Makosa Ya Msingi
Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa
Uislamu
بسم الله الرحمن
الرحيم
Utangulizi
Sifa zote njema anastahiki Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) na Rehema na Amani zimshukie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa wa sallam) na Radhi za Mola ziwafikie Maswahaba zake wote Kiramu na
kila mwenye kufuata nyayo zao mpaka siku ya Qiyaamah.
Kitabu ”MAKOSA YA MSINGI YALIYOMO NDANI YA
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MTAZAMO WA UISLAMU” ni mkusanyiko
wa Maudhui mbali mbali zilizotolewa na wahadhiri na wasemaji mbali mbali
katika semina maalumu juu ya maudhui
hiyo hapo juu iliyokusanya wanachuoni, wanasheria, walinganiaji na wasomi mbali
mbali waliojikusanya katika Ukumbi wa Chuo cha Wasichana cha UMMU SALAMAH,
mnamo tarehe 25 Swafar 1432 H sawa na 30 Januari 2011 M, lengo la semina hiyo
lilikuwa ni kutafakari maneno ya Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwataka wananchi wa Tanzania
wakiwemo wanadini kuchangia maoni katika
mchakato mzima wa kutungwa upya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Semina hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti Shaykh ‘Alliy
Adamu ‘Alliy kutoka Msumbiji ilitoa mapendekezo kwamba katika hatua ya awali
iko haja ya kueneza yaliyopatikana katika semina hiyo kwa njia ya makongamano
mengine katika kiwango cha wilaya, mikoa na Kitaifa, pia kwa njia ya mihadhara
mbali mbali, khutba za ijumaa na kwa kutumia vyombo vya habari, Magazeti,
Redio, Televisheni, na Makala mbali mbali.
Juhudi hii ni katika kutekeleza agizo hilo ambalo
tunaamini litaleta mwamko mpya hasa kwa Waislam kuijua hali waliyo nayo kwa
sasa na wanatakiwa wafanye nini.
Na kuwasaidia wale watakaoshiriki katika kutoa maoni
kwenye kamati ya kuratibu maoni ya uandishi wa katiba mpya.
Shukrani
Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani za dhati
kwa wale wote waliochangia mada hii hadi kupatikana kwa maandiko haya katika
umbo la kitabu. Mola Ajaalie Juhudi zao hizi ziwe katika Mizani ya Matendo yao
mema siku ya Qiyaamah.
Mkusanyaji:
Shaykh Salim ‘Abdur-Rahiym Barahiyan, (L.L.B.
Shari’ah, L.L.M. Shari’ah and Law)
P. O.BOX 1542,
TANGA
Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya
Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu.
SURA YA KWANZA
Kwa nini Mada hii?
Tuna sababu zifuatazo zinazotufanya tuzungumzie mada
hii:
1. Ni katika kulingania dini yetu kwa Jihadi ya hoja
na kuzuia Munkari (Maovu).
﴿فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُمْ بِهِ
جِهَادًا كَبِيرًا﴾(الفرقان:٥٢ قال تعالى:
Amesema Allaah:
“Na wala usiwatii Makafiri na pigana nao Jihadi ya
hoja ya (Quraan) Jihadi kubwa”. (Surat AlFurqaan: 52).
وقال تعالى:﴿ قُلْ
هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي
وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴾(يوسف:١٠٨).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Sema hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah kwa
ujuzi mimi na yule aliyenifuata na Ametakasika Allaah na kila upungufu nami si
katika washirikina”
(Surat Yuusuf: 108).
وقال صلى الله عليه
وسلم:(من رأى منكم منكرا فليغيره بيده فإن لم يستطع فبلسانه فإن لم يستطع فبقلبه
وذلك أضعف الإيمان)رواه مسلم.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
“Atakaeona miongoni mwenu ovu lolote aliondoe kwa
mkono yake, na kama hataweza basi na kwa ulimi wake na kama hataweza basi na
aliondoe kwa moyo wake (alichukie) na
hali hii (kulichukia kwa moyo) ni udhaifu mkubwa wa imani” (Imepokewa na Imaam
Muslim).
عن النعمان بن بشير
رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:(مثل القائم في حدود الله والواقع
فيها كمثل قوم استهموا على السفينة فصار بعضهم أعلاها وبعضهم أسفلها وكان الذين في
أسفلها إذا استقوا الماء مروا على من فوقهم فقالوا لو أنا خرقنا في نصيبنا خرقا ولم
نأذي من فوقنا،فإن تركوهم وما أرادواهلكوا جميعا وإن أخذوا على أيديهم نجوا ونجوا
جميعا).رواه البخاري.
Toka kwa Nu”umaan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ‘anhu)
amepokea toka kwa Nabii (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) akisema:
“Mfano wa yule aliesimama katika mipaka ya Allaah na
yule alievuka mipaka yake ni mfano wa watu walioingia kwenye Safina kwa kupiga
kura na wakawa miongoni mwao juu ya ile Safina na wengine chini (inaashiria
ukubwa wa hiyo Safina) ikawa wale waliokuwa chini wakitaka maji huyafuata kwa
kupitia kwa wale wa juu, wakasema (kwa kushauriana): kama tungetoboa hukuhuku
chini tungeyapata maji bila ya kuwaudhi wenzetu walio juu, kama wataachwa na
matakwa yao hayo wataangamia wote na kama wakizuiwa wataokoka wote).”
(Imepokewa na
Imaam Al-Bukhaariy).
قال الله تعالى:﴿
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ
وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ)( آل عمران:١١٠)
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Mmekuwa Umma bora utokanao na watu mnaamrishana mema
na mnakatazana mabaya na mnamwamini Allaah” (Surat Al-‘Imraan: 110).
2. Ni haki ya Kikatiba kwa kila Raia:
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania 18(1):
“Bila kuathiri
sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo
yake, na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake
kutoingiliwa”
3. Ni wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa Raia wa
nchi hii kuchangia maoni katika mchakato wa kuandikwa upya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania:
Katika Gazeti la MWANANCHI la Jumamosi tarehe 1
Januari 2011:
“Rais Jakaya
Kikwete ametangaza kuanza mchakato wa kuandikwa katiba Mpya.Katika salamu zake
za mwaka mpya kwa Taifa jana, Rais Kikwete alisema: “Nimeamua kuunda Tume
Maalumu ya Katiba yaani Constitutional Review
Commision. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa
na wajumbe wanaowakilisha makundi mbali mbali kutoka jamii yetu kutoka pande
mbili za Muungano, alisema jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza
na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za
kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbali mbali ya watu wote,
katika kutoa maoni wayatakayo kuhusu katiba ya nchi yao.”
4. Ni wajibu wetu kutoa Nasaha:
قال تعالى:﴿ وَإِنْ
أَحَدٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلَامَ
اللَّهِ (التوبة:٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Kama mmoja yeyote katika washirikina atakuomba awe
karibu nawe basi kuwa karibu nae ili apate kusikia maneno ya Allaah”
(Surat At-Tawbah: 6).
عن التميم الداري
رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:(الدين النصيحة.قلنا لمن يارسول
الله.قال:لله ولكتابه ولرسوله ولأئمة المسلمين وعامتهم).رواه مسلم.
Imepokewa na Tamiym Ad-Daariy (Radhiya Allaahu
‘anhu),
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu
‘alayhi wa wa sallam):
“(Dini ni nasaha) tukasema kwa ajili ya nani ewe
mjumbe wa Mwenyezi Mungu? akasema:kwa ajili ya Allaah na Kitabu Chake na Mtume
Wake na kwa viongozi wa Waislamu na watu wote)”
(Imepokewa na Imaam Muslim).
وقال صلى الله عليه
وسلم:(إذا استشار أحدكم أخاه فليشر عليه).رواه ابن ماجه.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
“Atakapotaka ushauri mmoja wenu kwa ndugu yake basi
amshauri”.
(Imepokewa na
Ibn Maajah).
5. Kuwatanabaisha baadhi ya masheikh ambao mara baada
ya Rais kutangaza mchakato wa Katiba mpya wakakurupuka na kutoa maoni kwamba
wanataka mahakama ya Qaadhi (Kadhi) na nchi kujiunga na OIC na Ijumaa iwe ni
siku ya mapumziko, na wameghafilika kwamba Katiba imewanyima haki zao za msingi
na kubwa kuliko mahakama ya Qaadhi na OIC na siku ya Ijumaa. Na wengine kuona
bado wakati wa kutoa maoni wamewausia WaIslamu wasiseme kitu wasubiri kamati ya
kukusanya maoni itakayoundwa na Mheshimiwa Rais.
Chanzo: Alhidaaya.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !