- Kitoloho
Headlines News :
Home » »

Written By Msamaa on Thursday, April 18, 2013 | 1:22 PM



Alhamisi, Aprili 18, 2013 06:08 Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam {MTANZANIA}

Sheikh Ponda Issa Ponda

LEO Watanzania, wanaelekeza masikio yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, kusikiliza uamuzi wa mahakama hiyo wa kumtia hatiani Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 au kuwaachia huru.


Sheikh Ponda na Salehe Mkadamu, wamekaa rumande kwa miezi sita, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kufuta dhamana yao.

Mahakama inatarajia kusoma hukumu dhidi ya washtakiwa hao, baada ya pande zote mbili zinazopingana ambazo ni upande wa mashtaka na utetezi kumaliza kusikiliza ushahidi na majumuisho ya kesi hiyo, yaliyowasilishwa kwa ajili ya kuisaidia mahakama katika kutoa uamuzi.

Hukumu hiyo, inatarajiwa kutolewa mahakamani hapo na Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, aliyesikiliza kesi hiyo kwa muda wa miezi sita mfululizo, tangu washtakiwa walipopanda kizimbani kwa mara ya kwanza Oktoba 18, mwaka jana.

Tangu kesi hiyo ilipofunguliwa na kuanza kusikilizwa katika mahakama hiyo, sura ya mahakama ilianza kubadilika, ulinzi mkali usio wa kawaida uliwekwa, huku wanausalama wakifunga mitambo maalumu kwa ajili ya ukaguzi wa kila aliyekuwa akiingia mahakamani siku ambazo kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa.

Mbwa na farasi wenye majina ya kila aina, walihudhuria mahakamani hapo kwa ajili ya kulinda usalama, bila kukosa kundi kubwa la maaskari waliokuwa na mavazi maalumu, ikiwemo maroboti, huku mifukoni wakiwa na mabomu ya machozi.

Magari yasiyokuwa na idadi yakiwa na askari wenye silaha yalikuwa yakionekana mahakamani hapo ndani na nje, waliokuwa wakifika kwa ajili ya kufuatilia kesi hiyo wengi walikuwa wakizuiwa katika lango kuu la kuingilia humo.

Sheikh Ponda na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka matano ya kula njama, kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T, uliopo Markaz Chang’ombe, wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 59 mali ya Kampuni ya Agritanza Limited.

Kesi ilianza kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuleta mashahidi 16 mahakamani kwa ajili ya kuthibitisha tuhuma dhidi ya washtakiwa wote, wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka.

Sheikh Ponda na wenzake, wanatetewa na mawakili Juma Nassoro pamoja na Yahaya Njama, ambao kwa kutaka kuionyesha mahakama kwamba wateja wao hawakutenda makosa hayo, waliita mashahidi 52, wakiwemo washtakiwa.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mahakamani majumuisho ya mwisho, ukiiomba mahakama iwatie hatiani washtakiwa wote kwa sababu upande huo umeweza kuthibitisha mashtaka bila kuacha shaka.

Wakili Nassoro aliomba mahakama iwaachie huru wateja wake kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha makosa dhidi yao bila kuacha shaka.

Oktoba 18, mwaka jana, washtakiwa walisomewa mashtaka na Wakili Kweka ambapo alidai, Oktoba 12, mwaka jana katika eneo la Markaz Chang’ombe, lililopo Wilaya ya Temeke, kwa jinai na pasipo sababu za msingi, washtakiwa hao walivamia kiwanja namba 311/3/4 kitalu T kinachomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali.

Kweka alidai washtakiwa hao walitenda kosa hilo la kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa, kinyume na kifungu cha 85 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka jana katika eneo hilo hilo, washtakiwa hao pasipo uhalali wowote na hali iliyosababisha uvunjifu wa amani, walijimilikisha ardhi hiyo mali ya Agritanza Limited.

Shtaka la tano linamkabili mshitakiwa wa kwanza, Ponda Issa Ponda na Shekhe Swalehe Mkadamu, ambao walidaiwa kuwa kati ya Oktoba 10 na 16 mwaka jana, Chang’ombe Markaz, walishawishi wafuasi wao kutenda makosa hayo.

Washtakiwa wote walikana mashtaka na kukubaliwa dhamana kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini dhamana ya Sh milioni moja, wote walitimiza masharti na kuwa nje kwa dhamana isipokuwa Ponda na Mkadamu ambao dhamana yao ilizuiliwa.

Kweka aliwasilisha mahakamani hati ya kuzuia dhamana iliyotoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) chini ya kifungu cha sheria namba 148(4) cha sheria ya makosa ya jinai.

Kifungu hicho, kinaifunga mikono mahakama kujadili na kutoa dhamana kwa washitakiwa hao, hivyo waliendelea kukaa rumande hadi DPP atakapowasilisha hati nyingine ya kuruhusu dhamana, hata hivyo hadi leo inaposomwa hukumu yao DPP hajatoa hati hiyo.

Msingi wa kesi hiyo ni uwanja wa Markaz wenye ekari nne ambao Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) lilibadilishana na Kampuni ya Agritanza mbayo iliwapa ekari 40 maeneo ya Kisarawe. Kitendo hicho hakikuwaridhisha Waislamu wengine
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template