- Kitoloho
Headlines News :
Home » »

Written By Msamaa on Wednesday, April 17, 2013 | 2:53 PM


Kwa Nini Waislamu Wanalalamika?

MWANDISHI: MAALIMU ALLY BASSALEH P.O.BOX 15653, DAR ES SALAAM, TANZANIA. MHARIRI NA MSAMBAZAJI: BARAZA KUU NA TAASISI ZA KIISLAMU, TANZANIA S.L.P 9701 TEL : 760228/170664

Siti bint Saad aliimba:
Siri sifunue kwa wino wa rangi fahamu ujue kuna mambo mengi wajila mwenyewe kwa ujinga mwingi

Alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho huko Dodoma Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Mheshimiwa William Benjamin Mkapa Alikemea wale wote wanaotaka kuligawa taifa hili kwa misingi ya kidini. Kwa kweli hakuna sumu mbaya zaidi inayoweza kuleta uhasama, mgawanyiko na hata umwagaji damu katika jamii kama udini. Katika taifa kama la Tanzania, ambalo wananchi wake ni mchaganyiko wa dini mbali mbali pamoja na wale wasiokuwa na dini ni hatari kupalilia au kushabikia udini. Serikali inatakiwa iwe makini sana kuona kuwa raia hawabaguliwi kwa misingi ya dini zao. Natumai hilo ndilo lililomsukuma Mheshimiwa Rais katika mkutano huo mkuu maalumu wa CCM kule Dodoma kuonya kuwa atatumia uwezo na nguvu zake zote kuzika mgawanyiko wa kijamii kwa misingi ya kidini. Kauli hiyo ya Mheshimiwa Rais siyo kwamba inahitaji kupongezwa tu bali inabidi iungwe mkono na kila yule anayeitakia heri Tanzania. Hakuna haja ya kutaka kujidanganya. Hivi sasa Tanzania tayari zimekwishajengeka hisia za udini, basi kama kweli Mheshimiwa Rais ana nia ya kulishughulikia jambo hilo kwa dhati inabidi kwanza aangalie kwa makini nini chanzo cha jambo hilo? Kutaka kulishughulikia jambo kubwa kama hili lenye kugusia imani za wengi, na haki za msingi za raia, bila ya kulifanyia uchunguzi wa kina ni sawa na kutumia jazba katika kutoa maamuzi makubwa. Kitendo kama hicho kinaweza kuleta madhara makubwa zaidi kuliko hata ile faida inayokusudiwa kupatikana.

Mara unapotajwa udini humu nchini, walengwa huwa ni Waislamu. Wao ndio wanaoshutumiwa kwa kutaka kupandikiza mbegu ya udini na kuhatarisha kuvuruga amani nchini, iliyoletwa na chama tawala na serikali yake chini ya uongozi wa mwasisi wa Taifa hili, Hayati Julius Kambarage Nyerere.

Mkongwe mmoja wa kisiasa humu nchini, na ambaye ni kada mkubwa wa CCM, Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru, hivi juzi, katika ule mkutano mkuu maalumu wa CCM, Dodoma, alisema kuwa pasipokuwa na haki hakuna amani. Hiyo ni kweli isiyopingika. Huwezi kutegemea kuwepo na amani ya kweli pale penye dhuluma na ubaguzi.

Katika kujaribu kuchunguza kwa nini waislamu waonekane ni wakorofi na wenye kutaka kupanda mbegu za udini, nimegundua kuwa waislamu wanahisi kuwa hawatendewi haki na Serikali iliyopo madarakani na kwamba wanabaguliwa kwa sababu tu ya dini yao. Nimebaini kuwa kuna mambo sita ambayo, kwa namna moja au nyingine, ndiyo yaliyowachochea waislamu wajitokeze hadharani na kuishitumu Serikali kwa kuendeleza bbbudini.

Jambo la kwanza ni kitabu cha Dkt. JOHN C. Sivalon, kinachoelezea mafungamano ya siri baina ya kanisa katoliki na serkali, dhidi ya uislamu na kwa faida ya kanisa hilo. Jambo la pili, ni kitabu cha Al-Hajj Aboud Jumbe Mwinyi kilichokuja kuwathibitishia waislamu kuwapo kwa udini huo. Tatu, ushahidi wakimazingira unathibitisha kuwa wakristo wengi ndio, siku zote, wanaopata fursa za kupata elimu ya juu, pamoja na kushika madaraka katika ofisi za Serikali na mashirika ya umma. Na jambo la mwisho, ni uhuru wa kusema, uliotokana na mageuzi, yaliyoondoa ukiritimba wa chama kimoja na kuleta demokrasia ya vyama vingi, ndio uliowapelekea waislamu wajitokeze kuelezea kero walizo nazo na kutetea haki zao hadharani.

Kitabu hiki kimekusudiwa kuiondoa ile dhana potofu inayoenezwa kuwa eti waislamu ni wakorofi, wanachanganya dini na siasa, kwa lengo la kuvuruga amani nchini, na kumbe wakorogaji wakubwa wa dini na siasa katika nchi hii ni kanisa katoliki kwa kushirikiana na Serikali, kama lnavyodhihirishwa hilo na Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake hicho. Pili, tumekusudia kuyaweka bayana yake aliyoyaeleza Dr. Sivalon katika kitabu chake juu ya jinsi kanisa katoliki kwa kushirikiana na Serikali, lilivyoandaa hila za siri zilizolipa mwanya kanisa hilo kuelekeza siasa Tanzania na hapo hapo kuudhibiti uislamu na waislamu.

Kwa kuwa sera ya Serikali yetu ya awamu ya tatu ni UKWELI NA UWAZI, tunataka viongozi wa Serikali na watanzania kwa jumla, kabla hawajaamua kuwalaumu na kushutumu waislamu. Waislamu wakisome kijitabu hiki kwa makini, wazingatie yaliyoandikwa humo, kisha waamue jee, upo udini nchini ulioanzishwa na kanisa katoliki pamoja na serkali ya awamu ya kwanza, chini ya uongozi na Mwalimu Nyerere au haupo? Jee, waislamu wana haki yakulalamika na kudai haki zao au hawana ? Na kama upo udini huo dhidi ya waislamu Serikali inakusudia kuchukua hatua gani za makusudi kuondoa hali hiyo?

Kulifumbia macho tatizo hilo si dawa hata didogo. Tusisahau ule usemi wa hekima wa kiswahili unaosema "Mdharau mwiba Mguu huota tende!" Kwa nini basi tungojee mpaka mguu uote tende? Huenda mkaona kuwa mtindo wa kitabu hiki ni kinyume kabisa na ule mtindo ya vitabu vingine mlivyovizoea kuvisoma, kwa kawaida, katika vitabu vyote, maelezo ya mwandishi huwa ndio yanayotawala kitabu kizima lakini, katika kitabu hiki, maelezo ya mwandishi ni machache sana. Mwandishi amechangia kutoa maswali tu, majawabu ya maswali hayo ni maelezo ya Padre wa kikatoliki, yaliyomo katika kitabu chake alichokiita "KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA - 1953 HADI 1985". Imefanywa hivyo, makusudi, ili isije ikasemwa, labda mwandishi wa kitabu hiki, ameandika uzushi, au ametia chumvi katika maneno yake.

MALALAMIKO YA WAISLAMU

Katika miaka ya karibuni, waislamu hapa nchini, wamekuwa wakisikika wanalalamika kuwa Serikali imekuwa haiwatendei haki. Wananchi kuwa wamekuwa wakipunjwa katika kupata elimu, hasa ile ya sekondari na Chuo Kikuu. Aidha, wamekuwa wakinyimwa nafasi za uongozi serikalini na katika mashirika ya umma. Na pale wanapotokezea viongozi wa kiislamu kukemea dhuluma wanazofanyika au kutetea haki zao, hupachikwa kila aina ya majina, siasa kali, mujahidina, wakorofi, wachochezi na wachanganya dini na siasa na hutumiwa vyombo vya dola kuwadhibiti.

Katika Baraza la Idd -el - fitr la mwaka jana, halmashauri ya waislamu, iliyokuwa ikiwakilisha madhehebu na taasisi mbali mbali za kiislamu, ilimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa William Benjamini Mkapa, risala iliyoorodhesha kero zote za Waislam. Mheshimiwa Mkapa alipokea risala hiyo, kwa mikono miwili, na akaahidi kuwa atayafanyia uchunguzi wa kisayansi malalamiko hayo ya waislam ili apate kuelewa kama ni ya kweli au ni ya uongo. Aliahidi kuwa atashauriana na Baraza lake la mawaziri juu ya jambo hilo, na pale uchunguzi utapothibitisha kuwepo kasoro zozote atafanya jitihada za kuziondoa kasoro hizo. Waislam wakafurahika sana, na wakaingiwa na matumaini makubwa

WAISLAMU WAPUUZWA

Jambo la kwanza lililowavunja moyo na kuwakatisha tamaa waislam, sio ule ukimya mkubwa tu wa Mheshimiwa Rais kutoshughulikia kero hizo bali kushindwa hata kuwaeleza waislamu juu ya matokeo ya uchunguzi wake. Na hata alipoandikiwa barua ya kumbukumbu na Dkt. Saleh Al-Miskry, aliyekuwa katibu mkuu wa muda wa halmashauri hiyo ya waislamu, na pia katibu mkuu wa Dar es salaam Islamic club, jawabu aliyojibiwa na Mheshimiwa Rais haikuwa maridhawa. Jawabu hiyo badala ya kuwapa waislamu matumaini ilizidi kuwakatisha tamaa. Kwa mfano, akijibu kwa nini Serikali ina uhusiano wa kibalozi na Vatikano, Makao makuu ya kanisa katoliki duniani, na ikakataa kujiunga na OIC.Alisema yeye akiwa ni Rais wa wanywa pombe na wasiokunywa pombe, wala nguruwe na wasiokula nguruwe, hawezi kuwasikiliza waislamu na akapuuzia maoni ya wasiokuwa waislamu. Waislamu wamechukizwa sana na jawabu hiyo na wameichukulia kama ni dharau kwao. Wameitafsiri kauli hiyo ya Mheshimiwa Rais kuwa Serikali ipo tayari kuyapa kipaumbele maoni yanayotolewa na viongozi wa kanisa, lakini haipo tayari kuyasikiliza madai ya waislamu.

Kuhusu kadhia ya mwembechai waislamu walijibiwa kuwa hakuna haja ya kufanya uchunguzi. Katika ghasia za mwembechai si chini ya waislamu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi. Kwa mujibu wa sheria, kifo chochote kinachotokana na polisi au magereza hubidi kifanyiwe uchunguzi maalumu wa kisheria unaoitwa "INQUEST" kwa lugha ya kitaalamu. Waislamu wameomba mahakamani kufungua "INQUEST" hiyo, lakini kwa muda wa miaka miwili wamekuwa wakizungushwa zungushwa, ingawa wakati naendelea kuandika maelezo haya, nimepata habari za kuaminika, kuwa mahakama ya Hakimu Mkaazi ya Kisutu, imekubali lile ombi la waislamu kufungua "INQUEST" katika mahakama hiyo. Lakini swali la kujiuliza ni kwa nini ichukue muda wote huo?.

Ingawa katika jawabu yake, Mheshimiwa Rais Mkapa, amekataa kuwapo kwa mpango wowote wa makusudi wa Serikali wa kuwabagua waislamu kwa ajili a dini yao, lakini waislamu kwa mujibu wa hali ya mazingira wanashindwa kukubaliana na Mheshimiwa Rais kwa hilo. Mheshimiwa Mkapa amekiri kutokuwapo uwiano baina ya wanafunzi wa kiislamu na wale wa kikristo katika shule za sekondari na vyuo vikuu na pia kuwapo idadi ndogo ya waislamu katika nafasi za uongozi, katika mawizara na ofisi za serikali, lakini alisema tofauti hizo hazitokani na mkakati wowote wa kiserikali ulioandaliwa makusudi kuwabagua waislamu. Amedai hali hiyo imetokana na sababu za kihistoria. Lakini waislmu wanahisi kuna mkono wa mtu unaosababisha hayo

KWA NINI WAISLAMU WANAONEKANA WAKOROFI?

Kama tulivyotangulia kusema kila wanapochomoza viongozi wa kiislamu kuelezea kasoro zilizopo, kukemea dhuluma dhidi ya waislmu, na kutetea haki zao, basi huonekana ni wakorofi wakaambiwa wanachanganya dini na siasa. Huandamwa na vyombo vya dola kwa madai kwamba wanataka kuhatarisha amani. Kuna wanaodai kuwa hakuna udini hapa nchini. Na kuna wanaodai kuwa kuna vyama vya siasa humu nchini vinavyochochea hali hiyo, kwa lengo hilo hilo la kuchafua amani. Kauli za aina hii ni kauli za jazba. Zinachukuliwa kijuu juu tu, hazilengi katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo, zinalenga katika kuuhadaa umma na kuficha ukweli. Wengi wa wale wanaodai kuwa hakuna udini na wakawaita waislamu wanaodai haki zao ni wakorofi ni wale wanaofaidika na mfumo huu uliopo au ni wale wanaojipendekeza kwa maslahi yao binafsi.

Katika uchunguzi nilioufanya juu ya jambo hili nimegundua kuwa kuna sababu nne kuu zilizowapelekea waislamu wajenge hisia za kuwapo udini hapa nchini, na pia wajitokeze kulalamika na kudai haki zao. 1. KITABU CHA DR. JOHN C. SIVALON Kwanza, kitabu kilichoandikwa na Dr. John C. Sivalon, alichokiita "KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA - 1953 HADI 1985" kimekuja kuwafunua macho waislam na kuwahakikishia kuwa zile hisia za udini ndani ya serikari, dhidi ya uislamu, ni zakweli Kitabu hicho kimedhihirisha wazi wazi kuwa kanisa katoliki, Tanzania chini ya uangalizi wa Vatikano, katika kipindi chote cha utawala wa awamu ya kwanza, chini ya uongozi wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, lilikuwa likichanganya dini na siasa, limekuwa likishirikiana na Serikari katika kulipendelea kanisa hilo na kuudhibiti uislamu waislamu na waislumu kwa jumla.

2. KITABU CHA AL-HAJJ ABOUD JUMBE MWINYI Pili, Kitabu kilichoandikwa na Al-Hajj Aboud Jumbe Mwinyi alichokiita "THE PARTNERSHIP" (Muungano wa Tanganyika na zanzibar Miaka 30 ya dhuruba") nacho kimechangia, kwa kiwango kikubwa kuwafanya waislamu waamini kuwa kweli wanabaguliwa. Katika kitabu hicho, cha Al - Hajji Jumbe kilichoandikwa kwa lugha ya kiingereza na kufasiriwa kwa lugha ya kiswahili na Ali Saleh kinaelezea na kutoa ushahidi kuwa, waislamu wa Tanzania Bara wamekuwa na uonevu ulioendelezwa na kukoseshwa haki zao za msingi pamoja na kuwa katiba ya 1977 ilikuwa na vipengele vya kuhakikisha haki za binadamu na usawa kwa raia wote.

Ushahidi wa ziada unaonesha kuwa kanisa nchini Tanzania ndilo linatoa maelekezo ya kisiasa, na mfumo wa kisiasa umekuwa ukifumwa kutoa upendeleo kwa wakristo, ambao tayari wamo katika kudhibiti nafasi mbali mbali katika taasisi za umma. (Sivalon, 1992)" uk - 125. Shutuma hizi dhidi ya Serikali na chama tawala, kutolewa na mtu kama Al -Hajji Jumbe ambaye kwa nyakati tofauti amewahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi katika chama tawala na Serikali yenyewe, na ni mtu aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama tawala na pia Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, zimewapelekea waislamu wengi, waamini kuwapo ubaguzi wa makusudi dhidi yao.

Kwa jinsi Al Hajji Jumbe anavyoelewa maana ya dhamana, mtu aliyekuwa kiongozi wa ngazi ya juu katika chama tawala na Serikali yake haiwezekani kabisa akurupuke na kuandika maneno, ambayo ni ya uongo, ambapo yanaweza kuchochea uhasama mkubwa nchini baina ya raia wenyewe kwa wenyewe, na pia baina ya raia na serikali yao. Huyu ni mtu mwenye kujua alichokuwa akikiandika na matokeo ya hicho alichokiandika, Kwa huyo hathubutu kuandika maneno ya uzushi lazima kile alichokandik kiwe na namna ya ukweli ndani yake.

3. USHAHIDI WA KIMAZINGIRA

Tatu, ushahidi wa kimazingira unathibitisha madai hayo ya waislamu. Kwa mfano, Al-Hajji Jumbe, katika kitabu chake hicho nilichokitaja, ametoa jadweli ifuatavyo, kuonesha uwiano wa wanafunzi wa kiislamu na wa kikiristo kwa shule za sekondari na kwa chuo kikuu cha Dar es salaam, baina ya mwaka 1971 hadi 1984. IDADI YA WANAFUNZI KIDATO CHA I MWAKA WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1978 28% 77% 1:3 1979 22% 78% 1:3 1980 23% 77% 1:3 1981 25% 75% 1:3 Uk. 132 IDADI YA WANAFUNZI KIDATO V MWAKA WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1978 12% 88% 1:7 1979 13% 87% 1:6 1980 13% 87% 1:6 1981 12% 88% 1:7 Uk. 132 IDADI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU DAR ES SALAAM MWAKA WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1971-72 13% 86% 1:6.6 1972-73 14% 84% 1:6.0 1973-74 13% 87% 1:6.6 1984-85 15% 85% 1:5.7 1986-87 16% 84% 1:5.7 1987-88 18% 82% 1:4.5 1988-89 18% 82% 1:4.5 Uk. 133

Kutokana na jedwali hiyo, inaonesha uwiano baina ya wanafunzi wa kiislamu na wenzao wakristo katika elimu ya sekondari, ni kwa kila mwanafunzi wa kiislamu mmoja anayepata nafasi ya kuingia shule ya sekondari, basi idadi ya wanafunzi wa kikiristo ni kama ilivyojitokeza kuwa, mwanafunzi mmoja kwa kila wanafunzi watano. Na anapata nafasi katika chuo kikuu, mambo huwa ni mabaya zaidi, kwa kila mwanafunzi mmoja wa kislamu anayeingia chuo kikuu, huingia wanafunzi watano mpaka saba wa kikristo.

Kuhusu mgawanyiko wa madaraka katika vyombo vya Serikali Al-Hajji Jumbe ametoa takwimu zifuatazo: Mwaka CHEO WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1993 Makatibu Waku 4 16 1:4 Wakuu wa Mikoa 5 15 1:3 Wakuu wa Wilaya 8 113 1:14 Uk. 136 Kwa mujibu wa takwimu hizi tutaona kuwa kati ya wakuu wa Wilaya 121 wanane tu ndio waislamu, na 113 ni wakiristo. Pia Makatibu wakuu wa Mawizara walio waislamu ni wachache, kwa vile cheo hicho kinataka wasomi wenye shahada za vyuo vikuu na waislamu wenye shahada kama hizo ni wachache, vipi basi na nafasi za wakuu wa Wilaya zishikwe, takriban na wakristo watupu. Jee Hakuna waislamu wenye sifa ya kushika nafasi hizo? Au ukuu wa Wilaya nao uanahitaji shahada za Chuo Kikuu?

Al-Hajji Jumbe, katika kitabu chake, anaeleza, "Picha inayooneshwa na taarifa za takwimu hizi ni kuwa waislamu, pamoja na kuonyeshwa kuwa kuna vifungu vya katiba vyenye kulinda haki hizo basi bado wao wananyimwa haki za usawa na za kutosha." Uk 138. Al-Hajji Jumbe ameendelea kusema, "Serikali iliyo madarakani lazima ikubali jukumu la vitendo vya kuvunja haki za kikatiba dhidi ya waislamu wa nchi hii.

Hakuna Serikali yoyote ambayo inajali maslahi ya taifa, inayoweza kupuuza madai ya ukweli ya raia wake. Hali ya kutochukua hatua kwa upande wa CCM na serikali yake, kumesababisha utamaduni wa ukiukaji wa katiba na mengi ya matendo hayo yakiwa dhidi ya uislam". Uk 138. Mwisho Al-Hajji Jumbe anahitimisha maelezo yake kwa kusema kwa hivyo naona ingekuwa bora tungelitazama swala la dini na siasa kwa hivyo tuweze kuipima hali hiyo. Jee Tanzania ni nchi ya kiislam, kikristo au haina dini? na siasa gani ambayo imetuburura na kutuingiza katika hali ambayo jamii moja iliyo kubwa ndani ya nchi yetu imedharauliwa na kushushwa kuwa daraja la pili?

Uk 138 Na ipo mifano mingine mingi ya ushahidi wa kimazingira, lakini michache itakidhi kuonyesha dhuluma walizofanyiwa Waislamu na Serikali ya Tanzania. Mfano wa kwanza ni kuvunjwa kwa Jumuiya ya Waislamu ya Afrika Mashariki (East African Muslim Welfare Society) mwaka 1968. Jumuiya hii ilifanya mambo mengi ya maendeleo kwa Waislamu wa Afrika Mashariki katika kipindi cha miaka 30 ya uhai wake. Wakati ilipokuwa ikivunjwa mwaka 1968, tayari ilikuwa imefanikiwa kujenga jumla ya shule 175 (70 kati ya hizo zilijengwa Tanzania), misikiti 149 (53 Tanzania), shule za ufundi tatu na hostel moja. Kadhalika iliunda mfuko wa maendeleo uliokuwa na akiba ya shs 660 milioni za Tanzania. Vyote vilivyokuwa Tanzania vilitaifishwa. Na hujuma kubwa zaidi ya yote ni kuuwa ule mpango kabambe wa kujenga Chuo Kikuu mjini Dar es Salaam kwa watoto wa Afrika Mashariki. Nchi kama Misri, Jordan na nyingine za Kiislamu zilichangia katika mfuko wa ujenzi wa chuo hicho.

Kiwanja kilichopangwa kujengwa chuo hicho hivi sasa kimegeuzwa shamba la kulimia mchicha. Kadhalika Jumuiya hiyo ilitenga viwanja karibu katika kila mkoa kwa ajili ya maendeleo ya Waislamu. Mkakati wa kuivunja Jumuiya hiyo ulilenga kuwadumaza waislamu na uislamu baada ya serikali ya mwalimu Nyerere kuishutumu jumuiya hiyo eti ilikuwa ikichanganya dini na siasa. Mfano wa Pili, ni Makubaliano ya Maelewano ya 1992 kati ya Serikali na umoja wa Mabaraza ya Makanisa nchini (Christian /Council of Tanzania na umoja Tanzania Episcopal Conference). Katika muafaka huo, Serikali ya Tanzania ilikubali kuwarejeshea wakristo shule za sekondari na hospitali zilizotaifishwa mwaka 1970, na pia kuahidi kutozitaifisha tena shule na hospitali hizo au zile zitakazojengwa na makanisa hapo baadaye.

Aidha, Serikali itajitahidi kutafuta fedha na misaada kutoka kwa wahisani wa nje, na hasa Serikali ya Ujerumani, kwa ajili ya kuendeleza huduma za kijamii zinazotolewa na kanisa. Chini ya muafaka huo Serikali ilipaswa kutenga nafasi maalumu katika vyuo vyake vya ualimu kwa ajili ya waalimu wa makanisa kwenda kusomea ualimu kwa lengo la kuimarisha ubora wa shule za Kikristo. Waislamu walifichwa muafaka huo ili makubaliano hayo kati ya serikali na makanisa yabakie kuwa siri. Lakini hata baada ya kuyagundua, waislamu walinyimwa fursa kama hizo licha ya BARAZA KUU la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (BARAZA KUU) kudai kwa muda mrefu bila ya mafanikio.

Mkataba huo haukuwatendea haki waislamu wa nchi hii. Katika taifa, suala la elimu ni muhimu na nyeti kwa sababu linahusu malezi ya kizazi cha kesho cha taifa hilo. Maamuzi mazito na makubwa kama haya yaliyofanywa na serikali yetu yalibidi yaafikiwe kwa kufuata taratibu zinazokubalika. Utaratibu uliofuatwa na Serikali ya Tanzania ulikuwa ni wa kutatanisha. Serikali iliridhia mkataba huo hata kabla ya Bunge kujadili suala hilo.

Chini ya mkataba huo wa tarehe 21/2/92, Serikali ilikubali kuzibinafsisha (de-nationalize) shule na hospitali kwa makanisa. Kifungu kimoja cha mkataba huo kinaeleza : "The government shall not nationalize schools hospitals, or any education or heath institutions owned by the Churches". Tafsri: "Serikali haitataifisha shule hospitali, au taasisi yoyote ya elimu au afya inayomilikiwa na makanisa." (Tazama : Part Four, Obligations, Article XLL). Jambo la pili, ni marekebisho ya Sharia ya Elimu Na : 25 yaliyofanywa na Serikali kuyawezesha makanisa kupewa shule zilizokuwa mali ya taifa. Waislamu walinyimwa fursa kama hiyo waliyopewa wenzao wa kikristo, licha ya waislamu kuendelea kudai kwa mwongo mzima sasa.

Kinyume chake, Serikali inaendelea kumiliki shule za waislamu zilizotaifishwa mwaka 1970. Baya zaidi ni kuwa Serikali siyo tu iliamua kuyadharau malalamiko ya waislamu, bali pia kupuuza kujibu barua ilizopelekewa na BARAZA KUU juu ya suala hilo. Kikao cha Bunge kilichofuata cha Aprili 1992 kilifuta ibara ya 30 ya Sheria ya Elimu Na 25 ya mwaka 1978 iliyohalalisha makanisa kurudishiwa shule hizo. chini ya Makubaliano, sera zote za elimu na afya katika shule na hospitali za makanisa zingebuniwa na Kamisheni ya huduma ya kikristo, kwani kifungu kimoja cha mkataba huo kinaeleza: "There shall be established a governing body to be known as the Christian Social Services Commission (hereinafter refferd to as the "Commission") whose primary functions shal be: (a) to make policies in all matters related to Education and Health services provided by the Churches" Tafsiri: Itaanzishwa bodi ya uendeshaji itakayojulikana kama "Kamisheni yakikristo ya Huduma za jamii (ambayo hapa itajulikana kama Kamisheni) ambayo kazi zake za msingi zitakuwa: (a) Kuandaaa sera juu ya mambo yote yanayohusiana na huduma za Elimu na Afya zinazotolewa na makanisa." (One, Institutions Article1(a). Serikali iliamua kuzirejesha kwa makanisa baadhi ya shule ambazo ni za serikali bila ya kuwataka ushauri waislamu na watanzania wengine ambao si wakristo.Serikali ilifanya hivyo huku ikijua kuwa kuna watoto ambao si wakristo waliokuwa wakisoma katika shule hizo. Serikali pia ilifanya hivyo huku ikijua kuwa imekabidhi kwa wakristo mamlaka ya kubuni sera zote za elimu katika shule hizo. Kwa kufanya hivyo ni dhahiri kuwa Serikali haikuona kama kulikuwa na haja au umuhimu wowote wa kuwahusisha wasiokuwa wakristo katika suala la elimu.

Aidha, kwa kufanya hivyo Serikali iliona ni vizuri, kwa maslahi ya taifa, kama ingejivua jukumu la kubuni sera za elimu na badala yake makanisa yakafanya kazi hiyo kwa niaba ya raia wote. Katika waraka wake wa April 1992 kwenda Serekalini, Baraza kuu lilitahadharisha kuwa serilai haikuwatendea haki waislaum wa nchi hii kwani zaidi ya miaka 20 sera za Serkali zilikuwa zikinadi na kujigamba juu ya kutetea na kulinda maslaha ya raia wote. Ikiwa katika shule zote za sekondari za serikali idadi yaWaislamu imekuwa chini ya asilimia 20, itakuwaje hatima ya waislamu katika shule za makansa, shule ambazo wakristo ndiyo wanaopanga sera zote? Uingereza ni nchi iliyoelendelea na ni ya Kikristo. Lakini hata huko, serikali inaheshimu hisia za watu wa dini nyingine.

Sheria ya Elimu ya Uingereza ya mwaka 1944, ambayo inaendelea kutumika hadi leo inatamka wazi kuwa watoto waelimishwe kulingana na matakwa na ridhaa ya wazazi wao. Kwanini basi serikali ya Tanzania ikaingia mkataba ambao utakuwa na madhara makubwa kwa watoto wa Waislamu? Wakati shule zilipokuwa zikitaifishwa mwaka 1970, lengo lilikuwa kuifanya elimu ya taifa kuwa ni nyezo muhimu sana ya kulishikamisha taifa lenye watu wa makabila na dini mbali mbali. Ikiwa mwelekeo mpya wa taifa ni kwa Serikali kujitoa katika suala la elimu, Serikali ilipaswa kuutangaza mwelekeo huo mpya ili kupata maoni ya wananchi wake kama ilivyokuwa mwaka 1970. Lakini badala yake, Serikali ikaamua kuwaacha waislamu gizani juu ya zile fikra za mwaka 1970 za kujenga mshikamano wa kitaifa.

Ikaamua pia kujifanya bubu ilipoulizwa juu ya fedha za umma zilizotumika kukarabati na kuziendeleza shule za hospitali hizo kwa kipindi cha miaka 22 au juu ya fedha zilizochangwa na wasiokuwa wakristo kuwafidia waliokuwa wamiliki ya shule na hospitali hizo hapo awali. (Tazama Ibara ya 30 (3) ya sheria ya elimu Na 25 ya 1978) Aidha Serikali ilikubali kutenda kasma maalum ya fedha kutoka kwa wahisani kwa ajili ya maendeleo ya shule hizo na ikakataa kusema chochote kama ilikuwa na mpango mbadala wa kuendeleza elimu ya raia wengine ambao si wakristo. Mwelekeo huo wa Serikali haukuwa na ishara wala nia njema kwa waislamu wa nchi hii. Kweli waislamu wa nchi hii wanasubira kubwa!!

4. MAGEUZI

Mageuzi ya kisiasa, yaliyoondoa ukiritimba wa chama kimoja na kuleta mfumo wa vyama vingi, kwa njia moja au nyengine, yamechangia sana kuleta demorasia, kwa kiwango fulani, iliyosaidia kuwapo uhuru wa kusema na mtu kutoa mawazo yake kwa njia ya vyombo vya habari, ndiyo yaliyowapelekea waislamu wajitokeze hadharani na kutoa malalamiko yao dhidi ya Serikali iliyopo madarakani. Katika utawala wa awamu ya kwanza, hata kama waislam walikuwa wakihisi wanabaguliwa, basi walikuwa wakinung’unika kichini chini, hawakuthubutu kulalamika waziwazi, walipojaribu kufanya hivyo, walipambana na rungu la dola. Wengine miongoni mwao walitiwa magerezani na wengine walihamishwa kutoka eneo moja la nchi hii na kupeleka katika eneo jingine na kuwekewa vizuizi wasitoke katika eneo hilo.

KUCHANGANYA DINI NA SIASA

Serikali inawasakama bure waislamu ya kuwa wanachanganya dini na siasa, wakati ushahidi kutoka katika kitabu cha Dr. Sivalon unadhihirisha wazi wazi kuwa tokea kuasisiwa kwa Jamhuri ya Tanganyika na kisha muungano wa Tanzania, kanisa katoliki kwa ushirikiano wa kichini chini na Serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Hayati Mwalimu Nyerere, limekuwa likikoroga hasa, dini na siasa na siyo kuchanganya tu

Aidha, na Serikali yenyewe imekuwa, siku zote, ikichanganya siasa na dini kwa kulipendelea zaidi kanisa katoliki na hata mara nyingine kuliachia liingilie maamuzi ya Serikali kama kitabu cha Dkt. Sivalon kinavyothibitisha hayo. Kitendo cha kanisa katoliki serikali na chama tawala kunyamazia kimya na kutokanusha maelezo aliyoyatoa Dr. Sivolon katika kitabu chake hicho ni sababu tosha inayoyafanya yale yalioelezwa humo yaonekane kuwa ni ya kweli. Kuhusu kitabu hicho AL-Hajj Abuod Jumbe anaeleza: "Upitizi wa makini wa kitabu cha Dr.John C.Sivalon kiitwacho KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA, 1953 HADI 1985, unatoa habari za ndani zisizo za kawaida juu ya kampeni dhidi ya uislam". Uk -127. Al-Hajj Jumbe anaendelea kusema, "... kwa maneno mengine, kitabu hicho, kwa kiasi fulani, ni kukiri kwa yeye mwenyewe mwandishi, juu ya shughuli za kanisa la katoliki haliwezi kutenganishwa na Vaticano, na ambalo ubalozi wake ni moja katika balozi kongwe nchini Tanzania. Kwa sababu zisizoeleweka kitabu hicho kimeandikwa na kuchapishwa na waumini wa kanisa hilo. Yaliomo ndani ya kitabu hicho hayajakanushwa na wala kubishiwa na serikari ya muungano au ya Tanganyika au na CCM, huu ukiwa ni ushahidi kamili juu ya ukweli wa kukiri juu ya neno hilo.

Kwa sababu na malengo yo yote ya kutolewa kitabu hicho,na lazima ziwepo sababu za msingi za kufanya hivyo kitabu hiki ni ufunuo mzuri juu ya mbinu za chini kwa chini za kanisa katika medani ya kisiasa Tanzania". UK. 128 Akizidi kufahamisha yale yaliomo ndani ya kitabu hicho cha Dr. Sivalon, AL- Hajj Jumbe anasema, "... kinaeleza kwa vipi kanisa katoliki lilijenga njia ambazo ziliwawezesha kuwa na mahusiano ambayo kitabu hicho kinaeleza yaliyokuwa ya karibu kabisa na TANU wakati wa miaka ya kupigania uhuru. Kinaonesha kuwa wameshika karibu nafasi zote muhimu katika serikali mpya ya kiafrika ya Tanganyika". UK.128 Akiendelea kuchambua yale yaliomo katika kitabu hicho, Al-Hajj Jumbe anaendelea kueleza, "Kinaeleza ni vipi serekali ya Jamuhuri ya muungano ilirithi mmfumo huo na kuupanua katika mamlaka ya Muungano, pia, katika mambo yahusuyo Tanganyika". UK.128 ALL-Hajj Jumbe anaendelea, "Kwa wale viongozi, wawe wa kanisa, CCM au serikali ya muungano, ambao walikuwa wakipigia kelele kutenganishwa kwa siasa na dini, wana kazi ngumu ya kuelezea kwa umma kwa ujumla lakini wao wenyewe wakiwa ndio waendelezaji wakubwa wa hilo, wana kazi ngumu ya kuelezea kwa umma kwa ujumla lakini zaidi kwa waislamu.

Sivalon anaelezea juu ya mpango na njama zinaendelea zikishirikisha kanisa katoliki, chama (TANU- CCM) na serikili ya muungano." Uk. 128-129. Mwisho, Al- Hajj Jumbe anasema, "Tangu njama hizo ziwekwe wazi 1992 hapakuwa na kauli moja ya kupinga au kutolea maelezo juu ya jambo hilo. Huku ni kukiri kwa dhahiri juu ya mipango na njama za kanisa zianazofanywa hali zikiwa zinaeleweka na mkono wa chama na serekali zake". UK 129

WAJIBU WA SERIKALI

Waislamu wanalalamika. Wanadai wanapunjwa katika elimu ya juu na nafasi za uongozi serikalini, ushahidi wa kimazingira unathibitisha kuwa hakuna uwiano baina ya waislamu na wenzao wakristo katika elimu na mgawanyo wa madaraka serikalini. Na kitabu cha Dkt. John C. Sivalon kinadhihirisha kuwa kanisa katoliki limekuwa likishirikiana na serikali katika kuwadhibiti waislamu na kulipendelea kanisa hilo. Juu ya kwamba si serikali, chama, wala kanisa katoliki, halikukana maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hicho cha Dkt. Sivalon, serikali inakataa kukiri habari hizo za udini na wala haitaki kufanya uchunguzi wa kina katika kuelawa ukweli ulivyo, badala yake, serikali imekuwa ikitoa vitisho kwa waislamu pamoja na kutumia vyombo vya dola kuwadhibiti waislamu.

Mabavu yanaweza kunyamazisha harakati za waislamu kudai haki zao kwa muda tu; lakini hayawezi kuzizima harakati hizo kabisa. Ni wajibu wa serikali kuyachunguza kwa kina malalamiko hayo ya waislamu pamoja na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Kutumia mkong’oto hakusaidii kitu! katika huu mfumo wa vyama vyingi na upanuzi wa demokrasia ni wajibu wa serikali kusikiliza matatizao ya raia wake ili kupata ridhaa ya raia hao. Mwandishi na mwanafalsafa mashuhuri wa Tanzania marehemu Shaban Robart aliandika katika moja ya vitabu vyake vingi alivyovitunga, "Serikali iliyofaulu ulimwengu ni ile iliyotawala nyoyo za raia wake, raia hao wataipenda Serikali kama hivyo na kushirikiana nayo, lakini ikitawala viwiliwili vyao itabidi kusukumana nao". Basi ni vyema Serekali ikijitahidi kutaka kutawala nyoyo za waislamu na siyo kutawala viwiliwili vyao.

SWALI LA KWANZA SABABU YA WAISLAMU KULALAMIKA

Kwanini Waslamu wanalalamika? Dkt John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : Lakini kwa upande mwingine idadi kubwa ya wakristo wenye elimu walishindwa kushiriki wazi katika TANU kwani aidha walikuwa waalimu au watumishi wa Serikali. Serikali ya wakoloni walikataza kisheria kushiriki kwenye vyama vya siasa. Hata hivyo wakati wa uhuru wengi kati ya wakristo hao wenye elimu na waliokuwa wakifanya kazi Serikalini na walikuwa na nafasi nzuri zaidi kushika madaraka ya uongozi. Kwa hali hiyo walionekana hasa na Waislamu kama watu waliofaidi matunda ya uhuru bila kushiriki katika mapambano.

SWALI LA PILI NYERERE "WAKALA" WA KANISA KATOLIKI?

Jee, Mwalimu Julias Kambarage alikuwa ni ‘Wakala’ wa Kanisa Katoliki hapa Tanzania? Dkt. John C.Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. Sura ya pili, inaonesha jinsi uhusiano wa pekee ulivyojiimarisha na kukua kati ya viongozi wa chama na Serikali wakati wa mapambano ya uhuru. Uhusiano huo ulitokana na mfumo wa mfumo wa elimu katika kipindi cha Ukoloni, michango kadhaa ya Kanisa kwa kusaidia TANU na vyama vya kitume kiungo cha pekee kati ya Chama na Kanisa Katoliki. Uhusiano huo unaelezwa kwanza kama msingi wa kuelewa jinsi gani na kwa kiasi gani viongozi wa Kanisa Katoliki walivyoingilia kati maendeleo ya siasa hapa Tanzania. UK.5 2. "Nyerere ambaye mwenyewe ni mkatoliki, alikuwa na uhusiano wa karibu sana na viongozi fulani wa kanisa na hivyo alionekana kuwa ni kiungo kati ya Kanisa na Serikali". Uk.11 3. Mfano mzuri ni Marian College Shule hii ilianzishwa mwaka 1957 na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kwa lengo la kuwaelimisha wasichana. Ilikuwa ni shule ya pili yenye kidato cha 1V kwa wasichana hapa Tanzania. Ingawa shule hii ilijengwa na kanisa katoliki na iliendeshwa na Masista wa Shirika la Marykonoll na wanawake Waafrika, iligharimiwa kifedha na Kanisa. Mwalimu mkuu wa wakati ule wa 1957 alisema kuwa ule ulikuwa wakati muhimu sana Tanzani.

TANU ilikuwa imepiga hatua kubwa na ilikonekana dhahiri kwamba uhuru ungepatikana. Hivyo basi masista walisisitiza kwa wanafunzi kwamba wao ndio watakaokuwa viongozi wa baadaye. Nyerere mwenyewe alikuwa anaitembelea shule hiyo mara kwa mara kuwaelezea nafasi yao baada ya uhuru kapatikana. Hivyo walimu na wanafunzi walijua fika kwamba mabadiliko yalikuwa yanakuja na kwamba wangekuwa na mchango wa kufanya. Ukichunguza kwa makini utaona kuwa idadi kubwa ya viongozi wa kike wa chama na serikali ni wahitimu wa "Marian College". Katika orodha ya wahitimu 224 wa mwaka 61 hadi 65, tukichukua baadhi yao kama mfano tunapata matokeo yafuatayo :

Jedwali la tatu ;- Kazi za jumla ya Wahitimu 22 wa Marian College: KAZI IDADI YA WENYE KAZI HIYO Walimu Wakuu 3 Walimu wa Chuo Kikuu 2 Walimu wa Vyuo 1 Viongozi ngazi ya mikoa 3 Walimu 5 Viongozi ngazi ya Taifa 5 Daktari 1 Mwuguzi 1 Kiongozi, idara ya Baraza la Maaskofu (TEC) 1 Vile vile mmoja wa hao 22 ni mke wa kiongozi katika kamati kuu ya chama, mwingine ameolewa na afisa wa balozi Uk. 12- 13 4. "Nilipokuwa nikimhoji kiongozi mwingine wa Serikali nyumbani kwake nilipata kuona uhusiano uliopo kati ya wanawake hawa, walikuja wageni mara tatu wakati wa mazungumzo yetu, kila mara alinitambulisha kuwa mgeni huyo naye ni mmoja kati ya wahitimu wa "Marian College" kisha akanielezea kazi yake. Mmoja alikuwa Katibu Muhtasi, mwingine Mwalimu Mkuu na wa tatu alikuwa mfanyakazi wa shirika moja la Umoja wa Mataifa.

Wote hawa walikuwa ni viongozi wa ngazi za juu Serikalini. Mahojiano haya yalithibitisha yaliyokuwa yamesemwa na wengine kwamba hiki ni kikundi mashuhuri kanisani, chenye sauti katika mwelekeo wa kisiasa na pia chenye uhusiano wa karibu sana na kanisa katoliki. Kikundi hiki cha wanawake wasomi kimepatikana kwa njia ya elimu ya kanisa katoliki, na mshikamano wao unaoendelea hadi sasa katika shughuli mbali mbali za kanisa na za kawaida . Uk.14 5. "Mchango mkubwa ni Nyerere mwenyewe.

Yeye ni Mkristu na mtu wa kanisa mwenye uhusiano mkubwa na baadhi ya Maaskofu na Mapadri. Uk. 19 6. "Uhusiano kati ya kanisa katoliki na Nyerere ulikwisha kugusiwa, Ingawa alifundishwa mafundisho ya ukatoliki kule shule ya msingi Mwisenge na rafiki yake Oswald Marwa, hakubatizwa mpaka alipomaliza masomo ya sekondari Tabora. Alijiunga na mfumo wa elimu ya kanisa katoliki kma mwalimu baada ya kumaliza masomo yake Makerere.riwa kama mwalimu katika shule ya St.Mary's, kisha alipendekezwa kwa masomo ya juu na viongozi wa Kanisa Katoliki na ndipo akapelekwa Edingurgh, Scotland na serikali. (15) Baada ya kumaliza masomo yake 1952, alirudi Dar es Salaam ambapo alifundisha katika Sekondari ya Mt.Francis, Pugu. Wakati huo Padri Walsh wa shirika la White Fathers alikuwa amehamishiwa Dar es Salaam kuwa katibu mtendaji wa idara ya elimu ya Kanisa.

Watu hawa wawili walikuwa wakizungumza katika jumba la "White Fathers." Moja ya mazungumzo hayo bila shaka yalikuwa juu ya Nyerere kujihusisha kikamilifu na siasa ya kutetea uhuru". Uk 19. 7. "Nimekuwa nikiuelezea uhusiano kati ya Nyerere na Padri Walsh. Uhusiano huu ulikuwa ni zaidi ya ushauri au urafiki. Mara nyingi Padri Walsh kama katibu wa elimu wa Kanisa Katoliki alishauriana na Serikali kwa niaba ya TANU na Nyerere." 8. Hivyo, kutokana na Nyerere kuwa mkatoliki, na kuwa kiini cha kundi la watawala, alikuja kuwa kiungo muhimu kati ya Kanisa na Serikali. Uhusiano huo uliimarishwa zaidi na shughuli za viongozi muhimu wa Kanisa ambao walimsaidia Nyerere katika mambo ya siasa na nafasi yake katika kuiongoza TANU. Nafasi yake kwa masomo ya juu, msaada wa fedha na vinginevyo ni baadhi tu ya vitu vilivyofanywa na viongozi wa Kanisa Katoliki kwa niaba yake, wakimtetea kuwa kiongozi mwenye msimamo unaokubalika.

Uk. 21. 9. "Bi Hancock alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule ya wasichana Tabora mwaka 1931 na baadaye shule ya wasichana Mbeya. Hatimaye alikuwa mkaguzi wa elimu. Alikuwa mshabiki mkubwa wa TANU na rafiki wa familia ya Nyerere. Kwa kupitia kazi zake, alianzisha na kuendeleza uhusiano kati yake na watumishi wengi wa Serikali, wanawake kwa wanaume nchini kote. Mwaka 1963 alichaguliwa na maaskofu kusimamia maendeleo ya wanawake katika idara ya jamii, TEC. Bi. Hancock alisambaza shughuli hizi za maendeleo ya akina mama nchini kote. Alisisitiza ushirikiano wa wanawake wakatoliki katika baraza la U W T, moja ya jumuia za Chama. Alihimiza vikundi vya wanawake wakatoliki kujiunga pamoja kuleta maendeleo na kushiriki kikamilifu katika sera za Serikali na TANU". 10. Baada ya Nyerere kuwataka mapadri waishi vijijini, viongozi wa Kanisa kwa pamoja walitafuta njia ya kuitikia mwito huo. Ilikuwa dhahiri kwamba idadi ya mapadri waliohitajika kama alivyotaka Nyerere haikuwepo.

Hivyo katika mkutano wao wa mwaka 1970, maaskofu waliamua kwamba " makatekista, moja kwa moja wawe ufumbuzi wa muda na hao makatekista wapewe mafunzo maalumu kwa kazi hii." (uk 57) Mfano wa mafunzo ya aina hii kwa ajili ya makatekista wenye mwelekeo wa ujamaa yalitolewa na "Komuge Catechetical Training Centre" Mkurugenzi wa chuo hicho, wakati huo alisema kuwa mipango yake ilitegemea sana ile ya Bukumbi Catechetical School Mwanza. Ratiba ya masomo ilikuwa pamoja na Biblia, Dini, Liturjia, Sosiolojia, Historia ya Kanisa na mbinu za kufundisha.

Wanafunzi pia walikuwa na shughuli za kilimo cha pamoja licha ya kuwa na mashamba katika familia zao. Mashamba ya mifano yalikuwepo na mafunzo juu ya ufugaji bora yalitolewa. Misingi ya ujamaa ilitiliwa mkazo katika masomo na shughuli zao za pamoja. Mkurugenzi huyu aliunga sana mkono mawazo ya ujamaa na alisema, "Nilivutiwa sana na Nyerere na katika kufundisha kwangu nilitilia mkazo matendo ya Mitume" na mafundisho ya Kristu juu ya haki. Pale shuleni tulikuwa nalo shamba la pamoja na kila tu alikuwa anafanya kazi kijamaa hadi wakati wa kuvuna na hii ikawa ndio sera ya shule. Kila mwaka tulivuna mahindi, mboga na karanga vitu ambavyo tuligawana kijamaa na mtazamo wote kwa jumla ulikuwa kwamba ujamaa na ukiristu vitakwisha sana.

Makatekista vile vile walihimizwa kufundisha watu vijijini mwao falsafa ya ujamaa (58). Mkurugenzi huyu aliarifu kuwa ishara ya mafanikio ya mpango huo ilikuwa idadi ya makatekista walioshika madaraka ya Chama na Serikali vijijini. Alisema kwa wastani asilimia 70 ya wahitimu wote aidha wamekuwa makatibu au wenyeviti wa vijiji, makatibu kata au makatibu tarafa. Hakuna takwimu kuthibitisha jambo hili kwa jumla. Lakini kutokana na mahojiano yangu katika majimbo ya Arusha, Mwanza, Mbeya na Musoma, waliohojiwa walikiri kwamba wale makatekista waliopata mafunzo ya miaka miwili na kufanya kazi vijijini, wengi wao walishika nafasi za uongozi katika chama na Serikali. Uk. 44-45. 11.

Nyerere alimudu kuwatoa hofu na mashaka kiasi kwamba mwenyekiti wa R S A T alisema: "Ningependa kuongeza kuwa hata kama walikuwepo waliokuwa na wasi wasi juu ya itikadi ya miongozo hapa Tanzania kama nchi ambayo imepania kujenga maisha ya kisoshalisti walikuwa ni wachache. Pia tunayo imani na wewe kama kiongozi wa nchi hii, mjamaa halisi na mkristu safi, labda sasa kuliko wakati wowote ule. Matatizo yetu siyo juu yako wewe, Chama chako au Serikali. Haya yanatoka katika ngazi ya chini kabisa ambapo tabia za watu zinaweza kuingilia. 12. Mwisho, askofu mwingine alipendekeza : "Tunachotakiwa kufanya hivi sasa ni kufufua lile "Baraza la Wazee" Awali baraza hili lilitusaidia sana kwani badala ya kupiga makelele hadharani, baadhi yetu maaskofu tuliweza kukutana na Nyerere na kutatua matatizo yetu kwa mila na desturi za kiafrika".

Kwa sababu hiyo basi, mambo fulani fulani yalisaidia kuelekeza msimamo wa maaskofu. Kwanza walidai kuwa hawakuhusikshwa kikamilifu katika muundo wa utume huo, Pili walijua kwa mapana na marefu hali ilivyokuwa huko Uganda na hivyo walithamini sana amani iliyokuwepo hapa Tanzania. Serikali na hasa Nyerere kwa kiasi kikubwa walipewa heko kwa utulivu huo ambao uliruhusu Kanisa Katoliki likue na kustawi. Jambo la tatu, ni kwamba maaskofu waliridhika na hali ilivyokuwa kwani walijiona kuwa waliweza kuwasiliana na viongozi wa Serikali kutatua matatizo yaliyojitokeza bila ulazima wa kushirikisha watu wa kawaida. Uk . 74 13. Mwisho, sura hii imeonyesha umuhimu wa uhusiano kati ya Nyerere na maaskofu. Alikuwa kama kiungo muhimu katika utume wao.

Katika mapambano ya miaka ya 1970, mara nyingi Nyerere aliwahimiza maaskofu kujiweka sambamba na ujamaa. Lakini kwa wakati huo alikuwa amebadilika msimamo wake. Alitoa baraka zake na kuwashukuru maaskofu kwa mawazo yao. Kwa maelekezo yake, mashirika ya dini yalisamehewa ushuru wa forodha na kodi ya mauzo kwa bidhaa walizokuwa wanaziagiza kutoka ng'ambo. Baadhi ya viongzi wa Kanisa Katoliki walipewa vibali vya Rais kuingiza vitu kutoka Kenya bila ushuru ingawa mpaka kati ya nchi hizi mbili ulikuwa umefungwa. Maagizo haya ya Nyerere yanaonyesha jinsi gani alivyothamini juhudi za Kanisa katika kufufua uchumi. Ama kwa hakika, ushirikiano huo uliruhusu viongozi wa Kanisa Katoliki kuwa na nguvu za kiuchumi wakati taifa likiwa kwenye hali mbaya. Uk 76. 14. Uongozi wa Kanisa Katoliki katika juhudi za kuelekeza ujamaa wa Kitanzania, ulihusika moja kwa moja na kikundi hiki cha wasomi. Mwanzo wa kipindi kati ya 1953 na 1966, uhusiano ulikwishaanza na kuimarika zaidi wakati wa mapambano ya uhuru hadi matokeo yake. Mahojiano yangu yamethibitisha kwamba licha ya uhusiano wa kawaida uliokuwepo kati ya viongozi wakatoliki wa Chama Serikali na uongozi wa Kanisa, mshikamano maalum umejitokeza hasa ukitilia maanani michango ya Kanisa katika kupatikana kwa uhuru. Michango hiyo ilikuwa hasa kwenye nyanja za elimu na mafunzo ya uongozi wa namna moja au nyingine. Licha ya kuonekana kasaidia kuleta uhuru, michango hiyo imesaidia kujenga na kuimarisha uhusiano wa kudumu kati ya uongozi wa Kanisa Katoliki na watawala wa Tanzania huru. Mshikamano huo mpaka sasa unaendelea. Hapana shaka kwamba Rais mstaafu Nyerere, ikiwa kiongozi mkuu wa Serikali, alichangia sana hali hiyo. Kanisa Katoliki lilimpendekeza kwa masomo ya juu zaidi na lilitoa misaada mingine. Alifanya kazi katika mfumo wa elimu wa Kikatoliki hapa Tanzania na matarajio yake kuhusu siasa yalitiwa moyo na baadhi ya mapadri na maaskofu ambao pia waliwaondolea wasi wasi wakoloni juu yake. Daima alitambuliwa na viongozi hawa kama mtu mwadilifu na mkristu safi. Kutokana na hali hiyo basi, uhusiano mkubwa kati yake na uongozi wa Kanisa ulisaidia nafsi ya viongozi wa Kanisa kuelekeza maana ya siasa ya ujamaa." Uk 77 - 78 15. Wakati huu mgumu, uliona kukua kwa nafasi ya viongozi wa kanisa katoliki katika maendeleo ya nchi kwa sababu ya uhusiano, wao na mashirika ya nje ambayo yalikuwa yakitoa misaada. Wakuu wa Serikali, wakiwa wamekabiliwa na matatizo makubwa kiuchumi, walikiri kwamba viongozi hawa wa kanisa walikuwa na mchango mkubwa kwa misaada ya dharura na katika kufufua uchumi wa taifa. Kutokana na hali hii viongozi wa kanisa walikuja kuwa na nguvu zaidi za kiuchumi. Lakini wakati huo huo uongozi wa kanisa nao ulikuja kutambua kuwa unamtegemea Rais Nyerere kama mlezi na mlinzi mkuu wa amani iliyowaruhusu kupata maendeleo ya namna nyingi.
Uk 79

SWALI LA TATU KANISA LILITOA MSAADA ILI KUELEKEZA SIASA TANZANIA

Jee Kanisa katoliki lilitoa misaada kwa lengo la kuelekeza siasa Tanzania? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. Kanisa Katoliki lilitoa michango kadhaa katika mapambano ya uhuru. Michango hiyo ilisaidia kuimarisha uhusiano kati ya viongozi wa kanisa wa Chama na kanisa. Huo uhusiano ukaweka viongozi wa kanisa katika nafasi nzuri ya kuelekeza maendeleo ya siasa ya Tanzania. Uk 9. 2. Licha ya hali ya kutatanisha kwa watumishi wakristo wa kanisa pamoja na viongozi kadhaa wa Kanisa. Waliohojiwa wamekubali kuwa viongozi wa kanisa katoliki na idara zake walitoa michango mbali mbali iliyosaidia kuleta uhuru. Vile vile, michango hiyo iliimarisha uhusiano kati ya viongozi wa kanisa katoliki na wa Serikali na Chama. Uk 10. 3. Hayo ndiyo yaliyotajwa katika maelezo ya wengi walihojiwa kuhusu michango ya kanisa katika mapambano ya uhuru. Na wakati huo huo michango hiyo imewezesha viongozi wa kanisa kujenga uhusiano kati yao na viongozi wa Chama na Serikali. Huo uhusiano umewapa viongozi wa kanisa nafasi ya pekee ya kuelekeza jinsi siasa ya ujamaa ilivyokuja kueleweka na kutekelezwa na viongozi wa Serikali.
Uk 24-25.

 

 

SWALI LA NNE KANISA KATOLIKI LILIMWUNGA MKONO NYERERE KWA FAIDA YA KANISA HILO

Jee, Kanisa Katoliki lilimwuunga mkono Nyerere na kumsaidia kwa ajili ya faida ya Kanisa hilo? Dkt. John C. Sivalon katika kitabu chake, anaeleza : 1. Maryknoll fathers wamekubali kulipa tiketi ya kwenda Amerika na kurudi England kwa vile huyu ni kiongozi wa kikatoliki, mtu kutoka jimbo la Musoma ambaye anaheshimiwa na mapadri wetu. Kwa vile ni nia ya Serikali ya Waingereza kuwaandaa wenyeji kwa madaraka, Shirika la Maryknoll limeona kutowa msaada wowote linaoweza kuwapatia viongozi wa kikatoliki utakuwa ni kulisaidia Kanisa. Huyu ni mkatoliki mzurti, mtu mwenye msimamo wa busara katika kutaka kuwaelekeza watu wake kwenye uhuru kamili. Hakosi kuwa na habari kwamba kuna wapinzani fulani wenye siasa kali zaidi katika Chama chake lakini anajitahidi kukiongoza kwa njia inayokubalika. Chama hiki kimeandikishwa rasmi serikalini na wala sio chama cha siri (17) : Uk 21. 2. "Katika kueleza uhusiano maalum baina ya viongozi wa Kanisa Katoliki na viongozi wa Chama na Serikali, tumeshagusia kidogo nia ya viongozi wa Kanisa katika kujenga uhusiano huo kwa njia ya utume wao wa kijamii. Kwa mfano, katika maneno ya yule askofu aliyekaririwa katika sura ya pili, alisisitiza kuwa lengo moja la mafundisho ya uongozi kwa walei lilikuwa kuzuia Chama cha kupigania uhuru kisianguke mikononi mwa mawakala wasiofaa. Katika barua iliyopelekwa Vatikano sababu moja wapo iliyotajwa ya kumuunga mkono Nyerere ilikuwa kwamba itakuwa kwa faida ya Kanisa siku zijazo. Hofu ya siasa ya ukomunisti ilikuwa sababu muhimu ya kuanzisha na kuendeleza vyama vya kitume kama "Social Guilds." Uk. 26. 3. "Kwa kumalizia, jambo lingine lililoonyesha ya kuwa utawala wa Serikali ulitambua kuunga mkono siasa ya ujamaa kwa baadhi ya viongozi wakatoliki lilitokea mnano mwaka 1974. Wakati huo Serikali ilikuwa inaanzisha shule ya sekondari kwa wasichana. Mpango wake wa masomo ulibuniwa ili ulingane na maisha ya vijijini na siasa ya ujamaa. Nyerere binafsi aliwaomba masista wa Shirika la Maryknoll, ambao ndio walikuwa waanzilishi wa "Marian College, "kuongoza shule hiyo. Ulipowadia wakati wa kufundisha na kuwajenga wasichana hao kijamaa, Nyerere aliwageukia tena masista Wakatoliki ambao ndio waliwafundisha akina mama wengi katika kundi la viongozi wa Chama na Serikali." Uk 50 --

SWALI LA TANO SIASA YA UJAMAA NI MSIMAMO WA KIKRISTO

Jee, Ujamaa ni siasa iliyo na msimano wa Kikristo? Dkt. John Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. "Barua hiyo inadhihirisha kuunga mkono ujamaa kwa kuwa ni siasa iliyo na misimamo wa kikristu hasa kwa kutetea haki, kujenga umoja na kutafuta usawa". uk 40 2. "Baada ya miezi minne, msimamo huo ulirudiwa tena na Pd. Robert Rweyemamu aliyekuwa katibu mkuu wa TEC. Alisisitiza jinsi Papulorum Progressio na Azimio la Arusha vilivyofanana. Aliviita mapacha. Uk. 42 3. Kundi la pili ni wale waliounga mkono. Kwa mfano Padri X. Katika mahojiano yangu naye. Huyo alisema kwamba aliamini kabisa kuwa ujamaa ni mfumo wa kikristu wa uchumi na siasa. Aliamini kwamba ujamaa una miongozo iwezeshayo ufalme wa Mungu kujengwa hapa duniani. Kutokana na imani hii aliona umuhimu wa kuanzisha kijiji cha ujamaa katika eneo la makao makuu ya parokia yake. Alifanya hivyo kwa kushirikiana na katekista ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti pamoja na majirani wachache. Uk. 43. 4. Idadi kubwa ya viongozi hawa walikubali kuwa misingi ya ujamaa ilikuwa sawa na mafundisho ya kikatoliki" Uk. 43. 5."Azimio la mkutano huo wa mwaka wa Semina za Mafunzo kuhusu ujamaa na maendeleo kitaifa lilisema : "Viongozi wa Kanisa wanaombwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii vijijini kwa uwezo wao wote na kufuata mipango ya Serikali". Kanisa linaombwa kusaidia kuwaelimisha watu kwa mtazamo mpya na maadili ya kikristu yaliyomo katika siasa ya ujamaa ambayo hutegemewa sana na maendeleo ya kisiasa (61) Ingawa hakukuwa na mipango madhubuti iliyoandaliwa kwa utekelezaji wa azimio hili, viongozi wote wa kitaifa katika vyama viwili vya walei walikuwa pia ni viongozi wa Serikali pamoja na chama. Hivyo katika uongozi wao wa vyama hivi, hawakusita kutilia mkazo siasa ya ujamaa. Pia, hata kule kujitokeza kwao katika uongozi wa Kanisa kulitia muhuri fulani uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na Chama. Pamoja na hayo, maaskofu nao waliamuru "Baraza la Walei" liwe na mpango kabambe kwa ajili ya vijiji vya ujamaa. Katika mkutano wao wa mwaka 1971 walisema : Wanabaraza katika vikundi wanapaswa kuamua kuanziasha vijiji vya ujamaa kwa maadili ya kikiristu ili viwe ni mfano wa kuigwa na vingine

(62). Uk 49SWALI LA SITA KIJIJI CHA UJAMAA NI PAHALI PAZURI KUENENZEA UKRISTO?

Jee, Kanisa Katoliki liliunga mkono kuanzishwa vijiji vya ujamaa kwa sababu kijiji cha Ujamaa ni pahali pazuri pa kueneza ukristo? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. "Kanisa halijawahi kuwa na nafasi nzuri kama hii katika kutekeleza shughuli zake katika jamii ya mchanganyiko. Ujamaa unaonekana kuwa na msimamo sawa sawa na ule wa Kanisa. Kwa hivyo basi, unalingana na mafundisho ya Kanisa na uko karibu sambamba na yale yaliyotajwa katika "Mater et Maistra. "Katika jumuiya ya watu wenye dini mbali mbali kama ilivyo Tanganyika, Kanisa lisingeweza kuomba nafasi zidi ya hiyo (37) Ulikuwa msimamo wa Pd. Robinson pamoja na mapadri wengine wengi kwamba ujamaa kama ilivyoelezwa na Nyerere ulikaribiana sana na mafundisho rasmi ya Kanisa Katoliki juu ya siasa na uchumi. UK 34. 2. Askofu ambaye alikuwa mfano wa kundi la pili katika jimbo lake ni Christopher Mwoleka. Aliona ujamaa kama nafasi ya pekee kwa Kanisa Katoliki na alisisitiza mchango wa Kanisa katika utekelezaji wake. Akifafanua jukumu hilo kama la kuelimisha raia mpaka wafikie kiwango cha kujenga ujamaa kamili. Aliandika. : Katika historia Kanisa halijapata nafasi kama hii ya kuonyesha kwa vitendo yale ambayo limekuwa likihubiri kwa karne nyingi. Kijiji ambapo kwa makusudi watu wake wanahimizwa kuwa sehemu ya mwili mmoja ni mahali pazuri kwa ukristu kufanikiwa kuliko kijiji cha kawaida ambapo watu wake wana dhamira mbali mbali za ushindani na kunyonyana. Hapa Tanzania uwanja umekwisha tayarishwa. Kinachobaki ni kueneza na kukuza Injili. Hivyo vijijini wakiisha waanzishe jumuiya ziwe kama sumaku kuwavuta wengine. Jumuiya ya kikiristu lazima iwe msukumo wa upendo na huduma kwa wengine (55). Askofu Mwoleka alifuata maadili haya kuwataka wakristu wote waishi vijijini ili wanufaike na maisha ya kidini huko. Yeye mwenyewe alijiunga na kijiji cha Nyamihanga. Aliwatafuta na kuwaitia moyo viongozi wa Kanisa ambao alitumaini wangeishi vijijini kama majirani wa wanakijiji. Juhudi hizi ingawa zilipata upinzani kutoka kwa viongozi wengine wa dini jimboni mwake zilifanikiwa kiasi. Mawakala ya Ujamaa na Jumuia za Kikiristu imebami kuwa mwaka 1976 kulikuwa na viongozi kumi na mmoja tu ambao ambao waliishi vijijini moja kwa moja. Uk 56

 

 

SWALI LA SABA KANISA LAHAMASISHA WAKATOLIKI KUWACHAGUA WAKATOLIKI WENZAO

Jee, Kanisa Katoliki, kwa kupitia katika taasisi zake huandaaa mikakati ya siri, kuwahamasisha wakatoliki kuwapigia kura wakatoliki wenzao katika chaguzi za kugombania ubunge? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. "SSY" ilimaliza mapendekezo yake kuhusu ujamaa kwa kutaka iundwe kamati ya kutafiti uwezekano, madhara na matatizo ya kuliunda upya Kanisa Katoliki katika maadili ya ujamaa wa kweli wa kikristu (63). Mwishowe, "SSY" ilitoa msisitizo juu ya jukumu la walei katika jamii. Haya yalitokea wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 1970. Ingawa hakuna utafiti uliofanywa kuonyesha uhusiano kati ya SSY na wabunge waliochaguliwa, mmoja kati ya watu waliohojiwa alidai kuwa : SSY na Baraza vimeleta msisimko huu ambao umewaamsha Wakatoliki kupigania viti katika uchaguzi wa wabunge na mimi nikiwa mmoja wao. Baadaye huko bungeni tulifanya utafiti usio rasmi na kugundua kwamba 75% ya waliochaguliwa walikuwa wakristu na kati ya hao 70 % walikuwa wakatoliki (64). Uk 49 2. "Hivyo basi "SSY" ilibainisha kuungwa mkono kwa ujamaa na viongozi wa Kanisa na muhimu pia kuwashirikisha walei wakati huo maalum katika historia ya ujamaa wa Tanzania. Kilikuwa ni chombo cha kuwaelimisha walei kuhusu mafundisho ya Kanisa juu ya Jamii. Pia iliwashawishi kugombea nafsi za uongozi Serikalini ambapo wangeweza kuathiri tafsiri ya ujamaa" Uk 49 -50

SWALI LA NANE MAAMUZI YA SERIKALI YAFANANA NA MAFUNDISHO YA KANISA KATOLIKI

Jee, Kanisa Katoliki lilimuunga mkono Nyerere na kumsaidia kwa ajili ya faida ya kanisa hilo? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1."Kwa hiyo, makanisa ya kikristu yaliweza kujivunia kuwa yamesaidia kuelimisha, kwa ngazi moja ama nyingine, idadi kubwa ya wale waliokuja kuwa viongozi wa Serikali na Chama. Kwa njia hiyo kulitokea nafasi kubwa ya kukuza uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa. Na wa Serikali na Chama. Uhusiano huu sio kwamba ulikomea darasani tu, bali unaendelea hata mpaka sasa kati ya wanafunzi kwa wanafunzi na walimu kwa wanafunzi.Uk 12. 2. "Muhimu zaidi ni kwamba shughuli na mazingira katika shule za bweni zimewezesha hadi sasa kukua kwa uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa na wa Serikali na Chama. Hali hii imefanya matendo, msimamo na uamuzi wa viongozi wa Serikali ufanane mara kwa mara kwa namna moja au nyingine na mafundisho na mwelekeo wa Kanisa". Uk 16 3."Kwa namna nyingi St. Mary`s na St. Francis ya Pugu zilichangia uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa Katoliki na wale wa Serikali. Kwanza vyombo hivi vya Kanisa Katoliki vilitoa elimu iliyowasaidia hao wahitimu kufikia ngazi hizi za uongozi. Pili, urafiki kati ya walimu wa St. Mary`s na St. Francis pamoja na urafiki kati ya wanafunzi wa vyuo hivi viwili ulichangia mshikamano wa viongozi Serikalini. Tatu, mawazo na fikra za watu hao juu ya ujamaa yalielekezwa na elimu yao ya Katoliki.

Uk. 16 SWALI LA TISA KANISA KATOLIKI LATAKA KUWEKA VIONGOZI WAKATOLIKI KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Jee, Ni mkakati kuweka viongozi wakatoliki katika nchi za Afrika Mashariki? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : Zaidi ya hayo kulikuwa na mpango wa kuanzisha Chuo cha Maendeleo ya jamii Tanzania. Chuo cha Maendeleo ya Jamii Nyegezi kilianzishwa na White Fathers kati ya vyuo vitatu vilivyokusudiwa kwa Afrika. Ilikusudiwa kwamba vyuo hivi vingetoa wanafunzi kwenda kwenye "International Institute" huko London, Chuo hiki kilichofahamika kama "Claver House" kule London, kilikuwa chini ya uongozi wa Padri Paul Crane, S.J. Nia ya vyuo hivi ilikuwa kuwaandaa viongozi katika sayasi ya kijamii na mafundisho ya Kanisa Katoliki. Walipokea wanafunzi wenye elimu ya darasa la kumi na mbili au kiwango kama hicho. Wanafunzi hawa hawakuchukuliwa moja kwa moja kutoka vyuoni, ilibidi wawe wameajiriwa serikalini, kwenye mashirika ama kwenye kampuni za watu binafsi. Padri Crane ambaye alitembelea Tanzania 1959 alidhihirisha madhumuni ya vikundi hivi vya kijamii kwa maneno yafuatayo : "Tatizo la Afrika ni kwamba watu wasiofaa wamewekwa katika nafasi za utawala. Tutaweza vipi kuweka watu wanaostahili katika nafasi hizi? Lazima tujitahidi kadiri ya uwezo wetu kupata wasomi wakatoliki ambao watashika nafasi muhimu kwenye ngazi zote za kijamii. Wakatoliki wetu walei wajitahidi kushika nafasi hizi. Tutaweza kuwaingiza kwenye nafasi hizi za uongozi wa njia ya kujenga vikundi vidogo vidogo vya wasomi wakatoliki …(21)" Uk 23

SWALI LA KUMI KANISA KATOLIKI LAUONA UISLAMU NI TISHIO KWA UKRISTO

Jee, Kanisa Katoliki pamoja na maaskofu waliuona Uislamu kuwa ni adui na tishio kwa ukristo? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. "Kwa upande mwingine lakini Maaskofu hao waliendelea kuuona Uislamu na falsafa ya Marx kama tishio" Uk 32 2. "Lakini, hata Pd. Robinson alikuwa na wasi wasi kama siasa ya ujamaa ingebaki na maana hiyo. Alihofia. Kama alivyojieleza, dini ya Uislamu na siasa ya ukomunisti. Kwanza, kuhusu Uislamu, alieleza : " Kuenea kwa dini ya Uislamu ni kwamba wakati makanisa ya kikristu yanajitahidi kuishi kwa uelewano na kushirikiana katika jamii ya mchanganyiko wa watu mbali mbali kwa kuheshimu uhuru wa mtu kufuata dini apendayo na mgawanyiko wa mamlaka ya serikali na dini, waislamu wanaonekana kuitumia nafasi hiyo kujinufaisha kidini na kisiasa wakitumia nafasi yao kudhoofisha makanisa ya kikristu. (38) 3. "Hali ya wasi wasi pia ilidhihirika katika idara hiyo kuhusu Uislamu. Ripoti moja ilisema hivi : Uislamu unazidi kuleta matatizo. Waislamu wamefaulu sana katika vyombo vya juu walijaribu kuleta maang`amizi yao huku wakifaidika na huduma zetu za kijamii, bila kukubaliana na masharti ya ushirikiano katika mfumo wa wengi jinsi ilivyotajwa kwenye Unity and Freedom. (54) Inaendelea kueleza jinsi Waislamu walivyokuwa wakijizatiti kuwa jumuiya kubwa, jumuiya kubwa, jambo ambalo lilikuwa ni hatari kubwa kwa hali ya Wakiristu baadaye. Ilionya kuhusu mkutano wa baadaye kati ya viongozi wa Bohora, Ismailia, Ithnasheri na Sunni. Kuletwa kwa makao makuu ya Chama cha Ustawi wa Waislamu hapa Dar es Salaam mwaka 1961 kulitajwa kama tishio lingine. Kufuatana na ripoti hii, ziara ya Masheikh kutoka Misri ambayo yalidhaminiwa na Mortamar (Pan Islamic Congress) yaliogopesha sana. Sehemu hii ya ripoti inamalizia kwa kusema kuwa tayari Waislamu walikuwa wameanza kuwashambulia Wakiristu. Jambo muhimu zaidi ni kwamba ripoti hii inaeleza mikakati ya kupambana na hatari hii. Ilipendekezwa kuwa kazi hii ifanywe na makatekista waafrika wenye ujuzi wa hali ya juu. Hata hivyo kutokana na hisia za jumuiya ya Waislamu ripoti inasema : Makatekista hao lazima waweze kufanya kazi katika idara za maendeleo ya jamii vijijini, iwe ni katika kilimo au katika shughuli nyingine za maendeleo kama vile ujenzi wa nyumba, bara bara n. k. (46) Hivyo kutokana na kazi ya idara ya mambo ya dini ya TEC kwa wastani, watenda kazi wote katika Kanisa Katoliki na jumuia zake walielimishwa juu ya hatari za ukomunisti na uislamu kama zilivyodhaniwa na viongozi wa Kanisa. Hii siyo kusema kwamba Wakatoliki wote walikubaliana na msimamo huu. Bali ni kwamba viongozi wa ngazi za juu waliohusika na utume wa Kanisa wa kijamii, kitaifa walijaribu kutumia utume huo kama mkakati wa kupambana na yaliyodhaniwa kuwa maadui wa Kanisa Ukomunisti na Uislamu " Uk 37 4."Licha ya hayo: Miongo hiyo mitatu toka mwaka 1952 hadi 1985 imefunuliwa miongozo ya kimsingi ya utume wa kijamii wa viongozi wa Kanisa Katoliki. Kwanza kwa muda wote maaskofu wameonesha hali ya wasi wasi juu ya kuenea kwa falsafa ya Marx pamoja na Uislamu. Pili, katika kipindi cha toka 1969 hadi 1975 walisita sana walipoona jinsi watu wengine walivyokuwa wanauelewa mwongozo na uelezaji wake juu ya demokrasia. Pia walipinga vikali. Walioona siasa hiyo ya demokrasia ikianza kuingilia utawala wao wa Kanisa." Uk 80

SWALI LA KUMI NA MOJA KANISA KATOLIKI LASHIRIKINA NA SERIKALI KUUDHIBITI UISLAMU

Jee, Kanisa Katoliki lilijenga uhusiano na Serikali kwa ajili ya kuudhibiti Uislamu? Dkt. John Sivalon katika kitabu chake, anaeleza : 1. Baada ya hayo nitaendelea kueleza katika sura ya tatu jinsi maaskofu na viongozi wengine wa ngazi za juu ya kanisa walivyoelewa utume wao wa kijamii yaani shughuli zile zote za kanisa zilizokuwa zinahusu wazi wazi siasa, uchumi, elimu na huduma nyingine za kijamii. Kwa kuchunguza barua za kichungaji za maaskofu za 1953 hadi 1966 na miongozo ya Baraza la Maaskofu wa Tanzania (TEC) kipindi hiki, itaonyeshwa kuwa hao viongozi wa Kanisa Katoliki walielewa nia ya utume huo kuwa hasa ni kuhami nafasi ya Kanisa katika jamii ya Tanzania. Walifanya hivi hasa wakizingatia ukuaji wa Ukomunisti na Uislamu. Uk 5-6 2. Katika sura ya tatu, nitaendelea kuchambua huduma ya kijamii katika Kanisa wakati huo kwa kuzingatia mafundisho ya maaskofu wa Tanzania kati ya mwaka 1953 - 1966. Mafundisho hayo yanaeleza rasmi lengo na madhumuni ya utume wa kijamii wa viongozi wa Kanisa. Itaonyeshwa kuwa viongozi wa Kanisa walikusudia kujenga uhusiano na viongozi wa Serikali ili wawe na nafasi nzuri katika kujihami dhidi ya uenezaji wa falsafa ya Marx na Uislamu. Uk 25 3. Lengo kubwa la utume wa kijamii wa viongozi wa Kanisa Katoliki kutoka mwaka 1953 hadi 1966 limekua likilinda nafasi ya Kanisa katika jamii kwa ujumla kwa kupinga kuenea kwa falsafa ya Kanisa katika jamii kwa ujumla kwa kupinga kuenea kwa falsafa ya Marx hapa Tanzania. Viongozi wakubwa wa Kanisa kwa kuangalia mienendo ya watu fulani na mwelekeo mwingine wa Chama na Serikali waliamini kuwa siasa ya Umarx ilikuwa imeshaanza kuota mizizi hapa Tanzania. Waliona kuwa utume wao wa kijamii ndio njia bora kuzuia kuenea kwake. Hali kadhalika itaonyeshwa kwamba viongozi hao hao walitumia utume wao wa kijamii kuhami nafasi ya Kanisa katika kupinga kuenea kwa dini ya Kiislamu. Kwa kifupi viongozi hao waliona kuwa walikuwepo maadui wawili wa Kanisa hapa Tanzania, yaani Uislamu na Umarx. Waliamua kutumia utume wao wa kijamii kama mkakati wa pekee kupambana na haya mawili. Uk 26 4. Kama ilivyoelezwa katika sura ya pili viongozi wa Serikali na Chama. Walitumia uhusiano huo kupatikana na mabadiliko yaliyotajwa hapo juu. Katika mafundisho rasmi mengine ya Kanisa kwa wakati ule msimamo wa Kanisa na msimamo wa ujamaa kama Nyerere alivyoueleza vilikubaliwa kuwa sambamba. Pd. Robinson alisilisitiza kuwa kuunga mkono ujamaa kwa viongozi wa Kanisa kulikuwa ni njia pekee ya kuzuia siasa ya ujamaa isibadilike.Vile vile alihofia kuenea kwa Uislamu na alishauri kutumia utume wa kijamii kama mkakati wa kuhami nafasi ya Kanisa katika jamii ya jamii ya Tanzania. Uk 38.

 

 

SWALI LA KUMI NA MBILI VATIKANO YAKUBALI KANISA KATOLIKI TANZANIA LUMWUUNGE MKONO NYERERE KWA FAIDA YA KANISA HILO

Jee, Vaticano, ambayo ndiyo Makao Makuu ya Kanisa katoliki lilikubali Kanisa Katoliki Tanzania limwunge mkono Nyerere kwa ajili ya faida siyo ya nchi bali ya Kanisa hilo? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : Katika kueleza uhusiano maalumu baina ya viongozi wa Kanisa Katoliki na viongozi wa Chama na Serikali, tumeshagusia kidogo nia ya viongozi wa Kanisa katika kujenga uhusiano huo kwa njia ya utume wao wa kijamii. Kwa mfano, katika maneno ya yule askofu aliyekaririwa katika sura ya pili, alisisitiza kuwa lengo moja la mafundisho ya uongozi kwa walei lilikuwa kuzuia Chama cha kupigania uhuru kisianguke mikononi mwa mwawakala wasiofaa. Katika barua iliyopelekwa Vatikano sababu moja wapo iliyotajwa ya kumuunga mkono Nyerere ilikuwa kwamba itakuwa kwa faida ya Kanisa siku zijazo.

SWALI LA KUMI NA TATU KANISA KATOLIKI LILISHINDWA KUIKOSOA SERIKALI ILI KULIPA FADHILA

Jee, Kanisa Katoliki lilishindwa kuikosoa Serikali kwa ajili ya kulipa fadhila kwa Serikali ? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake anaeleza : 1. Nia yangu katika sura hii ni kuchunguza baadhi ya mawazo ya viongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu hali hiyo ya kuanguka kwa uchumi, katika sehemu ya pili nitazungumzia msimamo wa uongozi wa Kanisa kufuatana na mafundisho ya maaskofu wakatoliki. Sehemu ya tatu itahusika na hisia za viongozi wa Kanisa waliosita kuikosoa serikali wazi wazi kwa vile uongozi wa juu wa Kanisa tayari ulikuwa katika uelewano mkubwa na utawala wa Serikali. Uk . 62. 2. Pili, Kanisa liliruhusiwa na Serikali kuingiza vitu vingi nchini bila ya ushuru wala kodi. Vitu vya miradi ya maendeleo pamoja na vile vya ujenzi vilianza kuagizwa na mwishoni hata mahitaji ya kawaida ya viongozi wa Kanisa. Mambo yote haya yalipunguza madai ya hali ngumu kwa viongozi hao wa Kanisa na kuwaweka katika nafasi yenye nguvu ya kiuchumi. Hiyo ilikuwa sababu nyingine iliyowafanya viongozi hao wa Kanisa wasite kukosoa watawala wa Serikali. Uk 68.

HITIMISHO

Wengi wamesikia jina la Shaaban Robert. Baadhi ya barabara na shule katika nchi zimepewa jina lake. Lakini sio wote wanaomfahamu nani Shaaban Robert! Huenda hata wale wanaokanyaga barabara au wanaosoma shule zilizopewa jina lake wasimwelewe mtu huyo! Shaaban Robert ni mwanafasihi mahiri na mwanafalsafa aliyebobea wa nchi hii, ambaye hatutakosea tukisema aliishi kabla ya wakati wake. Johari za hekima na vito vya busara vilivyojaa katika maandishi yake mbali mbali huhitaji vichwa vitulivu na akili pambanuzi kuweza kuzingatia. Moja katika almasi nyingi zilizomo katika utunzi wake ni ile kauli isemayo: "Serikali iliyofaulu ulimwenguni ni ile iliyotawala nyoyo za raia wake na siyo viwiliwili vyao" Maneno haya ingawa ni mafupi na yametamkwa na mswahili, lakini ni maneno mazito, yenye maana kubwa na yanayosheheni ukweli ndani yake. Serikali inayotawala kwa uadilifu itapendwa na raia wake na, kwa hivyo, itafanikiwa kutawala nyoyo za raia hao. Lakini serikali inayowabagua raia wake, itachukiwa na raia hao, na itajijengea upinzani nao. Itakuwa mara kwa mara ikiwapa mkong'oto raia hao na kuzidisha uhasama baina yao

 

 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template