UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116539
Fax:
255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC).
Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius
Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu,
2011.
Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada
ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.
Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu,
2011.
Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa
Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.
Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and
Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na
Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu,
2011.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES
SALAAM.
22 Desemba, 2011
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !