JINSI YA
KUMFURAHISHA MKEO
Namna ya
kumfurahisha Mkeo (How to make your wife happy) na Sheikh
Muhammad Abdul
Haliym Haamid.
1. Mapokezi
Mazuri. Baada ya kurudi kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale alipowatenganisheni:
· Anza kwa maamkizi mazuri
· Anza kwa Assalaamu 'Alaykum na
tabasamu.
Salaam ni
Sunnah na ni duaa kwake (mkeo) pia.
· Mpe mkono na ziache habari mbaya mpaka
baadae
2. Maneno mazuri na makaribisho ya kufurahisha
· Chagua maneno mema na jiepushe na
maneno mabaya.
· Shughulika nae unaposema au anaposema
yeye
· Sema kwa ufasaha na rejea maneno
inapohitajika mpaka afahamu/aelewe.
· Mwite kwa majina mazuri anayoyapenda,
mfano, Mpenzi wangu, honey (asali,
tamtam), (habibty), swaaliha
(mwanamke mwema), n.k
3. Urafiki na
maliwazo
· Tumia muda kuzungumza nae
· Mfikishie habari njema
· Kumbuka kumbukumbu zenu
nzuri za kuwa pamoja
4. Michezo na burudani
· Mfanyie mzaha na jiweke katika hali ya
furaha
· Chezeni na mshindane katika michezo na
mambo mengine
· Mchukue kuangalia aina za burudani
zilizo halali.
· Jiepushe na mambo ya haram katika
kuchagua aina ya burudani.
5. Msaada katika
kazi za nyumbani
· Fanya kile ambayo wewe mwenyewe
unaweza/unapenda kukifanya ili kumsaidia, hasa
anapokuwa mgonjwa au amechoka.
· La muhimu kuliko yote ni kumuonyesha
wazi kuwa unathamini unashukuru jitihada
zake katika kazi.
6. Kushauriana
(Shuura)
· Hususan katika masuala ya
familia
· Kumpa hisia kuwa maoni yake ni muhimu
kwako.
· Kuyazingatia maoni yake kwa makini
· Kuwa tayari kubadilisha maoni yako kwa
yake yeye iwapo yatakuwa ni bora zaidi.
· Mpe shukurani kwa msaada wake wa maoni.
7. Kutembelea wengine
· Chagua watu wenye malezi mema wa
kufanya mahusiano nao. Kuna
malipo makubwa
katika kuwatembelea jamaa na watu wacha Mungu. (Sio
kuwatembelea kwa
kupoteza wakati)
· Kuwa muangalifu kuhakikisha tabia za
Kiislamu wakati
mnapowatembelea
watu.
· Usimlazimishe kuwatembelea wale ambao
yeye hajisikii raha
kuwa nao.
8. Muongozo wakati wa kusafiri
· Muage vizuri na kumpa ushauri mwema
· Mtake akuombee dua
· Watake jamaa wacha Mungu na marafiki
kuiangalia familia
wakati wa kutokuwepo kwako.
· Mpe pesa za kutosha kwa mahitaji
anayoweza kuhitajia
· Jaribu kuwa na mawasiliano nae ama kwa
simu, e-mail (barua
pepe), barua, n.k.
· Rejea haraka iwezekanavyo.
· Mchukulie zawadi
· Jiepushe na kurejea nyakati
zisizotarajiwa au nyakati za
usiku.
· Mchukue (safarini) ikiwezekana.
9. Msaada wa
Kifedha
· Unatakiwa kuwa mtumizi kwa mujibu wa
uwezo wake wa kifedha.
Usiwe bahili na pesa zake (wala usiwe
mfujaji).
· Unapata malipo kwa matumizi yote
unayotumia kwa ajili ya
kumkimu (mkeo) hata kwa kipande kidogo cha
mkate ambacho unamlisha kwa mkono wako
(hadiyth).
· Unahimizwa sana kumpa kabla yeye
hajakuomba.
10. Kunukia vizuri na Kujipamba mwili
· Kufuata Sunnah ya kunyoa nywele za utupuni na kwapani.
· Daima uwe msafi na nadhifu.
· Jitie manukato kwa ajili yake (mkeo)
11. Jimai (Tendo la ndoa)
· Unawajibika kulifanya mara kwa mara
iwapo huna dharura (ugonjwa, n.k)
· Uanze kwa "Bismillah" na dua
zilizo sahihi.
· Umuingilie katika sehemu iliyo sahihi
tu (sio sehemu ya nyuma)
· Uanze kwa vitangulizi (vya jimai) ikiwa
ni pamoja na maneno ya mapenzi.
· Uendelee mpaka umtosheleze hamu yake.
· Mpumzike na mfanyiane mzaha mnapomaliza
· Epukana na jimai wakati wa damu ya
mwezi kwa sababu kufanya hivyo ni haram
· Fanya chochote unachoweza kuepuka
kuharibu kiwango chake cha haya alicho
nacho (haya na staha) mfano kuvua nguo pamoja
badili ya kumtaka avue yeye mwanzo huku
ukiwa unamuangalia.
· Epuka wakati wa jimai mkao ambao unaweza
kumuumiza mfano kumgandamiza katika kifua
inayopelekea kumzuilia pumzi, hususan iwapo wewe ni mzito.
· Chagua muda muwafaka kwa jimai na uwe
unamjali kwani wakati mwengine anaweza kuwa ni mgonjwa au amechoka.
12. Kudhibiti Siri
· Jiepushe na kutoa habari za siri mfano wa
siri za chumbani, matatizo yake binafsi na masuala mengine ya kibinafsi.
13. Kumuongoza katika Kumtii Allaah
· Muamshe katika sehemu ya tatu ya mwisho
ya usiku kusali "Qiyaam-ul-Layl" (sala
za
ziada za usiku zenye sujuud na ruku'u za muda mrefu).
· Mfundishe kile unachokijua katika
Qur'an na tafsiri zake.
· Mfundishe "Dhikr" (njia za
kumtaja Allaah kama alivyofundisha Mtume) za
asubuhi na jioni.
· Muhimize kutumia pesa kwa ajili ya
Allah (S.W.T.) kama vile kutoa sadaka.
· Mchukue katika safari ya Hijja na Umrah
wakati unapokuwa na uwezo.
14.
Kuonyesha Heshima kwa familia yake na marafiki zake
· Mchukue katika matembezi kwa familia na
jamaa,hususan wazazi wake
· Waalike kumtembelea na wakaribishe.
· Wapatie zawadi kunapokuwa na jambo
maalum (kama sikukuu).
· Wasaidie wanapokuwa na haja kwa msaada
wa fedha, nguvu, n.k.
· Endeleza
uhusiano mzuri na familia yake baada ya kifo chake iwapo atakufa mwanzo. Pia
kwa hali kama hii mume anahimizwa kufuata Sunnah na kutoa kile ambacho yeye
(mke) alizoea kutoa wakati wa uhai wake kuwapa rafiki ya jamaa zake.
15. Mafunzo ya Kiislam na Kumshauri kwa kumrekebisha
· Misingi ya Uislam
·
Haki na wajibu wake
· Kusoma na kuandika
· Kumhimiza kuhudhuria darsa na halaqah
(darsa duara za msikitini na majumbani)
· Hukumu za Kiislam zinazowahusu wanawake
· Kumnunulia vitabu vya Kiislam na kaseti
kwa ajili ya maktaba ya nyumbani.
16. Wivu unaokubalika
· Hakikisha kuwa anavaa hijaab kamili
anapotoka nyumbani.
· Usimruhusu kuchanganyika ovyo na
wanaume wasio- mahram
· Jiepushe na wivu uliozidi mno. Mfano
wake ni kama:
1. Kulichambua kila
neno na sentensi asemayo na kuyajaza maneno yake kwa maana ambazo
hakuzikusudia.
2.
Kumzuia kutoka nje ya nyumba hata kama kuna sababu zinazokubalika.
3.
Kumzuilia kujibu simu, n.k.
17. Subira na Upole
· Matatizo yanatarajiwa katika kila ndoa kwa
hivyo hili ni jambo la kawaida, Lililo kosa ni majibizano ya kupindukia na
kuyakuza matatizo mpaka yakapelekea kuvunjika kwa ndoa.
· Hasira lazima zionyeshwe pale anapochupa
mipaka ya Allaah (S.W.T.), kwa kuchelewesha Sala, kusengenya, kuangalia
yasiyofaa katika TV, n.k.
· Kumsamehe makosa anayokukosea wewe
(Angalia sehemu ya 18).
· Ni namna gani unaweza kumrekebisha
makosa yake?
1- Kwanza, mpe ushauri kwa njia
ya mzunguko na ya moja kwa moja mara kwa mara.
2-
Kisha kwa kumpa mgongo katika kitanda (kumuonyesha hisia zako).Tanabahi
kuwa hii haihusishi kuhamia chumba kingine, kuhamia nyumba nyingine, au kutomsemesha.
3-
Utatuzi wa mwisho ni kumpiga
kidogo (kwa namna ilivyoruhusiwa) Katika hali hii, mume ni lazima aangalie
yafuatayo:
- Ni lazima ujue kuwa Sunnah ni kuepuka
kumpiga kwani Mtume (S.A.W.) hakuwahi
kumpiga mwanamke wala mtumwa.
- Ni
lazima ufanye hivyo katika hali ya juu kabisa ya kutotii, mfano mara kwa mara
kukataa tendo la jimai bila ya sababu, mara kwa mara kutosali kwa wakati wake,
kuondoka nyumbani kwa muda mrefu bila ya ruhusa na kukataa kusema pahala
alipokuwepo, n.k
- Usifanye hivyo mpaka awe umeshampa mgomo
na kulijadili hilo suala pamoja nae ama ilivyoelezwa katika Qur'an.
- Usimpige pigo la nguvu la kumuumiza, au
kumpiga usoni au katika sehemu zilizo nyepesi kuathirika katika mwili wake.
- Jiepushe na kumdhalilisha kama kumpiga kwa
kiatu, n.k.
18. Kusamehe na makaripio yanayofaa
· Mhukumu kwa makosa makubwa tu.
· Msamehe
makosa aliyokukosea wewe bali mhukumu kwa makosa ya haki za Allaah, mfano
kuchelewesha Sala, n.k
· Kumbuka mazuri yote anayomfanyia kila
wakati anapofanya makosa.
· Kumbuka kuwa kila mwanaadamu hukosea na
umuwazie dharura mfano huenda
amechoka, ana
huzuni, yumo katika siku zake za mwezi au imani/mafungamano yake
katika Uislam bado
yamo katika kukua.
· Jiepushe na kumgombeza kwa mapishi mabaya kwani Mtume (S.A.W.)
hakuwahi
kumlaumu yeyote
katika wake zake kwa jambo hili. Iwapo amekipenda
chakula, hula na
iwapo hakukupenda hukiwacha na hatoi maoni yoyote.
· Kabla ya kumuwekea wazi kuwa amefanya
makosa, jaribu njia nyingine za mzunguko ambazo ni za hekima kuliko kumlaumu
wazi wazi.
· Epukana na kutumia jeuri au maneno
yanayoumiza hisia zake.
· Inapokuwa kuna ulazima wa kujadili tatizo
subiri mpaka mnapokuwa
faragha.
· Subiri mpaka hasira zipungue kidogo, hii
inasaidia kuweza kudhibiti maneno yako.
NYONGEZA YA AL HIDAAYA:
Mwisho, tafadhali
mumuombee du'aa aliyeandaa haya, Sheikh Muhammad Abdul Haliym Haamid, mfasiri
wa kwa kiingereza Al Akh Abu Talhah na mfasiri wa makala haya kwa kiswahili
Ukht Ummu Ummu Ayman, bila kuwasahau walioyatafuta na kuyachagua AL HIDAAYA
www.alhidaaya.com
Mwinyi I.
Msellem
(Health
Laboratory Scientific Officer)
Zanzibar
Malaria Control Programme
P.O.Box 503
Zanzibar -
Tanzania
Tel +255 24 223 64 51 (Res)
Cell Phone
+255 747 43 29 11 (Mob)
Fax +255 24 223 95 40
E:mail-
mmwinyi@hotmail.com
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !