Ponda ang’ang’aniwa. - Msamaa.
Headlines News :
Home » » Ponda ang’ang’aniwa.

Ponda ang’ang’aniwa.

Written By Unknown on Friday, April 5, 2013 | 1:42 PM

Ponda ang’ang’aniwa.

na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi ya sh milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam iwaone wana hatia kwa mujibu wa kesi inayowakabili na iwahukumu kwa mujibu wa sheria.
Katika kesi hiyo, Jamhuri inawakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali, Tumaini Kweka na Jessy Peter ambao waliwasilisha ombi hilo kwa njia ya maandishi mahakamani hapo jana kama walivyoamriwa na hakimu mkazi Victoria Nongwa Machi 21 mwaka huu.
Hakimu Nongwa alizitaka pande zote katika kesi hiyo ziwasilishe majumuisho yao ya mwisho yanayoomba mahakama iwaone washitakiwa wana hatia au la.
Wakili Kweka aliikumbusha mahakama kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kosa la kula njama kutenda kosa, kuingia kwa jinai, kujimilikisha ardhi ya kiwanja cha Chang’ombe Markas kinyume na sheria, wizi wa malighafi zenye thamani ya sh milioni 59 na kosa la uchochezi linalomkabili Ponda na mshitakiwa wa tano Mkadamu Swallehe.
Alidai katika kuthibitisha kesi yao waliweza kuleta jumla ya mashahidi 16 ambapo shahidi wa kwanza, tatu na nne waliieleza mahakama kuwa wao wanafanya kazi katika Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata).
Kwamba waliieleza mahakama kuwa eneo la Markas lilikuwa ni mali ya Bakwata, lakini ikaamua kulibadilisha na Kampuni ya Agritanza Ltd ambaye ndiye mmiliki halali wa eneo hilo na si mali ya Waislamu.
“Jamhuri imeweza kuleta ushahidi madhubuti ambao unatosha kuishawishi mahakama hii iwaone washitakiwa wote wana hatia katika makosa yanayowakabili,” alidai Kweka.
Aliongeza kuwa hakuna ubishi kwamba washtakiwa wote walikamatwa eneo la tukio (Markas), na Ponda wakati akitoa utetezi wake alidai kuwa kuna mgogoro wa umiliki wa eneo hilo na yeye kama kiongozi wa taasisi hiyo, alitoa agizo kwa viongozi wa misikiti kuwatangazia Waislamu wote kuwa kutakuwa na ujenzi wa msikiti wa muda katika eneo hilo lililoibwa ili waweze kulirejesha mikononi mwao.
“Kwa utetezi huo wa Ponda, sisi upande wa Jamhuri tunaona kisheria kuwa makosa yote yanayowakabili washitakiwa waliyatenda kwa makusudi na walikuwa wakijua wanavunja sheria za nchi, hivyo tunaiomba mahakama hii iwaone washitakiwa wote wana hatia,” aliadai Kweka.
Hakimu Nongwa alisema atatoa hukumu Aprili 14 mwaka huu.
Oktoba 18 mwaka huu, kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana Ponda na Mkadamu. {Chanzo: Tanzania Daima-Alkhamis 04-04-2013}
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Msamaa. - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template