Monday, December 31, 2012
Tamko la Tanzania Christian Forum (TCF)
TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF)
MKUTANO MKUU WA NNE WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA (TCF)
TAMKO RASMI
“ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA”
“ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA”
Utangulizi
Katika
Mkutano Mkuu wa Nne wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, Tanzania
Christian Forum – TCF, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na
Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini jijini Dar es
Salaam, tarehe 6 Desemba, 2012; Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota
kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja
na kutathmini juu ya wajibu wa Kanisa na Utume wake wa Kinabii kwa taifa
letu.
Jukwaa
la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha taasisi kuu za Umoja wa Makanisa nchini
kama ifuatavyo;-
- Jumuiya ya Kikristo Tanzania - CCT
- Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC
- Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania - PCT
- Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (observers)
Tafakari
Tafakari
yetu ilianza kwa kujiuliza yafuatayo:
- Ni mwenendo gani uliotusibu hivi karibuni kusababisha kukutana
kwetu hapa? Vikundi vya kihalifu vikiongozwa chini ya mwavuli wa
waamini wa Kiislamu vimekuwa vikishambulia kwa ukali na kikatili sana imani,
mali, majengo na makanisa ya Wakristo kwa jeuri na kujiamini.
- Kwa mwenendo huo ni kitu gani kilicho hatarini?
Vitendo na mienendo yote ya namna hiyo inahujumu sana Amani, Mapatano na
Uelewano kati ya watu wote nchini mwetu. Tunaelewa kwamba ni waamini wachache
tu wenye kutenda maovu hayo, lakini mienendo ya kikatili ya namna hii huchochea
shari miongoni mwa walengwa wa ukatili husika na kutaka kulipiza kisasi hata
kusababisha uvunjifu wa amani.
- Ni athari gani kwa nchi, katika muda ujao, iwapo mienendo hiyo
haitadhibitiwa na kukomeshwa kabisa? Katika nyakati zetu hizi,
tunashuhudia fadhaa na migogoro mingi ya kijamii. Kuna hasira kubwa ya
chinichini inayotokana na kasoro nyingi za kiutendaji katika mihimili mikuu ya
uongozi na utando mkubwa wa ufukara wa kutupwa kwa wananchi wengi usio na
matumaini ya kumalizika hivi karibuni. Hatari ya hali hii ni dhahiri kwamba
makundi nyemelezi (kisiasa, kiuchumi na kidini), kwa kutumia vikundi halifu
vilivyo katika hali ya ufukara na migogoro, yatavielekeza kimapambano na
kiharakati kutetea kijeuri ajenda hasimu za wale walio madarakani au washindani
wao kwa maslahi ya wanyemelezi. Hali tunayoelezea sio ya kufikirika kwani ndiyo
inayotokea huko nchini Nigeria, Kenya na nchi za Afrika ya Kaskazini hivi sasa.
Tanzania haina kinga ya kipekee kuiepusha kukumbwa na maovu ya namna hiyo bila
utaratibu na vyombo thabiti kuhimili mienendo hasi kama hii. Kutokana na matukio
na kauli zinazotolewa na watu mbalimbali hapa nchini, inawezekana tayari
wanyemelezi wako kazini wakiongoza vikundi kusukuma ajenda za kutekeleza maslahi
yao.
- Masuala yanayotakiwa kufafanuliwa na kudhibitiwa na Dola mapema
ili yasiendelee kupotoshwa:
- Hali ya mahusiano kuzorota pamoja na kashfa dhidi ya
Kanisa. Huu ni wakati wa kukubali kwamba misingi ya Haki, Amani na
Upendo katika Taifa letu imetikiswa kwa kiwango kikubwa. Uchochezi, kashfa,
matusi na uchokozi wa wazi na makusudi unaofanywa na baadhi ya waamini wa dini
ya Kiislamu, ukiendeshwa na kuenezwa kupitia vyombo vyao vya habari vya kidini
(redio na magazeti) mihadhara, kanda za video, CD, DVD, vipeperushi,
makongamano, machapisho mbalimbali na kauli za wazi za viongozi wa siasa na hata
viongozi wa dini husika (ushahidi wa mambo yote haya tunao) pasipo Serikali
kuchukua hatua yeyote huku bali imekuwa ikibakia kimya tu. Ukimya huu unatoa
taswira ya Serikali kuunga mkono chokochoko hizi. Jambo hili linavyoendelea
kuachwa hivi hivi linaashiria hatari kubwa ya kimahusiano siku zijazo.
- Hadhi ya Baba wa Taifa kuhifadhiwa. Huyu ni kiongozi
aliyetoa maisha yake kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu akitetea Watanzania wote
bila ubaguzi wowote, akiimarisha umoja wa Kitaifa, amani na upendo kwa watu
wote. Kashfa, kejeli na habari za uongo dhidi yake ni kukipotosha kizazi hiki na
hata vizazi vijavyo kwa kuondoa moja ya alama muhimu ambazo kiongozi huyo
alisimamia kwa ajili ya umoja wa kitaifa.
- “Memorandum of Understanding” (M.o.U) ya mwaka
1992, kwa ajili ya huduma za kijamii zitolewazo na Makanisa kwa
Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na huduma za hospitali, vituo vya afya na
zahanati na shule mbalimbali zinazoendeshwa na Makanisa nchini kote. Ni vema
ikaeleweka wazi kwamba makubaliano hayo (M.o.U) yalikuwa ni kati ya Makanisa ya
Tanzania na Makanisa ya nchini Ujerumani ambapo Serikali ya Tanzania ilihusishwa
tu, kwa vile raia wake ndio wangenufaika na misaada hiyo ambayo nchi ya
Ujerumani ingeitoa kupitia Makanisa hayo. Kanisa limeendelea
kujishughulisha na huduma hizi kwa jamii hata kabla ya uhuru na baada ya uhuru
pasipo ubaguzi. Ikibidi ni vema kuondoa hali hii, ya Kanisa kuendelea kutukanwa,
chuki na kukashifiwa viongozi wake kutokana na huduma hizi kwa jamii yote.Jukwaa
la Wakristo Tanzania tunaitaka Serikali itoe tamko la ufafanuzi juu
ya M.o.U hiyo, maana yake, makusudi yake na manufaa
yake kwa Watanzania wote.
- Hujuma ya kuchomwa Makanisa na mali za Kanisa, ni tukio la
uvamizi na uchokozi wa wazi, ulioyakuta makanisa yetu na waamini wake wakiwa
hawana habari na bila maandalizi yoyote. Ni muhimu kuanzia sasa, Wakristo wote
wakae macho na wawe waangalifu zaidi.
- Dhana ya kuwa Tanzania inaendeshwa kwa mfumo Kristo ni
potofu na potevu. Maneno hayo ni ushahidi wa uwepo wa ajenda za waamini
wenye imani kali na waliojiandaa kwa mapambano maovu kutetea dhana potovu
kinzani na misingi ya demokrasia na haki za binadamu kama ilivyotangazwa na
Umoja wa Mataifa na kuridhiwa na Serikali yetu. Jukwaa la Wakristo nchini
tunakanusha wazi wazi na kueleza bayana kuwa, nchi hii haiongozwi
kwa mfumo Kristo!. Kwa watu walio makini hakuna kificho kuwa
viongozi wote waandamizi wa ngazi ya juu Serikalini awamu ya sasa, asilimia 90
ni Waislamu (Rais wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu, Makamu wa Rais, Mkuu wa Usalama
wa Taifa, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi). Kwa mantiki hiyo haiingii akilini
kueleza watu kuwa nchi hii inaendeshwa kwa mfumo
Kristo! Kwa upande wa Zanzibar asilimia 100 ya viongozi ngazi za
juu Serikalini ni Waislamu, na sio kweli kwamba Zanzibar hakuna Wakristo wenye
sifa za kuongoza. Kisha, hata uwakilishi wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, theluthi mbili ya wajumbe wake ni Waislamu. Tunayo mifano
mingine mingi iliyo wazi, na hii ni baadhi tu. Watanzania wanapaswa kuelewa wazi
kuwa, nchi hii inaongozwa kwa misingi ya Utawala wa Kisheria na sio
vinginevyo.
- Matumizi hasi ya Vyombo vya Habari vya Kidini: Vyombo vya
habari vya kidini vinatumiwa na viongozi wa dini ya Kiislam kuukashifu Ukristo
na kuwachochea Waislamu hadharani kupitia vyombo hivyo wakiwataka wawaue
Maaskofu na Wachungaji, iwe kwa siri au hadharani. Japo
Serikali imesikia kashfa na uchochezi huo hatarishi, imendelea kukaa kimya, na
kuwaacha wachochezi hao wakiendelea kuhatarisha amani bila kuwadhibiti. Jambo
hili linatia mashaka makubwa juu ya umakini wa Dola kuhusu usalama wa wananchi
nchini mwao. Imani kali za namna hii huchochea vitendo viovu vya uasi na hujuma
sio tu dhidi ya waamini na viongozi wa dini fulani, bali hata na kwa Serikali na
viongozi waliopo madarakani, endapo waamini wa dini fulani katika taifa kama
Tanzania lililo na waamini wa dini nyingi tofauti, hawataheshimu na kutendeana
kiungwana baina yao na wale wasio wa dini na mapokeo yao. Hali hii inapelekea
kujiuliza kama je,huu ni wakati mwafaka kwa kila raia au kiongozi wa dini
kujilinda yeye mwenyewe na waamini wake dhidi ya wenye imani kali?
- Matukio yanayosababisha hasira na kutenda maovu: Tumejionea matukio kadhaa ambayo kwayo vikundi vya watu wenye hasira vilisababisha hujuma na uharibifu mkubwa wa mali za watu wengine. Hivyo ni viashiria tosha vya uchovu na unyonge mkubwa katika jamii yetu, ambamo jambo dogo tu na hata la kupuuzwa, likitendwa na afikiriwaye kuwa hasimu wa watu fulani, wahalifu hujipatia fursa ya kuonesha hasira yao kwa vitendo vya hujuma na shari, wakiharibu hata kuteketeza mali na nyenzo za maisha ya jamii. Suala hili lataka uchambuzi yakinifu na wa kiroho ili kupata majibu na maelezo sahihi na wala sio kwa kutumia nguvu za ziada za kijeshi au kwa majibu mepesi ya kisiasa. Hili ni suala lihusulo tunu na maadili ya jamii yote ya Watanzania katika ujumla wao. Kila mmoja wetu ni mhusika na sote tukitakiwa kuwajibikiana katika ujenzi wa amani iletayo mapatano na uelewano kati yetu.
- Hali ya mahusiano kuzorota pamoja na kashfa dhidi ya
Kanisa. Huu ni wakati wa kukubali kwamba misingi ya Haki, Amani na
Upendo katika Taifa letu imetikiswa kwa kiwango kikubwa. Uchochezi, kashfa,
matusi na uchokozi wa wazi na makusudi unaofanywa na baadhi ya waamini wa dini
ya Kiislamu, ukiendeshwa na kuenezwa kupitia vyombo vyao vya habari vya kidini
(redio na magazeti) mihadhara, kanda za video, CD, DVD, vipeperushi,
makongamano, machapisho mbalimbali na kauli za wazi za viongozi wa siasa na hata
viongozi wa dini husika (ushahidi wa mambo yote haya tunao) pasipo Serikali
kuchukua hatua yeyote huku bali imekuwa ikibakia kimya tu. Ukimya huu unatoa
taswira ya Serikali kuunga mkono chokochoko hizi. Jambo hili linavyoendelea
kuachwa hivi hivi linaashiria hatari kubwa ya kimahusiano siku zijazo.
Mapendekezo:
Kutokana
na muono wetu huo tunapendekeza yafuatayo:
- Tabia na mienendo ya kukashifiana ikomeshwe kabisa na badala yake tujengeane heshima/staha tukizingatia utu wa kila mmoja katika utofauti wetu.
- Tumwendee Mungu wetu na kumwomba atuongoze sote kufuata utashi wake tukitafuta huruma yake iliyo sheheni upendo wake mkuu, ili atujalie umoja wa kuishi pamoja kwa amani nchini mwetu.
- Tunaitaka Serikali yetu na vyombo vyake vya usalama, sheria na amani kutenda mara moja na bila kuchelewa, katika nyakati ambazo vikundi halifu kisiasa au kidini vinapoanza uchochezi ili kupambanisha wanajamii. Tabia ya kuachia uchochezi wa kidini kuendelea pasipo hatua mathubuti kuchukuliwa na Dola ni udhaifu mkubwa wa uongozi na uwajibikaji. Ikithibitika kwamba uharibifu uliofanywa ulitokana na kikundi mahususi chini ya uongozi wa dini au chama cha kisiasa au asasi isiyo ya kiserikali, basi taasisi husika iwajibishwe na kulipa fidia kwa uharibifu uliofanywa.
- Lianzishwe Baraza mahsusi lililo huru lisiloegemea chama chochote cha kisiasa wala dini yoyote na litamkwe na kuwezeshwa kikatiba likiwa na dhumuni kuu la kuilinda na kuiongoza Serikali kuto fungamana na dini yoyote na kuhakikisha kwamba dira na dhana ya utu katika mfumo wa uchumi wenye kujali maslahi ya wote havipotoshwi. Baraza hilo liwe na uwezo wa kuvichunguza vyombo vya sheria na usalama itokeapo matatizo makubwa yaashiriayo uvunjifu wa haki na kuteteresha usalama wa nchi.
- Na sisi viongozi wa dini za Kikristo, Kiislam, Kihindu na nyinginezo tuwajibike katika kufundisha, na katika majiundo ya waamini wetu, hasa vijana, ili kuwajengea uelewa na utashi wa kuvumiliana kwa upendo. Katika kushuhudia na kuadhimisha imani na ibada zetu sote tutambue , tulinde na kukuza maadili, tunu na desturi za imani za watu wengine wanazo ziheshimu na kuzitukuza. Vikundi vya imani kali na pambanishi kwa kutumia kashfa potoshaji sharti vidhibitiwe kwa weledi mkubwa wa viongozi wa dini husika wakisaidiana na usalama wa taifa. Stahamala [kustahimiliana] ni fadhila inayopaswa kufundishwa na kupenyezwa katika mifumo ya uongozi na maisha ya jamii na ihifadhiwe kwa kufuatiliwa kwa karibu sana.
Hitimisho:
Kwa
sasa Kanisa liko katika vita vya Kiroho, hivyo ni vyema Waamini wote wakakumbuka
kuwa, katika mapambano kama hayo Mungu mwenyewe, Mwenye enzi yote ndiye mlinzi
wa watu wake na Kanisa lake.
JIBU
LITAPATIKANA TU, KWA NJIA YA SALA, KUFUNGA NA MAOMBI!
Hivyo
siku ya Jumanne tarehe 25 Desemba 2012, inatangazwa rasmi nchini kote kuwa siku
ya sala na maombi kwa Wakristo wote na Makanisa yote nchini, pamoja na watu wote
wenye mapenzi mema, kuomba kwa imani, amani katika nchi yetu, na kumkabidhi
Mungu ashughulikie mipango yoyote iliyopo, ya wazi na ya kisirisiri ya kutaka
kuondoa amani ya taifa hili na kuyashambulia Makanisa nchini
Tanzania ishindwe na kuanguka pamoja na wale wote walio
nyuma ya mipango hiyo.
This is breathtaking! Nafurahi kuona wakristo wameamka! Haki ya kuabudu ni haki ya kikatiba na kimataifa! Muslims have minority complexities ndo mana muda wote wagomvi! Ukimya wa wakristo unachochea waislam kufanya wanayofanya under the excuse of religious grievancies! Ifike mahali they be stopped! Kama nchi inataka amani basi tuheshimiane! Sikumtuma mtu amchague Mtume Mohammad, ni personal choice sasa makasiriko ya nini kutuhamishia sisi? Tanzania kuna udini sana
ReplyDelete