Msijaribu kuubinafsisha mchakato wa Mtumishi wa Mungu Julius K. Nyerere kutangazwa kuwa Mwenyeheri! Ni Hatari!
Kardinali Pengo amewaonya baadhi ya watu wanaotaka kubinafsisha mchakato wa kumtangaza Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya sifa na utukufu wao binafsi kuwa mwelekeo wa namna hii unaojionesha hata ndani ya Kanisa na miongoni mwa wanasiasa ni hatari katika zoezi zima la mchakato wa Mwalimu Nyerere kutangazwa kuwa Mwenyeheri, hatua ambayo kwa sasa iko katika ngazi ya Kijimbo. Mwalimu Nyerere awe ni mfano bora wa kuigwa kwa majitoleo yake kwa ajili ya mafao ya wengi, ukuu na utakatifu wake, viwe ni sifa kwa Mwenyezi Mungu aliyetenda makuu katika maisha ya Mwalimu.
Kardinali Pengo ameyasema hayo wakati akitoa salam kwa watanzania na watu wenye mapenzi mema, waliohudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu, kama sehemu ya kumbu kumbu ya miaka kumi na mitatu, tangu Mtumishi wa Mungu Mwalimu Julius K. Nyerere alipofariki dunia, Ibada ya Misa iliyoongozwa na Askofu Mkuu Protas Rugambwa, Katibu mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimissionari.
Zifuatazo ni salam na matashi mema kwa watanzania kutoka kwa Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !