Jumatatu
Aprili 8, 2013
Kitaifa
Mkapa atema cheche; ataka viongozi wafuate misingi ya Nyerere
.
Na Phinias Bashaya, Mwananchi (email the author)
Posted Jumapili,Aprili7 2013 saa 20:58 PM
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa
kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo
yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa
kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo
yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.
Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa
Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni
kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.
“Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote
walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja na tofauti zetu za
kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia
wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii,” alisema Mkapa,
ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995-2005.
Mkapa alionya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara zote alisimamia umoja wa taifa.
“Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote
kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii,”
alisema.
Mkapa ambaye hakupanga kuongea lolote katika tukio hilo,
alitaka taifa lijenge utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya
cha uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.
Pia alitahadharisha kuwa zama hizi kumeibuka mitafaruku
mbalimbali na kuwakumbusha Watanzania kuwa ni wakati wa kumwabudu Mwenyezi
Mungu.
Mkapa alisema mara nyingi alishauriana na viongozi wa dini
katika masuala ya kijamii na kiroho na kumtaja askofu mpya wa Bukoba, Rwoma na
Mtangulizi wake aliyestaafu Nestory Timanywa kuwa alishirikiana nao katika
masuala ya wananchi. Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya
Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea Serikali yake haiongozi kwa misingi
ya ubaguzi.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alikwenda
mbali zaidi na kudai amekuwa akilalamikiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo
na yale ya Kiislamu.
Maneno ya Mkapa na Kikwete yamekuwa katika kipindi hiki taifa
likiwa limetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini. Matukio
makubwa yakiwa yale ya kuuawa wa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na Mchungaji
Mathayo Kachila wa Geita.
Pia kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa
tindikali kwa Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja huko Geita na
Tunduma.
Askofu Mpya wa Bukoba Rwoma alimshukuru Mkapa kwa kuzungumzia
umuhimu wa amani ya nchi, huku akisisitiza suala la upendo miongoni mwa
wananchi.
Wakati
huohuo, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye jana alitaja vyanzo vya vurugu
zinazoendelea nchini kuwa unatokana na tofauti kubwa kati ya walionacho na
wasionacho.
Alitoa
kauli hiyo jana wakati akizindua santuri ya nyimbo za dini kwa Kwaya ya Mt
Joseph, Mfanyakazi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Sumaye
alionya kuwa kama hali ya utajiri kwa baadhi ya watu itaachwa na kuendelea
hivyo, ni wazi kuwa nchi haitatawalika kwa amani.
“Binadamu mwenye njaa na
aliyekata tamaa kamwe hawezi kutawalika kwani kila wakati anahisi kutengwa na
kundi jingine,” alisisitiza Sumaye. {Mtanzania}.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !