- Msamaa.
Headlines News :
Home » »

Written By Unknown on Friday, May 3, 2013 | 1:10 PM

RAIS AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NA MAKAMISHNA WA IDARA MBALIMBALI


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza na maafisa
wengine.
Kaimu
Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo amesema Rais amemteuaBwana John Casmir Minja (pichani) kuwa Kamishna
Jenerali wa Magereza
 na kuwateua wengine kuwa maofisa kama ifuatavyo:
·
Dkt.
Juma Ally Malewa
 ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Sheria na
Uendelezaji wa Magereza.
 ·
Bwana
Deonice Lwamahe Chamulesile
 ameteuliwa kuwa Kamishna, Huduma za
Urekebishaji.
 ·
Bwana
Gaston Sanga
 ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Utawala na
Fedha.
Wengine ni:
·
 Bwana
Fidelis M. Mboya
 ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii
katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo kabla ya uteuzi huu Bw. Mboya alikuwa
Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza na;
 ·
Bwana
James B. Celestine
, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara
ya Huduma kwa jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amepandishwa cheo
na kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ambapo atarejea Magereza na kupangiwa kazi
nyingine.
 Kulingana na taarifa iliyotolewa leo,
Jumatatu, Oktoba 1, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw.
Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa
uteuzi huu umeanza tangu tarehe 25 Septemba, 2012.
Imetolewa
na
:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1
Oktoba, 2012
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template