WARAKA KWA MWANASHERIA MKUU WA TANZANIA JUU YA JINSI SERIKALI YA CCM ILIVYOLISHGHULIKIA VIBAYA SUALA LA MIHADHARA YA WAISILAMU
Bismillahir Rahmanir Rahiim
A. Aziz
S.L.P. 2847
Dar es Salaam
S.L.P. 2847
Dar es Salaam
Mwanasheria Mkuu,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
S.L.P. 9050,
DAR ES SALAAM
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
S.L.P. 9050,
DAR ES SALAAM
Kwa Ridhaa yako Mh. Mwanasheria Mkuu,
YAH: MAKASISI WAKATOLIKI, SERIKALI YA CCM NA HAKI YA WAISILAMU YA KULINGANIA
NA KUTANGAZA DINI
"....(Watu) hawa ni wa kupingwa kwa njia zote na kwa kila hali. Maana,
hata kama wanasema lililo kweli, hata hivyo, yule aipendae kweli asikubaliane
nao. kwani si (vitu) vyote vilivyo kweli ndiyo kweli. Wala ile kweli inapoonekana
(tu) kuwa ni kweli kwa mujibu wa maoni ya wanaadamu isichukuliwe badala
ya kweli iliyo kweli, ambayo ndiyo ile iliyo kwa mujibu wa imani."
Askofu Clement wa Alexandria (c.AD 150-215) alisema katika barua aliyomuandikia
mwanafunzi wake (aliyeitwa The Odore) katika kuikanusah Injili ya siri
ya Marko ("Secret Gospel" kilichoandikwa na Profesa Morton Smith wa Chuo
Kikuu cha Columbia).
"Ili tuweze kuifikia kweli katika vitu vyote, lazima siku zote tuwe
tayari kuamini kuwa kile kinachoonekana kwetu kuwa ni cheupe, ni cheusi,
kama uongozi wa kanisa unaelekeza hivyo." St. Ignatius Loyola, muasisi
wa Taasisi ya Kijesuit ya Kanisa Katoliki, ameagiza katika kitabu chake
"Spiritual Exercises."
Siku za Alkhamisi, tarehe 12 ya Februari 1998 na Ijumaa, tarehe 13 ya
Februari 1998, bila ya shaka zitakumbukwa katika historia ya Tanzania kama
mojawapo ya madhihirisho ya matukio ya kuchukiza yaliyoonyesha jinsi nguvu
za dola zilivyotumiwa kuwatisha na kuwanyamazisha Waisilamu katika kueneza
dini yao kwa uhuru, wakiingiliwa na kupondewa haki zao walizopewa na Mungu
na za kikatiba.
Waisilamu waliuliwa, walifanywa vilema, walikamatwa na walipigwa kinyama
na polisi wa vikosi vya kuzuia fujo (FFU) kwa hakika, hatua zilizochukuliwa
na serikali ya CCM, pamoja na matamshi ya viongozi wake yaliyofuatia, zimeiharibia
sana hadhi yake mbele ya macho ya Waislamu na Watanzania wote wapenda uhuru;
na itachukua muda mrefu kuirejesha tena hadhi hiyo.
Hakuna anayehoji haki ya serikali ya kuwapeleka askari wa kikosi cha
kuzuia fujo siku ile ya tarehe 13, pale mambo yalipokwisha kuharibika na
Watanzania wa imani na itikadi zote kujiingiza kwenye mlipuko uliokuja
geuka na kuwa mapambano na fujo dhidi ya serikali ya CCM: tazama jinsi
yalivyokuwa yameshambuliwa magari ya serikali na ya mashirika ya Umma tu,
na idadi ya Wakristo pia waliokamatwa katika kamata-kamata ya polisi.
Lakini ingawa ni kweli kuwa serikali ilikuwa na haki ya kikatiba na
kisheria kupeleka askari wa kuzuia fujo kwa ajili ya kuhifadhi amani na
usalama, mtu lazima ahoji hatua ya kibabe babe tu, isiyo na haki ya kisheria,
iliyochukuliwa na serikali ya CCM siku ya Alhamisi tarehe 12 Februari,
ya kuvunja milango na kuingia kwenye msikiti wa Mwembechai.
Lilikuwa tendo hili, ambalo halikuwa chochote bali uamuzi wa kibababe
tu wa kuingilia uhuru wa watu katika dini, ambalo ndilo hasa lilikuwa cheche
iliyoanzisha msululu wote wa matukio yaliyofikia kwenye mlipuko wa siku
ya Ijumaa ya tarehe 13.
Matokeo ya tendo lile, pamoja na hatua ya askari polisi kuingia msikitini
kwa vitisho huku wamevaa viatu, wakikamata na kuwashambulia watu waliokuwa
wanaswali humo, bila ya kuthamini kabisa na kuheshimu utakatifu wa jengo
lile na hisia za Waisilamu, yasipuuzwe.
Ikumbukwe kuwa kwa uchache kabisa kuwa tendo la polisi la kuingilia
utakatifu wa msikiti linaingilia nafasi na thamani tunayowekea utakatifu
huu katika jamii yetu kisheria na kisiasa. Hakuna jambo litalo chafua
na kulipua hisia za waumini, kama kuingia kwa kukufuru na najisi majumba
ya ibada.
Ni wazi serikali ya CCM inawataka Watanzania na watu wengine duniani
kuamini kuwa matendo yake yalikuwa halali kwa sababu Waisilamu walivunja
sheria kwa kuendesha mihadhara ya kashfa dhidi ya Ukristo na kwa namna
hiyo kuhatarisha amani na utulivu nchini Tanzania.
Kutokana na matamshi ya viongozi mbali mbali wa CCM na serikali ni dhahiri
kuwa serikali ya CCM inajaribu kutuuzia bango la bandia la "Uisilamu wa
Siasa kali." Serikali ya CCM inadai kuwa "Siasa kali" hii, ikiachiwa ienee,
itaizamisha nchi katika fujo na kutokuwapo amani kama inavyotokea kwenye
nchi kama Algeria, Somalia, Burundi na Lebanon.
Ni jambo la kuzingatiwa kuwa serikali ya CCM haiko peke yake katika
mashambulizi haya ya kisasa dhidi ya Waisilamu wa Tanzania. Vyombo vya
habari vya nchini navyo vimeyapokea mashambulizi haya kwa kutumia uandishi
wa habari kwa kutoa taarifa zinazochanganywa na mawazo binafsi ya kijuujuu
yaliyo na hisia za mashambulizi dhidi ya Uisilamu, na kuingiza majina na
maneno yale yale yaliyosukwa na kutayarishwa nchi za Magharibi, kama vile
"fanaticism" (uhemkwaji), "fundamentalism" (siasa kali) "extremism" na
"radicalism," yote yakiwa yamedhamiriwa kuupotosha Uisilamu na kuuonyesha
kuwa ni tishio kwa amani ya Tanzania.
Vyombo vya habari vya nchini kwa kujiingiza katika mtego wa kutumia
maneno yaliyojengewa maana mbaya kwa makusudi kama "siasa kali," vilijifunga
na kujilazimisha kusimama katika maamuzi ya upande mmoja, na kwa hiyo hawakuweza
kupata mizani sahihi na kuelewa hali kama ilivyokuwa kuhusu sababu halisi
zilizopelekea kwenye mlipuko wa Mwembechai.
Kwa sababu ya mawazo waliyokuwa nayo tayari kutoka kwa "Orientalists"
na mitazamo ya kiadui dhidi ya Uisilamu kutoka vyombo vya habari vya nchi
za Magharibi, na upotoshaji dhidi ya Uisilamu pamoja na upungufu wao wenyewe
juu ya dini ya Uisilamu, vyombo vya habari vya nchini vimekuwa vinaelekea
upande mmoja na vyenye msimamo wa uadui katika kuripoti mambo ya Mwembechai.
Kwa hiyo picha waliyoitoa ya Uisilamu na Mwembechai, licha ya kuwa ni
ya kupendelea upande mmoja, ni ya kutiwa chumvi na upondaji. Tangu hapo
upondaji ndio unaoleta biashara ya kuliuza gazeti.
Si magazeti yote yalichukua mwenendo huu. Kulikuwa na mengine ambayo
hayakujiingiza kwenye mtego huu. Mhariri wa "The African", Asha
Mzava kwenye gazeti la "The Guardian" na Makwaia wa Kuhenga kwenye
"The Guardian" na "Majira", ingawa hawakuzitambua sababu za
msingi na kwa hiyo wakawa na upungufu katika uchambuzi wao, walinasihi
na kuwaidhi serikali iwe na uangalifu, kujizuia na kuwa makini.
Mbali na magazeti yote, na lililojitokeza wazi wazi, lilikuwa gazeti
la Kiisilamu la kila wiki "AN-NUUR" ambalo kwa makala na maandishi
mengine mbali mbali kutoka kwa wasomi wa Kiisilamu na Waisilamu wengine
wa kawaida kila wiki mfululizo limekuwa likisisitiza kuwa kilichokuwa kiini
cha yote, na kinachopuuzwa si chochote bali uhuru wa Waisilamu kuitangaza
Dini yao.
Kwa hakika kama watendaji wa CCM wangekuwa waadilifu na watu wapendao
kusoma na wangelisoma gazeti la "AN-NUUR" bila upendeleo na kuathiriwa
na mawazo finyu, pengine wangelishughulikia suala la Mwembechai kwa njia
ya udilifu na fikra sahihi.
Lakini kwa maoni yangu, labda mshiriki mwenza na muhimu sana wa serikali
ya CCM katika kampeni hii dhidi ya Waisilamu umekuwa uongozi wa Kanisa
Katoliki. Haiwezi kukatalika kuwa ni uongozi wa kanisa Katoliki ambao
ndio uliochochea serikali ya CCM kuwachukulia hatua wahubiri wa Kiisilamu.
Tangu mwaka 1993 uongozi wa kanisa Katoliki umekuwa ukiyashambulia kwa
nguvu kweli kweli mahubiri ya Waisilamu wakidai kuwa wahubiri wa Kiisilamu
na Waisilamu "wenye siasa kali" mamekuwa tishio la amani nchini Tanznaia.
Tangu mwaka 1984 Waisilamu walipoanza kuwalingania watu kwenye Dini ya
Uisilamu kwa kutumia taaluma linganifu katika Dini, na kutokana na Wakristo
wengi kusilimu na kurudi kwenye Uisilamu, uongozi wa kanisa Katoliki umekuwa
ukiishinikiza serikali kupiga marufuku mihadhara ya Waisilamu, wakidai
kuwa ilikuwa inakashifu na kutukana Ukristo.
Ni muhimu kuzingatia kuwa ingawa uongozi wa Kanisa Katoliki umekuwa
ukiisukuma serikali kuifungia mihadhara ya Waisilamu tangu mwaka 1993,
serikali ya CCM imeongeza kasi yake ya kukamata wahubiri wa Kiisilamu tangu
Januari 1998.
Hatua hii ya serikali inaonyesha kuwa hii ilikuwa kampeni iliyopangwa
na kutekelezwa kwa uangalifu. Sidhani kuwa kampeni hii inayopendelea hadi
hii leo ilitokea na kuanza kwa bahati tu pale padri wa Parokia ya Mburahati
alipoitupia serikali changamoto kwenye tangazo la radio lililotolewa kwenye
Radio Tumaini, inayoendeshwa na Kanisa Katoliki, siku ya tarehe 8 Februari
1998. Padri Camillus Lwambano aliitupia changamoto serikali iache kutoa
ahadi tupu tu, ipige marufuku mahubiri ya kashfa na kuwachukulia hatua
kali wahubiri wa Kiisilamu. Padri Lwambano aliitaka serikali itamke wazi
wazi kuwa imeshindwa kuzuia mahubiri ya kashfa. Lilikuwa tangazo la uchokozi.
Bali pia lilikuwa tangazo lililo ashiria hatari.
Hapana shaka kuwa Padri Lwambano alipata matumaini na nguvu kutokana
na kauli za hadhara za kuwaunga mkono zilizotolewa na viongozi wa serikali
ambazo uongozi wa kanisa Katoliki walizipata kuhusiana na malalamiko yao
dhidi ya mahubiri ya Waislamu.
Tarehe 4 Januari, 1998 mjini Tabora kwenye sherehe za Jimbo la Magharibi
la Kanisa la Moravian, Rais Mkapa alitangaza vita dhidi ya "watu wanaopita
pita wakigawa kaseti, vijitabu na kuendesha mikutano ambamo wanatukana
na kukejeli dini nyingine" (Daily News la tarehe 5 Januari 1998). Ni wahubiri
wa Kiisilamu tu ndio wanaotumia kaseti na vijitabu, pamoja na mihadhara,
kwenye shughuli zao za kueneza Dini.
Ni maoni yangu kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya CCM zina udini
na za kuegemea upande mmoja. Tukichukua ukweli kwamba uongozi wa Kanisa
Katoliki ulishindwa kuthibitisha madai yao ya kashfa katika mkutano wa
Maaskofu na Masheikh ulioitishwa na Rais Mstaafu Mwinyi mwaka 1993.
Iwe iwavyo, kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba serikali ya CCM inaonyesha
kutokujali kabisa wajibu wake wa kuheshimu katiba na sheria za nchi. Serikali
ya CCM inaweza ikaelezea haja yake ya kutaka kuona kuwa haki na uhuru wa
kuabudu wa Watanzania wote vinalindwa, na kwamba sheria za nchi zitaheshimiwa
na kufuatwa kuwawezesha watu kuabudu, kuhubiri na kuendesha shughuli zao
za dini kwa uhuru. Ukweli wa mambo ni kwamba serikali ya CCM imechukua
hatua kiubabe-ubabe na wala haionyeshi kuelewa kiwango cha uzito na hatari
ilichokikaribishia nchi yetu. Kwa kuonyesha upendeleo, na kukubali kuhadaiwa
na uongozi wa kanisa Katoliki kuwa maombi ya Waisilamu yanautukana Ukristo,
serikali ya CCM imejiingiza katika mstari wa utendaji nchini ambao unaingilia
haki za Waisilamu kutangaza Dini yao, imekuwa ya utendaji wa kiubabe-ubabe
na wala haijali kufuata utaratibu wa kwenda kwa sheria.
Mahubiri ya Waisilamu yamepigwa marufuku. Waisilamu wanasumbuliwa
na wanakamatwa kinyume na sheria. Waisilamu wanauawa na kutiwa vilema.
Misikiti ya Waisilamu inaamrishwa kufungwa. Kwa kosa gani? Kwa sababu tu
Waisilamu wanasema kwamba Mungu ni mmoja, na hana mwana, mshirika au aliye
sawa naye!
Mh.Rais Mkapa alianza kazi yake na madai kuwa utawala wake ungekuwa
unafuata utawala wa sheria, kwa uchache hii maana yake ni kuwa, kila kitu
kingekuwa kitendeke kwa mujibu wa sheria. Badala yake tulicho nacho ni
serikali ya CCM kuvunja ahadi zake na kuingia kwenye utawala wa kutumia
nguvu za dola kiubabe-ubabe. Hivi ndio tuelewe kuwa kwa kila kinachowahusu
Waisilamu na Uisilamu, masuala ya utawala wa sheria na haki hayamo? Wasilamu
si raia wa Tanzania wanaostahili kupata haki na nafasi zote zilizomo kwenye
katiba na sheria nyingine za Tanzania.
Nimesema kuwa hatua za mabavu zilizochukuliwa na serikali ya CCM dhidi
ya Waislamu na mahubiri ya kiisilamu ni kinyume na katiba za udini, na
kwamba zilichochewa kwa makusudi na uongozi wa kanisa Katoliki katika kampeni
ya udanganyifu kwamba mahubiri ya Waisilamu ni ya kashfa. Ni vizuri, kwamba
itasaidia, kuingia tutazame kwenye dhati ya mahubiri ya Waisilamu tuone
kama kulikuwa na uvunjwaji wa sheria kutokana na mahubiri hayo, tuingie
pia kwenye jinsi uongozi wa kanisa katoliki ulivyoyachukulia mahubiri ya
Waisilamu; na jinsi serikali ya CCM ilivyoupokea uchochezi wa uongozi wa
kanisa katoliki.
Nimesema kuwa uongozi wa Kanisa Katoliki umeichochea serikali iyapige
marufuku mahubiri ya Waisilamu kwa madai kuwa yamekuwa yakikashifu na kutukana
Ukristo. Ni muhimu kwa hiyo, kuutazama, kwa ufupi na kuona nini inaweza
kuwa kashfa, kabla ya kuingia kwenye suala la mihadhara ya Waisilamu; inayoitwa
kanisa Katoliki, serikali ya CCM na vyombo vya habari kuwa ni kutukana,
kukashifu, michafu, ya kupakazia na kukejeli hadhi ya mengine.
("Definition") maelezo bayana ya kashifa
"Concise Oxford) English Dictionary" inaielezea kashfa/kufuru (blasphemy)
kuwa ni kusema kwa kutoyaheshimu mambo matakatifu; kusema kukufuru kuhusu
jambo; kutusi, kwa mujibu wa "Osbern law Dictionary" kashfa/kufuru ni kusema
kwa kukejeli hadharani au kwa makosa ya jinai juu ya mambo yanayomuhusu
Mungu, Yesu Kristo, Biblia .... kwa dhamira ya kuleta dharau na chuki dhidi
ya Kanisa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Kwa jumla kufuru/kashfa inaelezeka kuwa ni pale yanaposemwa mabaya juu
ya Mungu kwa lengo la kukejeli ili kushusha hadhi ya utukufu wa Mwenyezi
Mungu na kuyaondoa mawazo ya watu kwenye kumcha na kumpenda Mungu. Ni kutumia
maneno juu ya Mwenyezi Mungu makusudi kwa dhamiri na mpango wa kuzuia na
kuvunja heshima, unyenyekevu na imani anayoistahiki kama Muumba, mjuzi
wa kila kitu, mtawala na mhukumu wa dunia. Inaleta dhana ya kupuuza, inapotumika
juu ya Mungu, kama vile dharau mara kwa mara inavyokuwa na dhana hiyo pale
inapotumiwa juu ya mtu binafsi. Ni kwa makusudi na kwa nia mbaya kujaribu
kumuondolea mwanaadamu unyenyekevu wake kwa Mola wake kwa kukana kuwepo
kwake, au sifa zake kama Muumba mjuzi wa kila kitu, mtawala na anayehukumu
watu wote na kuwazuia watu wasiwe na imani naye.
Lazima kutofautisha baina ya kashafa/kufuru na uzurishi (heresy), ambayo
"Osborn Law Dictionary" inaielezea kuwa ni kosa la kanuni za kidini linalotokana
na mtu kuwa na mawazo ya uongo yanayochukiza na yasiyokubalika kwa kuhalifu
nguzo mojawapo ya imani ya Kikristo.
Kushambulia "kweli" ya Ukristo si kosa kwa mujibu wa common law.
"Digest of Criminal Law" (9th edition) ya Stephen inasema sheria ya
kashfa/kufuru kwa mujibu wa "common law" iko kama ifuatavyo: "Kila andiko
linahesabika kuwa ni kashfa pale linapokuwa na jambo lolote ambalo linadharau,
linatukana au linakejeli Mungu, Yesu kristo au Biblia au Kanuni za Kanisa
la Uingereza kama ilivyowekwa na sheria. Si kashfa kusema au kuandika na
kutoa mawazo ambayo yanapingana na dini ya Kikristo, au kukana kuwapo kwa
Mungu, kama matamshi/maandishi yenyewe yanayotolewa kwa lugha yenye heshima
na iliyo ya kistaarabu. Kipimo cha kutumia ni kutazama namna ya jinsi itikadi
zenyewe zinavyoelezewa na siyo juu ya kile kilichomo ndani ya itikadi hizo"
(msisitizo unaongezwa).
Katika kesi baina ya Bowman dhidi ya Secular Society (1917) Bunge la
juu la Uingereza (House of Lords) liliamua kuwa kuishambulia au kuikana
kweli ya Ukristo, bila ya kutia matusi, kejeli au utovu wa hesima juu ya
mambo matakatifu, si kuvunja sheria. Na kwenye kesi baina ya R na Lemon
(1979) ambapo wachapishaji wa gazeti la "Gay News" walipitisha shutuma
za kashfa zilizokuwa na maneno yaliyodhaniwa kukasirisha na kutukana hisia
za mkristo (kiasi ninavyomuheshimu na kumpenda Bwana Yesu (AS) siwezi kuyarudia
yale yaliyosemwa. Mahakama ya Rufaa iliamua kuwa kauli inaweza kuwa ya
kashfa kama hoja yake imekuwa ya kuumiza na kutukana; ikijiegemeza siyo
kwenye matumizi ya akili, bali kwenye hisia za kinyama na zisizo za kuungana
na maumbile ya mwanadamu. Baadaye kwenye kesi hiyo hiyo Bunge la juu ya
Uingereza likasisitiza kuwa, katika mashauri ya kashfa, kipimo kimo katika
uwezekana wa kukasirisha na kutukana na siyo uwezekano wa kuvunjika kwa
amani.
Kwa hiyo inajulikana na kukubalika kuwa kwa mujibu wa common law
si kashfa kushambulia misingi ya dini kama kanuni za kuweka heshima
na uungwana katika malumbano zitafuatwa. Kwa kweli Tume ya Sheria ya Uingereza
iliamua mwaka 1985 kuwa common law si chombo kinachofaa kuhakikisha
kuwa imani za dini zinaheshimiwa, na kwamba kosa la kashfa chini ya kanuni
za common law lifutwe hasa kwa sababu yamewekwa makosa mengine katika
sheria yanayoshughulikia mwenendo mbaya unaoingilia ibada za hadhara, au
mwenendo wa kutukana wafuasi wa vikundi mbalimbali vya dini ambao unaweza
kuletea kuvunjika kwa amani. Inahusika hapa kuzingatia kuwa nchini Uingereza
mashitaka dhidi ya makosa ya kashfa yamekuwa machache na kwa kweli kesi
ya lemon imekuwa mashitaka ya kwanza baada ya miaka sitini.
Sheria ya kashfa ina uhusiano wa karibu na haki ya msingi ya uhuru wa
dini. Kila mtu ana uhuru wa mawazo, uhuru wa nafsi na uhuru katika dini.
Ingawa uhuru wa dini umechanganya ndani yake haki ya kuitekeleza imani
kwa ibada na matendo, au kwa kufundisha na kutangaza sheria inaweka mipaka
kwa kiasi kile inavyolazimu kuhifadhi usalama wa umma, utaratibu katika
jamii, au maadili, au hali za msingi za watu wengine. Kwa hiyo kile kisichokatazwa
kinaruhusiwa mradi tu hakizuiliwi na sheria nyingine. Kwa mfano, katika
kosa la jinai ndani ya sheria ya kashfa. Hii haina maana, hata hivyo, kuwa
kile kinachoonekana kweli kwa wafuasi wa dini moja au kwa serikali inayoitetea
kwa niaba yao, kinaweza kwa madhumuni ya dini, kulazimishwa juu ya raia
wenye imani inayopingana na dini hiyo. Sheria inalinda makundi ya dini
yasitishiwe na ukandamizaji wa makundi mengine ya dini. Kwa hiyo mradi
tu udadisi na kuhoji, si kitu kuwa kinasumbua misimamo iliyopo tangu zama
kiasi gani inakuwa kwa ajili ya kutafuta na kufikia kweli hakukuwa kwenda
kinyume na sheria. Watu hawawezi kuadhibiwa kwa kufanya mambo yaliyo ndani
ya sheria kwa sababu tu kundi jingine la watu linalalamika.
Sheria za makosa ya jinai nchini Tanzania kwa msingi zimechukuliwa kutoka
sheria za Waingereza; sehemu kubwa ya Penal Code kutokana na "Draft Code"
ya Sir James Fitzjames Stephen ya mwaka 1878. Miaka ilivyopita kulifanyika
mabadiliko yaliyolazimishwa na matakwa ya hali halisi nchini. Kwa mfano
kwenye makosa ya jinai yanayohusiana na uhuru wa dini, sehemu zote zinazomtaja
Yesu Kristo, Ukristo na Kanisa la Uingereza, zilifutwa, bila ya shaka kwa
sababu ya kutambua kuwa Tanzania, hapo sheria hii ilipowekwa ni nchi ya
mchanganyiko wa urithi wa dini nyingi na tamaduni mbalimbali.
Hali halisi hii haijabadilika; sababu zilizopelekea kuwako kwa hali
halisi hii hazijabdilika. Kwa hiyo kifungu cha 129 cha "Penal Code" kinachoainisha
makosa ya jinai kwenye uhuru wa dini kama unavyotolewa na kifungu cha 19
cha katiba ya Jamhuri ya Muungano kinaeleza kuwa "Mtu yeyote ambaye, kwa
dhamiri za makusudi za kutaka kuumiza hisia za mtu yeyote, anatamka neno
lolote, au anatoa sauti yoyote inayosikiwa na mtu huyo, au anatoa ishara
yoyote inayoonekana na mtu huyo, atakuwa amefanya kosa."
Hatia ya kosa la kutamka maneno kwa dhamiri ya kuumiza hisia, inategemea
ushahidi kuwa maneno hayo yalitamkwa kwa dhamiri ya kuumiza hisia na kwamba
maneno hayo kweli yameumiza hisia.
Kwa hiyo, tukizingatia urithi wetu Tanzania wa kuwa na wananchi wa mchanganyiko
wa dini mbalimbali si kosa la jinai kwa ukristo kusema kuwa Yesu ni Mungu
au ni mwana wa Mungu, huo ukiwa ndio msingi wa imani ya kikristo. Wala
siyo kosa kwa Muisilamu kusema kuwa Yesu si Mungu au Mwana wa Mungu, hii
ikiwa nguzo katika imani ya Uisilamu kwamba Mungu ni mmoja tu na hakuna
waliosawa naye washirika, au wana. Si kosa vile vile kwa mkristo kusema
kuwa Yesu alisulubiwa na akafufuka; hii ikiwa msingi katika Ukristo. Na
wala si kosa kwa Muisilamu kusema kuwa Yesu hakusulubiwa wala hakufufuka;
hii ikiwa ni sehemu ya imani ya Uisilamu kwamba hakuna kutolewa muhanga
kwa ajili ya kufuta dhambi za wengine. La kweli ni kuwa kilicho kufuru
kwa Ukristo si kufuru katika Uisilamu na kilicho kufuru kwa Uisilamu si
kufuru kwa Ukristo.
Kuonyesha kuwa kifungu cha 129 hakikudhamiria kutafasiriwa kwa mujibu
wa imani ya kikristo au ya kiisilamu hebu tuutazame mfano mmoja miongoni
mwa mifano mingine chungu nzima ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Waisilamu.
Mfano huu, kwa kweli, unadhihirisha jinsi madai ya viongozi wa Kanisa Katoliki
yalivyo ya uongo, na kwa nini mihadhara ya Waisilamu si ya kashfa kama
inavyong'ang'anizwa na viongozi wa Kanisa Katoliki, serikali ya CCM na
vyombo vya habari nchini.
Kesi hii inawahusu wahadhiri wa Kiisilamu wale waliokamatwa tarehe 5
September 1996 kama ilivyoripotiwa na gazeti la "Daily News" la tarehe
6 September 1996; gazeti la serikali lenye sifa ya kubanwa sana katika
utoaji wake wa habari. Zingatia kuwa mwandishi wa serikali, katika habari
hiyo hiyo, anawaita washitakiwa mara mbii "Muslim Radicals" na "Muslim
Fundamentalists", "Waisilamu wenye siasa kali," kana kwamba washitakiwa
walikuwa wameshitakiwa kwa kuwa "maradical" na "wenye siasa kali", na sio
kwa hicho walichodhaniwa wamekifanya au wameacha kukifanya. Ni dhahiri
kuwa kwa mwandishi huyu na mhariri wake, si kitu kuwa yale yalikuwa ni
mashitaka tu bado, kwamba kulikuwa hakuna lolote lililokwisha thibitishwa
mahakamani dhidi ya washitakiwa, na kwamba kesi yenyewe ilikuwa bado iko
mahakamani na kwa hiyo haki isingetendeka kama washitakiwa wangeanza kupewa
majina ya namna hiyo.
Kwa waandishi hawa wa serikali waliokuwa na msimamo wa upendeleo wa
upande mmoja tayari, kilichokuwa muhimu ni kauli za kuvutia na hamu ya
kutaka kuandaa umma kwamba "maradical" na "mafundamentalisti" wa kiisilamu
wale wako kwenye "jihadi". Iwe iwavyo, taarifa hii inaendelea kusema kuwa
washitakiwa walitamka maneno ya kupinga Ukristo, kwenye hotuba yao ndani
ya msikiti wa Keko Magurumbasi mjini Dar es Salaam tarehe 4 Septemba 1996,
"yaliyodhamiriwa kuumiza hisia za Wakristo." Taarifa ile inaongeza kusema
kuwa washitakiwa wanasemekana kusema kuwa "Yesu Kristo hakuwa Mungu kama
inavyoelezwa kwenye itikadi ya Utatu Mtakatifu" Hakuna Muisilamu atakayeongeza
kwenye madai yake kwamba Yesu si Mungu maneno ya kauli za imani ya Kanisa
Katoliki ambazo yeye mwenyewe hakubaliani nayo.
Kiini cha mashitaka dhidi ya wahubiri wa kiisilamu ni kwamba walikataa
Uungu wa Yesu. Nasema kuwa hii yenyewe si kashfa wala kosa linalokusudiwa
na kifungu cha 129 cha sheria za Jinai. Ingawa inawezekana iwe kweli kuwa
kusema Yesu si Mungu kunaweza kuwa upingaji katika Ukristo, si kosa kwa
mujibu wa kifungu cha 129 au hata kuwa kashfa kwa; mujibu wa common
law kukana Uungu wa Yesu. Kwa Waisilamu, kwa mujibu wa Qur'an, Yesu
(AS) si Mungu bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwa kweli ni kufuru kusema
kuwa Yesu ni Mungu!
Tunaliona tatizo, kwa hiyo, la kukitaja sisi kifungu 129 maalum kwa
kufuata imani ya Kikatoliki. Nadhani linalotakiwa na kifungu cha 129 ni
zaidi ya hivyo tafsiri yake ni kama ile ya kesi ya Uingereza ya Lemon (1979)
niliyoitaja hapo mwanzo. Hakuna dhamiri mbaya au ya utovu wa heshima katika
kusema kuwa Yesu si Mungu. Kwa dhati kabisa huku ni kutafuta kuifikia kweli.
Na kuihoji kweli ya Ukristo hakuwezi kwenyewe, peke yake, kuwa msingi wa
kuendeshea mashtaka juu ya kosa la kashfa au kutamka maneno kwa dhamiri
ya kuumiza hisia za kidini. Vile vile, si kosa chini ya kifungu 129 kwa
Muisilamu kusema kuwa Biblia sio neno la Mungu, kwa sababu imani hii ya
Waisilamu inatokana na Qur'an inayosema kuwa mafundisho ya Manabii waliopita
yaliyomo kwenye maandiko yameingizwa mikono ya watu na kuchafuliwa na watu
ambao walikuwa hawaiamini dini ya Tawhid.
Lakini litakuwa kosa la jinai kusema Biblia au Qur'an ni takataka;
au kwamba Wakristo au Waisilamu ni wajinga, na kwamba Mtume Muhammad (SAW)
alikufa kwa ukimwi. Maana hakuna lolote la kisomi kwenye kauli hizi, isipokuwa
matusi yanayofurahisha hisia za maumbile ya kinyama.
Inatuhusu hapa kuzingatia kuwa kwa mujibu wa Criminal Procedure Act
ya 1985, kosa la makusudi kusema maneno yanayodhamiria kuumiza hisia za
kidini ni kosa linalohitaji waranti katika kumkamata mkosaji, na waranti
unatakiwa utolewe na hakimu pahali pa kazi kufuatia malalamiko, kabla mtu
hajakamatwa. Hii maana yake ni kwamba, kwa; maneno mepesi, kabla mtu yeyote
hajakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la makusudi kusema maneno yaliyodhamiria
kuumiza hisia za kidini, kwanza mtu lazima apeleke malalamiko yake na yatiliwe
mkazo kwa kiapo kwenye mahakama kabla ya waranti wa kumkamatia mtu haujatolewa.
Kwa hiyo ni kwenda kinyume cha sheria kumkamata mtu ambaye hakuna shitaka
lililotayarishwa au waranti wa kumkamatia kutolewa. Inafaa kuzingatia kuwa
polisi wa Tanzania hawajafuata utaratibu huu hata mara moja katika harakati
zao za kuwakamata wahubiri wa Kiisilamu, jambo ambalo linadhihirisha ama
kutojua kazi kwao, au hisia zao za udini.
Waite (watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema, na
ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea
katika njia yake, naye ndiye anayewajua walioongoka. (16:125)
Na ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu,
na akafanya vitendo vizuri na kusema; "Hakika mimi ni miongoni mwa Waisilamu.
(41:33)
(41:33)
Kuhubiri dini ni haki iliyotolewa na Mungu na kutambuliwa na kifungu
cha 19 cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Uisilamu, tangu mwanzo wa kuwapo kwa mwanadamu
duniani, dini ya kweli, au mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, daima umekuwa
mmoja. Watu wameuacha au wameuchafua mwongozo huu.
Mitume wa kweli wameletwa kuuhuisha na kuutakasa mwongozo huu. Bali
watu wa mataifa mbalimbali walipelekewa Mitume hawa mara kwa mara wamekuwa
wakibuni "michanganyiko" yao wenyewe, au dini, kutoka vyote viwili, kutoka
yale yaliyo kweli na kutoka yale yaliyokuwa yao wenyewe; nyongeza au tungo
zao.
Kwa kiasi kile walichukua yaliyo ya kweli tunapata mambo yanayofanana
katika "michanganyiko" mbali mbali, au dini nyingine mpya. Kwa kiasi kile
waliongeza mambo yao wenyewe tunapata tofauti kwenye "michanganyiko" au
dini.
Dini pekee ya kweli daima imefundisha imani juu ya utii kwa Mwenyezi
Mungu mmoja, na huo ndio Uisilamu. Kwa mujibu wa Qur'an hakuna dini za
kweli, ipo Dini ya kweli. Na manabii wote wametuita kwenye dini moja; kwenye
njia moja na lengo moja:
Amekupeni sheria ya dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tuliyokufunulia
wewe na tuliyowausia Ibrahimu, Musa na Issa; kwamba simamisheni dini wala
msifarakane kwayo.(42:13)
Dini ya kweli, au Uisilamu, daima imekuwa kitu kimoja wakati wote na
sehemu zote. Kauli kama "Uislamu umekuwa wa mwisho miongoni mwa dini zilizofunuliwa"
ni kauli ya makosa.
Manabii wote walikuwa Waisilamu ambapo maana yake wale wanaojisalimisha
kwa Mwenyezi Mungu. Ujumbe wao ulikuwa Uislamu; kuwaita watu wamuabudu
na kujisalimisha kwa Mungu mmoja tu. Adam alikuwa Muisilamu, Ibrahimu alikuwa
Muisilamu, Musa alikuwa Muisilamu, Issa alikuwa Muisilamu, Rama, kama alikuwa
Mtume wa kweli, alikuwa Muisilamu.
Mahubiri ya Waisilamu yanatokana na msimamo huu. Kutokana na kujua kuwa
hata baada ya mtu kufanya makosa na madhambi na kupotea njia, mwanadamu
bado ana nafasi na uwezo wa kurejea kwenye asili yake inayomtafuta Mungu;
kurejea kwenye njia iliyonyooka (dini ya kweli). Uisilamu umeweka njia
ya kuwahubiria watu (Da'wah), kuwarudisha au kuwaita watu kwenye Uisilamu.
Kuwatia watu kwenye Uisilamu maana yake hasa ni uwakaribisha. Maana
yake si kuwavutia kwa mbinu au kuwalazimisha. mtu hawezi kulazimishwa kuamini
au kutoamini. Qur'an inasema wazi wazi kwamba "Hakuna kulazimisha katika
dini" wakati huo huo inaposisitiza kuwa kweli na mwongozo sahihi vilivyoletwa
na Uisilamu vimekwisha tofautishwa mbali na upotofu. Ndipo kukaribisha
kuna maana ya kuwaita watu kwenye Uisilamu "kwa hekima na mawaidha mema."
Hata pale Mtume Musa (A.S) alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu aende kwa Firauni,
aliambiwa aseme naye kwa "maneno ya upole" na kumuwekea matumaini ya kumbadilisha.
Waisilamu, kwa hiyo wana wajibu wa kutimiza kwa watu wa imani nyingine;
kuwakaribisha kwenye Uisilamu na kwenye ibada ya kumuabudu Mungu mmoja
iliyotakaswa na Shirk zote zilizobuniwa na wanadamu. Kutokana na mahubiri
haya watu wanawezeshwa kuamua kurudi kwenye maumbile yao mema ya asili
na kuwa Waisilamu, au wanaweza kuamua kubaki kwenye dini zao.
Hakuwezi kuwapo hata na fununu tu ya majivuno au ubabe katika kuwakaribisha
watu, kung'ang'aniza au matumizi ya nguvu; kwani Qur'an imesisitiza: "Kusiwapo
kulazimishana katika dini" kwani "kweli imewekwa bayana mbali na uongo."
Kazi ya kuhubiri inatakiwa itekelezwe kwa kuzingatia ipasavyo maagizo ya
Qur'an yasemayo; "Waite katika njia ya Mola wako kwa hekima na mauidha
mema."
Wahubiri wa Kiisilamu wameichukua taaluma ya dini linganifu kuwakaribishia
kwenye Uisilamu Watanzania wenzao waliotelezea kwenye Ukristo. Kwenye shughuli
hii hutumia vitabu vyote viwili Biblia na Qur'an, kuwathibitishia Wakristo
kiasi gani wamepotea njia. Kwa kutumia Biblia haina maana kuwa hiyo ndiyo
njia pekee ya kufikia kwenye kweli ya Mwenyezi Mungu. Qur'an inazifafanua
imani za Ukristo kwa njia zilizo wazi kabisa zisizo shaka yoyote:
Dhambi hazirithiwi - Q:2:123, 6:164, 53:38-42. "Utatu" ni tungo za wanadamu
- 4:171-172, 5:73. Yesu si Mungu - 4:171-172, 5:17, 5:72-75, 5:116:118.
Yesu Kristo hakuuawa wala hakusulubiwa - 4:157-158.
Waisilamu wanatumia ushahidi wa maandiko ya kikristo kuthibitisha hoja
zao kwa sababu wanashughulikia akili za watu waliotayarishwa tangu utoto
kukubali ("dogmas"), itikadi; bila ya kutumia akili.
Wakristo wamekuwa wakifundishwa kwenye shule za watoto wadogo za siku
za jumapili, na wamekuwa wakisikia tangu wangali wadogo, kuwa Yesu ni Mwana
wa Mungu na kadhalika.
Ikumbukwe pia kuwa hali halisi ya nchi yetu Tanzania inalazimisha matumizi
ya mtindo huu. Shughuli ya kujenga makoloni na kutawala katika Africa iliyofanywa
na Wazungu katika kipindi cha karne mbili zilizopita iliambatana wakati
huo huo na uvamizi wa Africa uliofanywa na wamisheni wa Kikristo ambao,
kwa kutumia hadaa na taarifa za kupotosha, walifanikiwa kueneza Ukristo
kupitia vivutio vya shule na hospitali.
Inawawajibikia Waisilamu kuwasaidia ndugu zao wakristo kujikomboa kutokana
kwenye makongwa yaliyokuwa yanatawala vipawa vyao vya kufikiri kwa miaka
elflu mbili iliyopita:
Ninyi ndio umma bora katika umma zote zilizodhihirishiwa watu - mnaoamrisha
yayiliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.
Na kama wale waliopewa kitabu (Wayahudi na Wakristo) wangeliamini ingekuwa
bora kwani miongoni mwao wako wanaoamini, na wengi wao wanatoka katika
taa ya Mwenyezi Mungu.
Waisilamu wanatumia kitabu wanachokiamini Wakristo kuwaitia kwenye Uisilamu
kwa kuwaonyesha udhaifu wa imani wanazozifuata. Qur'an inawaamrisha Waisilamu
wadai ushahidi kutoka kwa Wayahudi na Wakristo wa madai yao kwamba "wokovu"
unapatikana kwao tu; "Leteni dalili zenu kama ninyi ni wasema kweli" 2:111.
Wamisheni wa kikristo wameichapisha Biblia katika lugha zaidi ya alfu
moja na kutawanya dunia nzima, wakiyatisha mataifa ya dunia kukubali kuwa
"kristo alikufa na madhambi ya wanadamu" na kwamba yeye ndiye "mwokozi
pekee". Wakati wote Biblia yenyewe ikiwathibishia kuwa madai haya si kweli.
Waisilamu, kwa hiyo, wanawajibika kuwakomboa Wakristo kutoka kwenye udanganyifu
huu na hakuna njia bora zaidi ya kufanya hivyo kuliko ile ya kutumia ushahdi
wao wenyewe na hoja zao wenyewe kuvunjia madai yao.
Kwa kutumia Biblia, Waisilamu hawaishambulii Biblia yenyewe. Kwa mujibu
wa Gary Miler, mtaalamu wa Hisabati Muisilamu wa Canada aliyerejea kwenye
Uisilamu, Waisilamu "hushambulia zile itikadi zisizo na ushahidi wowote,
zinazotolewa na wataalamu wa dini ya Ukristo kuhusu Biblia.
Waisilamu wanaamini kuwa Biblia ina maneno ya Mwenyezi Mungu, bali hawakikubali
kila kitu kilichomo humo. Kuamua sehemu gani za Biblia zinakubalika kwa
Waisilamu hakuji kwa mapenzi tu. Ni suala linalosimama kwenye kweli tu
daima. zile sehemu, na ni sehemu hizo tu, ambazo daima zinajidhihirisha
kwenye kweli, zinakubalika akilini zinajiddhirisha zenyewe kuwa ni maneno
ya wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, sehemu hizo ndizo zinazokubalika kwa
Waisilamu; (Gary Miller, "A. concise reply to Christianity: A Muslim
View, iliyomo kwenye "A Colleciton of Comparative Religion Booklets" na
Ahmed Deedat na wengine, Durban).
Katika kuwaita Wakristo kwenye Uisilamu, Waisilamu wanajua kuwa kuna
mambo mengi ya muhimu ambayo yanapatikana kwenye Uisilamu na Ukristo. Waisilamu
na Wakristo wanaamini na kuchangia mengi yanayofanana; imani, mambo ya
kuthaminiwa, maadili na kanuni za mienendo na tabia. Bikira Maria na mwanawe
Yesu (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao, wote) wanatajwa mara kwa mara
ndani ya Qur'an. Kwa kweli kuna sura nzima ya Qur'an iliyopewa jina la
Bibi Mariamu - inaitwa hivyo hivyo; Mariamu. Tofauti kubwa baina ya imani
hizi mbili inatokana na nafasi ya Yesu katika dini.
Yesu, katika Qur'an anaitwa Isa ibn Maryamu - Isa mwana wa Mariamu,
ni mmoja wapo wa manabii wakubwa wa Mwenyezi Mungu ambaye waisilamu wanamuweka
kwenye daraja ya juu ya mapenzi na heshima. Qur'an inathibitisha kuwa Yesu
alizaliwa na mama Bikira (Mariamu) kutokana na uwezo ule ule uliomuumba
Adam bila ya baba au mama:
Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimuumba
kwa udongo kisha akamwambia; "kuwa", basi akawa.(3:59)
Yesu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, alifanya miujiza mingi. Alipewa
uwezo wa kusema akiwa bado yungali mchanga, kuponya wangonjwa, kufufua
wafu na kufikia nyoyo za watu kwa mwongozo alioleta kutoka kwa Mungu. Na
mwisho, pale alipokuwa katika hatari ya kuuawa na watu wake mwenyewe, Mungu
"akamnyanyua," Qur'an inasema hakuuawa wala hakusulubiwa.
Qur'an inasisitiza kwenye aya chungu nzima kuwa Yesu si mwana wa Mungu,
kwamba yeye mwenyewe hakudai kuwa alikuwa mwana wa Mungu wa dhati ya Mungu
bali badala yake amewaagiza wafuasi wake wamuabudu Mwenyezi Mungu pekee.
Inasema pia kuwa dhana kwamba Mwenyezi Mungu aliye juu ana mtoto inadhalilisha
na iko mbali mno na utukufu na ukuu wake kiasi cha kuwa kufuru kubwa:
Maana Mwenyezi Mungu, muumba na mpaji riziki wa ulimengu huu, pamoja
na ukubwa wa mchanganyiko wake wote wa maumbile yasiyo mithilika, yuko
mbali na juu mno ya kitu chochote tunachoweza kukifikiria.
Upungufu wa maumbile ya vitu vyote hivi vilivyoumbwa ni udhaifu ambao
hatuwezi kuvihusisha na dhati ya Mwenyezi Mungu. Kama Yesu kweli angekuwa
mwana wa Mungu angekuwa mshiriki katika Uungu na yeye mwenyewe angekuwa
na dhati ya Uungu, na hapo Mungu angekuwa wakati huo huo amezaa, amezaliwa,
ameishi kama mwanadamu, na akafa. Dhana hii haistahili neno! Inahusiana
zaidi na ngano za kipangani; ambamo "Miungu" walizaa miungu-watu na wanawake
wa kibinadamu, kuliko na dini ya kweli inayotoka kwa Mwenyezi Mungu katika
misingi ya uhusiano unaopatikana baina ya Muumba na alivyoviumba. Ndiyo
maana dai kwamba Yesu ni mwana wa Mungu haliwezi kuwa chochote, kwa dhati
yake, ila la uongo kwa sababu linapingana na dhati na sifa za muumba mwenyewe,
likimporomosha kwenye daraja la viumbe aliowaumba. Kwa maneno ya Qur'an:
Uisilamu haulikubali dai kuwa Yesu alikufa msalabani na kwamba alikufa
muhanga kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Haulikubali wazo la dhambi ya
asili ambalo kosa la asili la Adam la kumuasi Mungu linarithiwa na kizazi
chake chote. Kwa maneno mengine, haukubali kuwa wanadamu wote duniani wana
dhambi kwa sababu ya uasi wa Adam kwa Mwenyezi Mungu. Adam alitubu, na
kuomba msamaha kwa makosa yake na Mwenyezi Mungu akamsamehe.
Uisilamu unasema kuwa wanadamu wote wanakuja duniani bilia hatia wala
dhambi. Mtoto mchanga habebi mzigo wa dhambi zilizofanywa na mzazi wake.
Hii ingekadhibisha sifa za Mwenyezi Mungu za haki na huruma.
Kudai pia kuwa dhambi hii kwa hakika itampeleka kila mwanadamu motoni
na adumu humo daima kama Mungu hajitoi muhanga kuifidia kwa ajili ya viumbe
wake, vile vile ni kuzikana sifa za haki na rehema za Muumba kwa waja wake.
Hakuna anayeweza kuokoka bila ya huruma na rehema za Mwenyezi Mungu na
kumkubali na kunyenyekea kwa muumba wake na mwongozo wake. Mtu anaweza
kurudi kwa muumba wake kwa utii na kutubu bila ya haja ya kuwapo mtu wa
kati au muombeaji:
Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine, wala hakitakubaliwa
kikomboleo kwake; wala maombezi hayatafaa, wala hawatanusuriwa.((2:123)
Tofauti nyingine kubwa kati ya Uisilamu na Ukristo iko kwenye itikadi
ya Utatu. Ikiwa Mungu ni mmoja tu, kama Wakristo wanavyodai wanaamini sawa
wanavyoamini Waisilamu, haiwezekani wakati huo huo tena awe watatu - kwamba
wako watatu ndani ya mmoja na mmoja ndani ya watatu! Hata mtoto mdogo sana
anaweza kuiona kweli ya hoja hii. Kwa kawaida Wakristo wanauelezea utatu
kuwa si kwamba wako waungu watatu bali sehemu tatu au nafsi tatu za Mungu
mmoja zenye kazi mbalimbali.
Lakini Mungu si kama keki au chungwa linaloweza kugawanywa katika theluthi
tatu zinazokuwa kitu kimoja: kama Mungu ni nafsi tatu au ana sehemu tatu,
Hawi tena ;Mungu mmoja tu, pekee, asiyegawanyika, ambavyo ndiyo Mungu alivyo
na ndivyo Wakristo wanavyodai alivyo! Kwa Waisilamu hili halileti maana
yoyote; na hata kama wataalamu wa dini ya Ukristo watatuelezea utatu kuwa
ni "Fumbo," lililo juu sana ya uwezo wa mwanadamu yeyote kulielewa, imani
ya utatu inachukuliwa na Uisiliamu kuwa ni aina ya kumshirikisha Mungu.
Na hata hivyo utatu haumo ndani ya Biblia. Neno utatu halimo ndani ya
Biblia au Kamusi za Biblia; haukufundishwa kabisa na Yesu, na wala hakuwahi
kuutaja hata mara moja. Hakuna ushahidi au pa kushikizia utatu ndani ya
Biblia ili ukubalike. Baadhi ya wasomi wa kikristo wamefikia uamuzi huu.
Tom Harpur, mwandishi mashuhuri wa nakala zinazozungumzia dini. Kwenye
gazeti la "Sunday Star", na Profesa wa zamani wa Agano Jipya kwenye Chuo
cha dini cha Toronto, anaandika kwenye kitabu chake mashuhuri "For Christs
sake" (Oxford Univerity Press, Toronto 1986):
"Kwa kweli ni wahubiri wachache sana wanaoweza kutoa maelezo yanayoeleweka
;juu ya itikadi ya utatu au juu ya itikadi ya mwanadamu kuwa Mungu au Mungu
kuwa mwanadamu; yaani Yesu aliku mtu kweli na wakati huu Mungu kamili.
Wanarudia rudia miundo ya kauli zilizosanifiwa, kwa magomvi na uadui mwingi,
kwenye karne za nne na tano, na watu ambao mahitaji yao katika maisha,
mtazamo wao juu ya maisha na jinsi walivyokuwa wanauelewa ulimwengu, kulikuwa
tofauti sana na vile tulivyo sisi. Miundo hii haina manufaa sasa badala
yake, inaweka vikwazo vikubwa sana kwa watu wengi ambao, vingine, wangeweza
kuwa wanafunzi wa Yesu wa zama zetu.
Linalolifedhesha kanisa ni ule ugumu wa kuzithibitisha itikadi hizi
kwa kutumia ushahidi wa maandiko ya agano Jipya. Huwezi ukaikuta itikadi
ya utatu ikielezewa pahali popote ndani ya Biblia .... .. Humkuti Yesu
popote akidai wazi wazi kuwa yeye ni nafsi ya pili katika utatu, akiwa
sawa na baba aliye mbinguni. Myahudi mcha Mungu; angetishwa na kuchukizwa
sana na wazo hilo.
Katika muda wa miaka kumi hivi iliyopita nimekuwa nikizungumza, kwa
muda mrefu, na kwa mara nyingi kama ilivyowezekana, na watu wa kawaida
na viongozi wa dini wa madhehebu yote juu ya itikadi hizi, na nilichokigundua
ni kuchanganyikiwa kwingi kila pahali - jambo ambalo peke yake ni baya.
Lakini kuna mabaya zaidi. Utafiti huu umenifanya niamini kuwa wengi sana
wa wale wanaokwenda makanisani, katika ibada zao ni watu wanaoamini miungu
watatu. Yaani, wanasema kuwa wanamuamini Mungu mmoja lakini kwenye ibada
zao wanaabudu miungu watatu.(uk.7)(msisitizo unaongezwa)
Katika juhudi zao zakuliunga mkono tamko la Nicene (Nicene Creed) juu
ya utatu, wataalamu wa dini wa Kikristo wanadai kuwa Yesu mwenyewe alisema;
Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa
jina la Baba, na Mwana, na roho Mtakatifu "(Mathayo 28:19) na kwa hiyo
itikadi ya utatu inaonekana kuungwa mkono na maandiko na kristo mwenyewe.
Lakini kwa mujibu wa harpur "Wataalamu wote wa dini ya kikristo, isipokuwa
wale waliobobea kwenye kung'ang'ania ya kale, wanakubaliana kuwa sehemu
ya pili ya amri hii (Mathayo 28:19) angalau ilikuja kupachikwa baadaye
"(For Christ's Sake, uk.84). Kwa vyovyote vile jambo la muhimu la kuzingatiwa
ni nafasi ya kila mmoja wao. Wapi inaposemwa kuwa watatu hawa wanachangia
usawa?
Ushahidi wa nguvu kabisa juu ya itikadi ya utatu unapatikana kwenye
Yohana 5:7-8 kwenye toleo la Biblia la King James ambamo inasemwa; "Kwa
maana wako watatu washuhudiao (mbinguni, Baba, na Neno na roho Mtakatifu,
watatu hawa ni umoja, kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na
maji na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja." Lakini sehemu hii;
"Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja "imetolewa sasa
katika Biblia za toleo la King James la mwaka 1971 na katika Biblia nyingine
nyingi kwa sababu ilikuwa nyongeza iliyojipenyeza kwenye maandiko ya asili
katika lugha ya kiyunani; (Kigiriki).
Yohana 5:7-8 kwenye Biblia ya toleo la King James inasomeka hivi, "Naye
roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu Roho ndiye kweli: kwa maana wako watatu
washuhudiao; Roho na maji na damu, na watatu hawa hupatana kwa habari moja."
Wakristo wengi pamoja na viongozi wao na wahubiri, hawalijui hili.
Tungo hii ya itikadi ya utatu iliyotayarishwa na Athanasius, "deacon"
Mmisri aliyeishi mjini Alexandria, iliidhinishwa katika mtaguso wa NIcea
mwaka 325 B.K., karne tatu na zaidi baada ya Yesu kutoweka. Bila shaka
upagani wa Kirumi - Mungu wa utatu ulihusika na itikadi hii. Kama vile
tarehe 25 Desemba, siku ya kuzaliwa Mithra, Mungujua wao, ilifanywa kuwa
siku ya kuzaliwa Yesu.
Huu, basi kwa kifupi, ndio msimamo wa Uisilamu kuhusu Yesu na Ukristo,
masuala yanayozungumziwa sana kwenye mihadhara yao, ambayo viongozi wa
Kanisa katoliki ndiyo wanayoisema kuwa ni ya kukashifu.
Sasa, kama yesu mwenyewe hakusema kuwa alikuwa mwana wa Mungu na mwokozi
wa dunia, imekuwaje basi kuwa Injili zimeleta madai hayo? Na imekuwaje
basi kuwa wakristo wamekuwa wakiyaamini hayo tangu zama hizo?
Lazima ikumbukwe kuwa si Wakristo wote, hata katika zama zetu hizi,
wanaoamini hivyo. Kuna makundi ya Wakristo amabo hawaamini kuwa Yesu ni
Mungu na katika zama za mwanzo wa Ukristo kulikuwako na madhehebu kadhaa
ya Wakristo; baadaye yakaja kuhesabiwa na mababa wa Kanisa kuwa ni ya uzushi,
hapo ilipokwisha "amuliwa" kuwa Yesu alikuwa Mungu, ambayo hayakukubali
kuwa alikuwa Mungu, wakishikilia kuwa alikuwa mwanadamu na Mtume wa Mwenyezi
Mungu. Miongoni mwao pia kulikuwako wengine ambao hawakuamini kuwa Yesu
alisulubiwa, bali waliamini kuwa mtu mwingine aliyekuwa amefanana naye
sana alisulubiwa badala yake.
Lazima ikumbukwe pia kuwa suala la wanadamu wa Yesu si suala jipya liloibuka
katika zama zetu baada ya watu kuanza kuyachambua maandiko ya Biblia, au
kwa kuja Uisilamu.
Historia yote ya Ukristo ni historia iliyojaa mijadala na malumbano
hayo. Na wala hakukuwako na uhaba wa Wakristo waliokana Uungu wa Yesu.
Huko nyuma sana mwaka 1546, katika mji wa Minister, nchini Uholanzi watu
30,000 waliuliwa kwa kukana Uungu wa Yesu, (E.M.Wilbur, "A History of Unitarianism:
Socianism and its Auticedents," Beacon Press, Boston, 1945 page 41.
Mwaka 1978, Profesa Robert Alley alifukuzwa kazi yake ya uenyekiti wa
idara ya Dini, Chuo Kikuu cha Richmond (Virginia), kwa sababu alikana kuwa
Yesu aliwahi kudai kuwa alikuwa mwana wa Mungu. Ni bahati yake kuwa nyakati
zimebadilika, vingine angepoteza maisha yake - kama Rev. John Gray, kiongozi
wa Kanisa la Pressby Beterian la Scotland, alivyoshindwa kujizuia kutamka
kwenye uzinduzi wa Kitabu cha John Hicks "The Myth of God Incarnate" mwezi
July, 1977; "... katika zama zile tulipokuwa wakali ningetoa shitaka la
uzushi "(heresy), (International Tribune, July 1977).
Iwe iwavyo, vikundi hivi vya "uzushi" vilikandamizwa na karibu vifutike
vyote. Suleiman Mufassir, msomi Muisilamu wa Marekani ameandika kwenye
kijaride chake "Jesus in the Qur'an (Plaiafield, Indiana uk.14) kuwa "Ni
jambo la kuzingatia kuwa zile itikadi ambazo Qur'an inazikubali zinaweza
kuthibitishwa kwa urahisi kuwa zilikuwa sehemu ya mafundisho yaliyotolewa
na wanafunzi wa awali wa Yesu, ambapo zile ambazo Qur'an inazikataa zinathibitika
kuwa ni nyongeza zilizopachikwa baadaye na Kanisa, zinazotokana na falsafa
na imani za kipagani, kiyunani na kirumi."
Na kuhusu dai kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mungu lazima ikumbukwe kuwa
Injili nne za Agano Jipya, Injili za Mathayo, Marko, Luka na Yohana, ziliandikwa
miaka chungu nzima baada ya wakati wa Yesu.
Utafiti wa Maandiko ya Biblia umethibitisha bila wasiwasi kuwa hakuna
hata mmoja katika waandishi wa Injili hizi ambaye alikuwa mwanafunzi wa
au, aliyekuwa pamoja na Yesu; aidha, hawakuandika Injili zao katika lugha
ya Yesu, Kiibrania, bali waliandika katika lugha ya kiyunani. Kufikia katika
wakati ule walipoandika juu ya maisha ya Yesu, mambo mengi yaliyomuhusa
Yesu yalikuwa "yamepotea" au kusauliwa na mengi mengine yalikuwa yamepenyezwa
na zaidi ya yote, Ukristo ulikuwa sasa umo katika kufinyangwa katika muundo
uliovutia zaidi kwa Wagiriki na Warumi kuliko kwa Wayahudi wa Palestina.
Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi
Mungu, na Masihi mwana wa Mariamu, hali hawakuamrishwa isipokuwa kumuabudu
Mungu mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa ila yeye. Ametakasika na yale
wanayomshirikisha nayo.(Q.9:31)
Wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao lakini Mwenyezi
Mungu amekataa isipokuwa kuitimiza nuru yake, ijapokuwa makafiki wanachukia.(Q9:32)
Enyi mlioamini! Wengi katika makasisi na wacha Mungu (wao) wanakula
mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu.
Mihadhara inayoendeshwa na Waislamu imefanikiwa katika kuwasilimisha
wakristo, baadhi yao wakiwa mapadre na wachungaji. Viongozi wa kanisa katoliki
wakaogofya sana na hali hii na kwa sababu hawana uwezo wakupambana na hoja
za Waisilamu kwa nguvu ya maandiko, wakaikimbilia serikali wakiichochea
ifungie mihadhara ya Waisilamu kwa madai kuwa ilikuwa inakashifu na kuutukana
Ukristo. na kwa kutia watu hofu, viongozi wa kanisa katoliki wakasingizia
kuwa mihadhara ya Waisilamu ilikuwa inahatarisha amani ya Tanzania.
Tunasema kuwa mbinu hii ya kanisa katoliki ilikuwa ni laghai na ya kutoa
taarifa za uongo. Ilikuwa ni mpango uliodhamiriwa kuwafanya waisilamu waonekana
maadui wa amani na kungiza serikali katika juhudi zao za kumshinda adui.
Mpe mbwa jina baya kisha muwauwe.
Ndipo Kadinali Pengo (wakati huo akiwa Askofu Mkuu Pengo), kwenye barua
yake ya kichungaji ya mwaka 1993 (St. paul Publications, Nairobi) kama
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, akasema kuwa "... chokochoko za kidini malumbano
yasiyo na msingi na mihadhara ya kashfa ya vikundi vya Waisilamu dhidi
ya dini ya kikristu ni ishara ya wazi ya kuingiliwa na Uisilamu wenye siasa
au msimamo mkali hapa Tanzania.
"Chokochoko za kidini, malumbano yasiyo na msingi na mihadhara ya kashfa
za vikundi vya Waislamu dhidi ya dini ya Kikristu ni ishara wazi ya kuingiliwa
na Uislamu wenye siasa au msimamo mkali hapa Tanzania. Tukijua matokeo
ya kushamiri kwa Uisilamu wenye siasa au msimamo mkali katika nchi au taifa
lolote tunakuwa na kila sababu ya kupata hofu na wasi wasi kuhusu kudumu
kwa amani katika nchi yetu kwa siku za mbele".
Barua ya kichungaji ya kadinali Pengo ilifuatiwa na Tamko la Maaskofu
lililotiwa saini na Mwenyekiti wake, Askofu Josephat Lebulu. Kwenye tamko
hili la mwaka 1993, maaskofu wa kikatoliki walisema," :
Katika mihadhara ya dini ya Waislamu wenye siasa kali dhidi ya dini
ya Kikristu yanashambuliwa mambo kadhaa ya msingi kwa imani ya Kikristu;
kwa mfano: Umungu wa Kristu, Ufufuko wa Kristu, Uwepo wa Kristu katika
Ekaristi Takatifu n.k.
"Kuna madharau ya wazi kabisa kwa dini ya Kikristu. Mihadhara ya kashfa,
kanda za kashfa na baadhi ya Magazeti yanaendelea kutukana. Tumetambua
ukimya wa Serikali kuwa ni kigezo cha kuhimiza kashfa na chuki hizo. Tumeng'amua
kuwa waumini na watu wote wenye mapenzi mema wa dini mbali mbali, wakiwemo
Waislamu, wamefikia kukinaishwa na maudhi ya kashfa hizo. Pia wamekinaishwa
na ukimya wa Serikali kutochukua hatua zinazostahili kukomesha kashfa hizo.
Tamko hilo laendelea kwa kusema:
"Lakini hali hii ya kashfa za kidini na ukimya wa serikali inabomoa
jitihada hizo zote. Hivyo badala ya amani hali hiyo inajenga mapambano;
badala ya upendo, chuki, badala ya utulivu, vurumai na badala ya uelewano,
mfarakano. Mwisho wake ni umwagaji wa damu".
Inafaa kuzingatia kuwa uongozi wa kanisa katoliki ulitoa mashambulizi
yao dhidi ya mahubiri ya Waisilamu wakati wa kipindi cha mwisho cha utawala
wa Rais Mwinyi, wakidokezea kuwa Rais Mstaafu huyu Muisilamu, alikuwa akiyaunga
mkono kwa kutoyachukulia hatua yoyote ya kuyazima. Lakini Mwinyi, kwa kutambua
dhati ya tatizo lenyewe, alijaribu kuleta suluhu kwa kuitisha mkutano wa
maaskofu na masheikh, usuluhishaji huu haukufanikiwa kwa sababu maaskofu
hawakuweza kuleta ushahidi wa madai yao. Lakini waliendelea na mashambulizi
yao, yaliyfikia kilele chake kwenye maonyo yaliyotolewa na Padre Lwambano
kwenye Radio Tumaini tarehe 8 ya Februari, 1998.
Iwe iwavyo, ni wazi kuwa mashambulizi ya viongozi wa kanisa katoliki
yalikuwa laghai ya uchokozi na yaliyojaa taarifa za uongo; hayakuwa na
msingi wowote wa kisheria na yalidhamiriwa kuwatisha na kuwakasirisha Watanzania
ili kuhakikisha kuwa serikali na wakristo wa kawaida wanauona Uisilamu
na waisilamu kuwa ni tishio kwa amani ya Tanzania.
Kulikuwa hakuna kabisa ushahidi wa matusi, chuki au tishio kwa amani
ya Tanzania. Wakristo wa kawaida (sio mapadre na wachungaji) na Waisilamu
walikuwa wakiendesha maisha yao, wakishirikiana pamoja katika maisha ya
pamoja au binafsi, wasiwe na habari kabisa ya tishio lolote; la kweli au
la kubuniwa, juu ya amani na usalam wao. Wasiwasi wao ulikuwa juu ya mfumuko
ya bei, uchumi ulioendeshwa hovyo hovyo wizi, rushwa ya hali ya juu, uhalifu
uliokuwa ukiongezeka kila leo na kumomonyoka kwa maadili kwenye jamii ya
Watanzania.
Kama kweli lazima isemwe kama kulikuwa na tishio lolote lililoletwa
na mihadhara ya Waisilamu, basi tishio hilo lilikuwa kwa uongozi wa kanisa
uliokuwa unaona kuwa mamlaka yao juu ya wakulima na wafanyakazi wa kikristo
yalikuwa hatarini. Maana viongozi wa kanisa waliingiwa na hofu walipoona
kuwa mihadhara ya waisilamu ilikuwa inawaharibia mambo; ilikuwa inawaamsha
na kuwaelimisha wakristo wakati wao, ili kuhifahdi masilahi yao, walitaka
wakristo waendelee kubaki kizani.
Kwa mtu ambaye haijui historia na utaratibu wa uendeshaji wa kanisa
katoliki itakuwa vigumu kuuelewa msimamo uliochukuliwa na viongozi wa kanisa
hili kutokana na ukweli kuwa wote, wakristo na waisilamu kukika uhusiano
wao, wanatambua kuwa kutangaza dini ndiko kiini cha imani yao.
Uhuru wa kutangaza na kubadili dini ni haki ya msingi inayotolewa na
Mungu. Kwa kiasi kile kile kanisa katoliki lingalivyopenda kuendelea
na shughuli zake za "kuwabatiza" waisilamu nalo, kwa kiasi hicho hicho,
lazima litambue uhuru wa waisilamu kutangaza dini yao na wa wakristo kubadili
dini na kuwa waisilamu kama wanataka kufanya hivyo. Kwa maana katikati
ya imani ya kikristo ni umuhimu na amri ya Mungu kuitangaza dini.
Kanisa katoliki lazima litambue kuwa watu wana haki ya kuikubali imani
wanayoletewa. Lakini inaonekana kuwa haya ni matumaini ya bure kwa sababu
viongozi wa kanisa katoliki wanawaagiza waumini wao wasijiingize kwenye
majadiliano na Waisilamu ingawa majadiliano kati ya imani na imani siku
zote yamekuwa yakihimizwa ndani ya Biblia; kwa mfano katika Isaya 1:18
-- "...Njooni tusemezane" msimamo unaochukuliwa na uongozi wa kanisa katoliki
si wa kikristo. Maana vipi mtu atatii amri ya "Basi, nendeni mkawafanye
mataifa yote," bila ya kwanza kuwaeleza ukweli wa namna fulani? Naam, vipi
waisilamu wanaweza kubatizwa na kuwa wakristo ili nao vile vile "kwa nguvu
ya neno waweze hapo apendapo Mungu, kuingizwa kwenye kanisa lake" bila
ya kwanza kuwashawishi, au kuwapa ushahidi wa "kupotea kwao kutoka imani
ya kweli ya ukatoliki?"
Haieleweki pia kwa nini viongozi wa kanisa katoliki wakwepe majadiliano
na uchunguzi ndani ya Injili ambazo kanisa lenyewe linadai kuwa ni maneno
ya Mungu. Ni kwa sababu uongozi wa kanisa katoliki, baada ya wao kushawishika
kuwa Injili hizi ni kweli, basi wanamtaka kila mtu wafuasi wao na hao wanaotaka
kuwabatiza, wawaamini na kuwafuata wao tu bila ya udadisi wowote? Au ni
kwa sababu uongozi wa kanisa katoliki unaamini kabisa kuwa dini haihusiani
na tashi za akili, mantiki na kiasi kwenye matumizi ya akili au tashi za
maumbile tu?
Tukianza na ile kweli kuwa misingi ya dini ya kweli lazima iwe inaeleweka
kwa mtu yeyote wa kawaida anayetumia akili na fahamu zake, dini yoyote
inayomtaka mtu asiyeiamini dini hiyo alikubali msingi wake kwa imani tu,
dini hiyo huwa ni kwa ajili ya waumini wake tu. Si hivyo tu bali imani
ya watu juu ya dini hiyo itaathirika vibaya pale itakapokuja pambanishwa
na udadisi wa kawaida au pale watu watakapokuwa huru kutumia akili zao.
Kwa upande mwingine dini ambayo misingi yake inakubaliana na tashi za
maumbile asilia ya mwanadamu wanadamu, hawatapoteza imani yao juu yake,
hata pale wafuasi wake wanapokuwa wafuasi wa majina tu.
Misingi ya dini ya kweli haipingani na tashi za maumbile asilia au matumizi
ya kawaida ya akili. Dini ya kweli haidai kuwa kwanza uamini halafu ndipo
utakapoiona kweli yake. dini ikiwa hivyo basi dini hiyo itaonyesha kuwa
baadhi ya watu wanazaliwa wasiweze kupokea mwongozo wa wokovu na kwamba
hakuna nafasi sawa kwa wanadamu za kufika peponi, kufuata "uzima wa milele".
Kweli ni kwamba kanisa katoliki lazima likubali kuwa Mungu amemuumba
mwanadamu na maumbile ya nafsi yenye kutambua mema na mabaya, na akili,
zenye uwezo wa kuchambua na kufafanua mambo. Mwanadamu pia ana uhuru wa
khiari; kupima na kuchambua hayo anayohubiriwa ili aweze kuona kuwa hayo
anayoambiwa ni kweli, yana mantiki na yanakubaliana na tashi za maumbile
yake asilia na kuamua kuyafuata kama akiamua hivyo.
Viongozi wa kanisa hawakupewa na kwa hiyo wasijipe, majukumu ya kumchagulia
mwanadamu nini cha kusikiliza na nini cha kuacha kusikiliza. Hata hivyo,
kwa sababu tunaambiwa kuwa wakristo wanaamini kuwa Roho Mtakatifu hukaa
ndani yao ili kuwaongoza kwenye kweli na ucha Mungu (Yohana 16:8, 16:13),
hakuna haja basi ya uongozi wa kanisa katoliki kuogopa majadilinao na mazungumzo
ya kutumia hoja juu ya kweli ya ukristo. Yaani kama kweli uongozi wa
kanisa unaiamini kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya wakristo na wao hawana
lolote la kuficha.
Tunatamka kuwa tabia hii ya viongozi wa kanisa katoliki ya kuzuia zuia
ukweli isijulikane na kutopenda kudadisiwa na majadiliano inatokana moja
kwa moja na historia ya Kanisa Katoliki na hasa hasa muundo wake wa uendeshaji.
Pamoja na yote yanayosemwa na Papa John Paul II katika ziara zake duniani
kwa mfano kule Cuba au Nigeria, ofisi ya Papa yenyewe haina historia ya
kutetea ukweli na uhuru wa mwanadamu.
Kwe kweli uongozi wa kanisa katoliki unaoshika mamlaka mwisho na pekee
kutokea juu, hauruhusu uhuru wowote na majadiliano kutoka kokote, ikiwa
ni wataalamu wa dini au wasomi wa Biblia wake wenyewe, ukiamini kwamba
eti uhuru na majadiliano husababisha kupotea kwa ukweli.
Peter de Rosa, aliyewahi kuwa Padre asemaye kuwa kazi yake ni kazi ya
"rafiki na siyo ya adui," anasema kwenye kitabu chake maarufu sana, "Vicars
of Christ" (Corg Books, London, 1984) kuwa madai kwamba ofisi ya Papa ni
mtetezi wa kweli na haki za wanadamu ni ya uongo"... Mbali na kwamba upapa
wa karne ya kumi- na ya kumi na tano - wenyewe ndio uliokuwa uzushi; kukanwa
kwa kila kitu alichokileta Yesu, mapapa wengi walifanya makosa ya kustaajabisha.
Mara kwa mara walipingana wenyewe kwa wenyewe na Injili. Wachache kwamba
hawakutetea hadhi ya mwanadamu, mara chungu nzima waliwanyima wakatoliki
na wasokuwa wakatoliki hata zile haki zao za kawaida tu.
Historia inavunja kabisa ngano za upapa usio na dosari kwenye masuala
ya kweli. Kwenye karne za unayama mapapa ndio waliokuwa viongozi wa unyama,
kwenye karne za mwanadamu kuingia kwenye meza mapapa waliokuwa nyuma kizani.
Na rekodi yao ilikuwa mbaya zaidi, kinyume na maagizo ya Injili pale walipojaribu
kuwalazimisha watu kuikubali "kweli" kwa nguvu." (uk.210).
Kwa mujibu wa de Rosa, kila wakati na kwa makarne, kanisa katoliki limekuwa
likitangaza kwa majivuno itikadi yake ya kutovumiliana katika dini. "Papa
baada ya papa wamekuwa wakishambulia uhuru kwa... ukali... walionyesha
kuogopa kuwa serikali ya watu, inapoendeshwa na watu, kwa ajili ya watu
ingetokezeshea madai hayo hayo kwenye kanisa. Gregory wa XVI, kwenye Mirari
Vos ya 1832 aliuelezea uhuru wa tashi ya nafsi (consiceince) kuwa ni wazo
la wehu; kiwendawazimu.
Uhuru wa dini umeelezewa kutokana na chemchemi yenye harufu ya uozo
wa kutokujali. Alilaani na kukuelezea uhuru wa ibada, vyombo vya habari,
kukusanyika pamoja na elimu, kama mfereji wa maji machafu uliojaa "matapishi
ya uzushi." Pius wa IX... kwenye Quanta Cura mnamo mwaka 1864... aliushambulia
uhuru wa dini na akaulinganisha na uhuru wa kifo.
Miongoni mwa mapendekezo aliyoyalaani katika barua yake ya kichungaji
"Syllabus of Errors" mojawapo lilikuwa hili. Siku hizi si busara tena kwamba
dini ya kikatoliki iwe ndiyo dini pekee ya taifa kwa kuzibagua na kuziacha
aina nyingine zote za ibada. leo XIII... Katika nyaraka zake za kichungaji
moja baada ya nyingine... aliuelezea uhuru wa dini kwa mitizamo ya zama
za "medieval".
Kanisa lina haki ya kuwa na ukiritimba wa dini kwenye taifa lolote
la kikatoliki. Kwa hiyo makanisa yasipewe uhuru wa kujisambaza. Uhuru na
kweli havipatani. Kweli lazima isimamiwe na taifa kwa amri ya kanisa kila
inapowezekana. Kila taifa... lazima lichukue imani ya kweli kuwa ndiyo
sera yake rasmi na kuvumilia uhuru wa tashi za nafsi kwa kisai kidogo iwezekanavyo
na kwa muda mfupi kabisa kama iwezekanavyo."
Lazima isisitizwe kuwa hizi si itikadi tu za mapapa wa karne ya 19.
Ni itikadi zinazowakilisha mfumo mzima wa mawazo ya uongozi wote wa kanisa
katoliki hata katika zama zetu hizi. Hata leo, aina fulani za uhuru ni
ngeni kwenye imani ya kikristo. Kwa mujibu wa mawazo ya papa John Paul
II kwake yeye kweli ya ukatoliki ni kweli tupu na utii kwa kweli hii ni
lazima ya kufa na kupona. Yeye, kama msemaji mpakwa mafuta wa Mungu; ana
lazima ya kutaka utii wa papo kwa papo na usio wa kusitasita kutoka kila
mtu, kutoka mdogo wa chini kabisa mpaka mwana teolojia wa kiwango cha juu
kabisa.
Ni muhimu isisahaulike kuwa kanisa katokiki ni jumuiya ya dini pekee
duniani leo ambavyo ni kanisa na wakati huo huo ni jumuia ya kisiasa.
Hii ndiyo sababu kwa nini kanisa hili pekee baina ya makanisa yote linalobadilishana
wawakilishi wa kibalozi na linachukua hadhi ya mwanachama huru wa jumuiya
za mataifa. linafanya hivi sio kama taifa dogo la Vatican, bali kama jumuiya
ya kidini iliyozagaa kila pahali duniani. Hii ndiyo sababu kwa nini, kwa
mfano kadinali Pengo, mmojawapo wa washauri wa Papa wa Roma ana uraia na
pasipoti za nchi mbili, uraia wa Taifa la Vatican na Taifa la Tanzania.
Vile vile ni muhimu kukumbuka kuwa kwa karne baada ya karne kanisa katoliki
ndilo lililokuwa mbele katika utawala. Liliweza kuingilia mambo ya utawala
wa kila nchi kila lilipotaka. Pius wa X alisema tarehe 9 November 1903.
"Tutawakasirisha watu wengi tunaposema kwamba ni muhimu kwetu kujishughulisha
na siasa. Lakini kila anayelihukumu suala hili kwa haki lazima atambue
kuwa Papa mwenye mamlaka, aliyepewa na Mungu Hukumu ya Juu, haina haki
ya kutenganisha mambo ya kisiasa kutoka uwanja wa imani na maadili," (uk.195,
Vicars of Christ).
Hivyo, kwa mujibu wa leo XIII, kisiasa, "kila siku ni jambo la haraka
bali ni wajibu wa kwanza kufikiria njia bora za kutumikia na kuendeleza
masilahi ya ukatoliki." Katika kila uchaguzi "Wakatoliki wanawajibika kuwapigia
kura wale ambao wanaahidi kuendeleza masilahi ya ukatoliki na kamwe usimchague
mwingine asiyependa dini (ya kikatoliki) badala yake." De Rosa amesema
kuwa kwa mujibu wa amri ya papa, kuna kura ya jumla, kura ya jumla
ya wakatoliki kwa ajili ya wagombea wa kikatoliki; na kushambulia ukatoli
ni shambulio juu ya ukatoliki tu.
Baada ya vita vya Dunia ya II Papa Pius wa XII alikuwa tayari kumfukuza
mkatoliki yeyote kwenye kanisa ambaye alimpigia kura Mkomunisti badala
ya mkatoliki (uk.208, Vicars of Christ').
Wasomi wanaona kuwa kuongezeka kwa amri za uongozi wa kanisa za kuzuia
itikadi za kanisa kufanyiwa uchunguzi na jinsi wanavyoogopa uhuru kunatokana
na kuongezeka kwa elimu duniani na maendeleo yaliyopatikana kwenye taaluma
ya uchimbaji, ugunduzi na utafiti wa mambo ya kale kwenye karne ya 19,
hasa hasa mchango wa taaluma hii katika uchunguzi wa maandishi (Scrolls)
ya Nagi Hammadi yaliyogunduliwa Misri mwaka wa 1945 na maandishi ya bahari
ya (Daad Sea Scrolls) yaliyogunduliwa kwenye mpango ya Qumran mwaka 1947
na 1956. Baada ya hapa ilikuwa ni suala la muda tu kabla maandiko hayo
kufikia zamu yake ya kufanyiwa uchunguzi wa kina - kuitenganisha kweli
kutoka ngano.
Labda mtu muhimu sana katika kazi hii ya kuhoji kweli halisi ya mafundisho
ya ukristo alikuwa mtaalamu wa dini na mwana historia wa kifaransa Ernest
Renaa, ambaye kitabu chake "The life of Jesus Christ" kiliondoa ufumbo-fumbo
katika ukristo. Kitabu hiki kilimuonyesha yesu kama "mtu asiye na mfano
wake," kiumbe mwanadamu halisi asiye na sifa yoyote ya Uungu. Kitabu cha
Renan kilibadilisha mtazamo wa watu juu ya taaluma ya uchunguzi wa Biblia
kabisa.
Kwenye kitabu chao "The Dead See Scrolls Deception "(Supra), Baigent
na Leigh wanasema yafuatayo kuhusu jinsi kanisa katoliki linavyolichukulia
suala la uchunguzi wa itikadi za kikatoliki. "Ikiandamwa na mashambulizi
kutoka sayansi, kutoka falsafa, kutoka `Art' na kutoka serikali zisizo
dini, Roma ikawa haijapata kutingishwa namna hiyo wakati wowote tangu mwanzo
wa mageuzi yaliyofanywa na Luther ... Ikachukua hatua kadhaa za pupa ya
mfa maji kujihami".
Mojawapo ya hatua hizo ilikuwa kutangazwa kwa itikadi ya papa Asiyekosa
(Papal Infellibility) na Papa Pius IX tarehe 18 July 1870. Hatua nyingine
ilikuwa kuanzishwa kwa umoja wa kileo wa kikatoliki wa wasomi wateule waliopewa
jukumu la kupambana na wapizani wa ukatoliki. Kizazi cha wasomi wa mambo
ya dini kilichofundishwa kwa uangalifu na kutayarishwa kulipatia kanisa
kikosi kilichoundwa maalumu kuihami kweli halisi ya maandiko.
Hata hivyo, kwa mujibu wa baigent na Leigh, kwa huzuni na masikitiko,
Roma ikaona kuwa mpango wao unawarudia wenyewe. Kadri walivyojaribu kuwapatia
mapadri hao vijana silaha zilizohitajika kwa mapambano kwenye majukwaa
ya malumbano ya kileo ndivyo kadri mapadri wao hao hoa walivyoanza kukimbia
kazi waliyotayaishiwa.
Uchunguzi wa kutafuta kweli halisi wa Biblia ukachimbua chungu nzima
ya khitilafu, makosa na matokeo ambayo yalikuwa ya hatari kwa itikadi za
Roma. Wataalamu wa kileo wenye haraka wakaanza kuhoji na kuyachimba chini
chini yale waliyokuwa wanatazamiwa kuyalinda. Bila ya shaka, kanisa katoliki
likalazimika kukigeuka chombo lilichokianziasha na kukitunza.
Hivyo mwaka 1903 Papa leo XIII akaunda Tume ya Papa ya Biblia (Pontifical
Biblical Commission) kusimamia na kuangalia kazi ya wasomi juu ya maandiko
ya kikatoliki. Mwaka 1904 Papa Pius wa X akatoa barua mbili za kiuchungaji
zilizopinga kazi za kisomi zote zilizohoji asili na historia ya mwanzo
wa zama za ukristo. Walimu wote wa kikatoliki walioshukiwa kuwa na "mawazo
ya kileo" wakafukuzwa mara moja kutoka kazi zao.
Kanisa katoliki liliuchukulia uchunguzi juu ya itiakadi za kiroma kwa
ukali mno kiasi kwamba Antonio Fogazzaro, mkatoliki mleli maarufu wa Italy,
alilazimika kusema kwenye kitabu chake "The Saint (London 1906) kuwa "Kanisa
Katoliki, likijiita lenyewe chemchemi ya kweli, leo linapinga utafutaji
wa kweli pale misingi yake vitabu vitakatifu, miundo ya itikadi zake, kutokufanya
makosa kunakosemwa, inapokuwa ndiyo walengwa wa utafiti. Kwetu sisi, hii
inaashiria kuwa halijiamini tena.
Kitabu cha Fagazzaro haraka sana kikawekwa kwenye orodha ya "Inquisition"
ya vitabu vilivyopigwa marufuku. Mnamo July 1907 makao makuu Roma ikatoa
amri iliyolaani hatua za wenye mawazo ya kileo za kuhoji itikadi za kanisa,
kutokukosea kwa papa na kweli ya kihistoria ya maandiko ya Biblia.
Mnamo Septemba 19907 mawazo ya kileo (modernism) yakatangazwa kuwa ni
uzushi na shughuli zake zote zikapingwa marufuku. Mwaka 1910 ilitolewa
amri iliyowataka wakatoliki wote walijishughulisha na kufundisha na kuhubiri
kula kiapo kukana "makosa yote ya mawazo ya kileo". Idadi kadha ya mwaandishi
wa kileo wakafkuzwa kanisani. Wanafunzi kwenye seminari na vyuo vya tekhnolojia
walikatizwa hata kusoma magazeti.
Kwa mujibu wa msomi muisilamu syed Abul A'ala Maududi kwenye kitabu
chake West versus islam" (1991, International islamic Publisher,s New Delhi)
mapambano haya kati ya kanisa na wateteaji wa uhuru wa mawazo yalikuwa
ni matokeo ya upinzani usio na mantiki wa upapa kiupofu upofu wakifuata
falsafa za kale na zilizokwisha makali za kigiriki kama ndio msingi wa
imani yao.
Kanisa lilihofu kuwa mashinikizo ya dini yao yataporomoka chini kama
utafiti wa kisayansi maeneo na magunduzi yake yatakubaliwa. utovu huu wa
kutokuelewa ulilipelekea kanisa na hata kutumia maguvu ya kinyama dhidi
ya nadharia mpya za kisayansi ugunduzi mpya. Waliunda "inquistion" na wanasayansi,
wagunduzi na wanafalsafa wakapewa adhabu za kinyama na za kutisha lakini
haikuwezekana na kuifuta kabisa kazi hii na ikaongeza nguvu na kasi kwa
sababu ilikuwa mwamko wa kweli.
Kufurika kwa uhuru wa mawazo huku mwishowe kukafutilia mbali mamlaka
ya Papa na uongozi wa kanisa juu ya watu. Vita hivi kati ya mawazo huru
ya maendeloe na dini au ukristo vilikuwa ndio mwanzo wa mtindo wa kutoamini
Mungu; wa uanadharia na wanafalsafa wakiwa wapingaji wakubwa wa kila wazo
la mamlaka ya Mungu, Mungu na mambo ya kiroho si kwa mantiki au kwa matumizi
ya akili, bali kutokana na upinzani wa kanisa dhidi ya mtindo wa utafiti
wa kisayansi na uhuru wa mawazo."
Kwa hiyo bila ya kuwa na habari ya uharibifu matokeo ya uzuiaji wao
unaomfanyia uhuru wa kujieleza na dini, hasa hasa katika kuwakimbiza wataalamu
na wasomi mbali na dini na labda bila ya kujali bali waking'ang'ania tu
kushika mamalaka juu ya kutafasiri maandiko, ungozi wa kanisa katoliki
unaenelea kuziba vinywa na kuzima kuhoji na utafiti wa kisomi wa Biblia.
Kwa mujibu wa New Catholic Encyclopedia (Vol.XI) kazi rasmi ya tume
ya kipapa ya Biblia iliyoundwa na Papa leo III mwaka 190-3, ni kujitahidi
kwa uanglaifu wote unaowezekana kuwa maneno ya Mungu yatakingwa, siyo tu
kutoka kila pumzi ya makosa, bali hata kutoka kila wazo la upinzani," na
kuhakikisha kuwa wasomi "wajaribu kulinda mamlaka ya kuandika na kuendeleza
tafsiri yake ya kweli. Hivyo, kwa mfano, Tume intangaza amri rasmi juu
ya njia sahihi za kufundisha maandiko. Hivyo, ka mfano, Tume imeweka" kwa
amri kuwa Musa ndiye aliyekuwa mwenyewe mwandishi wa kumbukumbu la Torati!
mwaka 1909 amri kana hiyo ikasisitiza uhakika wa mandishi na historia ya
sura tatu za kwanza na kitabu cha mwanzo. Na tarehe 21 April 1964 Tume
ikatoa amri iliyohusu usomi juu ya Biblia kwa jumla, na hususan juu ya
"kweli ya kihistoria ya Injili. Amri hii haikuuma uma maneno ilisema kuwa
"kwa muda wote mtafsiri lazima aweke ndani yake azma ya utii bila kusita
kwa mamalaka ya kanisa juu ya mafundisho.
Ni muhimu kuzingatia kuwa mkuu wa Tume ya papa ya Biblia vile vile ni
mkuu wa Kamati ya itikadi za Imani (Congregation for the Doctrine of the
Faith) kabla ya hapo ikiitwa Ofisi Takatifu (The Holy office) na kabla
ya hapo ikiitwa the Holy Inquisition." Kwa hiyo mkuu wa vyombo hivi viwili
vya kikatoliki ndiye kwa kweli mtesaji mkuu (Girand Inquisitor) wa kanisa
katika zama zetu hizi. Mwezi June mwaka 1971 vyombo viwili hivyo viliunganishwa
na Papa Paul VI karibuni kwenye kila kitu isipokuwa jina.
Kwa mujibu wa Baignet na Leigh, Mkuu rasmi wa kamati ya itikadi za Imani
siku zote ni Papa aliye madarakani na metenaji Mkuu wa Kamati hii leo anaitwa
katibu wake lakini katika zama za kale alikuwa anaitwa mtesaji mkuu (Grand
Inquisitor). Kamati hii ndiyo chombo chenye nguvu kuliko idara nyigine
zote za makao makuu ya Vatican (Roman Curia).
Mapadri chungu nzima wa siku hizi, na wahubiri, walimu na waandishi
wamezibwa vinywa kufukuzwa au ametolewa kwenye kazi zao na kamati hii katika
walioathirika walikuwamo wasomi wanateknolojia waliokuwa maarufu na hoadari
sana kwenye kanisa leo, kwa mfano Father Edward Schillebeck wa Chuo Kikuu
cha Nigwegea nchini Holland, ambaye kitabu chake "Jesus: An Experiment
in Chrstology (1974) kilionekana na wapinzani wake kuhoji kweli ya kufufuka
kwa Yesu na kuzaliwa na Bikira. Mwingine alikuwa mwana teolojia maarufu
wa Kiswiss, Dr. Hans Kung aliyehoji itikadi ya papa asiyekosa na pia akahoji
msimamo mgumu wa Papa John Paul juu ya maadili na itikadi.
Tarehe 18 Desember 1979, John Paul, kutokana na ushauri rasmi wa kamati,
akamvua Kung nafasi yake ya ukuu wa idara ya Dini kwenye chuo kikuu cha
tubngen na akamtangaza kuwa hafai tena kufundisha itikadi za Roma. Kwa
maneno yako mwenye Kung juu ya yale yaliyomsibu, "Nimehukumiwa na papa
ambaye ameyakataa maoni yangu juu ya teknolojia bila hata ya kusoma hata
kitabu changu kimoja na ambaye siku zote amekuwa akikataa kuniona. Ukweli
wa mambo ni kua Roma haisubiri mjadala; inasubiri utii." (Sunday Times
London 2, December 1984).
Baigent na Leight wanasema kuwa kamati hii, chini ya uongozi wa Kadinali
Joseph Ratzinger, katibu wake tangu 1981, imekuwa ikijichimbia mizizi zaidi,
na isiyokubali mabadiliko, ikijitahidi wakati wote kurudi kwenye ukatolki
wa siasa kali na kung'anga'niza kweli ya maandiko kama inavyofasiriwa na
itikadi zilizowekwa na Papa.
Mwezi Mai 1990 kamati ilitoa mswada wa katekisima ya Kanisa katoliki
kwa wote (Universal Catechism of the Catholic Church) mpya, iliyopitiwa
upya na ya kileo - miundo rasmi ya imani ambazo wakatoliki wanawajibika
kuziamini. Kwenye bara moja inayosisitiza itikadi katekisma mpya inaamrisha
kuwa "kazi ya kutoa tafsiri sahihi ya neno la Mungu imewekwa kwenye ofisi
hai ya mafundisho ya kanisa peke yake."
Mwezi June 1990 kamati ikatoa waraka mwiengine uliandikwa na Kadinali
Ratzinger mwenyewe na kukubaliwa na kuungwa mikono na papa mwenyewe. Kwa
mujibu wa waraka huu wanateknolojia wa kikatoliki hawana haki ya kupinga
chochote katika mafundisho ya kanisa, upingaji ukiwa umepewa hakumu ya
dhambi.... utovu wa imani kwa Roho Mtakatifu." Kwenye waraka huo huo, kadinali
Ratzinger anasema:
"Uhuru wa tendo la imani hauwezi kuhalalisha haki ya kupinga. Uhuru
huu hauingizi uhuru kwenye masuala ya kweli, bali unaingiza uamuzi wa mtu
wa imani kukubaliana na majukumu yake ya kimaadili hikubali kweli.
Baigent na Leigh wansema kuwa haya ni maelezo ya ajabu juu ya uhuru.
maana haki kamili ya kukubali mafundisho ya kanisa, lakini hawezi kuhoji
au kuyakataa. Uhuru hauwezi kudhihirishwa na kutamkwa ila kwa kukubali.
Baigent la Leigh wanamaliza kwa kusema kuwa pingamizi hizi ni za kinyama
hata zikilazimishwa juu ya wakatoliki peke yao - za kinyama kwa kiasi cha
madhara zitakazosababisha, madhara ya kisaikolojia na kihisia. Hisia za
kujiona wakosaji, za utovu wa uvumilivu na ukatili utakaojitokeza, maeneo
ya elimu na kuelewa mambo yakatayozuiliwa kufikiwa. Pingamizi hizi zinapohusu
imani huwa zinawafunga wale tu ambao kwa hiari yao wanakubali kuzifuata;
na jumuia za walimwengu ambao si wakatoliki ziko huru kuzipuuza.
Hii, kwa hiyo, kwa kifupi, ndiyo falsafa na mfumo wa mawazo unaotawala
mwenendo wa viongozi wa kanisa katoliki jinsi anavyoyaingia na kuyachukulia
majadiliano yoyote juu ya itikadi za kanisa. Natamka kuwa kwa sababu kanisa
katoliki linahimiza utii wa kipofu, kukubaliana na kila kitu na utii wa
kitumwa kiasi hiki kwa wafuasi wake, haliwezi kuaminiwa kuwa litakaribisha
mijadala na waisilamu, wacha kwamba waisilamu wawambie wakatoliki kuwa
viongozi wao wanakosea na wanawapoteza kutokana na dini yao ya kikristo.
Na hiki ndicho kiini cha mambo kwa kisi kile uhuru wa kueneza dini nchini
Tanznaia unavyohusika. Tanzania ni nchi isiyo na dini na siyo nchi ya utawala
wa dini ya kikatoliki kwa hiyo suala la uongozi wa kanisa katoliki kuwataka
wasiokuwa wakatoliki kufuata tafsiri za kanisa katoliki juu ya itikadi
za kanisa halipo. Wasiokuwa wakatoliki, pamoja na waisilamu, wana haki
ya kuhoji uhalali au kweli ya itikadi hizo. Hii ni haki ya msingi iliyotolewa
na Mungu na haina mjadala. Mradi tu kuhoji huku kunatokana na dhamiri ya
kweli ya kupata kweli ya maandiko, na hakujiingizi kwenye makosa ya jinai
kwa kutumia matusi, wote; viongozi wa kanisa katoliki na serikali, wanawajibika
kikatiba kuiheshimu haki hii.
Kwenye ibara zilizotanguali nimeonyesha kuwa kwa mujibu wa sheria za
Tanzania mihadhara ya waisilamu si ya kukufuru - au ya matusi ya kashfa
kama inavyoelezwa na viongozi wa kanisa katoliki, serikali na vyombo vya
habari vya nchini. Nimeonyesha pia kuwa ulikuwa ni uongozi wa kanisa katoliki
ulioichochea serikali ya CCM kuchukua hatua dhidi ya waisilamu na wahubiri
wa kiisilamu.
Lililobaki kutazamwa sasa ni kama uamuzi wa seirkali ya CCM wa kuchukua
hatua hizi ulikuwa halali kisheria au ni uingiliaji wa moja kwa moja wa
uhuru wa waisilamu kueneza imani yao.
Lazima ikumbukwe kuwa jumiya ya watu huru kweli ni ile inayoweza kuwa
jumuiya ya watu wenye imani mbalimbali nyingi. Jumuiya huru ni ile inayolenga
kwenye usawa wa kufaidi haki na misingi yote ya uhuru. kwa hakika uhuru
lazima ujengwe kwenye kuheshimu haki ya kuzaliwa na haki za asili alizonazo
mwanadamu.
Lazima ikumbukwe pia kuwa kiini cha dhana ya uhuru wadini ni haki ya
mtu kuwa na imani za dini kama mtu atakavyo haki ya mtu kutangaza na kujieleza
imani yake hadharani na bila ya woga wa kuzuiwa au kisasi, na haki ya kudhihirisha
imani za dini kwa ibada na matendo ya ibada au kwa kufundisha na kueneza.
Lakini dhana hii ni zaidi ya hvi. Kimsingi uhuru unaweza kuelezewa kuwa
ni kutokuwapo kulazimishwa au kubanwa. Kama mtu analazimishwa na serkali,
au amri ya mwingine kufanya au kutofanya jambo ambalo kama isingekuwa hivyo
asingechukua hatua hiyo, mtu huyo hafanyi kwa khiari yake mwenyewe na hawezi
akaambiwa kuwa yuko huru kweli.
Mojawapo ya madhumuni makubwa ya katiba ni kulinda, bila ya sababu watu
wasilazimishwe au wasizuiliwe kulazimisha siyo tu ni pamoja na vile vitendo
vya wazi wazi vya kulazimisha kama amri za moja kwa moja za kufanya au
kujizuia kufanya mambo kwa vitisho vya adhabu; kulazimisha kunajumlisha
namna nyingine za kudhibiti; zinazoshawishi au kuzuia njia nyingine za
uamuzi watu wanazoweza kuzichukua. Kwa maana yake pana uhuru unabeba vyote,
kutokuwapo kulazimisha na kuzuia na haki ya kudhihirisha imani na matendo.
Uhuru maana yake ni kwamba, bila ya kuathiri mipaka iliyo ya lazima
kuwapo kwa ajili ya kulinda usalama wa jumuia, utulivu au maadili au haki
za msingi za wengine, hakuna atakayelazimishwa kufanya mambo kinyume na
imani zake au tashi za nafsi yake.
Kwa mujibu wa katiba, Tanzania ni taifa lisilokuwa na dini, hata kama
dhana hiyo inachukiza sana kwa baadhi yetu kwa kuwa ni dhana ya "Freemason"
yenye dhamiri za "kumondoa" Mungu katika maeneo yote ya maisha ya jumla
ya uma na kuiachia dini eneo la mas-ala ya mtu binafsi tu.
Imesemwa kuwa "Taifa lisilo na dini ni taifa linalohakikisha kuwapo
kwa uhuru wa dini kwa mtu binafsi na kwa watu wote jumla, linamshughulikia
mtu kama rais bila ya kujali dini yake, kikatiba haikai upande wa dini
yoyote wala haitafuti kuendeleza ua kuingilia dini "(D.e. Smith - "india
as a Secular State," Princeton Univ. Press, 1963).
Taifa kutokuwa na dini kwa hiyo, linamaanisha kuwapo kwa mchanganyiko
wa mambo kadha - dini kutojiingiza kwenye siasa, taifa kutoibeba jumuiya
yoyote ya dini; kutokuwapo kwa miendano ya upendeleo wa kidini; kutokuwapo
kwa kuwabagua na kuwaweka kando watu wengine kwa misingi ya dini; kusiweko
na ubaguzi kwenye elimu, biashara au ajira kwa misingi ya dini, na kadhalika.
Kimsingi, taifa lisilo na dini linaiona jumuiya kuwa ni ya mchanganyiko
wa dini na tamaduni na muda wote linajiahidi kujenga umoja na mshikamano.
Haitoshi kwa serikali kujisemea tu "haina dini", lazima ijitahidi kuyafikia
malengo haya na lazima ionekana kuwa kweli haina dini.
Tukio la Mwembechai linathibitisha madai ya wasilamu ya kuvunjika kwa
mshikamano wa kisekula nchini Tanzania. Kutokujali kupuuza na kujihusisha
kulikotokea kwa viongozi wa serilai ya CCM, pamoja na Waziri wa Mambo ya
Ndani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Polisi (Taifa) Mkuu wa Polisi
Mkoa wa Dar es Salaam, katika juhudi zao za haraka haraka za kuridhisha
matakwa ya uongozi wa kanisa katoliki ya kuzuia uhuru wa dini wa watu wengine
kumetuwekea misingi ya kuamua kuwa sera za kisekula za nchi zimesahauliwa.
Polisi waliua na kuwatia vilema waisilamu na wakawapiga kinyama, na
kuwatendea mambo ya kinyama waisilamu na raia wengine wanyonge. Kwa kweli
polisi na kikosi cha kuzuia fujo walionekana kufanya kazi yao kama jeshi
lililotayarishwa na kupewa silaha maalumu kwa kazi ya kuwadhalilisha na
kuwaua waisilamu na "wamachinga. Kwa kweli mauaji yale na uumizaji ule
utakumbukwa kenye historia ya Tanzania kama mfano usiomithilika wa ukatili
na unyama uliofanywa na polisi.
Kwa hakika, kutokana na matukio ya Mwembechai na matukio mengine yanayohusiana
nayo, kuna Watanzania wengi - Waisilamu na waisokuwa waisilamu ambao sasa
wanaona kuwa usekula wa Tanzania ni matamanio tu; uongo na si kweli. Maana,
wacha serikali ya CCM kukubali wazi wazi wa uongozi wa kanisa katoliki
uisukume mpaka kufikia kuwatendea waisilamu mambo ya kinyama bila kukumbuka
kuwa umoja wa mataifa na sera za serikali za kisekula vilikuwa vinawekwa
hatarini vile vile kuna ishara nyingine zinazoashiria khatima mbaya, yaani
kutokuwapo kabisa kwa hata kauli za rambirambi za maneno ya kuwafariji
wale waliofiwa na ndugu zao kutoka kwa Raisi, ikiashiria kuwa serikali
ya CCM imeridhika na mauaji ya raia wasio na hatia kana kwamba walikuwa
wahalifu wa kawaida (hata wahalifu wa kawaida wanastahili kutendewa haki);
serikali ya CCM kukataa, kwa kiburi, wito wa Waisilamu wa kuunda Tume ya
uchunguzi huru ya kuchunguza mauaji ya Waisilamu waliouliwa na polisi Mwembechai,
ujumbe wa Waziri Mkuu Frederick Sumaye wa kumpongeza kadinali Pengo tarehe
19 January 1998 (Daily News' 20 January 1998) kwamba serikali imeunga mkono
kuteuliwa kwake kuwa kadinali na kumhakikishia kuwa serikali inamuunga
mkono kwenye majukumu yake peke yake linatia hofu kwenye taifa ambalo ni
la kisekula, linatia hofu zaidi kutokana na yale yaliyofuatia; ziara za
wazi wazi za Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwenye makanisa na misikiti
kama watendaji wa serikali na kutumia nafasi hizo za shughuli za kidini
kutoa kauli za kiserikali za kisekula; serikali ya CCM kukataa na kusita
kusajili jumuiya za kiisilamu na dini nyingine na tishio lake la kuzifutia
usajili bila ya sababu halali; tamko la Makamu wa Rais Bw. Omari Ali Juma,
kuwa serikali ya CCM inalitambua BAKWATA kama ndio chombo pekee rasmi cha
Waisilamu na kukataa kuwa baadhi ya shule kuwaruhusu wanafunzi wa kike
kuvaa vazi linaloagizwa na dini yao (sawa sawa na wafanyavyo masista wa
kiroma na masingasinga kwenye shule hizo hizo). Orodha haina mwisho.
Lazima isisitizwe kuwa yote haya yanafanywa bila ya kujali maagizo ya
katiba. Na yanafanywa na serikali ya CCM ambayo inahesabiwa kuwa ni ya
kimaendeleo, iliyoanza kipindi chake cha utawala na ahadi za kuendeshwa
na katiba, utawala wa sheria, ukweli na uwazai.
Ni jambo la kuzingati kwa hiyo, kuwa, maadamu Tanzania ni taifa lisilokua
na dini serikali ya CCM ingelishughulikia suala la mihadhara ya waisilamu
kwa uangalifu. Kwa kutambua umuhimu wa uamuzi wake juu ya suala linalohusu
uhuru wa dini, na ikijua kuwa Tanzania ina sheria na mahakama inaweza kushughulikia
malalamiko yaliyotolewa na uongozi wa kanisa katoliki, serikali ya CCM
ingechukua msimamo wa kukalia kiti na kukataa kuingilia, ikiacha sheria
ifanye kazi yake. Hii hasa ni kwa sababu muda wote huu kulikuwa hakujatokea
hata mara moja mihadhara ya waisilamu ikisababisha ungomvi au kuvunjika
kwa amani.
Ninaposema kuwa seirkali ingelikaa kando bila ya kuingilia na kuiacha
sheria ifanye kazi yake sina maana hata mara moja ya kupendekeza kuwa serikali
ingejitoa kabisa. Ikumbukwe kuwa kabla ya tamko la Raisi la tarehe 4 januari
l,1998 huko Tabora, serikali ilikuwa ikiyaacha mambo haya yashughulikiwe
na mkondo wa sheria. Tangu mwaka 1993 wahadhiri wa Kiisilamu wamekuwa wakikamatwa
na kushitakiwa mara kwa mara.
Kwa hiyo hakuna suala kuwa serikali haikuwa inajishughulisha na kushitakiwa
kwa wahubiri wa kiisilamu kwa madai ya kutukana ukristo. Hata hivyo katika
kuihimiza serikali ya CCM ikiri nataka tu kusisitiza kuwa suala la mihadhara
ya waisilamu, jambo linaohusu msingi wa uhuru wa waisilamu wa kuabudu na
kueneza dini yao, lilipotoshwa kwa makusudi kwa mpango wa kutoa taarifa
za uongo uliotayarishwa maalumu na kutekelezwa kwenye kampeni iliyoendeshwa
na uongozi wa kanisa katoliki.
Lilikuwa ni jambo la lazima kwa hiyo, kwa serikali inayotakiwa siku
zote kuwa msuluhishi aliyeegemea upande wowote, ikijiweka mbali na upendeleo
wa kidini na udini, kuchukua hatua kwa mujibu wa katiba ya Tanzania isiyo
na dini. Kwa hiyo ilikuwa ni muhimu sana, jambo la busara, kwa serikali
ya CCM kuliingilia suala hili kwa uangalifu wote uliohitajia.
Lakini hata kama tukichukua kuwa serikali ilazimika kuchukua hatua kwa
sababu hali ilikwisha kuwa ya vurugu (jambo ambalo si kweli na seirkali
ilikuwa hairidhiki na jinsi utaratibu wa sheria ulivyokuwa unayaendesha
masuala ya mihadhara, bado serikali ilikuwa na nafasi ya kutumia njia nyingine
halali na inayofaa ambayo ingeweza kutimua mazungumzo.
Rais Mstaafu Mwinyi alijaribu njia hii mwaka 1993 alipoitisha mkutano
Ikulu baina ya maaskofu na masheikh kuzungumza na kuyatafutia ufumbuzi
malalamiko ya uongozi wa kanisa katoliki. Mazungumzo haya hayakufanikiwa
kwa sababu viongozi wa kanisa walishindwa kuleta ushahidi wa malalamiko
yao waliyoahidi kuleta dhidi ya hoja za mihadhara ya Waisilamu.
Lakini hivi hivi tu, kwa sababu zisizojulikana Rais Mkapa mwanadiplomasi
aliyeiva, mwenye uzoefu wa siku nyingi kwa masuala ya matatizo ya migongano
ya kimataifa, alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, hakutaka kujishughulisha
kabisa na njia hii ya kutatulia migongano kwa mashauriano, njia ya maana
kweli kweli ya kujiepusha na magomvi hasa hasa kenye suala kama hili linalohusu
kutokubaliana kati ya dini. ka kweli kuna wasiwasi mkuba kama Rais Mkapa
hata alikuwa na dhamira hasa ya kutumia mazungumzo kama njia ya kulitafutia
ufumbuzi suala la mihadhara ya waisilamu.
Tunasema kuwa serikali nzuri yenye kuona mbali ingeliyatambua mapema
matokeo ya kutumia nguvu kuzuia mihadhara ya waisilamu. Serikali ya haki
na yenye kujali, kabla ya kutoa uamuzi au kuchukua hatua dhidi ya mihadhara
ya waisilamu, ingeita mazungumzo na wote waliohusika - walalamikaji (uongozi
wa kiisilam).
Mazungumzo kama haya, ambamo kila upande ungepata nafasi ya kuelezea
upande wake, yangeipatia serikali njia ya kuepusha mapambano ya aina kwa
ana na kwa hiyo kujiepusha na hali iliyojitokeza sasa ambapo, kwa haki
kabisa, serikali ya CCM inahesabiwa kuwa ni mshiriki mwenza katika sera
za uongozi wa kanisa katoliki za kuzima haki na uhuru wa dini kwa watu
wengine.
Mazungumzo na kushauriana kungeipatia serikali taarifa muhimu kabla
ya kujiingiza kwenye maeneo mapya ya kuingilia uhuru wa waisilamu wa kutangaza
dini yao. Ni muhimu kukumbuka kuwa siku zote ni rahisi kufanya mabadiliko
kwenye hatua ya uamuzi kuliko badaye.
Badala yake, sasa serikali ya CCM, baada ya kuyaharibu mambo, inalazimika
kushughulika na kazi ya kudhibiti uharibifu, ikilazimika pia kusaka vijisababu
chungu nzima ikiwa ni pamoja na kusaka wachawi. Mara, "wenye siasa kali"
ndio walisababisha vurugu za Mwembechai. Mara, ni nchi za kigeni (za kiisilamu)
na balozi za nje.
Wakati mwingine ni wafanya biahara wa humu humu nchini. Au ni vyama
vya upinzani. Tena, wasaliti wa ndani ya CCM, n.k. Sababu na dharura za
kila aina hutolewa kuhalalisha hatua zilizochukuliwa na serikali ya CCM.
Hakuna kujirudi kabisa, na kutafuta miongoni mwao wenyewe waone nini kiliharibika.
Iwe iwavyo ni muhimu kuzingatia kuwa Mheshimiwa Rais Mkapa hajatoa tamko
lolote hadharani kuonyesha ameisimamia wapi kuhusu mazungumzo na mashauriano.
Lakini yeye ni Mwenyekiti wa kamati |Kuu na Halmashauri Kuu za CCM (NEC
na CC).
Kamati hizi mbili za Chama, mara mbili, kila moja kwa wakati wake, ziliipongeza
serikali ya CCM kwa jinsi ilivyolishughulikia suala la mihadhara ya waisilamu.
Na tunajua kuwa kwa sababu ya utaratibu wa CCM wa uhuru wa kushika hatamu
kamati zile mbili za chama wajumbe wake ni pamoja na karibu mawaziri wote
wa serikali. Suala la kujipoongeza' au kujipigapiga mwenyewe mgongoni.
Kuna sababu, kwa hiyo, ya kuchukuliwa kuwa Rais Mkapa hana haja ya kutumia
mazungumzo na kushauriana kama njia ya kupatia magomvi ufumbuzi. Kwa bahati
mbaya sana, kwa hiyo, serikali imeikosa nafasi ya kupata ufumbuzi wa suala
hili kw amani na kikamilifu. Maana kwenye mazungumzo haya kweli ingeonekana
na serikali ya CCM ingekuwa na udhaifu wa madai ya viongozi wa kanisa katoliki.
Kama nilivyosema hapo mwanzo, Tanznaia ina sheria malumu na mahakama
zinazoshughulikia aina ya malalamiko yaliyotolewa na uongozi wa kanisa
katoliki. Hakujatolewa madai kuwa sheria hizi hazifai au kwamba mahakama
zimeshindwa kushughulikia kesi za `kashfa' walizopelekewa. Badala yake
utaratibu wa kushughukia kesi za jinai uliopo unatosheleza kabisa malalamiko
yote yaliyotolewa na viongozi wa kanisa katoliki kusghuulikiwa nazo.
Dosari pekee inayoweza kujitokeza ni uzembe wa polisi wa kutofuata taratibu
wakati wa kukamata washukiwa na kutotoa haki sawa sawa kunakofanywa na
waendesha mashitaka na mahakimu kwa kuwakatalia dhamana wahadhiri wa kiisilamu
kwa sababu zisizo na msingi. Itasaidia kuonyesha kwa kifupi sheria na taratibu
zenyewe:
1. Kifungu 19(2) cha katiba kimeweka uhuru wa kueneza dini, bila ya
kuathiri sheria zianzohusika.
2. Kifungu 129 cha sheria za Jinai limeweka kinga ya makosa kwenye uhuru
wa kueneza dini kwa kulifanya kosa kutamka maneno kwa dhamiri za kuumiza
hisia za dini.
3. `The Criminal Procedure Act, 1985 (CPA) imeweka kuwa kosa la kutamka
maneno kwa dhamiri za kuumiza hisia za dini ni kosa la waranti linalohitaji
taarifa kutolewa chini ya kiapo/affidavit kabla ya waranti wa kumkamatia
mtu kutolewa (kifungu 2(1), 13, 110, 112 na Frist shecule CPA). CPA pia
imeweka taratibu za kutoa dhamana na kusikiliza kesi kwenye mahakama za
chini.
Kutokana na hii, kwa hiyo, kwa sababu utaratibu wa sheria nchini Tanzania
umeweka mwenendo mzuri wa kushughulikia malalamiko ya viongozi wa kanisa
katoliki, mtu angeitazamia seirkali ya CCM, basi baada ya kuitupilia mbali
njia ya usuluhishaji magomvi kwa mazungumzo, angalau ingeiacha njia ya
sheria ifanye kazi yake -ingeutaka uongozi wa kanisa katoliki kufungua
mashitaka/malalamiko yao mbele ya hakimu kama inavyoagizwa na CPA; waranti
za kukamatia kutolewa na watuhumiwa kukamatwa; na kuwaacha watuhumiwa kesi
zao ziendeshwe na zisikilizwe mahakamani.
Lazima isisitizwe kuwa kiini cha tatizo hili kimo katika tafsiri ya
nini ndilo kosa la kusema maneno kwa dhamiri ya kuumiza hisia za dini au
kashfa. Jambo linaloleta utata ni kutokukabaliana kati ya viongozi wa kanisa
katoliki na waisilamu kuhusu nini ni kashfa. Ni mvutano unaohusu suala
la sheria. Hili ni sula la sheria la kuamuliwa na mahakama. Ni jukumu la
mahakama; ambazo ndizo watumishi na walinzi wa sheria. Si kazi ya seirkali
kuamua nini ni kashfa, na nini si kashfa.
Lakini, na kuua maana yake, seirkali ya CCM haikuuacha utaratibu wa
sheria kufanya kazi yake sawa sawa. Kwa kweli, serikali ya CCM haikuzijali
sheria wala katiba iliyokabidhiwa na wanachi kuzilinda. Serikali ya CCM
imesahau kuwa mamlaka yake hayaendi zaidi ya mipaka ya uwezo wake wa kikatiba
na kwamba imejiingiza kinyume cha sheria kwenye maeneo ya mahakama. Katika
haraka zake za kuwaridhisha Viongozi wa kanisa katoliki, serikali ya CCM,
huku ikisahau kuwa kuna tofauti ya maneno na mkazo kati ya madai ya viongozi
wa kansia katoliki na waisilamu, umeonyesha kuwa haiyaelewi kabisa maadili
ya kikatiba na ya kisheria. Sidhani ni lazima kurudia kulieleza kila tendo
na kila tamshi la serikali ya CCM wakati ilipokuwa inalishughulikia suala
hili. Matamshi ya viongozi wa serikali ya CCM tangu hapo yalikuwa yanarudiwa
rudiwa yale yale kiasi cha kuchafua roho. Lakini suala lote linaweza kupatikana
kutokana na taarifa za magazeti na za polisi (kama "haizikusanfiwa"). I
sitoshe tu kusema kuwa bada ya "tangazo la vita" dhidi ya mihadhara ya
waisilamu tarehe 4 Januari 1998 kule Tabora, mambo yakaanza kwenda haraka
haraka. Inawezekana kuwa jukumu la kupambana na wahubiri wa kiisilamu walikabidhiwa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Mkoa, Dar es salaam, Mkuu wa Polisi na
Mkuu wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam; Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wakiwa
wanajipenyeza penyeza hapa na pale. Baadhi ya magazeti nchini yalishiriki
kama vile yalipangiwa kazi ya kuchochea hisia za uhasama dhidi ya waisilamu.
Tukio lote hili linakumbusha mwaka 1968 pale TANU ilipoamua kuchukua
hatua za kudhibiti WAISILAMU kwa mbinu za kugawa na kutawala kwa kuipiga
marufuku East Africa Muslim Welfare Society, iliyokuwa inapendwa na kuwafanyia
kazi safi waisilamu na kuweka badala yake chombo cha BAKWATA. Wakati ule
(kama ilivyo sasa) walitumiwa viongozi wa serikali waisilamu wapenda madaraka
kuongoza kampeni ile; gazeti la serikali, "The Nationalist" likapewa kazi
kuchochea hisia na hamasa za kutwanga uisilamu. Lilikuwa suala la wachezaji
wa zamani ndani ya jezi mpya. Kwa kweli hii ni mojawapo ya sababu zinazowafanya
waisilamu waone kuwa yanayotokea sasa ni marudio tu ya yale yaliyotokea
mwaka 1968. Tofauti pekee mara hii ni kuwa wakati huu limekuwa ni jambo
zito likihusu haki ya waisilamu kutangaza dini, na watu wameuawa na kutendewa
kinyama na kama wanyama.
Kimsingi, matokeo ya kampeni ya serikali ya CCM ya safari hii yamekuwa
kuwatendea waisilamu mambo ya kinyama kuwaua na kuumiza waisilamu, kuwaghasi
waisilamu, kukamata kamata waisilamu bila sheria, kuwanyima waisilamu haki
ya kisheria kwa kuwanyima dhamana , vitisho vya kuzifungia jumuiya na taasisi
za kiisilamu usajili wao, jambo lisilopata kutokea la kufungia na kulinda
misikiti, kupiga marufuku mikutano ya amani ya waisilamu, kuwadhalilisha
kijinsia wanawake wa kiisilamu wakiwa mkononi mwa polisi na mwisho , bali
kwa uzito huo huo vitisho kwa waisilamu.
Njia bora zaidi ya kuielezea hatua ya seirkali ya CCM dhidi ya mihadhara
ya Waisilamu ni kuwa ilikiuka katiba, ilivunja sheria na ilikuwa ya udini.
Serikali ya CCM imetumia utaratibu wa kuendesha mashitaka kuwanyamazisha
waisilamu kwa sababu tu kuwa wasilamu wamekuwa wakitumia haki yao ya kikatiba
kutangaza dini yao. Hatua iliyochukuliwa na serikali ya CCM imekuwa ya
matumzi mabaya ya nguvu za serikali. Kuhoji wenye kufanya uhalifu, serikali
ya CCM ikiwa haijali ile kanuni ya msingi kuwa haki iliyopo ya uhuru wa
nafsi kujiamulia, na dini, inaizuia serikali kuwalazimisha waisilamu kujizuia
kutekeleza wajibu wao wa kuwazindua wakristo juu ya hicho kinachoitwa kweli
ya ukristo.
Aidha, serikali ya CCM, kwa kuchukua hatua za haraka haraka na bila
ya kupima mambo, imeingilia haki ya waisilamu kuhubiri dini yao. Kulazimisha
huku kulikofanywa na serikali ya CCM juu ya waisilamu wasiweze kuhoji itikadi
za kanisa kunamaanisha kuwa serikali ya CCM inaulinda ukatolki. Kulinda
dini moja kwenye taifa ambalo halina dini kumejenga mazingira ya ugawanyiko
ambao matokeo yake ni kuingilia uhuru wa dini unaowekwa na katiba.
Haipingiki kuwa kukubali kuwa serikali ya CCM ina haki ya kuwalazimisha
waisilamu wasihoji ukristo ni jambo ambalo halikubaliani na kweli ya kuhifadhi
na kutimiza uhuru wa kuabudu au urithi wa Watanzania wa kuwa Taifa la watu
wenye mchanganyiko wa dini mbalimbali. Kweli yenyewe ni kwamba waisilamu
wa Tanzania lazima watambue kuwa serkali ya CCM imewakumbusha wao wako
tofauti na hawamo kwenye utamaduni wa kikristo unaotumika kuendeshea nchi.
Lakini lazima isisitizwe kuwa si halali kwa serikali ya Tanzania kulazimisha
kuwa wote lazima wakubaliane na vile viongozi wa kanisa katoliki wanavyotaka.
Tanzania ni nchi ya kisekula na viongozi wa serikali ya CCM siku zote wanatukumbusha
kuwa "serikali haina dini." Nchi hiyo kikatiba, serikali ya CCM hina uwezo
wa kutumia nguvu za sheria zilizopo kufikia lengo la kidini, yaani kufuata
itikadi za kikatoliki kwa kuupendelea ukristo dhidi ya masilahi ya uisilamu.
Pamoja na kutenda kinyume cha katiba na sheria, sirkali ya CCM vile
vile imetudhihirishia utovu wa kuvumiliana usioeleweka na majivuno kwa
vile walivyoyakataa maombi ya waisilamu kufanyiwa haki na kwa uwajibikaji.
Kama vile serikali ya CCM ilivyolikataa mara moja ombi la waisilamu la
kuwekwa tume huru ya uchunguzi juu ya mauaji na kutia waisilamu vilema
waliyofanyiwa na polisi tarehe 13 Februari 1998. Kama vile Waziri wa Mambo
ya Ndani Ali Ameir Mohammed, alivyosema tarehe 4 Machi 1998, "serikali
inayoendeshwa kwa misingi ya utawala wa sheria (?!) haitashinikizwa na
mtu yeyote au kundi lolote kufanya vile wakatavyo wao."
Hii si chochote bali majivuno, hasa pale inapotoka kwa Waziri wa shughuli
za polisi ambao ndio wanaolalamikiwa malalamiko halali. Bila ya shaka yoyote
waziri hajali kuwa yeye anawajibika kwa wananchi kwa matendo ya polisi
wake.
Bwana Ali Ameir, kwa majivuno au kutojua, hajali kuwa utawala mzuri
na haki vinataka kuwa ni muhimu kwa serikali kufanya uchunguzi wa wazi
juu ya mwenendo wa kinyama unaofanywa na polisi kuonyesha kama kuna haja,
au hakuna ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa wa polisi wanaoonekana
kutumia nguvu za polisi zaidi ya vile ilivyo lazima.
Lakini hata kama kusingekuwako na maombi kutoka kwa waisilamu wa kuweka
Tume ya uchunguzi hata hapo, kwa matakwa ya haki na sheria, serikali ya
CCM, ikidai kuwa inajiendesha kwa utawala wa sheria kwa wananchi inawajibika
yenyewe kuteua Tume huru ya uchunguzi.
Lazima ikumbukwe kuwa mauaji na utiaji vilema haviwezi kutenganishwa
na suala la uhuru wa kuabudu. Kwa hiyo, kutokana na kweli kuwa mauaji yale,
bila ya shaka ni suala lenye umuhimu mkubwa kwa uma, serikali ya CCM inawajibika
kuweka chombo kitakachotafuta kweli kuisaidia kuamua juu ya hatua zinazostahili
kuchukuliwa kusahihisha mambo kwa kuyaondoa mabaya yatakayogundulika, na
kufanya yale mema ambayo serikali inayafikiria, kwa mfano, polisi iliyotayarishwa
na kupewa vifaa bora zaidi na vile vile fidia kwa wale waliofikiwa na misiba.
Uchunguzi utagundua chanzo cha mauaji na kutia watu vilema na kuturudishia
imani za watu. Kama uchunguzi wa maana hautafanywa, hisia za kudhulumiwa
na kubaguliawa zitaongezeka. Na wasiwasi, na kuhisi kutokuwapo amani malengo
ambayo serikali ya CCM hujitia kuyalingania pale watakapo kuhalalisha mambo.
Kama nilivyosema kenye utangulizi katika juhudi zake za kuhalalisha
mabavu aliyoyatumia, serikali ya CCM imeleta madai kuwa ililazimika kuchukulia
mihadhara ya kiisilamu hatua zile kwa sababu ya "tishio kwa amani na usalama"
wa Tanzania. Viongozi wa serikali ya CCM wameripotiwa kusema kuwa mihadhara
ya Waislamu ilikuwa inaendeshwa na "wakorofi wachache wenye siasa kali
na kwamba kama siasa kali hizi zikiruhusiwa kuenea zitatishia amani ya
nchi na kutumbukiza kwenye umwagaji damu kama ilivyotokea Algeria.
Ni dhahiri hakuna mantiki kwenye madai haya. Kuhifadhi amani kwa matendo
ya kibabe na matumizi ya mabavu. Kinyume chake, hali huchafuka zaidi kwa
matumizi ya hatua haramu na za kinyama, kuwalazimisha wale wanaotakiwa
kudhibitiwa kufikia pahali ambapo lazima wajihami. Watu wanaofikishwa ukutani
ni rahisi zaidi kujihami kwa nguvu hasa pale wanapoona kuwa wameonewa.
Historia imejaa mifano ya naman hii.
Na kama serikali ya CCM kweli ilikua na lengo la kulinda amani basi
ingejitahidi kutafuta na kutumia njia zote za kupata ufumbuzi wa mivutano
iliyotokana na mihadhara ya waisilamu kwa mazungumzo na kushauriana. Serikali
ya CCM iliikataa njia hii. Na hata kama mazungumzo yasingefaa kulikuwa
hakuna uhalali wa kutumia njia zinazokwenda kinyume na katiba na haramu
badala ya kuiacha sheria ifanye kazi yake.
Hata hivyo, hakuna hata chembe ya ushahidi, hakuna hata mtu mmoja hai
anayeweza kuthibitisha kuwa mihadhara ya waisilamu inahatarisha amani na
utulivu nchini Tanzania kinyume chake kuna ushahidi uliohifadhiwa kwenye
kaseti za video za mihadhara mbalimbali inayoonyesha kuwa mikutano ile
imekuwa ya amani kabisa na ya furaha. Na lililo la kuzingatia sana ni kuwa
mihadhara hii imekuwa ikisilimisha wakristo hadharani (wakati mmoja idadi
yao ilifikia ishirini kwenye mhadhara mmoja).
Watu ambao sasa hivi imani yao imekuwa "ikitukanwa", kama maaskofu wa
kikatoliki na mapadri wao wanavyotutaka tuamini, hawabadili dini na kusilimu,
wajiunge na watu wale wale waliokuwa "wanawatukana." Ni jambo rahisi hata
mtoto wa miaka kumi anaweza kuliona hili!
Kuhusu madai ya kuwapo kwa tishio la "Waisilamu wenye siasa kali Tanzania"
mimi nasema kuwa na hili nalo ni dai la kipuuzi na la hovyo linalotokana
na ushuku na Ishara za CNN" ("CNN Syndrome") - kutazama na kusikiliza sana
vipindi vya televisheni ya CNN ambamo jambo lolote linalohusiana na harakati
za Waisilamu wenye siasa kali." Siasa kali si chochote bali ni mtindo wa
kidini unaofuatwa na muhafidhina wa kiprotestanti wa marekani ulioazishwa
kwenye miaka ya 1920 ambamo wanadai kuwa kila neno la Biblia ni neo la
Mungu na kwa hiyo ni kweli. Hakuna "Uisilamu wenye siasa kali" au "Waisilamu
wenye siasa kali". Kwa mujibu wa Uisilamu, kuna waisilamu kweli na Waisilamu
wanafiki.
Vile vile si sahihi na kukosa mizani kwa viongozi wa serikali ya CCM
kutumia hali iliyopo Algeria kama mfano unaoelekeana na hali ya Tanzania.
Algeria ni moja kwa moja suala la kuingilia kwa jeshi kuwanyang'aya mamlaka
Islamic Salvation Front (FIS) ambao walikuwa wanashinda katika uchaguzi
wa kidemokrasia. Ilikuwa lazima kwa FIS kupinga mapinduzi haya ya jeshi
la kipinga maendeleo.
Kinachoendelea Algeia leo ni vita chafu inayoendeshwa na jeshi la Algeria
wakishirikiana na "serikali" na mgambo wanaodhibitiwa na serikali, kwa
madhumuni ya kuipakazia FIS. Katika vita hii maelfu na maelfu ya Waisilamu
wanaowaunga mkono FIS, au wanoashukiwa kuunga mkono wameuawa au kutiwa
vilema na jeshi la mgambo. "Kukamatwa bandia "kwa viongozi wa mgambo wa
kiraia kulikofanywa hivi juzi juzi baada ya shinikizo kutoka
Tume ya uchunguzi iliyopelekwa na jumuiya ya kimataifa - kulinithibitishia
hili. Kinyume chake, mamia ya mihadhara ya waisilamu hayajaleta, kama nilivyoonyesha
hata tukio moja la fujo. Na tena, mazingira ni tofauti. Nchini Algeria
suala ni juu ya nani ana haki ya kutawala baada ya ushindi halali kwenye
uchaguzi halali wa kidemokrasia. Na Tanzania, suala ni juu ya nani ana
haki ya kutafasiri sheria ya "kashfa" ni mahakama au viongozi wa kanisa
na serikali. Hakuna kufanana hata kidogo.
Ikumbukwe kuwa dhana hii liyozagaa dunia nzima kuwa kuna tishio la wausemao
kuwa ni Uisilamu wenye siasa kali ni uzushi wa watayarishaji wa sera za
nchi za nje wa serikali ya Marekani. Vita vya Baridi vilipokwisha, watayarishaji
wa sera za nchi za nje wa serikali ya Marekani waliamua kuwa "aina kali"
za Uisilamu zingejaza nafasi zilizoachwa wazi na kuporomoka kwa Soviet
Union na Ukomunist. "Uisilamu wenye siasa kali" kwa hiyo ukaonekana kuwa
ni tishio kwa masilahi ya Marekeni dunia nzima na utawala wa Bush ukaamua
kuwa "kuenea kwa Uisilamu wenye siasa kali ndio jambo moja linalowasumbua
watayarishaji sera." kwa hiyo sera za kupinga ukomunisti, kudhibiti na
kuizuia Urusi ya Soviet za serikali ya Marekani wakati wa vita baridi mahali
pake sasa pakajazwa na mtindo mwingine dada wa kupinga Uisilamu uliokazia
hasa kwenye makundi ya "siasa kali" ya Mashariki ya kati na Africa ya Kaskazini,
kwa mujibu wa P.J. Schraeder kwenye kitabu chake "US Foregin Policy Toward
Africa" (Cambridge Univ. Press, 1994) jinsi serikali ya Marekani ilivyoyashughulikia
masuala ya Algeria ni mfano dhahiri wa sera hii - kwamba kuudhibiti na
kuuzuia Uisilamu kumechukua nafasi ya kudhibiti na kuzuia Ukomunisti kama
lengo katika masuala ya usalama linachukua nafasi ya juu mbele ya demokrasia:
"Kinyume kabisa na vile serikali ya Marekani inavyolaani serikali za
kidikteta katika sehemu nyingine za Afrika, watayarishaji wa sera yake,
kwa kushangaza walibaki kimya kabisa pale jeshi la Algeria lilipofuta matokeo
ya uchaguzi wa kidemokrasia wa kwanza na ukachukua uendeshaji wa nchi kwa
mapinduzi ya kijeshi. Kimya cha Marekani hakikusababishwa na imani yao
kwa majenerali kama walinzi wa demokrasia bali kilitokana na sababu kwamba
chama cha Kiisilamu "chenye siasa kali" - Islamic Salvation Front (FIS)
ambacho kiliahidi, pamoja na nyinginezo kampeni, kuiendesha nchi kwa sharia,
kilikuwa karibu kichukue mamlaka ya nchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia"
(uk.258).
Ni jambo la kuzingatia pia kuwa serikali ya CCM vile vile ilijaribu
kuhalalisha mauaji na kuwatia vilema Waisilamu kwa madai kuwa polisi na
polisi wa kuzuia fujo walikuwa na haki ya kujihami nafsi zao. Huku ni kujipurukusha
na kuukataa wajibu inapotokea kwa watu wanaoendesha serikali ambao wajibu
wao ni kulinda na kuhifadhi maisha ya raia wao. Kwa kweli ni jambo linaloshangaza
na lisilokubalika kupendekeza, wacha kudhani, kuwa ilikuwa halali kwa polisi
kutumia sub-machine guns" na risasi moto kuwafyeka raia wenzi wao, pamoja
na watoto wa shule kwa kisingizio kwamba walikuwa wanatupiwa mawe. Kulikuwa
hakuna mashambulizi yaliyotishia maisha au kuumia vibaya kwa polisi ambao
walisimama mbali na watupa mawe.
Hakuna polisi aliyeumizwa au aliyepigwa na jiwe kabla ya kuanza kwa
mashambuli ya risasi. Matumizi ya risasi yalianza bila ya matangazo yoyote
kwa jina la Rais ya kuwaamuru watu waliohusika kutawanyika, wazi wazi vilikiukwa
vifungu 27 na 28 vya Penal Code. Ile kanuni ya kutumia nguvu isiyopelekea
kuua; kidogo au inapostahiki dhidi ya mashambulizi yaliyohatarisha maisha
inayosisitizwa kila mara kwenye mafunzo ya kudhibiti makundi na vurugu
ilikuwa wapi? tukichukulia kuwa mafunzo hayo bado yapo!
Vipi kinga za ngao na kofia za polisi? Hizi hazikutosha kuwalinda polisi
dhidi ya mawe walipokuwa wanatupiwa? Na nini yalikuwa madhumuni ya mabonu
ya kutoa machozi yaliyotumiwa kama si kuwafadhaisha na kupunguza nguvu
za watupa mawe? Wazi wazi ushahidi ulioonekana unaonyesha kuwa matumizi
ya risasi moto yalianza muda mrefu kabla ya vikosi vya kuzuia fujo kufika
na kabla ya tangazo la kuwataka watu kutawanyika kutolewa.
Ni kutokana na sababu hizi mtu anapopata nguvu kuamini kuwa kadinali
Pengo katika mazungumzo yake kwenye kipindi cha "Hamza Kassongo Hour" kilichotolewa
na DTV tarehe 12 Aprili, 1998, angeweza pia kutoa madai ya haki ya polisi
ya kujihami wenyewe, kwa kutumia simulizi za Daudi na Goliathi kuhalalishia
madai hayo. Nani alikuwa Daudi na nani alikuwa Goliathi katika mapambano
ya Mwembechai ambapo watu walikuwa wanaonyesha upinzani wao dhidi ya kuingiliwa
kwa haki yao ya kuhubiri neno la Mungu?
Yaliyotangulia, Mh. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa jumla ni waraka
wangu kwako kuhusu jinsi serikali ya CCM ilivyolishughulikia suala la mihadhara
ya Waisilamu. Ni waraka mrefu, na kutokana na uchache wa elimu yangu, unaweza
hata kuhesabiwa kuwa ni kujikweza. Lakini unatokana na imani yangu kuwa
si mengi ya kutosha yanayojulikana kuhusu mihandara ya Waisilamu na misimamo
ya viongozi wa kanisa katoliki juu ya uhuru wa dini. Siwezi kujidai kuwa
nimefanikiwa kikamilifu katika lengo hili kwani najua upungufu wangu kwenye
elimu inayohusu maswali yaliyozungumzwa. Lakini kama ningefanikiwa kukushawishi
uende ndani zaidi kwenye suala hili hapo juhudi zangu zitakuwa zimezaa
matunda.
Naharakisha kuongeza, hata hivyo kuwa nimelazimika kukuletea waraka
huu kwa sababu hakuna ushahidi kuwa serikali ya CCM na washauri wake wa
mambo ya sheria na siasa, wana dhamiri yoyote ya kujaribu kufikia kwenye
mzizi wa tatizo hili. Kwa kweli kwa kushangaza, kumekuwako na njama za
kuweka ukinifu miongoni mwa waendesha mambo ya kiserikali na kisheria.
Ni dhahiri, kwa vile sina nafasi ya kufikia na kupata taarifa kama serikali
ya CCM hufanya kazi yake kutokana na ushauri inaoupata kutoka kwa washauri
wake wa kisheia, sipo katika nafasi ya kusema kwa hakika ya dhati kabisa
kama ushauri wa kisheria ulitolewa na halikutolewa na kama ushauri huo
ulikubaliwa au ulikataliwa.
Iwe iwavyo kweli inabaki pale pale kuwa serikali ya CCM haikufanya juhusi
zozote za kulishughulikia suala hili kwa haki ili kugundua sababu zake
ni jinsi ya kupata ufumbuzi wake. Kinyume chake kumekuwako na majivuno
tu pamoja na matumizi mabaya ya nguvu za dola bila ya kujali kabisa matokeo
mabaya ya kujiingiza kwenye uhasama na Waislamu kuhusiana na hili, nadhani
ni muhimu kuwa serikali isikubali kuhadika na kushiriki na kuungwa mkono
na baadhi ya viongozi wa kiisilamu na watendaji kunakoonekana. Serikali
itafanya vizuri ikikumbuka kuwa siku zote kuna waisilamu wachumia tumbo
kama vile siku zote kuna wajipendekezaji kwenye siasa na shughuli za umma.
Katika kipindi chote cha "mapambano", serikali ya CCM imekuwa si wazi
na ilikuwa ikitumia ubabe ubabe ikionyesha kutokujali kwake utaratibu wa
kuendesha nchi kwa sheria na ikionekana kuwa dhamiri yake ilikuwa kukandamiza
uhuru wa Waisilamu wa kueneza dini yao. La muhimu zaidi, vile jinsi wakati
serikali ya CCM ilipokuwa inatekeleza jukumu lake halikuwaonyesha kuwa
ilikuwa inajali uhuru wa kuabudu au hata kuma ilikuwa inajali juu ya hisia
za mamilioni ya Waisilamu wa Tanzania.
Juhudi zangu kwa hiyo zimelenga kwenye kufikia haki na kweli, na kwenye
ufumbuzi wa matatizo yaliyosababishwa na utendaji mbaya wa serikali ya
CCM. Wewe, Mh. Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mlinzi wa sheria za Tanzania,
na mshauri mkuu wa serikali kwenye mambo ya sheria, una wajibu wa kudumu
na jukumu la lazima kuhakikisha kuwa mtindo wa kutumia utaratibu wa kuendesha
kesi za jinai kunyamazishia Waisilamu na Watanzania wengine unaachwa mara
moja. Aidha, una wajibu na jukumu la kusikiliza kilio cha Waisilamu kutaka
watendewe haki na kuheshimiwa kwa haki zao za kikatiba za kueneza dini
yao.
Mh. Mwanasheria Mkuu mwanzo wa waraka wangu nilisema kuwa hakuna mtu
anayehoji haki ya kikatiba na kisheria ya serikali kutumia vikosi vyake
vya polisi wa kuzuia fujo siku ya Ijumaa tarehe 13 kwa madhumuni ya kulinda
amani na usalama baada ya mambo kuharibika. Nilihoji, hata hivyo, kukamatwa
kiholela na kibabe-babe tu kwa wahubiri wa Kiisilamu na kwa polisi kuingia
kwa kunajisi msikiti wa Mwembechai kulikotokea Alkhamisi ya tarehe 12.
Nilihoji pia matumizi ya mabavu na nguvu za kinyama mara zote mbili.
Nilionyesha kuwa matendo yale hayakuwa chochote bali uingiliaji wa kibabe
wa uhuru wa Waisilamu wa kuabudu na kueneza dini yao. Pahali pengine nilionyesha
kuwa hakuna ushahidi kabisa wa kuthibitisha madai ya serikali ya CCM kuwa
hatua walizochukua zilikuwa lazima kwa sababu kulikuwa na haja ya kulinda
amani iliyokuwa inatishiwa na mihadhara ya Waisilamu.
Wakati wote, msimamo wangu umekuwa kwamba kuna jambo jingine. Kulikuwa
na kitu ambacho kilikuwa hakijajitokeza. Na linalohusika ni uhuru wa kuabudu
wa mamilioni ya Waisilamu wa Tanzania. Huoni kuwa inashangaza kuwa mpaka
kufikia tarehe 4 Januari 1998 kulikuwa hakujatokea hata tukio moja la fujo
au magomvi ambayo yangeweza kuhusishwa na mihadhara ya Waisilamu?
Kwa nini basi maaskofu wa kanisa katoliki na viongozi wa serikali walikuwa
wamekaa na madai kwamba mihadhara ya Waisilamu ilikuwa inahatarisha amani
ya Tanzania? Na kama kweli itasemwa kina nani hasa kwa hatari kweli kweli
walikuwa wanakazana kuichimba amani ya Tanzania? hawakuwa viongozi wa kanisa
katoliki na wa serikali ya CCM kwa kuchochea hisia za chuki kushitua watu
na hasira za watanzania kwa kuwajengea "picha ya hatari ijayo ya kuvamiwa
na Mujahidina" bila ya uhalali wala ushahidi wowote?
Wahubiri wa Kiisilamu bado mpaka leo hawajui sheria gani ya Tanzania
wanadaiwa kuivunja au kosa gani wamelifanya. Qur'an inawaambia kuwa Yesu
(AS) si mwana wa Mungu. ushahidi wa Biblia unathibitisha imani yao. Sheria
ya Tanzania inakubali kuwa kwa Muisilamu kusema kuwa yesu si mwana wa Mungu
bali ni Mtume wa Mungu si kosa chini ya kifungu 129 cha `penal Code' kwa
sababu ni imani ya kiisilamu. Katiba ya Tanzania imeweka uhuru wa waisilamu
kutangaza imani hii na imani zao nyingine.
Na hata hivyo waisilamu bado wanasumbuliwa, wanazimwa vinywa na wanashitakiwa
kwa kosa ambalo halitambuliwi na Mungu, katiba na sheia za Tanzania. Waisilamu
wataona nini katika haya? Waamini sasa kuwa Tanzania ni nchi ya utawala
wa dini ya kikatoliki; kwamba kosa chini ya kifungu 129 cha `Penal Code'
maana yake ni kuwa kusema yesu si mwana wa Mungu ni kuutukana ukristo;
na kwamba Waislamu hawana haki ya kutangaza dini yao? Hili ndilo linalotakiwa
na uongozi wa kanisa katoliki na wa serikali ya CCM?
Linalotakiwa na uongozi wa kanisa katoliki na wa serikali ya CCM ndilo
linalotakiwa na katiba ya kisekula ya Tanzania na sheria za Tanzania? Sidhani
. Nadhani kuwa muundo wa mchanganyiko wa tamaduni za jumuiya ya Tanzania
unataka zaidi ya hivyo Tanzania inajumuisha watu wa dini nyingi na tamaduni
nyingi ambao, kwa mujibu wa katiba ya kisekula wote wanahitaji kuheshimiwa
haki na uhuru wao, kutobaguliwa, kuvumiliana na amani kwa wa wote.
Rais, mkatoliki na kwa hiyo anatazamiwa kufuata amri na mafundisho ya
kanisa katoliki, akizungumza ex cathedra kwenye mkutano wa viongozi wa
makanisa, anaahidi kutumia uwezo aliopewa na katiba ya kisekula, kuzima
kabisa inapoonekana na kanisa katoliki kuwa inatukana ukristo, hawezi,
kwa kweli kuambiwa kuwa hakuwa anapendelea. Kwa kweli hawezi kuambiwa kuwa
hakuwa anafanya hivyo kinyume cha katiba. Kwa dhati kabisa nafikiri kuwa
Rais atafanya jambo jema kama ataiga mfano wa marehemu Rais Kennedy wa
Marekani ambaye, miaka arobaini iliyopita, katika kampeni zake za kugombea
Urais, akiwa anakabiliwa na mashitaka ya halali ya kutaka kuuvunja ukuta
unaotenganisha kanisa na serikali; alisema:
"Ninaamini kwenye Amerika ambamo kanisa na serikali vinatenganishwa
kabisa - ambamo hakuna kiongozi wa wakatoliki atamuamuru Rais jambo la
kufanya na hakuna mchungaji atakayewaamuru waumini wake nani wampigie kura...
Amerika ambayo rasmi si ya kikatoliki, kiprotestanti, wala ya kiyahudi
- ambamo hakuna mtumishi wa umma anayeomba au kukubali maagizo kuhusu sera
kutoka ... viongozi wowote wa dini... ambamo hamna kura ya wakatoliki;
hakuna kura ya kundi ya aina yoyote... na ambamo uhuru wa dini... haugawanyiki..
mimi si mgombea Urais wa Wakatoliki, mimi ni mgombea urasi wa Chama cha
Democrat ambaye ni mkatoliki. Sisemi kanisa langu kwenye mambo ya umma
na kanisa langu halinisemi" (K.207-208, "Vicars of Christ").
Kwa kauli hizi za kumalizia ningependa kupendekeza hatua chache ambazo
zitatusaidia kurudisha imani na turudie kwenye fahamu kamili. Najua naweza
kusemwa kuwa najivisha majoho ya wenyewe kwa kutoa baadhi ya mapendekezo
haya.
Siombi radhi. Hili, tangia hapo, si jambo binafsi la wachache bali la
umma lenye maana kubwa sana kuhusu uhuru wa mamilioni ya watanzania na
kuhusu amani na utulivu wa jumuiya yetu:
· marufuku yaliyopo hivi sasa juu ya mihadhara ya waisilamu yaondolewa
mara moja. Marufuku haya hayakubaliani na kifungu 19 cha katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanznaia ambayo imeweka haki ya msingi ya dhana ya kuabudu
pamoja na uhuru wa kutangaza dini.
· tume ya uchunguzi huru na isiyo ya upande wowote iundwe na
serikali ipate kuchunguza, inter alia':
(a) polisi kuingia kwa kunajisi msikiti wa Mwembechai tarehe 12 Februari
1998;
(b) mambo yaliyopelekea mlipuko wa tarehe 13 Februari 1998;
(c) Kupigwa risasi na kuuawa/kuumizwa kwa waisilamu watano kulikofanywa
na polisi tarehe 13 February 1998;
(d) Kuumiza na kutiwa vilema waisilamu na wengine ulikofanywa na polisi
tarehe 13 Februari 1998;
(e) Kudhalilishwa kijinsia kwa wanawake wa kisilamu wakiwa mikononi
mwa polisi pamoja na kukamatwa kwao hapo mwanzo;
(f) kukamatwa na kuteswa kwa Waislimau wakiwa mikononi mwa polisi;
(g) kukamtwa kwa waisilamu kwa kuwa nazo nakala na tafasiri za aya za
Qur'an zilizoonekana na polisi kuwa ni za kiadui kwa ukristo;
(h) kama kufungwa na kulindwa kwa msikiti wa Mwembechai kunakubaliana
na katiba na sheria zinazohusika;
(i) kama polisi na vikosi vya kuzuia fujo walifanya kazi zao kwa mujibu
wa taratibu za kudhibiti fujo na makundi ya watu zilizomo kwenye vifungu
77 na 78 vya Penal Code,' `Police Force Ordinance' na `Police Force General
Orders';
(j) kama mwenendo wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Polisi (Taifa)
na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kabla, wakati na baada ya matukio
ya Mwembechai ulikuwa unakubaliana na matakwa ya katiba, na sheria nyingine
zinazohusika, za Tanzania; na
(k) hasa hasa kama tofauti na kutokukubaliana kuliopo kati ya wakatoliki
na waisilamu juu ya mambo yanayohubiriwa na waisilamu kwenye mihadhara
yao zilishughulikiwa na serikali kwa kufuata katiba ya Jamhuri za Muungano
wa Tanzania na sheria nyingine za Tanzania zinazohusika.
· Tume ya uchunguzi iongozwe na Jaji wa Mahakama ya Rufaa na
wa mahakama kuu ya Tanzania na wajumbe wake wakiwa mmoja mmoja kutoka kanisa
katoliki Tanzania, Kanisa la Kilutheri la Tanzania, AL MALID, BAKWATA,
BARAZA KUU, Baraza Kuu la Shia Ithnaashari Tanzania, Tanganika Law Society,
TAWLA, Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu, Dar es Salaam, Idara ya Political
Science ya Kitivo cha Arts na Sayansi za Kijamii Chuo Kikuu, Dar es Salaam
na Taasisi ya masomo ya Maendeleo ya Kijamii Chuo Kikuu, Dar es Salaam
· tume itoe mapendekezo itakayoamua yanastahiki ya kurekebisha
uovu wote utakaoonekana na juu ya hatua zitakazofaa kurudisha mshikamano
wa kiserkali.
· Mwendesha mashitaka Mkuu azipitie upya kesi zote za tuhuma
za "kashfa" dhidi ya Waisilamu kuona kama taratibu za kisheria zilifuatwa
na kufuta mashitaka yote yatakapoonekana kuwa si sahihi.c
· Mwendesha mashitaka Mkuu (DPP) awaagize waendesha mashiaka
kuacha kuwazuilia dhamana washitakiwa waisilamu bila ya sababu na kwa hoja
za kipuuzi. Dhamana ni haki si tunzo.
· Viongozi wa serikali washauriwe kuwa wanakwenda kwenye nyumba
za ibada kwenye nafasi zao kama watu binafsi kuswali na kufanya ibada kama
raia wengine wa kawaida. Kwa hiyo waache mara moja tabia ya kuzigeuza nyumba
za ibada kuwa majukwaa ya kutoa matamshi au kauli zinazohusu mambo ya kisekula
na/au kisiasa na wakatae mialiko ya kuhudhuria shughuli za kidini katika
nafasi zao za kiserikali. Vile vile waache tabia ya kugeuza nyumba za ibada
kuwa ngome zenye ulinzi mkali na barabara zote zinazoelekea huko kufungwa
na polisi wa trafiki kila waendapo kuswali na kufanya ibada (bila ya shaka
wana askari kanzu wa kutosha kuwalinda kutokana na matishio yoyote, halisi
au yanayofikiriwa yanaweza kutokea kwa ajili ya usalama wao).
· Viongozi wa serikali, hasa makamu wa Rais, washauriwe kuwa
sawa na kanuni za serikali ya kisekula serikali haiitambui rasmi BAKWATA
mbele au badala ya taasisi nyingine za kiisilamu zote ziko sawa mbele ya
sheria. Kadhalika serikali iache tabia yake ya kuingilia shughuli za kuendesha
taasisi za kiisilamu au misikiti au kuwalazimisha wasilamu lini na wapi
wanaweza kutekeleza shughuli yoyote ya kiisilamu.
· Serikali ishauriwe kutoa maagizo kwa idara zake zote mashirika
yake na mashirika yake ya umma yote kuheshimu usekula wa katiba ya nchi
katika shughuli zao zote, pesa za umma zisitumike katika kugharamia shughuli
yoyote ya dini.
· Matumizi ya "machine-guns" yanayofanywa na polisi yaachwe mara
moja. Ni silaha ya vita inayotumiwa na wanajeshi dhidi ya adui mwenye silaha
kama hizo na hazikukusudiwa kutumiwa dhidi ya raia wasio na silaha.
Mh. Mwanasheria Mkuu, niruhusu nimalizie kwa maoni yafuatayo. Jambo
la kwanza, ni dhahiri, ni kwamba uhuru wa kuabudu ni kanuni ya msingi inayobeba
ndani yake thamani kubwa. Serikali za kidemokrasia zinaweza kuvunja, na
huvunja, haki za raia. Kwenye jumuiya ya kisekula ambayo ni ya mchanganyiko
wa dini na tamaduni mbalimbali kama yetu taratibu za kuendeshea nchi zenye
nguvu zinahitajika kuhakikisha kuwa thamani kubwa hii haiingiliwi. Watanzania
tukiungana, na kujitolea wote kikamilifu kulinda kweli na haki na tukiamua
kushika uzi ule ule, tutakuwa na hakika kuwa thamani hii, na nyingine hazitaingiliwa
na matendo ya kibabe babe ya kisiasa, au nguvu za dola, au matashi na mawazo
ya sehemu fulani ya jumuiya yetu. Kupingana na kusikilizana kati ya makundi
au masilahi yanayogongana yashughulikiwe kwa mujibu wa sheria na kushauriana.
Serikali na vyombo vyake watekeleze shughuli zao kwa mujibu wa wajibu wao
kisheria. Ni hapo tu ndipo tutakapokuwa na maendeleo katika hali ya utulivu.
Badala yake ni maisha ya samaki na uonevu.
Mapambano dhidi ya mihadhara ya waisilamu, ingawa yalichochewa na viongozi
wa kanisa katoliki, yanaonekana kuongezewa nguvu na kutujua, udini na mawazo
potofu juu ya Uisilamu. Uisilamu ni dini inayoeleweka vibaya sana. Mawazo
yaliyopo ya watu wengi ni kwamba Uisilamu ni mila ya kidini ya ajabu ajabu
ya kiarabu na waisilamu ni watu wa madadi na magaidi. Kwa kweli Uisilamu
umekuwa ukieleweka vibaya mno na kuelezewa vingine mno kiasi kwamba watu
wengi wanaufikiria kuwa ni adui wa aina yoyote ya utulivu, amani na maendeleo;
hawauamini, wanauogopa na wanauona kama tishio kubwa bila ya kuwa kawaida,
kujua chochoe juu yake isipokuwa yale yanayoandikwa na magazeti juu yake
ambayo karibuni mara zote, huwa wamekosea sana ngano za kubuni na makosa;
zaidi kuliko taarifa za kweli. Lakini Uisilamu ni jumuiya ya kidini ya
pili kwa ukubwa duniani leo, ya kwanza ni ukristo. Ni imani inayofuatwa
na karibu watu bilioni moja wanaoishi kwenye kila sehemu ya dunia. Vile
vile ni dini inayoijuwa kwa haraka zaidi kuliko zote duniani. Wamarekani
na Wazungu wanaacha ukristo kuingia Uisilamu.
Tunaishi kwenye zana za misukosuko mikubwa na kutokuwapo kwa hakika
ya maisha. Watu dunia nzima wanapapasa papasa kwa wasiwasi mkubwa kutafuta
cha kumnusuru mwanadamu aliyepoteza dira. Ni kweli, inaweza kuwa kweli,
kuwa leo tunaishi kwenye zama za kofia ya maendeleo na ustaarabu wa nyenzo
za maisha duniani, bali katika maeneo ya thamani na maadili mwanadamu yako
karibu na kufilisika. Kwa mujibu wa Uisilamu matatizo haya ni matokeo ya
mwanadamu kupoteza kule kutambua yeye ni nani mintaarafu ya yeye mwenyewe,
wanadamu wengine na zaidi ya wote, Mwenyezi Mungu ambaye kutoka kweake,
kuwa kwenyewe, na mahusiano ya wanadamu yote, ndiko chanzo. Na mpaka pale
atakapoweza kupata majibu sahihi na yenye maana kwa maswali kiini kwa majibu
wa matatizo yake majibu yanayopatikana na kushikana na hali halisi za msingi
katika maisha yake, na dhati yake halisi ya maumbile, maisha yake yatabaki
hivyo hivyo yananing'inia na kupeperuka bila ya kuwa na pakushikia na bila
ya dira; dhati yake itapotoka na kutawanyika; utu wake ukidhalilika kwa
kuruhusu unyama wake kushika hatamu; na kaumu zake zikiinamiwa na matatizo.
Uisilamu unadai kuwa unatoa, majibu na ufumbuzi, majibu ambayo yanaafikiana
na kupatana na akili, mantiki, hali halisi ya ulimwengu wa maada, na dhati
ya maumbile ya mwanadamu yenyewe. kwa sababu Uisilamu, zaidi ya yote, ni
taswira ya kuwa kwenyewe kamili, ikibeba, taswira hii, kuwapo kwa, na sifa
za Muumba, uhusiano wa mwanadamu naye, nafasi na jukumu lake humu duniani,
na uhusiano baina ya maisha ya sasa na maisha ya Akhera, ambao unaweka
kila kilichopo katika nafasi yake muafaka na unaweka mizani na dira kwenye
maisha ya wanadamu na kaumu zao.
Kwa hiyo ni muhimu kwa Watanzania wale wanaotaka kuelimika na kujua
mambo, kujivua na taarifa za mawazo ya uongo waliyonayo juu ya Uisilamu
ili wauelewe kihalisi, kama ulivyo na kwa taarifa za kweli. Watanzania
wengi wameanza kuyafanya haya. Watu dunia nzima, zaidi na zaidi, wanapata
taarifa sahihi juu ya Uisilamu. Nchini Marekani kuna idadi kubwa inayoongezeka
ya wana taaluma; madaktari, wauguzi, maprofesa, wahandisi wanasheria, walimu,
wafanyabiashara - pamoja na wafanyakazi za mezani na wanafunzi, wanaorejea
(wanaoingia) kwenye Uisilamu. `Prince Charles' wa Uingereza, kama alivyoripotiwa
na `Daily Nation' (Nairobi) la tarehe 29 Octoba 1993, pia ameona kuwa hukumu
juu ya Uisilamu "imepotoshwa kweli kweli kwa kuyachukulia yale ya ukali
zaidi kuwa ndiyo ya kawaida." Katika hotuba yake mbele ya wasomi 500, viongozi
wa jumuiya za kiisilamu, watu wa kanisa na mabalozi iliyotolewa kwenye
shedonian Theatre, Oxford, tarehe 28 Octoba 1993, waandalizi wakiwa "Islamic
Society of Oxford University" Prince Charles alisema kuwa: "Dunia ya Uisilamu
na ya watu wa Magharibi haziwezi tena kuendelea kuwa mbali mbali. Lazima
tushirikiane kwenye ujuzi, tujieleze kila mmoja kwa mwenzake. Uisilamu
unaweza kufundisha leo njia ya kuelewa mambo na kuishi duniani ambayo Ukristo
wenyewe hainayo, umeingia umasiki kwayo, kwa sababu umeipoteza."
Mwisho, kwa sababu suala la kuingiliwa kwa uhuru wa kuabudu kibabe kibabe
linahusu mamilioni ya Watanzania na dunia ya wapenda uhuru, napeleka nakala
za waraka huu kwa watu fulani fulani, balozi, vyama vya siasa, vyombo vya
habari na kwa watu na taasisi zote zinazohusika.
Abu Aziz
Muisilamu
15 May 1998
Nakala kwa:
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !