UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
Fax:
255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya
uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja wa Wizara, na Naibu Makatibu Wakuu 10 wa Wizara
mbalimbali.
Aidha, Rais
Kikwete amemhamisha Naibu Katibu Mkuu mmoja kutoka Wizara moja kwenda
nyingine.
Taarifa
iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu
Katibu Mkuu Kiongozi Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo wa maofisa hao
waandamizi wa Serikali unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011,
na wataapishwa Jumamosi wiki hii, Aprili 30, saa sita
mchana.
Taarifa hiyo
inasema kuwa katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bwana Job D. Masima kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo.
Aidha,
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemhamisha Injinia Mbogo
Futakamba aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji kwenda Wizara ya Kilimo,
Chakula na Ushirika.
Taarifa hiyo
inasema kuwa Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni kama
ifuatavyo:
·
Bwana Aphayo
Kidata ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi wake, Bwana
Kidata alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
·
Bwana Hab
Mkwizu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kabla
ya uteuzi wake, Bwana Mkwizu alikuwa Karani wa Baraza la
Mawaziri.
·
Bwana Charles
Amos Pallangyo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Kabla ya
uteuzi wake, Bwana Pallangyo alikuwa Mkurugenzi wa Uratibu – Ofisi ya Waziri
Mkuu.
·
Bibi Mwamini
Juma Malemi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi. Kabla ya hapo alikuwa Msaidizi wa Makamu
wa Rais katika masuala ya Maendeleo ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Jamii
na Uratibu wa Malalamiko ya Wananchi.
·
Injinia Mussa
Ibrahim Iyombe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi na JKT.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Usafiri katika Wizara
ya Ujenzi.
·
Injinia Dkt.
John Stanslaus Ndunguru ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Ujenzi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi katika wizara hiyo
hiyo ya Ujenzi.
·
Bwana John
Thomas James Mngodo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi.
Kabla ya uteuzi wake alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa
Chakula.
·
Bibi Anna T.
Maembe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Kabla ya uteuzi wake, Bibi Maembe alikuwa Mkurugenzi wa
Mazingira na Habari wa NEMC.
·
Bibi Sihaba
Nkinga ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika
Wizara ya Uchukuzi.
·
Injinia Bashir
J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya
uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya
Petroli.
Mwisho.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES
SALAAM.
27 Aprili,
2011
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !