kwa mtu yoyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote na aweza kutoa msamaha bila masharti au kwa masharti kwa mujibu wa sheria.

B) kumwachilia kabisa au kwa muda maalumu mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum.

C) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu.

D) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yote”.

 

 

8.    Uhuru Wa Kubadilisha Dini Anayotaka

 

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 19 (1):

“Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake”.

 

 

9.    Sera Ya Kugombea Uongozi Badala Ya Kugombewa

 

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 67 (3):

“Mtu hataweza kugombea uchaguzi kuwa mbunge wa kuwakilisha jimbo la uchaguzi katika uchaguzi mkuu wowote ikiwa wakati huo yeye amesimama katika uchaguzi kugombea kiti cha Rais, wala hataweza kugombea uchaguzi kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo wowote ikiwa yeye ni Rais”.

 

 

10.           Mfumo Wa Vyama Vingi Vya Siasa

 

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 3 (1):

“Jamhuri ya muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”.

 

 

11.           Kiongozi Mkuu Wa Nchi (Rais) Kuwa Juu Ya Sheria

 

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 46:

(1): wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashtaka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

 

(2) wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosea kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais…

 

 

12.           Matumizi Ya Mapambano (Jihadi) Yanakataliwa

 

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 20 (21):

“Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba na sera zake:

(c) kinakubali na kufungamana na matumizi ya nguvu au mapambano kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa”.

 

 

13.           Itikadi Ya Al-Walaa Wal-Baraa (Kupenda Kwa Ajili Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Na Kuchukia Kwa Ajili Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Inavunjwa

 

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Haki ya Usawa, kifungu 12(4):

Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.

 

Kifungu 12 (5):

Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja, haki, au mahitaji mengineyo kwa watu mbali mbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahali walipotokea, maoni ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali ya maisha kwa namna ambapo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa dhaifu au duni au kuwekewa vikwazo au masharti ya upingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa auwanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima isipokuwa kwamba neno “kubagua” halitafafanuliwa kwa maana ambayo “itazuia serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template