SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI
MHE. MUSTAFA HAIDI MKULO (MB.), AKIWASILISHA
BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA
MWAKA 2009/2010.(UK;55-62)
MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA, TOZO NA HATUA NYINGINE ZA
MAPATO.
69.Mheshimiwa Spika,pamoja na athari
za msukosuko wa kiuchumi unaoendelea duniani, Serikali itachukua hatua za
kuboresha ukusanyaji wa mapato. Kama nilivyoeleza hapo awali,hatua hizi zitajumuisha
kupanua wigo wa kodi ikiwa ni pamoja na kurejea sheria na taratibu
zinazosimamia misamaha ya kodi kwa nia ya kuipunguza na kudhibiti usimamizi
wake.
70.Mheshimiwa Spika,Serikali
inapendekeza kufanyia marekebisho mfumo wa kodi, ikiwemo kurekebisha baadhi ya viwango
vya kodi na tozo nyingine zisizo za kodi chini ya sheria mbalimbali na pia
taratibu za ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali. Marekebisho hayo
yanalenga kuweka mazingira mazuri zaidi ya uzalishaji hapa nchini ili kupunguza
makali ya msukosuko wa uchumi duniani na kurahisisha ukusanyaji wa kodi.
71.Mheshimiwa Spika, mapendekezo
haya pia yamezingatia misamaha ya kodi inayotolewa kwa makundi mbalimbali kama
vile wawekezaji ikijumuisha sekta ya madini, asasi zisizo za serikali na mashirika
ya dini. Tathmini inaonesha kwamba misamaha ya kodi imekuwa ikiongezeka kwa
kasi mwaka hadi mwaka na kufikia wastani wa asilimia 30 ya mapato ya kodi au
asilimia 3.5 ya Pato la Taifa katika mwaka 2007/08. Kiwango hiki ni kikubwaikilinganishwa
na viwango vya misamaha inayotolewa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Mathalani, katika nchi ya Kenya misamaha ya kodi inafikia asilimia 1
ya Pato la Taifa wakati Uganda ni asilimia 0.4 ya Pato la Taifa. Ongezeko la
misamaha linapunguza uwezo wa Serikali kutoa huduma muhimu kama vile
miundombinu ya kiuchumi na huduma za kijamii na hatimaye kupunguza kasi ya kuleta
maisha
bora kwa kila Mtanzania. Misamaha ya kodi pia imefungua
mwanya wa ukwepaji kodi na hivyo kuvuja kwa mapato. Ili kunusuru hali hii,
Serikali inapendekeza kurejea sheria
zinazotoa misamaha ya kodi na taratibu za usimamizi ili kubadilisha mwenendo wa
ukuaji wa misamaha ya kodi. Maboresho yanayopendekezwa yatakuwa chini ya sheria
zifuatazo:-
(a)Sheria ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani;
(b)Sheria ya Kodi ya Mapato;
(c)Sheria ya Ushuru wa Bidhaa;
(d)Sheria ya Ushuru wa Mafuta ya
Petroli;
(e)Sheria ya Fedha ya Serikali za
Mitaa;
(f)Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki; na
(g)Matangazo ya Serikali yanayotoa
Misamaha ya Kodi.
A. Sheria ya
Kodi ya Ongezeko la Thamani:-
72.Mheshimiwa Spika,inapendekezwa
kufanya marekebisho yafuatayo katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura
ya 148:-
(i)Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye matankimaalum
ya kuhifadhi maziwa (heat insulated milk cooling tanks) na vipipa vya alumini (alminium
jerry cans) vya kukusanya maziwa ili kuhamasisha matumizi ya vyombo hivi kwa
ajili ya kukusanya na kuhifadhi maziwa na hivyo kuongeza ubora wa maziwa na
kipato kwa wananchi;
(ii)Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye huduma za kilimo za kutayarisha mashamba, kulima, kupanda na kuvuna
ili kupunguza gharama za uzalishaji kwenye kilimo. Hivi sasa pembejeo za kilimo
na mbolea zinasamehewa kodi hii;
(iii)Kupanua wigo wa msamaha maalum
wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT Special Relief) unaotolewa kwenye maduka yasiyotoza
kodi ya Jeshi la Ulinzi (Defence Forces Duty Free Shops) ili kujumuisha majeshi
yote ya ulinzi na usalama (Armed Forces). Aidha, napendekeza kuweka utaratibu maalum
wa kusimamia msamaha ikiwa ni pamoja na kuandaa na kutangaza katika Gazeti la
Serikali orodha ya bidhaa zitakazohusika na msamaha huo ili kuzuia matumizi mabaya
ya msamaha huo kwa vyombo husika;
(iv)Kupunguza wigo wa msamaha maalum wa Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT Special Relief) kwa asasi na mamlaka za maji safi na taka nchini
ili msamaha huo uhusishe vifaa na huduma zitakazohusika katika ujenzi wa
miundombinu ya majisafi na taka pekee. Hatua hii inalenga kuziba mwanya wa matumizi
mabaya ya msamaha huo;
(v)Kuondoa msamaha wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwenye huduma za kukodi ndege (air charter services)kwani
huduma hizi hutolewa kibiashara kama huduma za kukodi vyombo vingine vya
usafiri ambazo kisheria hulipiwa kodi;
(vi)Kuondoa msamaha wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwenye chai na kahawa iliyozalishwa na kusindikwa hapa nchini
ili kuleta usawa na mazao mengine yaliyosindikwa ambayohutozwa Kodi ya Ongezeko
la Thamani. Hivi sasa mazao yote ambayo hayajasindikwa hayatozwi kodi hii;
(vii)Kuondoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mashine
za elektroniki za kutunza kumbukumbu za mauzo (electronic cash register) kwa
kuwa mashine hizi hazitumiki tena kwa kazi hiyo na badala yake Mamlaka ya
MapatoTanzania wataanzisha, kwa awamu, matumizi ya mashine mpya za elektroniki
za kutunza kumbukumbu za kodi (electronic tax register);
(viii)Kuondoa msamaha maalum wa Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT Special Relief) kwenye mali ghafi na vifungashio
kwa wazalishaji wa ndani wa madawa ya binadamu kwa kuwa wazalishaji wa ndani wa
madawa tayari wanapata unafuu wa kodi kupitia Jedwali la Kwanza ambapo
wanawajibika kulipa kodi na baadaye kurejeshewa. Ili kutoa muda wa kutosha kwa wazalishaji
kujiandaa bila kuathiri uzalishaji, inapendekezwa hatua hii ianze kutekelezwa
rasmi tarehe 1 Januari,2010;
(ix)Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma zaupangishaji
na ukodishaji wa nyumba na majengo (leased buildings and serviced apartments)
isipokuwa zile zinazotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa na Msajili wa Majengo
Hatua hii haitahusisha upangishaji wa nyumba na makazi ya kawaida ya wananchi
kwa vile mapato wanayopata wapangishaji kutoka kwenye ada ya pango hayafikii
kiwango cha usajili cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT registration threshold);
(x) Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye muda wa maongezi
kwenye simu kwa kutumia bei halisi inayoonyeshwa kwenye vocha badala ya bei
nafuu anayotozwa muuzaji wa jumla. Lengo ni kuhuisha mapato yatokanayo na chanzo
hiki cha kodi na kuziba mwanya wa ukwepaji kodi;
(xi)Kupunguza wigo wa msamaha maalum
wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT Special Relief) kwa kampuni za madini, mafuta
ya petroli na gesi ili msamaha huo uhusishe shughuli za utafiti na utafutaji
pekee ambao hufanywa na mwekezaji kabla ya kuanza uzalishaji;
(xii)Kuondoa msamaha maalum wa Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT Special Relief) kwa asasi zisizo za kiserikali (NGOs)
na mashirika ya dini. Hatua hii itahusisha madhehebu yote ya dini ambayo ni
pamoja na Waislamu, Wakristo, Wahindu, Mabohora nk. Hata hivyo, vifaa vya
kiroho na ibada vitaendelea kupata
msamaha wa kodi;
(xiii) Kufuta utaratibu wa sasa wa
kutambua baadhi ya vifaa kama bidhaa za mitaji kwa baadhi ya wawekezaji kwa nia
ya kuvipa unafuu wa kodi (deemed capital goods). Kwa mfano, wawekezaji katika
sekta ya hoteli na utalii hutumia
unafuu huu kuingiza vifaa kama
mashuka, glasi, vijiko, uma na visu ambavyo hutambuliwa kama bidhaa za mitaji;
(xiv) Kupunguza kiwango cha Kodi ya
Ongezeko la Thamani kutoka asimilia 20 ya mauzo hadi asilimia 18 ya mauzo ili kupunguza
makali ya athari za msukosuko wa uchumi duniani. Punguzo hili linatarajiwa
kujenga mazingira ya kuongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari; na
(xv) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye huduma za upakiaji na upakuaji mizigo kwenye meli za hapa nchini
kwa mizigo iliyotoka nje ya nchi na ambayo huduma ya kupakua mizigo kutoka
kwenye meli iliyoleta mizigo kutoka n
je ya nchi ilishatozwa kodi hii.
Hatua hii inalenga kuhamasisha wafanyabiashara kushusha mizigo katika bandari
zetu nyingine za Tanga na Mtwara na hivyo kupunguza msongamano wa meli na
mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.
Hatua hizi katika Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwa pamoja zitapunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
45,078 milioni.
KANISA LANENA.
Saturday, 13 June 2009
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, amesema kulingana na bajeti ya iliyosomwa bungeni jana, maisha bora kila Mtanzania ni ndoto.
Askofu Kilaini alisema Kanisa limesikitishwa na kusononeshwa mno na bajeti hiyo kwa vile imejaa ‘aya’ za kukatisha tamaa.
Alisema hatua ya serikali kufuta misamaha ya kodi kwa vitu vinavyoingizwa na taasisi za kidini kwa ajili ya huduma, imetangaza upya ugomvi na madehebu ya dini na jamii.
Aliongezeka kuwa haelewi sababu za serikali kupuuza kazi njema ya kutoa huduma inayofanywa na taasisi za kidini, hususan makanisa.
Askofu Kilaini alionya kwamba viongozi wa sasa wasijifanye wana busara kuliko Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyeasisi misamaha hiyo kwa sababu alijua serikali haina uwezo wa kutekeleza wajibu wake kikamilifu.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita, alisema hatua ya kufuta misamaha hiyo itaumiza zaidi Watanzania na kwamba, suala hilo linaweza kuwafanya maaskofu nchini ‘kuandamana’ hadi Ikulu. Dk Mtaita alisema huduma wanazotoa ni kwa ajili ya raia wote, akashangaa kuona serikali imeshindwa kuwasaidia.
“Kwa kifupi tutashindwa kuendelea kutoa huduma za afya na elimu tunazotoa, hii ni nyundo kwenye utosi wa wananchi maskini, ambao licha ya kukosa fedha, lakini hata huduma za afya zipo mbali nao,” alisema.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Furaha Tanzania, Jones Mola, alisema amesikitishwa na kufadhaishwa na kitendo cha serikali kufuta misamaha ya kodi kwa mashirika ya dini.
Askofu Mola alisema hakuna kiongozi wa dini anayeondoka na mali, bali miradi mbalimbali inaingizwa nchini kwa lengo la kunufaisha wananchi.
MAELEZO KWA HISANI YA Simon Mhina, Restuta James (Dar) na Salome Kitomari (Moshi).
Mwandishi: Nicky Mwangoka : saa
1:31:00 am
http://karibunyumbani.blogspot.com/2009/06/misamaha-ya-kodi-kwa-taasisi-za-dini.html
SAKATA LA TAARIFA YA CAG.
LHRC nao washinikiza.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) jana asubuhi kiliitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtaka Rais Kikwete awawajibishe mawaziri wote na watendaji wa Serikali wanaohusika katika tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema baada ya uchunguzi wa CAG kubaini kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wakati wa Rais Kikwete kufanya uamuzi wa haraka ya kuwawajibisha wote waliohusika.
“Kwa sasa tunaona wazi kwamba deni la taifa limeongezeka kutoka Sh10.5 trilioni mwaka 2010/2011 na mpaka kufikia mwaka deni hilo limeongezeka mpaka Sh14.4 trilioni na kwamba bado kuna misamaha ya kodi kiasi cha Sh1.02 trilioni jambo ambalo ni la hatari kwa uchumi wa taifa,” alisema Bisimba na kuongeza:
“Kama fedha hizi zingepata usimamizi mzuri, zingeweza kujenga kilometa 1,000 za barabara bila kuomba misaada kutoka kwa wafadhili. Jambo jingine la kushangaza ni kuwepo kwa mishahara hewa iliyolipwa kwa walimu wa vyuo vikuu 17 ambapo Serikali imepoteza Sh1.9 bilioni ambazo zingeweza kutumika kuwakopesha wanafunzi zaidi ya 1,000.”
“Tunamuomba Rais Kikwete alitilie uzito suala hili kwani kuna mambo mengi yamejitokeza wazi na kuonyesha kwamba mawaziri wake siyo watendaji makini kwani imefikia wakati wao kwa wao wanatofautiana katika uamuzi jambo ambalo sisi kama Watanzania linatushangaza.”
“Tumeshangazwa sana kuona utovu uliokithiri wa nidhamu na kukosekana kwa uwajibikaji unaofanywa na mawaziri kwani wamekuwa wakitofautiana wao kwa wao jambo ambalo hata viongozi wa juu kama Waziri Mkuu wamelinyamazia bila kuchukua hatua zozote hali ambayo inazidi kutuchanganya.”

Mawaziri ambao wizara zao zilibainika
kuwa na vitendo vya ubadhirifu wa mali ya umma katika ripoti hiyo ya CAG
na hivyo kushinikizwa kujiuzulu ni Waziri wa Nishati na Madini, William
Ngeleja; Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu; Waziri wa Fedha; Mustafa
Mkulo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, George
Mkuchika.
Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Waziri wa Viwanda na Biashara; Dk Cyril Chami.
Nape alisema Kamati Kuu iliyokutana jana ilipokea taarifa mbili ikiwemo uamuzi huo wa Rais kulisuka upya baraza la mawaziri kutokana na ripoti ya CAG.
Alisema pamoja na taarifa hizo, Kamati Kuu ilipokea taarifa ya jinsi Rais alivyopanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji serikalini na viongozi wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioainishwa na CAG, kamati za kudumu za Bunge na wabunge.

SOURCE:http://lectureskills.blogspot.com/2012/04/hatimaye-kamati-kuu-ya-chama-cha-ccm.html
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !