Kwa Nini
Waislamu Wanalalamika?
MWANDISHI: MAALIMU
ALLY BASSALEH P.O.BOX 15653, DAR ES SALAAM, TANZANIA. MHARIRI NA MSAMBAZAJI:
BARAZA KUU NA TAASISI ZA KIISLAMU, TANZANIA S.L.P 9701 TEL : 760228/170664
Siti bint Saad
aliimba:
Siri sifunue kwa wino wa rangi fahamu ujue kuna mambo mengi wajila mwenyewe kwa ujinga mwingi
Alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho huko Dodoma Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Mheshimiwa William Benjamin Mkapa Alikemea wale wote wanaotaka kuligawa taifa hili kwa misingi ya kidini. Kwa kweli hakuna sumu mbaya zaidi inayoweza kuleta uhasama, mgawanyiko na hata umwagaji damu katika jamii kama udini. Katika taifa kama la Tanzania, ambalo wananchi wake ni mchaganyiko wa dini mbali mbali pamoja na wale wasiokuwa na dini ni hatari kupalilia au kushabikia udini. Serikali inatakiwa iwe makini sana kuona kuwa raia hawabaguliwi kwa misingi ya dini zao. Natumai hilo ndilo lililomsukuma Mheshimiwa Rais katika mkutano huo mkuu maalumu wa CCM kule Dodoma kuonya kuwa atatumia uwezo na nguvu zake zote kuzika mgawanyiko wa kijamii kwa misingi ya kidini. Kauli hiyo ya Mheshimiwa Rais siyo kwamba inahitaji kupongezwa tu bali inabidi iungwe mkono na kila yule anayeitakia heri Tanzania. Hakuna haja ya kutaka kujidanganya. Hivi sasa Tanzania tayari zimekwishajengeka hisia za udini, basi kama kweli Mheshimiwa Rais ana nia ya kulishughulikia jambo hilo kwa dhati inabidi kwanza aangalie kwa makini nini chanzo cha jambo hilo? Kutaka kulishughulikia jambo kubwa kama hili lenye kugusia imani za wengi, na haki za msingi za raia, bila ya kulifanyia uchunguzi wa kina ni sawa na kutumia jazba katika kutoa maamuzi makubwa. Kitendo kama hicho kinaweza kuleta madhara makubwa zaidi kuliko hata ile faida inayokusudiwa kupatikana.
Siri sifunue kwa wino wa rangi fahamu ujue kuna mambo mengi wajila mwenyewe kwa ujinga mwingi
Alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho huko Dodoma Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Mheshimiwa William Benjamin Mkapa Alikemea wale wote wanaotaka kuligawa taifa hili kwa misingi ya kidini. Kwa kweli hakuna sumu mbaya zaidi inayoweza kuleta uhasama, mgawanyiko na hata umwagaji damu katika jamii kama udini. Katika taifa kama la Tanzania, ambalo wananchi wake ni mchaganyiko wa dini mbali mbali pamoja na wale wasiokuwa na dini ni hatari kupalilia au kushabikia udini. Serikali inatakiwa iwe makini sana kuona kuwa raia hawabaguliwi kwa misingi ya dini zao. Natumai hilo ndilo lililomsukuma Mheshimiwa Rais katika mkutano huo mkuu maalumu wa CCM kule Dodoma kuonya kuwa atatumia uwezo na nguvu zake zote kuzika mgawanyiko wa kijamii kwa misingi ya kidini. Kauli hiyo ya Mheshimiwa Rais siyo kwamba inahitaji kupongezwa tu bali inabidi iungwe mkono na kila yule anayeitakia heri Tanzania. Hakuna haja ya kutaka kujidanganya. Hivi sasa Tanzania tayari zimekwishajengeka hisia za udini, basi kama kweli Mheshimiwa Rais ana nia ya kulishughulikia jambo hilo kwa dhati inabidi kwanza aangalie kwa makini nini chanzo cha jambo hilo? Kutaka kulishughulikia jambo kubwa kama hili lenye kugusia imani za wengi, na haki za msingi za raia, bila ya kulifanyia uchunguzi wa kina ni sawa na kutumia jazba katika kutoa maamuzi makubwa. Kitendo kama hicho kinaweza kuleta madhara makubwa zaidi kuliko hata ile faida inayokusudiwa kupatikana.
Mara unapotajwa udini
humu nchini, walengwa huwa ni Waislamu. Wao ndio wanaoshutumiwa kwa kutaka
kupandikiza mbegu ya udini na kuhatarisha kuvuruga amani nchini, iliyoletwa na
chama tawala na serikali yake chini ya uongozi wa mwasisi wa Taifa hili, Hayati
Julius Kambarage Nyerere.
Mkongwe mmoja wa
kisiasa humu nchini, na ambaye ni kada mkubwa wa CCM, Mheshimiwa Kingunge
Ngombale Mwiru, hivi juzi, katika ule mkutano mkuu maalumu wa CCM, Dodoma,
alisema kuwa pasipokuwa na haki hakuna amani. Hiyo ni kweli isiyopingika.
Huwezi kutegemea kuwepo na amani ya kweli pale penye dhuluma na ubaguzi.
Katika kujaribu
kuchunguza kwa nini waislamu waonekane ni wakorofi na wenye kutaka kupanda
mbegu za udini, nimegundua kuwa waislamu wanahisi kuwa hawatendewi haki na
Serikali iliyopo madarakani na kwamba wanabaguliwa kwa sababu tu ya dini yao.
Nimebaini kuwa kuna mambo sita ambayo, kwa namna moja au nyingine, ndiyo
yaliyowachochea waislamu wajitokeze hadharani na kuishitumu Serikali kwa
kuendeleza bbbudini.
Jambo la kwanza ni
kitabu cha Dkt. JOHN C. Sivalon, kinachoelezea mafungamano ya siri baina ya
kanisa katoliki na serkali, dhidi ya uislamu na kwa faida ya kanisa hilo. Jambo
la pili, ni kitabu cha Al-Hajj Aboud Jumbe Mwinyi kilichokuja kuwathibitishia
waislamu kuwapo kwa udini huo. Tatu, ushahidi wakimazingira unathibitisha kuwa
wakristo wengi ndio, siku zote, wanaopata fursa za kupata elimu ya juu, pamoja
na kushika madaraka katika ofisi za Serikali na mashirika ya umma. Na jambo la
mwisho, ni uhuru wa kusema, uliotokana na mageuzi, yaliyoondoa ukiritimba wa
chama kimoja na kuleta demokrasia ya vyama vingi, ndio uliowapelekea waislamu
wajitokeze kuelezea kero walizo nazo na kutetea haki zao hadharani.
Kitabu hiki
kimekusudiwa kuiondoa ile dhana potofu inayoenezwa kuwa eti waislamu ni
wakorofi, wanachanganya dini na siasa, kwa lengo la kuvuruga amani nchini, na
kumbe wakorogaji wakubwa wa dini na siasa katika nchi hii ni kanisa katoliki
kwa kushirikiana na Serikali, kama lnavyodhihirishwa hilo na Dkt. John C.
Sivalon, katika kitabu chake hicho. Pili, tumekusudia kuyaweka bayana yake
aliyoyaeleza Dr. Sivalon katika kitabu chake juu ya jinsi kanisa katoliki kwa
kushirikiana na Serikali, lilivyoandaa hila za siri zilizolipa mwanya kanisa
hilo kuelekeza siasa Tanzania na hapo hapo kuudhibiti uislamu na waislamu.
Kwa kuwa sera ya
Serikali yetu ya awamu ya tatu ni UKWELI NA UWAZI, tunataka viongozi wa Serikali
na watanzania kwa jumla, kabla hawajaamua kuwalaumu na kushutumu waislamu.
Waislamu wakisome kijitabu hiki kwa makini, wazingatie yaliyoandikwa humo,
kisha waamue jee, upo udini nchini ulioanzishwa na kanisa katoliki pamoja na
serkali ya awamu ya kwanza, chini ya uongozi na Mwalimu Nyerere au haupo? Jee,
waislamu wana haki yakulalamika na kudai haki zao au hawana ? Na kama upo udini
huo dhidi ya waislamu Serikali inakusudia kuchukua hatua gani za makusudi
kuondoa hali hiyo?
Kulifumbia macho tatizo
hilo si dawa hata didogo. Tusisahau ule usemi wa hekima wa kiswahili unaosema
"Mdharau mwiba Mguu huota tende!" Kwa nini basi tungojee mpaka mguu
uote tende? Huenda mkaona kuwa mtindo wa kitabu hiki ni kinyume kabisa na ule
mtindo ya vitabu vingine mlivyovizoea kuvisoma, kwa kawaida, katika vitabu
vyote, maelezo ya mwandishi huwa ndio yanayotawala kitabu kizima lakini, katika
kitabu hiki, maelezo ya mwandishi ni machache sana. Mwandishi amechangia kutoa
maswali tu, majawabu ya maswali hayo ni maelezo ya Padre wa kikatoliki,
yaliyomo katika kitabu chake alichokiita "KANISA KATOLIKI NA SIASA YA
TANZANIA - 1953 HADI 1985". Imefanywa hivyo, makusudi, ili isije ikasemwa,
labda mwandishi wa kitabu hiki, ameandika uzushi, au ametia chumvi katika
maneno yake.
MALALAMIKO YA
WAISLAMU
Katika miaka ya
karibuni, waislamu hapa nchini, wamekuwa wakisikika wanalalamika kuwa Serikali
imekuwa haiwatendei haki. Wananchi kuwa wamekuwa wakipunjwa katika kupata
elimu, hasa ile ya sekondari na Chuo Kikuu. Aidha, wamekuwa wakinyimwa nafasi
za uongozi serikalini na katika mashirika ya umma. Na pale wanapotokezea
viongozi wa kiislamu kukemea dhuluma wanazofanyika au kutetea haki zao,
hupachikwa kila aina ya majina, siasa kali, mujahidina, wakorofi, wachochezi na
wachanganya dini na siasa na hutumiwa vyombo vya dola kuwadhibiti.
Katika Baraza la Idd
-el - fitr la mwaka jana, halmashauri ya waislamu, iliyokuwa ikiwakilisha
madhehebu na taasisi mbali mbali za kiislamu, ilimkabidhi Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa William Benjamini Mkapa, risala iliyoorodhesha
kero zote za Waislam. Mheshimiwa Mkapa alipokea risala hiyo, kwa mikono miwili,
na akaahidi kuwa atayafanyia uchunguzi wa kisayansi malalamiko hayo ya waislam
ili apate kuelewa kama ni ya kweli au ni ya uongo. Aliahidi kuwa atashauriana
na Baraza lake la mawaziri juu ya jambo hilo, na pale uchunguzi utapothibitisha
kuwepo kasoro zozote atafanya jitihada za kuziondoa kasoro hizo. Waislam
wakafurahika sana, na wakaingiwa na matumaini makubwa
WAISLAMU WAPUUZWA
Jambo la kwanza
lililowavunja moyo na kuwakatisha tamaa waislam, sio ule ukimya mkubwa tu wa
Mheshimiwa Rais kutoshughulikia kero hizo bali kushindwa hata kuwaeleza
waislamu juu ya matokeo ya uchunguzi wake. Na hata alipoandikiwa barua ya
kumbukumbu na Dkt. Saleh Al-Miskry, aliyekuwa katibu mkuu wa muda wa
halmashauri hiyo ya waislamu, na pia katibu mkuu wa Dar es salaam Islamic club,
jawabu aliyojibiwa na Mheshimiwa Rais haikuwa maridhawa. Jawabu hiyo badala ya
kuwapa waislamu matumaini ilizidi kuwakatisha tamaa. Kwa mfano, akijibu kwa
nini Serikali ina uhusiano wa kibalozi na Vatikano, Makao makuu ya kanisa
katoliki duniani, na ikakataa kujiunga na OIC.Alisema yeye akiwa ni Rais wa
wanywa pombe na wasiokunywa pombe, wala nguruwe na wasiokula nguruwe, hawezi
kuwasikiliza waislamu na akapuuzia maoni ya wasiokuwa waislamu. Waislamu
wamechukizwa sana na jawabu hiyo na wameichukulia kama ni dharau kwao.
Wameitafsiri kauli hiyo ya Mheshimiwa Rais kuwa Serikali ipo tayari kuyapa
kipaumbele maoni yanayotolewa na viongozi wa kanisa, lakini haipo tayari
kuyasikiliza madai ya waislamu.
Kuhusu kadhia ya
mwembechai waislamu walijibiwa kuwa hakuna haja ya kufanya uchunguzi. Katika
ghasia za mwembechai si chini ya waislamu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na
Polisi. Kwa mujibu wa sheria, kifo chochote kinachotokana na polisi au magereza
hubidi kifanyiwe uchunguzi maalumu wa kisheria unaoitwa "INQUEST" kwa
lugha ya kitaalamu. Waislamu wameomba mahakamani kufungua "INQUEST"
hiyo, lakini kwa muda wa miaka miwili wamekuwa wakizungushwa zungushwa, ingawa
wakati naendelea kuandika maelezo haya, nimepata habari za kuaminika, kuwa
mahakama ya Hakimu Mkaazi ya Kisutu, imekubali lile ombi la waislamu kufungua
"INQUEST" katika mahakama hiyo. Lakini swali la kujiuliza ni kwa nini
ichukue muda wote huo?.
Ingawa katika jawabu
yake, Mheshimiwa Rais Mkapa, amekataa kuwapo kwa mpango wowote wa makusudi wa
Serikali wa kuwabagua waislamu kwa ajili a dini yao, lakini waislamu kwa mujibu
wa hali ya mazingira wanashindwa kukubaliana na Mheshimiwa Rais kwa hilo.
Mheshimiwa Mkapa amekiri kutokuwapo uwiano baina ya wanafunzi wa kiislamu na
wale wa kikristo katika shule za sekondari na vyuo vikuu na pia kuwapo idadi
ndogo ya waislamu katika nafasi za uongozi, katika mawizara na ofisi za
serikali, lakini alisema tofauti hizo hazitokani na mkakati wowote wa
kiserikali ulioandaliwa makusudi kuwabagua waislamu. Amedai hali hiyo imetokana
na sababu za kihistoria. Lakini waislmu wanahisi kuna mkono wa mtu
unaosababisha hayo
KWA NINI WAISLAMU
WANAONEKANA WAKOROFI?
Kama tulivyotangulia
kusema kila wanapochomoza viongozi wa kiislamu kuelezea kasoro zilizopo,
kukemea dhuluma dhidi ya waislmu, na kutetea haki zao, basi huonekana ni
wakorofi wakaambiwa wanachanganya dini na siasa. Huandamwa na vyombo vya dola
kwa madai kwamba wanataka kuhatarisha amani. Kuna wanaodai kuwa hakuna udini
hapa nchini. Na kuna wanaodai kuwa kuna vyama vya siasa humu nchini
vinavyochochea hali hiyo, kwa lengo hilo hilo la kuchafua amani. Kauli za aina
hii ni kauli za jazba. Zinachukuliwa kijuu juu tu, hazilengi katika kutafuta
ufumbuzi wa matatizo, zinalenga katika kuuhadaa umma na kuficha ukweli. Wengi
wa wale wanaodai kuwa hakuna udini na wakawaita waislamu wanaodai haki zao ni
wakorofi ni wale wanaofaidika na mfumo huu uliopo au ni wale wanaojipendekeza
kwa maslahi yao binafsi.
Katika uchunguzi
nilioufanya juu ya jambo hili nimegundua kuwa kuna sababu nne kuu
zilizowapelekea waislamu wajenge hisia za kuwapo udini hapa nchini, na pia
wajitokeze kulalamika na kudai haki zao. 1. KITABU CHA DR. JOHN C. SIVALON
Kwanza, kitabu kilichoandikwa na Dr. John C. Sivalon, alichokiita "KANISA
KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA - 1953 HADI 1985" kimekuja kuwafunua
macho waislam na kuwahakikishia kuwa zile hisia za udini ndani ya serikari,
dhidi ya uislamu, ni zakweli Kitabu hicho kimedhihirisha wazi wazi kuwa kanisa
katoliki, Tanzania chini ya uangalizi wa Vatikano, katika kipindi chote cha
utawala wa awamu ya kwanza, chini ya uongozi wa Mwalimu Julias Kambarage
Nyerere, lilikuwa likichanganya dini na siasa, limekuwa likishirikiana na
Serikari katika kulipendelea kanisa hilo na kuudhibiti uislamu waislamu na
waislumu kwa jumla.
2. KITABU CHA AL-HAJJ
ABOUD JUMBE MWINYI Pili, Kitabu kilichoandikwa na Al-Hajj Aboud Jumbe Mwinyi
alichokiita "THE PARTNERSHIP" (Muungano wa Tanganyika na zanzibar
Miaka 30 ya dhuruba") nacho kimechangia, kwa kiwango kikubwa kuwafanya
waislamu waamini kuwa kweli wanabaguliwa. Katika kitabu hicho, cha Al - Hajji
Jumbe kilichoandikwa kwa lugha ya kiingereza na kufasiriwa kwa lugha ya kiswahili
na Ali Saleh kinaelezea na kutoa ushahidi kuwa, waislamu wa Tanzania Bara
wamekuwa na uonevu ulioendelezwa na kukoseshwa haki zao za msingi pamoja na
kuwa katiba ya 1977 ilikuwa na vipengele vya kuhakikisha haki za binadamu na
usawa kwa raia wote.
Ushahidi wa ziada
unaonesha kuwa kanisa nchini Tanzania ndilo linatoa maelekezo ya kisiasa, na
mfumo wa kisiasa umekuwa ukifumwa kutoa upendeleo kwa wakristo, ambao tayari
wamo katika kudhibiti nafasi mbali mbali katika taasisi za umma. (Sivalon,
1992)" uk - 125. Shutuma hizi dhidi ya Serikali na chama tawala, kutolewa
na mtu kama Al -Hajji Jumbe ambaye kwa nyakati tofauti amewahi kushika nafasi
mbali mbali za uongozi katika chama tawala na Serikali yenyewe, na ni mtu
aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama tawala na pia Makamu wa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, zimewapelekea waislamu wengi, waamini kuwapo
ubaguzi wa makusudi dhidi yao.
Kwa jinsi Al Hajji
Jumbe anavyoelewa maana ya dhamana, mtu aliyekuwa kiongozi wa ngazi ya juu
katika chama tawala na Serikali yake haiwezekani kabisa akurupuke na kuandika
maneno, ambayo ni ya uongo, ambapo yanaweza kuchochea uhasama mkubwa nchini
baina ya raia wenyewe kwa wenyewe, na pia baina ya raia na serikali yao. Huyu
ni mtu mwenye kujua alichokuwa akikiandika na matokeo ya hicho alichokiandika,
Kwa huyo hathubutu kuandika maneno ya uzushi lazima kile alichokandik kiwe na
namna ya ukweli ndani yake.
3. USHAHIDI WA
KIMAZINGIRA
Tatu, ushahidi wa
kimazingira unathibitisha madai hayo ya waislamu. Kwa mfano, Al-Hajji Jumbe,
katika kitabu chake hicho nilichokitaja, ametoa jadweli ifuatavyo, kuonesha
uwiano wa wanafunzi wa kiislamu na wa kikiristo kwa shule za sekondari na kwa
chuo kikuu cha Dar es salaam, baina ya mwaka 1971 hadi 1984. IDADI YA WANAFUNZI
KIDATO CHA I MWAKA WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1978 28% 77% 1:3 1979 22% 78% 1:3
1980 23% 77% 1:3 1981 25% 75% 1:3 Uk. 132 IDADI YA WANAFUNZI KIDATO V MWAKA
WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1978 12% 88% 1:7 1979 13% 87% 1:6 1980 13% 87% 1:6
1981 12% 88% 1:7 Uk. 132 IDADI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU DAR ES SALAAM MWAKA
WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1971-72 13% 86% 1:6.6 1972-73 14% 84% 1:6.0 1973-74
13% 87% 1:6.6 1984-85 15% 85% 1:5.7 1986-87 16% 84% 1:5.7 1987-88 18% 82% 1:4.5
1988-89 18% 82% 1:4.5 Uk. 133
Kutokana na jedwali
hiyo, inaonesha uwiano baina ya wanafunzi wa kiislamu na wenzao wakristo katika
elimu ya sekondari, ni kwa kila mwanafunzi wa kiislamu mmoja anayepata nafasi
ya kuingia shule ya sekondari, basi idadi ya wanafunzi wa kikiristo ni kama
ilivyojitokeza kuwa, mwanafunzi mmoja kwa kila wanafunzi watano. Na anapata
nafasi katika chuo kikuu, mambo huwa ni mabaya zaidi, kwa kila mwanafunzi mmoja
wa kislamu anayeingia chuo kikuu, huingia wanafunzi watano mpaka saba wa
kikristo.
Kuhusu mgawanyiko wa
madaraka katika vyombo vya Serikali Al-Hajji Jumbe ametoa takwimu zifuatazo:
Mwaka CHEO WAISLAMU WAKIRISTO UWIANO 1993 Makatibu Waku 4 16 1:4 Wakuu wa Mikoa
5 15 1:3 Wakuu wa Wilaya 8 113 1:14 Uk. 136 Kwa mujibu wa takwimu hizi tutaona
kuwa kati ya wakuu wa Wilaya 121 wanane tu ndio waislamu, na 113 ni wakiristo.
Pia Makatibu wakuu wa Mawizara walio waislamu ni wachache, kwa vile cheo hicho
kinataka wasomi wenye shahada za vyuo vikuu na waislamu wenye shahada kama hizo
ni wachache, vipi basi na nafasi za wakuu wa Wilaya zishikwe, takriban na
wakristo watupu. Jee Hakuna waislamu wenye sifa ya kushika nafasi hizo? Au ukuu
wa Wilaya nao uanahitaji shahada za Chuo Kikuu?
Al-Hajji Jumbe, katika
kitabu chake, anaeleza, "Picha inayooneshwa na taarifa za takwimu hizi ni
kuwa waislamu, pamoja na kuonyeshwa kuwa kuna vifungu vya katiba vyenye kulinda
haki hizo basi bado wao wananyimwa haki za usawa na za kutosha." Uk 138.
Al-Hajji Jumbe ameendelea kusema, "Serikali iliyo madarakani lazima
ikubali jukumu la vitendo vya kuvunja haki za kikatiba dhidi ya waislamu wa
nchi hii.
Hakuna Serikali yoyote
ambayo inajali maslahi ya taifa, inayoweza kupuuza madai ya ukweli ya raia
wake. Hali ya kutochukua hatua kwa upande wa CCM na serikali yake,
kumesababisha utamaduni wa ukiukaji wa katiba na mengi ya matendo hayo yakiwa
dhidi ya uislam". Uk 138. Mwisho Al-Hajji Jumbe anahitimisha maelezo yake
kwa kusema kwa hivyo naona ingekuwa bora tungelitazama swala la dini na siasa
kwa hivyo tuweze kuipima hali hiyo. Jee Tanzania ni nchi ya kiislam, kikristo
au haina dini? na siasa gani ambayo imetuburura na kutuingiza katika hali
ambayo jamii moja iliyo kubwa ndani ya nchi yetu imedharauliwa na kushushwa
kuwa daraja la pili?
Uk 138 Na ipo mifano
mingine mingi ya ushahidi wa kimazingira, lakini michache itakidhi kuonyesha
dhuluma walizofanyiwa Waislamu na Serikali ya Tanzania. Mfano wa kwanza ni
kuvunjwa kwa Jumuiya ya Waislamu ya Afrika Mashariki (East African Muslim
Welfare Society) mwaka 1968. Jumuiya hii ilifanya mambo mengi ya maendeleo kwa
Waislamu wa Afrika Mashariki katika kipindi cha miaka 30 ya uhai wake. Wakati
ilipokuwa ikivunjwa mwaka 1968, tayari ilikuwa imefanikiwa kujenga jumla ya
shule 175 (70 kati ya hizo zilijengwa Tanzania), misikiti 149 (53 Tanzania),
shule za ufundi tatu na hostel moja. Kadhalika iliunda mfuko wa maendeleo
uliokuwa na akiba ya shs 660 milioni za Tanzania. Vyote vilivyokuwa Tanzania
vilitaifishwa. Na hujuma kubwa zaidi ya yote ni kuuwa ule mpango kabambe wa
kujenga Chuo Kikuu mjini Dar es Salaam kwa watoto wa Afrika Mashariki. Nchi
kama Misri, Jordan na nyingine za Kiislamu zilichangia katika mfuko wa ujenzi
wa chuo hicho.
Kiwanja kilichopangwa
kujengwa chuo hicho hivi sasa kimegeuzwa shamba la kulimia mchicha. Kadhalika
Jumuiya hiyo ilitenga viwanja karibu katika kila mkoa kwa ajili ya maendeleo ya
Waislamu. Mkakati wa kuivunja Jumuiya hiyo ulilenga kuwadumaza waislamu na
uislamu baada ya serikali ya mwalimu Nyerere kuishutumu jumuiya hiyo eti
ilikuwa ikichanganya dini na siasa. Mfano wa Pili, ni Makubaliano ya Maelewano
ya 1992 kati ya Serikali na umoja wa Mabaraza ya Makanisa nchini (Christian
/Council of Tanzania na umoja Tanzania Episcopal Conference). Katika muafaka
huo, Serikali ya Tanzania ilikubali kuwarejeshea wakristo shule za sekondari na
hospitali zilizotaifishwa mwaka 1970, na pia kuahidi kutozitaifisha tena shule
na hospitali hizo au zile zitakazojengwa na makanisa hapo baadaye.
Aidha, Serikali
itajitahidi kutafuta fedha na misaada kutoka kwa wahisani wa nje, na hasa
Serikali ya Ujerumani, kwa ajili ya kuendeleza huduma za kijamii zinazotolewa
na kanisa. Chini ya muafaka huo Serikali ilipaswa kutenga nafasi maalumu katika
vyuo vyake vya ualimu kwa ajili ya waalimu wa makanisa kwenda kusomea ualimu
kwa lengo la kuimarisha ubora wa shule za Kikristo. Waislamu walifichwa muafaka
huo ili makubaliano hayo kati ya serikali na makanisa yabakie kuwa siri. Lakini
hata baada ya kuyagundua, waislamu walinyimwa fursa kama hizo licha ya BARAZA
KUU la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (BARAZA KUU) kudai kwa muda
mrefu bila ya mafanikio.
Mkataba huo
haukuwatendea haki waislamu wa nchi hii. Katika taifa, suala la elimu ni muhimu
na nyeti kwa sababu linahusu malezi ya kizazi cha kesho cha taifa hilo. Maamuzi
mazito na makubwa kama haya yaliyofanywa na serikali yetu yalibidi yaafikiwe
kwa kufuata taratibu zinazokubalika. Utaratibu uliofuatwa na Serikali ya
Tanzania ulikuwa ni wa kutatanisha. Serikali iliridhia mkataba huo hata kabla
ya Bunge kujadili suala hilo.
Chini ya mkataba huo wa
tarehe 21/2/92, Serikali ilikubali kuzibinafsisha (de-nationalize) shule na
hospitali kwa makanisa. Kifungu kimoja cha mkataba huo kinaeleza : "The
government shall not nationalize schools hospitals, or any education or heath
institutions owned by the Churches". Tafsri: "Serikali haitataifisha
shule hospitali, au taasisi yoyote ya elimu au afya inayomilikiwa na
makanisa." (Tazama : Part Four, Obligations, Article XLL). Jambo la pili,
ni marekebisho ya Sharia ya Elimu Na : 25 yaliyofanywa na Serikali kuyawezesha
makanisa kupewa shule zilizokuwa mali ya taifa. Waislamu walinyimwa fursa kama
hiyo waliyopewa wenzao wa kikristo, licha ya waislamu kuendelea kudai kwa
mwongo mzima sasa.
Kinyume chake, Serikali
inaendelea kumiliki shule za waislamu zilizotaifishwa mwaka 1970. Baya zaidi ni
kuwa Serikali siyo tu iliamua kuyadharau malalamiko ya waislamu, bali pia
kupuuza kujibu barua ilizopelekewa na BARAZA KUU juu ya suala hilo. Kikao cha
Bunge kilichofuata cha Aprili 1992 kilifuta ibara ya 30 ya Sheria ya Elimu Na
25 ya mwaka 1978 iliyohalalisha makanisa kurudishiwa shule hizo. chini ya
Makubaliano, sera zote za elimu na afya katika shule na hospitali za makanisa
zingebuniwa na Kamisheni ya huduma ya kikristo, kwani kifungu kimoja cha
mkataba huo kinaeleza: "There shall be established a governing body to be
known as the Christian Social Services Commission (hereinafter refferd to as
the "Commission") whose primary functions shal be: (a) to make
policies in all matters related to Education and Health services provided by
the Churches" Tafsiri: Itaanzishwa bodi ya uendeshaji itakayojulikana kama
"Kamisheni yakikristo ya Huduma za jamii (ambayo hapa itajulikana kama
Kamisheni) ambayo kazi zake za msingi zitakuwa: (a) Kuandaaa sera juu ya mambo
yote yanayohusiana na huduma za Elimu na Afya zinazotolewa na makanisa."
(One, Institutions Article1(a). Serikali iliamua kuzirejesha kwa makanisa
baadhi ya shule ambazo ni za serikali bila ya kuwataka ushauri waislamu na
watanzania wengine ambao si wakristo.Serikali ilifanya hivyo huku ikijua kuwa
kuna watoto ambao si wakristo waliokuwa wakisoma katika shule hizo. Serikali
pia ilifanya hivyo huku ikijua kuwa imekabidhi kwa wakristo mamlaka ya kubuni
sera zote za elimu katika shule hizo. Kwa kufanya hivyo ni dhahiri kuwa
Serikali haikuona kama kulikuwa na haja au umuhimu wowote wa kuwahusisha
wasiokuwa wakristo katika suala la elimu.
Aidha, kwa kufanya
hivyo Serikali iliona ni vizuri, kwa maslahi ya taifa, kama ingejivua jukumu la
kubuni sera za elimu na badala yake makanisa yakafanya kazi hiyo kwa niaba ya
raia wote. Katika waraka wake wa April 1992 kwenda Serekalini, Baraza kuu
lilitahadharisha kuwa serilai haikuwatendea haki waislaum wa nchi hii kwani
zaidi ya miaka 20 sera za Serkali zilikuwa zikinadi na kujigamba juu ya kutetea
na kulinda maslaha ya raia wote. Ikiwa katika shule zote za sekondari za
serikali idadi yaWaislamu imekuwa chini ya asilimia 20, itakuwaje hatima ya
waislamu katika shule za makansa, shule ambazo wakristo ndiyo wanaopanga sera
zote? Uingereza ni nchi iliyoelendelea na ni ya Kikristo. Lakini hata huko,
serikali inaheshimu hisia za watu wa dini nyingine.
Sheria ya Elimu ya
Uingereza ya mwaka 1944, ambayo inaendelea kutumika hadi leo inatamka wazi kuwa
watoto waelimishwe kulingana na matakwa na ridhaa ya wazazi wao. Kwanini basi
serikali ya Tanzania ikaingia mkataba ambao utakuwa na madhara makubwa kwa
watoto wa Waislamu? Wakati shule zilipokuwa zikitaifishwa mwaka 1970, lengo
lilikuwa kuifanya elimu ya taifa kuwa ni nyezo muhimu sana ya kulishikamisha
taifa lenye watu wa makabila na dini mbali mbali. Ikiwa mwelekeo mpya wa taifa
ni kwa Serikali kujitoa katika suala la elimu, Serikali ilipaswa kuutangaza
mwelekeo huo mpya ili kupata maoni ya wananchi wake kama ilivyokuwa mwaka 1970.
Lakini badala yake, Serikali ikaamua kuwaacha waislamu gizani juu ya zile fikra
za mwaka 1970 za kujenga mshikamano wa kitaifa.
Ikaamua pia kujifanya
bubu ilipoulizwa juu ya fedha za umma zilizotumika kukarabati na kuziendeleza
shule za hospitali hizo kwa kipindi cha miaka 22 au juu ya fedha zilizochangwa
na wasiokuwa wakristo kuwafidia waliokuwa wamiliki ya shule na hospitali hizo
hapo awali. (Tazama Ibara ya 30 (3) ya sheria ya elimu Na 25 ya 1978) Aidha
Serikali ilikubali kutenda kasma maalum ya fedha kutoka kwa wahisani kwa ajili
ya maendeleo ya shule hizo na ikakataa kusema chochote kama ilikuwa na mpango
mbadala wa kuendeleza elimu ya raia wengine ambao si wakristo. Mwelekeo huo wa
Serikali haukuwa na ishara wala nia njema kwa waislamu wa nchi hii. Kweli
waislamu wa nchi hii wanasubira kubwa!!
4. MAGEUZI
Mageuzi ya kisiasa,
yaliyoondoa ukiritimba wa chama kimoja na kuleta mfumo wa vyama vingi, kwa njia
moja au nyengine, yamechangia sana kuleta demorasia, kwa kiwango fulani,
iliyosaidia kuwapo uhuru wa kusema na mtu kutoa mawazo yake kwa njia ya vyombo
vya habari, ndiyo yaliyowapelekea waislamu wajitokeze hadharani na kutoa
malalamiko yao dhidi ya Serikali iliyopo madarakani. Katika utawala wa awamu ya
kwanza, hata kama waislam walikuwa wakihisi wanabaguliwa, basi walikuwa
wakinung’unika kichini chini, hawakuthubutu kulalamika waziwazi, walipojaribu
kufanya hivyo, walipambana na rungu la dola. Wengine miongoni mwao walitiwa
magerezani na wengine walihamishwa kutoka eneo moja la nchi hii na kupeleka
katika eneo jingine na kuwekewa vizuizi wasitoke katika eneo hilo.
KUCHANGANYA DINI NA
SIASA
Serikali inawasakama
bure waislamu ya kuwa wanachanganya dini na siasa, wakati ushahidi kutoka
katika kitabu cha Dr. Sivalon unadhihirisha wazi wazi kuwa tokea kuasisiwa kwa
Jamhuri ya Tanganyika na kisha muungano wa Tanzania, kanisa katoliki kwa
ushirikiano wa kichini chini na Serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa
Hayati Mwalimu Nyerere, limekuwa likikoroga hasa, dini na siasa na siyo
kuchanganya tu
Aidha, na Serikali
yenyewe imekuwa, siku zote, ikichanganya siasa na dini kwa kulipendelea zaidi
kanisa katoliki na hata mara nyingine kuliachia liingilie maamuzi ya Serikali
kama kitabu cha Dkt. Sivalon kinavyothibitisha hayo. Kitendo cha kanisa
katoliki serikali na chama tawala kunyamazia kimya na kutokanusha maelezo
aliyoyatoa Dr. Sivolon katika kitabu chake hicho ni sababu tosha inayoyafanya
yale yalioelezwa humo yaonekane kuwa ni ya kweli. Kuhusu kitabu hicho AL-Hajj Abuod
Jumbe anaeleza: "Upitizi wa makini wa kitabu cha Dr.John C.Sivalon
kiitwacho KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA, 1953 HADI 1985, unatoa
habari za ndani zisizo za kawaida juu ya kampeni dhidi ya uislam". Uk
-127. Al-Hajj Jumbe anaendelea kusema, "... kwa maneno mengine, kitabu
hicho, kwa kiasi fulani, ni kukiri kwa yeye mwenyewe mwandishi, juu ya shughuli
za kanisa la katoliki haliwezi kutenganishwa na Vaticano, na ambalo ubalozi
wake ni moja katika balozi kongwe nchini Tanzania. Kwa sababu zisizoeleweka
kitabu hicho kimeandikwa na kuchapishwa na waumini wa kanisa hilo. Yaliomo
ndani ya kitabu hicho hayajakanushwa na wala kubishiwa na serikari ya muungano
au ya Tanganyika au na CCM, huu ukiwa ni ushahidi kamili juu ya ukweli wa
kukiri juu ya neno hilo.
Kwa sababu na malengo
yo yote ya kutolewa kitabu hicho,na lazima ziwepo sababu za msingi za kufanya
hivyo kitabu hiki ni ufunuo mzuri juu ya mbinu za chini kwa chini za kanisa
katika medani ya kisiasa Tanzania". UK. 128 Akizidi kufahamisha yale yaliomo
ndani ya kitabu hicho cha Dr. Sivalon, AL- Hajj Jumbe anasema, "...
kinaeleza kwa vipi kanisa katoliki lilijenga njia ambazo ziliwawezesha kuwa na
mahusiano ambayo kitabu hicho kinaeleza yaliyokuwa ya karibu kabisa na TANU
wakati wa miaka ya kupigania uhuru. Kinaonesha kuwa wameshika karibu nafasi
zote muhimu katika serikali mpya ya kiafrika ya Tanganyika". UK.128
Akiendelea kuchambua yale yaliomo katika kitabu hicho, Al-Hajj Jumbe anaendelea
kueleza, "Kinaeleza ni vipi serekali ya Jamuhuri ya muungano ilirithi
mmfumo huo na kuupanua katika mamlaka ya Muungano, pia, katika mambo yahusuyo
Tanganyika". UK.128 ALL-Hajj Jumbe anaendelea, "Kwa wale viongozi,
wawe wa kanisa, CCM au serikali ya muungano, ambao walikuwa wakipigia kelele
kutenganishwa kwa siasa na dini, wana kazi ngumu ya kuelezea kwa umma kwa
ujumla lakini wao wenyewe wakiwa ndio waendelezaji wakubwa wa hilo, wana kazi
ngumu ya kuelezea kwa umma kwa ujumla lakini zaidi kwa waislamu.
Sivalon anaelezea juu
ya mpango na njama zinaendelea zikishirikisha kanisa katoliki, chama (TANU-
CCM) na serikili ya muungano." Uk. 128-129. Mwisho, Al- Hajj Jumbe
anasema, "Tangu njama hizo ziwekwe wazi 1992 hapakuwa na kauli moja ya
kupinga au kutolea maelezo juu ya jambo hilo. Huku ni kukiri kwa dhahiri juu ya
mipango na njama za kanisa zianazofanywa hali zikiwa zinaeleweka na mkono wa
chama na serekali zake". UK 129
WAJIBU WA SERIKALI
Waislamu wanalalamika.
Wanadai wanapunjwa katika elimu ya juu na nafasi za uongozi serikalini,
ushahidi wa kimazingira unathibitisha kuwa hakuna uwiano baina ya waislamu na
wenzao wakristo katika elimu na mgawanyo wa madaraka serikalini. Na kitabu cha
Dkt. John C. Sivalon kinadhihirisha kuwa kanisa katoliki limekuwa
likishirikiana na serikali katika kuwadhibiti waislamu na kulipendelea kanisa
hilo. Juu ya kwamba si serikali, chama, wala kanisa katoliki, halikukana
maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hicho cha Dkt. Sivalon, serikali inakataa
kukiri habari hizo za udini na wala haitaki kufanya uchunguzi wa kina katika
kuelawa ukweli ulivyo, badala yake, serikali imekuwa ikitoa vitisho kwa
waislamu pamoja na kutumia vyombo vya dola kuwadhibiti waislamu.
Mabavu yanaweza
kunyamazisha harakati za waislamu kudai haki zao kwa muda tu; lakini hayawezi
kuzizima harakati hizo kabisa. Ni wajibu wa serikali kuyachunguza kwa kina
malalamiko hayo ya waislamu pamoja na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Kutumia
mkong’oto hakusaidii kitu! katika huu mfumo wa vyama vyingi na upanuzi wa
demokrasia ni wajibu wa serikali kusikiliza matatizao ya raia wake ili kupata
ridhaa ya raia hao. Mwandishi na mwanafalsafa mashuhuri wa Tanzania marehemu
Shaban Robart aliandika katika moja ya vitabu vyake vingi alivyovitunga,
"Serikali iliyofaulu ulimwengu ni ile iliyotawala nyoyo za raia wake, raia
hao wataipenda Serikali kama hivyo na kushirikiana nayo, lakini ikitawala
viwiliwili vyao itabidi kusukumana nao". Basi ni vyema Serekali
ikijitahidi kutaka kutawala nyoyo za waislamu na siyo kutawala viwiliwili vyao.
SWALI LA KWANZA
SABABU YA WAISLAMU KULALAMIKA
Kwanini Waslamu wanalalamika?
Dkt John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : Lakini kwa upande mwingine
idadi kubwa ya wakristo wenye elimu walishindwa kushiriki wazi katika TANU
kwani aidha walikuwa waalimu au watumishi wa Serikali. Serikali ya wakoloni
walikataza kisheria kushiriki kwenye vyama vya siasa. Hata hivyo wakati wa
uhuru wengi kati ya wakristo hao wenye elimu na waliokuwa wakifanya kazi
Serikalini na walikuwa na nafasi nzuri zaidi kushika madaraka ya uongozi. Kwa
hali hiyo walionekana hasa na Waislamu kama watu waliofaidi matunda ya uhuru
bila kushiriki katika mapambano.
SWALI LA PILI
NYERERE "WAKALA" WA KANISA KATOLIKI?
Jee, Mwalimu Julias
Kambarage alikuwa ni ‘Wakala’ wa Kanisa Katoliki hapa Tanzania? Dkt. John
C.Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. Sura ya pili, inaonesha jinsi
uhusiano wa pekee ulivyojiimarisha na kukua kati ya viongozi wa chama na
Serikali wakati wa mapambano ya uhuru. Uhusiano huo ulitokana na mfumo wa mfumo
wa elimu katika kipindi cha Ukoloni, michango kadhaa ya Kanisa kwa kusaidia
TANU na vyama vya kitume kiungo cha pekee kati ya Chama na Kanisa Katoliki.
Uhusiano huo unaelezwa kwanza kama msingi wa kuelewa jinsi gani na kwa kiasi
gani viongozi wa Kanisa Katoliki walivyoingilia kati maendeleo ya siasa hapa
Tanzania. UK.5 2. "Nyerere ambaye mwenyewe ni mkatoliki, alikuwa na
uhusiano wa karibu sana na viongozi fulani wa kanisa na hivyo alionekana kuwa
ni kiungo kati ya Kanisa na Serikali". Uk.11 3. Mfano mzuri ni Marian
College Shule hii ilianzishwa mwaka 1957 na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC)
kwa lengo la kuwaelimisha wasichana. Ilikuwa ni shule ya pili yenye kidato cha
1V kwa wasichana hapa Tanzania. Ingawa shule hii ilijengwa na kanisa katoliki
na iliendeshwa na Masista wa Shirika la Marykonoll na wanawake Waafrika,
iligharimiwa kifedha na Kanisa. Mwalimu mkuu wa wakati ule wa 1957 alisema kuwa
ule ulikuwa wakati muhimu sana Tanzani.
TANU ilikuwa imepiga
hatua kubwa na ilikonekana dhahiri kwamba uhuru ungepatikana. Hivyo basi
masista walisisitiza kwa wanafunzi kwamba wao ndio watakaokuwa viongozi wa
baadaye. Nyerere mwenyewe alikuwa anaitembelea shule hiyo mara kwa mara
kuwaelezea nafasi yao baada ya uhuru kapatikana. Hivyo walimu na wanafunzi
walijua fika kwamba mabadiliko yalikuwa yanakuja na kwamba wangekuwa na mchango
wa kufanya. Ukichunguza kwa makini utaona kuwa idadi kubwa ya viongozi wa kike
wa chama na serikali ni wahitimu wa "Marian College". Katika orodha
ya wahitimu 224 wa mwaka 61 hadi 65, tukichukua baadhi yao kama mfano tunapata
matokeo yafuatayo :
Jedwali la tatu ;- Kazi
za jumla ya Wahitimu 22 wa Marian College: KAZI IDADI YA WENYE KAZI HIYO Walimu
Wakuu 3 Walimu wa Chuo Kikuu 2 Walimu wa Vyuo 1 Viongozi ngazi ya mikoa 3
Walimu 5 Viongozi ngazi ya Taifa 5 Daktari 1 Mwuguzi 1 Kiongozi, idara ya
Baraza la Maaskofu (TEC) 1 Vile vile mmoja wa hao 22 ni mke wa kiongozi katika
kamati kuu ya chama, mwingine ameolewa na afisa wa balozi Uk. 12- 13 4.
"Nilipokuwa nikimhoji kiongozi mwingine wa Serikali nyumbani kwake
nilipata kuona uhusiano uliopo kati ya wanawake hawa, walikuja wageni mara tatu
wakati wa mazungumzo yetu, kila mara alinitambulisha kuwa mgeni huyo naye ni
mmoja kati ya wahitimu wa "Marian College" kisha akanielezea kazi
yake. Mmoja alikuwa Katibu Muhtasi, mwingine Mwalimu Mkuu na wa tatu alikuwa
mfanyakazi wa shirika moja la Umoja wa Mataifa.
Wote hawa walikuwa ni
viongozi wa ngazi za juu Serikalini. Mahojiano haya yalithibitisha yaliyokuwa
yamesemwa na wengine kwamba hiki ni kikundi mashuhuri kanisani, chenye sauti
katika mwelekeo wa kisiasa na pia chenye uhusiano wa karibu sana na kanisa
katoliki. Kikundi hiki cha wanawake wasomi kimepatikana kwa njia ya elimu ya
kanisa katoliki, na mshikamano wao unaoendelea hadi sasa katika shughuli mbali
mbali za kanisa na za kawaida . Uk.14 5. "Mchango mkubwa ni Nyerere mwenyewe.
Yeye ni Mkristu na mtu
wa kanisa mwenye uhusiano mkubwa na baadhi ya Maaskofu na Mapadri. Uk. 19 6.
"Uhusiano kati ya kanisa katoliki na Nyerere ulikwisha kugusiwa, Ingawa
alifundishwa mafundisho ya ukatoliki kule shule ya msingi Mwisenge na rafiki
yake Oswald Marwa, hakubatizwa mpaka alipomaliza masomo ya sekondari Tabora.
Alijiunga na mfumo wa elimu ya kanisa katoliki kma mwalimu baada ya kumaliza
masomo yake Makerere.riwa kama mwalimu katika shule ya St.Mary's, kisha
alipendekezwa kwa masomo ya juu na viongozi wa Kanisa Katoliki na ndipo
akapelekwa Edingurgh, Scotland na serikali. (15) Baada ya kumaliza masomo yake
1952, alirudi Dar es Salaam ambapo alifundisha katika Sekondari ya Mt.Francis,
Pugu. Wakati huo Padri Walsh wa shirika la White Fathers alikuwa amehamishiwa
Dar es Salaam kuwa katibu mtendaji wa idara ya elimu ya Kanisa.
Watu hawa wawili
walikuwa wakizungumza katika jumba la "White Fathers." Moja ya
mazungumzo hayo bila shaka yalikuwa juu ya Nyerere kujihusisha kikamilifu na
siasa ya kutetea uhuru". Uk 19. 7. "Nimekuwa nikiuelezea uhusiano
kati ya Nyerere na Padri Walsh. Uhusiano huu ulikuwa ni zaidi ya ushauri au
urafiki. Mara nyingi Padri Walsh kama katibu wa elimu wa Kanisa Katoliki
alishauriana na Serikali kwa niaba ya TANU na Nyerere." 8. Hivyo, kutokana
na Nyerere kuwa mkatoliki, na kuwa kiini cha kundi la watawala, alikuja kuwa
kiungo muhimu kati ya Kanisa na Serikali. Uhusiano huo uliimarishwa zaidi na
shughuli za viongozi muhimu wa Kanisa ambao walimsaidia Nyerere katika mambo ya
siasa na nafasi yake katika kuiongoza TANU. Nafasi yake kwa masomo ya juu,
msaada wa fedha na vinginevyo ni baadhi tu ya vitu vilivyofanywa na viongozi wa
Kanisa Katoliki kwa niaba yake, wakimtetea kuwa kiongozi mwenye msimamo
unaokubalika.
Uk. 21. 9. "Bi
Hancock alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule ya wasichana Tabora mwaka 1931 na baadaye
shule ya wasichana Mbeya. Hatimaye alikuwa mkaguzi wa elimu. Alikuwa mshabiki
mkubwa wa TANU na rafiki wa familia ya Nyerere. Kwa kupitia kazi zake,
alianzisha na kuendeleza uhusiano kati yake na watumishi wengi wa Serikali,
wanawake kwa wanaume nchini kote. Mwaka 1963 alichaguliwa na maaskofu kusimamia
maendeleo ya wanawake katika idara ya jamii, TEC. Bi. Hancock alisambaza
shughuli hizi za maendeleo ya akina mama nchini kote. Alisisitiza ushirikiano
wa wanawake wakatoliki katika baraza la U W T, moja ya jumuia za Chama.
Alihimiza vikundi vya wanawake wakatoliki kujiunga pamoja kuleta maendeleo na
kushiriki kikamilifu katika sera za Serikali na TANU". 10. Baada ya
Nyerere kuwataka mapadri waishi vijijini, viongozi wa Kanisa kwa pamoja
walitafuta njia ya kuitikia mwito huo. Ilikuwa dhahiri kwamba idadi ya mapadri
waliohitajika kama alivyotaka Nyerere haikuwepo.
Hivyo katika mkutano
wao wa mwaka 1970, maaskofu waliamua kwamba " makatekista, moja kwa moja
wawe ufumbuzi wa muda na hao makatekista wapewe mafunzo maalumu kwa kazi
hii." (uk 57) Mfano wa mafunzo ya aina hii kwa ajili ya makatekista wenye
mwelekeo wa ujamaa yalitolewa na "Komuge Catechetical Training
Centre" Mkurugenzi wa chuo hicho, wakati huo alisema kuwa mipango yake
ilitegemea sana ile ya Bukumbi Catechetical School Mwanza. Ratiba ya masomo
ilikuwa pamoja na Biblia, Dini, Liturjia, Sosiolojia, Historia ya Kanisa na
mbinu za kufundisha.
Wanafunzi pia walikuwa
na shughuli za kilimo cha pamoja licha ya kuwa na mashamba katika familia zao.
Mashamba ya mifano yalikuwepo na mafunzo juu ya ufugaji bora yalitolewa. Misingi
ya ujamaa ilitiliwa mkazo katika masomo na shughuli zao za pamoja. Mkurugenzi
huyu aliunga sana mkono mawazo ya ujamaa na alisema, "Nilivutiwa sana na
Nyerere na katika kufundisha kwangu nilitilia mkazo matendo ya Mitume" na
mafundisho ya Kristu juu ya haki. Pale shuleni tulikuwa nalo shamba la pamoja
na kila tu alikuwa anafanya kazi kijamaa hadi wakati wa kuvuna na hii ikawa
ndio sera ya shule. Kila mwaka tulivuna mahindi, mboga na karanga vitu ambavyo
tuligawana kijamaa na mtazamo wote kwa jumla ulikuwa kwamba ujamaa na ukiristu
vitakwisha sana.
Makatekista vile vile
walihimizwa kufundisha watu vijijini mwao falsafa ya ujamaa (58). Mkurugenzi
huyu aliarifu kuwa ishara ya mafanikio ya mpango huo ilikuwa idadi ya
makatekista walioshika madaraka ya Chama na Serikali vijijini. Alisema kwa
wastani asilimia 70 ya wahitimu wote aidha wamekuwa makatibu au wenyeviti wa
vijiji, makatibu kata au makatibu tarafa. Hakuna takwimu kuthibitisha jambo
hili kwa jumla. Lakini kutokana na mahojiano yangu katika majimbo ya Arusha,
Mwanza, Mbeya na Musoma, waliohojiwa walikiri kwamba wale makatekista waliopata
mafunzo ya miaka miwili na kufanya kazi vijijini, wengi wao walishika nafasi za
uongozi katika chama na Serikali. Uk. 44-45. 11.
Nyerere alimudu kuwatoa
hofu na mashaka kiasi kwamba mwenyekiti wa R S A T alisema: "Ningependa
kuongeza kuwa hata kama walikuwepo waliokuwa na wasi wasi juu ya itikadi ya
miongozo hapa Tanzania kama nchi ambayo imepania kujenga maisha ya kisoshalisti
walikuwa ni wachache. Pia tunayo imani na wewe kama kiongozi wa nchi hii,
mjamaa halisi na mkristu safi, labda sasa kuliko wakati wowote ule. Matatizo
yetu siyo juu yako wewe, Chama chako au Serikali. Haya yanatoka katika ngazi ya
chini kabisa ambapo tabia za watu zinaweza kuingilia. 12. Mwisho, askofu
mwingine alipendekeza : "Tunachotakiwa kufanya hivi sasa ni kufufua lile
"Baraza la Wazee" Awali baraza hili lilitusaidia sana kwani badala ya
kupiga makelele hadharani, baadhi yetu maaskofu tuliweza kukutana na Nyerere na
kutatua matatizo yetu kwa mila na desturi za kiafrika".
Kwa sababu hiyo basi,
mambo fulani fulani yalisaidia kuelekeza msimamo wa maaskofu. Kwanza walidai
kuwa hawakuhusikshwa kikamilifu katika muundo wa utume huo, Pili walijua kwa
mapana na marefu hali ilivyokuwa huko Uganda na hivyo walithamini sana amani
iliyokuwepo hapa Tanzania. Serikali na hasa Nyerere kwa kiasi kikubwa walipewa
heko kwa utulivu huo ambao uliruhusu Kanisa Katoliki likue na kustawi. Jambo la
tatu, ni kwamba maaskofu waliridhika na hali ilivyokuwa kwani walijiona kuwa
waliweza kuwasiliana na viongozi wa Serikali kutatua matatizo yaliyojitokeza
bila ulazima wa kushirikisha watu wa kawaida. Uk . 74 13. Mwisho, sura hii
imeonyesha umuhimu wa uhusiano kati ya Nyerere na maaskofu. Alikuwa kama kiungo
muhimu katika utume wao.
Katika mapambano ya
miaka ya 1970, mara nyingi Nyerere aliwahimiza maaskofu kujiweka sambamba na
ujamaa. Lakini kwa wakati huo alikuwa amebadilika msimamo wake. Alitoa baraka
zake na kuwashukuru maaskofu kwa mawazo yao. Kwa maelekezo yake, mashirika ya
dini yalisamehewa ushuru wa forodha na kodi ya mauzo kwa bidhaa walizokuwa
wanaziagiza kutoka ng'ambo. Baadhi ya viongzi wa Kanisa Katoliki walipewa
vibali vya Rais kuingiza vitu kutoka Kenya bila ushuru ingawa mpaka kati ya
nchi hizi mbili ulikuwa umefungwa. Maagizo haya ya Nyerere yanaonyesha jinsi
gani alivyothamini juhudi za Kanisa katika kufufua uchumi. Ama kwa hakika,
ushirikiano huo uliruhusu viongozi wa Kanisa Katoliki kuwa na nguvu za kiuchumi
wakati taifa likiwa kwenye hali mbaya. Uk 76. 14. Uongozi wa Kanisa Katoliki
katika juhudi za kuelekeza ujamaa wa Kitanzania, ulihusika moja kwa moja na
kikundi hiki cha wasomi. Mwanzo wa kipindi kati ya 1953 na 1966, uhusiano
ulikwishaanza na kuimarika zaidi wakati wa mapambano ya uhuru hadi matokeo yake.
Mahojiano yangu yamethibitisha kwamba licha ya uhusiano wa kawaida uliokuwepo
kati ya viongozi wakatoliki wa Chama Serikali na uongozi wa Kanisa, mshikamano
maalum umejitokeza hasa ukitilia maanani michango ya Kanisa katika kupatikana
kwa uhuru. Michango hiyo ilikuwa hasa kwenye nyanja za elimu na mafunzo ya
uongozi wa namna moja au nyingine. Licha ya kuonekana kasaidia kuleta uhuru,
michango hiyo imesaidia kujenga na kuimarisha uhusiano wa kudumu kati ya
uongozi wa Kanisa Katoliki na watawala wa Tanzania huru. Mshikamano huo mpaka
sasa unaendelea. Hapana shaka kwamba Rais mstaafu Nyerere, ikiwa kiongozi mkuu
wa Serikali, alichangia sana hali hiyo. Kanisa Katoliki lilimpendekeza kwa
masomo ya juu zaidi na lilitoa misaada mingine. Alifanya kazi katika mfumo wa
elimu wa Kikatoliki hapa Tanzania na matarajio yake kuhusu siasa yalitiwa moyo
na baadhi ya mapadri na maaskofu ambao pia waliwaondolea wasi wasi wakoloni juu
yake. Daima alitambuliwa na viongozi hawa kama mtu mwadilifu na mkristu safi.
Kutokana na hali hiyo basi, uhusiano mkubwa kati yake na uongozi wa Kanisa
ulisaidia nafsi ya viongozi wa Kanisa kuelekeza maana ya siasa ya ujamaa."
Uk 77 - 78 15. Wakati huu mgumu, uliona kukua kwa nafasi ya viongozi wa kanisa
katoliki katika maendeleo ya nchi kwa sababu ya uhusiano, wao na mashirika ya
nje ambayo yalikuwa yakitoa misaada. Wakuu wa Serikali, wakiwa wamekabiliwa na
matatizo makubwa kiuchumi, walikiri kwamba viongozi hawa wa kanisa walikuwa na
mchango mkubwa kwa misaada ya dharura na katika kufufua uchumi wa taifa.
Kutokana na hali hii viongozi wa kanisa walikuja kuwa na nguvu zaidi za
kiuchumi. Lakini wakati huo huo uongozi wa kanisa nao ulikuja kutambua kuwa
unamtegemea Rais Nyerere kama mlezi na mlinzi mkuu wa amani iliyowaruhusu
kupata maendeleo ya namna nyingi.
Uk 79
Uk 79
SWALI LA TATU KANISA
LILITOA MSAADA ILI KUELEKEZA SIASA TANZANIA
Jee Kanisa katoliki
lilitoa misaada kwa lengo la kuelekeza siasa Tanzania? Dkt. John C. Sivalon,
katika kitabu chake, anaeleza : 1. Kanisa Katoliki lilitoa michango kadhaa katika
mapambano ya uhuru. Michango hiyo ilisaidia kuimarisha uhusiano kati ya
viongozi wa kanisa wa Chama na kanisa. Huo uhusiano ukaweka viongozi wa kanisa
katika nafasi nzuri ya kuelekeza maendeleo ya siasa ya Tanzania. Uk 9. 2. Licha
ya hali ya kutatanisha kwa watumishi wakristo wa kanisa pamoja na viongozi
kadhaa wa Kanisa. Waliohojiwa wamekubali kuwa viongozi wa kanisa katoliki na
idara zake walitoa michango mbali mbali iliyosaidia kuleta uhuru. Vile vile,
michango hiyo iliimarisha uhusiano kati ya viongozi wa kanisa katoliki na wa
Serikali na Chama. Uk 10. 3. Hayo ndiyo yaliyotajwa katika maelezo ya wengi
walihojiwa kuhusu michango ya kanisa katika mapambano ya uhuru. Na wakati huo
huo michango hiyo imewezesha viongozi wa kanisa kujenga uhusiano kati yao na
viongozi wa Chama na Serikali. Huo uhusiano umewapa viongozi wa kanisa nafasi
ya pekee ya kuelekeza jinsi siasa ya ujamaa ilivyokuja kueleweka na kutekelezwa
na viongozi wa Serikali.
Uk 24-25.
Uk 24-25.
SWALI LA NNE KANISA
KATOLIKI LILIMWUNGA MKONO NYERERE KWA FAIDA YA KANISA HILO
Jee, Kanisa Katoliki
lilimwuunga mkono Nyerere na kumsaidia kwa ajili ya faida ya Kanisa hilo? Dkt.
John C. Sivalon katika kitabu chake, anaeleza : 1. Maryknoll fathers wamekubali
kulipa tiketi ya kwenda Amerika na kurudi England kwa vile huyu ni kiongozi wa
kikatoliki, mtu kutoka jimbo la Musoma ambaye anaheshimiwa na mapadri wetu. Kwa
vile ni nia ya Serikali ya Waingereza kuwaandaa wenyeji kwa madaraka, Shirika
la Maryknoll limeona kutowa msaada wowote linaoweza kuwapatia viongozi wa
kikatoliki utakuwa ni kulisaidia Kanisa. Huyu ni mkatoliki mzurti, mtu mwenye
msimamo wa busara katika kutaka kuwaelekeza watu wake kwenye uhuru kamili.
Hakosi kuwa na habari kwamba kuna wapinzani fulani wenye siasa kali zaidi
katika Chama chake lakini anajitahidi kukiongoza kwa njia inayokubalika. Chama
hiki kimeandikishwa rasmi serikalini na wala sio chama cha siri (17) : Uk 21.
2. "Katika kueleza uhusiano maalum baina ya viongozi wa Kanisa Katoliki na
viongozi wa Chama na Serikali, tumeshagusia kidogo nia ya viongozi wa Kanisa
katika kujenga uhusiano huo kwa njia ya utume wao wa kijamii. Kwa mfano, katika
maneno ya yule askofu aliyekaririwa katika sura ya pili, alisisitiza kuwa lengo
moja la mafundisho ya uongozi kwa walei lilikuwa kuzuia Chama cha kupigania
uhuru kisianguke mikononi mwa mawakala wasiofaa. Katika barua iliyopelekwa
Vatikano sababu moja wapo iliyotajwa ya kumuunga mkono Nyerere ilikuwa kwamba
itakuwa kwa faida ya Kanisa siku zijazo. Hofu ya siasa ya ukomunisti ilikuwa
sababu muhimu ya kuanzisha na kuendeleza vyama vya kitume kama "Social
Guilds." Uk. 26. 3. "Kwa kumalizia, jambo lingine lililoonyesha ya
kuwa utawala wa Serikali ulitambua kuunga mkono siasa ya ujamaa kwa baadhi ya
viongozi wakatoliki lilitokea mnano mwaka 1974. Wakati huo Serikali ilikuwa
inaanzisha shule ya sekondari kwa wasichana. Mpango wake wa masomo ulibuniwa
ili ulingane na maisha ya vijijini na siasa ya ujamaa. Nyerere binafsi
aliwaomba masista wa Shirika la Maryknoll, ambao ndio walikuwa waanzilishi wa
"Marian College, "kuongoza shule hiyo. Ulipowadia wakati wa
kufundisha na kuwajenga wasichana hao kijamaa, Nyerere aliwageukia tena masista
Wakatoliki ambao ndio waliwafundisha akina mama wengi katika kundi la viongozi
wa Chama na Serikali." Uk 50 --
SWALI LA TANO SIASA
YA UJAMAA NI MSIMAMO WA KIKRISTO
Jee, Ujamaa ni siasa
iliyo na msimano wa Kikristo? Dkt. John Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza
: 1. "Barua hiyo inadhihirisha kuunga mkono ujamaa kwa kuwa ni siasa iliyo
na misimamo wa kikristu hasa kwa kutetea haki, kujenga umoja na kutafuta
usawa". uk 40 2. "Baada ya miezi minne, msimamo huo ulirudiwa tena na
Pd. Robert Rweyemamu aliyekuwa katibu mkuu wa TEC. Alisisitiza jinsi Papulorum
Progressio na Azimio la Arusha vilivyofanana. Aliviita mapacha. Uk. 42 3. Kundi
la pili ni wale waliounga mkono. Kwa mfano Padri X. Katika mahojiano yangu
naye. Huyo alisema kwamba aliamini kabisa kuwa ujamaa ni mfumo wa kikristu wa
uchumi na siasa. Aliamini kwamba ujamaa una miongozo iwezeshayo ufalme wa Mungu
kujengwa hapa duniani. Kutokana na imani hii aliona umuhimu wa kuanzisha kijiji
cha ujamaa katika eneo la makao makuu ya parokia yake. Alifanya hivyo kwa
kushirikiana na katekista ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti pamoja na majirani
wachache. Uk. 43. 4. Idadi kubwa ya viongozi hawa walikubali kuwa misingi ya
ujamaa ilikuwa sawa na mafundisho ya kikatoliki" Uk. 43. 5."Azimio la
mkutano huo wa mwaka wa Semina za Mafunzo kuhusu ujamaa na maendeleo kitaifa
lilisema : "Viongozi wa Kanisa wanaombwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo
ya jamii vijijini kwa uwezo wao wote na kufuata mipango ya Serikali".
Kanisa linaombwa kusaidia kuwaelimisha watu kwa mtazamo mpya na maadili ya
kikristu yaliyomo katika siasa ya ujamaa ambayo hutegemewa sana na maendeleo ya
kisiasa (61) Ingawa hakukuwa na mipango madhubuti iliyoandaliwa kwa utekelezaji
wa azimio hili, viongozi wote wa kitaifa katika vyama viwili vya walei walikuwa
pia ni viongozi wa Serikali pamoja na chama. Hivyo katika uongozi wao wa vyama
hivi, hawakusita kutilia mkazo siasa ya ujamaa. Pia, hata kule kujitokeza kwao
katika uongozi wa Kanisa kulitia muhuri fulani uhusiano kati ya Kanisa Katoliki
na Chama. Pamoja na hayo, maaskofu nao waliamuru "Baraza la Walei"
liwe na mpango kabambe kwa ajili ya vijiji vya ujamaa. Katika mkutano wao wa
mwaka 1971 walisema : Wanabaraza katika vikundi wanapaswa kuamua kuanziasha
vijiji vya ujamaa kwa maadili ya kikiristu ili viwe ni mfano wa kuigwa na
vingine
(62). Uk 49SWALI LA
SITA KIJIJI CHA UJAMAA NI PAHALI PAZURI KUENENZEA UKRISTO?
Jee, Kanisa Katoliki
liliunga mkono kuanzishwa vijiji vya ujamaa kwa sababu kijiji cha Ujamaa ni
pahali pazuri pa kueneza ukristo? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake,
anaeleza : 1. "Kanisa halijawahi kuwa na nafasi nzuri kama hii katika
kutekeleza shughuli zake katika jamii ya mchanganyiko. Ujamaa unaonekana kuwa
na msimamo sawa sawa na ule wa Kanisa. Kwa hivyo basi, unalingana na mafundisho
ya Kanisa na uko karibu sambamba na yale yaliyotajwa katika "Mater et
Maistra. "Katika jumuiya ya watu wenye dini mbali mbali kama ilivyo
Tanganyika, Kanisa lisingeweza kuomba nafasi zidi ya hiyo (37) Ulikuwa msimamo
wa Pd. Robinson pamoja na mapadri wengine wengi kwamba ujamaa kama ilivyoelezwa
na Nyerere ulikaribiana sana na mafundisho rasmi ya Kanisa Katoliki juu ya
siasa na uchumi. UK 34. 2. Askofu ambaye alikuwa mfano wa kundi la pili katika
jimbo lake ni Christopher Mwoleka. Aliona ujamaa kama nafasi ya pekee kwa
Kanisa Katoliki na alisisitiza mchango wa Kanisa katika utekelezaji wake.
Akifafanua jukumu hilo kama la kuelimisha raia mpaka wafikie kiwango cha
kujenga ujamaa kamili. Aliandika. : Katika historia Kanisa halijapata nafasi
kama hii ya kuonyesha kwa vitendo yale ambayo limekuwa likihubiri kwa karne
nyingi. Kijiji ambapo kwa makusudi watu wake wanahimizwa kuwa sehemu ya mwili
mmoja ni mahali pazuri kwa ukristu kufanikiwa kuliko kijiji cha kawaida ambapo
watu wake wana dhamira mbali mbali za ushindani na kunyonyana. Hapa Tanzania
uwanja umekwisha tayarishwa. Kinachobaki ni kueneza na kukuza Injili. Hivyo
vijijini wakiisha waanzishe jumuiya ziwe kama sumaku kuwavuta wengine. Jumuiya
ya kikiristu lazima iwe msukumo wa upendo na huduma kwa wengine (55). Askofu
Mwoleka alifuata maadili haya kuwataka wakristu wote waishi vijijini ili
wanufaike na maisha ya kidini huko. Yeye mwenyewe alijiunga na kijiji cha
Nyamihanga. Aliwatafuta na kuwaitia moyo viongozi wa Kanisa ambao alitumaini
wangeishi vijijini kama majirani wa wanakijiji. Juhudi hizi ingawa zilipata
upinzani kutoka kwa viongozi wengine wa dini jimboni mwake zilifanikiwa kiasi.
Mawakala ya Ujamaa na Jumuia za Kikiristu imebami kuwa mwaka 1976 kulikuwa na
viongozi kumi na mmoja tu ambao ambao waliishi vijijini moja kwa moja. Uk 56
SWALI LA SABA KANISA
LAHAMASISHA WAKATOLIKI KUWACHAGUA WAKATOLIKI WENZAO
Jee, Kanisa Katoliki,
kwa kupitia katika taasisi zake huandaaa mikakati ya siri, kuwahamasisha
wakatoliki kuwapigia kura wakatoliki wenzao katika chaguzi za kugombania
ubunge? Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1.
"SSY" ilimaliza mapendekezo yake kuhusu ujamaa kwa kutaka iundwe
kamati ya kutafiti uwezekano, madhara na matatizo ya kuliunda upya Kanisa
Katoliki katika maadili ya ujamaa wa kweli wa kikristu (63). Mwishowe,
"SSY" ilitoa msisitizo juu ya jukumu la walei katika jamii. Haya
yalitokea wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 1970. Ingawa hakuna utafiti uliofanywa
kuonyesha uhusiano kati ya SSY na wabunge waliochaguliwa, mmoja kati ya watu
waliohojiwa alidai kuwa : SSY na Baraza vimeleta msisimko huu ambao umewaamsha
Wakatoliki kupigania viti katika uchaguzi wa wabunge na mimi nikiwa mmoja wao.
Baadaye huko bungeni tulifanya utafiti usio rasmi na kugundua kwamba 75% ya
waliochaguliwa walikuwa wakristu na kati ya hao 70 % walikuwa wakatoliki (64).
Uk 49 2. "Hivyo basi "SSY" ilibainisha kuungwa mkono kwa ujamaa
na viongozi wa Kanisa na muhimu pia kuwashirikisha walei wakati huo maalum
katika historia ya ujamaa wa Tanzania. Kilikuwa ni chombo cha kuwaelimisha
walei kuhusu mafundisho ya Kanisa juu ya Jamii. Pia iliwashawishi kugombea
nafsi za uongozi Serikalini ambapo wangeweza kuathiri tafsiri ya ujamaa"
Uk 49 -50
SWALI LA NANE
MAAMUZI YA SERIKALI YAFANANA NA MAFUNDISHO YA KANISA KATOLIKI
Jee, Kanisa Katoliki
lilimuunga mkono Nyerere na kumsaidia kwa ajili ya faida ya kanisa hilo? Dkt.
John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1."Kwa hiyo, makanisa ya
kikristu yaliweza kujivunia kuwa yamesaidia kuelimisha, kwa ngazi moja ama
nyingine, idadi kubwa ya wale waliokuja kuwa viongozi wa Serikali na Chama. Kwa
njia hiyo kulitokea nafasi kubwa ya kukuza uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa.
Na wa Serikali na Chama. Uhusiano huu sio kwamba ulikomea darasani tu, bali
unaendelea hata mpaka sasa kati ya wanafunzi kwa wanafunzi na walimu kwa
wanafunzi.Uk 12. 2. "Muhimu zaidi ni kwamba shughuli na mazingira katika
shule za bweni zimewezesha hadi sasa kukua kwa uhusiano kati ya viongozi wa
Kanisa na wa Serikali na Chama. Hali hii imefanya matendo, msimamo na uamuzi wa
viongozi wa Serikali ufanane mara kwa mara kwa namna moja au nyingine na
mafundisho na mwelekeo wa Kanisa". Uk 16 3."Kwa namna nyingi St.
Mary`s na St. Francis ya Pugu zilichangia uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa
Katoliki na wale wa Serikali. Kwanza vyombo hivi vya Kanisa Katoliki vilitoa
elimu iliyowasaidia hao wahitimu kufikia ngazi hizi za uongozi. Pili, urafiki
kati ya walimu wa St. Mary`s na St. Francis pamoja na urafiki kati ya wanafunzi
wa vyuo hivi viwili ulichangia mshikamano wa viongozi Serikalini. Tatu, mawazo
na fikra za watu hao juu ya ujamaa yalielekezwa na elimu yao ya Katoliki.
Uk. 16 SWALI LA TISA
KANISA KATOLIKI LATAKA KUWEKA VIONGOZI WAKATOLIKI KATIKA NCHI ZA AFRIKA
MASHARIKI
Jee, Ni mkakati kuweka
viongozi wakatoliki katika nchi za Afrika Mashariki? Dkt. John C. Sivalon,
katika kitabu chake, anaeleza : Zaidi ya hayo kulikuwa na mpango wa kuanzisha
Chuo cha Maendeleo ya jamii Tanzania. Chuo cha Maendeleo ya Jamii Nyegezi
kilianzishwa na White Fathers kati ya vyuo vitatu vilivyokusudiwa kwa Afrika.
Ilikusudiwa kwamba vyuo hivi vingetoa wanafunzi kwenda kwenye
"International Institute" huko London, Chuo hiki kilichofahamika kama
"Claver House" kule London, kilikuwa chini ya uongozi wa Padri Paul
Crane, S.J. Nia ya vyuo hivi ilikuwa kuwaandaa viongozi katika sayasi ya
kijamii na mafundisho ya Kanisa Katoliki. Walipokea wanafunzi wenye elimu ya darasa
la kumi na mbili au kiwango kama hicho. Wanafunzi hawa hawakuchukuliwa moja kwa
moja kutoka vyuoni, ilibidi wawe wameajiriwa serikalini, kwenye mashirika ama
kwenye kampuni za watu binafsi. Padri Crane ambaye alitembelea Tanzania 1959
alidhihirisha madhumuni ya vikundi hivi vya kijamii kwa maneno yafuatayo :
"Tatizo la Afrika ni kwamba watu wasiofaa wamewekwa katika nafasi za
utawala. Tutaweza vipi kuweka watu wanaostahili katika nafasi hizi? Lazima
tujitahidi kadiri ya uwezo wetu kupata wasomi wakatoliki ambao watashika nafasi
muhimu kwenye ngazi zote za kijamii. Wakatoliki wetu walei wajitahidi kushika
nafasi hizi. Tutaweza kuwaingiza kwenye nafasi hizi za uongozi wa njia ya
kujenga vikundi vidogo vidogo vya wasomi wakatoliki …(21)" Uk 23
SWALI LA KUMI KANISA
KATOLIKI LAUONA UISLAMU NI TISHIO KWA UKRISTO
Jee, Kanisa Katoliki
pamoja na maaskofu waliuona Uislamu kuwa ni adui na tishio kwa ukristo? Dkt.
John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : 1. "Kwa upande mwingine
lakini Maaskofu hao waliendelea kuuona Uislamu na falsafa ya Marx kama
tishio" Uk 32 2. "Lakini, hata Pd. Robinson alikuwa na wasi wasi kama
siasa ya ujamaa ingebaki na maana hiyo. Alihofia. Kama alivyojieleza, dini ya
Uislamu na siasa ya ukomunisti. Kwanza, kuhusu Uislamu, alieleza : "
Kuenea kwa dini ya Uislamu ni kwamba wakati makanisa ya kikristu yanajitahidi
kuishi kwa uelewano na kushirikiana katika jamii ya mchanganyiko wa watu mbali
mbali kwa kuheshimu uhuru wa mtu kufuata dini apendayo na mgawanyiko wa mamlaka
ya serikali na dini, waislamu wanaonekana kuitumia nafasi hiyo kujinufaisha
kidini na kisiasa wakitumia nafasi yao kudhoofisha makanisa ya kikristu. (38)
3. "Hali ya wasi wasi pia ilidhihirika katika idara hiyo kuhusu Uislamu.
Ripoti moja ilisema hivi : Uislamu unazidi kuleta matatizo. Waislamu wamefaulu
sana katika vyombo vya juu walijaribu kuleta maang`amizi yao huku wakifaidika
na huduma zetu za kijamii, bila kukubaliana na masharti ya ushirikiano katika
mfumo wa wengi jinsi ilivyotajwa kwenye Unity and Freedom. (54) Inaendelea
kueleza jinsi Waislamu walivyokuwa wakijizatiti kuwa jumuiya kubwa, jumuiya
kubwa, jambo ambalo lilikuwa ni hatari kubwa kwa hali ya Wakiristu baadaye.
Ilionya kuhusu mkutano wa baadaye kati ya viongozi wa Bohora, Ismailia,
Ithnasheri na Sunni. Kuletwa kwa makao makuu ya Chama cha Ustawi wa Waislamu
hapa Dar es Salaam mwaka 1961 kulitajwa kama tishio lingine. Kufuatana na
ripoti hii, ziara ya Masheikh kutoka Misri ambayo yalidhaminiwa na Mortamar
(Pan Islamic Congress) yaliogopesha sana. Sehemu hii ya ripoti inamalizia kwa
kusema kuwa tayari Waislamu walikuwa wameanza kuwashambulia Wakiristu. Jambo
muhimu zaidi ni kwamba ripoti hii inaeleza mikakati ya kupambana na hatari hii.
Ilipendekezwa kuwa kazi hii ifanywe na makatekista waafrika wenye ujuzi wa hali
ya juu. Hata hivyo kutokana na hisia za jumuiya ya Waislamu ripoti inasema :
Makatekista hao lazima waweze kufanya kazi katika idara za maendeleo ya jamii
vijijini, iwe ni katika kilimo au katika shughuli nyingine za maendeleo kama
vile ujenzi wa nyumba, bara bara n. k. (46) Hivyo kutokana na kazi ya idara ya
mambo ya dini ya TEC kwa wastani, watenda kazi wote katika Kanisa Katoliki na
jumuia zake walielimishwa juu ya hatari za ukomunisti na uislamu kama
zilivyodhaniwa na viongozi wa Kanisa. Hii siyo kusema kwamba Wakatoliki wote
walikubaliana na msimamo huu. Bali ni kwamba viongozi wa ngazi za juu
waliohusika na utume wa Kanisa wa kijamii, kitaifa walijaribu kutumia utume huo
kama mkakati wa kupambana na yaliyodhaniwa kuwa maadui wa Kanisa Ukomunisti na
Uislamu " Uk 37 4."Licha ya hayo: Miongo hiyo mitatu toka mwaka 1952
hadi 1985 imefunuliwa miongozo ya kimsingi ya utume wa kijamii wa viongozi wa
Kanisa Katoliki. Kwanza kwa muda wote maaskofu wameonesha hali ya wasi wasi juu
ya kuenea kwa falsafa ya Marx pamoja na Uislamu. Pili, katika kipindi cha toka
1969 hadi 1975 walisita sana walipoona jinsi watu wengine walivyokuwa
wanauelewa mwongozo na uelezaji wake juu ya demokrasia. Pia walipinga vikali. Walioona
siasa hiyo ya demokrasia ikianza kuingilia utawala wao wa Kanisa." Uk 80
SWALI LA KUMI NA
MOJA KANISA KATOLIKI LASHIRIKINA NA SERIKALI KUUDHIBITI UISLAMU
Jee, Kanisa Katoliki
lilijenga uhusiano na Serikali kwa ajili ya kuudhibiti Uislamu? Dkt. John
Sivalon katika kitabu chake, anaeleza : 1. Baada ya hayo nitaendelea kueleza
katika sura ya tatu jinsi maaskofu na viongozi wengine wa ngazi za juu ya
kanisa walivyoelewa utume wao wa kijamii yaani shughuli zile zote za kanisa
zilizokuwa zinahusu wazi wazi siasa, uchumi, elimu na huduma nyingine za
kijamii. Kwa kuchunguza barua za kichungaji za maaskofu za 1953 hadi 1966 na
miongozo ya Baraza la Maaskofu wa Tanzania (TEC) kipindi hiki, itaonyeshwa kuwa
hao viongozi wa Kanisa Katoliki walielewa nia ya utume huo kuwa hasa ni kuhami
nafasi ya Kanisa katika jamii ya Tanzania. Walifanya hivi hasa wakizingatia
ukuaji wa Ukomunisti na Uislamu. Uk 5-6 2. Katika sura ya tatu, nitaendelea
kuchambua huduma ya kijamii katika Kanisa wakati huo kwa kuzingatia mafundisho
ya maaskofu wa Tanzania kati ya mwaka 1953 - 1966. Mafundisho hayo yanaeleza
rasmi lengo na madhumuni ya utume wa kijamii wa viongozi wa Kanisa. Itaonyeshwa
kuwa viongozi wa Kanisa walikusudia kujenga uhusiano na viongozi wa Serikali
ili wawe na nafasi nzuri katika kujihami dhidi ya uenezaji wa falsafa ya Marx
na Uislamu. Uk 25 3. Lengo kubwa la utume wa kijamii wa viongozi wa Kanisa
Katoliki kutoka mwaka 1953 hadi 1966 limekua likilinda nafasi ya Kanisa katika
jamii kwa ujumla kwa kupinga kuenea kwa falsafa ya Kanisa katika jamii kwa
ujumla kwa kupinga kuenea kwa falsafa ya Marx hapa Tanzania. Viongozi wakubwa
wa Kanisa kwa kuangalia mienendo ya watu fulani na mwelekeo mwingine wa Chama
na Serikali waliamini kuwa siasa ya Umarx ilikuwa imeshaanza kuota mizizi hapa
Tanzania. Waliona kuwa utume wao wa kijamii ndio njia bora kuzuia kuenea kwake.
Hali kadhalika itaonyeshwa kwamba viongozi hao hao walitumia utume wao wa
kijamii kuhami nafasi ya Kanisa katika kupinga kuenea kwa dini ya Kiislamu. Kwa
kifupi viongozi hao waliona kuwa walikuwepo maadui wawili wa Kanisa hapa
Tanzania, yaani Uislamu na Umarx. Waliamua kutumia utume wao wa kijamii kama
mkakati wa pekee kupambana na haya mawili. Uk 26 4. Kama ilivyoelezwa katika
sura ya pili viongozi wa Serikali na Chama. Walitumia uhusiano huo kupatikana
na mabadiliko yaliyotajwa hapo juu. Katika mafundisho rasmi mengine ya Kanisa
kwa wakati ule msimamo wa Kanisa na msimamo wa ujamaa kama Nyerere alivyoueleza
vilikubaliwa kuwa sambamba. Pd. Robinson alisilisitiza kuwa kuunga mkono ujamaa
kwa viongozi wa Kanisa kulikuwa ni njia pekee ya kuzuia siasa ya ujamaa
isibadilike.Vile vile alihofia kuenea kwa Uislamu na alishauri kutumia utume wa
kijamii kama mkakati wa kuhami nafasi ya Kanisa katika jamii ya jamii ya
Tanzania. Uk 38.
SWALI LA KUMI NA
MBILI VATIKANO YAKUBALI KANISA KATOLIKI TANZANIA LUMWUUNGE MKONO NYERERE KWA
FAIDA YA KANISA HILO
Jee, Vaticano, ambayo
ndiyo Makao Makuu ya Kanisa katoliki lilikubali Kanisa Katoliki Tanzania
limwunge mkono Nyerere kwa ajili ya faida siyo ya nchi bali ya Kanisa hilo?
Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake, anaeleza : Katika kueleza uhusiano
maalumu baina ya viongozi wa Kanisa Katoliki na viongozi wa Chama na Serikali,
tumeshagusia kidogo nia ya viongozi wa Kanisa katika kujenga uhusiano huo kwa
njia ya utume wao wa kijamii. Kwa mfano, katika maneno ya yule askofu
aliyekaririwa katika sura ya pili, alisisitiza kuwa lengo moja la mafundisho ya
uongozi kwa walei lilikuwa kuzuia Chama cha kupigania uhuru kisianguke mikononi
mwa mwawakala wasiofaa. Katika barua iliyopelekwa Vatikano sababu moja wapo
iliyotajwa ya kumuunga mkono Nyerere ilikuwa kwamba itakuwa kwa faida ya Kanisa
siku zijazo.
SWALI LA KUMI NA
TATU KANISA KATOLIKI LILISHINDWA KUIKOSOA SERIKALI ILI KULIPA FADHILA
Jee, Kanisa Katoliki
lilishindwa kuikosoa Serikali kwa ajili ya kulipa fadhila kwa Serikali ? Dkt.
John C. Sivalon, katika kitabu chake anaeleza : 1. Nia yangu katika sura hii ni
kuchunguza baadhi ya mawazo ya viongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu hali hiyo ya
kuanguka kwa uchumi, katika sehemu ya pili nitazungumzia msimamo wa uongozi wa
Kanisa kufuatana na mafundisho ya maaskofu wakatoliki. Sehemu ya tatu itahusika
na hisia za viongozi wa Kanisa waliosita kuikosoa serikali wazi wazi kwa vile
uongozi wa juu wa Kanisa tayari ulikuwa katika uelewano mkubwa na utawala wa
Serikali. Uk . 62. 2. Pili, Kanisa liliruhusiwa na Serikali kuingiza vitu vingi
nchini bila ya ushuru wala kodi. Vitu vya miradi ya maendeleo pamoja na vile
vya ujenzi vilianza kuagizwa na mwishoni hata mahitaji ya kawaida ya viongozi
wa Kanisa. Mambo yote haya yalipunguza madai ya hali ngumu kwa viongozi hao wa
Kanisa na kuwaweka katika nafasi yenye nguvu ya kiuchumi. Hiyo ilikuwa sababu
nyingine iliyowafanya viongozi hao wa Kanisa wasite kukosoa watawala wa
Serikali. Uk 68.
HITIMISHO
Wengi wamesikia jina la
Shaaban Robert. Baadhi ya barabara na shule katika nchi zimepewa jina lake.
Lakini sio wote wanaomfahamu nani Shaaban Robert! Huenda hata wale wanaokanyaga
barabara au wanaosoma shule zilizopewa jina lake wasimwelewe mtu huyo! Shaaban
Robert ni mwanafasihi mahiri na mwanafalsafa aliyebobea wa nchi hii, ambaye
hatutakosea tukisema aliishi kabla ya wakati wake. Johari za hekima na vito vya
busara vilivyojaa katika maandishi yake mbali mbali huhitaji vichwa vitulivu na
akili pambanuzi kuweza kuzingatia. Moja katika almasi nyingi zilizomo katika
utunzi wake ni ile kauli isemayo: "Serikali iliyofaulu ulimwenguni ni ile
iliyotawala nyoyo za raia wake na siyo viwiliwili vyao" Maneno haya ingawa
ni mafupi na yametamkwa na mswahili, lakini ni maneno mazito, yenye maana kubwa
na yanayosheheni ukweli ndani yake. Serikali inayotawala kwa uadilifu itapendwa
na raia wake na, kwa hivyo, itafanikiwa kutawala nyoyo za raia hao. Lakini
serikali inayowabagua raia wake, itachukiwa na raia hao, na itajijengea
upinzani nao. Itakuwa mara kwa mara ikiwapa mkong'oto raia hao na kuzidisha
uhasama baina yao
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !