Kauli ya Pinda inaweza kuchochea vurugu. - Kitoloho
Headlines News :
Home » » Kauli ya Pinda inaweza kuchochea vurugu.

Kauli ya Pinda inaweza kuchochea vurugu.

Written By Msamaa on Sunday, June 23, 2013 | 2:51 AM





MWANANCHI>Posted  Jumapili, Juni23  2013  saa 10:26 AM
Kwa ufupi
  • Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia askari polisi wetu wakitawanya mikusanyiko ya watu ikiwamo mikutano ya kisiasa kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kuachwa vilema.
SHARE THIS STORY.
Juzi, Ijumaa vyombo vya habari nchini likiwamo gazeti hili vilimkariri Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagiza vyombo vya dola kuwashughulikia kwa kuwapiga wale watakaokataa kutii amri na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Pinda alisema pale watu hao wanapokaidi amri halali wajue watakutana na makali ya vyombo hivyo ambavyo lazima viwapige.
Pinda alisema watu wanaokaidi amri wapigwe, hakuna namna nyingine na kwamba Serikali imechoka.

Tunachukua nafasi hii kutoa msimamo wetu kwa kulaani na kuipinga kauli hiyo ambayo tunaamini inaelekea katika kuchochea vurugu zaidi nchini.
Vilevile, kauli hii Waziri Mkuu tuamini inavunja misingi ya katiba ya nchi yetu licha ya kwamba kiongozi huyo haamini katika hili kama alivyoeleza bungeni.
Tunaamini katika ibara ya 13 na kifungu cha 6 (b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapoeleza: “Ni marufuku kwa mtu yoyote aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kuteswa kama mtu mwenye kosa, mpaka itakapothibitika anayo hatia kwa kutenda kosa hilo.
Pia, ibara hiyo hiyo kifungu cha 6 (e) kinasema: Ni marufuku kwa mtu yoyote, kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazoweza kumdhalilisha.”
Kwa maana hiyo, kauli ya Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi mkuu wa Serikali ni amri kwa wasimamizi wa vyombo vya dola, wakiwamo askari polisi.

Kama hivi sasa tunashuhudia askari polisi wetu wanatumia mabavu kumdhibiti mtu hata kama hajaleta upinzani wowote wakati wa kumkamata, hivi wakiruhusiwa kutumia mabavu siwataua?
Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia askari polisi wetu wakitawanya mikusanyiko ya watu ikiwamo mikutano ya kisiasa kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kuachwa vilema.
Baadhi ya matukio hayo ni lile la kutawanya maandamano ya wafuasi wa Chadema mjini Arusha waliokuwa wakielekea kwenye mkutano uliofanyika Uwanja wa NMC, Januari 5, mwaka juzi na kusababisha watu watatu kuuawa kwa kupigwa risasi.

Tukio lingine ni lile la kuwazuia wanachama wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi eneo la Nyololo mkoani Iringa Mei 2, mwaka jana.
Katika tukio hilo askari polisi wanatuhumiwa kutumia nguvu na kuwatawanya watu na kumuua kwa kumlipua na bomu mwandishi wa Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Tunaamini kuwa zipo njia nyingi za kudhibiti mikusanyiko ya watu ambayo siyo halali ikiwamo kutumia maji ya kuwasha au mabomu ya machozi, lakini siyo kutumia risasi za moto ambazo zimetumika katika baadhi ya matukio.
Tunachukua nafasi hii kumkumbusha Waziri Mkuu umuhimu wa kufuta kauli yake hiyo na hata kuwaomba radhi Watanzania kwa kauli yake.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template