Sheikh Issa Ponda arudishwa rumande - Msamaa.
Headlines News :
Home » » Sheikh Issa Ponda arudishwa rumande

Sheikh Issa Ponda arudishwa rumande

Written By Unknown on Thursday, May 15, 2014 | 1:08 AM

Na Hamida Shariff, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Mei15  2014  saa 24:0 AM

Morogoro. Kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ameendelea kusota rumande baada ya kesi yake kuahirishwa kwa mara nyingine kwa kuwa jalada la kesi yake, halijarudi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam lilikoitishwa kwa ajili ya mapitio.
Kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro mwaka jana, iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Moyo na imekuwa ikitajwa kwa zaidi ya miezi sita, huku Sheikh Ponda akiendelea kusota rumande baada ya kunyimwa dhamana.
Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu ya kutokutoa maneno yenye kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa ambayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10, 2013 jioni katika eneo la Kiwanja cha Ndege, Morogoro.
Jana, Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani akisindikizwa na polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi, huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzio wa Mahakama hiyo kwa sababu za kiusalama.
Mara baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Moyo alisema jalada la kesi hiyo, bado halijarudi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, hivyo kuiahirisha kesi hiyo hadi Mei 26, mwaka huu itakapotajwa tena.
Upande wa mashtaka uliwasilisha ombi mahakamani hapo kutaka Sheikh Ponda kuhojiwa na polisi kuhusiana na mashtaka yanayomkabili. Hakimu Moyo alikubali ombi hilo na kumtaka Sheikh Ponda kuwa na imani na Mahakama hiyo, akisema itatenda haki kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.
 
 Jana, Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani akisindikizwa na polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi, huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzio wa Mahakama hiyo kwa sababu za kiusalama.PICHA|MAKTABA
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template