Kwa nini Mwalimu Nyerere hakupenda serikali tatu? -2.
Na Elias Msuya, Mwananchi
(email the author)
Mwananchi: Jumatano,Juni19 2013 saa 12:42 PM
Mwananchi: Jumatano,Juni19 2013 saa 12:42 PM
Kwa ufupi
- Tukirudi kwenye Serikali tatu, wiki iliyopita nilitaja utata wa kwanza katika Muungano ambapo ziliundwa Serikali mbili, yaani ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wiki iliyopita nilieleza msimamo aliokuwa nao Baba wa Taifa
kuhusu utawala wa Serikali tatu, ambao sasa umependekezwa katika rasimu
inShare ya Katiba.
inShare ya Katiba.
Pamoja
na kuwashukuru wasomaji kwa kutuma ujumbe wa simu, naona kuna watu
hawakunielewa.Katika makala ile nilikuwa natoa historia ilivyokuwa hadi tukawa
na Serikali mbili. Sikumaanisha kwamba kila alichokiamini Nyerere ndiyo
Watanzania wakifuate.Kwanza ieleweke kwamba, tangu tunapata uhuru hatukuwahi
kuwa na utawala unaowashirikisha wananchi kikamilifu, hata kama kulikuwa na
chaguzi kila baada ya miaka mitano.
Tukirudi
kwenye Serikali tatu, wiki iliyopita nilitaja utata wa kwanza katika Muungano
ambapo ziliundwa Serikali mbili, yaani ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Watu
walijiuliza, iko wapi Serikali ya Tanganyika? Jibu la swali hilo alikuwa nalo
Nyerere peke yake na hakutaka watu waendelee kuuliza. Huu nao ulikuwa utata
mwingine.
Kumbuka
tangu mwaka 1962 baada ya Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika,
mabadiliko makubwa yalifanyika ikiwa ni pamoja na kudhoofisha utendaji wa asasi
za kiraia, vyombo vya habari na ilipofika mwaka 1965, mfumo wa vyama vingi
ukafutwa rasmi.
Hapo
ndipo Chama cha TANU kikashika hatamu za uongozi. Hakukuwa na uhuru wa kutosha
wa kujieleza kwa wananchi.
Nyerere
aliwadhibiti hata wale walioonekana kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa nje ya
Serikali yake.
Mfano
mzuri ni Mwenyekiti wa Chama cha Chausta, James Mapalala ambaye aliambulia
kutiwa vizuizini. Mwingine ni kada wa UDP, Lameck Bugohe ambaye pia alishiriki
kuanzisha TANU; na wengineo wengi. Haikushangaza mwaka 1983 kwa aliyekuwa Rais
wa Zanzibar, Aboud Jumbe akapoteza urais wake kwa kuhoji tu Muungano.
Mwalimu
aliendelea na msimamo wake huo hata baada ya kung’atuka mwaka 1984, na baadaye
alipostaafu uenyekiti wa CCM.
Hata
mwaka 1993, Nyerere alipambana na kundi la Wabunge (G55) waliotaka Serikali ya
Tanganyika.
Mwalimu aliandika kitabu cha ‘Uongozi wetu na
hatima ya Tanzania’ akimlaumu aliyekuwa Waziri Mkuu, John Malecela na aliyekuwa
Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba akidai kuwa hawakumshauri vizuri
Rais Ali Hassan Mwinyi kuhusu suala hilo.
Hadi anafariki, Nyerere hakuwahi kulegeza
msimamo, na sasa umeshikiliwa na CCM. Ni wakati wa wananchi kuamua
wanachokitaka bila kufungwa na historia, itikadi za vyama wala dini.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !