Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Afisa Elimu akiri kutaka
orodha ya wanafunzi
Adai amejieleza Wizarani
Atekeleza ombi la Katekesi
Na Mwandishi Wetu,
Morogoro
AFISA Elimu wa Manispaa ya Morogoro Bibi E. Mwangamila amekiri kwamba ofisi
yake ilitoa agizo kwa wakuu wa shule za msingi kumpa orodha ya wanafunzi
Wakatoliki.
Afisa Elimu huyo amedai kwamba amefanya hivyo kutekeleza ombi la
Mkurugenzi wa katekesi Jimbo la Morogoro Sr. M. Bonifacia C.P.S.
Bibi Mwangamila amesema alipokea ombi hilo alishindwa la kufanya kwani
alikuwa mgeni ofisini hapo, hata hivyo alipotaka ushauri kwa wale aliowakuta
ofisini, walimhakikishia kwamba halina tatizo na hufanyika kila mwaka.
Baada ya kupewa maelezo hayo alisema ndipo alitoa maelekezo kwa Bw. E.P.
Mpessa kutoa agizo kwa waalimu wakuu kutuma ofisini kwake majina ya wanafunzi wa
Kikristo.
Bibi E. Mwangamila amesema kwamba baada ya wananchi kuonyesha wasiwasi
kufuatia zoezi hilo, ameandika barua Wizara ya Elimu kutoa ufafanuzi ambapo
amedai kwamba nakala ya barua hiyo ameipeleka kwa Mheshimiwa Rais Benjamin
William Mkapa.
AN-NUUR imebahatika kupata nakala ya barua Na. DM/CAT/MTI-S/M/03/98
inayodaiwa kutoka idara ya Katekesi inayoomba majina ya wanafunzi Wakatoliki.
Hata hivyo, barua hiyo ikilinganishwa na ile ya Afisa Elimu wa Manispaa
inazua maswali mengi kuliko majibu.
Kwanza barua hiyo ya Sr. M. Bonifacia inaonyesha iliandikwa Machi 2, 1998 na
kuomba majina ya wanafunzi Wakatoliki yafike Idara ya Katekesi jimboni Morogoro
kabla ya Aprili 30, 1998. Hata hivyo barua hiyo inaonyesha ilipokelewa ofisini
kwa Afisa Elimu Manispaa Juni 1, 1998, miezi mitatu baadae, wakati ofisi hizo
mbili zinatenganishwa na umbali usiotimia hata robo kilo meta.
Lakini jingine ni kwamba wakati barua toka Afisa Elimu Manispaa kwenda kwa
wakuu wa shule inaonyesha kuandikwa Juni 9, vidokezo juu ya barua toka Idara ya
Katekesi inaonyesha kwamba waalimu walipewa maelekezo na kuandikiwa barua Juni
8, 1998.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !