Waislamu Tanzania wanaendelea kuandamwa na kupewa majina mabaya kila uchao lengo ni kuhakikisha hawapumui. Kila tukio baya huhusishwa na Waislamu licha ya kwamba hawahusiki na kubwa zaidi ni kudharauliwa madai yao ya msingi siku zote na kuitwa wachochezi. Pitia Tamko lifuatalo halafu uone jinsi serikali inavyolazimishwa kuwashughulikia Waislamu kwa hali yoyote ile iwayo ili Maaskofu na wafuasi wao wafurahi. Ukiona mtoto amekana kuhusika na jambo fulani, mtoto ambae hana nidhamu ya woga siku zote lazima mzazi apate khofu kwamba kama ni wizi basi huenda ukawa umefanywa na mtoto huyo. Hili ni sawa na Maaskofu Tanzania ambao hawana woga juu ya kuwajibu viongozi serikalini na hata Waislamu lakini wameonekana kushtushwa na madai ya Waislamu ya nchi kuendeshwa na "mfumo kristo". Ambapo Waislamu wanaishutumu serikali sasa leo iweje Maaskofu wajibu wao? Kwa mintarafu hiyo ni dhahiri kuwa nchi hii inaendeshwa na mfumo kristo. Na popote duniani nchi inayoendeshwa kwa mfumo kristo, wananchi hushambuliwa na dhiki, ukame na hali ngumu za maisha kama ilivyo Tanzania leo.
Pitia kwa makini tamko hili:-
TAMKO LA PAMOJA LA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA
JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA.
1.Utangulizi Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF)
linajumuisha Taasisi Kuu za Makanisa nchini kama ifuatavyo:- Jumuiya ya
Kikristo Tanzania – CCT Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania – TEC Jumuiya ya
Makanisa ya Kipentekoste Tanzania – PCT Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA
(Watazamaji) Katika Mkutano wake Mkuu wa Dharura uliofanyika katika Kituo cha
Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini,
Jijini Dar es Salaam, tarehe 8 Machi, 2013; Wajumbe walitafakari kwa undani juu
ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini
Tanzania, pamoja na mauaji na mashambulizi ya viongozi wa dini; na hatua
zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya uhalifu huo unaotekelezwa na Waislamu
wachache. Katika taswira hiyo, Kanisa lilitathmini juu ya wajibu, utume, na
sauti yake ya kinabii kwa taifa letu kuhusiana na mambo hayo.
2. Hali halisi ilivyo hivi sasa hapa nchini
kwa mtazamo wa Kanisa Ushahidi wa kihistoria na kimazingira unaonyesha wazi
kuwa kwa sasa Kanisa nchini Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo
(systematic persecution), kama vipindi vingine 10 vya mateso katika Historia ya
Kanisa hapa duniani. Pamoja na mateso haya ya kimfumo, tunatambua wazi kuwa
wanaotekeleza haya ni kikundi kidogo tu cha Waislamu wa Tanzania, kama wale
wengine wa Barani Afrika (k.m. Boko Haram kule Nigeria). Waislamu walio wengi
hawafurahii mambo yanayotokea. Wao pia wanaitazamia Serikali kuthibiti hawa
wachache wanaochafua dini ya Kiislamu na kuwafanya Waislamu wote waonekane kuwa
maadui wa Ukristo, jambo ambalo siyo kweli. Kutokana na hali hiyo, mkutano mkuu
wa dharura wa Jukwaa la Wakristo umeyaangalia maeneo makuu yenye migogoro ikiwa
ni pamoja na:
2.1. Mgororo wa nani anastahili kuchinja kitoweo Hivi
karibuni hapa nchini tumeshuhuduia mgogoro juu ya uchinjaji wa mifugo ambayo
nyama yake inapaswa kuuzwa kwa watu wa imani mbalimbali wakiwemo Wakristo na
Waislamu. Tunafahamu kwamba sheria ya nchi yetu inaweka bayana juu ya
usalama wa nyama hizo kiafya, lakini sheria haielekezi kuwa dini fulani ndiyo
waumini wake wanapaswa kuchinja mifugo hiyo. Kwa misingi hiyo Kanisa
linatamka kuwa:-
a) Hoja ya dini moja kudai kuhodhi (exclusive right)
uchinjaji wa mifugo kwa misingi ya imani yake ni kinyume cha haki ya uhuru
wa kuabudu ambayo amepewa kila mtu ndani ya nchi hii kikatiba katika Ibara 19.
b) Kwa kuwa kuchinja wanyama na ndege ni Ibada kwa
Waislamu, Kanisa litambue na kuheshimu jambo hilo. Lakini pamoja na kutambua
haki ya Waislamu kujichinjia wanyama na ndege kama Ibada kwao, Wakristo
wasilazimishwe kula nyama zilizochinjwa kwa misingi ya Ibada za Kiislamu. Kwa
kuwa wananchi wa Tanzania ni wa dini mbalimbali na mila za makabila mbalimbali,
tunaitaka Serikali itamke wazi kuwa kila raia ana uhuru wa kufuata imani yake
katika suala la uchinjaji.
c) Kuhusiana na jambo hili tunashindwa kabisa kuelewa
msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine
waandamizi wa Serikali. Wakati wa Serikali ya awamu ya pili chini ya Rais
Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Muislamu, ulipotokea ugomvi wa mabucha
ya nyama ya nguruwe Dar es Salaam, Rais huyu Mstaafu kwa kulinda Katiba ya nchi
ambayo aliapa kuilinda, alisema mwenyewe kwa nguvu zote kuwa kila mtu ana uhuru
wa kula anachotaka na mtu wa dini moja asimhukumu mtu wa dini nyingine kwa kile
anachokula. Baada ya Rais Mstaafu kukemea jambo hili, hali ikawa ya amani na
utulivu. Kwa nini Serikali yetu ya sasa inapata kigugumizi kuhusiana na
suala zima la nani achinje?
d) Kwa mantiki hiyo hapo juu katika kipengele cha a-c, Wakristo
wanaitaka Serikali iweke utaratibu wa kugawana machinjio na mabucha kati ya
Wakristo na Waislamu ili kila Mtanzania awe huru kujinunulia kitoweo mahali
anapotaka. Sambamba na kuitaka Serikali kufanya hivyo, tunawakumbusha
Wakristo wote Tanzania kuelewa kuwa watakuwa hawajavunja sheria yoyote ya nchi
wakiamua kujichinjia kitoweo chao wenyewe. Kuhusiana na tangazo hili kwa
Wakristo wote, tunaitaka mihimili ya dola (Serikali na Mahakama) kuheshimu
Katiba ya Nchi yetu, na kipekee kuhusiana na jambo hili Ibara ile ya 19.
e) Kwa upande mwingine, kwa kuwa tayari zipo bidhaa za
vyakula katika nchi hii ambazo zina nembo ya ‘halal’ na nyingine hazina nembo
hiyo, huu ni uthibitisho kuwa vyakula hivyo vimegawanywa kwa kufuata misingi ya
imani za kidini. Kwa hiyo, madai ya kugawanya machinjio na mabucha kwa kufuata
misingi ya dini sio jambo jipya kwa sasa katika nchi hii.
2.2 Uchomaji wa Makanisa ulioambatana na vitisho na
mauaji ya viongozi wa KanisaKanisa linalaani vikali mauaji ya kidini
yanayoendelea kufanywa pamoja na vitisho (systematic persecution) kwa viongozi
wa Kanisa na Wakristo wote kwa ujumla. Mtiririko wa matukio mbali mbali ya
nyuma yanatudhihirishia kuwa kumekuwepo na mpango wa muda mrefu wa haya
yanayotokea sasa hivi. Tarehe 15 Januari 2011, kundi la Waumini wa Kiislamu
walipokutana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, miongoni mwao walikuwamo
mashehe, walijadili hali ya nchi ya Tanzania kuongozwa kwa mfumo wa kidini.
Mkutano huo ulihitimishwa kwa kutoa tamko dhidi ya kile kilichoitwa mfumo
Kristo katika nchi yetu! Japo Serikali na vyombo vyake vya usalama wa Taifa
vimekuwa vikipata taarifa za vitisho dhidi ya viongozi wa Kanisa, mauaji,
kuchomwa kwa nyumba za ibada, pamoja na maneno ya uchochezi kupitia mihadhara,
vipeperushi, CD na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi zinazofahamika,
hata hivyo Serikali kwa kiasi kikubwa imeshindwa kuchukua hatua kwa wakati
muafaka na wanasubiri hadi maovu yatendeke ndipo ati waanze kufanya uchunguzi.
Kwa Serikali yetu inaonekana wazi kuwa katika hili ile methali kwamba “Kinga ni
bora kuliko tiba” haina maana yoyote. Hii ni kuonyesha udhaifu mkubwa wa
vyombo vya usalama wa Taifa au pia kwamba vyombo hivi vinafurahia kutoweka kwa
amani nchini mwetu, jambo ambalo linalifanya Kanisa nchini Tanzania liamini
kwamba matukio haya yanayoendelea kutokea ni dalili kuwa Serikali ina agenda ya
siri dhidi ya Ukristo. Kutokana na hayo Jukwaa la Wakristo Tanzania
linatamka kama ifuatavyo:
a) Tunatambua kwamba ni jukumu la Serikali kuwatendea
raia wake kwa usawa na bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 12 na 13 ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa wanatamka
kwamba Serikali imeshindwa kuheshimu Katiba juu ya hizi haki za raia wake na
kupelekea waamini wa dini ya Kikristo kukosa imani na Serikali iliyoko
madarakani, hasa kuhusu ulinzi na usalama wao na mali zao kama inavyoagizwa
kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Kama
Serikali inaona haiwezi kuwahakikishia wananchi usalama wa uhai wao na mali
zao, na hivyo kuwafanya waishi maisha ya hofu inayotokana na vitisho, basi kwa
mujibu wa Katiba ya nchi yetu, hakuna sababu ya Serikali iliyoko madarakani
kung’ang’ania kuongoza nchi.
b) Kwa kuwa ulinzi wa raia ni haki ya kikatiba na
kisheria, Serikali inatakiwa iwalinde raia wake. Kama Serikali imeshindwa
kuwalinda raia wake, Kanisa linataka Serikali ikiri hivyo ili Kanisa
liwaambie wananchi waiwajibishe Serikali na Viongozi wanaoifanya Serikali
ishindwe kutimiza wajibu wake. Jukwaa la Wakristo linasema: Kama
Serikali haitachukua hatua za makusudi dhidi ya mambo haya yaliyoainishwa hapo
juu, Kanisa litachukua hatua ya kuwaambia waamini wake kwamba Serikali iliyoko
madarakani inaibeba dini moja, na hivyo Kanisa litatafakari upya uhusiano wake
na Serikali.
3. Wakristo walioko Zanzibar Wakristo walioko Zanzibar
wanatishiwa maisha yao na mali zao zinaharibiwa mara kwa mara, kiasi cha
wengine kuamua kuhamia Tanzania Bara. Kigezo cha unyanyasaji huo ni suala la
udini na muungano. Inaonekana ni kama vile Watanzania waliozaliwa Bara hawana
haki ya kuishi Visiwani. Na kumbe wale waliozaliwa Visiwani wafikapo Barani
wana haki zote. Kanisa linaitaka Serikali iwahakikishie Wakristo walioko
Zanzibar usalama wao na wa mali zao maana hiyo ni haki yao ya Kikatiba. 4.
Vitisho na mauaji ya Wanakanisa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
ichukue hatua za makusudi za kuzuia vitisho na mauaji kwa Viongozi wa Kanisa na
Wakristo kwa ujumla. Vinginevyo Kanisa litautangazia ulimwengu kuwa Tanzania
ni nchi mojawapo inayovunja haki za binadamu kwa ubaguzi wa kidini na kulitesa
Kanisa kimfumo.
5. Matumizi ya Vyombo vya Habari: Kwa kuwa kuna baadhi ya
vyombo vya habari ambavyo vimeruhusu vitumiwe kuwatukana Viongozi wa Kanisa,
tunatoa nafasi kwa vyombo hivyo kuomba radhi; vinginevyo tutaitaka dunia
ivielewe kuwa navyo ni sehemu ya chanzo cha migogoro. Pia tunachukua nafasi hii
kuvitahadharisha vyombo mbalimbali vya habari kupima kwa kina ni nini
kinachosemwa na viongozi wa kidini ili kuviepusha vyombo hivyo kutumika kwa nia
ya uchochezi; yasije yakatukuta kama yale yaliyotokea kule Rwanda 1994.
6. Hitimisho: Kanisa linaendelea kusisitiza kuwa silaha
kuu ya Mkristo katika nyakati hizi ni maombi na kufunga. Kwa mantiki hiyo, Kanisa
linawataka Wakristo wote nchini Tanzania kuungana kwa pamoja katika maombi na
kufunga kwa muda wa siku saba kwa ajili ya hali hii iliyojitokeza hapa nchini.
Maombi hayo na mfungo vifanyike kabla ya Pasaka, yaani kuanzia, tarehe 24/3/2013 hadi 30/3/2013. Kwa niaba ya Maaskofu 177 walioshiriki
katika Mkutano Mkuu wa Dharura wa Jukwaa la Wakristo na kutoa maazimio hayo. 1.
Askofu Peter Kitula – Mwenyekiti CCT 2. Askofu Tarcisius J. M. Ngalalekumtwa
Rais TEC 3. Askofu David Batenzi Mwenyekiti PCT DAR ES SALAAM,
19.03.2013 source Oikos Tamko la Maaskofu kuhusu uchinjaji na hali ya mwelekeo wa
kisiasa nchini
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !