Ndugu zetu, Wazee wetu,
Assalaam Alaaykum,
UMOJA, UHURU, UADILIFU
Waraka Maalum Kwa Wakristo Zanzibar
Tunaleta hapa huu “Waraka maalumu kwa Wakiristo Zanzibar”. Waraka
huu umepatikana na Waislamu, Zanzibar katika nusu ya pili ya mwezi wa June,
2009. Waraka huu unaonesha dhaahir shaahir mbinu zao dhidi ya Waislamu,
Wazanzibari. Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala Inshaallah awashinde
na kila uwovu wao, Yaa Rabbi kula ajae na shari, waijua yake siri, ivunjé yake
dhamiri asiweze kusimama; Aamyn, Yaa Rabbi Aamyn. Tutajaribu kueleza juu ya
waraka huu kwa khati za Italic
kama ifuatavyo humu. Tulioyakoleza kwa khati nyekundu ndio tunaona khatari
yake zaidi na kutaka tuyafahamu zaidi na tujikinge nayo. Muhimu, tafadhali
tuusome waraka huu tupate kufahamu mbinu zao na chuki zao dhidi ya Waislamu,
Wazanzibari; ili tutahadhari nao. Muhimu tusisahau
Qauli ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Ta’aala alipotueleza juu ya uovu wa hawa
wenye kuwapiga vita Waislamu, Wazanzibari kwa jina la Ukiristo.
“يآأيها اّلذين آمنوا لا تتخذوا بطانة من دونكم لايألونكم خبالا، ودوا
ماعنتم، قد بدت البغضآء من أفواههم، وماتخفى صدورهم أكبر، قد بينا لكم اللآيات ان كنتم
تعقلون”. (آل عمران : 118).
Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi.
Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha
fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo fichwa na vifua vyao ni makubwa
zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini”.
(Al-‘Imraan : 118).
Lakinibasi, kuyafahamu ni ndivyo; bali kuyaondoa ni waajibu wa kila
mmoja wetu kwa kadiri ya uwezo wake. Hapana shaka ndugu zetu walioko kwenye
madaraka na uongozi na sisi,
waongozwa kushirikiana nao na kwa hikma na busara, wao ndio wenye wajibu zaidi wa kuchukuwa khatuwa za kuyaondoa maovu
hayo, tena hufuatia wenye vyombo vya khabari na mashekhe wanye kuwaidhi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala atujaalie
kila la kheri na baraka; Aamyn.
Wa Billahi Tawfiiq
Umoja wa Wazalendo
Zanzibar
June 24, 2009
WARAKA MAALUM KWA WAKRISTO ZANZIBAR
Wapendwa katika Bwana
Ndugu Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni
machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa Zanzibar,
yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna
yoyote. Hapana shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa bado
ni ndogo sana na wengi wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio
Wazanzibari kama wanavyosema wenyewe.
Wanatwambia, “….yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna
yoyote”. Qauli yao hii inadhihirisha vipi walivyo
azimia kuendeleza mbinu zao ovu dhidi ya Uislamu hapa kwetu, Zanzibar.
MAFANIKIO YETU
Kabla kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana
budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi sasa.
Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa
tumsifu Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui
zetu. Tunaamini kuwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, Bwana
atatupa ushindi na mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu
wazidi kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha
Zanzibar kidemografia ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho.
Mafanikio yetu yameenea katika kila upande - katika uchumi, siasa, huduma za
serikali, umiliki wa ardhi, ujenzi, elimu, n.k. Ili kupata picha kamili ni vyema
tuorodheshe kwa ufupi mafanikio hayo:
“Pamoja na jitihada zetu za muda
mrefu bado tunapaswa tumsifu Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu
dhidi ya maadui zetu”. Wameanza kwa
kusema, “Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu”, hii ni ithbati ya hali
kwamba mbinu zao dhidi ya Uislamu “ni za muda
mrefu”, wakaendelea kueleza,
“dhidi ya maadui zetu”, yaani sisi
Waislamu ndio “maadui wao”. Hivi kuwa wao Wakiristo wanatufanya sisi ni “maadui
zao”, hufaa tujiulize lipi la uadui tuliloufanyia Ukiristo sisi Wazanzibari,
tangu taarikh ya miaka, bali karne nyuma? Ingelikuwa vyema kama wangalitueleza
uadui tulioufanyia Ukiristo au Wakiristo sisi Wazanzibari. Hauko, wala
hawawezi kutaja hata moja; tunawataka wataje kama uko. Lakini ihsani nyingi
tumeufanyia Ukiristo hio miaka mingi iliopita, ni Ufalme wa Zanzibar uliowapa
Wamishinari hapa Zanzibar nyumba ya kuendeshea ibada zao na kuwapa waongozi wa
njia kuelekea barani Afrika kwa kuondokea hapa Zanzibar. Hapana shaka maneno
haya hayakubaliwi na ndugu zetu Wakiristo wa Kizanzibari ambao tumeishi miaka na
miaka kwa masikilizano na mapenzi, kwa la furaha na kwa la msiba; daima tuko
pamoja. Tumeishi katika ustahamilivu mkubwa wa imani mbalimbli, bali hata mila
mbalimbali, hapakuwepo yeyote kumbughudhi mwengine; sote tukiishi kuwa ni
Wazanzibari. Hakika ni kwamba hawa wenye maneno na mbinu hizi za ufisadi sio
Wakiristo wa kweli, hawa ni mishinari wenye kufanyakazi begakwabega na wakoloni
tangu karne na karne katika misingi ya siasa yao ya “WAGAWE ILI UWATAWALE”. Wanafanya hivi si kwa
maslaha ya Ukiristo, wanafanya hivi kwa maslaha yao ya kutoamini dini
“secularism”, na kuitumia imani kuwa ni njia ya chumo la kujaza mifuko yao.
Wamishinari hawa na wakoloni karne na karne mbinu zao ni fitna za kuwagawa Umma
ili waendeleze maslaha yao. Huwagawa Umma kwa kutumia dini, ukabila bali hata
rangi, kipato au madaraka.
1.
Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekua ya kuridhisha kupitia nafasi za serikali. Hivi sasa ni rahisi
na limekua jambo la kawaida katika kila matangazo ya wito wa masomo kusikia
majina ya Wakristo. Kati ya vijana saba hadi kumi,
ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka katika makanisa
yetu. Qauli yao kuwa “kupitia
nafasi za serikali”, hapana shaka, hivi
ni kwa kuwa Tanganyika wao ndio dola, wao ndio sirikali, wao ndio wenye kupanga
na kupangua kukhusu ilimu. Kati ya vijana
7 hadi 10, ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka katika makanisa
yetu. Ikiwa wao Wakiristo walioko
Zanzibar, ambao haidhaniwi kuwa wanafika 10% ya Wazanzibari; wanapata baina ya
20% hadi 30% ya fursa za masomo; itafahamika vyema mbinu wanazozitekeleza (wao
Wakiristo) katika kuwazuilia fursa za masomo Wazanzibari, Waislamu; hilo ni
miongoni mwa maazimio yao makuu. Waislamu, Wazanzibari wasipate ilimu ya maana;
walazimishwe kuishi katika ujinga.
2. Sambamba na matangazo ya elimu vijana
wetu wamekuwa wanapata nafasi nyingi za ajira katika Serikali ya
Zanzibar. Hali ya kutoelewana kisiasa
baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa Kikristo wenye asili
ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika zaidi kuliko vijana wa
Zanzibar. Tuizingatie hii qauli yao,
“vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi nyingi za ajira katika
Serikali ya Zanzibar”. Hali hii si
ajabu, kwa sababu wao Tanganyika ndio wenye sauti na amri ya kuajiri, tangu huko
bara na hapa visiwani. Inasemwa na wengi kwamba hapo BoT, (Bank of Tanzania)
(Bank of Tanganyika), hata mpika chai, licha ya dereva; anajiriwa kutoka bara,
Mzanzibari hafai. “Hali ya
kutoelewana kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa
Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika zaidi kuliko
vijana wa Zanzibar”. Naam, hii ndio
faida khasa ya wao kupanga na kutekeleza hali ya kutoaminiana na kuvutana
Wazanzibari, lakinibasi, hilo lishapitwa na wakati. Alhamdulillahi, leo
Wazanzibari wakiwa kwenye Umoja wao wa Wazalendo wote qauli yao ni moja juu ya
kila la Nchi yao, kwa maslaha ya Nchi yao, hawana tena siasa za kichama, siasa
zenye kutumika kwa kujenga mfarakano baina yao. Wajuwe na watambue hawa mabwana
wenye kujiita wakiristo kwamba uwaminifu wa vijana wa Kizanzibari kwa jumla ni
wa daraja ya juu kabisa, wachache ulimwenguni wa mfano wao. Hali hii si ajabu
hata kidogo, kwani haya ndio malezi ya wazee na wazee wa wazee wetu, uwaminifu,
mapenzi, kusaidiana, kushirikiana, kushauriana na ustahamilivu wa kidini ndio
sifa ya Wazanzibari tangu karne na karne. Suala la kuajriwa zaidi vijana wa
Kikiristo kuliko vijana wa Kiislamu, Kizanzibari; katika nchi yao wenyewe,
Zanzibar; ni miongoni mwa mbinu zao Wakiristo katika kuongeza idadi ya Wakiristo
hapa visiwani ili wajaze makanisa yao. Wanafanya hivyo ili waweze kudai misaada
kutoka huko Uzunguni, kutoka makanisani na/au watubinafsi, hivyo wapate fedha
hizo wajaze mifuko yao kwa kisingizio cha kueneza Ukiristo. Vilevile katika hivi
kuwapatia zaidi ajira vijana wa bara wanaowajaza hapa nchini mwetu bila ya
kitambulisho chochote cha uingiaji nchini, ni katika kuiandalia (CCM) “Catholic
Christian Movement”, “Chama Cha Mwalimu”, kuandaa wapigakura kwa makusudio ya
kuendelea madarakani katika kuitawala Zanzibar na kuendeleza mbinu zao dhidi ya
Waislamu, Wazanzibari. Ndugu zetu Wazanzibari mulioko kwenye uongozi, katika
vyama na/au Sirikalini, na Wazanzibari sote kwa jumla, haya ndivyo yalivyo;
tafadhalini tukumbuke hii Qauli ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala
anayotutaka tuokoe nafsi zetu na ahali zetu kutokana na adhabu kali ya
Moto:
“يآأيّها الّذين آمنوا قوا أنفسكم وأهليكم نارا وقودها النّاس والحجارة
عليها ملائكة غلاظ شداد لا يعصون الله مآأمرهم ويفعلون مايؤمرون.” (التحريم :
6).
" Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu
wenu, na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali,
wenye nguvu hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri zake; na wanatenda wanayo amrishwa
(yote)”. (At-tahriim : 6)..
3.
Hali tulioieleza juu imetuwezesha kuwa na Wakirsto wengi katika
nafasi za juu serikalini na katika chama tawala. Tunarejea tena kufahamishana sisi
Wazanzibari, Waislamu; yote haya wanajifanyia, au wanafanyiwa wao Wakiristo kwa
sababu wao ndio wenyewe dola, na wao ndio wenyewe khasa chama, bali wao ndio
khasa wenye khatamu za uongozi wa Tanganyika, Tanganyika ambayo ndio yenye
kuitawala Zanzibar baada ya kuivamia na kuimeza siku ile ya Januari 11, 1964.
Kutokana na hali hii, ilivyo ni hivi; Tanganyika inatawaliwa na Kanisa, Zanzibar
inatawaliwa na Tanganyika, kwahivyobasi, Zanzibar inatawaliwa na Kanisa.
Wazanzibari CCM sio yao, Wazanzibari, Waislamu; si wanachama wa “Chama Cha
Mwalimu, “Chama Cha Msalaba””, chama hichi wenyewe khasa ni wao wenyekujiita
wakiristo.. Hali hii ni lazima
iendelezwe katika ngazi zote kwani imekuwa ikitusaidia hasa katika kiwango cha
masheha na kamati zao kwani huku ndiko kunako mambo mengi ya kila
siku. Hizi ndizo mbinu zao ovu kuwatendea Waislamu, Wazanzibari.
Kwa hivi kuwa mbinu zote hizi zinafanywa kwa kushirikiana makanisa na utawala
Tanganyika; kwa vile wao Tanganyika ndio dola na ndio nchi, sisi Wazanzibari,
“Zanzibar si Nchi”, ndio kilasiku tunazidi kuangamizwa, sisi na vizazi vyetu.
Njia pekee ya kuondoa maafa haya ni
“Zanzibar kurejea kuwa Nchi, Dola Huru
Kaamili; kama ilivyokuwa Zanzibar yetu siku ile ya Disemba kumi, 1963 ilipopata
uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa (UN), taarikh kumi na sita, Disemba
hiohio ya 1963”. Kila jambo la kheri
linahitajia Umoja, mashauriano na mashirikiano, lakini hili la ukombozi wa Nchi
yetu linahitaji zaidi Umoja, ushirikiano na mashauriano. Kwahivyobasi, ni wajibu
wetu sote kuwacha mfarakano na kujenga mshikamano, ili tukomboe Nchi yetu,
Zanzibar irejee katika kheri na neema zake na itokane na idhalaali,
Aamyn.
4.
Tumepata fursa ya kutumia Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada
zetu hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na inaweza
kutupa nafasi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA. Tunarejea tena qauli yetu ileile kama tulivyojaaliwa kueleza hapo
juu, yaani kwa sababu tumevamiwa na tukafanywa kuwa “Zanzibar si Nchi”, ndio ikawa tunafikishiwa yote haya ya idhlaali na mbinu za uangamizi,
wetu sisi na khasa vizazi vyetu.
5.
Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua
ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi
zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa mabayo hapo awali hayakuwepo.
Jee, tunasemaje sisi Wazanzibari, Waislamu; wenye kuuza ardhi zetu,
bali hata mava zetu kilasiku? Haya ndio makusudio yao mabwana kwa kuzivamia
ardhi zetu. Tusisahau kwamba kwa kuwauzia ardhi zetu, mbali ya khasara kubwa ya
kuuza ardhi, tuna adhabu ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala kwamba ardhi
zetu ndizo zinazojengwa makanisa ndani yake. Tunauza Akhera yetu kwa khasara ya
duniani, tunakhasirika duniani na Akhera.. Khasara ilioje hii! Yaa Rabbi
tunusuru waja wako!! Ya Rabbi tunusuru waja wako!! Mweyezi Mungu Mtukufu
amrehemu Dr. Omar Ali Juma; aliyaona haya mapema na akatahadharisha, lakini
hayakupata sikio la kheri. Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala amlipiea
kwa kila aliemdhulumu na iwe ni upungufu wa makosa yake, Aamyn.
6. Idadi ya skuli na vituo vyetu (ambavyo
licha ya picha ya juu kuwa haviendeshwi kwa misingi ya Kikristo lakini kiukweli
ni vituo vya kimisionari) vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli
hizi nikuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo Mji Mkongwe
(Stone Town Youth Centre) na zinafanya
kazi vizuri katika kupandikiza mila za Kikristo. Haya ndio maneno yao wenyewe, hivi vituo vyao japo hujaribu
kudanganya kuwa haviendeshwi kwa msingi wa Kikiristo, lakini kiukweli ni vituo
vya kimishinari. Vituo hivi ni kuanzia skuli za watoto wadogo mpaka hiki cha
“Stone Town Youth Centre”. Vyote hivi ni kwa makusudio ya kueneza ukiristo dhidi ya
Uislamu, Wazanzibari. Lakinibasi, kama tulivyo tangulia kusema, vitimbi vyao
hivi ni vya tangu kale na kale; wala havijaleta lolote kuongeza huo ukiristo
wanaodai kuuwania. Na vipi isiwe hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa
Taáala ametueleza hayo bayana kabisa. Wamokutoa mali yao tangu karne na karne,
na wataendelea kutoa, lakini hali itabakia ileile, khasara na majuto. Mwenyezi
Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala hawi pamoja na mwenye kufisidi, wala mwenye
kumsaidia mwenye kufisidi. Fisadi yeyote yule, daima hufisidi nafsi yake.
" إنّ
الّذين كفروا ينفقون أموالهم ليصدّوا عن سبيل الله ، فسينفقونها ثمّ تكون عليهم
حسرة ثمّ يغلبون ،
و
الّذين كفروا إلي جهنّم يحشرون" . (الأنفال : 36 ).
“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili
kuzuia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na
kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye
Jahannam
(Al Anfaal : 36).
Hii ni Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala, haiendi
pogo hata mara moja, ni iwe tu; kun-faya-kun, bila kizuizi. Lakinibasi, ni
wajibu wetu kujitahidi kutekeleza na kuhifadhi Dini yetu kwa ajili ya dunia
yetu na Akhera yetu.
7.
Sera ziliopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji
Zanzibar imetusaidia sana katika uingiaji wetu
(Wakristo) kutoka Bara na hivyo kusaidia kufuta ile imani ya kuwa
Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu na eti Wazanzibari kwa zaidi ya aslimia 99 ni
Waislamu. Hii sera ya uingiaji na utokaji Zanzibar,
yaani bila ya vitambulisho sio tu imesaidia kuendeleza hujma dhidi ya Uislamu,
Wazanzibari; kwa kupitia mishinari, bali zaidi imeleta wimbi kubwa la uharamia
na ujambazi nchini Zanzibar. Zanzibar imegeuzwa chaka la watoro, watu wanaingia
vile wanavyotaka, hufanya ujambazi wao, huuwa, huiba; kisha hupanda vyombo na
kutoweka. Inafaa tukumbushane kwamba kila aliesaidia kuleta hali hii, hali ya
uovu kabisa, basi anafungu lake la ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,
Subhaanahu wa Taáala:
“من يشفع شفاعة حسنة يكن لّه نصيب مّنها، ومن يشفع شفاعة سيّئة يكن لّه
كفل منها، وكان الله على كلّ شىء مّقيتا.” (النساء : 85).
“Atakayeombea maombezi mema (atakayesaidia
maombezi mema hata yakatokea) atapata sehemu katika hayo. Na atakayeombea
maombezi mabaya atakuwa na sehemu katika mabaya hayo, na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye ujuzi wa kila kitu”. (Annissai : 85).
Maafa ya kuachiliwa watu kuingia Zanzibar bila kitambulisho, kila
Mzanzibari anayafahamu na analipa thamani yake kwa kila njia na kila hali.
Kwahivyobasi, ni waajibu wa kila mmoja kufanya kila analoweza kuhakikisha kwamba
kuingia Zanzibar – sawa na nchi yoyote ile ulimwenguni - ni kwa kutumia
vitambulisho vyenye kukubalika kikanuni. Wajibu huu ni juu ya ndugu zetu
Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi, tunawaomba walitilie hima suala hili mpaka
litekelezwe.
8.
Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka bara umewezesha kuongezeka kwa
idadi ya mabaa na klabu za pombe. Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona magari ya aina mbalimbali
yanayomilikiwa na eti Waislamu yanabeba
kreti za pombe kali. Maneno yao yanathibitisha
maelezo yetu kwamba hawa si “Wakiristo wa kweli”, hawa ni wamishinari ambao
tangu karne na karne ni wenye kufanyakazi na wakoloni begakwabega katika kuupiga
vita Uislamu nyuma ya pazia la Ukiristo. Kama wanavyosema, ujaji wa Wakristo wa
namna hii umeongeza idadi ya mabaa na klabu za pombe, bali pia umeongeza idadi
ya nyumba za uchafu. Haya ndio makusudio yao khasa, ujaji wao kwa wingi
haujaongeza idadi ya waumini wao; makanisa yao bado ni matupu, na yataendelea
kuwa matupu. Kuupiga vita Uislamu,
Wazanzibari; kwao ni muhimu zaidi kuliko kuujenga Ukiristo. Inafaa wafahamu kwamba mbinu zao hizi ovu hazitaleta
matunda, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala ameahidi
kuihifadhi Dini yake:
“يريدون ليطفئوا نورالله بأفواههم والله متمّ نوره ولو كره
الكافرون.” )الصّف : 8).
“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi
Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri
watachukia”. (Ass’af : 8 ).
Juhudi zao za kuupiga vita Uislamu ni za tangu karne na karne, lakini
Alhamdulillah; kama alivyoahidi Subhaanahu wa Taáala haiwaongezei wenye kujaribu
kuupigavita Uislamu isipokuwa khasara na ghamu. Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,
Subhaanahu wa Taáala kilasiku inazidi kukua na kushamiri, na Inshaallah
itaendelea hivyo daima dawamu. Kwa kuvamiwa Nchi yetu na kumezwa chini ya huu
wenyekuitwa muungano, tukawekwa katika hali mbaya kabisa ya kiuchimi, ndio
tumefika baadhi yetu kuingia katika upungufu wa imani kufika kushiriki katika
maasi haya ya ulevi. Kwa kitendo chetu hiki ndio hawa mabwana wanafika kutuita,
“eti Waislamu”; yaani Uislamu wetu wanaubeza.
9.
Kujiingiza kwetu katika Taasisi za dola katika ngazi za mitaa
kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara. Hapana shaka
kujiingiza kwao huku kunapata kuungwamkono na kusaidiwa na baadhi yetu sisi
wenyekuitwa “eti
Waislamu”. Tafadhali naturejelee
hayo maneno ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taála hapo juu, kukhusu malipo ya
mwenye kusaidia katika kitendo, au hata maneno; ikiwa kwa wema au kwa uovu.
Malipo ni kulingana na kitendo au maneno. Yaa Rabbi tujaalie wenye kusaidia
katika kheri.
Wakati huo huo kudhibiti mihadhara ya wazi ya Waislamu kwa kutumia
madai ya kashafa na kutatanisha maelewano mazuri baina ya watu wa dini
tafauti. Hii ndio sera na mwendo wao, hawana ukweli, nifaaq ndio
mwendo wao. Mbinu zao ni kutumia uwongo katika kutaka kuwazuilia Waislamu,
Wazanzibari kuendeleza Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala kama
alivyoamrisha. Hivi ndivyo walivyo tangu karne na karne, tangu siku za Mitume
a.s.w., kwa hii inadi yao Mwenyezi Mungu Mtukufu akawapiga mihuri ya upotofu.
10. Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya Mjini ambayo
yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa, Mwanakwerekwe, n.k.
ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje
kwa sasa hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni
matupu. Vingi ya viwanja hivi
wamevipata kwa kuvinunua kutoka kwetu sisi Waislamu, Wazanzibari; miongoni mwa
viwanja hivi pia ni “eka”, mali yalionyangánywa na kugaiwa vipande vipande.
Haramu hii ya unyangányi ya mali ya watu imeongezeka haramu kwa hivi kutumiwa
ardhi hizi kujengwa makanisa, si kwa kuabudiwa; kwani hao wakuabudu hawapo, bali
kwa kuleta idhlaali kwa Waislamu, Wazanzibari na utekelezaji wa mbinu zao za
kujaribu kuupigavita Uislamu.
Ndugu wapendwa katika bwana,
Mafanikio hayo yasitufanye tuka lewa na kusahau jukumu la kanisa la
kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo. Kosa lolote
tutakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa na huenda nafasi hii
tulionayo hivi sasa tusiipate kwa karne mpya ijayo. Mambo ya kufanya
yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu na kuona yale tuliokwisha yapata
hayatutoki na kuyafanyia dira kwa karne ijayo ni haya yafuatayo:
Tusahau tafauti zetu dhidi ya adui
Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa
Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja
ambaye hatutofaulu kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar
ni dini iliofungamana na mila na utamaduni hivyo kila itakapowezekana tusahau
tafauti zetu ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vyenginevyo tutarudi
kama wakati wa Karume. Wanabainisha tena fahamu yao
potofu kwamba “Waislamu na Uislamu wao ni
adui yetu namba moja”. Kama tulivyotangulia
kuelezana, sisi Waislamu, Wazanzibari hatuna uadui na Wakiristo, tumeishi pamoja
kwa furaha, amani na mapenzi kwa miaka na miaka.
Tuhakikishe tunapata ardhi
Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika jitihada
waliyofanya ni kupata ardhi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu majengo ya
hospitali shule zahanati vituo vya chekechea makanisa n.k. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala
pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya bwana na Muokozi wetu. Wazanzibari, hii ndio mbinu yao; wazipate ardhi zetu kwa
kuenezea hizo mbinu zao potofu, mbinu za ufisadi dhidi ya ubinaadamu, mbinu
wenyekuziita ukiristo, na hakika sio Ukiristo wa kweli. Katika hali hii, inafaa tuchukue kila hadhari kuhakikisha
kuwa hatuuzi ardhi zetu, khasa kwa waliokuwa si katika sisi, yaani
Waislamu, Wazanzibari. Ugawaji wa eka
umesaidia pakubwa katika wao kuzipata ardhi zetu na kuendeleza ujenzi wa
makanisa nchini mwetu. Tena tunarejelea Qauli ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa
Taáala tulioitaja hapo juu kukhusu kusaidia katika wema na katika uovu; na wewe
utapata sehemu yako, ikiwa ni kheri au ni shari. Tutahadhari na kuuza ardhi zetu. Tuhakikishe hatuuzi ardhi
zetu kwa hali yoyote ile. Kuuza ardhi sio kuondoa umasikini, bali ni kuzidisha
umasikini na ufukara na ni kujenga idhlaali kwa nafsi zetu na kwa vizazi
vyetu.
Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa makanisa
Inaonesha Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji
kwenye sirikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa
cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata viwanja kwa
ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu ni kununuwa viwanja
vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa itayowashawishi kuviuza na baadae
tutaweza kuvijenga au kugeuza nyumba hizo kuwa makanisa. Tuone jinsi wanavyopanga kila njia ovu za kutufisidi na
kujaribu kuifisidi Dini yetu. Hivi wao kubainisha uovu na mbinu zao, ni fursa
kwetu sisi kuchukuwa kila hadhari kujikinga na uovu wao huu. Neno
“Waislamu wenye siasa kali” tushalizowea, kila Muislamu mwenye kutekeleza wajibu wa
Dini yake, ndio hupangwa kila jina la uovu. Kwao wao sote sisi tuwe
“Waislamu kanzu” hio ndio haja yao, hapo tena ndipo watupe jina walipendalo,
“eti waislamu”. Madhali hawawezi kutubatiza, na Inshaallah hawataweza,
laa sisi wala vizazi vyetu, basi tuwe “Waislamu kanzu” itatosha kwao; Inshaallah
hatutakuwa hivyo. Alhamdulillahi, hao wanaowaleta hapa Zanzibar kialsiku
wanazidi kurejea kwenye Dini yao, yaani Uislamu; yaani wanasilimu. Haqi lazima
idhihiri, haqi haikubali kukaliwa juu, lazima ikae juu.
Tujenga shule na hospitali kwa wingi
Hizi ni taasisi pekee ambazo tunaweza kuzitumia kueneza neno la Bwana
kwa Waislamu walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umasikini unaowakabili wengi
ya Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri,
tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei ndogo kuweka
upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali visiweze kuvikaribia
vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza
mafundisho yetu, zaidi kwa watoto wadogo (Nursery). Mbinu za kutumia huduma hizi kwa uenezaji wa wenyekuitwa
ukiristo ni za kale, na Inshaallah kama wanavyosema wao wenyewe, Waislamu
Alhamdulillahi ndio wengi hapa Zanzibar, itaendelea hivihivi na miongoni mwao
Inshaallah watazidi kupata uwongozi na warejee kwenye Dini yao ya asli -
Uislamu, wote wanazaliwa Waislamu, ni wao ndio huwabatiza na kuwatia kwenye
Ukiristo. Suala la wao kutumia “umasikini
unaowakabili wengi ya Wazanzibari na uchache wa huduma hizo”, kama tulivyotangulia kufahamishana, huu umasikini wametutia
wao watawala wetu, Dodoma; ili waweza kutuendesha wanavyotaka, tangu kisiasa,
kidini na katika nyanja nyenginezo. Umasikini huu umekuja kwa kuivamia Nchi yetu
na kuimeza kwa kisingizio cha huu wenyekuitwa muungano. Kutokana na hali hii ndio hii leo Wazanzibari wakawa kwa hali
yoyote ile wanawania kurejea Dola yao ya Zanzibar na itokane na huu ukoloni wa
Tanganyika, ukoloni wa Kanisa; leo kabla ya kesho. Suala la kuzitumia hizi skuli za chekechea kwa kupotosha
imani ya wenetu, hili ni jambo la khatari sana na ni wajibu wetu kuchukua kila
hadhari. Kubwa la kufanya sisi ni kutowapeleka wanetu kwenye hizi skuli zao za
chekechea, hizo ni vidonge vya sumu vilivyozongereshwa sukari. Tuviepuke kama
tunavyoweza, tuviepuke kwa kujenga skuli zetu za chekechea na kuwapeleka wenetu
humo.
Tunadai muda zaidi katika Vyombo vya habari (Tv na
Redio)
Kwa muda mrefu sasa uislamu na waislamu wamehodhi vombo hivi vya
habari mbali na kuwa siku ya ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi vya
kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyengine kadhaa kwa vipindi vya kiislamu
na hata
kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali
kupendelea uislam ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka
25 ya TVZ tulizungumzia suala hili lakini inaonekana halikupata mtu wa
kulifanyia kazi. Sasa tuhakikishe kuwa ukristo unapata muda zaidi katika vyombo
hivyo au uislam nao upunguziwe nafasi. Kuzidi chuki
zao, dharau na ihana; wanasahau kuwa Zanzibar ni nchi ya Waislamu, kwa hivyo
kutumia vyombo vyao, khasa idhaa kwa kutumikia Dini yao ni waajibu juu yao.
Kuudhika kwao kwa kutiwa adhana katika idhaa yetu, halina msingi; bali tu ni
dalili ya chuki zao juu ya Uislamu, khaasa na juu ya Wazanzibari kwa jumla.
Tizama jinsi ya chuki na uovu wao, “wao
wapate muda zaidi na Waislamu wapunguziwe”, hii ndio sera ya hasidi, weye ukose, yeye apate. Lakini kwa
mipango ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala, hasidi daima haendelei, hasidi
yake ni khasara na idhlaali.
Tuongeze mihadhara ya wazi
Wakati Waislam wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi
kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Kwa kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone wakristo
wa Mjini na Mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria. Vipaza
sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la bwana linafika kila pahala. Mihadhara
ifanyike karibu na nyumba, misikiti na kwenye viwanja vya wazi. Ndio hayo! Hii ndio sera yao, Waislamu wazuiliwe, wao wapewe
na waongezewe.
Tuendelee kutumia shule na sehemu za Umma
Ili kuwafanya waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni
lazima kuendelea kutumia mashule na sehemu za Umma zilizo wazi kwa mambo yetu ya
ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona tafauti kati
yetu na wao. Kila ukiusoma waraka wao huu ndivyo
unavyozidi kutambua kuwa hawa “wenyekujiita wakiristo”, sio Wakiristo wa kweli;
Ukiristo wa kweli haunadi uadui na Uislamu. Hii leo, Bwana Pope; mara nyingi
amesikika kusema juu ya kuondoa mvutano baina ya dini, bali baina ya mataifa.
Kama wao hawa ni waumini wa kweli wa Ukiristo wengelifuata mwenendo wa Bwana
Pope. Lakini kamaitavyokuwa, sisi ni waajibu wetu kuchukuwa kila hadhari
kujilinda na mbinu za mabwana hawa wenye fikra na mipango ya kujenga chuki na
khasama baina ya waumini wa dini tafauti. Hadhari ni waajibu, hivyo ndivyo
alivyotuamrisha Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala katika hii Aya
tuliotangulia kuitaja humu. Kwa hivi kuwa nia na dhamiri yao mabwana hawa si
njema juu ya Uislamu, Wazanzibari; ndio inatufanya na sisi kulazimika zaidi
kujihami dhidi ya mbinu zao ovu kwa uwezo wetu. Hivi kujihami kwetu dhidi ya
mbinu zao ovu ndiko wanakosingizia kuwa ni “chuki”. Tunawahakikishia kuwa sisi
Waislamu, Wazanzibari; hatuna chuki na Ukiristo hata kidogo, lakini tuna waajibu
wa kufuata maamrisho ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala na Sunna za Mtume
wetu Mpenzi s.a.w. Miongoni mwa maamrisho hayo ni kuihami na kuihifadhi Dini
yetu tukufu kwa kila hali. Hapa tena ni waajibu kuzinduana na ndugu zetu walioko
kwenye madaraka juu ya mbinu hizi na kuwaomba kuchukuwa hadhari katika utumizi
wa hizi sehemu walizozitaja hawa mabwana kupanga kuzitumia ili kuepusha athari
ya sisi kusaidia katika utekelezaji wa njama zao ovu dhidi ya Uislamu,
Wazanzibari. Tusisahau kuwa mwenye kusaidia katika la kheri, nae hupata sehemu
ya kheri hio; na mwenye kusaidia katika shari nae hupata sehemu ya shari hio.
Yote hayo tutayakuta kwenye vitabu vyetu hio Kesho, na hii leo, hapahapa
ulimwenguni tutapata malipo yetu, qabla ya hio Kesho..
Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi
Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari waislamu.
Hali hii inafanya ongezeko la wakristo kuwa dogo au
halipo kabisa ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za kikristo.
Alhamdulillahi, kweli wanaitambua; lakini wamo
wanagombana nayo. Inshaallah daima dawamu, Waislamu, Wazanzibari hawata
nasarishwa, daima wataendelea katika Dini yao tukufu. Inshaallah na uwongofu
utawafikia na wao warejee kwenye Dini yao ya kuzaliwa. Binaadamu huzaliwa ni
Muislamu, ni wazee wake ndio wenye kumtoa katika Uislamu na kumtia kwenye
upotoful.
Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na Taasisi zetu ni
kuongezeka kwa wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo wengi
kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa kutumia udugu
wetu wa kikabila au asili ya Bara. Tunaposoma
maelezo yao haya tunafahamu bila taabu kwamba haja yao ni kuongezeka makanisa na taasisi
zao. Kuongezeka Wakiristo sio haja yao
khasa, kuongezeka Wakiristo kwao wao ni ngazi tu ya kufikia haja yao khasa,
yaani kuongezeka makanisa na taasisi zao.
Hii hakika wanaoshindwa kuificha, vitendo na mwenendo wao pia unathibitisha
hakika hii. Huu ujenzi wa makanisa na taasisi nyengine ni mtaji wa kujipatia
chumo binafsi hao viongozi wa hizi harakati za hawa “wenyekujiita wakiristo”
kutoka wafadhili wao huko Ulaya na kwengineko. Na kwa kuwa makanisa haya lazima
waonekane wenye kuyatumia, ndivyo hivi kupanga hata kuleta na kuhamisha watu
kutoka huku na huku. Ni vyema wawalete,
Inshaallah itakuwa ndio njia ya wao kurejea kwenye Dini yao ya asili; Uislamu;
kheri hutoka kwenye tumbo la shari.
Kwa kuwatumia ndugu zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe
kuwa suala la uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali.
Lugaha nzuri na ndivyo khasa, yaani “kwa kuwatumia”. Hawa
mabwana “wenyekujiita wakiristo”, mipango yao ni mbinu za uovu, kwahivyobasi;
ili kutekeleza mbinu zao hizo, ndio wakawa wanapanga “kuwatumilia” hao
wanaowaita “ndugu zao” waliomo sirikalini dhidi ya Waislamu, Wazanzibari -
“adui zao namba moja”. Tena, tunawaomba ndugu zetu, Wazanzibari, khasa waliomo
kwenye madaraka, tuzidi kuchukuwa hadhari na kujikinga na mbinu zao hizi. Suala
la uhamiaji na uingiaji nchini bila ya vitambulisho, kilasiku tunaona maafa
yake, tangu ujambazi na mengi mengineo. Na zaidi ni hili la kuwa ni mbinu ya
kupangwa khasa kwa kuongezeka makanisa nchini mwetu.
Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au
vitambulisho
Wakristo tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua
kufanya cho chote ili kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa wazanzibari
pekee basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu kwa Zanzibar.
“Mipango yao ya muda mrefu
itaathirika”, hii ndio qauli yao.
Iwapo sirikali ya Zanzibar italeta vitambulisho vya Wazanzibari, basi mipango
yao ya muda mrefu hawa mabwana wenyekujiita wakiristo itaathirika. Hii ni ilani
ya wazi kabisa kwamba kuondolewa vitambulisho vya Wazanzibari na kuletwa vya
Watanzania, wenye kunufaika khasa ni hawa mabwana wenyekujiita wakiristo. Ikiwa
Wazanzibari fikra zetu ni kwamba hivi vitambulisho ni kwa maslaha ya chama cha
kisiasa dhidi ya chama cha kisiasa, basi ndivyo hivi tunavyoelezwa wazi kabisa
kwamba vitambulisho ni mpango wa Wakiristo dhidi ya Waislamu, Wazanzibari.
Kwahivyobasi, vitu viwili ni muhimu kwa
Kanisa, (1) Uhamiaji, (2) Vitambulisho. Vitu viwili hivi ni dharura vibakie katika maslaha yao wao
hawa wenyekujiita wakiristo, ili waendeleze vita vyao dhidi ya Waislamu,
Wazanzibari. Tena, tunawaomba ndugu zetu
waliomo kwenye madaraka wayazingatie haya kwa hikma na busara na kutambuwa
dhamana zao na kuhisabika kwao katika dhamana zao, mbele ya Mwenyezi Mungu
Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala na mbele ya Umma wa
Kizanzibari.
Jitihada zozote za kuiimarisha Zanzibar kama Zanzibar na nje ya Utanzania ni
lazima tuelewe kuwa Uislamu utapata nguvu na kuwa tishio kwa hapa Zanzibar na
hata Bara. Kutokana na imani na siasa
yao hii, ndipo pale Januari 11, 1964 makanisa wakimtumia Nyerere akaleta majeshi
yake na kuivamia Dola Huru ya Zanzibar. Dola ambayo ilipata uhuru wake taarikh
10 Disemba, 1963; na kujiunga na Umoja wa Mataifa taarikh 16 Disemba hiohio
1963. Baada ya siku thalathini na tatu tu, yaani hio Januari 11, 1964 ndipo
makanisa kwa kumtumia Nyerere wakaivamia Zanzibar. Mavamizi haya lengo lake kuu
ni kuimeza kikamilifu Dola Huru ya Zanzibar, ndipo hapo siku ile ya April 26,
1964 ilipomezwa Zanzibar kwa kisingizio cha huu wenyekuitwa muungano kwa
kubuniwa zile “Articles of Union,
1964” na hapo tena ndipo ilipofanywa
“Zanzibar si
Nchi”.
Iwapo tutawajibika kuunga mkono ni kadi za Uraia na vitambulisho vya
Watanzania kwa Ujumla na sio Zanzibar peke yake. “Zanzibar si Nchi”
ndivyo alivyotwambia Mhishimiwa Waziri Mkuu
wa Tanganyika, Bwana Pinda; kwahivyobasi, madhali hatuna nchi na bado Zanzibar
ni koloni la Tanganyika, vitambulisho, kadi ya uraia, na hio passpoti, vyote
hivi tutaazimwa na bwana mtawala Tanganyika. Kabla ya Zanzibar kupata uhuru wake
siku ile ya Diemba 10, 1963, Wazanzibari wakipewa passpoti za “Zanzibar
Protectorate” yaani “Himaya ya Zanzibar”. Wakati huo juu ya kutawaliwa na
Muingereza lakini tulibakia kuwa Dola, lakinibasi; bwana mkoloni Tanganyika yeye
ameimeza nchi yetu na kuitia chini ya ukoloni wake, kisha akatwambia
“Zanzibar si Nchi”; mkoloni Muingereza hakufika kuimeza nchi yetu na kufika
kutwambia kuwa “Zanzibar si
Nchi”. Hapa ndipo inaposemwa
“kheri ya ukoloni mweupe kuliko ukoloni
mweusi”. Naam! Halina shaka hili! Hivi ndivyo
walivyosema wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, mnamo miaka ya sitini;
mara tu baada ya Tanganyika kupata uhuru.
Qauli hii ilimchoma na kumuudhi sana
Mwalimu Nyerere, hivyo akaamrisha kufungwa Chuo hiki kwa muda. Kweli ni chungu!
Tujipenyeze Vyamani na kushika nafasi muhimu
Lazima tuelewe kuwa chama cho chote cha siasa kinalenga kukamata
serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa ni mazuri kwa chama
hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha zaidi kwenye
CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika chama tawala na katika
jumuia zake. Ikiwa inavyosemwa ni hakika, kwamba
“CCM”, maana yake khasa ni “Catholic Christian Movement” au “Chama Cha Msalaba”;
basi si ajabu hata kidogo kuwa “watu wetu
wamefaulu kuingia kwa wingi katika chama tawala (CCM) na katika jumuia
zake”. Hali kuwa hivyo si ajabu, ingalikuwa
ajabu lau kama hali haingalikuwa hivyo. Baada ya maneno yaliowazi kabisa kama
haya, sawa na pale tulipoambiwa kuwa “Zanzibar si Nchi”, ni
kweli sisi Wazanzibari tuendelee kudhania kwamba CCM ni chama cha Wazanzibari?
Ni kweli baada ya chama hikihiki CCM kutueleza dhaahiri shaahiri, kwamba
“Zanzibar si Nchi”, bado sisi tuendelee kudhania kwamba CCM ni chama cha
Wazanzibari? Tutakuwa tunajidhulumu nafsi zetu kwa
kuzidanganya.
Tupenyeze wenzetu serikalini
Sambamba na suala tulilolielekeza juu hatuna budi kusomesha vijana
wetu na kuhakikisha kuwa tunatumia kila njia na ushawishi ili kuwaingiza
serikalini na hasa katika sehemu muhimu. Hii itarahisisha kuungwa mkono mipango
yetu na kupunguzwa vikwazo kwa mikakati yetu. Hapana shaka hii ni mbinu yenye kutekeleza makusudio bila ya
wasiwasi. Hali hii ndivyo ilivyo hivi sasa hapa kwetu, nyingi ya nafasi muhimu
za juu zimo mikononi mwa mabwana watawala, Tanganyika, Kanisa. Waswahili wa Tanganyika na Waswahili wa Zanzibar, bali na
Waswahili wa Kenya na Waswahili wa Uganda sote tumetiwa kikaango kimoja
tunakaangwa kwa matufa yetu wenyewe. Kwa mabwana hawa
wenyekujiita wakiristo, kosa letu sisi Waswahili, Waislamu ni Uislamu wetu.
Hivyo ndivyo ikavamiwa Uganda kuwaondosha watawala wa jadi, kina Kabaka na
machifu wao, na kuvamiwa kuondoshwa Sirikali ya utawala wa kina Idi Amin; yote
hayo ni vita dhidi ya Uislamu, Waswahili.
Tuunge mkono sera za utalii
Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanzibar hutokea nchi za
Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata
za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo
waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake. Waingereza wanasema, “when the drink is in, the truth comes out”; maana ya maneno haya ni kama hivi, “ulevi ukijaa (kichwani), ukweli hutoka nje”. Ulevi wa hawa mabwana wenyekujiita wakiristo, si pombe,
bali ni haya wenyekuyaita “mafanikio yao”. Haya mafanikio yao yamewalevya na
kufika hadi hivi wao kubwabwaja vile wanavyopenda bila ya wasiwasi wowote ule.
Tena Waingereza wanasema, “power corrupts,
obsulute power corrupts obusulutely”, maana
ya maneno haya ni kama hivi, “nguvu za
madaraka zinafisidi, na nguvu za madaraka yasio na kizuizi, hufisidi bila ya
kizuizi”. Hawa mabwana wenyekujiita
wakiristo, baada ya kupewa madaraka, kuvamiwa nchi yetu na kutiwa chini ya
ukoloni wao; wamelewa kwa utamu wa madaraka, hivyo ndio hivi wao kuzama katika
kuleta kila upotofu na ufisadi; kinyume kabisa na “Ukiristo wa kweli”. Kwa
kitendo chao hiki, badala ya kuutendea vyema Ukiristo; wamekuwa wanautia aibu na
fedheha Ukiristo wa kweli, Ukiristo ambao unaamini juu ya kuishi kwa salama,
amani na mapenzi na waumini wote.
Tujenge mabaa na kuongeza pombe
Waislamu wengi huchukia pombe na huweza kuhama iwapo duka la pombe au
baa ipo karibu nao. Waislamu hatari ni wale wanaosoma na kupata muda wa
kujishughulisha na dini yao.
Pombe ni kitu ambacho humtoa Muislamu katika Uislamu wa vitendo na
kumkaribisha na Ukristo. Jee, haya ndio maamrisho
ya Ukiristo, yaani kupanga kufisidi waumini wengine? Mzee Pope haidhaniwi hata
kidogo kama atakubaliana na mbinu fisadi kama hizi? Ukiristo wa kweli ni ule
wenye kujenga mapenzi baina ya waumini. Pombe sio humtoa Muislamu katika Uislamu
wa vitendo, bali pia humtoa Mkiristo katika Ukiristo wa kweli, bali humtoa hata
mpagani katika utu wake. Kutokana na uovu huu ndivyo pale pombe kukatazwa na
kila imani. Jee, ni kweli kwamba pombe humkaribisha mtu na Ukiristo? Haya mapya
kabisa! Inavyojuulikana ni kwamba pombe, na kila ulevi, bali maasi humtoa mtu
katika ubinaadamu wake na kumtia katika siubinaadamu. Pombe haingaliitwa mama wa
maasi lau kama si yenye kupelekea kwenye kila maasi. Jee, Ukiristo wa kweli
ndivyo unavyoamrisha kwamba binaadamu ajitie katika kila aina ya maasi, au
katika maasi? Hatudhani kuwa ni hivyo.
Tuwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie
Ukristo
Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo
katika matatizo.. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha kabla
hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa kuanzia ili
Bwana awateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni kuwa na wafuasi wengi
kadiri iwezekanavyo. Jee, ndugu zetu, mnaamini
kwamba hawa si Wakiristo wa kweli? Hawa basi ni wenyekujiita wakiristo, sio
Wakiristo. Hivyo ni kweli kwamba Ukiristo wa kweli ni kumpangia binaadamu hilaki
na kufisidika tu? “Wawarudishe kabla
hawajatulia na kupata elimu nzuri”. Ikiwa
mbinu hizi si ufisadi tuziite nini? Ni ufisadi wa hali ya juu kabisa. “Uzima wa
Ukristo ni kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyoo”, “uzima wa jengo”
haupimwi kwa ukubwa wake, bali hujuulikana kwa misingi yake, nguzo zake,
matumizi yake na watumizi wake.
Tuwafuate wanawake kwa misaada
Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwamkono duniani kote na hasa zile
za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia wanawake kwa jina la
kuwasaidia. Enyi mabwana wenyekujiita wakiristo,
hivyo kweli hamna hata mara moja nia ya matengenezo kwa ajii ya Ukiristo, licha
ya ubinaadamu; bali basi kwa kufisidi na kujionesha? “….. kuwavutia wanawake kwa jina la kuwasaidia”.
" ....... و
ما يمكرون إلا بأنفسهم و ما يشعرون ". (اللأنعام :
123).
“….. Na wala hawafanyii vitimbi isipo kuwa nafsi zao, nao
hawatambui”.
(Al Anaám : 123).
Vitimbi vyenu viovu, haviwaleteeni lolote isipokuwa kufisidi nafsi
zenu. Waswahili wanasema, “mchimba kisima huingia mwenyewe”, na “muomba chumvi
huombea chunguche”; na, “upandacho ndicho uvunacho”. Ajabu ya mabwana hawa na
hao wakuu wao, karne na karne sasa wamo katika vitimbi vya ufisadi wao; karne
zote hizi hawana lolote walilolipata, lakini bado hawajatanabahi, bado wamo
kwenye upotofu wao. Lakini hayo si ajabu hata kidogo, hivyo ndivyo alivyoahidi
Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala kwamba madhaalimu hawatopata
uwongofu.
“..........
إن الله لا يهدى القوم الظالمين “. (القصص :
50).
“…….Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye
kudhulumu”.
(Al-Qas’as’ : 50).
Kwa vile hawa mabwana ni madhaalimu, basi kwanza dhulma yao huwafikia
nafsi zao, yaani wao ni wenye kudhulumu nafsi zao kabla ya zile wanazopanga
kudhulumu na kufisidi. Muhimu la sisi kutanabahi hapa ni kwamba ikiwa hawa
hawana uwongofu, vipi itakuwa watowe uwongofu. Ni kanuni yenye kutambulika na
kukubalika, hata kiakili tu, kwamba; “ asiekuwa na kitu hatoi kitu”. Hili liko dhaahiri kabisa, hao wenye kughurika na kuwafuata wao,
ukiwatazama utagunduwa kuwa hawana lolote la uongofu katika maisha yao ya hapa
duniani, licha ya kesho Akher, na hivyo ndio wengi wao hawakawii kutambua na
kurejea kwenye Uislamu – Alhamdulillahi.
Tuongeze vituo vya mafunzo ya kikristo
Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Centre) kimekuwa
kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali
(bado) halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbali
mbali, jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo
mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili za
kidini. Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala
anatupenda sana waja wake, mapenzi ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala ni
kuliko ya mama kwa mwanawe. Uovu ni wetu sisi jinsi tunavyokuwa hatuthamini hata
kidogo haya mapenzi ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala juu yetu. Miongoni
mwa mapenzi hayo, ni hivi daima kutubainishia na kutufichulia vitimbi viovu vya
hawa mabwana wenyekujiita wakiristo. Tunaona jinsi vinavyobainika vitimbi vyao
viovu. Kama tulivyotangulia kusema, sumu yao daima huizongeresha kwa vidonge vya
sukari. Ndugu zetu wenye kutumia vituo vyao hivi, khasa hicho cha
(Stone Town Youth Centre), hii ndio qauli yao. Tunaendelea kuwaomba ndugu zetu waliomo
kwenye madaraka watuvue na wavue nafsi zao na uovu huu, khasa kwa vile wao ndio
wenye uwezo huo kikanuni. Inshaallah wapate tawfiiq wafanye hivyo,
Aamyn.
Tuwaowe wanawake wao kwa kusilimu kimajina
Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa
wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo patakuwa na
ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake wao.
Wao hawa mabwana wanasema, ”watuowe ili watubatize”. Alhamdulillahi hivi kutambuwa na kubaini kwamba hawana la “nguvu za
hoja” kuwatia watu katika huu upotofu wao, hivyo ndio wanamalizikia kwa “hoja za
nguvu” na “hoja za udanganyifu”. Yote haya si mapya, tangu siku za Mitume
a.s.w. wao hushindwa na “nguvu za hoja”, na ndipo walipokuwa wakimalizikia kwa
kutumia “hoja za nguvu”. Kwa kutumia “hoja za nguvu”, ndipo wakawa katika mbinu
za kutaka kuwauwa Mitume a..s.w. waliopelekewa na kuwatesa Waislamu. Hali zao,
uovu wao, vitimbi vyao, tangu karne na karne ndio vilevile, hapana
kilichobadilika. Wanaendelea kuishi katika giza la upotofu kwa kuukataa mwangaza
wa uwongofu. Wataendelea hivihivi mpaka wataposema yaalaiti ningelikuwa udongo:
".......
ياليتنى كنت ترابا ". (
النّباْ (عمّ ) : 50 ) ..
“…… Laiti ningeli kuwa udongo”.
(Annbaaa : 50).
Tunamuomba Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala atunusuru kuwa
miongoni mwa qaumu hio, Aamyn.
Tuanzishe NGOS na sisi tuwe viongozi
Kwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia ngos moja
kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya zetu ambazo
zitawashirikisha waislam lakini uongozi wa juu ni
lazima uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na
malengo yetu yanatekelezwa kwa kivuli hicho. Vitimbi vyao Inshaallah vitawarejea wenyewe. Hapana shaka
hawa wenye kuleta hizi waziitazo “Non Governmental Organizations”(NGOs) ni
hawahawa mabwana wasiotutakia kheri Waislamu, Wazanzibari. Ni tangu karne na
karne, wakoloni washirika wake wakuu ni hao mishinari. Msiba mkubwa ni hivi sisi
kuwafanya mabwana hawa ndio wenzutu, kitendo ambacho Mola wetu Mlezi, Subhaanahu
wa Taáala ametukataza na kutuhadharisha uovu wa mabwana hawa, lakini wapi; sisi
ndio kilasiku tunazidi kuwakumbatia na kuwafanya ndio wenzetu, bali hata
kuwafanya ni wasiri wetu. Ole wetu!! Tumo
tunajitia katika hilaki kwa mikono yetu wenyewe, Ole wetu!! Yaa Rabbi
tunusuru.
Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti
waislam
Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbali mbali
baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha na matawi ya vyama na kamati za
maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima
iongezeke ili udhibiti wa shughuli za waislam uwe mzuri zaidi na
wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya vyombo vya
dola na vyama vya siasa. “Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti
waislam”. Daima dhamiri zao sio
njema, yote walioeleza humu katika hizo mbinu zao yamo katika njia za uvunjaji
na ufisadi, sio ujengaji na utengenezaji. Hawapangi lolote la maendeleo yao, na
wanapopanga, basi wanapanga kwa hisabu ya kufisidi binaadamu. Wanasema
“wajenge ukaribu na
viongozi”, viongozi wanaokusudia hapa ni
ndugu zetu, Waislamu, Wazanzibari waliomo kwenye madaraka. Wajenge ukaribu huo
kwa nia ya kuwafisidi Waislamu, Wazanzibari; sio kwa nia ya kuutengenezea
Ukiristo. Ndugu zetu mliomo kwenye madaraka, hivi ndivyo vitimbi vyao hao
mabwana wenyekujiita wakiristo, kilasiku uovu wao unazidi kudhihiri. Ni juu
yetu tuzidi hadhari na tuzidi kupanga ili tuweze kufanikiwa na kujihami dhidi ya
ufisadi wa kila fisadi.
Tuwachonganishe mashehe wenye msimamo mkali
Mashehe wenye msimamo mkali wamekuwa ni tatizo kwa ukristo kwani wana
wafuwasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali
ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo
hatuna budi kuwaunga mkono mashehe wote ambo wamekuwa wakitusaidia kwa njia
mbali mbali. Huu ndio mwenendo wao, si ajabu hata
kidogo. Fitna ndio mtaji na turufu yao, uwongo ndio nyenzo ya fitna zao. Kama
wanavyosema, wakati wakiwemo katika fitna zao; wakati huohuo wafanye waweze
kuwanunua wale wanaokuwa tayari “kuuza Akhera
yao kwa dunia yao”, Akhera ya daima kwa
dunia yenye kupita. Muhimu tuwakumbushe hawa mabwana wenyekujiita “wakiristo”,
kwamba fitna ni mbaya kuliko kuuwa:
“........ و
الفتنة أكبر من القتل .......”. ( البقرة :
217).
“………… Na fitina ni mbaya zaidi kuliko
kuuwa………..”.
(Al Baqra : 217).
Na Mola wetu Mlezi Subhaanahu wa Taáala, ametwambia kwamba mwenye
kuwafitinisha Waumini kisha asitubie, basi malipo yake ni kudumu maisha milele
katika moto ya Wahannamu.
“إنّا الّذين فتنوا المؤمنين و المؤمنات ثمّ لم يتوبوا فلهم
عذاب جهنّم و لهم عذاب الحريق.”
(البروج : 10).
“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na
Waumini wanawake, kisha hawakutubia, basi watapata adhabu ya Jahannamu na
watapata adhabu ya kuungua”. (Al Buruuj :10).
Basi hawa mabwana wenyekujiita wakiristo, wajuwe na watambuwe kwamba
hayo ndio malipo ya wenye kutia fitna baina ya viumbe; makaazi yao ya milele ni
katika Jahannamu. Adhabu hii itawakuta vilevile wale wenye kushirikiana na
kusaidiana nao katika kuwafitini viumbe. Ajabu yao hawa mabwana wenyekujiita
wakristo, kwani ni dhana yao kwamba watawapata binaadamu wawafuate hali ya kuwa
wamo katika upotofu kiwango hiki? Ametwambia Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa
Taáala:
“من يشفع شفاعة حسنة يكن لّه نصيب مّنها، ومن يشفع شفاعة سيّئة يكن لّه
كفل منها، وكان الله على كلّ شىء مّقيتا.” (النساء:85).
“Atakayeombea maombezi mema (atakayesaidia
maombezi mema hata yakatokea) atapata sehemu katika hayo. Na atakayeombea
maombezi mabaya atakuwa na sehemu katika mabaya hayo, na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye ujuzi wa kila kitu”. (Annissai : 85).
Ikiwa Ukiristo ni dini ya mapenzi na maendeleo, tunawaasa watende
mema kwa ajili ya dini na waache njama na vitimbi dhidi ya binaadamu.
Tulenge kuifuta tabligh
Pamoja na kuwa tabligh sio hatari moja kwa moja kwa ukristo lakini
bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ni aina pekee ya mihadhara ya waislamu
inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua baadhi ya waislam ambao
ni vyema kubaki bila ya kuzinduliwa. Haya ndio
maneno yao, “tabligh haina khatari na ukiristo, lakini juu ya hivyo inastahili
kupigwa vita”. Kwa nini? Kwa sababu inaweza kuwazindua Waislamu, na ni vyema
kubaki bila ya kuzinduliwa. Ajabu ya mabwana hawa, sifahamu ni maadili yepi
wanayoyafuata; Uislamu unabainisha kwamba, “Hawi muumini wa kweli mmoja wenu mpaka ampendelee nduguye
lile analojipendelea nafsi yake”. Sasa hawa
mabwana wenyekujiita wakiristo, ikiwa wao hawawapendelei kheri binaadamu
wenziwao, vipi wanatarajia kupata mapenzi ya binaadamu wenziwao? Vipi
wanatarajia wapate mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala?
Hivyo ni kweli haya ndio mafunzo ya Ukiristo? Hapana shaka haya sio. La hakika
zaidi ni kwamba hawa sio Wakiristo wa kweli. Waswahili wanasema, “Chema chajiuza, kibaya chajitembeza”.
Tudai turudishiwe taasisi zetu
Serikali ya Zanzibar bado inaonekana kuwa ngumu kurudisha katika
milki ya makanisa ardhi na taasisi zetu. Dalili za huko nyuma zilionekana nzuri
kwani tulifanikiwa kupata hospitali yetu ya Welezo na eneo la kiungani hata
hivyo panakuwepo ugumu wa kurudishiwa shule zetu. Kwa kuwatumia wenzetu
waliomo serikalini na baraza la wawakilishi lazima tuzidishe harakati
na madai ya taasisi zote zilizobaki. Wao wanadai
kurejeshewa taasisi zao, tunawakumbusha kwamba Waislamu wameporwa Chuo chao
Kikuu Cha Ufundi, (MIOME), wamenyangánywa jumuia yao iliokuwa na manufaa
makubwa, “East African Muslim Welfare Society” (EAMWS), si kwa Waislamu tu; bali
kwa Afrika Mashariki, bali kwa Afrika nzima. Isitoshe, Waislamu daima dawamu
wananyimwa fursa za masomo ya juu, wananyimwa fursa ya kazi za dhamana, Jeshini,
Polisi, Vikosi vya Usalama, Magereza, Ubalozini na mwingi mwenginemo. Wananchi
katika nchi yao ambao kwa hio hisabu yao wao mabwana wenye khatamu za nchi, basi
Waislamu Tanganyika hawapungui 65% na Zanzibar hawapungui 98%, hii leo baada ya
mavamizi ya 1964 na kumezwa Dola Huru ya Zanzibar. Mzee Kambona baada ya kuona
maji yanazidi unga, yaani dhulma ya Nyerere juu ya Waislamu, alimnasihi
asiwabane sana Waislamu. Kambona haiwi kafanya hivyo isipokuwa zaidi ni kwa
manufaa ya hao wakiristo. Lakini wapi, Mwalimu hakuacha mbinyo wake juu ya
Waumini mpaka akafika mbele ya haqi.
Tulete waumini kutoka mashamba kuanza makanisa
Hivi sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo
hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa utaratibu uliopo hivi sasa
chini ya baadhi ya makanisa ni lazima uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi
hufikia mashamba hivyo pawekwe na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza
makanisa. Almuradi mumo mbioni tu, leo wa shamba
wapelekwe mjini, kesho wa mjini wapelekwe shamba, leo wa bara wapelekwe
visiwani, kesho wa visiwani wapelekwe bara. Leo wa Machui wapelekeni Mahonda,
kesho wa Mahonda wapelekeni Kama. Mabwana wakubwa! Wengi wa hawa munaowasema
“wakiristo”, ni wenye kutafuta riziki, dini kwao ni hadithi tu, huko mashamba
ndiko kwenye mbio zao za kujipatia riziki, riziki wajisaidie nafsi zao na watu
wao waioko huko mabara. Zanzibar wamekuja kutafuta riziki, kama walivyokuwa
wakifanya miaka na miaka, tafadhalini waacheni waishi kwa amani na mafahamiano
na wenyeji wao, wacheni kuwajengea fitna na bughdha na wanyeji wao kwa maslaha
yenu binafsi, wala si kwa huo ukiristo mnaojinasibu nao.
NENO LA MWISHO
Wapendwa katika Bwana.
Miongozo hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa
kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata hivyo kwa
uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu ni haya kufahamika
na kila mkiristo apendae kumtumikia Bwana. Pia
hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya mapinduzi ambao imefungua
milango kwa ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa.
Bwana awe nasi!
Nasi tunasema, “Enyi Wapendwa katika Bwana”, Enyi Wakiristo wa kweli,
tafadhalini inukeni muutakase Ukiristo na aibu kama hii unaopakwa. Aibu ya
kunasibishwa na kila uovu na njama dhidi ya binaadamu. Aibu ya kuitia Sirikali
ya Zanzibar katika ushirika wa njama hizi za uovu dhidi ya Waislamu,
Wazanzibari.
Kukumbushana ni Waajibu kwa Waumini
Ametutaka Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala tukumbushane; kwani
kukumbushana kunawafaa Waumini, Inshaallah tuwe wenye kunufaika.
وذكر فان الذكرى تنفع المؤمنين.” (الذاريات : 55).
“Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini”.
(Adhaariyaat : 55).
Kwa vile sisi ni Waumini ni wajibu wetu kukumbushana. Kwanza
tunawaomba ndugu zetu waliomo kwenye madarka na uongozi watumie wakati wao
thamini wausome huu waraka wa hawa jamaa wenyekujiita wakiristo. Wakishausoma,
kwa kituo; tunawaomba wazingatie vyema yaliomo kwenye waraka huu na wazingatie
wajibu wa dhamana yao, kuwa vile wao ndio viongozi wa huu Umma wa Waislamu,
Wazanzibari. Katika huko kuzingatia tunawaomba wazingatie yaliomo kwenye Quráni
Tukufu, khasa Aya tatu hizi. Tunawaombea viongozi wetu na Sirikali yetu ya
Zanzibar kwa jumla kila kheri na baraka na mafanikio katika utumishi
waliochukuwa dhamana ya kuutekeleza. Tunapenda kuzidi kuwahakikishia kwamba Umma
wa Zanzibar chini ya umoja wao, Umoja wa
Wazalendo, daima uko pamoja nao kwa kila hali kwa maslaha Nchi yetu
na vizazi vyetu.
" يآأيّها اّلذين آمنوا لا تتخذوا
بطانة من دونكم لايألونكم خبالا، ودوا ماعنتم، قد بدت البغضآء من أفواههم، وماتخفى
صدورهم أكبر، قد بينا
لكم اللآيات
ان كنتم تعقلون”. (آل عمران : 118).
Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi.
Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha
fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo fichwa na vifua vyao ni makubwa
zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini”.
(Al-‘Imraan : 118).
“يآأيّها الّذين آمنوا قوا أنفسكم وأهليكم نارا وقودها الناس والحجارة
عليها ملائكة غلاظ شداد لا يعصون الله مآأمرهم ويفعلون مايؤمرون.” (التحريم :
6).
" Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu
wenu, na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali,
wenye nguvu hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri zake; na wanatenda wanayo amrishwa
(yote)”. (At-tahriim : 6)..
“من يشفع شفاعة حسنة يكن لّه نصيب مّنها، ومن يشفع شفاعة سيّئة يكن لّه
كفل منها، وكان الله على كلّ شىء مّقيتا.” (النساء:85).
“Atakayeombea maombezi mema (atakayesaidia
maombezi mema hata yakatokea) atapata sehemu katika hayo. Na atakayeombea
maombezi mabaya atakuwa na sehemu katika mabaya hayo, na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye ujuzi wa kila kitu”. (Annissai : 85).
Tunamuomba Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala atujaalie kila kheri
na baraka na atuepushe na kila shari, na atuzidishie tawfiiq, uwezo na uwongozo
katika huu utumishi wa Dini yetu tukufu na wa’tani wetu ghali, Lillahi Taáala,
atuepushe na ria, atuepusehe na taájub, na atuepushe na kibri; Aamyn, Yaa Rabbi,
Aamyn.
Wa Billahi Tawfiiq
Umoja wa Wazalendo
Zanzibar
July 10, 2009
|
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !