KHATIMA
YA ZANZIBAR NA
MUSTAKBALI WA MUUNGANO
Na:
Seif Sharif Hamad
Katibu Mkuu
The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi)
Katibu Mkuu
The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi)
“[President
Nyerere] managed half the work of a python… He swallowed Zanzibar all right but he did not crush its
fighting force first. The live animal is a long time digesting, and its kicks
are being felt hurtfully, and possibly even fatally, deep inside Tanganyika ’s
body politic.”
- ‘The Perils of Nyerere’ in The Economist of June 1964
- ‘The Perils of Nyerere’ in The Economist of June 1964
Utangulizi
Mtafiti
mmoja kutoka Argentina ,
Boaventura Santos de Sousa, aliwahi kuandika kwamba ‘mwandishi ingawa huandika
kuhusu yaliyopita huwa anajaribu kueleza yaliyopo, siyo yaliyopita. Lakini, kwa
kufanya hivyo, huwa pia anajiweka mbali na hali ya sasa na kwa hakika anaandika
kwa ajili ya siku zijazo’.
Muungano
wa Zanzibar na Tanganyika
umepita katika masaiba kadhaa tokea kuasisiwa kwake takriban miaka 45 iliyopita
lakini mtikisiko ulioukumba katika siku za karibuni ni mkubwa sana . Ni mkubwa kwa sababu umegusa kiini cha
Muungano huu ambapo suala linaloulizwa ni iwapo kwa kule kukubali kushirikiana
katika baadhi ya mambo, je, Zanzibar na Tanganyika zimejifuta na hivyo kupoteza hadhi
zake kama nchi? Hilo
limekuwa ndiyo suala kubwa linaloulizwa na Wazanzibari hasa baada ya Waziri
Mkuu Mizengo Pinda kutamka Bungeni kwamba Zanzibar
si nchi.
Hakuna
awezaye kubisha kwamba tokea kuasisiwa kwake, Muungano huu umejengeka kutokana
na misingi ya khofu, kutiliana shaka na kutokuaminiana baina ya pande mbili
zinazouunda, ambako wakati mwengine kumepelekea hata kutishia uhai wa Muungano
wenyewe.
Muungano
umekuwa gumzo kuu katika takriban kila mjadala wa katiba na siasa katika nchi
yetu. Umejitokeza na kujionyesha hivyo katika mwaka wa mwanzo wa Muungano
kuhusiana na sakata la kuwa na Ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Magharibi kwa
upande wa Tanganyika na Ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwa upande wa
Zanzibar, kuhusiana na uwakilishi wa Zanzibar katika Bodi ya Sarafu ya Afrika
Mashariki na uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mwaka 1964 – 1966, wakati
wa kuunganisha vyama vya ASP na TANU kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka
1977, katika mjadala wa marekebisho ya Katiba wa 1983/84 na hatimaye kujiuzulu
kwa Rais wa pili wa Zanzibar Sheikh Aboud Jumbe, wakati wa kuondolewa katika
Uwaziri Kiongozi kwa mwandishi wa makala haya na hatimaye kufukuzwa katika CCM
na wenzake 6 mwaka 1988, katika harakati za madai ya kutaka kura ya maoni
kuhusiana na Muungano huo mwaka 1989/90, wakati wa mjadala wa kuanzishwa vyama
vingi mwaka 1991, katika sakata la Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za
Kiislamu (OIC) mwaka 1993, wakati wa mjadala wa G-55 kudai kuanzishwa kwa
Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano mwaka 1994, katika mjadala wa
marekebisho ya 11 na 14 ya Katiba ya Muungano mwaka 1994/95, wakati wa kampeni za
uchaguzi mkuu wa 1995 na ule wa 2000 na karibuni kabisa kuhusiana na suala la
matarajio ya ugunduzi wa mafuta visiwani Zanzibar na harakati za kuanzisha
Shirikisho la Afrika Mashariki.
Ukiondoa
kuibuka kwake katika mijadala mikubwa ya kikatiba na kisiasa nchini, kwa upande
mwengine katika uendeshaji wa shughuli za Serikali za kila siku, ‘matatizo na
vikwazo kadhaa ya kiutawala na kiutendaji’ vimekuwa vikiripotiwa kila mara
kwamba vinakwamisha uimarishaji wa Muungano.
Tume
na Kamati kadhaa zimeundwa kuainisha matatizo ya Muungano na kupendekeza njia
za kuyatatua. Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeunda Tume na Kamati zifuatazo,
miongoni mwa nyingi, kuhusiana na masuala haya:
1.
Kamati ya Mtei
2. Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991)
3. Kamati ya Shellukindo (1994)
4. Kamati ya Shellukindo 2 ya kuandaa Muafaka juu ya Mambo ya Muungano baina ya SMZ na SMT.
5. Kamati ya Jaji Mark Bomani (1995)
6. Kamati ya Jaji Robert Kisanga (1998)
7. Kamati ya 'Harmonization'
8. Kamati ya Masuala ya Simu (Kamati ya Kusila)
2. Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991)
3. Kamati ya Shellukindo (1994)
4. Kamati ya Shellukindo 2 ya kuandaa Muafaka juu ya Mambo ya Muungano baina ya SMZ na SMT.
5. Kamati ya Jaji Mark Bomani (1995)
6. Kamati ya Jaji Robert Kisanga (1998)
7. Kamati ya 'Harmonization'
8. Kamati ya Masuala ya Simu (Kamati ya Kusila)
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) nayo kwa upande wake iliunda Kamati zifuatazo
kwa madhumuni hayo hayo:
1.
Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992
2. Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamuhuna) ya 1997
3. Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti ya Jaji Kisanga (Kamati ya Salim Juma Othman)
4. Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar juu ya Kero za Muungano (Kamati ya
Ramia) ya 2000
5. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya Sera ya Mambo ya Nje
6. Kamati ya Rais ya Wataalamu juu ya Kero za Muungano ya 2001
7. Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
8. Kamati ya Mafuta
9. Kamati ya Madeni baina ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar
na Serikali ya Muungano wa Tanzania
10. Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ)
11. Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu
12. Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996 –1999)
13. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya matatizo na kero za Muungano na taratibu za kuyaondoa (2004)
2. Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamuhuna) ya 1997
3. Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti ya Jaji Kisanga (Kamati ya Salim Juma Othman)
4. Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi ya
5. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya Sera ya Mambo ya Nje
6. Kamati ya Rais ya Wataalamu juu ya Kero za Muungano ya 2001
7. Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
8. Kamati ya Mafuta
9. Kamati ya Madeni baina ya Serikali ya Mapinduzi ya
10. Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ)
11. Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu
12. Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996 –1999)
13. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya matatizo na kero za Muungano na taratibu za kuyaondoa (2004)
Ukiacha
Tume, Kamati na Ripoti hizo, kuanzia mwaka 1985 kulianzishwa utaratibu wa
Kamati ya Pamoja ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Waziri Kiongozi wa
Zanzibar pamoja na Mawaziri wa Serikali zetu mbili ambao ulitarajiwa uwe ndiyo
jukwaa la kuzungumzia matatizo kutoka kwa washiriki wakuu wa Muungano huu na
kuyapatia ufumbuzi unaofaa. Utaratibu huu uliachwa kwa muda mrefu lakini sasa
umerejeshwa upya kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa katika
mkutano na mawaziri na watendaji wakuu wa Serikali yake huko Ngurdoto, Arusha
mwezi Februari, 2006.
Mikutano,
Makongamano, Semina na Warsha vimefanywa kujadili masuala haya na kupendekeza
hatua za kuchukuliwa. Wasomi na wanafunzi wamefanya tafiti kadhaa na kujipatia
shahada na stashahada hadi ngazi ya Ph.D juu ya Muungano lakini bado matatizo
yako pale pale na yanaongezeka kila kukicha.
Yanayoonekana
na kuelezwa kama matatizo, mapungufu, dosari,
kasoro na, kwa msamiati wa sasa, kero yamekuwa ndiyo yale kwa yale. Nini basi
kiini cha haya? Na vipi tutayatatua?
Mimi
nimeamua kutoa changamoto kupitia waraka huu kwa kuitazama historia ya
Muungano, jinsi ulivyoundwa, matatizo yanayoukabili, nafasi na hadhi ya Zanzibar katika Muungano na nini khatima ya Zanzibar na mustakbali wa
Muungano huko tuendako. Nitakayoyaeleza yanaweza yakaonekana ni machungu kwa
wakati huu wa sasa lakini kama asemavyo Santos
de Sousa yanaweza yakawa ndiyo ufumbuzi kwa siku zijazo.
Asili
na Sababu za Muungano
Maoni
yanayotolewa kuhusu asili na sababu za Muungano yamekuwa yakitofautiana mno.
Wapo wanaouleza Muungano huu kuwa ni wa pekee katika bara la Afrika, kwani
ndiyo pekee ulioweza kudumu katika kutimiza azma na malengo ya kuleta umoja wa
Afrika (Pan-Africanism), na pia wapo wanauona kuwa ni ‘jaribio la kusisimia la
ukoloni mdogo wa nchi moja ya Kiafrika kuiteka na kuitawala nchi nyengine ya
Kiafrika.’
Kutokana
na maelezo na hoja nyingi na zinazokinzana kuhusu asili na sababu za Muungano,
si rahisi kusema moja kwa moja kuwa maelezo yepi au hoja ipi ni sahihi.
Utangulizi (Preamble) wa Mkataba wa Muungano wenyewe unataja sababu kuu ya
kuunganisha nchi za Zanzibar na Tanganyika kuwa ni ‘maingiliano ya muda mrefu
ya watu wa nchi mbili hizi na mahusiano yao ya kidugu na kirafiki … na …
kuendeleza umoja wa watu wa Afrika.’ Lakini miaka 45 sasa baada ya uzoefu wa
Muungano huu, Wazanzibari wanajiuliza kweli haya ndiyo madhumuni ya Muungano
huu?
Wazo
la kuungana linaweza kurudishwa nyuma tokea zama za harakati za ukombozi wa
nchi za Afrika. Waasisi na wakuu wa harakati za kupigania Uhuru waliiona mipaka
ya nchi zao iliyowekwa na wakoloni kuwa ni ‘mbinu za kibeberu’ zilizotekelezwa
kwa ajili ya manufaa na maslahi yao .
Kutokana na hisia hizo, mazungumzo ya kuanzisha aina fulani ya umoja miongoni
mwa nchi huru za Afrika yalitawala duru za siasa katika miaka ya 5o na 60.
Nadharia
mbili zilijichomoza. Ya kwanza, ikishadidiwa na Kwame Nkrumah wa Ghana ,
ilikuwa ikitaka kuasisiwa kwa nchi moja tu ya Afrika nzima iliyoungana ikiwa na
Serikali moja kwa bara zima. Nadharia hii ilipingwa na baadhi ya viongozi,
wakiongozwa na Julius Nyerere wa Tanganyika , ambao walisisitiza haja
ya kuanza na miungano ya maeneo (regional unions) chini ya mfumo wa Shirikisho
badala ya kuwa na mpango wa Serikali moja.
Katika
kulifikia lengo hilo , viongozi wa kisiasa wa
nchi tatu za Afrika Mashariki – Kenya ,
Uganda na Tanganyika – walikuwa wakifanya
mikutano ya mara kwa mara kipindi chote cha kati ya mwaka 1961 na 1963 kuona
jinsi gani wanaweza kutimiza ndoto hiyo. Mfumo wa Muungano uliokuwa ukiandaliwa
ulikuwa ni ule wa Shirikisho. Tamko la Pamoja la viongozi hao lilisema:
“Sisi,
viongozi wa wananchi na Serikali za nchi za Afrika Mashariki … tunayakinisha
nia zetu kuhusu kuwepo kwa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki. Mkutano
wetu wa leo unasukumwa na hisia za umoja wa Afrika (Pan-Africanism), na siyo
tamaa za maslahi binafsi ya eneo hili. … Ijapokuwa Zanzibar haikuwakilishwa
katika mkutano huu, tunapaaswa kuweka bayana kwamba nchi hiyo inakaribishwa
kushiriki kikamilifu katika mikutano yetu kwa ajili ya uundwaji wa Shirikisho
.”
Lakini
Umoja wa Afrika (Pan-Africanism) hauonekani kuwa ndiyo dhamira pekee au kama ndiyo dhamira halisi ya Muungano. Wengi wanaamini,
na mimi nikiwa mmoja wao, kwamba dhana hiyo ilitumiwa tu kuficha njama za muda
mrefu za Nyerere kutaka kuimeza na kuitawala Zanzibar . Katika mwaka 1961, wakati Tanganyika
inakaribia kupata Uhuru wake, Nyerere alinukuliwa akisema:
“If
I could tow that island [Zanzibar ] out in the
middle of the Indian Ocean , I would do it … I
fear it will be a very big headache for me.”
Yaani,
“Kama ningekuwa na uwezo wa kuvikokota visiwa vile [Zanzibar ]
na kuvitupa nje kabisa, katikati ya Bahari ya Hindi, basi ningefanya hivyo …
Nakhofia vitakuja kuniumiza kichwa sana ”.
Imani
hii inatiliwa nguvu na mahusiano ya karibu na ya muda mrefu yaliyokuwepo kati ya
chama kilichokuwa kikitawala Tanganyika ,
TANU, na ASP ambacho kilishika hatamu za utawala baada ya Mapinduzi ya Januari
12, 1964, mwezi mmoja tu baada ya Zanzibar
kupata uhuru wake kutoka Uingereza hapo Desemba 10, 1963. Zilikuwepo taarifa
tokea mwaka 1959 kwamba TANU na ASP zitakaposhika madaraka zitaziunganisha nchi
mbili hizi kuwa Jamhuri moja.
Wakati
juhudi za kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki zikiwa zinafifia, Nyerere
aliona fursa Zanzibar
ambayo hakutaka kuipoteza. Katika mazungumzo ya siri kati yake na Rais Abeid
Amani Karume wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ,
wakakubaliana kuziunganisha nchi mbili hizi. Hakukuwa na ushirikishwaji wa aina
yoyote ule wa wananchi wa nchi hizi mbili katika maamuzi haya makubwa. Usiri
uliogubika hatua hii kubwa unafichuliwa na si mwengine bali Nyerere mwenyewe
pale aliposema:
“[Tanganyika] tulipeleka polisi wetu
Zanzibar. Baada ya kuyashinda matatizo kadhaa tukaungana. Sisi wenyewe kwa
khiyari zetu tulikubaliana kuungana. Karume na mimi tulikutana. Peke yetu
wawili tu tulikutana. Nilipomtajia wazo la Muungano, Karume hakufikiri hata
mara mbili. Pale pale alinitaka kuita mkutano wa waandishi wa habari kutangaza
azma yetu. Nilimshauri asubiri kidogo kwani ilikuwa bado ni mapema mno kuweza
kuviarifu vyombo vya habari.”
Taarifa hizi ziliendelea kubaki kuwa siri
hadi tarehe 26 Aprili, 1964 pale Redio ya Tanganyika ilipotangaza kwamba siku
hiyo Marais wawili hao watakutana katika Bunge la Tanganyika kubadilishana Hati
za Muungano ambazo zimeunganisha Zanzibar na Tanganyika kuwa Jamhuri moja.
Hivyo inaonekana wazi kwamba tokea awali Muungano huu ulikosa ridhaa ya watu.
Haukuwa Muungano wa watu, ulioundwa na watu, kwa maslahi ya watu. Bali ulikuwa
na umeendelea kuwa ni Muungano uliosimamishwa kwa ridhaa ya watawala pekee.
Kiini cha matatizo ya Muungano
Ukitazama kwa jicho la sheria, kiini cha
matatizo ya Muungano kinatokana na tafsiri ya Mkataba wa Muungano (Articles of
Union) wa 1964. Hizi ndizo hati zinazounda, kupitia mkataba wa kimataifa,
Jamhuri ya Muungano. Suala kubwa lililoumiza na linaloendelea kuumiza vichwa
vya wengi na hivyo kuendelea kuulizwa ni mfumo gani wa Muungano ulikusudiwa
kuwekwa na Mkataba huu? Ni muungano wa moja kwa moja (unitary) au wa shirikisho (federal)?
Mfumo
uliopo sasa ambao ulianza kutekelezwa 1964 ni ule wa serikali mbili – ile ya
Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar .
Tanganyika
haikuwekewa serikali yake tofauti; madaraka yake kwa yale mambo yasiyo ya
Muungano yalielezwa kwamba yatasimamiwa na kuendeshwa na Serikali hiyo hiyo ya
Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, uhalali wa kisheria wa muundo huu umeendelea
kuhojiwa na hata kupingwa kwamba hauwakilishi ipasavyo makusudio yaliyomo
katika Mkataba ulioanzisha Muungano wenyewe.
Mkataba
wa Muungano wenyewe hauelezi bayana aina au mfumo wa muungano inaouanzisha
lakini uko wazi kuhusiana na mgawanyo wa madaraka (distribution of power)
inaouweka na idadi ya mamlaka (number of jurisdictions) zitakazokuwepo. Ibara
ya (iii) (a) ya Mkataba huo inaanzisha ‘Bunge na Mamlaka ya Utendaji’
(Parliament and Executive) ndani ya na kwa ajili ya Zanzibar
ikiwa na mamlaka kamili kuhusiana na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwa Zanzibar . Kwa upande
mwengine, Ibara ya (iv) ya Mkataba huo inaanzisha ‘Bunge na Mamlaka ya
Utendaji’ (Parliament and Executive) ya Jamhuri ya Muungano ikiwa na mamlaka
kamili katika eneo lote la Jamhuri ya Muungano kuhusiana na mambo ya Muungano
na, pia, ikiwa na mamlaka kamili ndani ya, na kwa ajili ya Tanganyika kuhusiana
na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwa Tanganyika. Kwa hivyo, katika sehemu
ya pili, mamlaka mbili tofauti zimechanganywa pamoja.
Mjadala
mkubwa na mkali umekuja kuhusiana na tafsiri ya Ibara hiyo ya (iv) na kule
kuchanganya kwake mamlaka mbili hizo.
Haya
si masuala ya kisheria tu kama ambavyo baadhi yetu wanataka tuamini (ingawa
nayo ni muhimu mno kama ilivyodhihirika hivi karibuni), bali pia ni masuala ya
kisiasa kwa vile yanahusisha uwezo wa maamuzi, madaraka na mamlaka, na zaidi
mchango wa gharama za uendeshaji na mgawanyo wa rasilimali na mapato kati ya
wahusika wakuu. Mambo haya, katika uzoefu wa nchi za wenzetu, ndiyo
yaliyopelekea kuvunjika kwa miungano yao
kwani huzaa kutiliana shaka na kutokuaminiana. Kwa vile yanachukua sura ya
kisiasa (kutokana na sababu nilizozitaja), haya hayana chama wala itikadi kama nitakavyoonyesha huko mbele. Kama
alivyowahi kusema Prof. Issa Shivji:
“Ultimately,
the question of the Union is primarily a
political question and no amount of rhetoric about blood and cultural ties will
matter when it comes to realpolitik.”
Yaani,
“Mwisho wa yote, suala la Muungano linabakia kimsingi kuwa ni suala la kisiasa,
na inapofikia kwenye siasa hasa, hotuba na kauli kali za jazba kuhusiana na
mahusiano ya damu na ya kidugu, zote hazitafaa kitu.”
Kwa
hakika, kinyume na inavyojaribiwa kuonyeshwa na wengi kwamba Tanganyika
imepoteza kila kitu katika muundo huu wakati Zanzibar imekabidhi sehemu tu ya
madaraka yake, muundo wa Serikali mbili umepelekea wengi kuamini kwamba
kilichofanyika ni kiini macho tu kwani ni Zanzibar iliyokabidhi sehemu muhimu
ya mamlaka yake (mahusiano ya nchi za nje, ulinzi na usalama, uraia, kodi na
ushuru, sarafu, nguvu kuu za kuendeshea uchumi na mengineyo) kwa Tanganyika na
kisha Tanganyika ikajigeuza jina na kujiita Jamhuri ya Muungano. Na haya si
maoni ya ngumbaru (kwa lugha ya Mwalimu Julius Nyerere) bali ni maoni ya watu
wazito wakiwemo aliyekuwa Spika wa Bunge na ambaye sasa ni Makamu Mwenyekiti wa
CCM, Pius Msekwa ambaye alisema kwa jinsi mambo yalivyofanyika, Zanzibar
inaonekana kama vile ni ‘invited guest’ (mgeni aliyealikwa) katika Muungano.
Naye msomi mashuhuri ulimwenguni, Prof. Ali Mazrui alisema baada ya Muungano
Zanzibar imepoteza kila kitu muhimu wakati Tanganyika
imebadilika jina tu na kuwa Tanzania
huku ikiwa na mamlaka zaidi lakini ikibaki na Rais wake, nembo yake ya Taifa,
wimbo wake wa Taifa na hata kiti chake katika Umoja wa Mataifa.
Mkataba
wa Muungano haujafuta Serikali ya Tanganyika
Katika
makubaliano ya kimataifa yaliyounda Muungano, ambayo hata hivyo katika muda
wote wa uhai wa Muungano yamekuwa hayafuatwi, hakuna kifungu hata kimoja
kilichotoa au kuagiza kwamba Serikali ya Tanganyika ifutwe kwa mujibu wa
makubaliano hayo. Serikali ya Tanganyika ,
kama ilivyo ile ya Zanzibar , imelindwa na
kifungu cha (v) kinachosomeka kwamba: “The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their
respective territories”. Kinachosemwa hapa ni kwamba “Sheria zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar
zitaendelea kufanya kazi na kuwa na nguvu katika maeneo yao .”
Wataalamu wa katiba na sheria wanafahamu kwamba katiba ndio sheria mama ya sheria zote za nchi. Hivyo Katiba yaTanganyika imelindwa na inapaswa
kuwepo na Serikali yake iwepo, pamoja na viongozi wake kuwepo na kusimamia
mambo yasiyo ya Muungano. Katiba na sheria za Tanganyika
ndizo zilizotakiwa zitumike katika eneo la Tanganyika
kwa yale mambo yaliyokuwa hayamo kwenye Muungano kama ambavyo Katiba (au kabla
ya hapo Matangazo ya Kikatiba – Constitutional Decrees) na sheria za Zanzibar zinavyotumika katika eneo la Zanzibar kwa yale mambo ambayo si ya Muungano.
Hiyo ndio tafsiri ya ‘maeneo yao ’.
Wazanzibari wanafahamu kwamba Serikali yaTanganyika
imefutwa kwa makusudi na Bunge la Tanganyika
kinyume na Makubaliano ya Muungano ili kujipa nafasi kuitumia Serikali ya
Muungano, kama kwamba ndio Serikali ya Tanganyika . Lengo ni hatimaye
kuiuwa Serikali ya Zanzibar na kufanya Tanganyika mpya ikiwa na jina jipya la Tanzania
lenye mipaka mipya, yaani kuwa nchi moja yenye Serikali Moja.
Wataalamu wa katiba na sheria wanafahamu kwamba katiba ndio sheria mama ya sheria zote za nchi. Hivyo Katiba ya
Wazanzibari wanafahamu kwamba Serikali ya
Hiyo
ndio ghilba iliyofanywa na viongozi wa Tanganyika mara baada ya kuwekwa
saini makubaliano. Kwa kusaidia kufichuwa ukweli wa hadaa hii, msomaji
anashauriwa asome Sheria Na. 22 ya mwaka 1964 inayoitwa “Union of Tanganyika
and Zanzibar Act, 1964.”
Sheria
hii ilipitishwa na Bunge la Tanganyika Aprili 25, 1964, siku moja kabla
Muungano kuanza kufanya kazi. Ilikusudiwa kuthibisha kukubalika Muungano huo wa
Tanganyika na Zanzibar upande wa Tanganyika (ratification). Kifungu
cha (viii) cha Makubaliano ya Muungano kinaagiza ifanyike hivyo kwa pande zote
mbili za Muungano.
Inasikitisha
kusoma katika kifungu Na. 2 cha sheria hiyo kwamba:
“Existing
law means the written and unwritten law as it exists immediately before Union
Day but does not include the Constitution of Tanganyika in so far as it
provides for the Government of the Republic
of Tanganyika or any
declaration or law or any provision which expires with effect from commencement
of the Interim Constitution”.
(“Sheria
iliyopo maana yake ni sheria iliyoandikwa na isiyoandikwa kama ilivyo kabla tu
ya siku ya Muungano lakini haijumuishi Katiba ya Tanganyika
kwa mintaraf ya kuiweka kwake Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika au tamko, sheria au
kifungu chochote ambacho kinafutika kwa kuanza kufanya kazi Katiba ya Muda (ya
Muungano)).”
Kwa
hivyo, wakati Bunge la Tanganyika
linapitisha sheria ya kuridhia, ratify, kuwepo kwa Muungano kwa upande wa Tanganyika ,
sheria hiyo ilianza kupinga vifungu vya makubaliano hayo. Mfano mwengine ni
kifungu Na. 7 cha sheria hiyo kinachosema:
“On
the commencement of the Interim Constitution of the United Republic of Tanganyika
and Zanzibar , the Constitution of Tanganyika
will cease to have effect for the Government of Tanganyika as a separate part
of the United Republic ”.
(“Itapoanza
kufanya kazi Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ,
Katiba ya Tanganyika itasita
kuwa na maana kwa Serikali ya Tanganyika
kama sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano.”)
Kwa
maneno mengine, sheria ambazo zilitakiwa zitumike kwa Tanganyika kwa mambo ambayo si ya Muungano
zilipewa maana mpya kwamba eti zisijumuishe Katiba ya Tanganyika .
Jambo moja lililo wazi, pamoja na hatua hii ya kuifuta Katiba yaTanganyika , ni kwamba kule kuendelea kutambua
kuwepo kwa sheria nyengine za Tanganyika
bado kunamaanisha kuwepo kwa mamlaka ya Tanganyika ambako sheria hizo kwa
mambo yote yasiyo mambo ya Muungano ziliendelea na zinaendelea kutumika hadi
leo.
Jambo moja lililo wazi, pamoja na hatua hii ya kuifuta Katiba ya
Zaidi,
inapaswa ifahamike kwamba kufuta Katiba ya Tanganyika
kulikofanywa na vifungu vya sheria hii hakukubadilisha makubaliano
yaliyokwishatiwa saini kati ya Serikali mbili zilizounda Muungano, yaliyosema
kwamba sheria za nchi mbili hizi zitaendelea kutumika katika maeneo yao . Bunge la Tanganyika ,
na hata hili la Muungano, halikuwa na mamlaka kutafsiri vifungu vya Mkataba wa
Muungano.
Utaratibu
wa kisheria ni kwamba kama Mkataba ulitakiwa
kutafsiriwa basi ni walioandika rasimu ya mkataba huo ndio walipaswa kutoa
tafsiri ya vifungu vyake, tafsiri ambayo ingepaswa iwe sehemu ya Mkataba huo.
Na wala makubaliano yale hayakufuta wadhifa wa Rais wa Tanganyika . Si hivyo tu, bali pia
Katiba ya Muungano ambayo ilitakiwa iwe ya muda tu kwa mwaka mmoja (interim)
ilikuwa ni ile ya Tanganyika
iliyofanyiwa marekebisho kwa ajili ya kutumika kwa Serikali ya Muungano.
Haikuruhusiwa
kutumika kuiongoza Tanganyika
kwa sababu Tanganyika
ilikuwa na Katiba yake na Rais wake. Mwalimu Nyerere alikuwa na vyeo viwili,
Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano na Katiba ya Muungano na
Rais wa Tanganyika kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika, kama alivyokuwa Mzee
Karume ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Makubaliano na Katiba ya Muungano na akaendelea kubaki kuwa Rais wa Zanzibar
kwa mujibu wa Tangazo la Katiba ya Zanzibar (Constitutional Decrees).
Hivyo
ndivyo makubaliano yalivyo hadi hii leo. Waliobadilika ni watu tu. Kufanya vyenginevyo
ni kinyume na makubaliano yale na ndio sababu ya migogoro ya Muungano.
Yaliyofanyika ni ujanja uliokuwa hauna nia njema kwa Zanzibar
kama alivyosema Prof. Issa Shivji, mtaalamu wa Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam .
“Lakini yote ya kuepusha Serikali yaTanganyika
kuwepo yalifanywa kwa makusudi kabisa, ili itumike Serikali ya Muungano kama
ndio Tanganyika .
Katika Sheria ile Na. 22 ya 1964, Rais wa Tanganyika
amejipa madaraka ya kutunga na kutoa maagizo yanayohusu Muungano kwa kutumia
amri (decrees) za sheria ya Tanganyika .
Siku ile inapopitishwa sheria ile zilipitishwa pia Decrees mbili zilizotokana na vifungu Na. 6 (3), cha 8 na cha 5 cha sheria hiyo Na. 22 ya 1964, yaani The Provisional Transitional Decree 1964, na ile ya Interim Constitution Decree 1964 ambazo zote hazikuwa halali maana ni Decrees zilizopitishwa na Bunge la Tanganyika zilizotokana na Sheria Na. 22 ya 1964 ya Tanganyika.”
Miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha kuwa hakukuwa na nia njema katika Muungano huu tokea awali ni pale wafanyakazi wa Serikali yaTanganyika
wote walipopandishwa vyeo kwa pamoja na kuwa wafanyakazi wa Muungano kama kifungu cha 3 (1) cha Provisional Transitional
Decree kinavyosema:
“Lakini yote ya kuepusha Serikali ya
Siku ile inapopitishwa sheria ile zilipitishwa pia Decrees mbili zilizotokana na vifungu Na. 6 (3), cha 8 na cha 5 cha sheria hiyo Na. 22 ya 1964, yaani The Provisional Transitional Decree 1964, na ile ya Interim Constitution Decree 1964 ambazo zote hazikuwa halali maana ni Decrees zilizopitishwa na Bunge la Tanganyika zilizotokana na Sheria Na. 22 ya 1964 ya Tanganyika.”
Miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha kuwa hakukuwa na nia njema katika Muungano huu tokea awali ni pale wafanyakazi wa Serikali ya
“Every
person who holds office in the service of the Republic
of Tanganyika immediately before the
Union Day, shall on Union Day be deemed to have been elected, appointed or
otherwise selected to the corresponding office in the service of the United Republic .”
Yaani
kila mfanyakazi aliyekuwa wa Serikali ya Tanganyika mara kabla ya siku ya
Muungano kufumba na kufumbuwa, pengine kwa uchawi wa kifimbo cha Mwalimu
Nyerere, anakuwa mara moja mfanyakazi wa Serikali ya Muungano kuanzia siku ya
Muungano. Huu tuuiteje kama si ujambazi wa
kikatiba (constitutional banditry)?
Vivyo
hivyo, kifungu cha 6 (i) cha Decree kinasema mara tu baada kuanza Muungano,
Mahkama ya Tanganyika
na Majaji wake wote nao watakuwa ndio Mahkama na Majaji wa Jamhuri ya Muungano
kinyume na Makubaliano ya Muungano. Mpaka leo Katiba zote mbili hazitambuwi
Mahkama (ukiondoa Mahkama ya Rufaa) kama ni
suala la Muungano. Nembo ya Tanganyika
inatumika kama nembo ya Serikali ya Muungano na Idara ya Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika inachukuliwa kama
Idara ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano.
Haya yote hayamo na ni kinyume na Makubaliano ya 1964. Yote haya na kile kifungu cha 7 cha Sheria Na. 22 ya 1964 kinachofuta kuwepo kwa Serikali yaTanganyika
hayakubadilisha na wala hayana mahusiano na Makubaliano ya Muungano ya 1964.
Yote haya yalifanywa na Bunge la Tanganyika
kwa maslahi ya Tanganyika
nje ya Makubaliano.
Haya yote hayamo na ni kinyume na Makubaliano ya 1964. Yote haya na kile kifungu cha 7 cha Sheria Na. 22 ya 1964 kinachofuta kuwepo kwa Serikali ya
Aliyekuwa
Spika wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Pius Msekwa, analifahamu
vyema suala hili. Katika waraka wake alioutoa kwenye Semina kuhusu Muungano
hapo Hoteli ya Mkonge, Tanga tarehe 25—27 Februari 1994 anasema:
“The
Transitional Decree, 1964 published on 01/05/64, transferred persons who were
holding office in the public service of the Republic of Tanganyika
to the corresponding office in the public service of the United Republic of
Tanzania. By the same decree the High Court of Tanganyika also became the High
Court of United Republic of Tanzania and the public seal of Tanganyika became public seal of the United Republic .”
Athari
za hatua hizi kwa Zanzibar
ziko wazi. Tanganyika
imejigeuza Tanzania na
imechukua mamlaka ya mambo muhimu ya Zanzibar
huku ikijipa hadhi ya kuwa juu ya Serikali ya Zanzibar kinyume na Mkataba wa Muungano. Hii
ndiyo siri ya viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kung’ang’ania mfumo
wa Serikali mbili na kukataa kata kata mabadiliko yoyote ya mfumo huo kwani Tanganyika
inanufaika nao kwa kuwa yenyewe ndiyo imekuwa ‘Muungano’. Kukubali muundo wa
Serikali tatu ni kuzifanya Tanganyika
na Zanzibar ziwe na hadhi na fursa sawa katika
Muungano, jambo ambalo Tanganyika
hailitaki maana kulikubali ni kukubali kupoteza fursa zote inazozipata hivi
sasa kwa kujikweza kwake na kujifanya kuwa ndiyo ‘Muungano’.
Ushahidi
wa wazi wa hoja yangu hii ni kwamba mtu anapoangalia taasisi zote za Muungano
zilizoundwa chini ya Katiba au sheria za Muungano ambazo zinazikutanisha
Serikali mbili zilizopo sasa, ataona kuwa wajumbe wanaowakilisha upande wa
Serikali ya Muungano wote ni kutoka Tanganyika . Hoja inayojitokeza ni
kwamba Serikali ya Muungano ni ya shirika ambapo Zanzibar
ni sehemu ya ushirika huo, kwa nini basi wajumbe wanaowakilisha Serikali hiyo
ya Muungano watoke upande wa Tanganyika
peke yake? Jawabu ni rahisi. Serikali ya Muungano kwa hakika ni Serikali ya Tanganyika
iliyojivika joho la Muungano.
Rais
Jakaya Kikwete amekaririwa hadharani akisema matatizo ya Muungano hayatokani na
muundo bali yanasababishwa na viongozi. Hoja, maelezo na mifano niliyoitoa hapo
juu inatosha kumuonyesha Rais kwamba kauli yake si sahihi. Vyote viwili –
muundo na pia kukosekana kwa nia njema upande wa viongozi – ni sababu za kuwepo
kwa matatizo yasiyokwisha ya Muungano.
Sisi
katika CUF tumesema wazi kwamba kuna haja ya kuuimarisha Muungano wetu kwa
kurekebisha kasoro hii ya msingi. Njia ya kufanya hivyo ni kuzionyesha wazi
wazi mamlaka zote tatu zilizomo katika Mkataba wa Muungano ili kuondosha khofu
za kudhani mmoja anafaidika katika muundo huu na mwengine anakandamizwa.
Serikali ya Zanzibar ionekane wazi wazi,
Serikali ya Tanganyika
ionekane wazi wazi, na Serikali ya Muungano ionekani wazi wazi. Hapo hapatakuwa
na hofu ya mkubwa kummeza mdogo, wala mdogo kupendelewa na kupewa uwakilishi
unaozidi kiwango chake.
Uvunjwaji
wa Mkataba wa Muungano
Mbali
na suala la muundo wa Muungano, maeneo mengine mengi yanayogusa msingi wa
Mkataba wa Muungano yaliendelea kuvunjwa na Serikali ya Tanganyika ikivaa joho la Muungano.
Kifungu
cha (viii) cha Mkataba wa Muungano kinaweka sharti kwamba Mkataba huo hautokuwa
halali hadi pale Bunge la Tangayika na Baraza la Mapinduzi likishirikiana na
Baraza la Mawaziri la Zanzibar
yatakapopitisha sheria za kuridhia Mkataba huo. Upo ushahidi wa kutosha kwamba
Bunge la Tanganyika
lilikutana na kuuridhia Mkataba huo tarehe 25 Aprili, 1964. Hakuna ushahidi
wowote kwamba Baraza la Mapinduzi likishirikiana na Baraza la Mawaziri la Zanzibar yalikaa kuuridhia
Mkataba huo. Kwa hakika ushahidi ulioibuliwa na Prof. Issa Shivji katika kitabu
chake cha karibuni kabisa, Pan-Africanism or Pragmatism? Lesssons of
Tanganyika-Zanzibar Union umeweka wazi pasina chembe ya wasiwasi kwamba Mkataba
huo haujaridhiwa na upande wa Zanzibar
hadi hii leo. Ndiyo kusema, Mkataba wa Muungano haujapata uhalali wa kisheria
hadi leo.
Kifungu
cha (iii) cha Mkataba wa Muungano kiliorodhesha mambo 11 tu ambayo ndiyo
yaliyokubaliwa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na
Jamhuri ya Tanganyika
kuwa mambo ya Muungano. Hata hivyo, kipindi cha miaka 45 ya Muungano
kimeshuhudia mambo hayo yakiongezwa isivyo halali kwa kutumia chombo kisicho na
mamlaka ya kufanya hivyo yaani Bunge la Muungano na sasa kufikia 23 lakini
ukiyanyumbua yanafikia 35. Ikumbukwe kwamba kila hatua ya kuongeza mambo ya
Muungano maana yake ni kuchukua mamlaka ya Zanzibar
na kuyahaulisha kwa Serikali ya Muungano ambayo kama tulivyokwisha onyesha kwa
hakika hasa ni Serikali ya Tanganyika .
Kifungu
cha (vii) cha Mkataba huo kinataka Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mashauriano
na makubaliano na Makamu wa Rais ambaye pia ni Rais wa Zanzibar kuunda Tume ya
Katiba kwa lengo la kutayarisha rasimu ya Katiba ya Kudumu ya Muungano na
baadaye kuifikisha rasimu hiyo mbele ya Bunge la Katiba (Constituent Assembly)
litakalokuwa na wajumbe idadi sawa kati ya Zanzibar na Tanganyika kama
watavyokubaliana viongozi hao wawili. Hatua hii muhimu sana kikatiba ilitakiwa itekelezwe ndani ya
kipindi cha mwaka mmoja tokea tarehe ya Muungano. Hadi hii leo hakuna Tume ya
Katiba iliyoundwa wala Bunge la Katiba lililoundwa na kuitishwa kwa madhumuni
ya kupitisha Katiba ya Kudumu ya Muungano. Kilichofanyika ni kuwa siku moja
kabla ya kumalizika mwaka mmoja uliotakiwa, Bunge la Muungano lilitakiwa
kupitisha sheria ya kuahirisha kwa muda usiojulikana tarehe ya kutekelezwa kwa
hatua hii na hadi leo imesahaulika kabisa.
Lakini
mbali na dhoruba hizo dhidi ya Mkataba wa Muungano, rungu kubwa zaidi ambalo
ndilo lililotumika kuimaliza Zanzibar
lilikuwa ni kule kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM huku
ikijipa madaraka juu ya vyombo vyengine vyote vya maamuzi katika nchi ikiwemo
Serikali na Bunge na Baraza la Wawakilishi. Chini ya dhana ya Chama kushika
hatamu (Party Supremacy) iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa lengo la
kujilimbikizia madaraka yeye na Chama alichokuwa akikiongoza kama milki yake
binafsi, CCM iliweza kutoa maagizo na maamuru mazito bila ya kujali madaraka ya
Serikali ya Zanzibar yaliyotolewa kupitia Mkataba wa Muungano na hivyo kujinyakulia
uwezo wote wa kuitawala Zanzibar ipendavyo huku viongozi wa Zanzibar wanaohoji
wakituhumiwa kwamba wanapinga nidhamu ya Chama.
Matatizo
yatokanayo na kiini cha tatizo
Kiini
cha tatizo la msingi la Muungano ambalo kwa mtazamo wa CUF ni muundo wake unaotokana
na tafsiri potofu ya Mkataba wa Muungano (Articles of Union) ndicho kimepelekea
kujitokeza kwa matatizo mengine katika miaka 45 hii na ambayo yanaongezeka kila
uchao.
Mtu
anapoangalia matatizo au hizi zinazoitwa kero atagundua kuwa karibu yote yanatokana
ama na mshirika mmoja (mara nyingi Zanzibar) kutokuuamini au kuutilia shaka
upande mwengine, au mshirika wa pili (mara nyingi Tanganyika ikivaa joho la
Muungano) kuamini kwamba ina haki ya moja kwa moja kuamua na kutekeleza mambo
fulani bila ya kulazimika kupata ridhaa ya upande wa pili ambao inahisi kama
imeubeba tu. Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa tatizo linarudi kwenye
muundo. Zanzibar haifahamu mamlaka ya Muungano
katika Serikali ya Muungano yanaishia wapi ambapo mamlaka kwa mambo yasiyo ya Muungano
kwa ajili ya Tanganyika
yanaanza. Tanganyika nayo
kwa ‘kuwemo’ kwake katika Serikali ya Muungano kunaifanya ‘ishindwe kufahamu’
ni vipi na wapi Zanzibar inapata mamlaka ya
kuhoji mambo ambayo ‘yameshatamkwa’ kwamba ni ya Muungano hata kama hayakuwemo katika Mkataba wa asili wa Muungano. Hali hii inaonekana katika kila kile kinachoitwa ‘kero’ za Muungano.
Mifano inaweza kutolewa kwa takriban mambo
yote, lakini kwa madhumuni ya waraka huu tuchukue mifano ya mambo matatu
yafuatayo yanayozusha malalamiko:
1. Umilikaji wa Mafuta na Gesi asilia.
2. Uchangiaji katika gharama za Muungano na
mgawanyo wa mapato yanayotokana na Muungano.
3. Uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge la
Muungano.
Umilikaji wa Mafuta na Gesi asilia
Kwanza, kuingizwa kwake katika orodha ya
mambo ya Muungano (kama ilivyo kwa mambo mengi yaliyoongezwa baadaye)
hakukufuata taratibu za Serikali ya Muungano (ambayo pia ni Serikali ya
Tanganyika kwa mambo yasiyo ya Muungano) kuishauri na kupata ridhaa ya
Zanzibar. Pili, Zanzibar inataka kujua ikiwa mafuta yanapaswa kuwa suala la
Muungano na hivyo mapato yatakayopatikana yanufaishe pande zote mbili, kwa nini
madini mengine yanayopatikana Bara kama vile dhahabu, almasi au tanzanite
hayakufanywa pia kuwa ya Muungano na hivyo kunufaisha pande mbili pia? Kwa hivi
sasa, ambapo si mambo ya Muungano, mapato yake yanaponufaisha Tanganyika peke
yake, yanaingia katika mfuko (account) upi wa matumizi? Tatu, ikiwa mapato
yatakayopatikana kutokana na mafuta yataingia katika mfuko wa Muungano, kuna
uhakika gani wa kutumika kwa shughuli za Muungano tu wakati hakuna mifuko
tofauti ya fedha kwa shughuli za Muungano na zile za Tanganyika zisizo za
Muungano?
Uchangiaji katika gharama za Muungano na
mgawanyo wa mapato yanayotokana na Muungano
Je, mtu anaposema Zanzibar haichangii gharama
za uendeshaji wa vyombo na taasisi za Muungano kwa sababu tu Serikali ya
Zanzibar haitoi fungu la fedha na kuliingiza katika Serikali ya Muungano,
Tanganyika ambayo hata Serikali haina inachangia vipi na kiasi gani? Ikiwa
mchango wake unatolewa na Serikali ya Muungano, kwani hii siyo serikali ya
shirika ambapo Zanzibar ni mbia? Vipi basi Zanzibar itakiwe ichangie mara mbili
kwa kutumia hadhi mbili tofauti? Na ikichangia (iwapo itachangia), ina uhakika
upi kwamba itakachotoa hakitatumiwa na Serikali ya Muungano kwa shughuli za
Tanganyika zisizo za Muungano ikitumia mamlaka yake kwa madhumuni hayo? Vivyo
hivyo kwa mapato yatokanayo na vyombo na taasisi za Muungano, tunajua Zanzibar
inapata mgao wake na kiasi chake kimewekwa wazi (ingawa hakikubaliki kwa
Wazanzibari). Masuala yanakuja: Yale mapato yanayobaki katika Serikali ya
Muungano, kuna kipi cha kuonyesha mpaka wa matumizi yake kwa Muungano na kwa
shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano? Uadilifu na uwajibikaji wa matumizi
yatokanayo na mgao huu wa mapato utaonekana vipi?
Uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge la
Muungano
Wananchi wengi wa Tanganyika wanahoji vipi
Zanzibar iliyo ndogo na ambayo ina watu wasiozidi milioni moja inawakilishwa na
wabunge wa kuchaguliwa 50 wakati Dar es Salaam yenye wananchi wengi zaidi ina
wabunge wa kuchaguliwa 7 tu? Wabunge hawa wanashiriki mijadala yote ya Bunge
ikiwemo ya mambo yasiyo ya Muungano (ambayo kwa usahihi yatakuwa ni mamlaka ya
Tanganyika kwa mambo yasiyo ya Muungano yanayosimamiwa na Serikali ya
Muungano). Wanapata wapi uhalali wa kufanya hivyo wakati Wazanzibari
hawapangiwi shughuli hizo (kwa mfano elimu, afya, kilimo, maji, umeme, habari,
michezo, biashara, viwanda, serikali za mitaa n.k.) na Serikali ya Muungano
wala hawasimamiwi katika mambo hayo na Bunge la Muungano? Uko wapi mpaka wa
mamlaka ya Wazanzibari katika ushiriki wa Bunge hilo wakati wao wana Serikali
yao inayopanga na Baraza la Wawakilishi lao linalosimamia mambo yao kama hayo
yasiyo ya Muungano?
Mifano hii inatosha kuonyesha kwamba karibu
matatizo yote, kama si yote, yanatokana na mkanganyiko na mgongano wa maslahi
kati ya pande mbili ambao nao unasababishwa na mfumo usio wazi kuhusiana na
mgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka tatu za Muungano zinazotambuliwa katika
Mkataba wa Muungano.
Nafasi ya Zanzibar katika Muungano
Baada ya kuangalia kiini cha matatizo ya
Muungano kinachotokana na muundo wa Muungano, sasa tuangalie nafasi ya Zanzibar
katika Muungano huu, hasa kufuatia kauli za kuidhalilisha Zanzibar zilizotolewa
na wanasiasa wa Tanganyika hivi karibuni wakiongozwa na Waziri Mkuu Mizengo
Pinda.
Kutokana na kule kule kujaribu kujisahaulisha
kuwepo kwa Mkataba wa Muungano ambao ndio sheria kuu (grundnorm) ya Muungano na
kuifanya Katiba inayoitwa ya Jamhuri ya Muungano kuwa ndiyo Katiba mama na
hivyo kuikweza kwamba eti iko juu ya Katiba ya Zanzibar, zimetolewa kauli
kwamba kufuatia hatua ya kuungana na Tanganyika, Zanzibar imepoteza hadhi na
sifa ya kuwa nchi.
Waliosema hivi wanasahau kwamba Zanzibar ina
Katiba yake ambayo ina hadhi sawa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na kwamba
zote mbili zinapaswa kutafsiri kisawa sawa Makubaliano ya Muungano.
Katiba ya Zanzibar inatamka wazi wazi kwamba
Zanzibar ni nchi. Utangulizi (Preamble) wa Katiba hiyo ambao unaeleza dhamira
ya Wazanzibari wakiwa ndiyo wenye Katiba hiyo (sponsors of the Constitution)
unabainisha wazi wazi dhamira ya Wazanzibari kulinda na kudumisha nchi yao na
yale yote yanayoitambulisha Zanzibar kama nchi. Sehemu ya Utangulizi huo
inasomeka:
"NA KWA KUWA tunazingatia na kuthamini
kazi nzuri ya Kimapinduzi iliyofanywa na Viongozi wa Mapinduzi, wakiongozwa na
Mwasisi wa Chama cha ASP na Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, Marehemu Mzee Abeid
Amani Karume, ambaye fikra zake zitaendelezwa na kudumishwa daima, kizazi baada
ya kizazi katika kupambana na Ukoloni, Ubepari Unyonge, Uonevu na Dharau, na
badala yake kudumisha Uhuru na Umoja, Haki na Usawa, Heshima na Utu;"
Ni bahati mbaya kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakinukuu vibaya kifungu cha (1) cha Katiba ya Zanzibar kinachosema “Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” kumaanisha kwamba kwa kuwa kwake sehemu ya Jamhuri ya Muungano kunaiondolea na kuipotezea Zanzibar hadhi yake ya kubakia kuwa nchi. Tafsiri hiyo si sahihi kama ilivyofafanuliwa na Jaji Abdullahi D. Zuru kutoka Nigeria, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kupitia Sheria (Law Review Commission) Zanzibar.
Ni bahati mbaya kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakinukuu vibaya kifungu cha (1) cha Katiba ya Zanzibar kinachosema “Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” kumaanisha kwamba kwa kuwa kwake sehemu ya Jamhuri ya Muungano kunaiondolea na kuipotezea Zanzibar hadhi yake ya kubakia kuwa nchi. Tafsiri hiyo si sahihi kama ilivyofafanuliwa na Jaji Abdullahi D. Zuru kutoka Nigeria, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kupitia Sheria (Law Review Commission) Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilimuagiza
Jaji Zuru kuipitia Katiba ya Zanzibar na kupendekeza marekebisho ikibidi. Jaji
Zuru amesema katika ripoti yake kuhusu kifungu cha (1) cha Sura ya Kwanza,
Sehemu ya Kwanza ya Katiba ya Zanzibar kuwa:
"Mtu akisoma kwa makini Utangulizi (Preamble) na Katiba yote kwa jumla, ataelewa kwamba Zanzibar ni dola yenye mamlaka yake kamili (sovereign state) na kwamba wale waliotunga Katiba hii hawakuwa na nia ya kusalimisha na kuachia mamlaka (sovereignty) ya Zanzibar wakati wa kuundwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, ambao ulizaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, mtu akisoma maelezo ya kifungu cha (1) cha Katiba anapigwa na butwaa na kushangaa kwa nini kifungu hicho cha kwanza kwa kinyemela (surreptiously) kimesalimisha au kimepuuza mamlaka hayo."
Jaji Zuru anaendelea kusema kuwa anaamini kwamba waanzilishi wa hatua ya kuzileta pamoja Zanzibar na Tanganyika kuwa Jamhuri moja, hawajakusudia kuwa hatua hiyo ipoteze (erode) uhuru wa nchi yoyote kati ya nchi mbili kamili zilizohusika.
Kinyume na hayo, maoni yake ni kwamba nia ilikuwa kuimarisha uhuru wa kila moja ya nchi hizo mbili sambamba na ule wa Muungano utakaozaliwa. Mtaalamu huyo anafahamisha kwamba kisheria, "Haki mbili zikikutana ndani ya mtu mmoja, ni sawa na kusema kwamba ziko ndani ya watu wawili."
Labda tuiweke kwa Kiingereza, kama alivyoandika mwenyewe, kwa kufahamika zaidi: "It is a trite law that when two rights meet in one person, it is the same as if that were in two persons."
"Mtu akisoma kwa makini Utangulizi (Preamble) na Katiba yote kwa jumla, ataelewa kwamba Zanzibar ni dola yenye mamlaka yake kamili (sovereign state) na kwamba wale waliotunga Katiba hii hawakuwa na nia ya kusalimisha na kuachia mamlaka (sovereignty) ya Zanzibar wakati wa kuundwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, ambao ulizaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, mtu akisoma maelezo ya kifungu cha (1) cha Katiba anapigwa na butwaa na kushangaa kwa nini kifungu hicho cha kwanza kwa kinyemela (surreptiously) kimesalimisha au kimepuuza mamlaka hayo."
Jaji Zuru anaendelea kusema kuwa anaamini kwamba waanzilishi wa hatua ya kuzileta pamoja Zanzibar na Tanganyika kuwa Jamhuri moja, hawajakusudia kuwa hatua hiyo ipoteze (erode) uhuru wa nchi yoyote kati ya nchi mbili kamili zilizohusika.
Kinyume na hayo, maoni yake ni kwamba nia ilikuwa kuimarisha uhuru wa kila moja ya nchi hizo mbili sambamba na ule wa Muungano utakaozaliwa. Mtaalamu huyo anafahamisha kwamba kisheria, "Haki mbili zikikutana ndani ya mtu mmoja, ni sawa na kusema kwamba ziko ndani ya watu wawili."
Labda tuiweke kwa Kiingereza, kama alivyoandika mwenyewe, kwa kufahamika zaidi: "It is a trite law that when two rights meet in one person, it is the same as if that were in two persons."
Anaendelea
kusema kwamba ni imani ya Tume yake kabisa kuwa ulipoundwa Muungano, Zanzibar ilikusudia na
ilisisitiza juu ya kuendeleza mamlaka yake ndani ya utaratibu wa Muungano.
Anafafanua:
"Kutokana na haya, tunaamini kwamba hadhi yaZanzibar
kama inavyoelezwa katika kifungu cha (1) imepotoshwa kwa sababu (kifungu)
hakielezi nia ya wenye katiba (sponsors of this constitution) na madaraka
yaliyotolewa na watu wa Zanzibar ..."
Labda turudi nyuma kidogo tufahamishe kuwa Tume ya Jaji Zuru imeeleza mwanzoni kuwa madaraka waliyo nayo Baraza la Wawakilishi, ambalo ndilo lililotunga Katiba hiyo mwaka 1984, yanatokana na wananchi na kwamba Baraza linayashikilia madaraka hayokama amana (trust) kwa niaba ya
wananchi hao. "Kwa hiyo, kushindwa kwa Serikali kusimamia misingi ya
katiba ni sawa na kwenda kinyume na amana waliyokabidhiwa na watu wa Zanzibar ."
Haya yanaelezwa wazi katika kifungu cha 9 cha Katiba yaZanzibar kinachosema,
"Kutokana na haya, tunaamini kwamba hadhi ya
Labda turudi nyuma kidogo tufahamishe kuwa Tume ya Jaji Zuru imeeleza mwanzoni kuwa madaraka waliyo nayo Baraza la Wawakilishi, ambalo ndilo lililotunga Katiba hiyo mwaka 1984, yanatokana na wananchi na kwamba Baraza linayashikilia madaraka hayo
Haya yanaelezwa wazi katika kifungu cha 9 cha Katiba ya
"9.-(1)
Zanzibar
itakuwa ni nchi ya kidemokrasia na haki za kijamii.
(2) Kwa hiyo hapa inaelezwa rasmi kwamba:-
(a) Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe."
Tukiendelea na hoja, Jaji Zuru anasema maelezo ya kifungu cha (1) cha Katiba, ambacho ndicho kama mlango wa kuingilia kwenye Katiba yenyewe, yanampa msomaji wa nje sura ya kwambaZanzibar
si nchi yenye mamlaka yake wenyewe. "Kwa hiyo, tunachukulia maelezo haya
kama ni kwenda kinyume na nia ya watu wa Zanzibar
ambayo iko wazi na bayana katika Utangulizi (Preamble) na sehemu nyengine
zinazohusika katika Katiba."
Kutokana na haya Tume imependekeza kifungu hiki kiandikwe upya ili kuwakilisha nia ya watu waZanzibar .
Kisomeke kama ifuatavyo:
"Zanzibar ni, na itabaki dola yenye mamlaka, na itakuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa matakwa na masharti yaliyotajwa katika Mkataba wa Muungano baina ya Dola ya Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika.”
Kwa madhumuni ya uelewa zaidi tutanukuu tena kwa Kiingereza kama alivyoandika mwenyewe Jaji Zuru:
(2) Kwa hiyo hapa inaelezwa rasmi kwamba:-
(a) Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe."
Tukiendelea na hoja, Jaji Zuru anasema maelezo ya kifungu cha (1) cha Katiba, ambacho ndicho kama mlango wa kuingilia kwenye Katiba yenyewe, yanampa msomaji wa nje sura ya kwamba
Kutokana na haya Tume imependekeza kifungu hiki kiandikwe upya ili kuwakilisha nia ya watu wa
"Zanzibar ni, na itabaki dola yenye mamlaka, na itakuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa matakwa na masharti yaliyotajwa katika Mkataba wa Muungano baina ya Dola ya Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika.”
Kwa madhumuni ya uelewa zaidi tutanukuu tena kwa Kiingereza kama alivyoandika mwenyewe Jaji Zuru:
"Zanzibar is and shall remain a sovereign state, and shall
exist as an integral part of the United Republic of Tanzania, in accordance
with the terms and conditions stipulated in the Articles of Union between the
State of Zanzibar and the Republic
of Tanganyika .”
Kifungu cha 2 (2) cha Katiba yaZanzibar
kinasema, "Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais wa
Jamhuri ya Muungano akishauriana na Rais anaweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo
mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa."
Tume inasema kwa vile Rais waZanzibar ndiye
mlinzi wa dhamana (custodian) wa mamlaka ya watu wa Zanzibar ,
anapaswa kuchukuwa jukumu la mbele (vital role) katika uamuzi na ukataji wa
mipaka ya kiutawala ya Zanzibar .
Hivyo, haitoshi 'kushauriana' tu, bali lazima ridhaa na kauli (consent and
approval) ya Rais wa Zanzibar
ipatikane.
Mapendekezo ya Tume ya Jaji Zuru yalipelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Disemba 19, 2001, lakini hadi hii leo Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar
haijachukua hatua zozote kuyafikisha mbele ya Baraza la Wawakilishi ili
kurekebisha mapungufu ya kiuandishi ya Katiba ya Zanzibar
na kutafsiri kisawasawa dhamira ya wananchi wa Zanzibar .
Tukiachana na mapendekezo hayo, tuangalie Sura ya Kumi na Tatu ya Katiba yaZanzibar . Kifungu cha 132
(1) kinachosema:
"132.- (1) Hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumikaZanzibar
mpaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe
kulingana na maelezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.
(3) Pale sheria ndogo inapoundwa kwa mujibu wa uwezo uliowekwa chini ya vifungu vya (1) na (2) sheria hii itatumika tu pale itapotimiza shuruti zote zilizowekwa kwa matumizi ya Sheria mamakama
ilivyoamrishwa katika kifungu hiki."
Hapa mambo mawili yanajitokeza.Kwanza kati ya
mambo yote ya Muuungano, zaidi ya yale kumi na moja ya asili, yaliyoongezwa
katika orodha ya mambo ya muuungano (xii –xxiii) ni moja tu, kuhusu
uandikishwaji wa vyama vya siasa, ambapo mswada ulipelekwa Baraza la
Wawakilishi, ukajadiliwa na kupitishwa.
Ndiyo maana imo katika vitabu vya sheria (Statute Books) vya Sheria zaZanzibar . Mambo mengine
yote hayamo katika vitabu ya sheria vya Zanzibar
na anayevitekeleza anaweza kushtakiwa kwa kwenda kinyume na matakwa ya Katiba
ya Zanzibar .
Kifungu cha 2 (2) cha Katiba ya
Tume inasema kwa vile Rais wa
Mapendekezo ya Tume ya Jaji Zuru yalipelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Disemba 19, 2001, lakini hadi hii leo Serikali ya Mapinduzi ya
Tukiachana na mapendekezo hayo, tuangalie Sura ya Kumi na Tatu ya Katiba ya
"132.- (1) Hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika
(2) Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.
(3) Pale sheria ndogo inapoundwa kwa mujibu wa uwezo uliowekwa chini ya vifungu vya (1) na (2) sheria hii itatumika tu pale itapotimiza shuruti zote zilizowekwa kwa matumizi ya Sheria mama
Hapa mambo mawili yanajitokeza.
Ndiyo maana imo katika vitabu vya sheria (Statute Books) vya Sheria za
Mambo
hayo yaliyoongezwa juu ya Makubaliano ya Muungano ya asili, yaani, yale kumi na
moja (11) ni haya, kama yanavyoelezwa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano:-
(xii) Mambo yote yanayohusika na Sarafu na Fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
(xiii) Leseni za Viwanda na Takwimu.
(xiv) Elimu ya Juu.
(xv) Maliasili ya Mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa za mafuta, na gesi asilia.
(xvi) Baraza la Taifa la MitihaniTanzania
na mambo yanayohusika na kazi za Baraza hilo .
(xvii) Usafiri na Usafirishaji wa Anga.
(xviii) Utafiti.
(xix) Utabiri wa Hali ya Hewa.
(xx) Takwimu.
(xxi) Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano.
(xxii) Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana nayo.
(xxiii) Uvuvi wa Bahari Kuu.
Yote haya yameingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano kinyume na sheria na taratibu, na bila ya ridhaa yaZanzibar
kwa mujibu wa Katiba. Hivyo ni batili na hayana nguvu za kisheria.
Pili, Matamko na Matangazo ya Kisheria ya Rais wa Muungano (Presidential Decrees and Orders) ambayo hutolewa kutokana na nguvu anazopewa ama na katiba au sheria mama pale yanapokuwa yanahusu mambo ya Muungano yaliyoongezwa isivyo halali ambayo yenyewe yanatokana na sheria batili zilizotungwa kinyume na matakwa ya kifungu cha 132 (3) cha Katiba ya Zanzibar nayo yatakuwa ni batili na hayatakuwa na nguvu za kuweza kusimama kisheria.
Mfano ni Amri ya Rais (Presidential Order) iliyotangazwa mwaka 1969 wakati wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzishwa kwa Shirika la Uendelezaji PetroliTanzania (TPDC), na kulipa mamlaka shirika hilo kuwa na nguvu kisheria hadi katika Visiwa vya Zanzibar itakuwa ni batili chini ya masharti ya kifungu
cha 132 (3) cha Katiba ya Zanzibar .
Kifungu kinachofuata yaani 133 (1) kinasema:
"133.-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi au kwa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu ya kisheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
(2) Masharti yaliyomo katika kijifungu hiki hayatalizuwia Bunge kutumia mamlaka ya kutoza kodi ya aina yoyote inayohusiana na mambo ya Muungano kwa mujibu wa madaraka ya Bungehilo ,
kwa kujuwa kwamba mashauriano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano yamefanywa na kukubalika sehemu zote mbili
kabla kupitishwa sheria."
(xii) Mambo yote yanayohusika na Sarafu na Fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
(xiii) Leseni za Viwanda na Takwimu.
(xiv) Elimu ya Juu.
(xv) Maliasili ya Mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa za mafuta, na gesi asilia.
(xvi) Baraza la Taifa la Mitihani
(xvii) Usafiri na Usafirishaji wa Anga.
(xviii) Utafiti.
(xix) Utabiri wa Hali ya Hewa.
(xx) Takwimu.
(xxi) Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano.
(xxii) Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana nayo.
(xxiii) Uvuvi wa Bahari Kuu.
Yote haya yameingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano kinyume na sheria na taratibu, na bila ya ridhaa ya
Pili, Matamko na Matangazo ya Kisheria ya Rais wa Muungano (Presidential Decrees and Orders) ambayo hutolewa kutokana na nguvu anazopewa ama na katiba au sheria mama pale yanapokuwa yanahusu mambo ya Muungano yaliyoongezwa isivyo halali ambayo yenyewe yanatokana na sheria batili zilizotungwa kinyume na matakwa ya kifungu cha 132 (3) cha Katiba ya Zanzibar nayo yatakuwa ni batili na hayatakuwa na nguvu za kuweza kusimama kisheria.
Mfano ni Amri ya Rais (Presidential Order) iliyotangazwa mwaka 1969 wakati wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzishwa kwa Shirika la Uendelezaji Petroli
Kifungu kinachofuata yaani 133 (1) kinasema:
"133.-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi au kwa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu ya kisheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
(2) Masharti yaliyomo katika kijifungu hiki hayatalizuwia Bunge kutumia mamlaka ya kutoza kodi ya aina yoyote inayohusiana na mambo ya Muungano kwa mujibu wa madaraka ya Bunge
Si
jambo la siri kwamba kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya Serikali ya Awamu ya
Tano ya Dk. Salmin Amour na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusiana na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hadi leo wananchi wa Zanzibar
wanaiona TRA kama ndiye adui mkubwa wa uchumi
wao, iliyoua biashara visiwani na kuwatia Wazanzibari katika ufukara
usiosemeka.
Ni wazi basi kwamba uundwaji wa TRA haujatimiza masharti ya kifungu cha 133 (2) cha Katiba yaZanzibar .
Inawezekana kukazuka hoja kwamba pale Katiba yaZanzibar inapopingana na Katiba ya Muungano
ni ile ya Muungano ndio yenye nguvu. Ndio. Hii ni kuhusu vifungu vinavyowiana
na Makubaliano ya Muungano kama yalivyokuwa yamekubaliwa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika hapo mwaka 1964.
Vyengine vyote ni batili na hapo moja kwa kwa moja Katiba ya Zanzibar ndiyo itakayosimama.
Kwa msingi wa hoja hizi, ni ukweli usio na ubishi kwamba Zanzibar imeendelea kubaki na hadhi yake kama nchi hata baada ya kuingia katika Muungano na Tanganyika na ndiyo maana Katiba yake, pamoja na mapungufu madogo madogo, bado imelinda kwa nguvu zote hadhi hiyo.
Ni wazi basi kwamba uundwaji wa TRA haujatimiza masharti ya kifungu cha 133 (2) cha Katiba ya
Inawezekana kukazuka hoja kwamba pale Katiba ya
Kwa msingi wa hoja hizi, ni ukweli usio na ubishi kwamba Zanzibar imeendelea kubaki na hadhi yake kama nchi hata baada ya kuingia katika Muungano na Tanganyika na ndiyo maana Katiba yake, pamoja na mapungufu madogo madogo, bado imelinda kwa nguvu zote hadhi hiyo.
Naelewa
kwamba kuna watu wanatumia uamuzi wa Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano
katika kesi maarufu ya Machano Khamis Ali na wenzake 18 dhidi ya SMZ uliotamka
kwamba Zanzibar si nchi na kwamba kosa la uhaini haliwezi kutendeka Zanzibar
kuwa ni msingi wa hoja kwamba vifungu nilivyovitaja vya Katiba ya Zanzibar
vinakuwa havina maana yoyote pale vinaposititiza hadhi ya Zanzibar kama nchi.
Ni
muhimu kueleweka kwamba uamuzi huu wa Mahkama ya Rufaa umejaa utatanishi. Kwanza , ulitolewa wakati Serikali ikiwa tayari imeondosha
mashtaka dhidi ya watuhumiwa na kuwaachia huru. Kwa msingi huo, mtu anajiuliza
uamuzi huo wa Mahkama ya Rufaa wakati unatolewa ulikuwa na uhalali upi
kisheria. Lakini pili, mtaalamu wa masuala ya katiba anayeongoza hapa Tanzania , Prof. Issa Shivji amefanya mapitio ya
uamuzi huo na kubainisha makosa mengi sana
ya kisheria yaliyomo. Kubwa katika makosa hayo ni kule Majaji wanaohusika
kudharau na kutoitumia kabisa Katiba ya Zanzibar
katika kufikia uamuzi wao. Katika hitimisho lake, Prof. Shivji anasema:
“The
conclusion from this quick examination of the Zanzibar Constitution is that
Zanzibar is a sovereign and a state, albeit its sovereignty is limited and the
jurisdiction of the Executive and the Legislature is limited to non-Union
matters in Zanzibar while its Judiciary, as epitomised by the High Court, has
unlimited jurisdiction. A Mzanzibari owes allegiance to the State of Zanzibar
and therefore an offence of treason can be committed against the state of Zanzibar . This is
irrespective of the fact that treason may be stipulated as an offence in the
union law; nevertheless it can be tried in the courts of Zanzibar .”
“Hitimisho
la upembuzi huu wa haraka wa Katiba ya Zanzibar ni kwamba Zanzibar ni dola na
ni nchi, ijapokuwa nguvu yake ya kidola ina mipaka na uwezo wa Mamlaka ya
Utawala na Mamlaka ya Kutunga Sheria umewekewa mipaka kwa mambo yasiyo ya
Muungano ndani ya Zanzibar wakati Mamlaka ya Utoaji Haki, ikiwa inaongozwa na
Mahkama Kuu, ina uwezo kamili usio na mipaka. Mzanzibari ana utii kwa Dola ya Zanzibar na hivyo kosa la uhaini linaweza kutendeka dhidi
ya Dola ya Zanzibar .
Hii ni bila ya kujali kwamba uhaini unaweza kuainishwa kuwa ni kosa kupitia
sheria ya Muungano; lakini bado kosa hilo
linaweza kuhukumiwa katika Mahkama za Zanzibar .”
Muungano wa Serikali tatu utaongeza gharama?
Baada ya kuangalia nafasi ya Tanganyika na ya
Zanzibar katika Muungano na madaraka yao, na kuonyesha kwamba njia pekee ya
kushughulikia matatizo ya msingi ya Muungano ni kwa kurejea katika Mkataba wa
Muungano na hivyo kuanzisha mfumo wa Serikali tatu, ni vyema tutafakari kidogo
suala la gharama za uendeshaji wa mfumo huo.
Wapinzani wa Muungano imara chini ya msingi
madhubuti wa Shirikisho la Serikali tatu wamekuwa wakiibua mara kwa mara hoja
ya kuongezeka kwa gharama za utawala na uendeshaji kama kikwazo cha kukwamisha
juhudi za kuuimarisha Muungano.
Hoja hii imeonekana ni dhaifu na isiyo na
msingi kabisa kufuatia kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Fedha (Joint Finance
Commission) ambayo ripoti zake za awali zimekaliwa na Serikali ya Muungano hadi
leo baada ya kutoa picha halisi ya jinsi mchango wa Muungano unavyopaswa uwe.
Tume hiyo imeipa kazi kampuni ya PriceWaterhouseCoopers kufanya uchambuzi
halisi wa mambo yepi ni ya Muungano halisi na yepi ni ya Tanganyika na yepi ni
ya Zanzibar. Baada ya orodha kupatikana, watafiti wakatafuta matumizi halisi ya
bajeti ya vifungu hivyo kwa muda wa kiasi cha miaka 10 iliyopita. Watafiti hao
walikwenda mbali zaidi ya hapo na kukusanya mapato yote kwa kila kifungu cha
mambo ya Muungano halisi. Mwishowe, wakalinganisha iwapo mapato yanakidhi
matumizi au yana nakisi (upungufu)?
Kilichojitokeza ni kwamba kwa mwaka wa fedha
2003/2004 pekee, matumizi halisi kwa vifungu vya Muungano yalikuwa Shs.
537,258.4 bilioni na mapato halisi kwa mwaka huo yalikuwa ni Shs. 1,030,826.1
bilioni. Tofauti ya vifungu hivyo vimetoa ziada ya ya Shs. 493,567.7 bilioni
kwa mwaka huo. Ziada hii haiingizi mapato yanayotokana na misaada kutoka nje au
mikopo. Ziada hii hutumika kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano.
Ukweli huu unaonyesha hata kama kungekuwa na
Serikali tatu kusingekuwa na haja yoyote kwa Serikali ya Zanzibar na ile ya
Tanganyika kulipia fedha za ziada kama wahusika watatunza na kuweka kumbukumbu
sahihi za mapato na matumizi ya mambo ya Muungano halisi badala ya yale ya
Tanganyika kuchanganywa na ya Muungano. Mambo yasiyokuwa ya Muungano ya
Tanganyika yalipotengwa nje ya yale ya Muungano, gharama za mambo ya Muungano
zimejidhihirisha wazi bila ya kujificha na kuonesha kwamba zinaweza kulipiwa
kupitia mapato ya mambo ya Muungano pekee na ziada kubaki. Lakini hili limekuwa
rahisi kwa kukubali ukweli kwamba kuna mafungu matatu ya mapato na matumizi
katika Serikali zetu mbili. Mafungu hayo ni la SMZ kwa mambo yake yasiyo mambo
ya Muungano, la Serikali ya Muungano kwa mambo ya Muungano, na la Serikali ya
Muungano inayofanya kazi za Tanganyika kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano.
Kinachohitajika sasa ni hili kuliweka wazi kwa viongozi kuweka nia njema na
kuuweka sawa muundo wa Muungano wetu ili uzionyeshe waziwazi mamlaka zote tatu.
Vipi tutoke hapa tulipo?
Inakaribia miaka 45 sasa tangu uundwe
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulikuwa na wakati wa kutosha kurekebisha
kasoro zilizopo. Hilo halikuwezekana kutokana na ubabe wa Mwalimu Nyerere
ambaye aliamua kuwatia shemere Wazanzibari na kuhakikisha Muungano unakwenda
kama alivyotaka yeye hata baada ya ‘kuondoka madarakani’.
Si jambo la kuficha kwamba wananchi wa pande
zote mbili za Muungano wamechoshwa na unafiki uliopo na wanadai Katiba ya kweli
kweli itakayoweka misingi mipya ya ushirikiano.
Kama nilivyoeleza mwanzoni, kiini cha
matatizo ya Muungano ni kutokuheshimiwa kwa Mkataba wa Muungano (Articles of
Union) ambao kisheria ni Mkataba wa Kimataifa unaopaswa kuheshimiwa kwa
kuzingatia masharti yote yanayohusu mikataba ya kimataifa.
Haidhuru sasa ni takriban miaka 45 tokea
kuanza kwa hatua za kuukanyaga kanyaga Mkataba wa Muungano mara tu baada ya
kutiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,
na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
lakini ukweli utabaki kuwa huo ulikuwa ndiyo msingi pekee, nasisitiza tena,
pekee, uliokubaliwa na viongozi hao wawili kuongoza mahusiano ya nchi zetu
mbili kupitia Muungano.
Wakati sasa umefika tukubali kwamba suluhisho
la matatizo haya siyo kuendelea kuunda Tume au Kamati au kuandaa warsha,
semina, makongamano na mikutano. Suluhisho ni kutekeleza kwa dhati Mkataba wa
Muungano (Articles of Union) ambao ni mkataba wa kimataifa wa nchi mbili huru.
Kujaribu kulazimisha kutumia Katiba inayoitwa
ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyo sasa ambayo inakosa uhalali wa kisheria
kuzima madai ya wananchi wa Zanzibar hakuwezi kukubalika tena katika zama hizi.
Kwa msingi huo, hakuna njia ya mkato ya
kuyashughulikia matatizo ya Muungano bila ya kwenda kwenye kiini cha matatizo
hayo ambacho ni kutokuheshimiwa kwa Mkataba wa Muungano. Wahenga wamesema,
Mwiba uchomeapo ndipo utokeapo. Ili kuyaheshimu Makubaliano ya Muungano,
yafuatayo ni lazima yafanyike:
1. Kwa kuwa Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar la mwaka 1964 ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuuridhia (ratify) Mkataba wa Muungano, hivyo basi kwanza kabisa, na kabla ya kuchukua hatua nyengine yoyote, ni lazima Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuuridhia Mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar na hivyo kuupa uhalali wa kisheria Muungano wenyewe kama yalivyo masharti ya kifungu cha (viii) cha Mkataba huo wa Muungano.
1. Kwa kuwa Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar la mwaka 1964 ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuuridhia (ratify) Mkataba wa Muungano, hivyo basi kwanza kabisa, na kabla ya kuchukua hatua nyengine yoyote, ni lazima Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuuridhia Mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar na hivyo kuupa uhalali wa kisheria Muungano wenyewe kama yalivyo masharti ya kifungu cha (viii) cha Mkataba huo wa Muungano.
2. Kwa ujumla tuupitie tena Mkataba wa
Muungano na kurekebisha vifungu vyenye utatanishi. Kama Muungano huu haukuwa na
mtego, ulikuja kwa ridhaa za Serikali zetu mbili, vipi tunashindwa kukaa tena
tukaupitia baada ya miaka 45 na kuuweka kwenye hali ya kuvutia hata majirani
zetu wakajiunga?
3. Katiba ya Zanzibar itumike Zanzibar kwa
mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (v)
cha Mkataba wa Muungano.
4. Katiba ya Tanganyika (ile iliyokuwepo
kabla ya kurekebishwa kuingiza mambo ya Muungano) nayo irejee kutumika
Tanganyika kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kama yalivyo masharti ya
kifungu cha (v) cha Mkataba wa Muungano.
5. Kwa kutumia Katiba ya Tanganyika, iundwe
Serikali ya Tanganyika inayoshughulika na mambo yasiyo ya Muungano, kama
Serikali ya Zanzibar inavyoshughulika na mambo yake ambayo si ya Muungano.
6. Serikali ya Muungano ishughulike na yale
mambo 11 tu ya asili yaliyokubaliwa kuwa ndiyo mambo ya Muungano kwa mujibu wa
kifungu cha (iv) cha Mkataba wa Muungano.
7. Mambo mengine yote 12 yaliyoongezwa katika
orodha ya mambo ya Muungano kinyume na Mkataba wa Muungano yaondolewe katika
orodha hiyo na yarudi katika mamlaka za Zanzibar na Tanganyika.
8. Wafanyakazi wa Tanganyika wasihusike na
mambo ya Muungano, wawe katika “civil service” (mfumo wa wafanyakazi
Serikalini) wa Tanganyika, kama walivyo wa Zanzibar kwa Zanzibar (wasio wa
taasisi za Muungano).
9. Urejee utaratibu wa kuwepo kwa Makamu
wawili wa Rais wa Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (iii) (b) cha
Mkataba wa Muungano ambapo Rais wa Zanzibar na Rais wa Tanganyika wawe Makamu
wa Rais wa Muungano kwa mujibu wa nyadhifa zao.
10. Iundwe Tume ya kutayarisha rasimu ya
Katiba ya Kudumu ya Muungano ambayo itakuwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka
Zanzibar na Tanganyika kama yalivyo matakwa ya kifungu cha (vii) (a) cha
Mkataba wa Muungano.
11. Liundwe Bunge la Katiba (Constituent
Assembly) litakalokuwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Zanzibar na Tanganyika
ambalo litakuwa na majukumu ya kupokea rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Katiba
na baada ya hapo kupitisha rasmi Katiba ya Kudumu ya Muungano kama yalivyo
matakwa ya kifungu cha (vii) (b) cha Mkataba wa Muungano.
Itaonekana kwamba msingi wa hatua zote
zilizoorodheshwa hapa ni kuheshimu mapatano ya nchi zetu mbili yaliyomo katika
Mkataba wa Muungano. Haya yalibidi yafanyike ndani ya mwaka mmoja tokea
kusainiwa kwa Makubaliano ya Muungano. Hata hivyo, Waingereza wanasema, “Better
late than never” (Bora kuchelewa kuliko kutofanya kabisa). Wakati ndio huu
ikiwa tunataka Muungano wa kweli, Muungano wa haki kwa pande zote mbili.
Wasioitakia mema CUF wanaweza kudai kwamba
hatua hizi zinazopendekezwa haziashirii nia njema ya kuendeleza na kuimarisha
Muungano. Sisi katika CUF hatuamini hivyo. Tunaamini katika kuwa wakweli na
wawazi, kwamba hivyo ndivyo yalivyo makubaliano katika Mkataba unaoanzisha
Muungano.
Ulimwengu unabadilika kwa kasi. Zama za
kuendesha mambo kwa ubabe na ukichwa ngumu zimepitwa na wakati. Tuache ile
tabia ya kuyaona mapendekezo ya kubadili mfumo wa Muungano kuwa yana nia ya
kuuvunja Muungano huo. Muungano ili udumu unahitaji ridhaa ya walioungana.
Muasisi wa Muungano huu, Mwalimu Nyerere mwenyewe, aliwahi kueleza umuhimu wa
ridhaa katika masuala haya na kuonyesha kwamba ridhaa ya mshirika mmojawapo
ikiondoka, Muungano hauwezi kusimama. Alisema mwaka 1968:
“If
the mass of the people of Zanzibar should,
without external manipulation, and for some reason of their own, decide that
the Union was prejudicial to their existence,
I could not bomb them into submission … The Union would have ceased to exist
when the consent of its constituent members was withdrawn.”
“Iwapo
wananchi walio wengi wa Zanzibar
wataamua, bila ya msukumo wa kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, kwamba
Muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao, siwezi kuwalazimisha kwa kuwapiga
mabomu … Muungano utasita kuendelea pale ridhaa ya washirika wake
itakapoondolewa.”
Wazanzibari
ni watu wenye historia ya maingiliano ya jamii za watu mbali mbali na hivyo
hawawezi kukataa umoja, alimradi tu umoja huo uwe na maslahi na faida kwao.
Mfumo uliopo sasa hauinufaishi Zanzibar
na hivyo haukubaliki kwa Wazanzibari. Koti la Muungano kama lilivyo sasa
linabana sana .
Wakati umefika tushone koti jipya kwa mujibu wa mahitaji ya zama hizi.
Hitimisho:
Mazungumzo ya dhati yenye nia njema ndiyo njia
CUF,
kama ulivyo Muungano tunaoujadili, imekumbana
na dhoruba nyingi katika kipindi kifupi cha kuwepo kwake. Miongoni mwa dhoruba
hizo ni kupakaziwa kila ubaya ili kuwazuia wananchi wasikiunge mkono ikiwemo
hoja kwamba hakiutaki Muungano na kwamba pindi kikishika madaraka kitauvunja
Muungano huo. Hoja hii ni dhaifu mno inayolenga kutimiza malengo ya kisiasa
badala ya kushughulikia hasa kiini cha matatizo ya msingi ya Muungano.
Si
siri kwamba kwa kushindwa kushughulikia kiini cha matatizo haya kumewapelekea
wananchi kuona kwamba Muungano huu haupo kwa maslahi yao . Na kwa Wazanzibari, kutokana na Serikali
ya Muungano kila uchaguzi unaopokaribia kuamua kumimina maelfu kwa maelfu ya
askari wa vikosi vyake ambao, kwa kushirikiana na askari wa vikosi vya SMZ,
wamekuwa wakitumika kuwaadhibu Wazanzibari kwa kujaribu kutumia haki yao ya
kidemokrasia na kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka, wanafikia hatua hata ya
kuuona ni Muungano wa kikandamizaji. Hisia za namna hii zinapata nguvu zaidi
pale wanapomuona Rais wa Jamhuri ya Muungano anafikia kujua na kukiri kwamba
chama chake hakina nafasi ya kushinda uchaguzi huru na wa haki lakini viongozi
wake watatumia mabavu kubaki madarakani na yeye akashirikiana nao kufanikisha hilo . Mwandishi mashuhuri
wa kimataifa, Jonathan Power, anaripoti:
“The
governing party [in Zanzibar ]
is part of the mainland’s goverining CCM, but, as [President] Mkapa says, there
are some militant people in my party. They don’t want to lose power even if it
means fiddling the vote.”
“Chama
kinachotawala [Zanzibar ] ni sehemu ya chama cha
CCM kinachotawala Bara, lakini kama anavyosema
[Rais] Mkapa, kuna wahafidhina katika chama changu. Hawako tayari kuachia
madaraka hata kama hiyo inamaanisha wizi wa
kura.”
Yaliyofuata
katika utekelezaji wa mpango huo yataingia katika historia ya Tanzania kama mojawapo ya matukio ya unyama
mkubwa kuwahi kufanywa na askari wazalendo dhidi ya wananchi wenzao kwa sababu
tu ya itikadi tofauti za kisiasa na kuwazuia wasitekeleze haki yao ya kidemokrasia na
kikatiba. Matukio hayo yenyewe ni matokeo ya kupuuzwa kwa njia ya mazungumzo na
makubaliano ya Muafaka ambayo awali Rais mstaafu Mkapa aliahidi mbele ya
Watanzania na ulimwengu kwamba atayasimamia kikamilifu.
Wakati
wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2005, niliandika makala katika gazeti la
Mwananchi Jumapili nikiwa na lengo la kuwaondolea mashaka wenzetu wa chama
kinachotawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa ujumla kuhusu mambo
kadhaa tunayotuhumiwa nayo. Kuhusu Muungano niliandika:
“…
Muungano ni nguzo moja nyengine ya nguvu na maslahi ya Zanzibar na ya Wazanzibari wenyewe. Wanaosema
kwamba CUF haitaki Muungano na kwamba itauvunja ni waongo. CUF, kama ilivyo CCM, ni chama chenye nguvu Visiwani na Bara.
Na kama CCM ina uwezo wa kutawala pande zote,
CUF ina uwezo huo mara mbili zaidi. Msimamo wetu ni kwamba kuna hitilafu na
kasoro mbali mbali katika Muungano lakini hizo tutazijadili kwa pamoja na
Serikali ya Muungano na naamini tutaweza kuzipatia ufumbuzi.”
Na
huo unabaki kuwa ndiyo msimamo wa CUF katika kutatua hizi zinazoitwa kero za
Muungano. Mazungumzo makini, ya kina na yenye kuambatana na nia njema kwa
wahusika wote ndiyo njia pekee ya matumaini katika kuyapatia ufumbuzi matatizo
yanayolikabili Taifa letu. Hakuna mbadala wa mazungumzo. Nje ya mazungumzo ni
fujo.
Lakini
wakati tunazungumzia namna ya kutatua matatizo haya kwa lengo la kuwa na
Muungano imara, ni vyema tuelewe kwamba tunahitaji kwanza kuhakikisha kuwa
tumetatua tatizo la mgogoro wa kisiasa Zanzibar
ambao unaendelea kumong’onyoa misingi ya umoja wa visiwa hivi na kuathiri
maendeleo yake. Tunahitaji kuwa na Zanzibar
imara isiyoyumba ili kuwa na Muungano imara usiyoyumba. Naomba nifikie
Hitimisho kwa kunukuu kutoka katika Utangulizi wa Manifesto ya Uchaguzi ya CUF,
pale tuliposema:
“Mtazamo
wetu ni kwamba Wazanzibari tutakuwa na nguvu na sauti licha ya udogo wetu ikiwa
tutakuwa na mfumo shirikishi badala ya tenganishi na kwamba tunaweza kuyafikia,
kwa umoja wetu, mengi ambayo hatukuweza kuyafikia kwa kugawanyika kwetu.”
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !