MAJIRA: 16 August 2013
PONDA SEGEREA
- ADAIWA KUKAMATWA NA MAKACHERO HOSPITALI
- POLISI ALIYEPIGA RISASI MORO NAYE AKAMATWA
Na
Waandishi Wetu
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda, inadaiwa jana amekamatwa na kupelekwa mahabusu
katika Gereza la Segerea, Dar es
Salaam.Inadaiwa
kuwa, Shekhe Ponda alikamatwa na makachero wa polisi saa chache baada ya
kuruhusiwa na daktari wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), ambako alikuwa
akipatiwa matibabu ya jeraha alilodai kupigwa risasi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, msemaji wa familia ya Shekhe Ponda,
aliyejitambulisha kwa jina la Bw.Isihaka Rashidi alisema ndugu yao alikamatwa
na polisi dakika tatu baada ya kupewa ruhusa ya kuondoka MOI."Taratibu
za kumkamata ndugu yetu hazikufuatwa...sisi tunaamini makachero wa polisi wamemteka
Shekhe Ponda ambaye hali yake bado haikuwa nzuri.
"Kiutaratibu,
mimi ndiye niliyepaswa kukabidhiwa mgonjwa wangu (Shekhe Ponda)...polisi
wamemchukua bila kubeba dawa zake jambo ambalo hatujui atakuwa salama kiasi
gani."Da
k i k a t a t u b a a d a y a kuruhusiwa, walikuja polisi na kumwambia uko
chini ya ulinzi, wamemchukua na kumpeleka mahabusu Segerea...Shekhe Ponda
alishtuka sana aliporuhusiwa hivyo aliomba aongezewe siku mbili ili apate
unafuu kidogo lakini daktari alikataa na kusema amemruhusu”.
Alisema
karatasi ya ruhusa inaonesha jina la daktari aliyemruhusu anaitwa Swai ambapo
Shekhe Ponda alipandishwa kwenye gari aina ya Land Cruser yenye vioo vyeusi
chini ya ulinzi mkali na msafara wa magari manne.
"Nilipata
taarifa kuwa ndugu yangu amechukuliwa na polisi, nilipofika hapa MOI na kuomba
karatasi ya ruhusa ya mgonjwa, niliambiwa kuna bili ya sh. milioni 1.1.
"Uongozi wa MOI
ulisema naweza kulipa au kuacha jambo ambalo bado najiuliza kama Shekhe Ponda
hatalipa fedha hizi nani anayehusika kulipa deni hili," alisema Bw.
Rashidi.
Alisema kitendo hicho
kimeishtua familia yao kwani hawaamini kama polisi waliomchukua wana nia njema
na mgonjwa wao na mpango wa kumkamata ulikuwepo muda mrefu akiwa MOI.
"Inaonesha wazi
Jeshi la Polisi wameshinikiza mgonjwa atolewe kabla ya kupata nafuu ili
wamchukue jambo ambalo ni kinyume cha sheria na haki ya mgonjwa," alisema.
Aliongeza kuwa,
familia itakabidhi tukio hilo kwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini ili
iweze kutoa uamuzi wake.
Msemaji MOI
Kwa upande wake,
Msemaji wa MOI, Bw.Almas Jumaa alikiri kuruhusiwa kwa mgonjwa huyo (Shekhe
Ponda) na alipoulizwa kama amepelekwa Segerea, alisema jambo hilo hawezi
kulizungumzia kwani lipo nje ya uwezo wake.
Tukio la kukamatwa
Shekhe Ponda limemkuta siku moja baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili akiwa
kitandani na wakili wa Serikali Mwandamizi Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hellen Liwa.
Shekhe Ponda anadaiwa
kuchochea vurugu sehemu mbalimbali nchini. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti
28 mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia
askari polisi anayedaiwa kufyatua risasi hewani
katika jaribio la kumkamata Shekhe Ponda,
Agosti 10 mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari Dar
es Salaam jana, Msemaji wa jeshi hilo nchini, Advera Senso, alisema jeshi hilo
limeunda timu ya uchunguzi wa hali halisi ya tukio hilo kabla na baada ya
purukushani zilizosababisha wafuasi wa Shekhe Ponda kurusha mawe na askari
polisi kufyatua risasi hewani.
"Uhalali wa timu kwenda eneo la
tukio unatokana na kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi zinazoelekeza
kufunguliwa jalada la uchunguzi kwa askari yeyote atakayefyatua risasi iwe kwa
bahati mbaya au mazingira yanayomlazimu," alisema.Alisema timu hiyo tayari imeanza kazi
na inaendelea vizuri hivyo aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati jambo hilo likiendelea
kushughulikiwa kisheria ambapo vurugu, fujo au maandamano yasiyo na tija hayatavumiliwa.
Habari hii imeandikwa
na Kassim Mahege, Revina John na Frank Monyo
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !