Makosa Ya Msingi
Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa
Uislamu
SURA YA PILI
Nini Maana Ya
Katiba Ya Nchi? Kwa Mtazamo Usio Wa Kidini.
Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi
unategemea Katiba. Katiba ni sheria kuu
au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote zinategemea au
zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba hutafsiriwa kuwa ni
mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi (watawaliwa). Ni makubalianao
ya wananchi husika juu ya ni jinsi gani taratibu za kanuni za uendeshaji wa
mambo mbali mbali katika nchi yao unapaswa kuwa.
(Angalia kitabu HAKI Tolea la 5 Namba 4 Dec. 2002 Uk.
6).
Ni muafaka wa Kitaifa juu ya misingi mikuu ya
kuendesha nchi.
(Maneno ya Pro.Shivji katika
kongamano tarehe 15/1/2011Dar es Salaam.)
Maana ya katiba ya nchi kwa mtazamo
wa Kiislamu
Sheria kuu na Sheria Mama katika nchi kwa mujibu wa
Uislamu ni Qur-aan na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa sallam).
قال تعالى:﴿ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ
فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ﴾.(النساء:٥٩).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Ikiwa mkikindana (kukhitalifiana) katika jambo
lolote basi lilerejesheni (jambo hilo) kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake”
(Surat An-Nisaa: 59).
قال تعالى:﴿ وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا
مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ
الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ
ضَلَالًا مُبِينًا ﴾(الأحزاب:٣٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na haifai kwa muumini mwanamme au mwanamke pale
atakapolitolea hukumu jambo lolote Mwenyezi Mungu na Mtume wake wawe na hiari
katika kulitekeleza Jambo hilo, na anae muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake
hakika amepotea upotevu wa wazi)”
(Surat
Al-Ahzaab: 36).
Historia Ya Katiba
Katika Nchi Zilizotawaliwa Na Makafiri
“Kwa ujumla nchi
nyingi hasa zile zinazoendelea zina katiba zilizoandikwa.nyingi kati ya katiba
hizo zilitungwa na kurekebishwa na watawala wa kikoloni, na nyingine zilitungwa
baada ya makubaliano na tawala za kikoloni kabla ya kuondoka.Katiba hizo ni
maridhiano ambayo yalilinda maslahi ya pande zote mbili:
(1)Tawala za
kikoloni zilizokuwa zikiandika.
(2)Nchi iliyokuwa
ikipata uhuru(Angalia Jarida la HAKI Toleo la 5 uk.7), (Angalia pia Shetani wa
mwalimu uk.6):
"Katiba nyingi katika nchi zilizoendelea zina
uhusiano na Katiba na Tawala za kikoloni.
Historia ya katiba
hapa Tanzania
pia ina uhusiano na tawala za kikoloni zilizokuwa zinatawala kabla ya uhuru".Angalia
HAKI toleo la 5 uk.7(Kamati ya Msaada ya Kisheria).
Historia Ya Mabadiliko Ya Katiba
Tanzania
1961Katiba ya kwanza ya uhuru iliyowekwa na
waingereza (Independence Constitution).
1962Katiba ya Jamhuri (The Republic Constitution)
iliitambua Tanganyika kama Jamhuri na ilipunguza madaraka ya Bunge(Imewekwa na
Waingereza).
1965Iliwekwa katiba ya muda (The Interim
Constitution)
1977Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ilitungwa na bunge maalum (Constitutional Assembly), (wananchi
hawakuhusishwa).Angalia HAKI toleo la 5 uk.10).
Pr.Issa Shirji anabainisha haya pia katika kongamano
la Katiba lililoandaliwa na wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam,
Jumamosi tarehe 15/1/2011 angalia Gazeti la MWANANCHI uk.4 tarehe 16/1/2011.
Mabadiliko Makubwa Yaliyotokea
Katika Katiba
1961Katiba iliruhusu mfumo wa vyama vingi,
Vyama vifuatavyo vilisajiliwa:TANU, United Tanganyika
Party(UTP), African National Congress(ANC), The Peoples Democratic Party(PDP),
Peoples Convertion Party(PNP), National Enterprise Party(NEP), All Muslim
Nationalist Union of Tanganyika(AMNUT), African Independence Movement(AIM).
1963Halmashauri kuu ya TANU ilipitisha maamuzi
kufanya Tanganyika kuwa nchi ya chama kimoja.
1965Sheria ya chama kimoja iliingizwa kwenye Katiba.
1977Haki za binaadamu ziliingizwa rasmi katika
Dibaji.
1984Katika katiba ya Jamhuri haki za binaadamu
ziliingizwa rasmi katika katiba.
1992Katiba iliruhusu tena mfumo wa vyama vingi kwa
shinikizo la nchi za kibeberu (kikafiri).
Katika kitabu: Elimu ya Demokrasia shirikishi (Kitabu
kilichotolewa na CTP Dom uk.7) chasema hivi:
"Wanasayansi wa mambo ya siasa wanaelekea kukubali
kwamba demokrasia ya vyama vingi imeingizwa toka nje kwa kutokana na masharti
ya kupata misaada ya fedha".
Katiba Ya Allaah
(Subhaanahu Wa Ta’ala) Haibadiliki
قال تعالى:﴿ وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنْ
كِتَابِ رَبِّكَ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ﴾(الكهف:٢٧).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):”Nawasomee
kilichoteremshwa kwako kwa wahyi (Ufunuo) katika kitabu cha Mola wako ambacho
hayabadiliki maneno yake)” (Surat Al
Kahfi: 27).
قال تعالى:﴿ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ. لَا
يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنْزِيلٌ مِنْ
حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴾
(فصلت:٤١-٤٢)
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na hakika hiyo (Qur-aan) ni Kitabu kitukufu,
hakiingiliwi na batili yoyote mbele yake wala nyuma yake imeteremka kutoka kwa
Mwenye hekima ya hali ya juu na Mwenye kushukuriwa sana)”
(Surat Fusswilat: 41- 42).
SURA YA TATU
Mambo Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya
Katiba Yanayokwenda Kinyume Na Uislam
1. Mfumo Wa Demokrasia
Nini maana ya Democracy?
Ni neno lenye asili ya kigiriki (Demo – crates)
yaani utawala wa watu.
"Ni mfumo wa kuendesha serikali ya watu iliyochaguliwa
na watu kwa manufaa ya watu, madaraka na mamlaka, ya mwisho ya serikali hiyo
yako mikononi mwa watu"
(Angalia Jifunze Uraia kwa shule za msingi kitabu cha
nne na S. A.
Numisi uk. 10).
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania, sehemu ya pili, Serikali na watu, sheria ya 1984 na.15, 16.6,
“Jamhuri ya muungano
wa tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki za kijamii na kwa
hiyo:
a) Wananchi ndiyo
msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa katiba hii.
b) Lengo kuu la
serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi serikali itawajibika kwa wananchi”
2. Mamlaka Ya Kutunga Sheria Yako
Mikononi Mwa Watu Badala Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania kifungu 64 (1):
“Mamlaka yote ya
kutunga sheria juu ya mambo yote yahusuyo Tanzania bara yatakuwa mikononi mwa
bunge”
Kifungu 106 (3):
Madaraka yote ya
kutunga sheria katika zanzibar katika mambo yote yasiyo mambo ya muungano
yatakuwa mikononi mwa baraza la wawakilishi wa Zanzibar.
3. Mfumo Wa Kutenganisha Dini Na
Mamlaka Ya Nchi (Siasa)
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania kifungu 19 (2):
“Bila kuathiri
sheria zinazohusika za jamhuri ya muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya
ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya
nchi”.
Katika katiba toleo la 2005 ibara ya 3:
3 (1) “Jamhuri ya
muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini yenye kufuata
mfumo wa vyama vingi vya siasa”.
4. Mfumo Wa Kufuata Siasa Ya Ujamaa Kwa Mujibu Wa Katiba Ya
Jamhuri Ya Muungano
Kifungu cha 9:
“Lengo la katiba
hii ni kuendesha ujenzi wa jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu wa amani kutokana na
kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa
misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika jamhuri ya
muungano”.
5. Mfumo Wa Kukataza Kuanzishwa Chama
Cha Siasa Chenye Lengo La Kukuza Dini
Kwa mujibu wa katiba kifungu 20 (2):
“Kwa kujali
masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa
kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake:
A) kinakusudia
kukuza au kupigania maslahi ya:
I) “imani au kundi
lolote la dini”.
6. Sera Ya Kulazimisha Kila Raia
Kufuata Na Kutii Katiba Ya Jamhuri Na Sheria Zake Hata Kama Zinakhalifu
Shari”ah Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 26 (1):
“Kila mtu ana
wajibu wa kufuata na kutii katiba hii na sheria za jamhuri ya muungano”.
7. Kiongozi Wa Nchi (Rais) Kupewa
Madaraka Ya Kuchupa Mipaka (Udikteta)
Ka mujibu wa katiba ya jamhuri kifungu 45 (1):
“Bila ya kuathiri
masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, rais anaweza kutenda lolote kati
ya mambo yafuatayo:
A) kutoa msamaha
kwa mtu yoyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote na
aweza kutoa msamaha bila masharti au kwa masharti kwa mujibu wa sheria.
B) kumwachilia
kabisa au kwa muda maalumu mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa ajili ya
kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo wakati wa muda huo
maalum.
C) kuibadilisha
adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu.
D) kufuta adhabu
yote au sehemu ya adhabu yote”.
8. Uhuru Wa Kubadilisha Dini Anayotaka
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 19 (1):
“Kila mtu
anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini,
pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake”.
9. Sera Ya Kugombea Uongozi Badala Ya
Kugombewa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 67 (3):
“Mtu hataweza
kugombea uchaguzi kuwa mbunge wa kuwakilisha jimbo la uchaguzi katika uchaguzi
mkuu wowote ikiwa wakati huo yeye amesimama katika uchaguzi kugombea kiti cha
Rais, wala hataweza kugombea uchaguzi kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo wowote
ikiwa yeye ni Rais”.
10. Mfumo Wa Vyama
Vingi Vya Siasa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 3 (1):
“Jamhuri ya
muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama
vingi vya siasa”.
11. Kiongozi Mkuu Wa
Nchi (Rais) Kuwa Juu Ya Sheria
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 46:
(1): wakati wote
Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, itakuwa
ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashtaka ya aina yoyote juu yake mahakamani
kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) wakati wote
Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii,
haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au
alilokosea kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya
kushika madaraka ya Rais…
12. Matumizi Ya
Mapambano (Jihadi) Yanakataliwa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 20 (21):
“Bila ya kujali
masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa
kuandikishwa ambacho kutokana na katiba na sera zake:
(c) kinakubali na
kufungamana na matumizi ya nguvu au mapambano kama njia ya kufikia malengo yake
ya kisiasa”.
13. Itikadi Ya
Al-Walaa Wal-Baraa (Kupenda Kwa
Ajili Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Na Kuchukia Kwa Ajili Ya Allaah
(Subhaanahu Wa Ta’ala) Inavunjwa
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Haki ya Usawa,
kifungu 12(4):
Ni marufuku kwa
mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yote inayotekeleza madaraka yake chini
ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya
nchi.
Kifungu 12 (5):
Kwa madhumuni ya
ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja,
haki, au mahitaji mengineyo kwa watu mbali mbali kwa kuzingatia utaifa wao,
kabila, pahali walipotokea, maoni ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali ya
maisha kwa namna ambapo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa dhaifu au
duni au kuwekewa vikwazo au masharti ya upingamizi ambapo watu wa aina nyingine
wanatendewa auwanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima
isipokuwa kwamba neno “kubagua” halitafafanuliwa kwa maana ambayo “itazuia
serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika
jamii.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !