MWANANCHI>Posted Jumapili, Juni23 2013 saa 10:26 AM
Kwa
ufupi
- Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia askari polisi wetu wakitawanya mikusanyiko ya watu ikiwamo mikutano ya kisiasa kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kuachwa vilema.
SHARE
THIS STORY.
Juzi,
Ijumaa vyombo vya habari nchini likiwamo gazeti hili vilimkariri Waziri Mkuu
Mizengo Pinda akiagiza vyombo vya dola kuwashughulikia kwa kuwapiga wale
watakaokataa kutii amri na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Pinda
alisema pale watu hao wanapokaidi amri halali wajue watakutana na makali ya
vyombo hivyo ambavyo lazima viwapige.
Pinda
alisema watu wanaokaidi amri wapigwe, hakuna namna nyingine na kwamba Serikali
imechoka.
Tunachukua
nafasi hii kutoa msimamo wetu kwa kulaani na kuipinga kauli hiyo ambayo
tunaamini inaelekea katika kuchochea vurugu zaidi nchini.
Vilevile,
kauli hii Waziri Mkuu tuamini inavunja misingi ya katiba ya nchi yetu licha ya
kwamba kiongozi huyo haamini katika hili kama alivyoeleza bungeni.
Tunaamini
katika ibara ya 13 na kifungu cha 6 (b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inapoeleza: “Ni marufuku kwa mtu yoyote aliyeshtakiwa kwa kosa la
jinai kuteswa kama mtu mwenye kosa, mpaka itakapothibitika anayo hatia kwa
kutenda kosa hilo.
Pia,
ibara hiyo hiyo kifungu cha 6 (e) kinasema: Ni marufuku kwa mtu yoyote,
kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazoweza kumdhalilisha.”
Kwa
maana hiyo, kauli ya Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi mkuu wa Serikali ni amri
kwa wasimamizi wa vyombo vya dola, wakiwamo askari polisi.
Kama
hivi sasa tunashuhudia askari polisi wetu wanatumia mabavu kumdhibiti mtu hata
kama hajaleta upinzani wowote wakati wa kumkamata, hivi wakiruhusiwa kutumia
mabavu siwataua?
Katika
siku za hivi karibuni tumeshuhudia askari polisi wetu wakitawanya mikusanyiko
ya watu ikiwamo mikutano ya kisiasa kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi za
moto na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kuachwa
vilema.
Baadhi
ya matukio hayo ni lile la kutawanya maandamano ya wafuasi wa Chadema mjini
Arusha waliokuwa wakielekea kwenye mkutano uliofanyika Uwanja wa NMC, Januari
5, mwaka juzi na kusababisha watu watatu kuuawa kwa kupigwa risasi.
Tukio
lingine ni lile la kuwazuia wanachama wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi eneo
la Nyololo mkoani Iringa Mei 2, mwaka jana.
Katika tukio hilo askari polisi wanatuhumiwa
kutumia nguvu na kuwatawanya watu na kumuua kwa kumlipua na bomu mwandishi wa
Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Tunaamini kuwa zipo njia nyingi za kudhibiti
mikusanyiko ya watu ambayo siyo halali ikiwamo kutumia maji ya kuwasha au
mabomu ya machozi, lakini siyo kutumia risasi za moto ambazo zimetumika katika
baadhi ya matukio.
Tunachukua nafasi hii kumkumbusha Waziri Mkuu
umuhimu wa kufuta kauli yake hiyo na hata kuwaomba radhi Watanzania kwa kauli
yake.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !