…FBI watua kuchunguza
“Ndugu zangu, nawapa pole sana, Serikali yenu inakesha usiku na mchana, napenda kuwaambia leo (jana) tumepokea askari wa FBI hapa kwetu wamekuja kuongeza nguvu ya kuwasaka wahalifu hawa.
“Tunawaomba mwendelee kutusaidia kwa kila aina na taarifa zenu tutazifanyia kazi muda wote, tutahakikisha wote waliohusika wanatiwa mbaroni,” alisema Mulongo.
Kwa upande wake, Pinda alisema amesikitishwa na tukio hilo ambalo mpaka jana jioni limesababisha vifo vya watu watatu.
Alisema kwa wale wote ambao wamefariki, Serikali itagharamia mazishi yao kwa gharama na watazikwa kwa heshima zote zinazotakiwa.
“Nimemwagiza RC Mulongo, kuhakikisha wanafuatilia wale wote ambao wamefariki wanazikwa kwa gharama zote za serikali.
“Pia nimemwagiza ahakikishe majeruhi wote wanaendelea kutibiwa kwa gharama za Serikali na hata wale ambao wameruhusiwa kwenda majumbani mwao, wafuatilie ili kujua wanaendeleaje,” alisema Pinda.
Alisema taarifa alizonazo, ni kwamba majeruhi mmoja aliyekuwa akikimbizwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu alifia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
“Majeruhiwa wengine 24, wameruhusiwa kwenda nyumbani na wengine wanaendelea na matibabu.”
Alisema hadi jana jioni, polisi walikuwa bado wanamshikilia mtuhumiwa mmoja, Victor Ambrose (20), ambaye anadaiwa kuwa alirusha bomu hilo.
“Mpaka leo (jana), kuna Victor Ambrose anashikiliwa na polisi, nawashukuru watu wote waliomfukuza na kumkamata baada tu ya tukio hili kutokea,” alisema Pinda.
Alisema Serikali katika tukio hili, kamwe haitakwepesha ukweli na itatoa taarifa zote kwa wananchi.
Naye Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), aliwaambia waumini hao kuwa Yesu alikufa msalabani na mwisho wa siku alifufuka na kushinda dhambi na mauti.
SOURCE:MTANZANIA.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !