- Kitoloho
Headlines News :
Home » »

Written By Msamaa on Friday, May 3, 2013 | 1:14 PM

RAIS KIKWETE AMTEUA MEJA JENERALI SAMUEL ALBERT NDOMBA KUWA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, JENERALI RAPHAEL MUGOYA MUHUGA KUWA MKUU WA JKT



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba  (pichani kushoto) kuwa Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Aidha,
Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali. Taarifa
iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais –
Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.

Taarifa
hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba
alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Jenerali
Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman  A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu
wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
            
Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema
kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (pichani kulia) kuwa Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012. 
    

  Aidha,
Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali. Kabla
ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Imetolewa
na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Septemba, 2012
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

ZILIZOSOMWA SANA.

Followers

Blog Archive

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Kitoloho - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template