- Kitoloho
Headlines News :

Written By Msamaa on Sunday, June 9, 2013 | 12:57 PM

Dk. Shein: Siitambui Kamati ya Maridhiano Zanzibar

Written by  //  08/06/2013  //  Habari  //  24 Comments

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema haitambui kamati ya maridhiano inayotetea Zanzibar kuwa na mamlaka kamili kama taifa linalojitegemea na kuwa na kiti katika Umoja wa Mataifa.

Dk. Shein alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baada ya kukamilisha ziara ya kikazi nchini China juzi.
Alisema kwamba haitambui kamati hiyo lakini alikiri kukutana nayo mara tatu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ilikwenda kumpongeza Ikulu baada ya kuibuka na ushindi, mara ya pili walifika kumpa mkono wa pole kufuatia ajali ya meli ya Spice Islanders kabla ya kukutana nao kwa mara ya mwisho.

Alisema shughuli zinazofanywa na kamati hiyo hazina baraka zake na wala hatambui mtu aliyeunda au kuteua kamati hiyo ambayo imekuwa ikifanya kampeni kubwa za Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili na kuwahusisha viongozi wastaafu akiwemo Rais wa Awamu ya Tano, Dk. Salmin Amour Juma ‘Komandoo’ na Rais wa Awamu ya Sita, Dk. Amani Abeid Karume.
“Waulizeni nani aliyeunda kamati hiyo na nani aliyeteua kama wakishindwa nitawaeleza mimi katika mkutano nitakaouitisha kuzungumza na waandishi wa habari, na walipokuja kwangu wanajua nini nilichowaeleza waseme,” alisema Dk. Shein.

Kamati hiyo ambayo ilikuwa ikitetea sera ya Muungano wa mkataba inaundwa na wanachama watatu kutoka CCM na watatu kutoka CUF, ikiongozwa na waziri wa kwanza wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hassan Nassor Moyo(CCM), Makamu Mwenyekiti Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Abubakar Khamis Bakari(CUF), Katibu wake ni Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu(CUF) na wajumbe ni pamoja na Waziri wa zamani wa SMZ na Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yusuph Himid(CCM) na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma Salim Bimani(CUF).

Hivi karibuni, kamati hiyo iliandaa mkutano wa hadhara na kutangaza mambo 10 yanayopaswa kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, ikiwa ni siku chache kabla ya Mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Joseph Warioba kuzindua rasimu ya katiba ya awali.
Kutokana na hali hiyo joto la kisiasa na vuguvugu la mabadiliko ya katiba mpya limechukua sura na mitizamo mbalimbali kutoka kwa wanasiasa, wanaharakati na wasomi ambao baadhi yao wamewanyooshea vidole wanasiasa wakiwataka kutoingilia mchakato wa katiba na kuipa nafasi tume ya mabadiliko ya katiba ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia jambo hilo kwa mujibu wa sheria.
CHANZO: NIPASHE
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template