- Kitoloho
Headlines News :
Home » »

Written By Msamaa on Saturday, April 20, 2013 | 2:37 AM


MIPAKA YA KAZI ZA MWANAMKE KATIKA UISLAMU.

 
Utangulizi

 

Sifa njema anastahiki Allah aliyeumba na akafanya sawa sawa alivyoviumba, akakadiria na akaongoza. Rehema na Amani zimwendee bwana wetu, kiongozi na mwalimu wetu Nabii Muhammad, na juu ya Swahaba zake na Ahli zake.

 

Nimekuwa nikiguswa sana na mambo mbalimbali yanayozungumzwa kuhusiana na mwanamke katika Uislamu. Katika kitabu  hiki nitazungumzia jambo moja muhimu linalohusiana na mwanamke ambalo limekuwa ni sehemu ya kejeli na hata kujadiliwa na watu mara nyingi. Tena kumekuwa na watu wengi wakiuliza maswali kuhusiana na Uislamu unavyosema juu ya jambo hilo, nalo ni MIPAKA YA KAZI ZA MWANAMKE KATIKA UISLAMU.

 

Awali ya yote ifahamike kuwa suala la mipaka ya kazi za mwanamke linakuja katika Uislamu kama jibu dhidi ya kile kilichotokea Ulaya wakati wa Mapinduzi ya Viwanda yaliyoteka huko Ulaya katika karne ya 19.

 

Kimsingi kadhia na dhana nzima ya mwanamke kutoka na kwenda kufanya kazi nje ya nyumba yake ni kadhia ambayo haiko katika kivuli cha Uislamu dini ambayo inajulikana wazi kuwa inadhamini malezi ya mwanamke katika maisha yake yote tangu kuzaliwa hadi kufa kwake.

 

Naingia katika Maudhui hii kwa kuanza na kauli ya Ustaadh Muhammad Qutub katika kitabu chake; "شبهات حول الإسلام"  “Shubhaatun hawlal Islaam” ukurasa wa 108 hadi wa 111:

"إن الثورة الصناعية شغّلت النساء والأطفال، فحطمت روابط الأسرة وحلت كيانها. ولكن المرأة هى التى دفعت أفدح الثمن من جهدها وكرامتها، وحاجاتها النفسية والمادية. فقد نكل الرجل عن إعالتها من ناحية، وفرض عليها أن تعمل لتعول نفسها حتى لو كانت زوجة وأمًّا، واستغلتها المصانع أسوأ استغلال من ناحية أخرى، فشغّلتها ساعات طويلة، وأعطتها أجرًا أقل من الرجل الذى يقوم معها بذات العمل فى ذات المصنع. ولا تسأل لماذا حدث ذلك، فهكذا هي أوروبا، جاحدة بخيلة، لا تعترف بالكرامة للإنسان من حيث هو إنسان ولا تتطوع بالخير حيث تستطيع أن تعمل الشر وهى آمنة. تلك طبيعتها على مدار التاريخ، في الماضي والحاضر والمستقبل إلا أن يشاء الله لها الهداية والارتفاع. وإذا كان النساء والأطفال ضِعَافًا، فما الذي يمنع استغلالهما والقسوة عليهما إلى أقصى حد؟ إن الذي يمنع شيء واحد فقط، هو الضمير، ومتى كان لأوروبا ضمير؟!! ومع ذلك فقد وُجدت قلوب إنسانية حية لا تُطيق الظلم، فهبت تدافع عن المستضعفين من الأطفال. نعم الأطفال فقط! فراح المصلحون الاجتماعيون ينددون بتشغيلهم فى سن مبكرة، وتحميلهم من الأعمال ما لا تطيقه بنيتهم الغضَّة التي لم تستكمل نصيبها من النمو، وضآلة أجورهم بالنسبة للجهد العنيف الذى يبذلونه. ونجحت الحملات، فرفعت أجورهم، ورفعت رويدًا رويدًا سن التشغيل، وزادت الأجور وخفضت ساعات العمل.أما المرأة فلم يكن لها نصير. فنصرة المرأة تحتاج إلى قدر من ارتفاع المشاعر لا تطيقه أوروبا! لذلك ظلَّت في محنتها تنهك نفسها فى العمل – مضطرة لإعالة نفسها - وتتناول أجرًا أقل من أجر الرجل، مع اتحاد الإنتاج والجهد المبذول. وجاءت الحرب العظمى الأولى ثم الثانية، وقتل عشرات الملايين من الشباب الأوربيين والأمريكان. وواجهت المرأة قسوة المحنة بكل بشاعتها. فقد وجدت ملايين من النساء بلا عائل، إما لأن عائلهن قد قتل فى الحرب، أو شُوِّه، أو فسدت أعصابه من الخوف والذعر والغازات السامة الخانقة، وإما لأنه خارج من حبس السنوات، يريد أن يستمتع ويرفه عن نفسه، ولا يريد أن يتزوج ويعول أسرة تكلفه شيئا من المال والأعصاب. ومن جهة أخرى لم تكن هناك أيدٍ عاملة من الرجال تكفى لإعادة تشغيل المصانع لتعمير ما خرَّبته الحرب. فكان حتمًا على المرأة أن تعمل وإلا تعرَّضت للجوع هي ومن تعول من العجائز والأطفال. وكان حتمًا عليها كذلك أن تتنازل عن أخلاقها. فقد كانت أخلاقها قيدًا حقيقيًا يمنع عنها الطعام! إن صاحب المصنع وموظفيه لا يريدون مجرد الأيدى العاملة، فهم يجدون فرصة سانحة، والطير يسقط من نفسه – جائعًا – ليلتقط الحَب، فما الذي يمنع من الصيد؟  وما دامت قد وجدت – بدافع الضرورة – امرأة تبذل نفسها لتعمل، فلن يتاح العمل إلا للتى تبذل نفسها للراغبين. ولم تكن المسألة مسألة الحاجة إلى الطعام فحسب. فالجنس حاجة بشرية طبيعية لا بد لها من إشباع. ولم يكن فى وسع الفتيات أن يشبعن حاجتهن الطبيعية ولو تَزَوَّج كل من بقى حيًا من الرجال، بسبب النقص الهائل الذى حدث فى عدد الرجال نتيجة الحرب. ولم تكن عقائد أوربا وديانتها تسمح بالحل الذى وضعه الإسلام لمثل هذه الحالة الطارئة، وهو تعدد الزوجات. لذلك لم يكن بُدٌّ للمرأة أن تسقط راضية أو كارهة لتحصل على حاجة الطعام وحاجة الجنس، وترضى شهوتها إلى الملابس الفاخرة، وأدوات الزينة، وسائر ما تشتهيه المرأة من أشياء. وسارت المرأة فى طريقها المحتوم، تبذل نفسها للراغبين، وتعمل في المصنع والمتجر، وتشبع رغباتها عن هذا الطريق أو ذاك. ولكن قضيتها زادت حِدَّة. فقد استغلت المصانع حاجة المرأة إلى العمل، واستمرَّت في معاملتها الظالمة التى لا يبررها عقل ولا ضمير، فظلت تمنحها أجرًا أقل من أجر الرجل الذى يؤدى ذات العمل في ذات المكان. ولم يكن بد من ثورة. ثورة جامحة تحطِّم ظلم أجيال طويلة وقرون. وماذا بقى للمرأة؟ لقد بذلت نفسها وكبرياءها وأنوثتها، وحرمت من حاجتها الطبيعية إلى أسرة وأولاد تحس بكيانها فيهم، وتضم حيواتهم إلى حياتها، فتشعر بالسعادة والامتلاء. أفلا تنال مقابل ذلك – على الأقل – المساواة فى الأجر مع الرجل وهو حقها الطبيعي الذي تقرره أبسط البديهيات؟ ولم يتنازل الرجل الأوربى عن سلطانه بسهولة. أو قُلْ: لم يتنازل عن أنانيته التى فُطر عليها. وكان لا بد من احتدام المعركة، واستخدام جميع الأسلحة الصالحة للعراك. استخدمت المرأة الإضراب والتظاهر. واستخدمت الخطابة فى المجتمعات. واستخدمت الصحافة. ثم بدا لها أنها لا بد أن تشارك فى التشريع لتمنع الظلم من منبعه، فطالبت أولاً بحق الانتخاب، ثم بالحق الذى يلى ذلك بحكم طبائع الأشياء، وهو حق التمثيل فى البرلمان. وتعلمت بذات الطريقة التي يتعلم بها الرجل؛ لأنها صارت تؤدى ذات العمل، وطالبت كنتيجة منطقية لذلك أن تدخل وظائف الدولة كالرجل، ما داما قد أُعدَّا بطريقة واحدة، ونالا دراسة واحدة. تلك قصة "كفاح المرأة لنيل حقوقها" فى أوروبا. قصة مسلسلة، كل خطوة فيها لا بد أن تؤدى إلى الخطوة التالية، رَضِيَ الرجل أو كره، بل رضيت المرأة أو كرهت، فهي نفسها لم تعد تملك أمرها فى هذا المجتمع الهابط المنحل الذى أفلت منه الزمام. ومع ذلك كله فقد تعجب حين تعلم أن انجلترا – أم الديمقراطية – لا تزال إلى هذه اللحظة تمنح المرأة أجرًا أقل من أجر الرجل فى وظائف الدولة، رغم أن فى مجلس العموم نائبات محترمات!!"

 

Maneno haya yana maana ya kuwa; “Mapinduzi ya Viwanda yaliyofanyika huko Ulaya yaliwashughulisha na kuwaathiri zaidi wanawake na watoto kuliko wanaume, hivyo yakawa ni sababu ya kuvunja mafungamano na mifumo ya kijamii. Katika hali hii mwanamke ndiye aliyelipa gharama kubwa zaidi kwa juhudi, heshima, na mahitajio yake ya kiroho. Ni katika hali hii mwanamume, alizembea na kuacha kumhudumia mwanamke, hivyo mwanamke akajikuta analazimika kufanya kazi ili aikimu nafsi yake hata kama yeye ni mke wa mtu au ni mama mwenye watoto. Kwa upande mwingine viwanda vilimtumia mwanamke vibaya sana, vilimtumia kikazi kwa mda mwingi zaidi huku akipewa malipo kidogo kulingana na mwanamume anayefanya kazi kama hiyo katika sehemu hiyo hiyo. Hilo si jambo la kushangaza hata kidogo kwa Ulaya ambayo ilikuwa imegubikwa na ubakhili, ukatili, ubinafsi, utimbakwiri, nk. Kwani historia inaonyesha dhahiri shahiri kuwa kuna wakati Ulaya ilifika pahala ikawa haitambui utu wa mwanadamu, na hivyo ikashindwa kumfanyia mwanadamu heri yoyote badala yake ikajikuta ikimfanyia shari tena kwa kufurahia madhila hayo, na kuyafanya pasina kujisikia tabu yoyote. Katika hali hii ambayo ndiyo ilikuwa kawaida ya Ulaya, wanawake na watoto wadogo ambao kwa maumbile yao ni wanyonge walijikuta wakifanyiwa ukatili wa kutisha na kutumiwa visivyo pasina kuwepo wa kuwatetea. Ambacho kingeweza kuwanusuru na hali hii ni kitu kimoja tu nacho ni utashi na dhamira ya kweli, ambavyo vyote viwili havikuwepo Ulaya. Kwa bahati nzuri wakapatikana watu wachache waliokuwa na nyoyo zilizokuwa hai ambao hawakuweza kuona na kuvumilia dhulma na hali hizi zikiendelea ambao kwanza walianza kuwatetea watoto. Wanaharakati hawa walianza na masuala mazima ya kumfanyisha kazi mtoto katika umri mdogo, kumfanyisha kazi ambazo umbile lake changa haliwezi kuzimudu, na ujira mdogo anaopewa ambao haukuwa ukilingana na kazi nzito alizokuwa akifanyishwa. Harakati hizi hatimaye zilifanikiwa, ikawa malipo ya kazi ya mtoto yakapandishwa, kidogokidogo, umri wa kufanya kwake kazi ukaongezwa, na saa zake za kufanya kazi zikapunguzwa. Ama mwanamke yeye hakuwa na wa kumuokoa au kumunusuru. Maana kumunusuru mwanamke kulihitaji hisia kubwa ambazo Ulaya haikuwa nazo. Hivyo mwanamke akajikuta akibaki kazini ili aweze kujihudumia, huku akifanya kazi nzito na malipo yakiwa kidogo sana ukilinganisha na mwanamume anayefanya kazi hiyo hiyo tena sehemu moja. Kisha vikaja vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambapo mamilioni ya vijana wa Ulaya na Amerika waliouliwa. Hapo mwanamke akakabiliwa na tabu zaidi kutokana na mamilioni ya wanawake kubaki pasina familia; kwa kuwa ima familia zao ziliuliwa vitani, kuharibiwa kimwili na kisaikolojia kutokana na wasiwasi au gesi za sumu zilizotumika katika vita hivyo, au kutokana na wanaume kutoka kizuizini ambapo walikuwa kwa mda mrefu na hivyo wakawa wanataka wapumzike, wastarehe bila kuoa na kuhudumia familia ambazo zingewagharimu mali na nguvu. Kwa upande mwingine, hakukuwa na wafanya kazi wa kutosha wa kiume ili kuendesha viwanda na kujenga majengo yaliyoharibiwa na kubomolewa na vita. Hivyo ikawalazimu wanawake kutoka na kwenda kufanya kazi, la sivyo wangejikuta katika njaa na shida kubwa nao wana watoto pamoja na vikongwe ambao hawakuwa na wa kumtegemea ila wao. Katika mazingira haya wanawake walijikuta wakipoteza maadili yao. Kumbe wenye viwanda hawakuwa wakitaka wafanyakazi tu ambao kwa sasa walikuwa wanawake bali walipata fursa nyingine kwa wanawake hao nayo ni kutupa mbegu au punje katika mitego mbele ya ndege wenye njaa ili wadonee mbegu hizo! Hivyo katika hali kama hiyo watasalimikaje ndege hao na kudonoa mbegu hizo? Kwa kuwa wamepatikana katika mlango wa dharura wanawake wanaojitahidi watoke ili wafanye kazi, na kazi nazo sasa wakawa hawapewi ila wale wanawake ambao wanajitahidi wajitoe na kuwa vyakula vya wenye kuwataka kijinsia. Kwa hiyo mas’ala hayakuwa ya haja ya chakula tu basi bali maharamia waajiri wa wanawake walichukua fur’sa hii kuwatafuna wanawake watakavyo. Matamanio ya kijinsia ni miongoni mwa mahitajio ya kimaumbile ya binadamu ambayo ni lazima ayakidhi. Wala isingewezekana kwa wanawake wakati ule kukidhi haja za maumbile yao hata kama kila mwanamme aliyebaki hai wakati ule angeoa kutokana na upungufu mkubwa uliojitokeza wa wanaume kwa sababu ya vita hivi. Kwa bahati mbaya zaidi itikadi na dini za Ulaya hazikuwa ni zenye kuruhusu suluhisho lililowekwa na Uislamu katika hali za dharura kama hizi ambalo ni kuoa mke zaidi ya mmoja. Hivyo ikawa hapana budi kwa wanawake kuangukia kwa kupenda au kutokupenda katika Zinaa ili tumbo na tupu zao zipate kushiba. Bali wakajikuta kuwa wanahitaji kuyaridhisha matamanio yao ili wapate mavazi ya kifaghari, mapambo na vitu mbalimbali miongoni mwa vitu walivyokuwa wakitamani. Wakawa wanawake hawana budi tena ila kutoa miili yao kwa wanaowataka, na wakifanya kazi katika viwanda na sehemu nyingine pamoja na malipo waliyokuwa wakiyapata wakawa pia wanaendelea kuyashibisha matamanio yao ya kijinsia kwa njia za haramu.  Tatizo likazidi kuwa kubwa zaidi pale wenye viwanda walipochukulia shida ya wanawake ya kutoka kwenda kufanya kazi kama fursa ya kuwatesa, kuwanyanyasa na kuwadhulumu pasina sababu yoyote yenye maana kimantiki ya kuwafanyia hivyo kiakili au kidhamira. Wakawa wakipewa ujira mdogo mno kuliko wanaume wanaofanya nao kazi kama hiyo katika sehemu hiyo hiyo. Hapo ikawa hakuna budi lazima yafanyike mapinduzi kuiondoa hali hii ya dhulma iliyodumu kwa mda mrefu tena vizazi kwa vizazi. Lakini baada ya mageuzi haya wanawake walijitahidi kwa nafsi zao, na kuonyesha kuwa nao wanaweza na hawashindwi kitu. Hapo wakajikuta wanazikimbia haja zao za kimaumbile walizoumbiwa na Allah za kuhitaji familia na hivyo bila wao kupenda wakajikuta wakiwakimbia watoto wao wenye kuwahitaji sana katika sehemu za maisha yao ili waweze kukua vizuri. Wanawake wakaamua sasa wabaki hivyo hivyo hata pale ambapo bado waliendelea kupata kiwango kidogo cha ujira kulingana na wanaume wanaofanya nao kazi sehemu moja tena kazi moja. Wanaume wa Ulaya kimaumbile walijikuta hawako tayari kuachia ngazi kirahisi na kuwa sawa na wanawake katika mambo mengi. Hapo wanawake wakajikuta hawana budi waingie katika migomo na maandamano, wapaze sauti katika makongamano, na vyombo vya habari ili kuwashinikiza wanaume wawapatie fursa na haki sawa kama walivyokuwa wakidai. Kisha baadaye wakaona kuwa hawana budi washiriki katika rasimu za kutunga Sheria ili waweze kuizuia dhulma waliyokuwa wakiiona kuanzia katika mzizi hadi katika matawi yake. Hapa wakadai haki ya kushirikishwa katika chaguzi mbalimbali, na haki ya kushiriki kuwakilisha bungeni. Wakajifunza kwa njia ile ile wanayojifunza mwanamume kwa kuwa sasa wanafanya kazi ile ile wanayofanya wanaume. Kimantiki wakawa sasa wanadai waingie katika shughuli za kiserikali kama wanaume maadamu wote yaani wanaume na wanawake wameandaliwa kwa njia moja na wamepata somo moja. Hicho ndicho kisa cha wanawake wa Ulaya katika kutafuta haki zao ambacho wanawake wetu hawakifahamu. Kama ulivyoona kuwa ilikuwa ni hatua kwa hatua, hatua moja ilipelekea hatua nyingine, wanaume wapende au wasipende, bali wanawake wapende au wasipende walijikuta wanavutwa na hatua hizo. Pamoja na haya yote wanawake hawakuzingatiwa kuwa wanamiliki nafsi zao katika jamii hii iliyokuwa imeporomoka vibaya kimaadili na kupoteza mwelekeo kabisa. Pamoja na yote haya utastaajabu kuona Uingereza ambayo inadai kuwa ni mama wa demokrasia duniani bado hadi sasa inawapa wanawake ujira kidogo ukilinganisha na wanaume katika kazi za serikali pamoja na kuwepo katika bunge la Uingereza wawakilishi wa kike wenye kuheshimiwa”.

 

Tunaweza kuongeza katika haya aliyosema Muhammad Qutub kuwa Mwanamke hadi sasa bado anapata ujira mdogo Marekani na nchi nyingine nyingi za Ulaya wala si Uingereza tu, na bado anapigania apate malipo sawa na mwanamume bila mafanikio yoyote. 

 

Katika Suratu Yuusuf aya ya 111 Allah anasema: “Bila shaka katika hadithi zao hizi limo fundisho kwa wenye akili. Si maneno yaliyozuliwa, bali ni hakikisho la yale yaliyokuwa kabla yake (miongoni mwa vitabu vya Mwenyezi Mungu) na ni maelezo pia ya kila kitu (kinachohitajiwa katika dini), na ni uwongofu na rehema kwa watu wenye kuamini”  (12:111)

 

 

MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUFANYA KAZI MWANAMKE

 

Msimamo wa Uislamu katika kufanya kazi mwanamke umewekwa wazi na kisa cha Nabii Mussa na Mabinti Wawili wa Shu‘ayb ‘Alayhim Sswalaatu Wassalaamu. Katika kisa hicho tunaona kuwa Nabii Mussa alitoka Misri hali ya kuwa anakimbia kuadhibiwa na Firiawni. Kapita Nabii huyu wa Allah jangwa la Sinai peke yake hali ya kuwa ni mwenye njaa na kiu kikali, huku akiogopa na kugeukageuka kuangalia kama kuna mtu anayemfuata kwa nyuma au anamfukuza. Akafika katika mji wa Madyani nje kidogo ya mipaka ya Mashariki ya mji wa Misri. Hapo aliona pembeni kuzunguka kisima cha maji idadi kubwa ya wafugaji wakisongamana na kusukumana katika kuwanywesha wanyama wao. Mbali kidogo na vurugu na misongamano hii ya wachungaji katika kunyesha wanyama wao aliwaona mabinti wawili wakiwaswaga na kuwazuia wanyama wao. Walikuwa wakifanya hivi hadi watakapomaliza watu wengine kuwanyesha wanyama wao ndipo na wao wapate kuwanywesha wanyama wao. Kwa kuwa Nabii ni kama baba wa Umma aliwaendea wale wasichana wawili ili apate kujua kulikoni na apate kutulizana kwa kuwasaidia pale atakapojua nini shida yao. Wale wanawake wakamwambia kuwa baba yao ni mzee sana na hali ya afya yake haimruhusu kuja na kuwanywesha wanyama. Hivyo wamelazimika wao kufanya kazi ile kwa kuwa hawana kaka au waume wa kuwafanyia kazi ile. Na pale walikuwa wanasubiri hadi watu wengine wanyeshe mifugo yao na waondoke kisha na wao ndipo wanyweshe. Walikuwa wanafanya hivi kwa kuchelea wasije wakasukumana na kuchanganyika na wanaume wasiokuwa maharimu wao. Kusikia hivyo Nabii Mussa akawaonea huruma. Haraka haraka akawasaidia kunywesha mifugo yao ili wapate kuondokana na tabu ili na kuchanganyika na wanaume. Mabinti wale wawili wakamshukuru Nabii Mussa na kuondoka. Nabii Mussa akaelekea katika kivuli cha mti akakaa chini ya kivuli hicho huku akimuomba na kumnong’oneza Mola Wake.

 

Baada ya muda si mrefu akamuona mmoja kati ya wale mabinti wawili akimjia tena karibu ajikwae na kuanguka kutokana na soni aliyokuwa nayo wakati akija. Huku akiwa anaufunika uso wake kwa Niqaab na akishindwa hata kunyanyua macho yake juu ya ardhi kutokana na haya iliyokithiri, alimwambia Nabii Mussa kuwa baba yao ametambua alichofanya katika wema ule wa kuwahudumia binti zake wawili na hivyo anapenda awe mgeni wake na amlipe kwa kazi ile nzuri aliyofanya. Nabii Mussa alikubali na akaongozana naye kwenda kwa baba yao lakini alimtangulia binti yule japo alikuwa hapajui kwao ila alimtaka binti yule awe akimwambia apinde aidha kulia au kushoto hadi wafike nyumbani kwao. Hapa yule binti aliyemwendea Mussa na kumwambia kuwa baba yake anamuita, walipofika kwao alitoa rai kwa baba yake kuwa amwajiri Mussa awe akichunga na kuwanywesha wanyama wao badala yao. Pia alimweleza baba yake nguvu za Nabii Mussa na Uaminifu wake; na hizi ni sifa mbili za msingi kwa mfanya kazi bora. Mwanamke yule mwenye akili aliyajua yale kutokana na busara ya akili yake kuwa bila shaka Nabii Mussa ana nguvu sana maana aliweza kunyanyua peke yake jiwe lililokuwa likifunika mdomo wa kisima ambalo watu kadhaa walikuwa wakishindwa kulinyanyua lakini yeye peke yake aliweza kulinyanyua. Ama Uaminifu wake dalili yake ni kuwa Mussa alikataa binti yule amtangulie kutokana na kuhifadhi kwake macho kwani kwa dada yule kutangulia ingeweza ikatokea upepo ukapepea nguo zake na hivyo kumfanya Mussa ambaye si mahrimu wake aone maumbile yake. Baba wa mabinti wale wawili ambaye ni Shu‘ayb alikubali fikra ile iliyotoka kwa mmoja wa mabinti wake ya kumuajiri Nabii Mussa na wakakubaliana na Mussa afanye kazi ile miaka minane ambayo pia ndiyo itakuwa ndiyo mahari ya mmoja wa binti zake wale kama alivyopendekeza mzee yule mwenye hekima. Muda aliotaka mzee yule ulikuwa ni miaka minane (8) lakini kama Mussa atatimiza miaka kumi hiyo ni kwa mapenzi yake. Lakini Nabii Mussa akaamua kufanya kazi ile kwa miaka kumi, malipo yakiwa ni chakula na kuhifadhi utupu yake. Baada ya Mussa kumaliza miaka minane alifungishwa ndoa. Hichi ndicho kisa cha Nabii Mussa na mabinti wawili wa mzee Shu‘ayb kama Allah alivyokieleza katika Suratul Qaswas na vilvile kimetajwa katika Taurati. Ndani ya Qur’ani Tukufu Allah anasema katika aya ya 23 hadi 28 ya Suratul Qaswas:

 

{وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِنْ دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا قَالَتَا لاَ نَسْقِي حَتَّى يُصْدِرَ الرِّعَاءُ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ * فَسَقَى لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّى إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنْزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ * فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لاَ تَخَفْ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ * قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ * قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنْكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَى أَنْ تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِنْدِكَ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّالِحِينَ * قَالَ ذَلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ أَيَّمَا الأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلاَ عُدْوَانَ عَلَيَّ وَاللَّهُ عَلَى مَا نَقُولُ وَكِيلٌ}

 

Aya hizi zina maana ya kuwa; “Na alipoyafikia maji ya Madyani (mahali wanapoteka maji watu wa hapo), alikuta kundi la watu wananywesha (wanyama wao), na akakuta kando yao wanawake wawili wanazuia (wanyama wao wasiende kunywa maji pamoja na wale wanyama wengine). Akasema (Mussa): “mna nini”? (Mbona hamteki na nyinyi na mkanywesha wanyama wenu)? Wote wawili wakasema: “hatunyweshi mpaka wachungaji warudishe (wanyama wao; hatuwezi kupigna nao vikumbo), na baba yetu ni mzee sana. Basi (Mussa) akawanyweshea, kisha akarudi kivulini, na akasema: “Mola wangu! bila shaka mimi ni mhitaji wa heri utakayoniteremshia”. Basi akamjia mmoja katika wale wawili, anakwenda na huku anaona haya, akasema: “baba yangu anakuita ili akulipe ujira wa kutunyweshea”. Basi alipomfikia na kumsimulia kisa chote, alisema: “usiogope umekwisha kuokoka na watu madhalimu”. Akasema mmoja wa wale wawili: “ewe baba yangu! mkodi huyu (awe anachunga wanyama wako badili yetu). Bila ya shaka mbora uwezaye kumuajiri ni ambaye mwenye nguvu, mwaminifu (Na huyu ana sifa zote hizi). Akasema: “Mimi nataka nikuoze mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane; na kama ukitimiza kumi ni hiari yako, lakini mimi sitaki kukutaabisha: utanikuta Inshaallah miongoni mwa watu wema”. Akasema (Mussa): “mapatano hayo yamekwisha kuwa baina yangu na baina yako; muda mmojawapo nitakaoumaliza basi nisidhulumiwe; na Mwenyezi Mungu ni mlinzi juu ya haya tunayoyasema”. (Qaswas: 23-28)

 

Kalamu haiwezi kukiandika na kukimaliza kila kilichopo katika aya hizi sita miongoni mwa Adabu, Mazingatio na Shari’ah zenye kumhakikishia mtu mafanikio katika dunia na akhera. Si makusudio yangu kueleza mambo hayo hapa lakini nitajitahidi kutohoa katika aya hizo mipaka ya wanawake kufanya kazi nje ya nyumba zao na jukumu la kila upande katika kumchunga adabu na nyajibu zinazotakikana kwa wote wanawake na wanaume. Aya zinawawekea wazi wenye kutafakari mambo yafuatayo;

 

1.   Haifai kwa wanawake kutoka kwenda kufanya kazi nje ya nyumba zao ila katika hali ya dharura kubwa. Na kubwa zaidi ya dharura hizo ni kukosekana kwa wanaume katika maharimu zao wenye kufanya kazi. Mabinti wale wawili walimwambia Nabii Mussa kuwa wao wamelazimika kufanya kazi ile kwa kuwa baba yao ni mzee sana na hivyo hana uwezo wa kufanya kazi na hawakuwa na mwanamume mwingine ambaye angeweza kufanya kazi ile. Hawakuwa na ndugu wa kiume kama kaka, mjomba, baba mdogo, au baba mkubwa ambaye angefanya kazi ile badala yao. Hivyo wamejikuta wanalazimika kutoka kwenda kuchunga na kuwanywesha wanyama wao ili wasije wakafa kwa njaa na kiu. 

  

2.   Wanawake wanapolazimika kutoka kwenda kufanya kazi basi iwe ni kwa Heshima na Uchaji Mungu (Taq’wa) na wasijichanganye na wanaume wasiokuwa maharimu zao.  Kisa cha mabinti hao kinatueleza kuwa Nabii Mussa aliwaona mabinti wale wawili wakiwazuia wanyama wao wasiende kunywa maji pamoja na wale wanyama wa watu wengine mpaka wale wachungaji wengine warudishe wanyama wao ndipo na wao waende kunywesha wanyama wao kwa kuchelea kusongamana na kupigana vikumbo nao, jambo ambalo lingeweza kupelekea mathalani mtu muovu kuwasogelea. Kwa kufanya vile walivyofanya wakawa wamefunga mlango wa fitna za shetani na matamanio ya kuyaendea machafu ya Zinaa. Jingine ni kuwa walikuwa hawasemi na yeyote. Na lau kama si Nabii Mussa kuwauliza kwa heshima na adabu ili awasaidie basi wasingesema na yeyote. Unaona pia walimwachia awafanyie kazi ile nzito ya kuteka maji kwa ajili ya wanyama.

 

3.   Wanawake kuzungumza na wanaume wa mbali ambao si maharimu zao ni dharura tu tena mazungumzo hayo yawe katika kiwango cha lazima cha kusherehesha hali hiyo ya dharura pasina kuzidisha zaidi ya hapo kama inavyoonyeshwa katika kisa hicho ambacho zaidi ya hapo binti yule aliyekuja kumuita Nabii Mussa alilazimiana na adabu, heshima, haya na aibu.

 

4.   Ni juu ya wenye madaraka au wenye uwezo katika jamii miongoni mwa wanaume wafanye kila wawezalo katika kuwaondolea wanawake tabu na shida za kufanya kwao kazi nje ya majumba yao. Kwa kufanya hivyo watawalinda na madhila ya kuchanganyika na wanaume. Ndipo utaona kuwa Nabii Mussa alifanya haraka katika kuwasaidia kuwanywesha wanyama wao. Lau kama tungekuwa tunafanya kama Nabii Mussa alivyofanya basi tungeweza kuondoa katika jamii yetu shida na majanga mengi yanayowasibu wanawake ambayo sote tunayajua vyema. Na ni juu ya wanawake kumshukuru Allah pale wanapopata neema ya wanaume wanaosimama katika kufanya kazi badala yao.

 

5.   Tunaona vile vile kuwa wanawake wale wawili walikubali hali ya kuwa ni wenye kushukuru msaada wa Nabii Mussa na wakapupia katika kuitumia fursa ile kumshauri na kumuomba baba yao amwajiri Nabii Mussa ili awe akifanya kazi ile nao waweze kuondokana na tabu za kazi nje kama kazi ile ya kuchunga wanyama na kuwanywesha. Wala hawakumwambia baba yao kuwa awape nafasi kama ile ya “hawavumi lakini wamo” yaani wajitegemee, na kuhakiki kuwa wao wanajiweza na kuwa hawana haja na kusaidiwa na wanaume kama wanavyodai wale wanawake wa “khamsini kwa khamsini” katika lile tangazo maarufu la jinsia na haki sawa hapa nchini Tanzania; ni kweli kuwa “mkono ubebao mwana ndio uleao taifa”, lakini hilo ni “neno la haki ambalo ndani yake itafutwao ni batili”. Au kama wale wanawake wasemao katika makongamano yaliyoanzia kule Beijing China kuwa wanawake ni kama wanaume katika kila kazi.      

 

6.   Baba ambaye ni msimamizi wa mabinti wale wawili haraka haraka aliamua kumuajiri Nabii Mussa ili awe akifanya kazi badala ya watoto wake ili kuwahifadhi watoto wake na tabu, mitihani, na fitna kwa kufanya kwao kazi nje ya nyumba. Bali kisa hiki kinatufundisha kuwa inafaa kwa mzazi kumwambia kijana mcha Mungu kuwa amuoe binti wake, wala hapana aibu juu ya mzazi wa binti kufanya hivyo kwa binti wake kwani kijana mwema na mchaji Mungu atamchunga binti huyo na kumhifadhi na mambo ya haramu na mambo mabaya. Na tunaona vile vile Hikma ya Mzee Shu‘ayb, katika kurahisisha ndoa ya mtoto wake. Nabii Mussa alitoka Misri bila mali yoyote, wala asingeweza kulipa mahari lakini Mzee Shu‘ayb akamfanyia Nabii Mussa utaratibu ambao Nabii Mussa kama mgeni katika mji ule angeweza kuoa nao ni kumuajiri. Na hapa kuna dalili kuwa mahari yanafaa kuwa huduma na si lazima yawe fedha au dhahabu tu. Katika kitambo cha Nabii Mussa kufanya kazi kwa Mzee Shu‘ayb palipatikana manufaa kwa pande zote mbili, matatizo ya wale mabinti wawili yaliondoka upesi baada ya baba yao kuafikishwa na Allah kufanyia kazi ombi na ushauri wa mmoja wa binti zake wale wawili wa kutaka Nabii Mussa aajiririwe ili awe akifanya kazi ile badala yao, na Allah kumuwafikisha Mzee Shu‘ayb kumuozesha Nabii Mussa mmoja wa wale binti zake wawili kwa mahari ambayo yalikuwa ni ujira wa kazi aliyokubaliana na Nabii Mussa aifanye. Allah aliwatosheleza mabinti wale wawili kufanya kazi nje ya nyumba yao na baba yao akapumua kutokana na wasiwasi wa kutoka kwao kila mara kwenda kulisha na kunywesha wanyama wao. Vile vile Nabii Mussa alipata kazi tukufu, makazi,  na Allah akamruzuku mmoja wa mabinti wawili kuwa mke.

 

Katika kisa hichi tunajifundisha pia kuwa inapasa kuepuka vitu vinavyochochea Shaka na Shubha. Utaona kuwa mwananamke yule alimwambia Nabii Mussa kuwa baba yake ndiye anayemuita na wala si yeye ndiye aliyekuwa anamuita. Vile vile tunaona kuwa Nabii Mussa alikataa kutembea nyuma au pembeni ya msichana yule kwa kuhofia isije ikatokea upepo ukamfunua au ukawa ndio sababu ya yeye kuona umbile lake au uchi wake. Ni wazi kuwa Shari’ah ya nyumati zilizotangulia ni Shari’ah yetu maadamu haijaja katika sheria yetu kinachopingana nayo au kuifuta Shari’ah hiyo. Kwa mantiki hii basi mipaka hii ya kazi na kutoka nje kwa wanawake iliyoonyeshwa katika kisa cha Nabii Mussa na Mzee Shu‘ayb inawahusu Waislamu pia au Ummah huu hadi siku ya Qiyama kwani kila ujumbe wa mbinguni sifa yake kuu ni moja ambayo ni Kumpwekesha Allah na kuwalea watu katika Tabia njema.

 

Katika kukokoteza hilo Sunnah na Sira ya watoto na wake wa Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama na tarjama za wanawake wa kiswahaba na wakitaabiina vimeweka wazi mipaka ya mwanamke kufanya kazi. Hapa tutatosheka na mifano michache.

 

Mfano wa kwanza: Huu unaenda kwa Bi Khadija mke wa Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama. Tunakuta kuwa Bi Khadija alimwajiri Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama alipokuwa kijana kutokana na sifa ya ukweli na uaminfu wake ili amfanyie biashara yake. Akamtuma kwenda katika mji wa Shamu katika msafara wa kibiashara pamoja naye kijana wake aliyekuwa akiitwa Maysara kama inavyojulikana katika Sira. Hapa kuna funzo kubwa kwa wanawake wanaofanya kazi au biashara nalo ni kuwa hakuna ruksa ya kukaa faragha na wanaumme wanaomfanyia kazi wala hairuhusiwi kusafiri nao kwa hoja ya kazi. Angalia Bi Khadija alimtuma Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama pamoja na kijana wake Maysara wala hakuchukua fursa ile ili asafiri naye na aweze kubadlishana mazungumzo kwa hoja ya kuwa eti wanafanya biashara. Wala Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama akiwa bado hajapewa Utume na akiwa bado hajamuoa Khadija hakuwahi kukaa naye Faragha hata siku moja hadi pale rafiki yake wa kike wa Khadija alipomwambia Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama kuwa amuoe Khadija naye Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama akakkubali na uchumba ukafanyika ukifuatiwa na ndoa na hapo ndipo Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama akakaa faragha na Khadija.

 

Mfano wa pili: Mfano huu unaenda katika kile anachokisimulia Imamu Bukhaar Rahimahu Llaahu katika mlango aliouita “Kufanya kazi mwanamke katika nyumba ya mume wake”.  Katika mlango huo ameleta hadithi, Imamu ‘Aliy Radhiya Llaahu ‘Anhu anasimulia namna mkewe Faatwimah Radhiya Llaahu ‘Anhaa alivyokuwa akipata tabu na kuchoshwa na kazi za nyumbani kwake. Jiwe la kusagia nafaka lilikuwa likiiumiza mno mikono yake na hadi mara nyingine kumchubua na kuvifanya kuwa vigumu vidole vyake. Hadi ilifikia wakati akamuomba baba yake yaani Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama amtafutie mfanyakazi au mtumishi wa kufanya kazi hiyo. Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama akamwambia mwanawe Faatwimah: “Hivi nisikujulishe jambo lililobora zaidi ya huyo mfanyakazi unayemtaka? Msabbihi Allah wakati wa kulala mara thelathini na tatu (33), na Umuhimidi mara thelathini na tatu (33), na Umkabbir mara thelathini na nne (34)”. Ushahidi hapa ni kuwa Faatwimah alikuwa akifanya mwenyewe shughuli za nyumbani kwake. Imepokewa katika vitabu vya Tarjama kuwa Imamu ‘Aliy Radhiya Llaahu ‘Anhu alikubaliana na mke wake Bi Faatwimah Radhiya Llaahu ‘Anhaa kuwa mkewe Faatwimah awe akifanya kazi za ndani ya nyumba na mumewe ‘Aliy Radhiya Llaahu ‘Anhu awe akitoka kufanya kazi za nje. Na hii ndiyo asili na njia nzuri ya kudumisha maisha ya ndoa na malezi bora kwa watoto. Kwa hakika kuwalea vijana mashababu wawili ambao ni alama na nyota katika Ummah huu yaani Hassan na Hussayn ni zaidi ya kutafuta chakula, mavazi na malazi.

 

Vile vile amepokea Imamu Bukhaar Rahimahu Llaahu hadithi muhimu sana katika mlango wa “Wivu” ambayo inakusanya mambo muhimu katika durusu au masomo na Hikma zikibaini mipaka ya kutoka mwanamke kwenda kufanya kazi au kwa ajili ya dharura nyingine. Anatusimulia Imamu Bukhaari Rahimahu Llaahu kisa kilichomtokea Asmaa Binti Abii Bakr Allah Amuwie Radhi yeye na baba yake. Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa alikuwa mke wa Zubayir Ibnul ‘Awaam Radhiya Llaahu ‘Anhu. Alihama kutoka Makkah ili aishi na mume wake Madina. Hawakuwa na mali yoyote isipokuwa ngamia mmoja ambaye walikuwa wakimtumia kubeba maji kutoka katika kisima kilichokuwa mbali kidogo na kuyaleta nyumbani na farasi mmoja ambaye Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu alikuwa akimtumia kwa ajili ya kupigania vita na  Mtume Llaahu ‘Alayhi Wasallama na kwa ajili ya safari. Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu alikuwa akienda kufanya kazi nje kutafuta Rizki na Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa akibaki nyumbani kufanya kazi za nyumbani ikiwemo kumlisha farasi. Kutokana na hali yao nguvu ya maisha Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa alilazimika kutoka na kutembea takriban kilomita tatu hivi kwenda katika kipande cha ardhi alichokuwa amepewa Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu na Mtume Llaahu ‘Alayhi Wasallama. Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa alikuwa akienda shambani huko ili kuokota kokwa za tende ili aje azisake na kumlisha farasi wao. Siku moja Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa akiwa amebeba kokwa za tende akirudi nyumbani alikutana na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama akiwa pamoja na baadhi ya Swahaba zake Radhiya Llaahu ‘Anhum. Hapo Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama akamuinamisha chini ngamia wake ili Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa aweze kupanda nyuma yake. Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama alifanya hivi kutokana na kumuonea huruma shemeji yake kutokana na uzito wa kokwa alizokuwa amebeba. Lakini Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa aliona haya na akakumbuka wivu wa mumewe Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu. Kwa kwa maneno aya Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa ni kuwa mumewe Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu alikuwa ni mtu mwenye wivu sana. Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama kwa akili yake ya hali ya juu alilijua hilo, akaondoka na kumuacha na jambo lake pasina kumsemesha chochote.  Na alipokuja Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa alimsimulia kilichotokea na kuwa alikataa kupanda na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama kutokana na kujiweka mbali na vitu ambavyo vinaweza kuchochea wivu wa mumewe. Hapo Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu akamwambia mkewe Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa: “Wallahi kubeba kwako kokwa za tende kulikuwa kuzito kwangu kuliko kupanda kwako na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama” Asmaa aliongeza kuwa baba yake Abuu Bakr Radhiya Llaahu ‘Anhu alimtumia mfanyakazi kwa ajili ya kumchunga na kumlisha farasi yule na hivyo kumpumzisha Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa na kazi ile. Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa anaelezea kuwa ni kama alikuwa ameachwa huru akimaanisha kuwa mfanya kazi yule alimpumzisha na kazi nzito ambazo alijiona ni kama mtumwa nje ya nyumba.  Katika kisa hichi tunaweza kwa ufupi tukabaini mipaka ya kazi ya mwanamke bali kutoka kwake nje ya nyumba yake kwa dharura yoyote ile kama ifuatavyo:

 

1.   Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa hakutoka kwenda kutafuta kokwa za tende katika ardhi ya mbali takribani kilometa tatu isipokuwa ni kwa kuwa Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu hakuwepo, wala hakukuwa na njia kwa Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa ya kuikwepa kazi ile ya kumlisha farasi kokwa zile ambazo alikuwa anazileta kutoka mbali. Vile vile utaona kuwa Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa hakutumia zaidi ya muda wa lazima kwa kazi ile. Jingine hapa ni kuwa Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa kama mtoto wa Abuu Bakr Swiddiki Radhiya Llaahu ‘Anhu alikuwa akitoka kuiendea kazi ile kwa heshima na adabu na katika hali ya kuwa amevaa hijabu yake kamili na kujisitiri kama Shari’ah ya Kiislamu inavyoamrisha.

 

2.   Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa hakuzungumza na mwanamume yeyote miongoni mwa wale Maswahaba waliokuwa na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama, wala hakuna Swahaba yeyote aliyezungumza naye miongoni mwa wale Swahaba, bali hakuzungumza hata na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama ambaye ni Ma‘asuum na yuko juu ya mstari wa Shubha, tena Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama ni shemeji yake kwani ni  mume wa dada yake ‘Aishah Radhiya Llaahu ‘Anhaa. Pamoja na haya yote aliona haya kama hadithi inavyotuonyesha maana katika hadithi hiyo Asmaa anasema: “Nikajisikia haya kutembea nyuma ya wanaume”, kama alivyoheshimu Asmaa hisia za mumewe, ambaye alikuwa hayuko kwa kuleta hisia za kuwepo kwake, lau kama angekuwepo ingekuwaje. Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhu ni mtoto wa  Swafiyya Radhiya Llaahu ‘Anhaa ambaye alikuwa ni shangazi wa Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama na miongoni wa watu wa mwanzo kabisa kuingia katika Uislamu, na mmoja kati aya watu kumi waliobashiriwa pepo na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama. Swahaba kama huyu si rahisi hata mara moja awe na shaka na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama, Mtume ambaye Allah kamsifu kuwa ana tabia nzuri na iliyotukuka kabisa. Katika hadithi iliyoko katika sahihul Bukhaar mlango wa “Wivu” ‘Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu alimwambia Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama nitaonaje wivu juu yako ewe Mtume hali ya kuwa wewe ni mchaji Mungu na mwanadamu uliyetwaharika na mwanadamu uliye mkubwa sana?

 

3.   Japo Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama ni Ma‘asumu naye ni kama baba kwa Ummah huu na hivyo kila mwanamke ni kama maharimu wake kwa muktadha huu, lakini anatufundisha kuwaheshimu wanawake na hasa wale ambao shida zimewalazimu kutoka na kwenda kufanya kazi au kutibiwa, na hilo si kisingizio cha wao kuchanganyika na wanaume. Bali inayopasa ni kuwaacha wanawake katika hali yao na wala si kama tunavyoona katika masiku haya ambayo kuna matani mengi, kuzungumza sana kati ya wanawake na wanaume wasiokuwa maharimu wanaofanya kazi. Ndipo utaona kuwa Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama alimwacha Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa aendelee na jambo lake pasina kumsemesha na kwa kuchunga wivu wa mume wake na akakiri kwa hilo kanuni ya udharura wa wote kuheshimu hisia zake.

 

4.   Abuu Bakr Radhiya Llaahu ‘Anhu kwa nafasi yake anatufundisha somo muhimu hapa nalo ni kuwa pindi aliposikia kilio cha binti wake alimpelekea mfanya kazi kwa ajili ya kumchunga na kumpa chakula farasi. Na hili linaweka wazi jukumu linalohitajika kwa kila mas’uulu wa mambo awe ni baba, mume au hakimu, katika kuwalea wanawake na kuwaondelea kazi nzito zenye kuwataabisha nje ya nyumba zao na kuwasaidia wafaniklishe lile ambalo ni muhimu zaidi kwao nalo ni kulea na kuwakuza watoto malezi na makuzi bora na kuwashughulikia waume zao vizuri, na kushughulikia mambo ya nyumba kwa ujumla. Ni kwa msingi wa Tabia njema na Akhlaq kama hizi Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa aliwalea mafahali wawili katika Uislamu nao ni Khalifa shujaa ‘Abdillah Ibn Zubayir na Musomi mkubwa ‘Uruwatu Ibn Zubayir Radhiya Llaahu ‘Anhumaa.

 

5.   Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa anatufundisha kuwa pamoja na kujiheshimu na kuepuka kuchanganyika na wanaume, wanawake wa Kiislamu wakubali kufanya kazi za nyumbani pale inapotokea kuwa kuna wanaume wa kufanya kazi kwa niaba yao. Kwa hiyo kufanya kwake kazi Asmaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa nje ya nyumba ni kutokana na dharura ya kukosekana wa kufanya kazi hiyo. Lakini pale Allah alipoleta faraja hiyo ya Asmaa kuletewa mfanya kazi na baba yake alifurahi sana hadi akakizingatia kitendo kile cha baba yake kumletea mfanya kazi kama neema ya kuachwa huru.

 

Kwa ufupi tunaweza kusema baada ya yote hayo kuwa inafaa kwa mwanamke kutoka na kwenda kufanya kazi nje ya nyumba yake katika hali ya dharura na kulazimika kwake kufanya hivyo, lakini kwa sharti la kujiheshimu na kusalimika na fitna na kuwa kazi yenyewe iwe ni ya halali Kishari’ah na mwanamke huyo ajiweke mbali na kuchanganyika na wanaume wasiokuwa maharimu wake na kuwa kazi hiyo isiathiri majukumu ya nyumba yake, watoto na haki za mume wake.  

 

DHARURA ZA KIJAMII

 

Miongoni mwa sehemu ambazo inafaa wanawake kufanya kazi nje ya nyumba zao ni pamoja na takhasusi au “specializations” maalumu na sehemu za dharura kwao mfano Tiba ya Wanawake, Uzazi au Ukunga, Kutahiri, na Kufundisha Wanawake katika hatua zote za elimu.  Katika historia tukufu ya Uislamu kuna mifano inayoonyesha maeneo ambayo wanawake wanalazimika kufanya kazi hata kama ni nje ya nyumba zao.

 

1.   Eneo la kitabibu: katika eneo hili wanawake walifanya kazi hata wakati wa Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama. Hapa tunamkuta Ummu ‘Atiyyatul Answaariyyatu Radhiya Llaahu ‘Anhaa alikuwa akifanya kazi ya kutahiri na pia kuzalisha wanawake. Kazi hii inaweza ikafananishwa na kazi ya kutibu na kuuguza wanawake katika zama hizi. Rufaidah Al aslamiyyat Radhiya Llaahu ‘Anhaa alikuwa akishughulika na kutibu majeraha na huduma ya kwanza. Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama alimruhusu kutengeneza hema ndani ya msikiti wa Mtume Madina. Akawa akipelekewa wagonjwa katika nyakati za dharura mfano katika vita vya Ahzaabu au Khandaq na akiwapa huduma ya kwanza. Jambo la wazi ni kuwa hakukuwa katika mji wa Madina na wanaume waliokuwa wana takhasusi au ujuzi huu kwani lau kama wangekuwepo basi Mtume angeliwataka wamtibu Saad Bin Mua’adh Radhiya Llaahu ‘Anhu alipojeruhiwa siku ya Uhud, lakini tunakuta Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama katika hali ya dharura aliamrisha Saad Radhiya Llaahu ‘Anhu apelekwe akatibiwe na bi Rufaida Radhiya Llaahu ‘Anhaa katika hema lake. Lakini Qadar ya Allah ikashinda juhudi za bi Rufaidah Radhiya Llaahu ‘Anhaa za kutaka kuokoa maisha ya Sa’ad Radhiya Llaahu ‘Anhu. Kwa hakuna ikhitilafu ya wanachuoni kuwa katika udharura wa hali ya kitabibu na uuguzaji wa wanawake wenzao. Hakuna pia ikhitilafu vile vile kwa wanawake kuwafundisha wanawake wenzao katika hatua zote za elimu. Imethibiti kuwa Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama alimwamrisha Shaffaa bint ‘Abdillah Radhiya Llaahu ‘Anhaa kumfundisha Ruq’ya kama alivyoeleza Ibn Sa’ad Rahimahu Llaahu na kuboresha hati kama walivyotaja wengine. Hii ni dalili ya kuwa wanawake wanatakiwa wawatibu wanawake wenzio. Hivyo katika hali ya kuwepo walimu wajuzi wa kike wa kutosha katika kila hatua ya elimu haitakiwi kwa wanaume kuwafundisha wanawake. Mtu ambaye hili halimfurahishi basi na arejee ripoti za wataalamu wa elimu Ulaya na Marekani ambao wanataka wanawake na wanaume watenganishwe na wanawake katika hatua zote za masomo kutokana na matatizo mbalimbali yanayojitokeza kwa sababu ya wanawake kuchanganyika na wanaume. Kisha swali ni kuwa; ni kwa nini watu wang’ang’anie wanawake lazima wafundishwe na wanaume hata kama wako wanawake wajuzi na wa kutosha wa kuwafundisha wanawake?

 

2.   Inawezekana kwa wanawake kutoa msaada wa chakula na dawa kwa wanajeshi inapotokea kukosekana wanaume wanaofanya kazi hiyo au kuwa wachache. Imamu Bukhaari Rahimahu Llaahu amepokea hadithi nyingi zikithibitisha kushiriki kwa wanawake katika kazi ya kusaidia kuuguza wanajeshi vitani. Miongoni mwa hadithi hizo ni kuwa ‘Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu alimpa nguo ya thamani sana Ummu Sulayt Radhiya Llaahu ‘Anhaa (mama yake na Abii Saidil Khudriy Allah Amuwie radhi) na akakataa kumpa mke wake Ummu Kulthum Radhiya Llaahu ‘Anhaa (mtoto wa Imamu ‘Alii Radhiya Llaahu ‘Anhu). Akasema Faaruq ‘Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu kuwa Ummu Sulayt Radhiya Llaahu ‘Anhaa anastahiki zaidi, na akatoa sababu ya kufanya hivyo kuwa Ummu Sulayt Radhiya Llaahu ‘Anhaa ni miongoni mwa watu waliombai Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama na alikuwa akitengeneza viroba vya kunywea maji siku ya vita vya Uh’udi. Na amepokea Imamu Bukhaar Rahimahu Llaahu kutoka kwa Rabiu binti Muhawadh Allah amuwie radhi amesema: “Tulikuwa pamoja na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama tukiwanywesha watu maji, na tukitibu majeruhi na tukiwarejesha waliouwawa Madina”. Na amepokea Imamu Bukhaar Rahimahu Llaahu kutoka kwa Anas Allah amuwie Radhi amesema: “Tulipokuwa Uhudi watu walimkimbia Mtume, na kwa hakika nilimuona ‘Aishah binti Abii Bakr na Ummu Sulaym Radhiya Llaahu ‘Anhumaa wakiwa wananyanyua nguo zao, niliona vikuku katika nyayo zao, wakibeba viroba vya maji mingoni mwao, kisha wakimimina maji midomoni mwa majeruhi, kisha wakirudi na kwenda kuvijaza katika kisima kisha wakija navyo na kuwamiminia majeruhi mdomoni”. Hadithi hizi na nyingine ni dalili kuwa mwanamke anaruhusiwa kufanya kazi katika kutoa msaada wa chakula, maji na tiba panapokuwa na haja na dharura ya kufanya hivyo, pindi wanaume wanaposhughulika na vita au katika nyakati za majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi, vimbunga, volkano, mafuriko na kadhaalika.

 

3.   ‘Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu alimwachia usimamizi wa soko la Madina na kudhibiti bei na kuwapiga wafanya biashara walaghai Sshaffaa Radhiya Llaahu ‘Anhaa ambaye alikuwa anaweza kusoma vizuri na kuandika na pia alikuwa anajua vizuri hesabu na alikuwa mkali sana dhidi ya wafanya biashara wenye kuhadaa na kudanganya Waislamu. Alifanikiwa sana kuzuia na kudhibiti kupanda kiholela kwa bei na pia pia katika kufanikisha kupatikana bidhaa ghafi kwa waislamu.

 

4.   Uislamu umesisitiza na kuhimiza kuwalea wajane na masikini ili kuwahifadhi na udhalili na madhila mbalimbali jambo ambalo linaweza kusababisha wao kuingia katika njia mbaya wasipopata msaada katika jamii. Amepokea Imamu Bukhaari na Abuu Dawuud kauli ya Mtume aliopsema: “Mwenye kuwaendea na kuwahudumia au kuwatunza wajane na masikini ni kama mwenye kupigania jihadi katika dini ya Allah, au ni kama yule anayefunga mchana na kusimama usiku akifanya ibada”. Ni ujira gani basi ulio mkubwa kuliko Jihadi na mtu kufanya Ibada siku zote za uhai wake? Amepokea pia Imamu Bukhar Rahimahu Llaahu katika mlango wa “Vita vya Hudaybia” kuwa Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu alitoka na mtumishi wake kwenda sokoni njiani akakutana na mwanamke mmoja ambaye alikuwa bado kijana, akamwambia Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu ewe kiongozi wa Waislamu, mme wangu kafariki, na kaacha watoto wadogo, Wallah sipati hata kwato za mbuzi au mifupa ili niwapikie, wala hawana nafaka wala wala maziwa nami naogopa wasije wakaliwa na fisi na mimi ni mtoto wa Khufaaf Ibn Iymaal Ghifaariy Radhiya Llaahu ‘Anhu ambaye alishiriki vita vya Hudaybiya na Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama. Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu kusikia hivyo akasimama na mwanamke yule pasina kuondoka na akamwambia karibu nasaba ya karibu, kisha akaondoka kwenda kwenye ngamia aliyekuwa na nguvu, akambebesha gunia mbili zilizokuwa zimejaa chakula yaani unga na tende, na vyakula vingine, na akampelekea matumizi na nguo, kisha akamwambia watumie bidhaa zile bila wasiwasi na kuwa Allah atawaletea kheri, kwa maana ya kwamba yeye atawapa chakula na mahitaji mengine kabla chakula kile hakijaisha. Pia kuna kisa kingine mashughuri kuwa ‘Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu alimkuta mwanamke mwanamke mmoja aiyekuwa akiweka maji pasina cha kupika ili awatulize watoto wake waliokuwa na njaa. ‘Umar Radhiya Llaahu ‘Anhu aliamua abebe chakula cha mwanamke yule mgongoni au kichwani mwake. Haya yote yanaonyesha umuhimu na wajibu wa dola kusimamia wajane na Mayatima na Masikini kwa kuwapa mahitaji muhimu ya maisha yao kutoka katika hazina ya Serikali au mfuko maalumu wa Serikali unaohusika na shughuli hii. Basi la kama dola au serikali ingesimamia jukumu hili pasingekuwa na haja ya wanawake hawa wajane na watalikiwa kutoka na kwenda kufanya kazi nje ya nyumba zao. Na kama wana ndugu wa kiume kama baba au kaka au mtoto anayefanya kazi basi anawatosha juu ya suala hili la kutoka kwao kwenda kufanya kazi. 

 

TOFAUTI ZA KIMAUMBILE KATI YA MWANAMKE NA MWANAMUME.  

 

Sio nususu tu peke yake ndizo zinazoonyesha kuwa kuna tofauti kati ya Wanawake na Wanaume bali hata maumbile yaliyo salama, na fikra ya kiakili, na kielimu iliyo salama na utafiti pia. Hebu jaribu kumuuliza kila mwanamke mwenye akili timamu hivi; kipi kilicho bora zaidi kwake; kuwa awe na mtu mwenye kumtunza na kumtimizia haja zake zote na haja za watoto wake, hivyo apate kupumzika kutokana na tabu na shida za kutoka na kwenda kufanya kazi naye ashughulike na kuwalinda, kuwakuza na kuwalea watoto wake ambacho ndiyo kitu cha thamani kabisa anachomiliki au abaki peke yake akitoka na kwenda kupambana kiwendawaziwendazimu katika kutafuta chakula, kinywaji, kivazi na dawa nk, katika mahitaji ya maisha. Jambo ambalo pia litamuweka mbali na watoto wake kwa kitambo kirefu cha mda wake wa siku nzima; jambo ambalo litawaweka watoto na kuwaacha waking’aa ng’aa macho hadi mama yao huyo atakaporudi jioni au usiku, akiwa amechoka sana kiasi kuwa hawezi kufanya kazi yoyote ya ndani na hata kuwahudumia na kuwakumbusha watoto wake majukumu yao. Je hilo ni jambo jema kwake au kukaa na watoto wake na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili. Hivi ni kweli mwanamke anathubutu kuwaacha watoto wake wachafuliwe na mfanyakazi na vyombo vya habari kama Tv ambavyo vinaonyesha mara nyingine habari ambazo zinaathiri tabia ya watoto. Atajibuje mwanamke huyo? Sidhani kama jawabu la mwanamke mwenye akili litakuwa lingine zaidi ya kukataa yote hayo. Bali atakataa hata kutoka tu nje ya nyumba yake na kuwaacha watoto pasina sababu yoyote. Nadhani kuwa hisia zake kama mama haziwezi kutawaliwa na madai ya Umagharibi ya kutaka kujitosheleza mwenyewe na kujihakikishia uhuru wa kila kitu. Kwa kuwa hikma ni kuweka kila kinachostahiki katika pahala pake kinapostahiki, kwa hiyo hikma hii katika sehemu ya kazi inatuambia waziwazi kuwa kazi ya kuchunga, kulea na kuwafundisha watoto ni ya mama. Yeye anaweza zaidi kulea watoto kuliko mwanamume. Na hilo ni kutokana na uwezo wake na sifa za kimaumbile alizoumbiwa na Allah. Mwanamume kimsingi hana sifa hizo na hawezi kufanya shughuli hizo kwa ukamilifu wake kwa kukosa sifa hizo kwani mwanamume kwa kawaida yake ni mgumu na wala si mlaini kama mwanamke na hivyo kazi zake ni za sulubu zenye tabu, zinazohitaji nguvu zaidi kiakili na kimwili. Ama mwanamke yeye maumbile yake ni malaini, yenye sifa ya upole, ambayo ni muafaka kwa watoto wadogo ili wapate kuwa karibu na joto lake na kulala kifuani kwake wakicheza naye kwa utulivu bila wasiwasi wowote. Haya yote hayawezi kupatikana kwa thamani yoyote iwe ni mali au kazi. Wala mtumishi au mfanya kazi hawaezi kuchukua nafasi ya mama katika kulea watoto abdani. Anayestaajabishwa na haya na atuambie basi ni kwa nini Allah amejaalia mimba, kuzaa na kunyonyesha ni katika shughuli na sifa za mwanamke na si kwa mwanamume. Je hayo ni kwa bahati mbaya? Hivi hii haitoshi kuwa ni dalili ya wazi kuwa Allah kamuumba mwanamke kwa ajili ya wadhifa maalumu wenye kutofautiana na wadhifa wa mwanamume? Nataraji jawabu halitakuwa ni marekebisho ya kimwili na upasuaji wa kumlazimisha mwanamume ili aweze kubeba mimba, kuzaa na kunyonyesha ili kuhakiki usawa wa kindoto wa kimagharibi unaodaiwa kati ya mwanamke na mwanamume. Ni kwa nini zaidi ya 70% ya wanawake wanaofanya kazi Marekani wanalazimika kuacha kazi na kutafuta shughuli nyingine? Takwimu zinaonyesha kuwa sababu kubwa kabisa ya wao kufanya hivyo ni kutokana na kubakwa na kudhalilishwa kijinsia na wanaume makazini. Na hili linatokea hata kwa askari wa kike nao hawajasalimika vile vile. Kwa hiyo linatosha kuonyesha wazi utukufu wa nidhamu ya Kiislamu katika kulinda haki za mwanamke ndani ya nyumba na kuwa wanawake wasifanye kazi nje ya nyumba isipokuwa kwa dharura kubwa. Watu wengi hawajui kuwa wasomi wengi wa Kimagharibi sasa hivi wanaona kuwa iliyo bora kwa mwanamke ni kukaa nyumbani akihudumia nyumba na watoto wake. Miongoni mwa wasomi hao ni mwanafalsa mkubwa wa kifaransa August Comte aliyezaliwa January 17 mwaka 1798 na ambaye anadaiwa kuwa mwasisi wa Elimu ya Sosholojia na Saikolojia: “Inapasa maisha ya mwanamke yawe ndani ya nyumba yake, wala asikalifishwe kufanya  kazi za wanaume, kwani hilo linazuia kati yake na kazi zake za kimaumbile, na linaharibu vipaji vyake vya kiasli. Inawapasa wazazi watoe mali katika kuwahudumia wanawake pasina kungojea wao wafanye kazi kama wanavyotoa kuwapa waandishi wa vitabu, washairi na wanafalsafa. Ikiwa watu hawa wanahitaji muda mwingi ili kazi zao ziweze kuleta matunda ni hivyo hivyo pia nao wanawake wanahitaji muda mwingi ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kijamii kama kubeba mimba, kuzaa, kunyonyesha na kulea watoto. Kwa upande mwingine lau kama tungewaruhusu wanawake kwa unyonge wao wafanye kazi nje ya nyumba utaona kuwa bila shaka watakutana na ushindani mkubwa sana na wanaume. Wataishia kupata kazi za kinyonge kabisa ambazo wanaume wanazikimbia na hata malipo yao yatakuwa chini sana. Hivyo watajikuta wakiingia katika umasikini. Na kazi zenyewe hawatapata isipokuwa mabinti wadogo achilia mbali madhara yatakayoikumba jamii yao kutokana na kutoka kwao kwenda kufanya kazi na kughalifu kanuni sahihi za maisha”. Tunaona kuwa mwanafalsafa huyu mkubwa akili na fikra yake ya kimantki imempelekea atafiti na kuona kuwa mfumo wa kifamilia alioweka Allah ni sahihi sana na kuwa kazi ya mwanamke ni ile aliyowekewa na Uislamu nayo ni kazi ya kulea watoto. Kayasema haya japo hakuwa Mwislamu. Na huenda aliyasema haya kwa kuwa hakuwa anafahamu Uislamu unasemaje kuhusiana na kazi za mwanamke. Na hii inatia nguvu zaidi hoja yangu dhidi ya wasiokuwa Waislamu wanaohimiza mwanamke kutoka na kwenda kufanya kazi kwa kuwa maneno hayo yamesemwa na mwanafikra mwenzao. Fikra yake imempeleka pasina yeye kujua katika kukubaliana na Uislamu unavyosema kuhusiana na wanawake kukaa majumbani mwao na wasitoke kwenda kufanya kazi ila ni kwa dharura kubwa sana na kuwa wanaume wana jukumu la kuwatunza na kuwalinda wanawake na kuwahami na kazi za tabu na fitna ya wao kufanya kazi nje ya nyumba zao. Lau msomi huyu angekuwa Mwislamu basi Ulaya nzima ingezizima kwa makelele lakini kwa kuwa ni mtu wao hakuna mbwa aliyeweza kunyanyua mkia achilia mbali mdomo wake ili kumbwekea!!!

 

Antony Lamalaf mtafiti wa Kirusi katika utafiti wake wa tofauti za kimaumbile kati ya mwanamume na mwanamke anakubaliana na dhana kuwa usawa kati ya mwanamke na mwanamume ni jambo muhali. Anasema Antoni Lamalaf: “Inatupasa tusizidanganye nafsi zetu kuwa tunaweza kusimamisha usawa kati ya mwanamke na mwanamue katika maisha ya kivitendo. Sisi tulijitahidi sana kusawazisha kati ya mwanamke na mwanamme katika Umoja wa Kisovieti kiasi hakuna watu duniani waliowahi kujitahidi juu ya jambo hili mfano wetu, na tuliweka sheria ili kuhakikisha hili linafanikiwa lakini kwa hakika hali ya mwanamke katika familia na katika jamii haikubalika sana”.                      

 

Na anasema Alex Crane kuwa: “kuna tofauti kati ya mwanamke na mwanamume katika fikra na maandalizi ya kiakili katika kupokea elimu”

 

Anna Dyma ambaye alikuwa mwakilishi wa mambo ya kijamii Ulaya anasema: “Kushiriki kwa mwanamke katika shughuli za kijamii kunazidi lakini kwa pole pole sana, ulimwengu wa biashara na kazi unadhihirisha tofauti kati ya jinsia hizi mbili kwa sura ya wazi sana, kwani idadi ya wafanya kazi wa kiume katika mashirika inazidi sana idadi ya wafanyakazi wa kike sehemu zote za ulaya”. Anaongeza kwa kusema: “Kuweka sawa kati ya kazi na maisha ya familia inazingatiwa kuwa ni tatizo kubwa kwa wanawake wanaofanya kazi katika mashirika na vile vile tatizo la kushuka kwa ujira wa mwanamke kwa takribani 16% kulinganisha na ujira wa mwanamme.”

 

La kushangaza sana ni kuwa wao walifanya sherehe kubwa Swizilandi kuhusiana na siku ya mwanamke duniani. Miongoni mwa wageni mashuhuri waalikwa katika sherehe hizi alikuwako Baraanida Baarinisa ambaye alitangaza kujiuzulu kazi yake nono katika shirika moja la kimataifa la vinywaji. Ni kazi nono kwa sababu dada huyu alikuwa akipata kwa mwaka kiwango cha dola milioni mbili za kimarekani. Katika kuelezea sababu ya kujiuzulu kwake japo alikuwa anapata kiwango kikubwa kama hicho ambacho ni takribani bilioni mbili na milioni mia sita na arobaini ukilinganisha na shilingi za Tanzania alisema kuwa: “Nimegundua kuwa starehe ya mume na watoto wangu ni bora zaidi kwangu kuliko kazi yangu na kuliko mamilioni ya dola na kuwa katika nyumba yangu ndiyo sehemu pekee ninapopata kupumzika na inarandana sawia na maumbile yangu”   

                         

Hali hii iliendelea Uingereza, ambapo tunakuta vile vile kuwa mtoto wa Habii Niisi ambaye alikuwa mkuu wa tawi la shirika la maji ya gesi duniani alijiuzulu ili azae na na apate nafasi nzuri ya kumlea mtoto wake.

 

La kushangaza zaidi ya hayo ni kuwa mhariri mkuu wa gazeti la Haa ambaye alikuwa maarufu sana kuwatetea wanawake kutoka na kwenda kufanya kazi alipeleka barua yake ya kujiuzulu ili akae nyumbani alee watoto wake.

 

Na akasema mkuu wa gazeti la Tahrirul Mustaqiili Lyda Kisler: “Mimi sijaacha kazi yangu kwa sababu ya watoto wangu kunihitajia mimi zaidi bali mimi kuwahijajia wao zaidi. Nataka kuishi na watoto wangu katika nyumba yetu kwa utulivu”.

 

Hivi ndivyo Allah alivyowafanya wanawake wa Magharibi waisemee haki kwa vinywa vyao na wakawa wanautetea mfumo wa familia uliowekwa na Uislamu bila wao kukusudia au kujua kuwa Uislamu unasemaje juu ya hilo au kuwa na elimu ya Uislamu juu ya hilo.

 

Amesema Samwel Smith ambaye ni mwanafikra mashuhuri wa Uingereza: “Mfumo wa kuwatumikisha wanawake katika viwanda na maabara vyovyote utakavyoongeza katika uzalishaji, kwa hakika madhara yake ni mengi sana na ni ya hatari zaidi kwa kuwa unavunja nguzo ya mhimili wa nyumba na familia”

 

Gazeti la Thought la Uingereza linasema: “Balaa kubwa sana liko katika kutoka mwanamke katika nyumba yake na kwenda kutafuta kazi za wanaume, jambo ambalo linazidisha kuwepo wanawake mbali na familia zao na kukithiri kwa watoto wa nje ya ndoa, kama aibu kubwa na mzigo kwa jamii, na hivyo hivyo kusongamana wanawake na wanaume kutaleta maafa makubwa”

 

Mwisho anasema mwandishi mashuhuri Haa Mass Annaa Rudi katika makala iliyoko ndani ya gazeti la Sittuuna Miil: “Kufanya kazi binti zetu nyumbani ni kheri zaidi na hakuna balaa kama kufanya kwao kazi katika viwanda na maabara. Natamani miji yetu iwe kama miji ya Kiislamu ambapo wanawake wananeemeka kwa usafi, ucha Mungu na maisha ya utulivu wala hawafikwi na madhila kama sisi”

 

MANENO HAYA NA HISIA HIZI ZA WANAWAKE WA ULAYA HAYATAJI UFAFANUZI MAANA YAKO WAZI SANA. NI JUU YAKO KUCHAGUA PAURO AU PAPURO!

 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template