Mizengo Pinda: Nasema wapigwe tu
Na Waandishi Wetu (email the author)
MWANANCHI>Posted Alhamisi,Juni20 2013 saa 20:57 PM
MWANANCHI>Posted Alhamisi,Juni20 2013 saa 20:57 PM
Kwa
ufupi
Lazima
tuwakamate na kama katika kuwakamata watafanya jeuri, jeuri, watapigwa tu kabla
ya kupelekwa tunapotakiwa kuwapeleka, kwa sababu hatuwezi kuendelea na hali
hii, mkadhani kwamba tutafika tunapokwenda.
SHARE
THIS STORY
Dodoma/Dar
es Salaam.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda ameagiza vyombo vya dola kuwashughulikia kwa kuwapiga wale
watakaokataa kutii amri wakati wakifanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Akizungumza
katika Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma
jana, Pinda alisema watu wanapokaidi wanajitakia matatizo na vyombo vya dola.
Alisema
hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM),
Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na
kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi
cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola
vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama
Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”
Waziri
Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya
dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi,
utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii
tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa
kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri
zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna
nyingine... maana tumechoka.”
Pinda
alisema Serikali imedhamiria kurejesha amani nchini ikiwamo mkoani Mtwara na
kuwataka Watanzania waiache Serikali ifanye kazi hiyo. Alisema Serikali ina orodha
ya watu wanaosemekana kuwa ni vyanzo vya vurugu na matatizo yaliyotokea Mtwara
na kushangaa wale wanaopinga kukamatwa kwao.
“Lazima
tuwakamate na kama katika kuwakamata watafanya jeuri, jeuri, watapigwa tu kabla
ya kupelekwa tunapotakiwa kuwapeleka, kwa sababu hatuwezi kuendelea na hali
hii, mkadhani kwamba tutafika tunapokwenda. Nami nasema vyombo vya dola
vijipange imara vihakikishe vinadhibiti hali hii,” alisema.
Hata
hivyo, jibu hilo lilipata upinzani wakati Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said
Haji alipomwuliza Waziri Mkuu: “Hapo awali umetoa kauli nzito ya kuliambia
taifa hili kwamba wale raia wote, ambao watakaokuwa wakaidi wapigwe tu na
watapigwa tu; naomba ninukuu Katika Ibara ya 13 na Kifungu cha 6B cha Katiba ya
Jamhuri ya Muungano.
“Ni
marufuku kwa mtu yeyote aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kuteswa kama mtu mwenye
kosa, mpaka itakapothibitika anayo hatia kwa kutenda kosa hilo.
“Pia
ibara hiyohiyo Kifungu cha 6 E; kinasema ni marufuku kwa mtu yoyote, kuteswa,
kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazoweza kumdhalilisha. Kwa kauli yako
uliyoitoa huoni kwamba umevunja Katiba?” Akijibu swali hilo, Pinda alisema ni
lazima kutofautisha kati ya mtu aliyekwishakamatwa na kufikishwa mbele ya
vyombo vya sheria... “Mimi ninayemzungumza hapa ni mtu yule ambaye ameamua
kufanya vitendo hajakamatwa na ndiyo maana nilikwambia usiandamane... hapa
mahali hutakiwi kwenda wewe ukaamua kutumia mabavu kwa sababu mko wengi, ndiyo
maana nikasema, hawa watu tutashughulika nao hivyohivyo.”
Mbunge
huyo hakuridhishwa na majibu hayo na kumtaka Waziri Mkuu kuyafuta.
Hata
hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliingilia katika na kumweleza mbunge huyo
kuwa kila mtu alikuwa amemwelewa Waziri Mkuu na hakukuwa na haja ya kuendelea
na hoja hiyo.
Kabla ya swali lake la nyongeza, Mangungu
aliuliza: “Ukisikiliza nyimbo nyingi za taifa katika Afrika zinasema hekima,
umoja na amani ndiyo ngao zetu. Je, hali ambayo imejitokeza katika nchi yetu na
matatizo yaliyojitokeza Arusha na maeneo mengine kama Mtwara. Nini tamko la
Serikali?
Waziri Mkuu alijibu: “Swali lililoulizwa na
Mheshimiwa Mangungu ni jambo linalotugusa sisi wote. Suala la amani, ulinzi,
utulivu ndiyo hasa tunu ya kila nchi ingependa kuwa nayo. Ni kweli hivi
karibuni kumejitokeza vurugu za hapa na pale kwa hiyo angependa tuwaeleze
Watanzania kama Serikali tunafikiria tufanye nini.
Alisema ipo haja ya jukumu hilo kuachwa kwa
viongozi wa kisiasa bila ya kujali itikadi zao... “Yako mambo ambayo lazima
tukubali kwamba ni jukumu letu sisi wote na kila mmoja lazima azungumze lugha
moja.
Ninyi wote ni mashahidi. Chadema waliposhinda
hapa, wao walikuja waziwazi, wakasema tutahakikisha nchi hii haitawaliki. Sasa,
inawezekana pengine ndiyo mwendelezo wa utekelezaji wa kauli hizo.
“La pili ni upande wa Serikali, lazima
tuhakikishe kwamba wale wote ambao kwa kweli wanajaribu kuvunja amani kwa namna
yoyote ile, kazi kubwa tuliyonayo ni kubanana, kupambana kwelikweli kwa njia
zozote zile zinazoonekana zinastahili.
“Sasa mimi ninaomba sana Watanzania, maana kila
juhudi zinapoonekana zinaelekea huko, unapata watu wengine wanajitokeza,
unajua...unajua. Acheni Serikali itimize wajibu wake kwa sababu jambo hili ni
la msingi, lazima tulilinde kwa nguvu zetu zote.
“Rai yangu kwa Watanzania kila mmoja ajue kwamba
siku tukiingia katika vurugu, hakuna mshindi. Wote tutaumia, sasa wote
tuhakikishe hili jambo tunalisimamia vizuri.”
Chadema waja juu.
Akizungumzia kauli hiyo, Mkurugenzi Habari na
Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema: “Kauli ya Pinda inakiuka Katiba ya nchi
na imethibitisha kwamba matumizi mabaya ya vyombo vya dola na kusababisha
mauaji ya raia yana baraka za Serikali.”
Alisema kauli ya Pinda kama ilivyokuwa ya Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi zinatoa
mwelekeo kwamba mauaji ya Arusha yana baraka za Serikali.
Wanasheria wakerwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema Waziri Mkuu hakustahili
kutoa kauli kama hiyo.
Alisema Pinda hapaswi kuwa na jazba, bali
anatakiwa kuwa na busara na kuzungumza kwa kuzingatia sheria za nchi badala ya
kutoa matamshi ambayo siyo mwafaka kwa nchi inayoongozwa kwa kufuata sheria na
taratibu.
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS),
Francis Stola alisema kauli hiyo ya Waziri Mkuu, mbali ya kwenda kinyume cha
Katiba na sheria ya nchi, inaweza kuhatarisha amani.
Stola alisema matumizi ya nguvu kupita kiasi
kudhibiti hali yoyote korofi hayaruhusiwi.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !