- Msamaa.
Headlines News :
Home » »

Written By Unknown on Thursday, May 2, 2013 | 7:25 AM

Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba 1998:
Afisa Elimu akiri kutaka orodha ya wanafunzi
Adai amejieleza Wizarani
Atekeleza ombi la Katekesi
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
AFISA Elimu wa Manispaa ya Morogoro Bibi E. Mwangamila amekiri kwamba ofisi yake ilitoa agizo kwa wakuu wa shule za msingi kumpa orodha ya wanafunzi Wakatoliki.
Afisa Elimu huyo amedai kwamba amefanya hivyo kutekeleza ombi la
Mkurugenzi wa katekesi Jimbo la Morogoro Sr. M. Bonifacia C.P.S.
Bibi Mwangamila amesema alipokea ombi hilo alishindwa la kufanya kwani alikuwa mgeni ofisini hapo, hata hivyo alipotaka ushauri kwa wale aliowakuta ofisini, walimhakikishia kwamba halina tatizo na hufanyika kila mwaka.
 
Baada ya kupewa maelezo hayo alisema ndipo alitoa maelekezo kwa Bw. E.P. Mpessa kutoa agizo kwa waalimu wakuu kutuma ofisini kwake majina ya wanafunzi wa Kikristo.
Bibi E. Mwangamila amesema kwamba baada ya wananchi kuonyesha wasiwasi kufuatia zoezi hilo, ameandika barua Wizara ya Elimu kutoa ufafanuzi ambapo amedai kwamba nakala ya barua hiyo ameipeleka kwa Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa.
AN-NUUR imebahatika kupata nakala ya barua Na. DM/CAT/MTI-S/M/03/98 inayodaiwa kutoka idara ya Katekesi inayoomba majina ya wanafunzi Wakatoliki.
Hata hivyo, barua hiyo ikilinganishwa na ile ya Afisa Elimu wa Manispaa inazua maswali mengi kuliko majibu.
 
Kwanza barua hiyo ya Sr. M. Bonifacia inaonyesha iliandikwa Machi 2, 1998 na kuomba majina ya wanafunzi Wakatoliki yafike Idara ya Katekesi jimboni Morogoro kabla ya Aprili 30, 1998. Hata hivyo barua hiyo inaonyesha ilipokelewa ofisini kwa Afisa Elimu Manispaa Juni 1, 1998, miezi mitatu baadae, wakati ofisi hizo mbili zinatenganishwa na umbali usiotimia hata robo kilo meta.
Lakini jingine ni kwamba wakati barua toka Afisa Elimu Manispaa kwenda kwa wakuu wa shule inaonyesha kuandikwa Juni 9, vidokezo juu ya barua toka Idara ya Katekesi inaonyesha kwamba waalimu walipewa maelekezo na kuandikiwa barua Juni 8, 1998.
 
 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template