UTEUZI WA WAGURUGENZI NA UDINI. - Kitoloho
Headlines News :
Home » » UTEUZI WA WAGURUGENZI NA UDINI.

UTEUZI WA WAGURUGENZI NA UDINI.

Written By Msamaa on Friday, April 19, 2013 | 11:27 PM

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteua Wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam leo, Jumatano, Mei 30, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu, 2012.

Walioteuliwa ni Ndugu Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Ndugu Naimi Aziz ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda; Ndugu Celestine Mushy ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa; Ndugu Yahya Simba ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati, na Ndugu Bertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.

Wengine ni Ndugu Irene Kasyanju aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria; Ndugu Dorah Msechu ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika, Ndugu Mbelwa Kairuki ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia, na Ndugu Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kibwana alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, Ndugu Naimi Aziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Simba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, na Ndugu Somi alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.

Naye Ndugu Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Msechu alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikulu na Ndugu Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.


..……..Mwisho……….


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

DAR ES SALAAM.


30 Mei, 2012
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template