Hivi karibuni, Jumuiya ya Wanafunzi Wakatoliki Watanzania Wanaosoma Roma, iliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumbu kumbu ya miaka kumi na mitatu tangu alipofariki dunia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, muasisi wa Taifa la Tanzania.
Ilikuwa ni fursa
maalum kwa ajili ya kumpongeza na kumkaribisha Askofu mkuu Protas Rugambwa, Katibu
mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya
Kimissionari ya Kipapa, aliyeteuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Benedikto wa
kumi na sita. Ilikuwa ni nafasi ya kuwakaribisha wanafunzi wapya waliotumwa na Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania, Majimbo na Mashirika mbali mbali ya Kitawa na Kazi
za Kitume.
Wanafunzi wa Umoja huu walitumia fursa hiyo pia, kuwapongeza wanafunzi waliopewa Madaraja mbali mbali ndani ya Kanisa pamoja na kuwaombea ndugu zao marehemu waliotangulia mbele ya haki wakiwa na tumaini la ufufuko na uzima wa milele.
Ifuatayo ni risala fupi iliyosomwa na Mheshimiwa Padre Richard Tiganya, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki Watanzania wanaosoma mjini Roma.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu Protase Rugambwa, Mgeni rasmi, Mwadhama Polycarp Kard. Pengo, Wahashamu Maaskofu wageni wa heshima, Mheshimiwa sana Dr. James Alex Msekela, Balozi wa Tanzania nchini Italia, waheshimiwa maafisa mbalimbali katika ubalozi, wapendwa Wakuu wa Mashirika, wapendwa Mapadre, Mashemasi na Masisita, wapendwa Walezi wetu na Wanafamilia ya Mungu! Tumsifu Yesu Kristo. Kwa heshima na taadhima kuu ninawakaribisha kwa furaha katika sherehe yetu tunapoadhimisha sikukuu ya Mwalimu Julius K. Nyerere.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu, ni siku ya furaha na shangwe kwetu sisi wanafunzi Wakatoliki Watanzania tunaosoma hapa Roma, kukutana pamoja ili kusherehekea siku ya Mwalimu Nyerere, siku ambayo tunataka kuenzi mambo mema aliyotuachia Mwalimu na zaidi kumwombea ili Mungu Baba adhihirishe utakatifu wake mbele ya Kanisa, kwa sifa na utukufu wake. Kwa kazi njema ya Mwalimu, kwa maisha yake ya kikristu, tumepata heshima kubwa mbele ya mataifa hasa kwa kile kinachosemwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani na usalama.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu, tunaposherehekea sikukuu ya Mwalimu tunachukua nafasi hii pia kukukaribisha na kukupongeza kwa kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu, mwenyekiti wa Mashirika ya Kipapa na Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa linaloshughulikia Uinjilishaji wa Watu. Ni jambo la heshima kubwa kwa kuteuliwa kwako na Baba Mtakatifu Benedikto XVI, ili uweze kushiriki utume wa Kanisa la Ulimwengu.
Ni Heshima kubwa sana, maana sura ya Tanzania katika Kanisa la ulimwengu lililo kanisa la kimisionari inazidi kukua. Kwa hakika haya ndiyo matunda ya Uinjilishaji uliofanywa na wamisionari nchini petu. Ni heshima kubwa kwako na kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, lakini pia ni wajibu nyeti kwa ajili ya taifa la Mungu. Hivi leo kwa sababu ya wajibu huo pamoja na kukupongeza tunakuombea baraka za Mungu ili uweze kutekeleza utume huo kwa furaha na uchangamfu daima.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu pamoja na jukumu hilo kubwa ulilolipokea tunakuomba kwa heshima kuu sisi wanao tuwe pia sehemu ya utume wako na kwa jinsi hiyo tutapata kuimarika katika umoja wetu wa Wanafunzi ambao unahitaji daima sala za wachungaji wakuu wa Kanisa letu. Baba Askofu Mkuu, kwa kukubali kuja kushiriki nasi na kuweza kutugawia mapaji ya Mungu kwa njia ya Misa Takatifu inatudai kukupongeza pia na kukushukuru na kwa jinsi hiyo tunakuhaidi ushirikiano mkubwa na msaada wa sala.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu, tunapomuenzi Mwalimu na kukupongeza wewe Baba Askofu tunayofuraha kubwa pia, kuwakaribisha wanafunzi wenzetu ambao wanaanza rasmi mwaka wa masomo wengine katika ngazi ya udaktari na wengine katika ngazi ya Licenciate na Bachelor. Hili ni jambo la furaha maana wataundwa vizuri kwa ajili ya Kanisa la Tanzania na ulimwengu kwa ujumla.
Tunawapongeza Mababa Maaskofu wote na kwa namna ya pekee Mababa zetu walioko hapa pamoja nasi, na tunawapongeza Wakuu wa Mashirika kwa kuwatuma hapa kwa ajili ya specialization na majiundo ya kipadre. Basi wapendwa wanafunzi wapya, karibu sana mkaanze shughuli nzito ya kunoa akili zikae sawasawa kwa kazi ya kuchunga taifa la Mungu!
Pamoja na kuwakaribisha wanafunzi wapya pia tunawapongeza wanafunzi ambao wamepokea daraja la Upadre: Pd Patience Ntahonyi wa Jimbo la Rulenge - Ngara na waliopewa daraja la Ushemasi, yaani Shemasi Evaristi Guzuye wa Jimbo la Kigoma, Shemasi Taitus Nkane, na Shemasi Alphonce Holela, wakiwa wanachama wa Shirika la Wabenediktini. Tunawatakia utume mwema katika madaraja, zawadi za Mungu mlizokabidhiwa. Mmepewa bure toeni bure.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu, mahali palipo na Jumuiya kwa vyovyote vile kunaweza kujitokeza shida pia, kumbe katiba yetu inalitazama hilo na hivi tunaalikwa kuwaombea marehemu waliotutangulia. Kwanza tunamkumbuka marehemu Mhashamu Baba Askofu Paschael Kikoti wa jimbo la Mpanda, apumzike kwa amani. Tunawaombea pia, mapadre wawili ambao ni Pd. James Mbwama wa Jimbo la Mbeya, ambaye aliaga dunia akiwa hapa Italia na Pd. Amon Kibunga wa Shirika la Wasalvatoriani ambaye aliaga dunia akiwa Tanzania. Tumewapoteza pia wazazi wetu yaani Mzee Dastan Mpangile Baba mzazi wa Pd. Revocatus, Bi Agnes, Mama mzazi wa Pd Juvenalis Wengaa wa Jimbo la Arusha, Sweetbert Kamugisha, kaka yake Pd Venance Rweyunga wa White Fathers, Placide Mdoga, kaka yake na Sr Honorina wa masista wa Ivrea na Bi Severina Ncharukula, mama mzazi wa Frt Coelestine Mahurage. Tunaomba Mungu awajalie raha ya milele mbinguni.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu, yafaa kukupeni kidogo juu yaumoja wetu, umoja wetu huu ni kati ya jumuiya mbalimbali zilizopo hapa Italia na unaitwa UMOJA WA WANAFUNZI WAKATOLIKI WANAOSOMA ROMA. Ni umoja ambao unayo katiba, na malengo yake ni kuwaunganisha Wanafunzi wawe familia moja na kwa namna hiyo kuanza kujenga network ya kichungaji. Ni katika kukuza umoja wa kichungaji pia wajisikie utaifa wa taifa letu la Tanzania na hasa wanapokabiliana na changamoto ya dunia kuwa kama kijiji kimoja.
Ni umoja unaotaka kuimarisha misingi ya amani ya nchi yetu na pia kutoa sura angavu ya nchi yetu hapa Italia. Umoja huu hujiendesha kwa michango ya wanachama wenyewe katika hali yao nyeti ya uanafunzi wakisaidiwa na WALEZI WAO pamoja na WAFADHILI. Walezi na Wafadhili ni wale wafanyakazi watanzania walioko hapa Roma. Mhashamu Baba Askofu Mkuu tunaamini kuteuliwa kwako ni zawadi nzuri kwetu, tayari unachukua nafasi ya Mlezi Mkuu, nasi tunasema asante kwa Mungu na kwa Baba Mtakatifu.
Tunapenda kutoa shukrani za pekee kwako Baba Askofu Mkuu, kwa Ibada ya Misa Takatifu kwa kile kitu chema ulichotulisha, tumekula na kushiba na sasa ni kazi yetu kukitumia katika kujenga maisha na utume wetu . Kwa hakika amejitoa kwa furaha ili tuweze kufurahia na kujazwa na Neno la Mungu. Baba asante sana kwa kazi njema.
Shukrani za pekee zimwendee Baba Mwadhama Polycarp Kard. Pengo kwa kukubali kuja kushiriki nasi furaha hii. Baba Mwadhama asante sana. Tunatoa shukrani za pekee kwa Baba Askofu Libena kwa kuja kushiriki nasi furaha hii. Tunachukua nafasi hii pia kukupongeza kwa kuteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Askofu mwanzilishi wa Jimbo la Ifakara. Mungu akupe afya njema na akujalie utume wa kutukuka.
Mwisho nawapongeza wote kwa mwitiko makini na wa nguvu kwa ajili ya maadhimisho haya ya furaha, Mungu azidi kuwabariki na kuwaimarisha katika maisha yenu yote. Ninawakaribisheni katika sehemu ya pili ya sherehe ambapo Baba Askofu Mkuu, Baba Mwadhama na Mhashamu Libena watapata nafasi ya kutoa Neno la kutujenga sisi sote wanafamilia ya Mungu.
Imeandaliwa na Mwenyekiti wa Wanaumoja
Padre Richard Tiganya , C.PP.S.
14-10-2012.

http://sw.radiovaticana.va/storico/2012/10/25/siku_ile_wanafunzi_wakatoliki_watanzania_wanaosoma_roma_walipokutan/kws-632851
Harrah's Resort SoCal Casino - Mapyro
ReplyDeleteFind Harrah's Resort SoCal 제천 출장샵 Casino, United States, United States, ratings, 수원 출장샵 photos, prices, expert advice, traveler 강원도 출장샵 reviews and tips, and more information from Rating: 안성 출장안마 4.3 · 인천광역 출장안마 8 votes · Price range: $$