- Msamaa.
Headlines News :
Home » »

Written By Unknown on Thursday, May 2, 2013 | 5:58 AM

Maoni yetu

Kama hodari wa kuhojiTuhoji pia Tume ya Majeshi ya Vita
Na kile chama cha Wanajeshi wa Kikiristo Je!
VIBAKA wamekuwa ni kero kubwa katika miji mingi nchini kwetu. Linaloshangaza ni kuwa pamoja na kushuhudia wenzao ama wakipondwa vichwa kwa matofali au kuvishwa matairi na kupigwa kiberiti, vibaka hawajifunzi.
Badala ya kutia vichwa vyao maji baada ya kuona wenzao wakinyolewa, hubuni mbinu mpya ya kuendeleza uporaji wao. Upo mtindo ulioibuka Jijini Dar es Salaam, hivi sasa ambapo kibaka akikurupushwa hutimua mbio huku naye akipiga kelele za "Mwizi huyo" "Mwizi huyoo". Au akamgeukia aliyempora na kumwita Mwizi. Katika hali hiyo wenye usongo na kibaka wasipochukua tahadhari humpita mkuku kibaka halisi wakaenda kumshughulikia mtu asiye na hatia au yule yule aliyeporwa.
Na vibaka sio wa kupora mikufu na saa pekee. Wapo pia vibaka wa haki za wengine katika jamii na siasa. Watusi watawakandamiza na kuwaonea Wahutu, wakihoji wataambiwa waasi na magaidi!
Majahudi wanawapora Wapalestina haki zao wakisimama kujitetea wataambiwa siasa kali, magaidi n.k.
 
Waislamu watavamiwa na polisi msikitini kwao wakijitetea wataambiwa "wameleta vurugu", "wahuni" na "wanahatarisha amani!" Ni yale yale; kibaka kakwapua anampigia kelele za mwizi mtu aliye mbele yake ili yeye asalimike kuvishwa tairi na kupigwa kiberiti.
Watu na vyombo rasmi vinahoji. Vipi "Islamic Club"! Kwanini "Islamic".
Kwanini Mawaziri na Maafisa waandamizi Serikalini wajihusishe na "Islamic Club"!.
Octoba 15, 1997 wanajeshi Wakristo wapatao 150 walikutana katika hoteli ya Sheraton mjini Kampala, Mada Kuu (Theme) ya mkutano wao ikiwa "Serving to lead _ The Christian in the Armed Forces."
 
Mkutano huo haukuwa wa siri, kwani ulifunguliwa rasmi na Mhe. Rebecca Kadaga, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda na kutangazwa na vyombo vya habari.
Wanajeshi kama Watanzania wengine wana haki ya ama kuwa Waislamu au Wakristo. Ila jeshi halina dini. Na kule Uganda wanajeshi wetu Wakristo hawakwenda kama watu binafsi, bali walikwenda kama wanachama wa "Association of Military Christian Fellowships for East and North-East Africa. Kule wakakutana na wanajeshi Wakristo wenzao wa Ghana, Congo (Kinshasa), Ethiopia, Kenya, Rwanda, Eritria na Uganda. Kama si mbinu ya kibaka mzoefu, vipi mtu ahoji "Islamic Club" ya kunywa chai asihoji wale maafisa wanajeshi walio Wakristo waliwakilisha jeshi gani katika mkutano wa wanajeshi Wakristo!
Amani ya nchi itahatarishwa na "Club" ya kula mishikaki na kunywa soda au Tume ya Majeshi ya Vita! Taarifa rasmi zimewasilishwa serikalini kuhoji vipi baadhi ya madhehebu ya dini yawe na Tume za Majeshi ya Vita (Armed Forces). Serikali ipo kimya na wanaohoji kwa nini "Islamic Club" nao wapo kimya!
 
La kushangaza kama kawaida yake, akikohoa "paroko" lazima serikali igwaye; haraka haraka Wizara ya Mambo ya Ndani ikatoa ufafanuzi kuwatoa hofu wanaohoji kwanini "Islamic Club". Uhodari huu wa kuharakia kuwatoa wananchi wasiwasi mbona hawautumii katika hili la Tume ya Majeshi ya Vita! Hawa wenye kuharakia kuwatoa wananchi wasiwasi, mbona hatuwaoni wakiwatoa wasiwasi wananchi juu ya ule mkutano wa Maafisa wa jeshi Wakristo waliokutana Kampala!
Katika wanaohoji kwa nini "Islamic Club" wapo waliotupa mpaka orodha ya washiriki wa hafla ya kuzindua "Islamic Club". Pengine wangetupa pia orodha ya wajumbe wa Tume ya Majeshi ya Vita (Armed Forces) ya Kanisa Katoliki; halikadhalika ile orodha ya wanajeshi Wakristo kutoka Jeshi la Tanzania (JWTZ) waliokutana Kampala Oktoba 15, 1997.
 
Meja Generali (Mej. Gen) Elly Tumwine ndiye Mwenyekiti wa wanachama wa chama cha Wanajeshi Wakristo huko Uganda. Hawa wanaotupa orodha ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa "Club" ya kunywa chai watuambie jina pamoja na cheo cha Mwenyekiti wa Wanachama wa Chama cha Wanajeshi Wakristo wa Tanzania. Lakini wangetueleza pia upo uhusiano gani kati ya Chama hiki na hii Tume ya Majeshi ya Vita ya Kanisa Katoliki! Kule Uganda wale Wanajeshi Wakristo walitumwa na nani, walizungumzia agenda gani na walimwakilisha nani! Kuna "Crusade" (Vita vya Msalaba) gani inakuja?
 
Baada ya "Islamic Club", baadhi ya watu na vyombo vya habari vinampa changamoto Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere naye aanzishe "Tanzanian Christian Club". Wale wanaanzisha Islamic Club ili kutafuta sehemu za kunywa chai na kutafuna mishikaki bila kuathiriwa na mazingira ya wale ambao hawakubahatika kuachiwa urithi wowote na babu zao ila "tembo" la kuzikoroga bongo zao. Sasa Christian Club ya nini wakati hata kwenye duka la sembe, urithi wao upo!
"Christian Club" leo Mwalimu aanzishe ya nini wakati Watanzania wote wanadhaniwa ni wanachama wa COBA! Ndiyo maana tuna Ubalozi wa Vatican, lakini OIC ni haramu! Wanaosema Yesu si Mungu wanasota rumande, wakati waliosema Mtume Muhammad (s.a.w.) kafa kwa ukimwi wapo nje wanatamba!
"Christian Club" ya nini wakati Paroko akikohoa polisi hutumwa Msikitini wakavunja msikiti na kuua na bado walioua wakaendelea na nyadhifa zao!
Christian Club ya nini wakati Serikali ishatoa makamanda ambao huthubutu kuwadungua Waislamu risasi na wakapongezwa!
Christian Club ya nini wakati hata Masheikh wanabakia na majoho tu. Vijana wao wanalengwa shabaha kwa risasi; mabinti, wake zao na mama zao wanavuliwa nguo wao ndio kwanza wanavaa kanzu safi na kujitia manukato tasbih mkononi wanakwenda kwenye shughuli!
Christian Club ya nini wakati hata Waheshimiwa Wabunge wakitaka Tume iundwe kuchunguza mauaji ya Waislamu yaliyofanywa na polisi, Spika wa Bunge hupinga!
Jumuiya na Taasisi za dini huanzishwa ili ama kupigania haki na maslahi ya waumini wao au kujiletea maendeleo.
 
Sasa Tanzania Christian Club (T.C.C.) ya nini wakati masista wakipinga, ujenzi wa msikiti serikali hutekeleza matakwa yao! T.C.C. ya nini wakati washapewa 'hati miliki' ya kuhodhi sehemu zote nyeti nchini mpaka "Parole"! T.C.C. ya nini wakati hospitali za serikali hukosa hata aspirin, lakini Serikali hiyo hiyo hutoa mabilioni ya fedha kuendeshea hospitali za Kanisa! T.C.C. ya nini wakati Mwenyekiti Reinhard Bonnke mhadhara wake wa wiki nzima wa kusema Yesu ni Mungu hupewa heshima kubwa na Serikali huku Magezi Shaaban akisota rumande kwa Kusema Yesu si Mungu!
Mwalimu Nyerere aunde Christian Club kupigania nini wakati kutokana na kazi ya COBA na "Marian Spirit" Dk. Sivalon anatuambia "matendo, msimamo na uamuzi wa viongozi wa serikali unafanana mara kwa mara kwa namna moja au nyingine na mafundisho na mwelekeo wa Kanisa!"
 
Lakini pengine hawa wanaohoji juu ya Islamic Club wangetueleza nini COBA (Catholic Old Boys Association); ilianza lini yapi yalikuwa madhumuni yake na watupe majina ya viongozi wa serikali (kama walivyotupa yale ya I.C.) ambao ni wanachama wa COBA au waliwahi kuwa wanachama na viongozi wa COBA.
Ule ujinga wa kumfukuza aliyeibiwa na kumwacha kibaka, Alhamdulillah umewatoka Waislamu na wazalendo wa nchi hii.
 
Kila mwananchi anabaki sawa na mwingine katika masuala ya imani, siasa na jamii kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Kama tunahoji Islamic Club, tuhoji pia Tume ya Majeshi ya Vita na Association of Military Christian Fellowships.
 
Chanzo: Annur
Na.154 Safar 1419, Juni 19-25, 1998.

 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template