Wazanzibari wanaodai Serikali Tatu bungeni watishwa - Kitoloho
Headlines News :
Home » » Wazanzibari wanaodai Serikali Tatu bungeni watishwa

Wazanzibari wanaodai Serikali Tatu bungeni watishwa

Written By Msamaa on Thursday, April 17, 2014 | 1:19 AM




Dodoma.
Wakati U-unguja na U-pemba ukianza kuibuka bungeni, mbunge wa Mwanakwerekwe (CCM), Haji Juma Seleweji, amesema wanaounga mkono serikali tatu wasijute watakaporudi Zanzibar.
Wajumbe wengi kutoka Zanzibar, badala ya kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba ili kuiboresha, walishambuliana kwa maneno, wakishindwa kuficha hisia za ubaguzi.
Kila kundi lilituhumu jingine kuwa lilikuwa pinzani hata kabla ya mapinduzi. Haji Juma Seleweji alianza kwa kutahadharisha wanaoishi Bara watajuta.
Aliwaonya Wazanzibari wanaunga mkono serikali tatu bungeni, kuwa watakapofika Zanzibar wasizungumze lolote na wasijute kwani watasulubiwa.
“Hata mkiingia shimoni, msije kujuta na kusema hamkufahamu, tumewaonya lakini hamkusikia,”alisema .
Abubakari Hamisi, alisema kuna Wazanzibari ambao kwa makusudi na kwa nia isiyo njema, wanaigawa Zanzibar ili waendelee kuikandamiza.
Naye Waziri Rajabu Salimu, aliwatuhumu wajumbe wanaounda mkono serikali tatu, kwamba ni vizazi vya waliopinduliwa katika mapinduzi matukufu mwaka 1964.
“Wapinzani wa Zanzibar kabla ya mapinduzi matukufu, vizazi vyao vipo na ndivyo vinasumbua kwa kuwa wapinzani wa muungano hadi sasa,”alisema.
Aliwatuhumu Wapemba kwamba, hawaoni hasara kuvunja muungano kwasababu udugu wao na Watanganyika siyo wa karibu kama ilivyo kwa Waunguja ambao udugu wao na Watanganyika ni wa damu.
Alisema Wapemba kubeba mizigo, maduka yao na kwenda kwao siyo tatizo kama ilivyo kwa Waunguja ambao kwa vyovyote ilivyo, hawataweza kugawanywa na Watanganyika.
Naye Issa Gavu, alisema wanaotaka serikali tatu wamekuwa maadui wa mapinduzi ya Zanzibar, tangu enzi.
“Maadui wa Mapinduzi bado wapo, wanaendelea kuzaliwa kila kukicha lakini haiwezekani na haitawezekana kuendelea na mpango huo, tumechoka,”alisema Gavu.
Aliwataka Wajumbe kutoka Zanzibar kutozungumza lolote kuhusu shida na raha za Wazanzibari, badala yake wamwachie Dk Ali Mohamed Shein.

Chanzo: Mwananchi; 17/04/2014
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template