Makosa Ya Msingi
Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa
Uislamu.
SURA YA SITA
Tafsiri Sahihi Ya Baadhi Ya Maneno
Na Vifungu Vya Katiba Ya Jamhuri
1. Neno Ibada: Kwa
Mtazamo Wa Uislam Ni Pana Sana
Wanachuoni wetu wanakubaliana kwamba ibada ni:
"كل ما يحب الله ويرضاه من الأقوال والأعمال
الظاهرة والباطنة”
“Ni kila anachokipenda Mwenyezi Mungu na kukiridhia
katika maneno na matendo ya dhahiri na ya siri (moyoni)”.
Malengo ya Kuumbwa kwetu:
قال تعالى:﴿ وَمَا
خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ﴾(الذريات:٥٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Sikuumba majini na watu isipokuwa kwa ajili ya
kuniabudu Mimi tu”
(Adh-Dhaariyaat: 56).
Kumuabudu
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hakuna maana ya kuswali, kufunga, kuhiji
tu. Bali ndoa, kazi, biashara kuhukumiana kwa shari’ah ni ibada.
قال تعالى:﴿ قُلْ
إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ
الْعَالَمِينَ﴾(الأنعام:١٦٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika Swalah yangu na Ibada yangu (kuchinja) na
uhai wangu na kifo changu ni kwa ajili ya Allaah Mola wa viumbe wote)”
(Surat Al-An’aam: 162).
Kuhukumu kwa haki ni Ibada.
قال تعالى:﴿ إِنِ
الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ﴾(يوسف:٤٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hukumu ni miliki ya Allaah Ameamrisha musiabudu
(chochote) isipokuwa Yeye tu)”
(Surat Yuusuf: 40).
قال شمس الأئمة
السرخسى:إعلم أن القضاء بالحق من أقوى الفرائض بعد الإيمان بالله تعالى وهو من
أشرف العبادات(المبسوط:١٦٥ ص٥٩،٦٠).
Amesema Shamsu Al-Aimmah As-Sarkhasi:
“Elewa kwamba kuhukumu kwa haki ni miongoni mwa
faradhi kubwa baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu na hiyo ndio Ibada tukufu”
(Al-Mabsuutw, uk. 59-60).
2. Neno Halali Ni Hukmu Ya Kishari’ah
Ni Kila Aliloliridhia Mola Kufanywa Kwa Mujibu Wa Shari’ah
Kwa mujibu wa katiba ukiuza pombe maadam unalipa
leseni, kodi na pombe si ya magendo basi kazi hii ni Halali.
Kufanya muamala wa riba ni halali.
Kamari ni halali.
قال تعالى:﴿
إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنْصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِنْ
عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ﴾(المائدة:٩٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika pombe na kamari na mizimu ni uchafu utokanao
na matendo ya Shaytwaan jiepusheni nayo”
(Surat Al-Maaidah: 90).
وقال تعالى:﴿
وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ﴾(البقرة:٢٧٥).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na Amehalalisha Mwenyezi Mungu biashara na
ameharamisha riba”
(Surat Al-Baqarah: 275).
3. Neno Haki Ya Kuishi
Mtu akiua hauawi kwa sababu eti ana haki ya kuishi.
Katika kesi ya Attorney (Mwendesha mashtaka wa
serikali) V/s Mbushumi (Kesi ya jinai Na.14, Dodoma 1991.) Katika kesi hii
mtuhumiwa Mbushumi Mnywaga alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ambapo kwa
mujibu wa sheria, adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Mshtakiwa (mtuhumiwa) katika kesi hii alidai
mahakamani haki ya msingi ya kuishi kwa mujibu wa katiba.
Mahakama ilkubaliana nae na hivyo kumhukumu
mshitakiwa kwenda jela maisha badala ya kunyongwa hadi kufa.
(Angalia kitabu, Haki na wajibu wa raia uk.23
kilichotolewa na C.P.T (Christian Prof.of Tanzania).
Katika Uislamu mtu anaeua kwa dhulma nae anauliwa
kutekeleza kisasi.
قال تعالى:﴿
وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ﴾(البقرة:١٧٩).
Amesema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na mna (nyinyi)
kwenye kisasi uhai enyi wenye akili”
(Surat Al-Baqarah:
179).
4. Haki Ya Usawa Kwa Wote
Katika Uislamu binaadam wote ni sawa katika asili,
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ
ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ
أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ﴾(الحجرات:١٣)
”Enyi wtu hakika Sisi Tumewaumbeni kutokana na
mwanamme mmoja (Aadam) na mwanamke mmoja (Hawwaa) na Tukawajaalia kuwa mataifa
mbali mbali na makabila ili mpate kujuana, hakika mbora wenu mbele ya Allaah ni
Mcha Mungu zaidi kwenu”
(Surat Al-Hujuraat: 13).
Lakini hii haina maana kwamba mwanamme na mwanamke
wamepewa haki na majukumu sawa kwa kila kitu.
Katika tangazo la haki za binaadam:
Kifungu 16(1) la mwaka 1948:
“Mwanamme na
mwanamke pindipo wakifikia umri wa baleghe watakuwa na haki ya kuoana na
kuasisi familia bila kikwazo kwa sababu ya nasaba, utaifa au dini, kwani wao
wote wana haki sawa katika ndoa na wakati wa kusimamisha maisha ya ndoa na
wakati wa mtengano’’ (uk.74).
(أنظر كتاب حقوق الإنسان في الإسلام للدكتور سليمان بن
عبدالرحمن الحقيل(ط الثانية ١٤١٥ﻫ١٩٩٤ﻡ)
Tazama kitabu cha HAKI ZA BINADAMU KATIKA UISLAMU cha
Dr. Suleiman Ibn Abdulrahmani Al Huqail chapa ya pili 1415H, 1994.
Tanzania ilitia saini mkataba wa kimataifa wa haki za
binaadam 1966 na ukatiwa katika katiba mwaka 1966 ibara ya 9(f) nayo inasema
hivi:
“Kwamba heshima ya
binaadam inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata kanuni za tangazo la dunia
kuhusu haki za binaadam”.
قال تعالى:﴿ يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ
اللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا
تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ لَا هُنَّ حِلٌّ لَهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ
لَهُنَّ وَآَتُوهُمْ مَا أَنْفَقُوا وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَنْ تَنْكِحُوهُنَّ
إِذَا آَتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ
الْكَوَافِرِ﴾(الممتحنة:١٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Enyi ambao mulioamini watakapowajieni wanawake
Waumini wenye kuhama basi wapeni mtihani Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi kuhusu
kuamini kwao, kama mkijua kwamba wao ni Waumini basi musiwarejeshe kwa
makafiri, hao (wanawake) sio halali kwao wala wao sio halali kwao (kwa vile ni
makafiri, na wapeni walichotoa (mahari), na wala si vibaya kwenu kuwaoa wao
kama mtawapa mahari zao wala musiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha
ndoa zenu”
(Al-Mumtahinah: 10).
Kifungu hiki cha katiba kimempa mwanamke usawa wa mia
kwa mia na mwanamme, katika Mirathi na Uongozi.
قال تعالى:﴿
فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنْثَيَيْنِ﴾(النساء:١٧٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Basi mwanamme ana mara mbili ya fungu la mwanamke”. (Surat
An-Nisaa: 172).
وقال تعالى:﴿
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَى
بَعْضٍ﴾(النساء:٣٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Wanaume ni wasimamizi (viongozi) wa wanawake ni
katika yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaboresha baadhi yenu kwa baadhi.”
(Surat An-Nisaa: 34).
Waislam hawawezi kuwa sawa na watu waovu:
وقال تعالى:﴿
أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ﴾(القلم:٣٥).
Amesema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hivi tunawafanya
Waislamu ni kama waovu!”
(Surat Al-Qalam:
35).
وقال صلى الله عليه
وسلم:(لن يفلح قوم ولو أمرهم امرأة)رواه البخاري.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
“Hawatofaulu kamwe watu waliomfanya mwanamke kutawalia jambo lao”.
(Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy).
Katika tangazo la Haki na Usawa la umoja wa mataifa
kafiri anaweza kuwa sawa na muislam, hivyo kafiri anaweza kuoa binti wa
Kiislam, katika Uislam jambo hilo halikubaliwi.
قال تعالى:﴿ وَلَا
تُنْكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّى يُؤْمِنُوا ﴾(البقرة:٢٢١).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Wala musiwaoze washirikina mpaka waamini”. (Surat al
Baqarah:221).
وقال تعالى:﴿ وَلَا
تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ﴾(الممتحنة:١٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na wala msiwaweke wanawake wa kikafiri katika
kifungo cha ndoa zenu”
(Surat Al-Mumtahinah: 10).
5. Haki Ya Kumiliki
Pamoja na kwamba Uislamu unampa mtu haki ya kumiliki
na kutasarafu na mali aliyoichuma,
قال تعالى:﴿
لِلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِمَّا اكْتَسَبُوا وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِمَّا
اكْتَسَبْنَ﴾(النساء:٣٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Wana wanaume fungu katika vile walivyovichuma na
wanawake wana fungu katika vile walivyochuma”
(Surat An-Nisaa: 32).
Lakini, mtu hawezi kumuandikia mrithi wasia na huyo
ambaye ameandikiwa wasia haruhusiwi kupewa zawadi ya 1/3 ya mali ya mtu.
قال صلى الله عليه
وسلم:(إن الله قد أعطى كل ذي حق حقه فلا وصية للوارث)(رواه أبي داود وابن ماجه).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
”Hakika Allaah Amempa kila mwenye haki haki yake, hakuna usia kwa mrithi)”
(Wameipokea Abu Daawuud na Ibn Maajah).
وقال صلى الله عليه
وسلم:(الثلث،والثلث كثير(رواه البخاري ومسلم).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) juu
ya kiwango anachostahiki kuandikiwa wasia :
“Theluthi, na theluti pia ni nyingi”
)Wameipokea Imaam
Al-Bukhaariy na Muslim).
Sheria za nchi ni kinyume cha hayo kwa madai ya
kutetea haki za kikatiba.
Katika kesi ya rufaa Na.5/1997 iliyosikilizwa na mahakama
ya rufaa Dsm, kati ya Anwar Z. Mohamed vs Saidi Selemani Masuka, katika hukumu
yake June 10, 1997, Jaji Ramadhani alihoji hukumu ya Jaji Msumi ya sept, 5,
1996, aliyetengua wasia unaodaiwa kuachwa na Rukia Ahmed kwamba mume wake Anwar
Z. Mohamed arithi mali yake yote.
Katika hukumu yake Jaji Msumi wa mahakama kuu wakati
huo alitoa hoja kwmba kwa mujibu wa shari’ah za Kiislam hakuna wasia kwa mrithi
na hakuna wasia zaidi ya 1/3 ya mali.
Uamuzi huo wa Jaji Msumi ulipingwa na Jaji Korosso
(wakili katika kesi hii) akiitaka mahakama ipuuze na itupilie kwa mbali
shari’ah hiyo ya Kiislam kwa madai kwamba inavunja haki ya kikatiba kifungu cha
24 kinachompa mtu haki ya kumiliki na kutumia atakavyo. Hata hivyo Jaji Msumi
alisisitiza kwamba Shari’ah na mirathi za Kiislam ni sehemu katika Qur-aan na
ni lazima Waislam warithiane kwa Shari’ah hii. Na akaonya kuichezea Shari’ah
hiyo ni sawa na kuichezea Qur-aan, jambo ambalo alisema Jaji Msumi hadhani
kwamba yupo mtu mwenye kutakia mema nchi hii anaweza kulikaribia.
Jaji Ramadhani kwa upande wake alidai kwamba Jaji
Msumi amejichanganya mwenyewe katika hukumu yake kwamba amezingatia “Udini” na
uzalendo badala ya sheria. Na alisisitiza kanuni ya kutotambua sheria au kanuni
zinazokiuka haki za kikatiba.
Waliotengua hukumu hiyo ni waheshimiwa majaji wa
mahakama ya rufaa:
L. M. Makanja, D. Z. Lubavu na B. A. Samatta.
Katika kesi hiyo ya Anwar dhidi ya Saidi aliyekuwa
mume wa marehemu Rukia Ahmed mwanamke aliyeolewa na Bw.Saidi. Marehemu
aliandika wasia wa mali yake yote kwa mumewe Bw.Saidi akimwacha mwanawe wa
kuzaa ndugu Anwar bila ya urithi wowote. Ndugu Anwar alikuwa mtoto wa marehemu
lakini kwa mume mwingine. Mtoto wa marehemu alipinga kutambuliwa kwa wasia huo
kwani ni kinyume cha Shari’ah za Kiislam na akakoseshwa kurithi.
(Angalia Sheria za Kiislam ya Mirathi na wasia) cha
Mahmud A.Sameya uk.91 na 92).
6. Kufuta Adhabu Ya Viboko Ni Kinyume
Cha Shari’ah Ya Kiislam
Kifungu 13(6) (e) Kinasema:
Ni marufuku kwa
mtu kuteswa kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtesa au kumdhalilisha.
Uislam unaruhusu adhabu ya viboko.
قال تعالى:﴿
الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِئَةَ
جَلْدَةٍ﴾(النور:٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanaume wapigeni kila
mmoja mijeledi mia moja”
(Surat An-Nuur: 2).
وقال تعالى:﴿
وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ
فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً﴾(النور:٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na wale ambao wanawasingizia machafu wanawake wenye
kujihifadhi na (machafu) kisha hawakuleta mashahidi wanne wapigeni mijeledi
thamanini”
(Surat An-Nuur: 4).
وقال صلى الله عليه وسلم:(مروا أولادكم الصلاة
وهم أبناء سبع واضربوهم عليها إذا بلغوا عشرة)(رواه أبوداود).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
”Waamrisheni watoto wenu Swalah wakiwa na umri wa
miaka saba na wapigeni kwa kuacha Swalah watakapofika umri wa miaka kumi”
(Imepokewa na Abu Daawuud).
HITIMISHO
Wakati tukiwa katika hatua za mwisho za uandishi wa
kitabu hiki, wananchi wote tumeshtukiziwa na Mswaada wa Sheria ya mwaka 2011
ambayo umekusudia kuweka masharti ya uanzishaji wa Tume, pamoja na sekretarieti
kwa madhumuni ya kuendesha na kusimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Cha kushangaza serikali ilitoa hati ya dharura kwa
maana ya kwamba wananchi wachangie maoni juu ya Mswaada huu haraka haraka ili
upitishwe na bunge kwa njia ya haraka. Muda uliotolewa ni mfupi mno na vituo
vya kutoa maoni, vilipangwa kuwa ni vitatu tu Dar es Salaam, Dodoma na
Zanzibar.
Wananchi wengi hawakuridhishwa na mchakato huu, jambo
ambalo limepelekea zoezi hili kuakhirishwa ili wananchi wapewe muda zaidi wa
kutoa maoni.
Baada ya kufaulu kupata nakala ya Mswaada huu
tumegundua Mswaada huu una mapungufu mengi lakini makubwa katika hayo ni lile la kuwafunga wananchi wasiyaguse yale
ambayo kwa mtazamo wa waliotunga Mswaada huu ni tunu na maadili matakatifu ya
kitaifa hivyo yasipingwe katika hayo ni yale yaliyokuja katika kipengele cha 9
(2) :
(a) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
(b) Msingi /Asili ya Usekula (kutenganisha siasa na
dini) ya Jamhuri ya Muungano.
Masharti haya hayakubaliki kwa sababu yanawanyima
raia ambao ndio watunzi halisi wa katiba, Uhuru wa Maoni ambao wamepewa na
kipengele cha 18 (1) na 19 (1) cha Katiba ya nchi hii.
Upande wetu Waislamu wazo la kuifanya nchi hii idumu
kuwa ni ya kisekula inayotenganisha Dini na Utawala ni wazo lisilokubalika hasa
ukizingatia kwamba wazo lenyewe asili yake ni Dini ya Kikristo kama tulivyoona
katika kitabu hiki. Wazanzibari kwa mfano ambao wana nchi yao yenye wakazi
asilimia 99 Waislam wana haki ya kutangaza kwamba nchi yao ni ya Kiislamu yenye
kufuata Shari’ah za Kiislam, wenyewe wana haki ya kufanya maamuzi haya.
Kitabu hiki tunataraji kitakua ni msaada mkubwa wa
Rejea kwa kila anaetaka kuchangia maoni ya Utunzi wa Katiba mpya, kwa sababu
kimetoa picha ya Makosa ya Msingi yaliyomo ndani ya Katiba iliyopo. Hivyo
marekebisho yoyote ni lazima yachunge mtazamo huo.
Mola Atupe Tawfiq.
18/5/1432 H sawa na 22/4/2011 M
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !