Makosa Ya Msingi
Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa
Uislamu
SURA YA TANO
Mtazamo Wa Uislamu Kuhusu:
1. Mfumo Wa Democracy
Ni matunda ya mapinduzi ya Kifaransa.
Demokrasia ni ushirikina Kwa sababu inampa Mwanaadamu
Mamlaka na Madaraka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
Historia Ya Mapinduzi Ya Ufaransa
Kanisa la Ki-Roma lilitawala nchi za Ulaya kwa muda
mrefu katika nchi za Ulaya. Kanisa lilidhulumu haki nyingi za raia wa Ulaya kwa
jina la dini, hii ilipelekea kujitokeza wanaharakati kupinga dhulma hii ya
kanisa, harakati hizo zilipelekea kufanyika Mapinduzi makubwa huko Ufaransa
mwaka 1789 jambo ambalo limepelekea kanisa kuvuliwa madaraka ya Kisiasa na
athari ya mapinduzi hayo ndiyo yaliyozusha mfumo wa:
1.
Democracy: Watu ndio wenye mamlaka ya kila kitu.
2.
Secularism: Kutenganisha Dini na Mamlaka ya nchi (Siasa).
Mfumo wa Demokrasia ni Ushirikina kwa sababu unampa
mwanaadamu mamlaka ya Mungu.
قال تعالى:﴿ لَا تُشْرِكْ بِاللَّهِ إِنَّ
الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ﴾ (لقمان:١٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Wala usimshirikishe Allaah hakika ya ushirikina ni
dhulma kubwa)”
(Surat al-Luqmaan:13).
وقال تعالى: ﴿ وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ
وَالْأَرْضِ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾ (آل عمران:١٨٩)
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Ni milki ya Allaah tu vilivyomo mbinguni na Ardhini
na Allaah juu ya kila kitu ni muweza.”
(Surat al-‘Imraan: 189).
2. Ni Nani Mwenye Haki
Ya Kuweka Sheria?
قال تعالى: ﴿ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ
وَالْأَمْرُ﴾ (الأعراف:٥٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Eleweni ni miliki yake yeye tu (Allaah) kuumba na
kuamrisha)”
(Surat Al-A’araaf: 54)
وقال تعالى: ﴿ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ
أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ﴾ (يوسف:٤٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“(Hukumu ni ya Allaah (peke yake) ameamrisha
musiabudu chochote isipokuwa yeye tu)”Surat Yusuf: 40).
وقال تعالى: ﴿ اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ
وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا
أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَهًا وَاحِدًا لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ
سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴾ (التوبة:٣١).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“(Wamewafanya (Mayahudi na manaswara) wanazuoni wao
na watawa wao na ‘Iysa mtoto wa Maryamu kuwa ni miungu kinyume na Allaah, na
hali ya kuwa hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu mmoja hakuna mungu
mwingine anaepasa kuabudiwa isipokuwa Yeye tu utakasifu ni Wake na kila kile
ambacho wanachomshirikisha nacho)”
(Surat At-Tawbah: 31)
Katika Aya hii, Mayahudi na Manaswara wamelaumiwa kwa
kuwageuza wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni Miungu kwa sababu
waliwahalalishia yaliyoharamishwa na Mola na wao wakawatii na waliwaharamishia
yaliyoharamishwa na Mola na wao wakawatii. Kazi ya kuweka Sheria ni ya Allaah
tu peke yake sio ya Mtu wala Bunge.
وقال تعالى: ﴿ أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ
يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْمًا لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴾
(المائدة:٥٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Hivi wanataka wahukumiwe na hukumu ya Kijahili?! Na
ni Nani (hakuna) mwenye hukumu ya sawa (zaidi ya Allaah) kwa watu wenye
kuyakinisha?”
(Surat Al-Maaidah: 50).
Sheria Ya Ndoa Ya 1971 Iliyotungwa
Na Binaadam Ilivyokiuka Shari’ah Za Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Za Ndoa
Kifungu 160:
Mwanamme na
mwanamke wakiishi pamoja kwa muda wa miaka 2 mfululizo huweza kuchukuliwa ni
mke na mme mbele ya sheria japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa.
Ndoa hii haitambuliwi katika Uislam bali inahesabiwa
ni uzinifu.
قال تعالى: ﴿ وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا
إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴾ (الإسراء:٣٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Musiikaribie zinaa hakika hiyo (zinaa) ni uchafu na
njia mbaya”
(Surat Al-Israa 32).
Kifungu cha 18 (1):
Iwapo mwanamme na
mwanamke wanaotaka kuoana, itawabidi kutoa taarifa ya nia yao ya kuoana kwa
msajili au ofisa wa usajilishaji kwa siku 21 kwa uchache, kabla ya siku
wanayotaka kuoana kufika.
Kifungu Cha 114:
Inakatazwa katika
kifungu hiki mtu kuoa au kuolewa na mzazi wake, mtoto au mjukuu wake, kama ni dada yake, mama au shangazi au baba na mjomba
wake, baba au mama wa kambo na mwanae aliyemfanya mwanae (adopted child).
Katika Uislam
anaelelewa anaweza kuolewa na mwenye kumlea.
Sheria ya Kiislamu
Haiwezi Kuvunja Sheria ya Ndoa 1971
Kwa Mujibu wa
Sheria iliyotungwa na Binaadam:
(Cap. (Kiambatanisho 453: The rules of cust Omary law
and the rules of Islamic law shall not apply in regard to any matter provided for
in the law of Marriage Act 1971 (Angalia Sheria ya Kiislamu ya Mirathi na Wasia
– na Mahmoud A. Sameja) uk. 37
Paragraph 1 of Government Notice No.196 of 1971 made
under Sect.102 of The Law of Marriage Act Categorically states that:
The above Boards (Marriage
Conciliation Boards) must comply with the provisions of the law of marriage Act
and any other provisions hereunder.
(Angalia Bakwata and the Administration of Islamic
law: Problems: A case study of DSM by Mohammad Awadh).
Tafsiri (Isiyo Rasmi):
Kanuni za sheria za kimila na kanuni za sheria ya
Kiislam haitoruhusiwa kutumika katika suala lolote linalohusiana na sheria za
Ndoa ya mwaka 1971.
((Angalia Sheria ya Kiislamu ya Mirathi na Wasia – na
Mahmoud A. Sameja) UK.37).
Kipengele cha 1 cha Tangazo la serikali namba 196 ya
1971 iliyotungwa chini ya kifungu cha 102 cha sheria ya Ndoa katika mfululizo
inayosema kwamba:
Kamati tajwa hapo juu (Kamati za usuluhishi wa Ndoa)
lazima zifuate vifungu vya sheria ya Ndoa na vipengele vingine.
(Angalia Bakwata and the Administration of Islamic
law: Problems: A case study of DSM by Mohammad Awadh).
Kifungu 153 (1):
Mtu yeyote ambaye
ni mmoja wa wafunga ndoa au anaeshiriki kwenye shughuli ya ndoa iwapo:
(a) mke
anaekusudiwa yuko chini ya umri wa miaka 18 na idhini ya ndoa kama
inavyotakiwa na fungu la 17 haikutolewa
au;
(b) taarifa ya nia
ya kufunga ndoa, kama inavyotakiwa na fungu la 18, haikutolewa.
Basi mtu huyu
atakuwa ni mkosa na atakapoonekana kuwa ana hatia astahiki kifungo kwa muda
usiozidi miezi sita.
Kwa Makusudio ya fungu la 148 mpaka 155 kushiriki kwa
shughuli ya ndoa yake:
a. Kufungisha ndoa
hiyo, au
b. Kutoa idhini
katika ndoa hiyo
c. Kuwa shahidi wa ndoa hiyo
Wakati sheria hizi zinatungwa 1971 BAKWATA ilishindwa
kutetea Uislam na moja ya malengo ya kuundwa kwake yamebainishwa ndani ya
katiba yao:
MADHUMUNI 9,
“Madhumuni ya
Baraza Kuu la waislam Tanzania yatakuwa haya yafuatayo:
2. kusimamia na
kutetea haki za Msingi za Waislam nchini na kukemea mambo yanayoleta kero kwa
waislam”
Je Sheria ya Ndoa ya Kiislam sio katika haki za
kimsingi za waislam? Mbona BAKWATA imekaa kimya juu ya hili?
3. Mfumo Wa
Kutenganisha Dini Na Dola (Mamlaka/Utawala) Wa Nchi
Uislam hautenganishi mamlaka ya nchi (siasa) na dini
kwani Dini inatuongoza waislam katika kila kipengele cha maisha ibada, jamii,
siasa uchumi n.k.
قال تعالى: ﴿قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي
وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴾ (الأنعام:١٦٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Waambie Swalah yangu na ibada zangu (kuchinja
kwangu) na uhai wangu na kifo changu ni kwa ajili ya Allaah Mola wa viumbe
wote”
(Surat Al-An’aam: 162).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) na
Makhalifa wake walikuwa ni viongozi wa mamlaka ya Dini na Nchi (siasa).
Kutekeleza Sheria
za Jinai ni katika sehemu ya Dini
قال تعالى: ﴿ الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي
فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِئَةَ جَلْدَةٍ وَلَا تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا
رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ
الْآَخِرِ﴾ (النور:٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanaume wapigeni kila
mmoja wao mijeledi mia moja wala isiwachukueni huruma katika kutekeleza Dini ya
Mwenyezi Mungu ikiwa (kweli) mnamuamini Allaah na siku ya mwisho”
(Surat An-Nuur: 2).
Kutekeleza sheria za jinai ni sehemu ya dini na
imani, hii ni hoja dhidi ya wale waislam wanaotaka u-Qaadhi wa ndoa, talaka,
mirathi wakfu, malezi na wasia tu na sio u-Qaadhi wa shari’ah zote.
Kiongozi Wa Nchi Ya Kiislam Ni
Kiongozi Wa Kisiasa Pia
وقال أبوالحسن الماوردي الشافعي رحمه الله
(ﺕ٤٣٠):الإمامة موضوعة الخلافة النبوة في حراسة الدين وسياسة الدنيا وعقدها لمن
يقوم بها في الأمة واجب بالإجماع(الأحكام السلطانية\ص ٥).
“Na amesema Abu Al-Hasan
Al-Mawardiy mfuasi wa Imaam Ash-Shafi’iy (aliekufa mwaka 430 H.), Uongozi ni
shemu ya Ukhalifa wa utume Katika kulinda Dini na siasa ya dunia na
kuusimamisha kwa yule anaesimamia hilo katika umma ni wajibu kwa makubaliano ya
wanazuoni.
(Kitabu Al-Ahkaam
As-Sultaaniyyah, uk. 2).
قال ابن تيمية رحمه الله:(فالواجب اتخاذ
الإمارة دينا وقربا يتقرب بها إلى الله فإن التقرب إليه فيها بطاعته وطاعة رسوله
من أفضل القربات:(السياسة الشرعية\١١٩).
Amesema Shaykh wa Uislamu Ibnu Taymiyyah (Allaah
Amrehemu):
‘‘Basi ni wajibu kuweka uongozi kwa ajili ya Dini na
kujikurubisha kwa Allaah hakika kujikurubisha kwa Allaah kwa kumtii na kumtii
Mtume wake ni katika vikurubisho (Ibada) bora.’’
(Kitabu As-Siyaasatu Ash-Shar’iyah, uk, 119).
Viongozi Wa Majimbo Walikuwa
Wanasiasa Zama Za Makhalifa
ولى الفاروق عمار بن ياسر على الكوفة،ثم كتب
أهلها شكوى ضد عمار بأنه ليس بأمير ولا يحتمل،فاستدعى عمر رضي الله عنه عمار بن
ياسر رضي الله عنه فأقبل ومعه جمع من أهل الكوفة فسألهم عمر فقالوا:هو والله غير
كاف ولا يجزأ ولا عالم بالسياسة ولا يدري علام استعملته.فسأله عمر بحضورهم عن أمور
ولايته ممتحنا إياه لمعرفة مدى خبرته في الحكم.فلم يجب بما يرضى عمر فعزله.(تاريخ
الطبرى ج\٤،ص ١٦٢).
(Al Faruuq ‘Umar Ibn Al Khattwaab alimpa utawala
‘Ammaar Bin Yaasir huko Kuuufah, kisha watu wake wakamshitaki kwamba si
kiongozi anaefaa na wala si mvumilivu, akamwita ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu)
afike kwake akafika akiwa na kundi la watu wa Kuufah, akawauliza ‘Umar (Radhiya
Allaahu ‘anhu) wakasema, huyu tunaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa wala hafai wala
hajui siasa jambo gani umemtawalisha nalo, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu)
akamuuliza mbele yao kuhusu utawala wake akimjaribu ili ajue kiwango cha uelewa
wake katika uongozi akawa hakutoa majibu yaliyomkinaisha ‘Umar (Radhiya Allaahu
‘anhu) na akamvua madaraka).
(Kitabu cha Taariykh At-Twabariy, juzuu ya 4, uk.
162).
Kauli Ya Aboud Jumbe:(Rais Mstaafu Wa
Zanzibar Na ‘‘Makamu Wa Mwenyekiti Wa CCM
Mstaafu).
Kwa Uislam basi
dini haiwezi kutenganishwa na siasa kwa sababu ni sehemu ya maisha.’’
(Angalia The Partnership uk.131).
Wakristo Wanakiri Kwamba Uislam Ni
Njia Kamili Ya Maisha
Katika kitabu “KUWASHIRIKISHA WAISLAMU UPENDO WA
MUNGU na Bill Danett UK 21.
“Uislam unaingia
katika mambo yote ya maisha”
“Ni muhimu
kufahamu kuwa uislam ni njia ya maisha yote. Waislam huamini kuwa ummah wao
ndio bora ulio inuliwa kwa ajili ya binadamu
(Quraan 3: 110), maongozi
ya ummah huo yanathibitika katika uadilifu,
usafi, ukarimu, na uhusiano bora katika familia.
Uislamu hukusiana na mambo yote ya maisha: dini, maadili, jamii, utamaduni, uchumi, na
siasa. Hutawala kila dakika ya maisha yao saa
ishirini na nne kila siku tangu kuzaliwa hadi kufa. Mwislamu si mtu
binafsi tu, bali mshiriki katika
jamii iliyo na uhusiana wa karibu sana na ndani ya jamii hii, ushiriki pia katika familia yenye
uhusiano uliyo wa karibu hapa zaidi.
(Kimechapwa 1992 na life challenge Africa s.l.p 50770, city square 00200, Nairobi, Kenya).
Wakristo Nao Pia
Wanakiri Kwamba Uislam Haukutenganisha Dini Na Siasa Tangu Zamani
Anasema Fredrick Fredolin Portmann katika kitabu
chake: DINI MBALI MBALI NA UTUME WETU.
“Zamani Quraan ilikuwa sheria ya maisha yote
si ya dini tu, ila pia ya
serikali na siasa’’ uk. 30
Mfumo wa kutenganisha dini na siasa (mamlaka ya nchi)
ni wa kikristo, na Waingereza (wakristo) walipoasisi katiba ya nchi hii ndio
walituwekea msingi huu, Katika Biblia Yesu amenukuliwa akisema,
“Basi mpeni
Kaizari vilivyo vyake na vya Mungu vilivyo vyake (Matayo 22:20) na amesema
ufalme wangu sio wa ulimengu huu’’ (Yohana 18:36)
katika Kitabu Wana
wa Ibrahim UK. 156, chasema hivi:
a. Kwa waislamu mungu na kaysar ni
mmoja, yaani asili ya uislamu
ilitaka kuchanganya dini na utawala, muhammad
alianzisha ujamaa wa pekee ukiwa na sheria ambamo kuna siasa na utawala, na dini na sheria mbali mbali kuhusu
yatima, urithi, ndoa,
uhusiano na wanafiki, na
wapagani, usafi na unajisi, vita na jihadi kisasi, namna ya kuwaendea mahaini na watumwa
na wanawake.hayo yote yanaitwa “hudud
Allaah” yaani sheria za mungu
(kuran 2:188) ni kama mipaka ambayo hairuhusiwi kuivuka”.
b. Wakristo waliotaka utawala wa kidini
katika karne zilizopita hawakufanya vile kwa agizo la yesu, kwa sababu agizo lake ni hili: ”vya kaesari, mpeni kaesari, na
vya mungu mpeni mungu (lk 20: 25) maana yake wapeni watawala heshima na utii
wanayostahili katika mambo ya dunia, na
mpeni mungu heshima na utii katika mambo ya roho. Yesu hataki kuchanganya
ufalme wa dunia na ufalme wa mungu…dini ni tofauti na serikali, kwa vile dini inaweza kuwashauri
watawala ili watawale vyema (ef:6:9) lakini hautaki kutawala badala yao… uk.
158.
4. Siasa Ya Ujamaa
Maana ya Ujamaa ni mfumo wa fikra za kisiasa na
uchumi ambazo zimejengwa katika kuamini kwamba kila mtu ana haki sawa katika
kupata sehemu ya utajiri wa nchi na kwamba serikali ndiyo inayomiliki njia zote
kuu za uchumi.
Uislam haujapinga mtu binafsi kujitajirisha maadamu
anatoa Zakaah.
قال تعالى: ﴿ لِلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِمَّا
اكْتَسَبُوا وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِمَّا اكْتَسَبْنَ ﴾ (النساء:٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Wanaume wana fungu katika mali walizochuma na
wanawake wana fungu katika mali walizochuma”
(Surat An-Nisaa: 4).
وقال تعالى: ﴿ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآَتُوا
الزَّكَاةَ﴾ (البقرة:٤٣).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na simamisheni Swalah na toeni Zakaah.’’
(Surat Al-Baqarah: 43).
وقال تعالى: ﴿ أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَةَ
رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُمْ مَعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا
وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِيَتَّخِذَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا
سُخْرِيًّا وَرَحْمَةُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ ﴾ (الزخرف:٣٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
“Je wao ndio wanaogawa Rehema za Mola wako?! Sisi
ndio tuliogawa maisha yao hapa duniani na tukawanyanyua baadhi yao kuwazidi
wengine kwa daraja nyinyi ili wawafanye baadhi yao wengine kuwa watumishi wao,
na rehema ya Mola wako bora kuliko kile wanachokikusanya”
(Surat Az-Zukhruf: 32).
وقال صلى الله عليه وسلم:(فأعلمهم أن الله فرض
عليهم صدقات تأخذ من أغنيائهم وترد على فقرائهم)(رواه البخاري).
Na amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa
sallam): ‘‘Na waelimishe kuwa Allaah Amewawajibishia Sadaka (Zakaah) ambayo
huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa masikini wao.’’
(Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy).
Uislam hauna mipaka ya kujitajirisha maadamu chumo ni
la halali, na hakuna sera za kutaifisha mali za watu kwa dhulma.
قال تعالى: ﴿ وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ
بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا
فَرِيقًا مِنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ﴾
(البقرة:١٨٨).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na wala msile mali zenu kati yenu kwa batili na
kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali za watu kwa dhambi na
nyinyi mnajua”
(Surat Al-Baqarah: 188).
Kwa siasa ya ujamaa watu walidhulumiwa haki zao kwa
uonevu kwamba ni mabepari na mabwenyenye, makabaila na wanyonyaji kinyume hata
na katiba ya nchi kifungu No.22 (2):
Bila ya kuathiri
masharti ya ibara ndogo ya (1): ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali
yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya
sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili.
5. Mfumo Wa Kukataza
Kuanzisha Chama Cha Siasa Chenye Lengo La Kukuza Dini
Katika Uislamu mfumo huu haukubaliki kwa sababu Dini
ndio inayotuongoza katika kila kitu amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
قال تعالى:﴿ شَرَعَ لَكُمْ مِنَ الدِّينِ مَا
وَصَّى بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ
إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا
فِيهِ﴾(الشورى:١٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
‘‘Amekuwekeeni shari’ah itokanayo na Dini aliyomuusia
Nuuh na ambayo tumekuteremshia wahyi kwako na tuliyomuusia Ibraahiym na Muusa
na ‘Iysa kwamba musimamishe Dini wala msifarikiane (kwenye Dini).’’
(Surat Ash-Shuuraa: 13).
وقال تعالى:﴿ قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو
إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ﴾(يوسف:١٠٨).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
‘‘Waambie hii ndio ndio njia yangu nalingania kwa
Allaah kwa ujuzi)”
(Surat Yuusuf: 108).
Kutangaza Dini ni wajibu wa kila Muislam akiwapo
mwanasiasa, lakini katiba inazuia mwanasiasa kusimamisha dini.
6.
Sera Ya Kulazimisha Kila Raia Kufuata Na Kutii Katiba Na Sheria Za Nchi
Hata Zikikhalifu Shari’ah Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) (Kitabu Na Sunnah)
Waislamu wanalazimika kufuata shari’ah za Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala) na sio za twaghuut.
قال تعالى:﴿ أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ
يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آَمَنُوا بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ
قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ
يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا
بَعِيدًا﴾(النساء:٦٠).
Amesema Allaah: (Subhaanahu wa Ta’ala):
‘‘Hivi hauwaoni wale ambao wanadai kwamba wameamini
yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako (kisha) wanataka
wahukumiwe na Twaghuti (asiekuwa Allaah) hali ya kuwa wameamrishwa kumkufuru
huyo (Twaghuti) na anataka Shaytwaan kuwapotosha upotoshi wa mbali)”
(Surat An-Nisaa: 60).
Waislam tunaamrishwa kufuata Qur-aan:
وقال تعالى:﴿ وَهَذَا كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ
مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴾(الأنعام:١٥٥).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na hiki Kitabu Tumekiteremsha chenye Baraka
kifuateni na mcheni (Allaah) ili mpate kurehemewa”
(Surat Al-An’aam: 155).
وقال تعالى:﴿ ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَى
شَرِيعَةٍ مِنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا
يَعْلَمُونَ ﴾(الجاثية:١٨).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Kisha tukakufanya ufuate shari’ah itokanayo na amri
(ya Allaah) ifuate shari’ah hiyo wala usifuate matamanio ya wale wasiojua)”
(Surat Al-Jaathiyah: 18).
وقال تعالى:﴿ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ
إِلَى أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ
لَمُشْرِكُونَ﴾(الأنعام:١٢١).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na hakika Mashaytwaan huwatia maneno wapendwa wao
ili wakujadilini (kwa kupinga) na kama mkiwatii hakika yenu nyinyi mtakuwa ni
washirikina”
(Surat Al-An’aam: 121).
وقال صلى الله عليه وسلم: لا طاعة المخلوق في
معصية الخالق(رواه البخاري)
Na amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
”Hakuna kumtii kiumbe kwenye jambo la kumuasi Muumba”
(Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy).
لما بايع المسلمون أبابكر الصديق رضي الله عنه
بيعة .... في السقيفة جلس في اليوم التالي للبيعة العامة ثم قام خطيبا في الناس
فحمد الله وأثنى عليه بما هو أهله ثم قال:أما بعد ايها الناس فإني قد وليت عليكم
ولست بخيركم فإن أحسنت فأعينوني وإن أسأت فقوموني الصدق أمانة والكذب خيانة
والضعيف فيكم قوي عندي حتى آخذ علته إن شاء الله وإن القوي فيكم ضعيف حتى آخذ منه
الحق إن شاء الله لا يدع القوم الجهاد في سبيل الله إلا جربهم الله بالذل ولا تشيع
الفاحشة في قوم إلا عمهم الله بالبلاء اطيعوني ما أطعت الله ورسوله فإن عصيت
الله ورسوله فلا طاعة لي عليكم.(السيرة
لابن كثير ج\٣ ص ٤٩٢ ط\دار المعرفة)
“Walipomba’ii (kumkubali kuwa kiongozi) waislamu Abu
Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika bustani alikaa siku ya pili yake ili aba’iiwe
na watu wote kisha akasimama na kuhutubu akasema: ‘‘Baada ya hayo, enyi watu
mimi nimetawalishwa kuwa mtawala wenu lakini sio mimi ndio mbora wenu kama
nikifanya vizuri nisaidieni na kama nikifanya vibaya nirekebisheni, ukweli ni
amana na uongo ni hiyana dhaifu wenu kwangu ndio mwenye nguvu mpaka nimrejeshee
haki yake, na mwenye nguvu kwenu ni dhaifu kwangu mpaka nichukue haki yake,
In-shaa Allaah., hawatoacha watu jihadi katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) isipokuwa Mwenyezi Mungu huwapa udhalili na hayataenea maovu kwa watu
isipokuwa Allaah Atawanezea mabalaa. Nitiini muda nitakapokuwa namtii Allaah na
Mtume Wake na kama nikimuasi Allaah na Mtume Wake msinitii” (Kitabu Ibn Kathiyr
Juzuu 3, uk. 492, chapa ya Daar Al Maarifah).
قال تعالى:﴿ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا
أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ
مِنْكُمْ﴾(النساء:٥٩).
Na amsema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“(Enyi ambao mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume
na waliotawalia mambo miongoni mwenu”
(Surat An-Nisaa: 59).
عن ابن عمر رضي الله عنهما أن النبي صلى الله
عليه وسلم قال:(على المرء المسلم السمع والطاعة فيما أحب وكره إلا أن يؤمر بمعصية
فإذا امر بمعصية فلا سمع ولا طاعة)(متفق عليه).
Na amepokea Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) amesema: ”Inampasa Muislamu kusikia
na kutii kwenye kitu anachokipenda au anachokichukia isipokuwa akiamrishwa
Maasi kama akiamrishwa Maasi asisikilize wala kutii” (Wameipokea Al-Bukhaariy
na Muslim).
7.
Kiongozi Wa Nchi Kupewa Madaraka Ya Kusamehe Au Kupunguza Adhabu
Katika Uislam kiongozi anaweza kusamehe au kupunguza
adhabu za taaziyr tu na hana uwezo wa
kusamehe huduud na haki za watu.
أسامة بن زيد شفع لدى رسول الله صلى الله عليه
وسلم في المرأة المخزومية:(قرشية التي سرقت فقال صلى الله عليه وسلم:ياأسامة أتشفع
في حد من حدود الله ثم قام فقال:إنما هلك الذين من قبلكم أنهم كانوا إذا سرق فيهم
الشريف تركوه،وإذا سرق الضعيف اقاموا عليه الحد وأيم اتلله لو أن فاطمة بنت محمد
سرقت لقطعت يدها.(رواه البخاري).
“Swahaba Usaamah bin Zayd alitaka alimwombea kwa
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) mwanamke wa koo la Makhzumiy
litokanalo na kabila la ma-Quraysh mwanamke ambae aliiba. Mtume akamwambia Usama:
‘‘Ewe Usaamah unafanya maombezi kwenye Had
(Adhabu) miongoni mwa Huduud za
Allaah, kisha akatoa khutbah Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema:
‘‘Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu ilkuwa akiiba mtukufu miongoni mwao
humuacha (bila ya Adhabu) na kama akiiba dhaifu humsimamishia Had (Adhabu) juu yake. Naapa kwa Allaah
hata kama Faatwimah bint Muhammad (yaani binti yake) akiiba nitakata mkono
wake”
(Ameipokea Al-Bukhaariy).
8.
Uhuru Wa Kubalidisha Dini
Katika Uislamu mtu akishakuwa Muislamu basi hana
uhuru kubalidilisha dini na akibalidisha basi atatakiwa arudi na akikataa basi
anauawa.
قال صلى الله عليه وسلم:(من بدل دينه
فاقتلوه)(رواه البخاري).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
”(Mwenye kubadili Dini yake (Uislamu) basi muueni)”
(Ameipokea Al-Bukhaariy).
قال تعالى:﴿ وَمَنْ يَرْتَدِدْ مِنْكُمْ عَنْ
دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي
الدُّنْيَا وَالْآَخِرَةِ وَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا
خَالِدُونَ﴾(البقرة:٢١٧).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Mwenye kuacha Dini yake miongoni mwenu na akafa hali
ya kuwa ni kafiri hao matendo yao yatakuwa yameporomoka duniani na akhera na
hao ni watu wa motoni watakaa humo milele”
(Surat Al-Baqarah: 217).
ويقول رسول الله صلى الله عليه وسلم:(لا يحل دم
امرئ مسلم يشهد أن لاإله إلا الله وأني رسول الله إلا بإحدى ثلاث:الثيب
الزاني،والنفس بالنفس والتارك لدينه المفارق للجماعة(رواه البخاري).
Na anasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa
sallam):
”Si halali (haramu) kuimwaga damu ya Muislamu yeyote
mwenye kushuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah
na mimi ni Mtume wa Allaah isipokuwa kwa kufanya moja ya mambo matatu: mzinifu
alieoa au kuolewa, aliyeua, aliyeiacha Dini yake mwenye kuacha umoja”
(Ameipokea Al-Bukhaariy).
Shubha: (Hoja ya
wapinzani)
Msimano huu wa Uislam ni kinyume na Tangazo la
ulimwengu la Haki za Binaadam la mwaka 1945 kifungu 18(b) kwa mtu ana uhuru wa
kubalidisha dini anayotaka
Jawabu:
La kushangaza katika nchi nyingi za kisekula mtu
akifanya kosa la uhaini (treason) anauliwa kwa sababu tu amekwenda kinyume na
nidhamu ya Dola kwa lengo la kugeuza nidhamu ya utawala uliopo, mbona Uislamu
unalaumiwa kwa jambo ambalo likifanywa na wengine hawalaumiwi?
9.
Sera Ya Kuupapatikia Uongozi Na Kuugombania
Katika Uislam ni Haramu mtu kuomba au kupapatikia
uongozi.
عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه قال:(دخلت
على النبي صلى الله عليه وسلم أنا ورجلان من الأشعريين فقال أحدهما يارسول الله أمرنا على بعض ما ولاك
الله وقال الآخر مثل ذلك فقال:إنا لا نولي على هذا العمل أحدا سأله ولا أحد حرص عليه قال صلى
الله عليه وسلم لعبد الرحمن بن صخرة :ياعبدالرحمن لا تسأل
الإمارة فإنك إن أعطيتها عن مسألة وكلت إليها وإن أعطيتها من غير مسألة أعنت عليها(رواه مسلم).
Imepokewa kutoka
kwa Abuu Muusa Al-Ash’ariy (Radhiya Allaahu ‘anhu) Amesema: ”Niliingia kwa
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) mimi na watu wengine wawili
watokanao na Al-Ash’ariy (koo/kabila) mmoja wao akasema ewe mjumbe wa Mwenyezi
Mungu nipe uongozi kwenye baadhi ya vile alivyokutawalisha Allaah, na yule
mwingine akasema hivyo hivyo. Akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa
sallam) sisi hatumpi kazi hii ya uongozi mtu yeyote yule aliyeiomba au mtu
aliyepupia, akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) kwa
Abdur-Rahmaan Ibn Swakhrah (Radhiya Allaahu ‘anhu): Ewe Abdur-Rahmaan usiuombe
uongozi kwani wewe ukipewa huo uongozi kwa kuuomba utaachiwa bila kusaidiwa na kama ukipewa uongozi bila ya kuuomba utasaidiwa”
(Ameipokea Muslim).
عن أبي هريرة رضي الله عنه:أن رسول الله صلى
الله عليه وسلم قال:إنكم ستحرصون على الإمارة وستكون
ندامة يوم القيامة(رواه البخاري).
Amepokea Abuu
Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa
sallam) amesema:
”Hakika nyinyi
mtapapia uongozi kisha itakuwa ni majuto kweni siku ya Qiyaamah”
(Ameipokea
Al-Bukhaariy).
10. Mfumo Wa Vyama Vingi Vya Kisiasa
Katika Uislam vyama ni viwili (2) tu chama cha Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala) na chama cha Shaytwaan.
Si ruhusa katika Uislam kuunda makundi ambayo hujiita
vyama vya upinzani kazi yao ni kupinga serikali iliyo madarakani haijawahi
kutokea tangu zama za Makhalifa hadi Khalifa wa Mwisho hakujawa na mfumo wa
vyama vingi.
Sera ya vyama vingi umeasisiwa Firauni na hatimae
imeletwa na Makafiri hapa nchini.
قال تعالى:﴿ إِنَّ
فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ
طَائِفَةً مِنْهُمْ﴾(القصص:٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika Firauni alijikweza katika hii Ardhi na
kuwagawa watu wake makundi tofauti na akawadhoofisha baadhi yao”
(Surat Al-Qaswasw: 4).
Katika kitabu: ELIMU YA DEMOKRASIA SHIRIKISHI (Kitabu
cha 4 kimotolewa na C.P.T. DSM UK.7:
“Wanasayansi wa
mambo ya siasa wanaelekea kukubali kwamba demokrasia ya vyama vingi imeanzishwa
toka nje kwa kutokana na shinikizo la masharti ya kupata misaada ya fedha.’’
Uislamu Unatutaka
Waislam Tuwe Kitu Kimoja
قال تعالى:﴿ وَاعْتَصِمُوا
بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا﴾(آل عنران:١٠٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Shikamaneni na kamba (Dini) ya Mwenyezi Mungu nyote
wala msitofautiane”
(Al-‘Imraan 103).
وقال تعالى:﴿ إِنَّ
الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَسْتَ مِنْهُمْ فِي
شَيْءٍ﴾(الأنعام:١٥٩).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Hakika wale
ambao wameacha Dini zao na kuwa makundi makundi wewe hauhusiki nao kwa
lolote.”
(Surat Al-An’aam: 159).
11. Kiongozi Wa Nchi
(Rais) Kuwa Juu Ya Sheria
Katika Uislam mtawala na mtawaliwa wote wako sawa
katika sheria.
قال صلى الله عليه
وسلم:(لو أن فاطمة بنت محمد سرقت لقطعت يدها)(رواه البخاري).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
”Hata kama Faatwimah mtoto wa Muhammad akiiba nitakata mkono wake”
(Imepokewa na Al-Bukhaariy).
Kisa cha Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) alipowaaga Waislam
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) wakati wa
maradhi yake aliyokufa nayo alitoka nje kwa kutolewa na Al-Fadhli bin ‘Abbaas (Radhiya
Allaahu ‘anhu) na ‘Alliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuwekwa juu
ya mimbari kisha akasema:
(أيها الناس من كنت جلدت له ظهرا فهذا ظهري فليستقد
منه ومن كنت شتمت له عرضا فهذا عرضي فليستقد منه ومن أخذت له مالا فهذا مالي
فليأخذ ماله ولا يخشى الشحناء من قبلي فإنها ليست من شأني ألا وإن أحبكم إلي من
أخذ مني حقا إن كان له أو حللت فلقيت ربي وأنا طيب النفس ثم نزل فصلى الظهر ثم رجع
إلى المنبر فعاد لمقالته الأولى(الكامل في التاريخ ج٢ ص ١٣٢ لابن الآثير).
“Enyi watu yoyote yule ambaye nimemchapa mgongo wake
basi huu ni mgongo wangu na aje kulipiza kisasi, na kwa yule ambaye nimemvunjia
heshima yake basi hii ni heshima yangu na aje kulipiza kisasi na yule
niliyemchukulia mali yake basi hii ni mali yangu na aje kuchukua haki yake, na
wala usiogopwe uadui toka kwangu kwani hilo sio katika shani yangu, na mjue
kuwa kipenzi zaidi kwangu katika nyinyi ni yule aliechukua haki yake toka
kwangu na akanisamehe na nikakutana na Mola wangu hali ya kwamba nafsi yangu
imetakasika, kisha akashuka na kuswali Adhuhuri kisha akarejea kutamka maneno
yake ya mwanzo.
(Angalia Kitabu Al-Kaamil Fiy Taariykh Juzuu 2, uk.
132 cha Ibn Athiyr).
Kisa Cha Khalifa ‘Alliy Alipomushtaki Yahudi Mbele
Ya Qaadhi Shurayh
Ambapo Khalifa alipoteza ngao yake ya vita, kisha
akaiona kwa Myahudi hakuichukua kutoka kwake bali alimshitaki kwa Qaadhi mkuu
Shurayh, akakosa Khalifa ushahidi, akahukumu Qaadhi Shurayh kuwa ile ngao ni ya
Yahudi, na hivyo Yahudi kuwa ni mshindi katika kesi hii.
عَنْ أَبِى فِرَاسٍ
قَالَ: خَطَبَنَا عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رَضِىَ اللَّهُ عَنْهُ فَقَالَ فِى
خُطْبَتِهِ: أَلاَ وَإِنِّى لَمْ أَبْعَثْ إِلَيْكُمْ عُمَّالِى لِيَضْرِبُوا
أَبْشَارَكُمْ وَلاَ لِيَأْخُذُوا أَمْوَالَكُمْ وَلَكِنْ بَعَثْتُهُمْ
لِيُعَلِّمُوكُمْ دِينَكُمْ وَسُنَنَكُمْ فَمَنْ فُعِلَ بِهِ غَيْرُ ذَلِكَ
فَلْيَرْفَعْهُ إِلَىَّ فَأُقِصَّهُ مِنْهُ. من كتاب السنن الكبرى للبيهقي.
Imepokewa Na Abuu
Firaasi Amesema:
”Alihutubu
‘Umar Ibn Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema katika hotuba yake,
‘‘Eleweni kuwa mimi sijawatuma kwenu viongozi wangu ili wawapige na kuchukua
mali zenu lakini nimewatuma kwenu ili wawafundisheni Dini yenu na Sunnah zenu
atakaefanyiwa kinyume na hivyo basi ashitaki kwangu na nitamlipizia kisasi kwa
huyo kiongozi”.
(As-Sunanu Al-Kubraa
ya Imaam Al Bayhaqiy).
عَنْ أَبِى سَعِيدٍ الْخُدْرِىِّ
قَالَ: بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ –صلى الله عليه وسلم يَقْسِمُ شَيْئًا أَقْبَلَ
رَجُلٌ فَأَكَبَّ عَلَيْهِ فَطَعَنَهُ رَسُولُ اللَّهِ –صلى الله عليه وسلم
بِعُرْجُونٍ كَانَ مَعَهُ فَجُرِحَ الرَّجُلُ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ –صلى
الله عليه وسلم:« تَعَالَ فَاسْتَقِدْ ». فَقَالَ: بَلْ عَفَوْتُ يَا رَسُولَ
اللَّه(من كتاب السنن الكبرى للبيهقي)
Na imepokewa na
Abu Sa’id Al-Khudriy amesema: ”Wakati Mtume anagawa kitu fulani ghafla akatokea
mtu na kumwangukia, akmchoma Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) yule
mtu na mti aliokuwa ameushika na kumjeruhi, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa
sallam) akamwambia yule mtu njoo ulipize kisasi, akasema: '‘Bali nimesamehe ewe
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu).
(As-Sunanu Al-Kubraa ya Imaam Al Bayhaqiy).
12. Sera Ya Kukataza Matumizi Ya Nguvu (Jihadi) Katika Kufikia Malengo Ya
Kisiasa
Uislam haujakataza moja kwa moja kutumia nguvu katika
kudai haki hasa kama mtawala anafanya dhulma za wazi na Waislamu wakiwa
wamejianda kwa nguvu za silaha.
قال تعالى:﴿
وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ
تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ﴾(الأنفال:٦٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Waandalieni hao (makafiri) kila mnachokiweza katika
nguvu na na ngome ya farasi ili muwatishe maadui wa Allaah na maadui wenu”
(Surat Al-Anfaal: 60).
وقال تعالى:﴿
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آَمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ
يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَئِكَ
هُمُ الصَّادِقُونَ ﴾(الحجرات:١٥).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika Waumini wa kweli ni wale ambao wamemuamini
Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kisha hawakuingiwa na mashaka na wakapigana kwa
mali zao na nafsi zao katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hao ndio
waumini wa kweli kabisa”
(Surat
Al-Hujuraat: 15).
وقال تعالى:﴿ أَمْ
حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّهُ الَّذِينَ
جَاهَدُوا مِنْكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴾(آل عمران:١٤٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hivi mnadhani kuwa mtaingia peponi kabla ya
(kujaribiwa) na Allaah na kujua ni wapi kati yenu wenye kuipigania Dini ya
Allaah na ni wapi wenye Subira”
(Surat Al-‘Imraan: 142).
وقال تعالى:﴿
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ
لِلَّهِ﴾(البقرة:١٩٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na wapigeni vita hao (makafiri) mpaka kusiwe na
fitna na iwe Dini ni ya Allaah (inayofuatwa)”
(Surat Al-Baqarah: 193).
Ulimwengu umekiri matumizi ya nguvu katika nchi zifuatazo
baada ya raia kudhulumiwa haki zao :
-Zanzibar katika mapinduzi ya mwaka 1964
-Msumbiji na Frelimo
-Kenya na Mau Mau
-Biafra Nigeria na
Rais Nyerere alishabikia mtengano kwa sababu wakristo walikuwa wakidhulumiwa na
Waislamu na aliandika kitabu 1966 (rejea gazeti la Majira la tarehe 16/11/2011
Uk.3) akidai kwamba umoja wa Kitaifa hauna maana endapo baadhi ya raia
wanadhulumiwa.
13. Sera Ya Kukanusha Itikadi Ya Al-Walaa
Wal-Baraa
Katika Uislam
kutobaguana kwa msingi wa kidini ni kinyume cha Itikadi muhimu ya Al-Walaa
wal-Baraa (kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah).
Udugu unaokubalika
katika Uislam ni wa Imani tu.
﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ﴾(الحجرات:١٠).
Amesema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
“Hakika waumini
(tu) ndio ndugu”
(Al-Hujuraat:10).
Kafiri sio ndugu
wala rafiki wa waumini.
Amesema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
﴿قَدْ
كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ
قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآَءُ مِنْكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ
اللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ
وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّى تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَحْدَهُ﴾(الممتحنة:٤).
“Hakika kuna mfano
mzuri kwenu kwa Ibraahiym na walio pamoja nae waliopowaambia watu wao, sisi
tuko mbali na nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah tumewakanusha nyinyi
na umedhihiri uadui na bughdha baina yetu sisi na baina yenu milele mpaka
mumuamini Allaah Peke yake.’’
(Al-Mumtahinah: 4)
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا
عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ
كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُمْ مِنَ الْحَقِّ﴾(الممتحنة:١)
Na amesema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
“Enyi Mlioamini
msiwafanye adui yangu na adui wenu kuwa ni marafiki (wasaidizi) mna waangushia
mapenzi na kwa hakika wamekufuru yale yaliowajieni katika haki”
(Al-Mumtahinah: 1)
Ama kubaguana kwa
misingi ya Utaifa, Ukabila, Urangi, Uzawa, Uzalendo na msingi wa Kilugha ni
jambo lililokatazwa katika Uislam.
Amesema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ
ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ
أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ﴾(الحجرات:١٣)
“Enyi watu hakika
sisi tumewaumbeni kutokana na mwanamme mmoja na mwanamke mmoja na tukawajaalia
kuwa mataifa mbali mbali na makabila mbali mbali ili mjuane, hakika mbora wenu
mbele ya Allaah ni Mcha Mungu wenu zaidi.”
(Al-Hujuraat: 13).
Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) alikemea sana ugomvi baina ya Muhajirina (waliohama
toka Makkah) na Answaar (wazawa wa Madiynah) kwa misingi ya Uzawa na Akasema:
“Enyi Waislam
(mnagombana) kwa wito wa msingi wa Kijahiliya (Kikafiri) na mimi niko pamoja
nanyi baada ya Allaah kuwaongoza katika Uislam? Uacheni kwani huo ni uvundo”
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !