- Kitoloho
Headlines News :
Home » »

Written By Msamaa on Thursday, May 2, 2013 | 5:29 AM


Mauaji ya Waislam-Mwembechai.
Sehemu ya mazungumo ya Mheshimiwa Kitwana Kondo (MB) mbele ya waandishi wa habari Mei 27, 1998.

JUZI tarehe 21 ya mwezi huu, niliwaambia ya kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, na kiongozi wa CCM,
na nina wajibu mimi wa kufuata maagizo na maelekezo yote ya CCM. Niliwaambia pia ya kwamba nina wajibu
mimi wa kutetea maamuzi ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Lakini nilisema pia kwamba pia nina wajibu wa kuishauri serikali yangu pale ninapoona inafanya makosa.
Wajibu huu mie ninao.

Nililolisema na ninalisema tena leo ni kwamba serikali imekuwa Insensitive kwa mambo yanayowahusu
Waislamu na mambo mengine. Na kwa kuwa serikali inakuwa insensitive Waislamu wanatafsiri ile insensivity
ya serikali kuwa bila shaka serikali haiwapendi.

Siku ile nilitoa mfano wa kuingia Msikitini Polisi wa serikali walikuwa hawana sababu ya kuingia Msikitini.

Lakini lile limetokea na ghasia ambazo serikali yenyewe ili contribute (ilichangia). Kabla ya siku ile polisi
wamekuwa wakiwakamata Masheikh majumbani kwao kimya kimya.

Kama serikali ingekuwa inataka kumkamata Magezi wangeweza kumkamata Magezi nyumbani kwake.

Lakini serikali katika busara zake iliona Magezi imkamate Msikitini baada ya swala ya Alasiri pale mahala
pamejaa watu. Huku ikijua kwamba Magezi ana wafuasi wake.

Kwanini isimkamate Magezi asubuhi nyumbani kwake? Kwanini isimkamate Magezi usiku nyumbani kwake?
Wakaamua kumkamata pale. Kitendo kile ndicho kilicholeta rabsha ya tarehe 12.

Watu walipozidiwa nguvu wakakimbilia ndani ya Msikiti. Msikiti ule una wanawake ambao hawakuwahi
kutoka.

Sasa mimi bado narudia kwamba kama serikali ingetaka ingeweza kuuzingira ule Msikiti wale wangetoka tu. Ni
insensitivity yao ya kusema potelea mbali (kwanza) kwanini wangoje mpaka saa nane za usiku, wakavunja
mlango ambao mpaka leo haujatengenezwa wakaingia ndani. Walishawakatia umeme na nini. Wakavunja
Msikiti wakaingia ndani. Na si hivyo tu, wakawakamata, wakawapiga wale wanawake wakawapiga. Na
wakawamwagia unga ambao unawasha. Mimi nilizungumza na wale wanawake wanaeleza mambo hayo.

Sasa mimi nasema hilo linaonyesha insensivity ya serikali.

Na imefanya kosa kuwashitaki wale Waislamu wa Mwembechai kwa kusema Yesu si Mungu. Au kusema Yesu
si mwana wa Mungu au kusema Yesu hakusulubiwa. Imefanya kosa kubwa kuwashitaki wale. Kwa kusema
maneno ambayo ndiyo anayoyaamini miaka yote. Kila mahali palipo na Uislamu maneno hayo yapo.

Sasa naambiwa habari ya mahakama. Mimi sisemi habari ya mahakama. Nasema habari ya serikali. Mahakama
inapelekewa kesi. Sasa kesi ya kusema Yesu si Mungu haikutoka kwenye mahakama.

Haya yametoka nje, polisi ndio waliomshitaki mtu huyu kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali ambayo haina
dini!

Mwaka 1996 walimamatwa vijana wawili Lushoto. Walikuwa Msikitini wanatoa mawaidha wakasema Yesu si
Mungu. Wakangojewa nje walipokuwa wanakwenda sokoni wakakamatwa. Wakashitakiwa kwa kosa, kwa
kashfa ya dini nyingine. Dini gani nyingine?

Kashfa yenyewe ni nini wamesema Yesu si Mungu. Na hivi juzi juzi, mambo ndio hayo hayo.

Sasa mimi nasema serikali inafanya kosa kubwa, serikali isiyokuwa na dini inafanya kosa kuwashitaki watu
kwa sababu ya imani yao.

Hivi karibuni Muadhama Kadinali Pengo amesema kwenye Kiti Moto ya kwamba kwa Muislamu kusema Yesu
si Mungu si kashfa. Kwasababu ndio imani yake. Na amesema mimi yaani yeye Kadinali Pengo naamini ya
kwamba Mtume Muhammad si Mtume wa mwisho. Hivyo ndivyo imani yangu. Si kashfa kwa dini yoyote.

Si hivyo tu, juzi kwenye gazeti la Dar Leo ... kuna maneno Maaskofu wamuunga mkono K.K. Hawa ni Maaskofu
wa Kanisa la Protestant, na wao wanasema kwa Muislamu kusema Yesu si Mungu si kashfa. Na kwa Mkristo
kusema Yesu Mungu si kashfa.

Haya ni maneno ambayo yamesemwa na Mabishops, sasa ikiwa dini yenyewe inayosemwa ni kashfa ni dini ya
Kikristo, Wakristo wenyewe wanasema si kashfa. Sasa serikali inasema kashfa kwa dini nyingine, dini gani?

Sasa mimi nilichowaomba mnisaidie siku ile ni kuiomba serikali ifute count hii. Serikali kusema lakini kesi iko
mahakamani si kweli. Serikali bado ina uwezo wa kwenda mahakamani na kusema tunafuta count hii.

Kuwashitaki kwasababu wanasema maneno yaliyoko ndani ya Qur’an ndio kusema serikali inaona Qur’an ni
kitabu cha uchochezi.

Unapomshitaki mtu mahakamani kwa uchochezi kwa kusema maneno yaliyo ndani ya Qur’an, lazima useme na
kitabu chenyewe ni kitabu cha uchochezi.

Sasa ninachosema mimi kwa bahati mbaya hawa kina Bwana walioshtakiwa kwa count hii moja wamepata
conviction maana yake, mahakama itakuwa inasema kitabu hiki ni kitabu cha uchochezi.

Swali langu mimi, serikali itaifungia Qur’an? Serikali wataifungia dini ya Kiislamu? Huo ndio woga wangu
mimi ... hiki kitabu ni kitabu cha uchochezi inabidi kifungiwe. Hawawezi kuwaambia Waislamu semeni yote
lakini haya Yesi si Mungu msiseme. Sasa hii ndio hatari ninayoiona mimi.

Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima ushahidi uliokuwa pale. Hawa
watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa. Jana gazeti moja limesema
Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa jela. Na wengine.

Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie watu wa magazeti hamna huruma,
mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa kwa kuua anaweza kupata
dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata dhamana.

Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna
adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.

Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali! Sasa huenda akafa mmoja, mmoja
mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba wafe mmoja mmoja. Sasa dhana
can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.

Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima ushahidi uliokuwa pale. Hawa
watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa. Jana gazeti moja limesema
Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa jela. Na wengine.

Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie watu wa magazeti hamna huruma,
mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa kwa kuua anaweza kupata
dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata dhamana.

Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna
adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.

Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali! Sasa huenda akafa mmoja, mmoja
mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba wafe mmoja mmoja. Sasa dhana
can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.

Sasa isisemwe maneno ya kwamba mahakama ndio inayowaweka. Si kweli. Mahakama inaamua baada ya
kuambiwa. Waliokuwa wakipinga dhamana siku zote ni serikali. Sasa wakati ule walikuwa wazima afadhali,
sasa wagonjwa. Kwahiyo, serikali isibabaishe hapa ikasema oh kesi ipo mahakamani.

Viongozi wangu baadhi wanasema kuwa mimi natafuta umaarufu. Mimi sitafuti umaarufu. Mimi maarufu. Mimi
sitafuti umaarufu. Mimi tayari maarufu. Kwahiyo, si kweli kwamba mimi natafuta umaarufu.

Mimi nimeanza ubunge 1965. Na tokea nimeanza ubunge sijagombea nafasi yoyote mimi nikashindwa. Yoyote.
Sasa umaarufu unakuaje.

Nimegombea ubunge mara nne nimeshinda mara zote nne. Nimegombea udiwani mara tatu nimeshinda mara zote
tatu. Nimegombea ubunge juzi juzi, nimeshinda. Nimegombea ujumbe wa kamati ya siasa ya mkoa juzi juzi
nimeshinda. Sasa umaarufu unakuwaje. Mie sitafuti umaarufu.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template