THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax:
255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Walioteuliwa
ni Jaji Semistodes S.
Kaijage na Jaji Kipenka M.
Musa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu,
2012.
Kabla
ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57)
alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007.
Aliteuliwa
kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka
2000.
Naye
Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Pia
amewahi kuwa Wakili wa
Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama Kuu Septemba 13, 2004.
……..Mwisho………..
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Mei,
2012
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !