RAIS KIKWETE AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME YA YA MAADILI YA UONGOZI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Jaji Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na wajumbe wa tume hiyo katika sherehe zilizofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wajumbe wa tume hiyo ambao pia waliapishwa ni pamoja na Jaji Hamis Msumi na Ndugu Gaudios Tibakweitira.Pichani Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kupokea miongozo ya kazi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Tume ya Maadili ya uongozi muda mfupi baada ya kuwaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto ni Jaji Hamis Amir Msumi,Ndugu Gaudios Tibakweitira na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Jumanne, Mei 11, 2010, amewaapisha wajumbe wa Baraza la Maandili ya Uongozi.
Katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwapisha Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji Damian S. Lubuva.
Rais pia amewaapisha wajumbe wawili wa Baraza hilo ambao ni Jaji Hamisi Amir Msumi na Mheshimiwa Gaudiose Tibakweitira.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
11 Mei, 2010
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !