Dodoma/Dar.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Tundu
Lissu amesema Tanganyika ilikufa kwa amri iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere
na siyo kwa makubaliano katika hati ya Muungano.
Lissu alitoa kauli hiyo jana alipopata fursa ya kukamilisha
dakika 16 za hotuba yake ya ufafanuzi wa maoni ya walio wachache iliyokuwa
imekatishwa baada ya matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni ya Taifa (TBC1)
kukatika Jumamosi iliyopita.
Huku akinukuu maneno yaliyopo katika vitabu vilivyoandikwa na
Profesa Issa Shivji na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, Lissu
alisema Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bila uhalali wa kisheria kwa kuwa
hayakuwapo makubaliano ya kila upande wa Muungano.
Alisema Aprili 26, 1964 (Siku ya Muungano), Mwalimu Nyerere
alitoa amri ya masharti ya mpito ya mwaka 1964 ambayo pamoja na mambo mengine
iliifuta Tanganyika. Akichambua kitabu cha ‘50 Years of Independence: A Concise
Political History of Tanzania’ (Miaka 50 ya Uhuru: Historia fupi ya Tanzania),
kilichoandikwa na Msekwa na kuchapishwa Januari mwaka huu, Lissu alisema:
“Msekwa anasema katika kitabu hicho kuwa amri hiyo ilichapishwa
katika Gazeti la Serikali la siku hiyo. Kwanza, iliwabadilisha waliokuwa
watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.”
Alisema hata Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwa Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano na nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Tanganyika iligeuzwa
kuwa nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.
Alisema tarehe hiyohiyo, Mwalimu Nyerere alitoa amri ya Katiba
ya muda ya mwaka 1964 na ilitangaza kuwa Katiba ya Tanganyika ndiyo iwe Katiba
ya muda ya Jamhuri ya Muungano.
“Kifungu cha nne cha amri hii ndicho kilichoipatia Serikali ya
Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano yote
na vilevile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika,” alisema
Lissu huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo.
Alisema Juni 15, 1964, Mwalimu Nyerere alitoa amri nyingine
iliyoitwa ‘Amri ya Masharti ya Mpito’ ambayo ilieleza kwamba mahali popote
ambako sheria zilizokuwapo zimetaja jina la ‘Tanganyika’ basi jina hilo lifutwe
na badala yake jina la ‘Jamhuri ya Muungano’ liwekwe.
Huku akimnukuu Msekwa, Lissu alisema kigogo huyo wa CCM katika
kitabu chake amesema, “Uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri.
Athari za jumla za amri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndiyo ilikuwa
Tanganyika lilitolewa uhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu hata
jina la eneo la kijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi
libadilishwe na kuwa Tanzania Bara.”
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lissu aliyoitoa
jana, Msekwa alisema: “Kitabu kipo na ukikisoma kwa umakini utagundua kuwa
alichokisema Lissu siyo ambacho kimeandikwa. Sasa umhoji kuhusu hayo
aliyoyasema, muulize ameyapata wapi?”
Kuhusu Shivji
Akimnukuu Profesa Shivji katika kitabu chake ‘Pan Africanism or
Pragmatism? Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union’, Lissu alisema Profesa huyo
ameeleza kuwa Muungano huo ulilazimishwa.
“Profesa Shivji amethibitisha kwamba kile kinachoitwa Sheria ya
Kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964 iliandaliwa na
kuandikwa na maofisa wa sheria wa Tanganyika wakiwa Tanganyika,” alisema.
Alisema kuwa Profesa huyo ameeleza sababu ya ukweli wa kisiasa
uliokuwapo wakati huo ambao Baraza la Mapinduzi kwa jumla wake halikukaa
kuukubali Muungano.
“Profesa Shivji alisema hakuna shaka kwamba Muungano
‘ulilazimishwa.’ Hivyo, maofisa wa kisheria wa kigeni wa Serikali ya Tanganyika
(waliokuwa pia marafiki wa Nyerere) walitumia mbinu ya kisheria ya kuchapisha Sheria
ya kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964,” alisema huku
akikatishwa mara kwa mara na wajumbe waliokuwa wakiomba miongozo ya mwenyekiti.
“Profesa ameeleza kuwa, kwa sababu utaratibu huo ulikiukwa,
kitendo cha kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika
hakikupata baraka za Baraza la Mapinduzi na kuthibitishwa na kikao halali cha
Baraza la Mawaziri la Zanzibar,” alisema Lissu na kuongeza: “Jamhuri ya
Muungano ilizaliwa bila uhalali wowote wa kisheria kwa maneno ya Profesa
Shivji.”
Alisema hata aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu
wa Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Salim Said
Rashid kati ya Januari 18 na Juni 1964, alitamka kuwa:
“Hakuwahi kupokea maagizo kutoka kwa Rais wa Zanzibar kwa ajili
ya kuitisha kikao cha kujadili na kupitisha mkataba wa kuunganisha Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika,” alisema Lissu.
Alisema katika kitabu hicho, Profesa Shivji alieleza jinsi
Rashid alivyoeleza utaratibu wa kisheria uliotakiwa kufuatwa: “... Kwa mujibu
wa amri ya mwaka 1964; kila jambo lilitakiwa kujadiliwa na kikao cha Baraza la
Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu kuarifiwa atayarishe ‘presidential decree’ kwa
mujibu wa utaratibu.”
Alisema baadaye yeye (Rashid), akiwa Katibu wa Baraza la
Mapinduzi na Baraza la Mawaziri Zanzibar alitakiwa asaini na kisha Rais wa
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na baadaye kutolewa katika gazeti la Serikali.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo ya Lissu kuhusu kitabu
chake, Profesa Shivji alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno akisema: “Itakuwa
vizuri ukisoma wewe mwenyewe.”
Mbowe: Takwimu za Tume zimetengenezwa na
vigogo wa Serikali
Akichangia maoni ya walio wachache
kutoka Kamati Namba Nane, Freeman Mbowe alisema kitendo cha wajumbe wanaotokana
na CCM kubeza takwimu za Tume ya Jaji Joseph Warioba ni kuwakana Watumishi wa
Serikali akisema ilikuwa na watumishi wa Serikali 190 wakiwamo wanasheria
waandamizi.
Akimnukuu Profesa Shivji katika kitabu chake ‘Pan Africanism or
Pragmatism? Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union’, Lissu alisema Profesa huyo
ameeleza kuwa Muungano huo ulilazimishwa.
“Profesa Shivji amethibitisha kwamba kile kinachoitwa Sheria ya
Kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964 iliandaliwa na
kuandikwa na maofisa wa sheria wa Tanganyika wakiwa Tanganyika,” alisema.
Alisema kuwa Profesa huyo ameeleza sababu ya ukweli wa kisiasa
uliokuwapo wakati huo ambao Baraza la Mapinduzi kwa jumla wake halikukaa
kuukubali Muungano.
“Profesa Shivji alisema hakuna shaka kwamba Muungano
‘ulilazimishwa.’ Hivyo, maofisa wa kisheria wa kigeni wa Serikali ya Tanganyika
(waliokuwa pia marafiki wa Nyerere) walitumia mbinu ya kisheria ya kuchapisha
Sheria ya kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964,” alisema
huku akikatishwa mara kwa mara na wajumbe waliokuwa wakiomba miongozo ya
mwenyekiti.
“Profesa ameeleza kuwa, kwa sababu utaratibu huo ulikiukwa,
kitendo cha kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika
hakikupata baraka za Baraza la Mapinduzi na kuthibitishwa na kikao halali cha
Baraza la Mawaziri la Zanzibar,” alisema Lissu na kuongeza: “Jamhuri ya
Muungano ilizaliwa bila uhalali wowote wa kisheria kwa maneno ya Profesa
Shivji.”
Alisema hata aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu wa
Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Salim Said
Rashid kati ya Januari 18 na Juni 1964, alitamka kuwa:
“Hakuwahi kupokea maagizo kutoka kwa Rais wa Zanzibar kwa ajili
ya kuitisha kikao cha kujadili na kupitisha mkataba wa kuunganisha Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika,” alisema Lissu.
Alisema katika kitabu hicho, Profesa Shivji alieleza jinsi
Rashid alivyoeleza utaratibu wa kisheria uliotakiwa kufuatwa: “... Kwa mujibu
wa amri ya mwaka 1964; kila jambo lilitakiwa kujadiliwa na kikao cha Baraza la
Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu kuarifiwa atayarishe ‘presidential decree’ kwa
mujibu wa utaratibu.”
Alisema baadaye yeye (Rashid), akiwa Katibu wa Baraza la
Mapinduzi na Baraza la Mawaziri Zanzibar alitakiwa asaini na kisha Rais wa
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na baadaye kutolewa katika gazeti la Serikali.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo ya Lissu kuhusu kitabu
chake, Profesa Shivji alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno akisema: “Itakuwa
vizuri ukisoma wewe mwenyewe.”
Mbowe: Takwimu za Tume zimetengenezwa na
vigogo wa Serikali
Akichangia maoni ya walio wachache
kutoka Kamati Namba Nane, Freeman Mbowe alisema kitendo cha wajumbe wanaotokana
na CCM kubeza takwimu za Tume ya Jaji Joseph Warioba ni kuwakana Watumishi wa
Serikali akisema ilikuwa na watumishi wa Serikali 190 wakiwamo wanasheria
waandamizi.
“Tunapohukumu Tume imefanya kazi chafu
ya kuchakachua takwimu hizi, mjue zimetengenezwa na watumishi waandamizi kutoka
Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Kwa hiyo wanaobeza taarifa ya
Tume, wajue wanaikana Serikali, wanawakana watu ambao wana dhamana ya kusimamia
nchi hii,” alisema na kuongeza:
“Tunapata wapi ujasiri wa kuwadhalilisha
wajumbe wa Tume ya Rais iliyoongozwa na Warioba?... Tume iliyojaa viongozi
walioitumikia nchi hii kwa uaminifu mkubwa, tunafanyaje jambo hili?”
Mbowe alisema Jaji Warioba aliwahi
kushika nyadhifa mbalimbali za juu ikiwamo Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa
Rais na kuhoji wajumbe wanapataje ujasiri wa kuwadhalilisha. Aliwataja wajumbe
wengine wa tume hiyo wanaoheshimika kuwa ni pamoja na Jaji Mkuu mstaafu,
Agustino Ramadhan na Waziri Mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim.
Mbowe pia alishangaa kiwango cha fedha
kilichotumiwa na tume hiyo Sh68.88 bilioni kufanya utafiti ambao leo wajumbe
walio wengi kutoka CCM wanaukana.
Alisema endapo wajumbe wanapuuza msingi
wa Rasimu iliyotokana na Tume ya Jaji Warioba, ni vyema Bunge hilo lisiwepo ili
CCM wakae upya na kutengeneza rasimu wanayoitaka ya serikali mbili. Alisema
Tanzania haiwezi kupata Katiba Mpya kwa uongo na rushwa na kuzuia watu kujadili
kasoro za muungano kwa uhalisia wake.
Jussa awabana mawaziri SMZ
Akitoa ufafanuzi kuhusu maoni ya wajumbe
walio wachache wa Kamati Namba Sita, Ismail Jussa aliwabana mawaziri watatu wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kwa kushindwa kueleza udhaifu wa muundo
wa serikali mbili bungeni wakati kwenye semina ya Baraza la Wawakilishi kuhusu
mchakato wa katiba walisema hivyo wazi.
Alisema mawaziri hao walilalamikia jinsi wanavyodhalilishwa na
muundo wa serikali mbili wanapokwenda nje ya nchi.
“Kuna rekodi hata ya CD, siyo ya Hansard tu (kumbukumbu rasmi za
Bunge), hata ukiitaka mheshimiwa mwenyekiti nitakupatia. Haya yalikuwa katika
semina ya Baraza la Wawakilishi iliyoitishwa na Spika wetu, Mzee Pandu Ameir
Kificho,” alisema.
Aliwataja mawaziri hao kuwa ni Dk Mwinyi Haji Makame, Haroun
Ally Seleman na Omary Yusuf Mzee. “Walichofanywa Dodoma sijui mheshimiwa
mwenyekiti, lakini wote pamoja na wengine walionyesha jinsi mfumo huu (serikali
mbili) hautusaidii Zanzibar na umetukwamisha,” alisema.
Alitoa mfano mwingine kuwa kuna siku Zanzibar walikuwa
wakijadili muswada wa utalii ambapo yeye alipendekeza waweke kipaumbele cha
ajira kwa Wazanzibari kwa kuwa wizara hiyo si ya Muungano na kilikataliwa.
“Mimi na Asha Bakari tu wa CCM tulitoka nje na akalalamika kuwa
wenzake wamemgeuka. Kwa tabia hii mheshimiwa mwenyekiti tunapokuwa Zanzibar,
tunasema wengine tunapokuja Dodoma tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu,”
alisema.
Awali akisoma maoni ya walio wengi, Mwenyekiti wa Kamati Namba
Sita, Stephen Wassira alisema walio wengi walipendekeza muundo wa serikali
mbili kwa sababu unatoa fursa kubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa pande
zote mbili na kuondoa tabaka la ukabila na udini ndani ya Jamhuri.
“Mfumo wa serikali mbili ukifanyiwa marekebisho ya kikatiba
utaondoa kero na manung’uniko ambayo yameelezwa kuwa msingi wa mapendekezo ya
Tume ya kutaka mfumo wa serikali tatu,” alisema.
CHANZO:
Na Fidelis Butahe na
Daniel Mjema, Mwananchi [Posted Jumanne,Aprili15 2014 saa
24:0 AM]
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !