WARAKA KWA MWANASHERIA MKUU WA TANZANIA JUU YA
JINSI SERIKALI YA CCM ILIVYOLISHGHULIKIA VIBAYA SUALA LA MIHADHARA YA
WAISILAMU
Bismillahir Rahmanir Rahiim
A. Aziz
S.L.P. 2847 Dar es Salaam
Mwanasheria Mkuu,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, S.L.P. 9050, DAR ES SALAAM
Kwa Ridhaa yako Mh. Mwanasheria Mkuu,
YAH: MAKASISI WAKATOLIKI, SERIKALI YA CCM NA HAKI YA WAISILAMU
YA KULINGANIA NA KUTANGAZA DINI
"....(Watu) hawa ni wa kupingwa kwa njia zote na kwa kila
hali. Maana, hata kama wanasema lililo kweli, hata hivyo, yule aipendae kweli
asikubaliane nao. kwani si (vitu) vyote vilivyo kweli ndiyo kweli. Wala ile
kweli inapoonekana (tu) kuwa ni kweli kwa mujibu wa maoni ya wanaadamu
isichukuliwe badala ya kweli iliyo kweli, ambayo ndiyo ile iliyo kwa mujibu wa
imani."
Askofu Clement wa Alexandria (c.AD 150-215) alisema katika barua
aliyomuandikia mwanafunzi wake (aliyeitwa The Odore) katika kuikanusah Injili
ya siri ya Marko ("Secret Gospel" kilichoandikwa na Profesa Morton
Smith wa Chuo Kikuu cha Columbia).
"Ili tuweze kuifikia kweli katika vitu vyote, lazima siku
zote tuwe tayari kuamini kuwa kile kinachoonekana kwetu kuwa ni cheupe, ni
cheusi, kama uongozi wa kanisa unaelekeza hivyo." St. Ignatius Loyola,
muasisi wa Taasisi ya Kijesuit ya Kanisa Katoliki, ameagiza katika kitabu
chake "Spiritual Exercises."
Siku za Alkhamisi, tarehe 12 ya Februari 1998 na Ijumaa, tarehe
13 ya Februari 1998, bila ya shaka zitakumbukwa katika historia ya Tanzania
kama mojawapo ya madhihirisho ya matukio ya kuchukiza yaliyoonyesha jinsi
nguvu za dola zilivyotumiwa kuwatisha na kuwanyamazisha Waisilamu katika
kueneza dini yao kwa uhuru, wakiingiliwa na kupondewa haki zao walizopewa na
Mungu na za kikatiba.
Waisilamu waliuliwa, walifanywa vilema, walikamatwa na walipigwa
kinyama na polisi wa vikosi vya kuzuia fujo (FFU) kwa hakika, hatua
zilizochukuliwa na serikali ya CCM, pamoja na matamshi ya viongozi wake
yaliyofuatia, zimeiharibia sana hadhi yake mbele ya macho ya Waislamu na
Watanzania wote wapenda uhuru; na itachukua muda mrefu kuirejesha tena hadhi
hiyo.
Hakuna anayehoji haki ya serikali ya kuwapeleka askari wa kikosi
cha kuzuia fujo siku ile ya tarehe 13, pale mambo yalipokwisha kuharibika na
Watanzania wa imani na itikadi zote kujiingiza kwenye mlipuko uliokuja geuka
na kuwa mapambano na fujo dhidi ya serikali ya CCM: tazama jinsi yalivyokuwa
yameshambuliwa magari ya serikali na ya mashirika ya Umma tu, na idadi ya
Wakristo pia waliokamatwa katika kamata-kamata ya polisi.
Lakini ingawa ni kweli kuwa serikali ilikuwa na haki ya kikatiba
na kisheria kupeleka askari wa kuzuia fujo kwa ajili ya kuhifadhi amani na
usalama, mtu lazima ahoji hatua ya kibabe babe tu, isiyo na haki ya kisheria,
iliyochukuliwa na serikali ya CCM siku ya Alhamisi tarehe 12 Februari, ya
kuvunja milango na kuingia kwenye msikiti wa Mwembechai.
Lilikuwa tendo hili, ambalo halikuwa chochote bali uamuzi wa
kibababe tu wa kuingilia uhuru wa watu katika dini, ambalo ndilo hasa
lilikuwa cheche iliyoanzisha msululu wote wa matukio yaliyofikia kwenye
mlipuko wa siku ya Ijumaa ya tarehe 13.
Matokeo ya tendo lile, pamoja na hatua ya askari polisi kuingia
msikitini kwa vitisho huku wamevaa viatu, wakikamata na kuwashambulia watu
waliokuwa wanaswali humo, bila ya kuthamini kabisa na kuheshimu utakatifu wa
jengo lile na hisia za Waisilamu, yasipuuzwe.
Ikumbukwe kuwa kwa uchache kabisa kuwa tendo la polisi la
kuingilia utakatifu wa msikiti linaingilia nafasi na thamani tunayowekea
utakatifu huu katika jamii yetu kisheria na kisiasa. Hakuna jambo litalo
chafua na kulipua hisia za waumini, kama kuingia kwa kukufuru na najisi
majumba ya ibada.
Ni wazi serikali ya CCM inawataka Watanzania na watu wengine
duniani kuamini kuwa matendo yake yalikuwa halali kwa sababu Waisilamu
walivunja sheria kwa kuendesha mihadhara ya kashfa dhidi ya Ukristo na kwa
namna hiyo kuhatarisha amani na utulivu nchini Tanzania.
Kutokana na matamshi ya viongozi mbali mbali wa CCM na serikali
ni dhahiri kuwa serikali ya CCM inajaribu kutuuzia bango la bandia la
"Uisilamu wa Siasa kali." Serikali ya CCM inadai kuwa "Siasa
kali" hii, ikiachiwa ienee, itaizamisha nchi katika fujo na kutokuwapo
amani kama inavyotokea kwenye nchi kama Algeria, Somalia, Burundi na Lebanon.
Ni jambo la kuzingatiwa kuwa serikali ya CCM haiko peke yake
katika mashambulizi haya ya kisasa dhidi ya Waisilamu wa Tanzania. Vyombo vya
habari vya nchini navyo vimeyapokea mashambulizi haya kwa kutumia uandishi wa
habari kwa kutoa taarifa zinazochanganywa na mawazo binafsi ya kijuujuu
yaliyo na hisia za mashambulizi dhidi ya Uisilamu, na kuingiza majina na
maneno yale yale yaliyosukwa na kutayarishwa nchi za Magharibi, kama vile
"fanaticism" (uhemkwaji), "fundamentalism" (siasa kali)
"extremism" na "radicalism," yote yakiwa yamedhamiriwa
kuupotosha Uisilamu na kuuonyesha kuwa ni tishio kwa amani ya Tanzania.
Vyombo vya habari vya nchini kwa kujiingiza katika mtego wa
kutumia maneno yaliyojengewa maana mbaya kwa makusudi kama "siasa
kali," vilijifunga na kujilazimisha kusimama katika maamuzi ya upande
mmoja, na kwa hiyo hawakuweza kupata mizani sahihi na kuelewa hali kama
ilivyokuwa kuhusu sababu halisi zilizopelekea kwenye mlipuko wa Mwembechai.
Kwa sababu ya mawazo waliyokuwa nayo tayari kutoka kwa
"Orientalists" na mitazamo ya kiadui dhidi ya Uisilamu kutoka
vyombo vya habari vya nchi za Magharibi, na upotoshaji dhidi ya Uisilamu
pamoja na upungufu wao wenyewe juu ya dini ya Uisilamu, vyombo vya habari vya
nchini vimekuwa vinaelekea upande mmoja na vyenye msimamo wa uadui katika
kuripoti mambo ya Mwembechai.
Kwa hiyo picha waliyoitoa ya Uisilamu na Mwembechai, licha ya
kuwa ni ya kupendelea upande mmoja, ni ya kutiwa chumvi na upondaji. Tangu
hapo upondaji ndio unaoleta biashara ya kuliuza gazeti.
Si magazeti yote yalichukua mwenendo huu. Kulikuwa na mengine
ambayo hayakujiingiza kwenye mtego huu. Mhariri wa "The
African", Asha Mzava kwenye gazeti la "The Guardian"
na Makwaia wa Kuhenga kwenye "The Guardian" na "Majira",
ingawa hawakuzitambua sababu za msingi na kwa hiyo wakawa na upungufu katika
uchambuzi wao, walinasihi na kuwaidhi serikali iwe na uangalifu, kujizuia na
kuwa makini.
Mbali na magazeti yote, na lililojitokeza wazi wazi, lilikuwa
gazeti la Kiisilamu la kila wiki "AN-NUUR" ambalo kwa makala
na maandishi mengine mbali mbali kutoka kwa wasomi wa Kiisilamu na Waisilamu
wengine wa kawaida kila wiki mfululizo limekuwa likisisitiza kuwa kilichokuwa
kiini cha yote, na kinachopuuzwa si chochote bali uhuru wa Waisilamu
kuitangaza Dini yao.
Kwa hakika kama watendaji wa CCM wangekuwa waadilifu na watu
wapendao kusoma na wangelisoma gazeti la "AN-NUUR" bila
upendeleo na kuathiriwa na mawazo finyu, pengine wangelishughulikia suala la
Mwembechai kwa njia ya udilifu na fikra sahihi.
Lakini kwa maoni yangu, labda mshiriki mwenza na muhimu sana wa
serikali ya CCM katika kampeni hii dhidi ya Waisilamu umekuwa uongozi wa
Kanisa Katoliki. Haiwezi kukatalika
kuwa ni uongozi wa kanisa Katoliki ambao ndio uliochochea serikali ya CCM
kuwachukulia hatua wahubiri wa Kiisilamu.
Tangu mwaka 1993 uongozi wa kanisa Katoliki umekuwa
ukiyashambulia kwa nguvu kweli kweli mahubiri ya Waisilamu wakidai kuwa
wahubiri wa Kiisilamu na Waisilamu "wenye siasa kali" mamekuwa
tishio la amani nchini Tanznaia. Tangu mwaka 1984 Waisilamu walipoanza
kuwalingania watu kwenye Dini ya Uisilamu kwa kutumia taaluma linganifu
katika Dini, na kutokana na Wakristo wengi kusilimu na kurudi kwenye
Uisilamu, uongozi wa kanisa Katoliki umekuwa ukiishinikiza serikali kupiga
marufuku mihadhara ya Waisilamu, wakidai kuwa ilikuwa inakashifu na kutukana
Ukristo.
Ni muhimu kuzingatia kuwa ingawa uongozi wa Kanisa Katoliki
umekuwa ukiisukuma serikali kuifungia mihadhara ya Waisilamu tangu mwaka
1993, serikali ya CCM imeongeza kasi yake ya kukamata wahubiri wa Kiisilamu
tangu Januari 1998.
Hatua hii ya serikali inaonyesha kuwa hii ilikuwa kampeni iliyopangwa
na kutekelezwa kwa uangalifu. Sidhani kuwa kampeni hii inayopendelea hadi hii
leo ilitokea na kuanza kwa bahati tu pale padri wa Parokia ya Mburahati
alipoitupia serikali changamoto kwenye tangazo la radio lililotolewa kwenye
Radio Tumaini, inayoendeshwa na Kanisa Katoliki, siku ya tarehe 8 Februari
1998. Padri Camillus Lwambano aliitupia changamoto serikali iache kutoa ahadi
tupu tu, ipige marufuku mahubiri ya kashfa na kuwachukulia hatua kali
wahubiri wa Kiisilamu. Padri Lwambano aliitaka serikali itamke wazi wazi kuwa
imeshindwa kuzuia mahubiri ya kashfa. Lilikuwa tangazo la uchokozi. Bali pia
lilikuwa tangazo lililo ashiria hatari.
Hapana shaka kuwa Padri Lwambano alipata matumaini na nguvu
kutokana na kauli za hadhara za kuwaunga mkono zilizotolewa na viongozi wa
serikali ambazo uongozi wa kanisa Katoliki walizipata kuhusiana na malalamiko
yao dhidi ya mahubiri ya Waislamu.
Tarehe 4 Januari, 1998 mjini Tabora kwenye sherehe za Jimbo la
Magharibi la Kanisa la Moravian, Rais Mkapa alitangaza vita dhidi ya
"watu wanaopita pita wakigawa kaseti, vijitabu na kuendesha mikutano
ambamo wanatukana na kukejeli dini nyingine" (Daily News la tarehe 5
Januari 1998). Ni wahubiri wa Kiisilamu tu ndio wanaotumia kaseti na
vijitabu, pamoja na mihadhara, kwenye shughuli zao za kueneza Dini.
Ni maoni yangu kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya CCM
zina udini na za kuegemea upande mmoja. Tukichukua ukweli kwamba uongozi wa
Kanisa Katoliki ulishindwa kuthibitisha madai yao ya kashfa katika mkutano wa
Maaskofu na Masheikh ulioitishwa na Rais Mstaafu Mwinyi mwaka 1993.
Iwe iwavyo, kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba serikali ya CCM
inaonyesha kutokujali kabisa wajibu wake wa kuheshimu katiba na sheria za
nchi. Serikali ya CCM inaweza ikaelezea haja yake ya kutaka kuona kuwa haki
na uhuru wa kuabudu wa Watanzania wote vinalindwa, na kwamba sheria za nchi
zitaheshimiwa na kufuatwa kuwawezesha watu kuabudu, kuhubiri na kuendesha
shughuli zao za dini kwa uhuru. Ukweli wa mambo ni kwamba serikali ya CCM
imechukua hatua kiubabe-ubabe na wala haionyeshi kuelewa kiwango cha uzito na
hatari ilichokikaribishia nchi yetu. Kwa kuonyesha upendeleo, na kukubali
kuhadaiwa na uongozi wa kanisa Katoliki kuwa maombi ya Waisilamu yanautukana
Ukristo, serikali ya CCM imejiingiza katika mstari wa utendaji nchini ambao
unaingilia haki za Waisilamu kutangaza Dini yao, imekuwa ya utendaji wa
kiubabe-ubabe na wala haijali kufuata utaratibu wa kwenda kwa sheria.
Mahubiri ya Waisilamu yamepigwa marufuku. Waisilamu
wanasumbuliwa na wanakamatwa kinyume na sheria. Waisilamu wanauawa na kutiwa
vilema. Misikiti ya Waisilamu inaamrishwa kufungwa. Kwa kosa gani? Kwa sababu
tu Waisilamu wanasema kwamba Mungu ni mmoja, na hana mwana, mshirika au aliye
sawa naye!
Mh.Rais Mkapa alianza kazi yake na madai kuwa utawala wake
ungekuwa unafuata utawala wa sheria, kwa uchache hii maana yake ni kuwa, kila
kitu kingekuwa kitendeke kwa mujibu wa sheria. Badala yake tulicho nacho ni
serikali ya CCM kuvunja ahadi zake na kuingia kwenye utawala wa kutumia nguvu
za dola kiubabe-ubabe. Hivi ndio tuelewe kuwa kwa kila kinachowahusu
Waisilamu na Uisilamu, masuala ya utawala wa sheria na haki hayamo? Wasilamu
si raia wa Tanzania wanaostahili kupata haki na nafasi zote zilizomo kwenye
katiba na sheria nyingine za Tanzania.
Nimesema kuwa hatua za mabavu zilizochukuliwa na serikali ya CCM
dhidi ya Waislamu na mahubiri ya kiisilamu ni kinyume na katiba za udini, na
kwamba zilichochewa kwa makusudi na uongozi wa kanisa Katoliki katika kampeni
ya udanganyifu kwamba mahubiri ya Waisilamu ni ya kashfa. Ni vizuri, kwamba
itasaidia, kuingia tutazame kwenye dhati ya mahubiri ya Waisilamu tuone kama
kulikuwa na uvunjwaji wa sheria kutokana na mahubiri hayo, tuingie pia kwenye
jinsi uongozi wa kanisa katoliki ulivyoyachukulia mahubiri ya Waisilamu; na
jinsi serikali ya CCM ilivyoupokea uchochezi wa uongozi wa kanisa katoliki.
Nimesema kuwa uongozi wa Kanisa Katoliki umeichochea serikali
iyapige marufuku mahubiri ya Waisilamu kwa madai kuwa yamekuwa yakikashifu na
kutukana Ukristo. Ni muhimu kwa hiyo, kuutazama, kwa ufupi na kuona nini
inaweza kuwa kashfa, kabla ya kuingia kwenye suala la mihadhara ya Waisilamu;
inayoitwa kanisa Katoliki, serikali ya CCM na vyombo vya habari kuwa ni
kutukana, kukashifu, michafu, ya kupakazia na kukejeli hadhi ya mengine.
("Definition") maelezo bayana ya kashifa
"Concise Oxford) English Dictionary" inaielezea
kashfa/kufuru (blasphemy) kuwa ni kusema kwa kutoyaheshimu mambo matakatifu;
kusema kukufuru kuhusu jambo; kutusi, kwa mujibu wa "Osbern law
Dictionary" kashfa/kufuru ni kusema kwa kukejeli hadharani au kwa makosa
ya jinai juu ya mambo yanayomuhusu Mungu, Yesu Kristo, Biblia .... kwa
dhamira ya kuleta dharau na chuki dhidi ya Kanisa kwa mujibu wa sheria
zilizopo.
Kwa jumla kufuru/kashfa inaelezeka kuwa ni pale yanaposemwa
mabaya juu ya Mungu kwa lengo la kukejeli ili kushusha hadhi ya utukufu wa
Mwenyezi Mungu na kuyaondoa mawazo ya watu kwenye kumcha na kumpenda Mungu.
Ni kutumia maneno juu ya Mwenyezi Mungu makusudi kwa dhamiri na mpango wa
kuzuia na kuvunja heshima, unyenyekevu na imani anayoistahiki kama Muumba,
mjuzi wa kila kitu, mtawala na mhukumu wa dunia. Inaleta dhana ya kupuuza,
inapotumika juu ya Mungu, kama vile dharau mara kwa mara inavyokuwa na dhana
hiyo pale inapotumiwa juu ya mtu binafsi. Ni kwa makusudi na kwa nia mbaya
kujaribu kumuondolea mwanaadamu unyenyekevu wake kwa Mola wake kwa kukana
kuwepo kwake, au sifa zake kama Muumba mjuzi wa kila kitu, mtawala na
anayehukumu watu wote na kuwazuia watu wasiwe na imani naye.
Lazima kutofautisha baina ya kashafa/kufuru na uzurishi
(heresy), ambayo "Osborn Law Dictionary" inaielezea kuwa ni kosa la
kanuni za kidini linalotokana na mtu kuwa na mawazo ya uongo yanayochukiza na
yasiyokubalika kwa kuhalifu nguzo mojawapo ya imani ya Kikristo.
Kushambulia "kweli" ya Ukristo si kosa kwa mujibu wa
common law.
"Digest of Criminal Law" (9th edition) ya Stephen
inasema sheria ya kashfa/kufuru kwa mujibu wa "common law" iko kama
ifuatavyo: "Kila andiko linahesabika kuwa ni kashfa pale linapokuwa na
jambo lolote ambalo linadharau, linatukana au linakejeli Mungu, Yesu kristo
au Biblia au Kanuni za Kanisa la Uingereza kama ilivyowekwa na sheria. Si
kashfa kusema au kuandika na kutoa mawazo ambayo yanapingana na dini ya
Kikristo, au kukana kuwapo kwa Mungu, kama matamshi/maandishi yenyewe
yanayotolewa kwa lugha yenye heshima na iliyo ya kistaarabu. Kipimo cha
kutumia ni kutazama namna ya jinsi itikadi zenyewe zinavyoelezewa na siyo juu
ya kile kilichomo ndani ya itikadi hizo" (msisitizo unaongezwa).
Katika kesi baina ya Bowman dhidi ya Secular Society (1917)
Bunge la juu la Uingereza (House of Lords) liliamua kuwa kuishambulia au
kuikana kweli ya Ukristo, bila ya kutia matusi, kejeli au utovu wa hesima juu
ya mambo matakatifu, si kuvunja sheria. Na kwenye kesi baina ya R na Lemon
(1979) ambapo wachapishaji wa gazeti la "Gay News" walipitisha
shutuma za kashfa zilizokuwa na maneno yaliyodhaniwa kukasirisha na kutukana
hisia za mkristo (kiasi ninavyomuheshimu na kumpenda Bwana Yesu (AS) siwezi
kuyarudia yale yaliyosemwa. Mahakama ya Rufaa iliamua kuwa kauli inaweza kuwa
ya kashfa kama hoja yake imekuwa ya kuumiza na kutukana; ikijiegemeza siyo
kwenye matumizi ya akili, bali kwenye hisia za kinyama na zisizo za kuungana
na maumbile ya mwanadamu. Baadaye kwenye kesi hiyo hiyo Bunge la juu ya Uingereza
likasisitiza kuwa, katika mashauri ya kashfa, kipimo kimo katika uwezekana wa
kukasirisha na kutukana na siyo uwezekano wa kuvunjika kwa amani.
Kwa hiyo inajulikana na kukubalika kuwa kwa mujibu wa common
law si kashfa kushambulia misingi ya dini kama kanuni za kuweka heshima
na uungwana katika malumbano zitafuatwa. Kwa kweli Tume ya Sheria ya
Uingereza iliamua mwaka 1985 kuwa common law si chombo kinachofaa
kuhakikisha kuwa imani za dini zinaheshimiwa, na kwamba kosa la kashfa chini
ya kanuni za common law lifutwe hasa kwa sababu yamewekwa makosa
mengine katika sheria yanayoshughulikia mwenendo mbaya unaoingilia ibada za
hadhara, au mwenendo wa kutukana wafuasi wa vikundi mbalimbali vya dini ambao
unaweza kuletea kuvunjika kwa amani. Inahusika hapa kuzingatia kuwa nchini
Uingereza mashitaka dhidi ya makosa ya kashfa yamekuwa machache na kwa kweli kesi
ya lemon imekuwa mashitaka ya kwanza baada ya miaka sitini.
Sheria ya kashfa ina uhusiano wa karibu na haki ya msingi ya
uhuru wa dini. Kila mtu ana uhuru wa mawazo, uhuru wa nafsi na uhuru katika
dini. Ingawa uhuru wa dini umechanganya ndani yake haki ya kuitekeleza imani
kwa ibada na matendo, au kwa kufundisha na kutangaza sheria inaweka mipaka
kwa kiasi kile inavyolazimu kuhifadhi usalama wa umma, utaratibu katika
jamii, au maadili, au hali za msingi za watu wengine. Kwa hiyo kile
kisichokatazwa kinaruhusiwa mradi tu hakizuiliwi na sheria nyingine. Kwa
mfano, katika kosa la jinai ndani ya sheria ya kashfa. Hii haina maana, hata
hivyo, kuwa kile kinachoonekana kweli kwa wafuasi wa dini moja au kwa
serikali inayoitetea kwa niaba yao, kinaweza kwa madhumuni ya dini,
kulazimishwa juu ya raia wenye imani inayopingana na dini hiyo. Sheria
inalinda makundi ya dini yasitishiwe na ukandamizaji wa makundi mengine ya
dini. Kwa hiyo mradi tu udadisi na kuhoji, si kitu kuwa kinasumbua misimamo
iliyopo tangu zama kiasi gani inakuwa kwa ajili ya kutafuta na kufikia kweli
hakukuwa kwenda kinyume na sheria. Watu hawawezi kuadhibiwa kwa kufanya mambo
yaliyo ndani ya sheria kwa sababu tu kundi jingine la watu linalalamika.
Sheria za makosa ya jinai nchini Tanzania kwa msingi
zimechukuliwa kutoka sheria za Waingereza; sehemu kubwa ya Penal Code
kutokana na "Draft Code" ya Sir James Fitzjames Stephen ya mwaka
1878. Miaka ilivyopita kulifanyika mabadiliko yaliyolazimishwa na matakwa ya
hali halisi nchini. Kwa mfano kwenye makosa ya jinai yanayohusiana na uhuru
wa dini, sehemu zote zinazomtaja Yesu Kristo, Ukristo na Kanisa la Uingereza,
zilifutwa, bila ya shaka kwa sababu ya kutambua kuwa Tanzania, hapo sheria
hii ilipowekwa ni nchi ya mchanganyiko wa urithi wa dini nyingi na tamaduni
mbalimbali.
Hali halisi hii haijabadilika; sababu zilizopelekea kuwako kwa
hali halisi hii hazijabdilika. Kwa hiyo kifungu cha 129 cha "Penal
Code" kinachoainisha makosa ya jinai kwenye uhuru wa dini kama
unavyotolewa na kifungu cha 19 cha katiba ya Jamhuri ya Muungano kinaeleza
kuwa "Mtu yeyote ambaye, kwa dhamiri za makusudi za kutaka kuumiza hisia
za mtu yeyote, anatamka neno lolote, au anatoa sauti yoyote inayosikiwa na
mtu huyo, au anatoa ishara yoyote inayoonekana na mtu huyo, atakuwa amefanya
kosa."
Hatia ya kosa la kutamka maneno kwa dhamiri ya kuumiza hisia,
inategemea ushahidi kuwa maneno hayo yalitamkwa kwa dhamiri ya kuumiza hisia
na kwamba maneno hayo kweli yameumiza hisia.
Kwa hiyo, tukizingatia urithi wetu Tanzania wa kuwa na wananchi
wa mchanganyiko wa dini mbalimbali si kosa la jinai kwa ukristo kusema kuwa
Yesu ni Mungu au ni mwana wa Mungu, huo ukiwa ndio msingi wa imani ya
kikristo. Wala siyo kosa kwa Muisilamu kusema kuwa Yesu si Mungu au Mwana wa
Mungu, hii ikiwa nguzo katika imani ya Uisilamu kwamba Mungu ni mmoja tu na
hakuna waliosawa naye washirika, au wana. Si kosa vile vile kwa mkristo
kusema kuwa Yesu alisulubiwa na akafufuka; hii ikiwa msingi katika Ukristo.
Na wala si kosa kwa Muisilamu kusema kuwa Yesu hakusulubiwa wala hakufufuka;
hii ikiwa ni sehemu ya imani ya Uisilamu kwamba hakuna kutolewa muhanga kwa
ajili ya kufuta dhambi za wengine. La kweli ni kuwa kilicho kufuru kwa
Ukristo si kufuru katika Uisilamu na kilicho kufuru kwa Uisilamu si kufuru
kwa Ukristo.
Kuonyesha kuwa kifungu cha 129 hakikudhamiria kutafasiriwa kwa
mujibu wa imani ya kikristo au ya kiisilamu hebu tuutazame mfano mmoja
miongoni mwa mifano mingine chungu nzima ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya
Waisilamu. Mfano huu, kwa kweli, unadhihirisha jinsi madai ya viongozi wa
Kanisa Katoliki yalivyo ya uongo, na kwa nini mihadhara ya Waisilamu si ya
kashfa kama inavyong'ang'anizwa na viongozi wa Kanisa Katoliki, serikali ya
CCM na vyombo vya habari nchini.
Kesi hii inawahusu wahadhiri wa Kiisilamu wale waliokamatwa
tarehe 5 September 1996 kama ilivyoripotiwa na gazeti la "Daily
News" la tarehe 6 September 1996; gazeti la serikali lenye sifa ya
kubanwa sana katika utoaji wake wa habari. Zingatia kuwa mwandishi wa
serikali, katika habari hiyo hiyo, anawaita washitakiwa mara mbii
"Muslim Radicals" na "Muslim Fundamentalists",
"Waisilamu wenye siasa kali," kana kwamba washitakiwa walikuwa
wameshitakiwa kwa kuwa "maradical" na "wenye siasa kali",
na sio kwa hicho walichodhaniwa wamekifanya au wameacha kukifanya. Ni dhahiri
kuwa kwa mwandishi huyu na mhariri wake, si kitu kuwa yale yalikuwa ni
mashitaka tu bado, kwamba kulikuwa hakuna lolote lililokwisha thibitishwa
mahakamani dhidi ya washitakiwa, na kwamba kesi yenyewe ilikuwa bado iko
mahakamani na kwa hiyo haki isingetendeka kama washitakiwa wangeanza kupewa
majina ya namna hiyo.
Kwa waandishi hawa wa serikali waliokuwa na msimamo wa upendeleo
wa upande mmoja tayari, kilichokuwa muhimu ni kauli za kuvutia na hamu ya
kutaka kuandaa umma kwamba "maradical" na
"mafundamentalisti" wa kiisilamu wale wako kwenye
"jihadi". Iwe iwavyo, taarifa hii inaendelea kusema kuwa
washitakiwa walitamka maneno ya kupinga Ukristo, kwenye hotuba yao ndani ya
msikiti wa Keko Magurumbasi mjini Dar es Salaam tarehe 4 Septemba 1996,
"yaliyodhamiriwa kuumiza hisia za Wakristo." Taarifa ile inaongeza
kusema kuwa washitakiwa wanasemekana kusema kuwa "Yesu Kristo hakuwa
Mungu kama inavyoelezwa kwenye itikadi ya Utatu Mtakatifu" Hakuna Muisilamu
atakayeongeza kwenye madai yake kwamba Yesu si Mungu maneno ya kauli za imani
ya Kanisa Katoliki ambazo yeye mwenyewe hakubaliani nayo.
Kiini cha mashitaka dhidi ya wahubiri wa kiisilamu ni kwamba
walikataa Uungu wa Yesu. Nasema kuwa hii yenyewe si kashfa wala kosa
linalokusudiwa na kifungu cha 129 cha sheria za Jinai. Ingawa inawezekana iwe
kweli kuwa kusema Yesu si Mungu kunaweza kuwa upingaji katika Ukristo, si
kosa kwa mujibu wa kifungu cha 129 au hata kuwa kashfa kwa; mujibu wa common
law kukana Uungu wa Yesu. Kwa Waisilamu, kwa mujibu wa Qur'an, Yesu (AS)
si Mungu bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwa kweli ni kufuru kusema kuwa
Yesu ni Mungu!
Tunaliona tatizo, kwa hiyo, la kukitaja sisi kifungu 129 maalum
kwa kufuata imani ya Kikatoliki. Nadhani linalotakiwa na kifungu cha 129 ni
zaidi ya hivyo tafsiri yake ni kama ile ya kesi ya Uingereza ya Lemon (1979)
niliyoitaja hapo mwanzo. Hakuna dhamiri mbaya au ya utovu wa heshima katika
kusema kuwa Yesu si Mungu. Kwa dhati kabisa huku ni kutafuta kuifikia kweli.
Na kuihoji kweli ya Ukristo hakuwezi kwenyewe, peke yake, kuwa msingi wa
kuendeshea mashtaka juu ya kosa la kashfa au kutamka maneno kwa dhamiri ya
kuumiza hisia za kidini. Vile vile, si kosa chini ya kifungu 129 kwa
Muisilamu kusema kuwa Biblia sio neno la Mungu, kwa sababu imani hii ya
Waisilamu inatokana na Qur'an inayosema kuwa mafundisho ya Manabii waliopita
yaliyomo kwenye maandiko yameingizwa mikono ya watu na kuchafuliwa na watu
ambao walikuwa hawaiamini dini ya Tawhid.
Lakini litakuwa kosa la jinai kusema Biblia au Qur'an ni
takataka; au kwamba Wakristo au Waisilamu ni wajinga, na kwamba Mtume
Muhammad (SAW) alikufa kwa ukimwi. Maana hakuna lolote la kisomi kwenye kauli
hizi, isipokuwa matusi yanayofurahisha hisia za maumbile ya kinyama.
Inatuhusu hapa kuzingatia kuwa kwa mujibu wa Criminal Procedure
Act ya 1985, kosa la makusudi kusema maneno yanayodhamiria kuumiza hisia za
kidini ni kosa linalohitaji waranti katika kumkamata mkosaji, na waranti
unatakiwa utolewe na hakimu pahali pa kazi kufuatia malalamiko, kabla mtu
hajakamatwa. Hii maana yake ni kwamba, kwa; maneno mepesi, kabla mtu yeyote
hajakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la makusudi kusema maneno yaliyodhamiria
kuumiza hisia za kidini, kwanza mtu lazima apeleke malalamiko yake na
yatiliwe mkazo kwa kiapo kwenye mahakama kabla ya waranti wa kumkamatia mtu
haujatolewa. Kwa hiyo ni kwenda kinyume cha sheria kumkamata mtu ambaye
hakuna shitaka lililotayarishwa au waranti wa kumkamatia kutolewa. Inafaa
kuzingatia kuwa polisi wa Tanzania hawajafuata utaratibu huu hata mara moja
katika harakati zao za kuwakamata wahubiri wa Kiisilamu, jambo ambalo
linadhihirisha ama kutojua kazi kwao, au hisia zao za udini.
Waite (watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha
mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako ndiye
anayemjua aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anayewajua walioongoka.
(16:125)
Na ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko aitaye kwa Mwenyezi
Mungu, na akafanya vitendo vizuri na kusema; "Hakika mimi ni miongoni
mwa Waisilamu.
(41:33)
Kuhubiri dini ni haki iliyotolewa na Mungu na kutambuliwa na
kifungu cha 19 cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Uisilamu, tangu mwanzo wa kuwapo kwa
mwanadamu duniani, dini ya kweli, au mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
daima umekuwa mmoja. Watu wameuacha au wameuchafua mwongozo huu.
Mitume wa kweli wameletwa kuuhuisha na kuutakasa mwongozo huu.
Bali watu wa mataifa mbalimbali walipelekewa Mitume hawa mara kwa mara
wamekuwa wakibuni "michanganyiko" yao wenyewe, au dini, kutoka
vyote viwili, kutoka yale yaliyo kweli na kutoka yale yaliyokuwa yao wenyewe;
nyongeza au tungo zao.
Kwa kiasi kile walichukua yaliyo ya kweli tunapata mambo
yanayofanana katika "michanganyiko" mbali mbali, au dini nyingine
mpya. Kwa kiasi kile waliongeza mambo yao wenyewe tunapata tofauti kwenye
"michanganyiko" au dini.
Dini pekee ya kweli daima imefundisha imani juu ya utii kwa
Mwenyezi Mungu mmoja, na huo ndio Uisilamu. Kwa mujibu wa Qur'an hakuna dini
za kweli, ipo Dini ya kweli. Na manabii wote wametuita kwenye dini moja;
kwenye njia moja na lengo moja:
Amekupeni sheria ya dini ile ile aliyomuusia Nuhu na
tuliyokufunulia wewe na tuliyowausia Ibrahimu, Musa na Issa; kwamba
simamisheni dini wala msifarakane kwayo.(42:13)
Dini ya kweli, au Uisilamu, daima imekuwa kitu kimoja wakati
wote na sehemu zote. Kauli kama "Uislamu umekuwa wa mwisho miongoni mwa
dini zilizofunuliwa" ni kauli ya makosa.
Manabii wote walikuwa Waisilamu ambapo maana yake wale
wanaojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu. Ujumbe wao ulikuwa Uislamu; kuwaita watu
wamuabudu na kujisalimisha kwa Mungu mmoja tu. Adam alikuwa Muisilamu,
Ibrahimu alikuwa Muisilamu, Musa alikuwa Muisilamu, Issa alikuwa Muisilamu,
Rama, kama alikuwa Mtume wa kweli, alikuwa Muisilamu.
Mahubiri ya Waisilamu yanatokana na msimamo huu. Kutokana na
kujua kuwa hata baada ya mtu kufanya makosa na madhambi na kupotea njia,
mwanadamu bado ana nafasi na uwezo wa kurejea kwenye asili yake inayomtafuta
Mungu; kurejea kwenye njia iliyonyooka (dini ya kweli). Uisilamu umeweka njia
ya kuwahubiria watu (Da'wah), kuwarudisha au kuwaita watu kwenye Uisilamu.
Kuwatia watu kwenye Uisilamu maana yake hasa ni uwakaribisha.
Maana yake si kuwavutia kwa mbinu au kuwalazimisha. mtu hawezi kulazimishwa
kuamini au kutoamini. Qur'an inasema wazi wazi kwamba "Hakuna
kulazimisha katika dini" wakati huo huo inaposisitiza kuwa kweli na
mwongozo sahihi vilivyoletwa na Uisilamu vimekwisha tofautishwa mbali na
upotofu. Ndipo kukaribisha kuna maana ya kuwaita watu kwenye Uisilamu
"kwa hekima na mawaidha mema." Hata pale Mtume Musa (A.S) alipoamrishwa
na Mwenyezi Mungu aende kwa Firauni, aliambiwa aseme naye kwa "maneno ya
upole" na kumuwekea matumaini ya kumbadilisha.
Waisilamu, kwa hiyo wana wajibu wa kutimiza kwa watu wa imani
nyingine; kuwakaribisha kwenye Uisilamu na kwenye ibada ya kumuabudu Mungu
mmoja iliyotakaswa na Shirk zote zilizobuniwa na wanadamu. Kutokana na
mahubiri haya watu wanawezeshwa kuamua kurudi kwenye maumbile yao mema ya
asili na kuwa Waisilamu, au wanaweza kuamua kubaki kwenye dini zao.
Hakuwezi kuwapo hata na fununu tu ya majivuno au ubabe katika
kuwakaribisha watu, kung'ang'aniza au matumizi ya nguvu; kwani Qur'an
imesisitiza: "Kusiwapo kulazimishana katika dini" kwani "kweli
imewekwa bayana mbali na uongo." Kazi ya kuhubiri inatakiwa itekelezwe
kwa kuzingatia ipasavyo maagizo ya Qur'an yasemayo; "Waite katika njia
ya Mola wako kwa hekima na mauidha mema."
Wahubiri wa Kiisilamu wameichukua taaluma ya dini linganifu
kuwakaribishia kwenye Uisilamu Watanzania wenzao waliotelezea kwenye Ukristo.
Kwenye shughuli hii hutumia vitabu vyote viwili Biblia na Qur'an,
kuwathibitishia Wakristo kiasi gani wamepotea njia. Kwa kutumia Biblia haina
maana kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kufikia kwenye kweli ya Mwenyezi Mungu.
Qur'an inazifafanua imani za Ukristo kwa njia zilizo wazi kabisa zisizo shaka
yoyote:
Dhambi hazirithiwi - Q:2:123, 6:164, 53:38-42. "Utatu"
ni tungo za wanadamu - 4:171-172, 5:73. Yesu si Mungu - 4:171-172, 5:17,
5:72-75, 5:116:118. Yesu Kristo hakuuawa wala hakusulubiwa - 4:157-158.
Waisilamu wanatumia ushahidi wa maandiko ya kikristo
kuthibitisha hoja zao kwa sababu wanashughulikia akili za watu
waliotayarishwa tangu utoto kukubali ("dogmas"), itikadi; bila ya
kutumia akili.
Wakristo wamekuwa wakifundishwa kwenye shule za watoto wadogo za
siku za jumapili, na wamekuwa wakisikia tangu wangali wadogo, kuwa Yesu ni
Mwana wa Mungu na kadhalika.
Ikumbukwe pia kuwa hali halisi ya nchi yetu Tanzania
inalazimisha matumizi ya mtindo huu. Shughuli ya kujenga makoloni na kutawala
katika Africa iliyofanywa na Wazungu katika kipindi cha karne mbili
zilizopita iliambatana wakati huo huo na uvamizi wa Africa uliofanywa na
wamisheni wa Kikristo ambao, kwa kutumia hadaa na taarifa za kupotosha,
walifanikiwa kueneza Ukristo kupitia vivutio vya shule na hospitali.
Inawawajibikia Waisilamu kuwasaidia ndugu zao wakristo
kujikomboa kutokana kwenye makongwa yaliyokuwa yanatawala vipawa vyao vya
kufikiri kwa miaka elflu mbili iliyopita:
Ninyi ndio umma bora katika umma zote zilizodhihirishiwa watu -
mnaoamrisha yayiliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamuamini Mwenyezi
Mungu. Na kama wale waliopewa kitabu (Wayahudi na Wakristo) wangeliamini
ingekuwa bora kwani miongoni mwao wako wanaoamini, na wengi wao wanatoka
katika taa ya Mwenyezi Mungu.
Waisilamu wanatumia kitabu wanachokiamini Wakristo kuwaitia
kwenye Uisilamu kwa kuwaonyesha udhaifu wa imani wanazozifuata. Qur'an
inawaamrisha Waisilamu wadai ushahidi kutoka kwa Wayahudi na Wakristo wa
madai yao kwamba "wokovu" unapatikana kwao tu; "Leteni dalili
zenu kama ninyi ni wasema kweli" 2:111.
Wamisheni wa kikristo wameichapisha Biblia katika lugha zaidi ya
alfu moja na kutawanya dunia nzima, wakiyatisha mataifa ya dunia kukubali
kuwa "kristo alikufa na madhambi ya wanadamu" na kwamba yeye ndiye
"mwokozi pekee". Wakati wote Biblia yenyewe ikiwathibishia kuwa
madai haya si kweli. Waisilamu, kwa hiyo, wanawajibika kuwakomboa Wakristo
kutoka kwenye udanganyifu huu na hakuna njia bora zaidi ya kufanya hivyo
kuliko ile ya kutumia ushahdi wao wenyewe na hoja zao wenyewe kuvunjia madai
yao.
Kwa kutumia Biblia, Waisilamu hawaishambulii Biblia yenyewe. Kwa
mujibu wa Gary Miler, mtaalamu wa Hisabati Muisilamu wa Canada aliyerejea
kwenye Uisilamu, Waisilamu "hushambulia zile itikadi zisizo na ushahidi
wowote, zinazotolewa na wataalamu wa dini ya Ukristo kuhusu Biblia.
Waisilamu wanaamini kuwa Biblia ina maneno ya Mwenyezi Mungu,
bali hawakikubali kila kitu kilichomo humo. Kuamua sehemu gani za Biblia
zinakubalika kwa Waisilamu hakuji kwa mapenzi tu. Ni suala linalosimama
kwenye kweli tu daima. zile sehemu, na ni sehemu hizo tu, ambazo daima
zinajidhihirisha kwenye kweli, zinakubalika akilini zinajiddhirisha zenyewe
kuwa ni maneno ya wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, sehemu hizo ndizo
zinazokubalika kwa Waisilamu; (Gary Miller, "A. concise reply to
Christianity: A Muslim View, iliyomo kwenye "A Colleciton of Comparative
Religion Booklets" na Ahmed Deedat na wengine, Durban).
Katika kuwaita Wakristo kwenye Uisilamu, Waisilamu wanajua kuwa
kuna mambo mengi ya muhimu ambayo yanapatikana kwenye Uisilamu na Ukristo.
Waisilamu na Wakristo wanaamini na kuchangia mengi yanayofanana; imani, mambo
ya kuthaminiwa, maadili na kanuni za mienendo na tabia. Bikira Maria na
mwanawe Yesu (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao, wote) wanatajwa mara kwa
mara ndani ya Qur'an. Kwa kweli kuna sura nzima ya Qur'an iliyopewa jina la
Bibi Mariamu - inaitwa hivyo hivyo; Mariamu. Tofauti kubwa baina ya imani
hizi mbili inatokana na nafasi ya Yesu katika dini.
Yesu, katika Qur'an anaitwa Isa ibn Maryamu - Isa mwana wa
Mariamu, ni mmoja wapo wa manabii wakubwa wa Mwenyezi Mungu ambaye waisilamu
wanamuweka kwenye daraja ya juu ya mapenzi na heshima. Qur'an inathibitisha
kuwa Yesu alizaliwa na mama Bikira (Mariamu) kutokana na uwezo ule ule uliomuumba
Adam bila ya baba au mama:
Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam;
alimuumba kwa udongo kisha akamwambia; "kuwa", basi akawa.(3:59)
Yesu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, alifanya miujiza mingi.
Alipewa uwezo wa kusema akiwa bado yungali mchanga, kuponya wangonjwa,
kufufua wafu na kufikia nyoyo za watu kwa mwongozo alioleta kutoka kwa Mungu.
Na mwisho, pale alipokuwa katika hatari ya kuuawa na watu wake mwenyewe,
Mungu "akamnyanyua," Qur'an inasema hakuuawa wala hakusulubiwa.
Qur'an inasisitiza kwenye aya chungu nzima kuwa Yesu si mwana wa
Mungu, kwamba yeye mwenyewe hakudai kuwa alikuwa mwana wa Mungu wa dhati ya
Mungu bali badala yake amewaagiza wafuasi wake wamuabudu Mwenyezi Mungu
pekee. Inasema pia kuwa dhana kwamba Mwenyezi Mungu aliye juu ana mtoto
inadhalilisha na iko mbali mno na utukufu na ukuu wake kiasi cha kuwa kufuru
kubwa:
Maana Mwenyezi Mungu, muumba na mpaji riziki wa ulimengu huu,
pamoja na ukubwa wa mchanganyiko wake wote wa maumbile yasiyo mithilika, yuko
mbali na juu mno ya kitu chochote tunachoweza kukifikiria.
Upungufu wa maumbile ya vitu vyote hivi vilivyoumbwa ni udhaifu
ambao hatuwezi kuvihusisha na dhati ya Mwenyezi Mungu. Kama Yesu kweli
angekuwa mwana wa Mungu angekuwa mshiriki katika Uungu na yeye mwenyewe
angekuwa na dhati ya Uungu, na hapo Mungu angekuwa wakati huo huo amezaa,
amezaliwa, ameishi kama mwanadamu, na akafa. Dhana hii haistahili neno!
Inahusiana zaidi na ngano za kipangani; ambamo "Miungu" walizaa
miungu-watu na wanawake wa kibinadamu, kuliko na dini ya kweli inayotoka kwa
Mwenyezi Mungu katika misingi ya uhusiano unaopatikana baina ya Muumba na
alivyoviumba. Ndiyo maana dai kwamba Yesu ni mwana wa Mungu haliwezi kuwa
chochote, kwa dhati yake, ila la uongo kwa sababu linapingana na dhati na
sifa za muumba mwenyewe, likimporomosha kwenye daraja la viumbe aliowaumba.
Kwa maneno ya Qur'an:
Uisilamu haulikubali dai kuwa Yesu alikufa msalabani na kwamba
alikufa muhanga kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Haulikubali wazo la dhambi
ya asili ambalo kosa la asili la Adam la kumuasi Mungu linarithiwa na kizazi
chake chote. Kwa maneno mengine, haukubali kuwa wanadamu wote duniani wana
dhambi kwa sababu ya uasi wa Adam kwa Mwenyezi Mungu. Adam alitubu, na kuomba
msamaha kwa makosa yake na Mwenyezi Mungu akamsamehe.
Uisilamu unasema kuwa wanadamu wote wanakuja duniani bilia hatia
wala dhambi. Mtoto mchanga habebi mzigo wa dhambi zilizofanywa na mzazi wake.
Hii ingekadhibisha sifa za Mwenyezi Mungu za haki na huruma.
Kudai pia kuwa dhambi hii kwa hakika itampeleka kila mwanadamu
motoni na adumu humo daima kama Mungu hajitoi muhanga kuifidia kwa ajili ya
viumbe wake, vile vile ni kuzikana sifa za haki na rehema za Muumba kwa waja
wake. Hakuna anayeweza kuokoka bila ya huruma na rehema za Mwenyezi Mungu na
kumkubali na kunyenyekea kwa muumba wake na mwongozo wake. Mtu anaweza kurudi
kwa muumba wake kwa utii na kutubu bila ya haja ya kuwapo mtu wa kati au
muombeaji:
Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine, wala
hakitakubaliwa kikomboleo kwake; wala maombezi hayatafaa, wala
hawatanusuriwa.((2:123)
Tofauti nyingine kubwa kati ya Uisilamu na Ukristo iko kwenye
itikadi ya Utatu. Ikiwa Mungu ni mmoja tu, kama Wakristo wanavyodai wanaamini
sawa wanavyoamini Waisilamu, haiwezekani wakati huo huo tena awe watatu -
kwamba wako watatu ndani ya mmoja na mmoja ndani ya watatu! Hata mtoto mdogo
sana anaweza kuiona kweli ya hoja hii. Kwa kawaida Wakristo wanauelezea utatu
kuwa si kwamba wako waungu watatu bali sehemu tatu au nafsi tatu za Mungu
mmoja zenye kazi mbalimbali.
Lakini Mungu si kama keki au chungwa linaloweza kugawanywa
katika theluthi tatu zinazokuwa kitu kimoja: kama Mungu ni nafsi tatu au ana
sehemu tatu, Hawi tena ;Mungu mmoja tu, pekee, asiyegawanyika, ambavyo ndiyo
Mungu alivyo na ndivyo Wakristo wanavyodai alivyo! Kwa Waisilamu hili
halileti maana yoyote; na hata kama wataalamu wa dini ya Ukristo watatuelezea
utatu kuwa ni "Fumbo," lililo juu sana ya uwezo wa mwanadamu yeyote
kulielewa, imani ya utatu inachukuliwa na Uisiliamu kuwa ni aina ya
kumshirikisha Mungu.
Na hata hivyo utatu haumo ndani ya Biblia. Neno utatu halimo
ndani ya Biblia au Kamusi za Biblia; haukufundishwa kabisa na Yesu, na wala
hakuwahi kuutaja hata mara moja. Hakuna ushahidi au pa kushikizia utatu ndani
ya Biblia ili ukubalike. Baadhi ya wasomi wa kikristo wamefikia uamuzi huu.
Tom Harpur, mwandishi mashuhuri wa nakala zinazozungumzia dini. Kwenye gazeti
la "Sunday Star", na Profesa wa zamani wa Agano Jipya kwenye Chuo
cha dini cha Toronto, anaandika kwenye kitabu chake mashuhuri "For
Christs sake" (Oxford Univerity Press, Toronto 1986):
"Kwa kweli ni wahubiri wachache sana wanaoweza kutoa
maelezo yanayoeleweka ;juu ya itikadi ya utatu au juu ya itikadi ya mwanadamu
kuwa Mungu au Mungu kuwa mwanadamu; yaani Yesu aliku mtu kweli na wakati huu
Mungu kamili. Wanarudia rudia miundo ya kauli zilizosanifiwa, kwa magomvi na
uadui mwingi, kwenye karne za nne na tano, na watu ambao mahitaji yao katika
maisha, mtazamo wao juu ya maisha na jinsi walivyokuwa wanauelewa ulimwengu,
kulikuwa tofauti sana na vile tulivyo sisi. Miundo hii haina manufaa sasa
badala yake, inaweka vikwazo vikubwa sana kwa watu wengi ambao, vingine,
wangeweza kuwa wanafunzi wa Yesu wa zama zetu.
Linalolifedhesha kanisa ni ule ugumu wa kuzithibitisha itikadi
hizi kwa kutumia ushahidi wa maandiko ya agano Jipya. Huwezi ukaikuta itikadi
ya utatu ikielezewa pahali popote ndani ya Biblia .... .. Humkuti Yesu popote
akidai wazi wazi kuwa yeye ni nafsi ya pili katika utatu, akiwa sawa na baba
aliye mbinguni. Myahudi mcha Mungu; angetishwa na kuchukizwa sana na wazo
hilo.
Katika muda wa miaka kumi hivi iliyopita nimekuwa nikizungumza,
kwa muda mrefu, na kwa mara nyingi kama ilivyowezekana, na watu wa kawaida na
viongozi wa dini wa madhehebu yote juu ya itikadi hizi, na nilichokigundua ni
kuchanganyikiwa kwingi kila pahali - jambo ambalo peke yake ni baya. Lakini
kuna mabaya zaidi. Utafiti huu umenifanya niamini kuwa wengi sana wa wale
wanaokwenda makanisani, katika ibada zao ni watu wanaoamini miungu watatu.
Yaani, wanasema kuwa wanamuamini Mungu mmoja lakini kwenye ibada zao
wanaabudu miungu watatu.(uk.7)(msisitizo unaongezwa)
Katika juhudi zao zakuliunga mkono tamko la Nicene (Nicene
Creed) juu ya utatu, wataalamu wa dini wa Kikristo wanadai kuwa Yesu mwenyewe
alisema; Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza
kwa jina la Baba, na Mwana, na roho Mtakatifu "(Mathayo 28:19) na kwa
hiyo itikadi ya utatu inaonekana kuungwa mkono na maandiko na kristo
mwenyewe. Lakini kwa mujibu wa harpur "Wataalamu wote wa dini ya
kikristo, isipokuwa wale waliobobea kwenye kung'ang'ania ya kale,
wanakubaliana kuwa sehemu ya pili ya amri hii (Mathayo 28:19) angalau ilikuja
kupachikwa baadaye "(For Christ's Sake, uk.84). Kwa vyovyote vile jambo
la muhimu la kuzingatiwa ni nafasi ya kila mmoja wao. Wapi inaposemwa kuwa
watatu hawa wanachangia usawa?
Ushahidi wa nguvu kabisa juu ya itikadi ya utatu unapatikana
kwenye Yohana 5:7-8 kwenye toleo la Biblia la King James ambamo inasemwa;
"Kwa maana wako watatu washuhudiao (mbinguni, Baba, na Neno na roho
Mtakatifu, watatu hawa ni umoja, kisha wako watatu washuhudiao duniani],
Roho, na maji na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja." Lakini
sehemu hii; "Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja
"imetolewa sasa katika Biblia za toleo la King James la mwaka 1971 na
katika Biblia nyingine nyingi kwa sababu ilikuwa nyongeza iliyojipenyeza
kwenye maandiko ya asili katika lugha ya kiyunani; (Kigiriki).
Yohana 5:7-8 kwenye Biblia ya toleo la King James inasomeka
hivi, "Naye roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu Roho ndiye kweli: kwa
maana wako watatu washuhudiao; Roho na maji na damu, na watatu hawa hupatana
kwa habari moja." Wakristo wengi pamoja na viongozi wao na wahubiri,
hawalijui hili.
Tungo hii ya itikadi ya utatu iliyotayarishwa na Athanasius,
"deacon" Mmisri aliyeishi mjini Alexandria, iliidhinishwa katika
mtaguso wa NIcea mwaka 325 B.K., karne tatu na zaidi baada ya Yesu kutoweka. Bila
shaka upagani wa Kirumi - Mungu wa utatu ulihusika na itikadi hii. Kama vile
tarehe 25 Desemba, siku ya kuzaliwa Mithra, Mungujua wao, ilifanywa kuwa siku
ya kuzaliwa Yesu.
Huu, basi kwa kifupi, ndio msimamo wa Uisilamu kuhusu Yesu na
Ukristo, masuala yanayozungumziwa sana kwenye mihadhara yao, ambayo viongozi
wa Kanisa katoliki ndiyo wanayoisema kuwa ni ya kukashifu.
Sasa, kama yesu mwenyewe hakusema kuwa alikuwa mwana wa Mungu na
mwokozi wa dunia, imekuwaje basi kuwa Injili zimeleta madai hayo? Na
imekuwaje basi kuwa wakristo wamekuwa wakiyaamini hayo tangu zama hizo?
Lazima ikumbukwe kuwa si Wakristo wote, hata katika zama zetu
hizi, wanaoamini hivyo. Kuna makundi ya Wakristo amabo hawaamini kuwa Yesu ni
Mungu na katika zama za mwanzo wa Ukristo kulikuwako na madhehebu kadhaa ya
Wakristo; baadaye yakaja kuhesabiwa na mababa wa Kanisa kuwa ni ya uzushi,
hapo ilipokwisha "amuliwa" kuwa Yesu alikuwa Mungu, ambayo
hayakukubali kuwa alikuwa Mungu, wakishikilia kuwa alikuwa mwanadamu na Mtume
wa Mwenyezi Mungu. Miongoni mwao pia kulikuwako wengine ambao hawakuamini
kuwa Yesu alisulubiwa, bali waliamini kuwa mtu mwingine aliyekuwa amefanana
naye sana alisulubiwa badala yake.
Lazima ikumbukwe pia kuwa suala la wanadamu wa Yesu si suala
jipya liloibuka katika zama zetu baada ya watu kuanza kuyachambua maandiko ya
Biblia, au kwa kuja Uisilamu.
Historia yote ya Ukristo ni historia iliyojaa mijadala na
malumbano hayo. Na wala hakukuwako na uhaba wa Wakristo waliokana Uungu wa
Yesu. Huko nyuma sana mwaka 1546, katika mji wa Minister, nchini Uholanzi
watu 30,000 waliuliwa kwa kukana Uungu wa Yesu, (E.M.Wilbur, "A History
of Unitarianism: Socianism and its Auticedents," Beacon Press, Boston,
1945 page 41.
Mwaka 1978, Profesa Robert Alley alifukuzwa kazi yake ya
uenyekiti wa idara ya Dini, Chuo Kikuu cha Richmond (Virginia), kwa sababu
alikana kuwa Yesu aliwahi kudai kuwa alikuwa mwana wa Mungu. Ni bahati yake
kuwa nyakati zimebadilika, vingine angepoteza maisha yake - kama Rev. John
Gray, kiongozi wa Kanisa la Pressby Beterian la Scotland, alivyoshindwa
kujizuia kutamka kwenye uzinduzi wa Kitabu cha John Hicks "The Myth of
God Incarnate" mwezi July, 1977; "... katika zama zile tulipokuwa
wakali ningetoa shitaka la uzushi "(heresy), (International Tribune,
July 1977).
Iwe iwavyo, vikundi hivi vya "uzushi" vilikandamizwa
na karibu vifutike vyote. Suleiman Mufassir, msomi Muisilamu wa Marekani
ameandika kwenye kijaride chake "Jesus in the Qur'an (Plaiafield,
Indiana uk.14) kuwa "Ni jambo la kuzingatia kuwa zile itikadi ambazo
Qur'an inazikubali zinaweza kuthibitishwa kwa urahisi kuwa zilikuwa sehemu ya
mafundisho yaliyotolewa na wanafunzi wa awali wa Yesu, ambapo zile ambazo
Qur'an inazikataa zinathibitika kuwa ni nyongeza zilizopachikwa baadaye na
Kanisa, zinazotokana na falsafa na imani za kipagani, kiyunani na
kirumi."
Na kuhusu dai kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mungu lazima ikumbukwe
kuwa Injili nne za Agano Jipya, Injili za Mathayo, Marko, Luka na Yohana,
ziliandikwa miaka chungu nzima baada ya wakati wa Yesu.
Utafiti wa Maandiko ya Biblia umethibitisha bila wasiwasi kuwa
hakuna hata mmoja katika waandishi wa Injili hizi ambaye alikuwa mwanafunzi
wa au, aliyekuwa pamoja na Yesu; aidha, hawakuandika Injili zao katika lugha
ya Yesu, Kiibrania, bali waliandika katika lugha ya kiyunani. Kufikia katika
wakati ule walipoandika juu ya maisha ya Yesu, mambo mengi yaliyomuhusa Yesu
yalikuwa "yamepotea" au kusauliwa na mengi mengine yalikuwa
yamepenyezwa na zaidi ya yote, Ukristo ulikuwa sasa umo katika kufinyangwa
katika muundo uliovutia zaidi kwa Wagiriki na Warumi kuliko kwa Wayahudi wa
Palestina.
Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala
ya Mwenyezi Mungu, na Masihi mwana wa Mariamu, hali hawakuamrishwa isipokuwa
kumuabudu Mungu mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa ila yeye. Ametakasika na
yale wanayomshirikisha nayo.(Q.9:31)
Wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao lakini
Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kuitimiza nuru yake, ijapokuwa makafiki
wanachukia.(Q9:32)
Enyi mlioamini! Wengi katika makasisi na wacha Mungu (wao)
wanakula mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu.
Mihadhara inayoendeshwa na Waislamu imefanikiwa katika
kuwasilimisha wakristo, baadhi yao wakiwa mapadre na wachungaji. Viongozi wa
kanisa katoliki wakaogofya sana na hali hii na kwa sababu hawana uwezo
wakupambana na hoja za Waisilamu kwa nguvu ya maandiko, wakaikimbilia
serikali wakiichochea ifungie mihadhara ya Waisilamu kwa madai kuwa ilikuwa
inakashifu na kuutukana Ukristo. na kwa kutia watu hofu, viongozi wa kanisa
katoliki wakasingizia kuwa mihadhara ya Waisilamu ilikuwa inahatarisha amani
ya Tanzania.
Tunasema kuwa mbinu hii ya kanisa katoliki ilikuwa ni laghai na
ya kutoa taarifa za uongo. Ilikuwa ni mpango uliodhamiriwa kuwafanya
waisilamu waonekana maadui wa amani na kungiza serikali katika juhudi zao za
kumshinda adui. Mpe mbwa jina baya kisha muwauwe.
Ndipo Kadinali Pengo (wakati huo akiwa Askofu Mkuu Pengo),
kwenye barua yake ya kichungaji ya mwaka 1993 (St. paul Publications,
Nairobi) kama Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, akasema kuwa "... chokochoko
za kidini malumbano yasiyo na msingi na mihadhara ya kashfa ya vikundi vya
Waisilamu dhidi ya dini ya kikristu ni ishara ya wazi ya kuingiliwa na
Uisilamu wenye siasa au msimamo mkali hapa Tanzania.
"Chokochoko za kidini, malumbano yasiyo na msingi na
mihadhara ya kashfa za vikundi vya Waislamu dhidi ya dini ya Kikristu ni
ishara wazi ya kuingiliwa na Uislamu wenye siasa au msimamo mkali hapa
Tanzania. Tukijua matokeo ya kushamiri kwa Uisilamu wenye siasa au msimamo
mkali katika nchi au taifa lolote tunakuwa na kila sababu ya kupata hofu na
wasi wasi kuhusu kudumu kwa amani katika nchi yetu kwa siku za mbele".
Barua ya kichungaji ya kadinali Pengo ilifuatiwa na Tamko la
Maaskofu lililotiwa saini na Mwenyekiti wake, Askofu Josephat Lebulu. Kwenye
tamko hili la mwaka 1993, maaskofu wa kikatoliki walisema," :
Katika mihadhara ya dini ya Waislamu wenye siasa kali dhidi ya
dini ya Kikristu yanashambuliwa mambo kadhaa ya msingi kwa imani ya Kikristu;
kwa mfano: Umungu wa Kristu, Ufufuko wa Kristu, Uwepo wa Kristu katika
Ekaristi Takatifu n.k.
"Kuna madharau ya wazi kabisa kwa dini ya Kikristu.
Mihadhara ya kashfa, kanda za kashfa na baadhi ya Magazeti yanaendelea
kutukana. Tumetambua ukimya wa Serikali kuwa ni kigezo cha kuhimiza kashfa na
chuki hizo. Tumeng'amua kuwa waumini na watu wote wenye mapenzi mema wa dini
mbali mbali, wakiwemo Waislamu, wamefikia kukinaishwa na maudhi ya kashfa
hizo. Pia wamekinaishwa na ukimya wa Serikali kutochukua hatua zinazostahili
kukomesha kashfa hizo.
Tamko hilo laendelea kwa kusema:
"Lakini hali hii ya kashfa za kidini na ukimya wa serikali
inabomoa jitihada hizo zote. Hivyo badala ya amani hali hiyo inajenga
mapambano; badala ya upendo, chuki, badala ya utulivu, vurumai na badala ya
uelewano, mfarakano. Mwisho wake ni umwagaji wa damu".
Inafaa kuzingatia kuwa uongozi wa kanisa katoliki ulitoa
mashambulizi yao dhidi ya mahubiri ya Waisilamu wakati wa kipindi cha mwisho
cha utawala wa Rais Mwinyi, wakidokezea kuwa Rais Mstaafu huyu Muisilamu,
alikuwa akiyaunga mkono kwa kutoyachukulia hatua yoyote ya kuyazima. Lakini
Mwinyi, kwa kutambua dhati ya tatizo lenyewe, alijaribu kuleta suluhu kwa
kuitisha mkutano wa maaskofu na masheikh, usuluhishaji huu haukufanikiwa kwa
sababu maaskofu hawakuweza kuleta ushahidi wa madai yao. Lakini waliendelea
na mashambulizi yao, yaliyfikia kilele chake kwenye maonyo yaliyotolewa na
Padre Lwambano kwenye Radio Tumaini tarehe 8 ya Februari, 1998.
Iwe iwavyo, ni wazi kuwa mashambulizi ya viongozi wa kanisa
katoliki yalikuwa laghai ya uchokozi na yaliyojaa taarifa za uongo; hayakuwa
na msingi wowote wa kisheria na yalidhamiriwa kuwatisha na kuwakasirisha
Watanzania ili kuhakikisha kuwa serikali na wakristo wa kawaida wanauona
Uisilamu na waisilamu kuwa ni tishio kwa amani ya Tanzania.
Kulikuwa hakuna kabisa ushahidi wa matusi, chuki au tishio kwa
amani ya Tanzania. Wakristo wa kawaida (sio mapadre na wachungaji) na
Waisilamu walikuwa wakiendesha maisha yao, wakishirikiana pamoja katika
maisha ya pamoja au binafsi, wasiwe na habari kabisa ya tishio lolote; la
kweli au la kubuniwa, juu ya amani na usalam wao. Wasiwasi wao ulikuwa juu ya
mfumuko ya bei, uchumi ulioendeshwa hovyo hovyo wizi, rushwa ya hali ya juu,
uhalifu uliokuwa ukiongezeka kila leo na kumomonyoka kwa maadili kwenye jamii
ya Watanzania.
Kama kweli lazima isemwe kama kulikuwa na tishio lolote
lililoletwa na mihadhara ya Waisilamu, basi tishio hilo lilikuwa kwa uongozi
wa kanisa uliokuwa unaona kuwa mamlaka yao juu ya wakulima na wafanyakazi wa
kikristo yalikuwa hatarini. Maana viongozi wa kanisa waliingiwa na hofu
walipoona kuwa mihadhara ya waisilamu ilikuwa inawaharibia mambo; ilikuwa
inawaamsha na kuwaelimisha wakristo wakati wao, ili kuhifahdi masilahi yao, walitaka
wakristo waendelee kubaki kizani.
Kwa mtu ambaye haijui historia na utaratibu wa uendeshaji wa
kanisa katoliki itakuwa vigumu kuuelewa msimamo uliochukuliwa na viongozi wa
kanisa hili kutokana na ukweli kuwa wote, wakristo na waisilamu kukika
uhusiano wao, wanatambua kuwa kutangaza dini ndiko kiini cha imani yao.
Uhuru wa kutangaza na kubadili dini ni haki ya msingi
inayotolewa na Mungu. Kwa kiasi kile kile kanisa katoliki lingalivyopenda
kuendelea na shughuli zake za "kuwabatiza" waisilamu nalo, kwa
kiasi hicho hicho, lazima litambue uhuru wa waisilamu kutangaza dini yao na
wa wakristo kubadili dini na kuwa waisilamu kama wanataka kufanya hivyo.
Kwa maana katikati ya imani ya kikristo ni umuhimu na amri ya Mungu
kuitangaza dini.
Kanisa katoliki lazima litambue kuwa watu wana haki ya kuikubali
imani wanayoletewa. Lakini inaonekana kuwa haya ni matumaini ya bure kwa
sababu viongozi wa kanisa katoliki wanawaagiza waumini wao wasijiingize kwenye
majadiliano na Waisilamu ingawa majadiliano kati ya imani na imani siku zote
yamekuwa yakihimizwa ndani ya Biblia; kwa mfano katika Isaya 1:18 --
"...Njooni tusemezane" msimamo unaochukuliwa na uongozi wa kanisa
katoliki si wa kikristo. Maana vipi mtu atatii amri ya "Basi, nendeni
mkawafanye mataifa yote," bila ya kwanza kuwaeleza ukweli wa namna
fulani? Naam, vipi waisilamu wanaweza kubatizwa na kuwa wakristo ili nao vile
vile "kwa nguvu ya neno waweze hapo apendapo Mungu, kuingizwa kwenye
kanisa lake" bila ya kwanza kuwashawishi, au kuwapa ushahidi wa
"kupotea kwao kutoka imani ya kweli ya ukatoliki?"
Haieleweki pia kwa nini viongozi wa kanisa katoliki wakwepe
majadiliano na uchunguzi ndani ya Injili ambazo kanisa lenyewe linadai kuwa
ni maneno ya Mungu. Ni kwa sababu uongozi wa kanisa katoliki, baada ya wao
kushawishika kuwa Injili hizi ni kweli, basi wanamtaka kila mtu wafuasi wao
na hao wanaotaka kuwabatiza, wawaamini na kuwafuata wao tu bila ya udadisi
wowote? Au ni kwa sababu uongozi wa kanisa katoliki unaamini kabisa kuwa dini
haihusiani na tashi za akili, mantiki na kiasi kwenye matumizi ya akili au
tashi za maumbile tu?
Tukianza na ile kweli kuwa misingi ya dini ya kweli lazima iwe
inaeleweka kwa mtu yeyote wa kawaida anayetumia akili na fahamu zake, dini
yoyote inayomtaka mtu asiyeiamini dini hiyo alikubali msingi wake kwa imani
tu, dini hiyo huwa ni kwa ajili ya waumini wake tu. Si hivyo tu bali imani ya
watu juu ya dini hiyo itaathirika vibaya pale itakapokuja pambanishwa na udadisi
wa kawaida au pale watu watakapokuwa huru kutumia akili zao.
Kwa upande mwingine dini ambayo misingi yake inakubaliana na
tashi za maumbile asilia ya mwanadamu wanadamu, hawatapoteza imani yao juu
yake, hata pale wafuasi wake wanapokuwa wafuasi wa majina tu.
Misingi ya dini ya kweli haipingani na tashi za maumbile asilia
au matumizi ya kawaida ya akili. Dini ya kweli haidai kuwa kwanza uamini
halafu ndipo utakapoiona kweli yake. dini ikiwa hivyo basi dini hiyo
itaonyesha kuwa baadhi ya watu wanazaliwa wasiweze kupokea mwongozo wa wokovu
na kwamba hakuna nafasi sawa kwa wanadamu za kufika peponi, kufuata
"uzima wa milele".
Kweli ni kwamba kanisa katoliki lazima likubali kuwa Mungu
amemuumba mwanadamu na maumbile ya nafsi yenye kutambua mema na mabaya, na
akili, zenye uwezo wa kuchambua na kufafanua mambo. Mwanadamu pia ana uhuru
wa khiari; kupima na kuchambua hayo anayohubiriwa ili aweze kuona kuwa hayo
anayoambiwa ni kweli, yana mantiki na yanakubaliana na tashi za maumbile yake
asilia na kuamua kuyafuata kama akiamua hivyo.
Viongozi wa kanisa hawakupewa na kwa hiyo wasijipe, majukumu ya
kumchagulia mwanadamu nini cha kusikiliza na nini cha kuacha kusikiliza. Hata
hivyo, kwa sababu tunaambiwa kuwa wakristo wanaamini kuwa Roho Mtakatifu
hukaa ndani yao ili kuwaongoza kwenye kweli na ucha Mungu (Yohana 16:8,
16:13), hakuna haja basi ya uongozi wa kanisa katoliki kuogopa majadilinao na
mazungumzo ya kutumia hoja juu ya kweli ya ukristo. Yaani kama kweli
uongozi wa kanisa unaiamini kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya wakristo na wao
hawana lolote la kuficha.
Tunatamka kuwa tabia hii ya viongozi wa kanisa katoliki ya
kuzuia zuia ukweli isijulikane na kutopenda kudadisiwa na majadiliano
inatokana moja kwa moja na historia ya Kanisa Katoliki na hasa hasa muundo
wake wa uendeshaji. Pamoja na yote yanayosemwa na Papa John Paul II katika
ziara zake duniani kwa mfano kule Cuba au Nigeria, ofisi ya Papa yenyewe
haina historia ya kutetea ukweli na uhuru wa mwanadamu.
Kwe kweli uongozi wa kanisa katoliki unaoshika mamlaka mwisho na
pekee kutokea juu, hauruhusu uhuru wowote na majadiliano kutoka kokote, ikiwa
ni wataalamu wa dini au wasomi wa Biblia wake wenyewe, ukiamini kwamba eti
uhuru na majadiliano husababisha kupotea kwa ukweli.
Peter de Rosa, aliyewahi kuwa Padre asemaye kuwa kazi yake ni
kazi ya "rafiki na siyo ya adui," anasema kwenye kitabu chake
maarufu sana, "Vicars of Christ" (Corg Books, London, 1984) kuwa
madai kwamba ofisi ya Papa ni mtetezi wa kweli na haki za wanadamu ni ya
uongo"... Mbali na kwamba upapa wa karne ya kumi- na ya kumi na tano -
wenyewe ndio uliokuwa uzushi; kukanwa kwa kila kitu alichokileta Yesu, mapapa
wengi walifanya makosa ya kustaajabisha. Mara kwa mara walipingana wenyewe
kwa wenyewe na Injili. Wachache kwamba hawakutetea hadhi ya mwanadamu, mara
chungu nzima waliwanyima wakatoliki na wasokuwa wakatoliki hata zile haki zao
za kawaida tu.
Historia inavunja kabisa ngano za upapa usio na dosari kwenye
masuala ya kweli. Kwenye karne za unayama mapapa ndio waliokuwa viongozi wa
unyama, kwenye karne za mwanadamu kuingia kwenye meza mapapa waliokuwa nyuma
kizani. Na rekodi yao ilikuwa mbaya zaidi, kinyume na maagizo ya Injili pale
walipojaribu kuwalazimisha watu kuikubali "kweli" kwa nguvu."
(uk.210).
Kwa mujibu wa de Rosa, kila wakati na kwa makarne, kanisa katoliki
limekuwa likitangaza kwa majivuno itikadi yake ya kutovumiliana katika dini.
"Papa baada ya papa wamekuwa wakishambulia uhuru kwa... ukali...
walionyesha kuogopa kuwa serikali ya watu, inapoendeshwa na watu, kwa ajili
ya watu ingetokezeshea madai hayo hayo kwenye kanisa. Gregory wa XVI, kwenye
Mirari Vos ya 1832 aliuelezea uhuru wa tashi ya nafsi (consiceince) kuwa ni
wazo la wehu; kiwendawazimu.
Uhuru wa dini umeelezewa kutokana na chemchemi yenye harufu ya
uozo wa kutokujali. Alilaani na kukuelezea uhuru wa ibada, vyombo vya habari,
kukusanyika pamoja na elimu, kama mfereji wa maji machafu uliojaa
"matapishi ya uzushi." Pius wa IX... kwenye Quanta Cura mnamo mwaka
1864... aliushambulia uhuru wa dini na akaulinganisha na uhuru wa kifo.
Miongoni mwa mapendekezo aliyoyalaani katika barua yake ya
kichungaji "Syllabus of Errors" mojawapo lilikuwa hili. Siku hizi
si busara tena kwamba dini ya kikatoliki iwe ndiyo dini pekee ya taifa kwa
kuzibagua na kuziacha aina nyingine zote za ibada. leo XIII... Katika nyaraka
zake za kichungaji moja baada ya nyingine... aliuelezea uhuru wa dini kwa
mitizamo ya zama za "medieval".
Kanisa lina haki ya kuwa na ukiritimba wa dini kwenye taifa
lolote la kikatoliki. Kwa hiyo makanisa yasipewe uhuru wa kujisambaza. Uhuru na
kweli havipatani. Kweli lazima isimamiwe na taifa kwa amri ya kanisa kila
inapowezekana. Kila taifa... lazima lichukue imani ya kweli kuwa ndiyo sera
yake rasmi na kuvumilia uhuru wa tashi za nafsi kwa kisai kidogo iwezekanavyo
na kwa muda mfupi kabisa kama iwezekanavyo."
Lazima isisitizwe kuwa hizi si itikadi tu za mapapa wa karne ya
19. Ni itikadi zinazowakilisha mfumo mzima wa mawazo ya uongozi wote wa
kanisa katoliki hata katika zama zetu hizi. Hata leo, aina fulani za uhuru ni
ngeni kwenye imani ya kikristo. Kwa mujibu wa mawazo ya papa John Paul II
kwake yeye kweli ya ukatoliki ni kweli tupu na utii kwa kweli hii ni lazima
ya kufa na kupona. Yeye, kama msemaji mpakwa mafuta wa Mungu; ana lazima ya
kutaka utii wa papo kwa papo na usio wa kusitasita kutoka kila mtu, kutoka
mdogo wa chini kabisa mpaka mwana teolojia wa kiwango cha juu kabisa.
Ni muhimu isisahaulike kuwa kanisa katokiki ni jumuiya ya dini
pekee duniani leo ambavyo ni kanisa na wakati huo huo ni jumuia ya
kisiasa. Hii ndiyo sababu kwa nini kanisa hili pekee baina ya makanisa yote
linalobadilishana wawakilishi wa kibalozi na linachukua hadhi ya mwanachama
huru wa jumuiya za mataifa. linafanya hivi sio kama taifa dogo la Vatican,
bali kama jumuiya ya kidini iliyozagaa kila pahali duniani. Hii ndiyo sababu
kwa nini, kwa mfano kadinali Pengo, mmojawapo wa washauri wa Papa wa Roma ana
uraia na pasipoti za nchi mbili, uraia wa Taifa la Vatican na Taifa la
Tanzania.
Vile vile ni muhimu kukumbuka kuwa kwa karne baada ya karne
kanisa katoliki ndilo lililokuwa mbele katika utawala. Liliweza kuingilia
mambo ya utawala wa kila nchi kila lilipotaka. Pius wa X alisema tarehe 9
November 1903.
"Tutawakasirisha watu wengi tunaposema kwamba ni muhimu
kwetu kujishughulisha na siasa. Lakini kila anayelihukumu suala hili kwa haki
lazima atambue kuwa Papa mwenye mamlaka, aliyepewa na Mungu Hukumu ya Juu,
haina haki ya kutenganisha mambo ya kisiasa kutoka uwanja wa imani na
maadili," (uk.195, Vicars of Christ).
Hivyo, kwa mujibu wa leo XIII, kisiasa, "kila siku ni jambo
la haraka bali ni wajibu wa kwanza kufikiria njia bora za kutumikia na
kuendeleza masilahi ya ukatoliki." Katika kila uchaguzi "Wakatoliki
wanawajibika kuwapigia kura wale ambao wanaahidi kuendeleza masilahi ya
ukatoliki na kamwe usimchague mwingine asiyependa dini (ya kikatoliki) badala
yake." De Rosa amesema kuwa kwa mujibu wa amri ya papa, kuna kura ya jumla,
kura ya jumla ya wakatoliki kwa ajili ya wagombea wa kikatoliki; na
kushambulia ukatoli ni shambulio juu ya ukatoliki tu.
Baada ya vita vya Dunia ya II Papa Pius wa XII alikuwa tayari
kumfukuza mkatoliki yeyote kwenye kanisa ambaye alimpigia kura Mkomunisti
badala ya mkatoliki (uk.208, Vicars of Christ').
Wasomi wanaona kuwa kuongezeka kwa amri za uongozi wa kanisa za
kuzuia itikadi za kanisa kufanyiwa uchunguzi na jinsi wanavyoogopa uhuru
kunatokana na kuongezeka kwa elimu duniani na maendeleo yaliyopatikana kwenye
taaluma ya uchimbaji, ugunduzi na utafiti wa mambo ya kale kwenye karne ya
19, hasa hasa mchango wa taaluma hii katika uchunguzi wa maandishi (Scrolls)
ya Nagi Hammadi yaliyogunduliwa Misri mwaka wa 1945 na maandishi ya bahari ya
(Daad Sea Scrolls) yaliyogunduliwa kwenye mpango ya Qumran mwaka 1947 na
1956. Baada ya hapa ilikuwa ni suala la muda tu kabla maandiko hayo kufikia
zamu yake ya kufanyiwa uchunguzi wa kina - kuitenganisha kweli kutoka ngano.
Labda mtu muhimu sana katika kazi hii ya kuhoji kweli halisi ya
mafundisho ya ukristo alikuwa mtaalamu wa dini na mwana historia wa kifaransa
Ernest Renaa, ambaye kitabu chake "The life of Jesus Christ"
kiliondoa ufumbo-fumbo katika ukristo. Kitabu hiki kilimuonyesha yesu kama
"mtu asiye na mfano wake," kiumbe mwanadamu halisi asiye na sifa
yoyote ya Uungu. Kitabu cha Renan kilibadilisha mtazamo wa watu juu ya
taaluma ya uchunguzi wa Biblia kabisa.
Kwenye kitabu chao "The Dead See Scrolls Deception
"(Supra), Baigent na Leigh wanasema yafuatayo kuhusu jinsi kanisa
katoliki linavyolichukulia suala la uchunguzi wa itikadi za kikatoliki.
"Ikiandamwa na mashambulizi kutoka sayansi, kutoka falsafa, kutoka `Art'
na kutoka serikali zisizo dini, Roma ikawa haijapata kutingishwa namna hiyo
wakati wowote tangu mwanzo wa mageuzi yaliyofanywa na Luther ... Ikachukua
hatua kadhaa za pupa ya mfa maji kujihami".
Mojawapo ya hatua hizo ilikuwa kutangazwa kwa itikadi ya papa
Asiyekosa (Papal Infellibility) na Papa Pius IX tarehe 18 July 1870. Hatua
nyingine ilikuwa kuanzishwa kwa umoja wa kileo wa kikatoliki wa wasomi
wateule waliopewa jukumu la kupambana na wapizani wa ukatoliki. Kizazi cha
wasomi wa mambo ya dini kilichofundishwa kwa uangalifu na kutayarishwa kulipatia
kanisa kikosi kilichoundwa maalumu kuihami kweli halisi ya maandiko.
Hata hivyo, kwa mujibu wa baigent na Leigh, kwa huzuni na
masikitiko, Roma ikaona kuwa mpango wao unawarudia wenyewe. Kadri
walivyojaribu kuwapatia mapadri hao vijana silaha zilizohitajika kwa
mapambano kwenye majukwaa ya malumbano ya kileo ndivyo kadri mapadri wao hao
hoa walivyoanza kukimbia kazi waliyotayaishiwa.
Uchunguzi wa kutafuta kweli halisi wa Biblia ukachimbua chungu
nzima ya khitilafu, makosa na matokeo ambayo yalikuwa ya hatari kwa itikadi
za Roma. Wataalamu wa kileo wenye haraka wakaanza kuhoji na kuyachimba chini
chini yale waliyokuwa wanatazamiwa kuyalinda. Bila ya shaka, kanisa katoliki
likalazimika kukigeuka chombo lilichokianziasha na kukitunza.
Hivyo mwaka 1903 Papa leo XIII akaunda Tume ya Papa ya Biblia
(Pontifical Biblical Commission) kusimamia na kuangalia kazi ya wasomi juu ya
maandiko ya kikatoliki. Mwaka 1904 Papa Pius wa X akatoa barua mbili za
kiuchungaji zilizopinga kazi za kisomi zote zilizohoji asili na historia ya
mwanzo wa zama za ukristo. Walimu wote wa kikatoliki walioshukiwa kuwa na
"mawazo ya kileo" wakafukuzwa mara moja kutoka kazi zao.
Kanisa katoliki liliuchukulia uchunguzi juu ya itiakadi za
kiroma kwa ukali mno kiasi kwamba Antonio Fogazzaro, mkatoliki mleli maarufu
wa Italy, alilazimika kusema kwenye kitabu chake "The Saint (London
1906) kuwa "Kanisa Katoliki, likijiita lenyewe chemchemi ya kweli, leo
linapinga utafutaji wa kweli pale misingi yake vitabu vitakatifu, miundo ya
itikadi zake, kutokufanya makosa kunakosemwa, inapokuwa ndiyo walengwa wa
utafiti. Kwetu sisi, hii inaashiria kuwa halijiamini tena.
Kitabu cha Fagazzaro haraka sana kikawekwa kwenye orodha ya
"Inquisition" ya vitabu vilivyopigwa marufuku. Mnamo July 1907
makao makuu Roma ikatoa amri iliyolaani hatua za wenye mawazo ya kileo za
kuhoji itikadi za kanisa, kutokukosea kwa papa na kweli ya kihistoria ya
maandiko ya Biblia.
Mnamo Septemba 19907 mawazo ya kileo (modernism) yakatangazwa
kuwa ni uzushi na shughuli zake zote zikapingwa marufuku. Mwaka 1910
ilitolewa amri iliyowataka wakatoliki wote walijishughulisha na kufundisha na
kuhubiri kula kiapo kukana "makosa yote ya mawazo ya kileo". Idadi
kadha ya mwaandishi wa kileo wakafkuzwa kanisani. Wanafunzi kwenye seminari
na vyuo vya tekhnolojia walikatizwa hata kusoma magazeti.
Kwa mujibu wa msomi muisilamu syed Abul A'ala Maududi kwenye
kitabu chake West versus islam" (1991, International islamic Publisher,s
New Delhi) mapambano haya kati ya kanisa na wateteaji wa uhuru wa mawazo
yalikuwa ni matokeo ya upinzani usio na mantiki wa upapa kiupofu upofu
wakifuata falsafa za kale na zilizokwisha makali za kigiriki kama ndio msingi
wa imani yao.
Kanisa lilihofu kuwa mashinikizo ya dini yao yataporomoka chini
kama utafiti wa kisayansi maeneo na magunduzi yake yatakubaliwa. utovu huu wa
kutokuelewa ulilipelekea kanisa na hata kutumia maguvu ya kinyama dhidi ya
nadharia mpya za kisayansi ugunduzi mpya. Waliunda "inquistion" na
wanasayansi, wagunduzi na wanafalsafa wakapewa adhabu za kinyama na za
kutisha lakini haikuwezekana na kuifuta kabisa kazi hii na ikaongeza nguvu na
kasi kwa sababu ilikuwa mwamko wa kweli.
Kufurika kwa uhuru wa mawazo huku mwishowe kukafutilia mbali
mamlaka ya Papa na uongozi wa kanisa juu ya watu. Vita hivi kati ya mawazo
huru ya maendeloe na dini au ukristo vilikuwa ndio mwanzo wa mtindo wa
kutoamini Mungu; wa uanadharia na wanafalsafa wakiwa wapingaji wakubwa wa
kila wazo la mamlaka ya Mungu, Mungu na mambo ya kiroho si kwa mantiki au kwa
matumizi ya akili, bali kutokana na upinzani wa kanisa dhidi ya mtindo wa
utafiti wa kisayansi na uhuru wa mawazo."
Kwa hiyo bila ya kuwa na habari ya uharibifu matokeo ya uzuiaji
wao unaomfanyia uhuru wa kujieleza na dini, hasa hasa katika kuwakimbiza
wataalamu na wasomi mbali na dini na labda bila ya kujali bali
waking'ang'ania tu kushika mamalaka juu ya kutafasiri maandiko, ungozi wa
kanisa katoliki unaenelea kuziba vinywa na kuzima kuhoji na utafiti wa kisomi
wa Biblia.
Kwa mujibu wa New Catholic Encyclopedia (Vol.XI) kazi rasmi ya
tume ya kipapa ya Biblia iliyoundwa na Papa leo III mwaka 190-3, ni
kujitahidi kwa uanglaifu wote unaowezekana kuwa maneno ya Mungu yatakingwa,
siyo tu kutoka kila pumzi ya makosa, bali hata kutoka kila wazo la
upinzani," na kuhakikisha kuwa wasomi "wajaribu kulinda mamlaka ya
kuandika na kuendeleza tafsiri yake ya kweli. Hivyo, kwa mfano, Tume
intangaza amri rasmi juu ya njia sahihi za kufundisha maandiko. Hivyo, ka
mfano, Tume imeweka" kwa amri kuwa Musa ndiye aliyekuwa mwenyewe mwandishi
wa kumbukumbu la Torati! mwaka 1909 amri kana hiyo ikasisitiza uhakika wa
mandishi na historia ya sura tatu za kwanza na kitabu cha mwanzo. Na tarehe
21 April 1964 Tume ikatoa amri iliyohusu usomi juu ya Biblia kwa jumla, na
hususan juu ya "kweli ya kihistoria ya Injili. Amri hii haikuuma uma
maneno ilisema kuwa "kwa muda wote mtafsiri lazima aweke ndani yake azma
ya utii bila kusita kwa mamalaka ya kanisa juu ya mafundisho.
Ni muhimu kuzingatia kuwa mkuu wa Tume ya papa ya Biblia vile
vile ni mkuu wa Kamati ya itikadi za Imani (Congregation for the Doctrine of
the Faith) kabla ya hapo ikiitwa Ofisi Takatifu (The Holy office) na kabla ya
hapo ikiitwa the Holy Inquisition." Kwa hiyo mkuu wa vyombo hivi viwili
vya kikatoliki ndiye kwa kweli mtesaji mkuu (Girand Inquisitor) wa kanisa
katika zama zetu hizi. Mwezi June mwaka 1971 vyombo viwili hivyo
viliunganishwa na Papa Paul VI karibuni kwenye kila kitu isipokuwa jina.
Kwa mujibu wa Baignet na Leigh, Mkuu rasmi wa kamati ya itikadi
za Imani siku zote ni Papa aliye madarakani na metenaji Mkuu wa Kamati hii
leo anaitwa katibu wake lakini katika zama za kale alikuwa anaitwa mtesaji
mkuu (Grand Inquisitor). Kamati hii ndiyo chombo chenye nguvu kuliko idara
nyigine zote za makao makuu ya Vatican (Roman Curia).
Mapadri chungu nzima wa siku hizi, na wahubiri, walimu na
waandishi wamezibwa vinywa kufukuzwa au ametolewa kwenye kazi zao na kamati
hii katika walioathirika walikuwamo wasomi wanateknolojia waliokuwa maarufu
na hoadari sana kwenye kanisa leo, kwa mfano Father Edward Schillebeck wa
Chuo Kikuu cha Nigwegea nchini Holland, ambaye kitabu chake "Jesus: An
Experiment in Chrstology (1974) kilionekana na wapinzani wake kuhoji kweli ya
kufufuka kwa Yesu na kuzaliwa na Bikira. Mwingine alikuwa mwana teolojia
maarufu wa Kiswiss, Dr. Hans Kung aliyehoji itikadi ya papa asiyekosa na pia
akahoji msimamo mgumu wa Papa John Paul juu ya maadili na itikadi.
Tarehe 18 Desember 1979, John Paul, kutokana na ushauri rasmi wa
kamati, akamvua Kung nafasi yake ya ukuu wa idara ya Dini kwenye chuo kikuu
cha tubngen na akamtangaza kuwa hafai tena kufundisha itikadi za Roma. Kwa
maneno yako mwenye Kung juu ya yale yaliyomsibu, "Nimehukumiwa na papa
ambaye ameyakataa maoni yangu juu ya teknolojia bila hata ya kusoma hata
kitabu changu kimoja na ambaye siku zote amekuwa akikataa kuniona. Ukweli wa
mambo ni kua Roma haisubiri mjadala; inasubiri utii." (Sunday Times
London 2, December 1984).
Baigent na Leight wanasema kuwa kamati hii, chini ya uongozi wa
Kadinali Joseph Ratzinger, katibu wake tangu 1981, imekuwa ikijichimbia
mizizi zaidi, na isiyokubali mabadiliko, ikijitahidi wakati wote kurudi
kwenye ukatolki wa siasa kali na kung'anga'niza kweli ya maandiko kama
inavyofasiriwa na itikadi zilizowekwa na Papa.
Mwezi Mai 1990 kamati ilitoa mswada wa katekisima ya Kanisa
katoliki kwa wote (Universal Catechism of the Catholic Church) mpya,
iliyopitiwa upya na ya kileo - miundo rasmi ya imani ambazo wakatoliki
wanawajibika kuziamini. Kwenye bara moja inayosisitiza itikadi katekisma mpya
inaamrisha kuwa "kazi ya kutoa tafsiri sahihi ya neno la Mungu imewekwa
kwenye ofisi hai ya mafundisho ya kanisa peke yake."
Mwezi June 1990 kamati ikatoa waraka mwiengine uliandikwa na
Kadinali Ratzinger mwenyewe na kukubaliwa na kuungwa mikono na papa mwenyewe.
Kwa mujibu wa waraka huu wanateknolojia wa kikatoliki hawana haki ya kupinga
chochote katika mafundisho ya kanisa, upingaji ukiwa umepewa hakumu ya
dhambi.... utovu wa imani kwa Roho Mtakatifu." Kwenye waraka huo huo,
kadinali Ratzinger anasema:
"Uhuru wa tendo la imani hauwezi kuhalalisha haki ya
kupinga. Uhuru huu hauingizi uhuru kwenye masuala ya kweli, bali unaingiza
uamuzi wa mtu wa imani kukubaliana na majukumu yake ya kimaadili hikubali
kweli.
Baigent na Leigh wansema kuwa haya ni maelezo ya ajabu juu ya
uhuru. maana haki kamili ya kukubali mafundisho ya kanisa, lakini hawezi
kuhoji au kuyakataa. Uhuru hauwezi kudhihirishwa na kutamkwa ila kwa
kukubali.
Baigent la Leigh wanamaliza kwa kusema kuwa pingamizi hizi ni za
kinyama hata zikilazimishwa juu ya wakatoliki peke yao - za kinyama kwa kiasi
cha madhara zitakazosababisha, madhara ya kisaikolojia na kihisia. Hisia za
kujiona wakosaji, za utovu wa uvumilivu na ukatili utakaojitokeza, maeneo ya
elimu na kuelewa mambo yakatayozuiliwa kufikiwa. Pingamizi hizi zinapohusu
imani huwa zinawafunga wale tu ambao kwa hiari yao wanakubali kuzifuata; na
jumuia za walimwengu ambao si wakatoliki ziko huru kuzipuuza.
Hii, kwa hiyo, kwa kifupi, ndiyo falsafa na mfumo wa mawazo
unaotawala mwenendo wa viongozi wa kanisa katoliki jinsi anavyoyaingia na
kuyachukulia majadiliano yoyote juu ya itikadi za kanisa. Natamka kuwa kwa
sababu kanisa katoliki linahimiza utii wa kipofu, kukubaliana na kila kitu na
utii wa kitumwa kiasi hiki kwa wafuasi wake, haliwezi kuaminiwa kuwa
litakaribisha mijadala na waisilamu, wacha kwamba waisilamu wawambie
wakatoliki kuwa viongozi wao wanakosea na wanawapoteza kutokana na dini yao
ya kikristo.
Na hiki ndicho kiini cha mambo kwa kisi kile uhuru wa kueneza
dini nchini Tanznaia unavyohusika. Tanzania ni nchi isiyo na dini na siyo
nchi ya utawala wa dini ya kikatoliki kwa hiyo suala la uongozi wa kanisa
katoliki kuwataka wasiokuwa wakatoliki kufuata tafsiri za kanisa katoliki juu
ya itikadi za kanisa halipo. Wasiokuwa wakatoliki, pamoja na waisilamu, wana
haki ya kuhoji uhalali au kweli ya itikadi hizo. Hii ni haki ya msingi
iliyotolewa na Mungu na haina mjadala. Mradi tu kuhoji huku kunatokana na
dhamiri ya kweli ya kupata kweli ya maandiko, na hakujiingizi kwenye makosa
ya jinai kwa kutumia matusi, wote; viongozi wa kanisa katoliki na serikali,
wanawajibika kikatiba kuiheshimu haki hii.
Kwenye ibara zilizotanguali nimeonyesha kuwa kwa mujibu wa
sheria za Tanzania mihadhara ya waisilamu si ya kukufuru - au ya matusi ya
kashfa kama inavyoelezwa na viongozi wa kanisa katoliki, serikali na vyombo
vya habari vya nchini. Nimeonyesha pia kuwa ulikuwa ni uongozi wa kanisa
katoliki ulioichochea serikali ya CCM kuchukua hatua dhidi ya waisilamu na
wahubiri wa kiisilamu.
Lililobaki kutazamwa sasa ni kama uamuzi wa seirkali ya CCM wa
kuchukua hatua hizi ulikuwa halali kisheria au ni uingiliaji wa moja kwa moja
wa uhuru wa waisilamu kueneza imani yao.
Lazima ikumbukwe kuwa jumiya ya watu huru kweli ni ile inayoweza
kuwa jumuiya ya watu wenye imani mbalimbali nyingi. Jumuiya huru ni ile
inayolenga kwenye usawa wa kufaidi haki na misingi yote ya uhuru. kwa hakika
uhuru lazima ujengwe kwenye kuheshimu haki ya kuzaliwa na haki za asili
alizonazo mwanadamu.
Lazima ikumbukwe pia kuwa kiini cha dhana ya uhuru wadini ni
haki ya mtu kuwa na imani za dini kama mtu atakavyo haki ya mtu kutangaza na
kujieleza imani yake hadharani na bila ya woga wa kuzuiwa au kisasi, na haki
ya kudhihirisha imani za dini kwa ibada na matendo ya ibada au kwa kufundisha
na kueneza.
Lakini dhana hii ni zaidi ya hvi. Kimsingi uhuru unaweza
kuelezewa kuwa ni kutokuwapo kulazimishwa au kubanwa. Kama mtu analazimishwa
na serkali, au amri ya mwingine kufanya au kutofanya jambo ambalo kama
isingekuwa hivyo asingechukua hatua hiyo, mtu huyo hafanyi kwa khiari yake
mwenyewe na hawezi akaambiwa kuwa yuko huru kweli.
Mojawapo ya madhumuni makubwa ya katiba ni kulinda, bila ya
sababu watu wasilazimishwe au wasizuiliwe kulazimisha siyo tu ni pamoja na
vile vitendo vya wazi wazi vya kulazimisha kama amri za moja kwa moja za
kufanya au kujizuia kufanya mambo kwa vitisho vya adhabu; kulazimisha
kunajumlisha namna nyingine za kudhibiti; zinazoshawishi au kuzuia njia
nyingine za uamuzi watu wanazoweza kuzichukua. Kwa maana yake pana uhuru
unabeba vyote, kutokuwapo kulazimisha na kuzuia na haki ya kudhihirisha imani
na matendo.
Uhuru maana yake ni kwamba, bila ya kuathiri mipaka iliyo ya
lazima kuwapo kwa ajili ya kulinda usalama wa jumuia, utulivu au maadili au
haki za msingi za wengine, hakuna atakayelazimishwa kufanya mambo kinyume na
imani zake au tashi za nafsi yake.
Kwa mujibu wa katiba, Tanzania ni taifa lisilokuwa na dini, hata
kama dhana hiyo inachukiza sana kwa baadhi yetu kwa kuwa ni dhana ya
"Freemason" yenye dhamiri za "kumondoa" Mungu katika
maeneo yote ya maisha ya jumla ya uma na kuiachia dini eneo la mas-ala ya mtu
binafsi tu.
Imesemwa kuwa "Taifa lisilo na dini ni taifa
linalohakikisha kuwapo kwa uhuru wa dini kwa mtu binafsi na kwa watu wote
jumla, linamshughulikia mtu kama rais bila ya kujali dini yake, kikatiba
haikai upande wa dini yoyote wala haitafuti kuendeleza ua kuingilia dini
"(D.e. Smith - "india as a Secular State," Princeton Univ.
Press, 1963).
Taifa kutokuwa na dini kwa hiyo, linamaanisha kuwapo kwa
mchanganyiko wa mambo kadha - dini kutojiingiza kwenye siasa, taifa kutoibeba
jumuiya yoyote ya dini; kutokuwapo kwa miendano ya upendeleo wa kidini;
kutokuwapo kwa kuwabagua na kuwaweka kando watu wengine kwa misingi ya dini;
kusiweko na ubaguzi kwenye elimu, biashara au ajira kwa misingi ya dini, na
kadhalika.
Kimsingi, taifa lisilo na dini linaiona jumuiya kuwa ni ya
mchanganyiko wa dini na tamaduni na muda wote linajiahidi kujenga umoja na
mshikamano. Haitoshi kwa serikali kujisemea tu "haina dini", lazima
ijitahidi kuyafikia malengo haya na lazima ionekana kuwa kweli haina dini.
Tukio la Mwembechai linathibitisha madai ya wasilamu ya
kuvunjika kwa mshikamano wa kisekula nchini Tanzania. Kutokujali kupuuza na
kujihusisha kulikotokea kwa viongozi wa serilai ya CCM, pamoja na Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Polisi (Taifa) Mkuu wa
Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, katika juhudi zao za haraka haraka za
kuridhisha matakwa ya uongozi wa kanisa katoliki ya kuzuia uhuru wa dini wa
watu wengine kumetuwekea misingi ya kuamua kuwa sera za kisekula za nchi
zimesahauliwa.
Polisi waliua na kuwatia vilema waisilamu na wakawapiga kinyama,
na kuwatendea mambo ya kinyama waisilamu na raia wengine wanyonge. Kwa kweli
polisi na kikosi cha kuzuia fujo walionekana kufanya kazi yao kama jeshi lililotayarishwa
na kupewa silaha maalumu kwa kazi ya kuwadhalilisha na kuwaua waisilamu na
"wamachinga. Kwa kweli mauaji yale na uumizaji ule utakumbukwa kenye
historia ya Tanzania kama mfano usiomithilika wa ukatili na unyama uliofanywa
na polisi.
Kwa hakika, kutokana na matukio ya Mwembechai na matukio mengine
yanayohusiana nayo, kuna Watanzania wengi - Waisilamu na waisokuwa waisilamu
ambao sasa wanaona kuwa usekula wa Tanzania ni matamanio tu; uongo na si
kweli. Maana, wacha serikali ya CCM kukubali wazi wazi wa uongozi wa kanisa
katoliki uisukume mpaka kufikia kuwatendea waisilamu mambo ya kinyama bila
kukumbuka kuwa umoja wa mataifa na sera za serikali za kisekula vilikuwa
vinawekwa hatarini vile vile kuna ishara nyingine zinazoashiria khatima
mbaya, yaani kutokuwapo kabisa kwa hata kauli za rambirambi za maneno ya
kuwafariji wale waliofiwa na ndugu zao kutoka kwa Raisi, ikiashiria kuwa
serikali ya CCM imeridhika na mauaji ya raia wasio na hatia kana kwamba
walikuwa wahalifu wa kawaida (hata wahalifu wa kawaida wanastahili kutendewa
haki); serikali ya CCM kukataa, kwa kiburi, wito wa Waisilamu wa kuunda Tume
ya uchunguzi huru ya kuchunguza mauaji ya Waisilamu waliouliwa na polisi
Mwembechai, ujumbe wa Waziri Mkuu Frederick Sumaye wa kumpongeza kadinali Pengo
tarehe 19 January 1998 (Daily News' 20 January 1998) kwamba serikali imeunga
mkono kuteuliwa kwake kuwa kadinali na kumhakikishia kuwa serikali inamuunga
mkono kwenye majukumu yake peke yake linatia hofu kwenye taifa ambalo ni la
kisekula, linatia hofu zaidi kutokana na yale yaliyofuatia; ziara za wazi
wazi za Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwenye makanisa na misikiti kama
watendaji wa serikali na kutumia nafasi hizo za shughuli za kidini kutoa
kauli za kiserikali za kisekula; serikali ya CCM kukataa na kusita kusajili
jumuiya za kiisilamu na dini nyingine na tishio lake la kuzifutia usajili
bila ya sababu halali; tamko la Makamu wa Rais Bw. Omari Ali Juma, kuwa
serikali ya CCM inalitambua BAKWATA kama ndio chombo pekee rasmi cha
Waisilamu na kukataa kuwa baadhi ya shule kuwaruhusu wanafunzi wa kike kuvaa
vazi linaloagizwa na dini yao (sawa sawa na wafanyavyo masista wa kiroma na
masingasinga kwenye shule hizo hizo). Orodha haina mwisho.
Lazima isisitizwe kuwa yote haya yanafanywa bila ya kujali maagizo
ya katiba. Na yanafanywa na serikali ya CCM ambayo inahesabiwa kuwa ni ya
kimaendeleo, iliyoanza kipindi chake cha utawala na ahadi za kuendeshwa na
katiba, utawala wa sheria, ukweli na uwazai.
Ni jambo la kuzingati kwa hiyo, kuwa, maadamu Tanzania ni taifa
lisilokua na dini serikali ya CCM ingelishughulikia suala la mihadhara ya
waisilamu kwa uangalifu. Kwa kutambua umuhimu wa uamuzi wake juu ya suala
linalohusu uhuru wa dini, na ikijua kuwa Tanzania ina sheria na mahakama
inaweza kushughulikia malalamiko yaliyotolewa na uongozi wa kanisa katoliki,
serikali ya CCM ingechukua msimamo wa kukalia kiti na kukataa kuingilia,
ikiacha sheria ifanye kazi yake. Hii hasa ni kwa sababu muda wote huu
kulikuwa hakujatokea hata mara moja mihadhara ya waisilamu ikisababisha
ungomvi au kuvunjika kwa amani.
Ninaposema kuwa seirkali ingelikaa kando bila ya kuingilia na
kuiacha sheria ifanye kazi yake sina maana hata mara moja ya kupendekeza kuwa
serikali ingejitoa kabisa. Ikumbukwe kuwa kabla ya tamko la Raisi la tarehe 4
januari l,1998 huko Tabora, serikali ilikuwa ikiyaacha mambo haya
yashughulikiwe na mkondo wa sheria. Tangu mwaka 1993 wahadhiri wa Kiisilamu
wamekuwa wakikamatwa na kushitakiwa mara kwa mara.
Kwa hiyo hakuna suala kuwa serikali haikuwa inajishughulisha na
kushitakiwa kwa wahubiri wa kiisilamu kwa madai ya kutukana ukristo. Hata
hivyo katika kuihimiza serikali ya CCM ikiri nataka tu kusisitiza kuwa suala
la mihadhara ya waisilamu, jambo linaohusu msingi wa uhuru wa waisilamu wa
kuabudu na kueneza dini yao, lilipotoshwa kwa makusudi kwa mpango wa kutoa
taarifa za uongo uliotayarishwa maalumu na kutekelezwa kwenye kampeni
iliyoendeshwa na uongozi wa kanisa katoliki.
Lilikuwa ni jambo la lazima kwa hiyo, kwa serikali inayotakiwa
siku zote kuwa msuluhishi aliyeegemea upande wowote, ikijiweka mbali na
upendeleo wa kidini na udini, kuchukua hatua kwa mujibu wa katiba ya Tanzania
isiyo na dini. Kwa hiyo ilikuwa ni muhimu sana, jambo la busara, kwa serikali
ya CCM kuliingilia suala hili kwa uangalifu wote uliohitajia.
Lakini hata kama tukichukua kuwa serikali ilazimika kuchukua
hatua kwa sababu hali ilikwisha kuwa ya vurugu (jambo ambalo si kweli na
seirkali ilikuwa hairidhiki na jinsi utaratibu wa sheria ulivyokuwa
unayaendesha masuala ya mihadhara, bado serikali ilikuwa na nafasi ya kutumia
njia nyingine halali na inayofaa ambayo ingeweza kutimua mazungumzo.
Rais Mstaafu Mwinyi alijaribu njia hii mwaka 1993 alipoitisha
mkutano Ikulu baina ya maaskofu na masheikh kuzungumza na kuyatafutia
ufumbuzi malalamiko ya uongozi wa kanisa katoliki. Mazungumzo haya
hayakufanikiwa kwa sababu viongozi wa kanisa walishindwa kuleta ushahidi wa
malalamiko yao waliyoahidi kuleta dhidi ya hoja za mihadhara ya Waisilamu.
Lakini hivi hivi tu, kwa sababu zisizojulikana Rais Mkapa
mwanadiplomasi aliyeiva, mwenye uzoefu wa siku nyingi kwa masuala ya matatizo
ya migongano ya kimataifa, alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, hakutaka
kujishughulisha kabisa na njia hii ya kutatulia migongano kwa mashauriano,
njia ya maana kweli kweli ya kujiepusha na magomvi hasa hasa kenye suala kama
hili linalohusu kutokubaliana kati ya dini. ka kweli kuna wasiwasi mkuba kama
Rais Mkapa hata alikuwa na dhamira hasa ya kutumia mazungumzo kama njia ya
kulitafutia ufumbuzi suala la mihadhara ya waisilamu.
Tunasema kuwa serikali nzuri yenye kuona mbali ingeliyatambua
mapema matokeo ya kutumia nguvu kuzuia mihadhara ya waisilamu. Serikali ya
haki na yenye kujali, kabla ya kutoa uamuzi au kuchukua hatua dhidi ya
mihadhara ya waisilamu, ingeita mazungumzo na wote waliohusika - walalamikaji
(uongozi wa kiisilam).
Mazungumzo kama haya, ambamo kila upande ungepata nafasi ya
kuelezea upande wake, yangeipatia serikali njia ya kuepusha mapambano ya aina
kwa ana na kwa hiyo kujiepusha na hali iliyojitokeza sasa ambapo, kwa haki
kabisa, serikali ya CCM inahesabiwa kuwa ni mshiriki mwenza katika sera za
uongozi wa kanisa katoliki za kuzima haki na uhuru wa dini kwa watu wengine.
Mazungumzo na kushauriana kungeipatia serikali taarifa muhimu
kabla ya kujiingiza kwenye maeneo mapya ya kuingilia uhuru wa waisilamu wa
kutangaza dini yao. Ni muhimu kukumbuka kuwa siku zote ni rahisi kufanya
mabadiliko kwenye hatua ya uamuzi kuliko badaye.
Badala yake, sasa serikali ya CCM, baada ya kuyaharibu mambo,
inalazimika kushughulika na kazi ya kudhibiti uharibifu, ikilazimika pia
kusaka vijisababu chungu nzima ikiwa ni pamoja na kusaka wachawi. Mara,
"wenye siasa kali" ndio walisababisha vurugu za Mwembechai. Mara,
ni nchi za kigeni (za kiisilamu) na balozi za nje.
Wakati mwingine ni wafanya biahara wa humu humu nchini. Au ni
vyama vya upinzani. Tena, wasaliti wa ndani ya CCM, n.k. Sababu na dharura za
kila aina hutolewa kuhalalisha hatua zilizochukuliwa na serikali ya CCM.
Hakuna kujirudi kabisa, na kutafuta miongoni mwao wenyewe waone nini
kiliharibika.
Iwe iwavyo ni muhimu kuzingatia kuwa Mheshimiwa Rais Mkapa
hajatoa tamko lolote hadharani kuonyesha ameisimamia wapi kuhusu mazungumzo
na mashauriano. Lakini yeye ni Mwenyekiti wa kamati |Kuu na Halmashauri Kuu
za CCM (NEC na CC).
Kamati hizi mbili za Chama, mara mbili, kila moja kwa wakati
wake, ziliipongeza serikali ya CCM kwa jinsi ilivyolishughulikia suala la
mihadhara ya waisilamu. Na tunajua kuwa kwa sababu ya utaratibu wa CCM wa
uhuru wa kushika hatamu kamati zile mbili za chama wajumbe wake ni pamoja na
karibu mawaziri wote wa serikali. Suala la kujipoongeza' au kujipigapiga
mwenyewe mgongoni.
Kuna sababu, kwa hiyo, ya kuchukuliwa kuwa Rais Mkapa hana haja
ya kutumia mazungumzo na kushauriana kama njia ya kupatia magomvi ufumbuzi.
Kwa bahati mbaya sana, kwa hiyo, serikali imeikosa nafasi ya kupata ufumbuzi
wa suala hili kw amani na kikamilifu. Maana kwenye mazungumzo haya kweli
ingeonekana na serikali ya CCM ingekuwa na udhaifu wa madai ya viongozi wa
kanisa katoliki.
Kama nilivyosema hapo mwanzo, Tanznaia ina sheria malumu na
mahakama zinazoshughulikia aina ya malalamiko yaliyotolewa na uongozi wa
kanisa katoliki. Hakujatolewa madai kuwa sheria hizi hazifai au kwamba
mahakama zimeshindwa kushughulikia kesi za `kashfa' walizopelekewa. Badala
yake utaratibu wa kushughukia kesi za jinai uliopo unatosheleza kabisa
malalamiko yote yaliyotolewa na viongozi wa kanisa katoliki kusghuulikiwa
nazo.
Dosari pekee inayoweza kujitokeza ni uzembe wa polisi wa
kutofuata taratibu wakati wa kukamata washukiwa na kutotoa haki sawa sawa
kunakofanywa na waendesha mashitaka na mahakimu kwa kuwakatalia dhamana
wahadhiri wa kiisilamu kwa sababu zisizo na msingi. Itasaidia kuonyesha kwa
kifupi sheria na taratibu zenyewe:
1. Kifungu 19(2) cha katiba kimeweka uhuru wa kueneza dini, bila
ya kuathiri sheria zianzohusika.
2. Kifungu 129 cha sheria za Jinai limeweka kinga ya makosa
kwenye uhuru wa kueneza dini kwa kulifanya kosa kutamka maneno kwa dhamiri za
kuumiza hisia za dini.
3. `The Criminal Procedure Act, 1985 (CPA) imeweka kuwa kosa la
kutamka maneno kwa dhamiri za kuumiza hisia za dini ni kosa la waranti
linalohitaji taarifa kutolewa chini ya kiapo/affidavit kabla ya waranti wa
kumkamatia mtu kutolewa (kifungu 2(1), 13, 110, 112 na Frist shecule CPA).
CPA pia imeweka taratibu za kutoa dhamana na kusikiliza kesi kwenye mahakama
za chini.
Kutokana na hii, kwa hiyo, kwa sababu utaratibu wa sheria nchini
Tanzania umeweka mwenendo mzuri wa kushughulikia malalamiko ya viongozi wa
kanisa katoliki, mtu angeitazamia seirkali ya CCM, basi baada ya kuitupilia
mbali njia ya usuluhishaji magomvi kwa mazungumzo, angalau ingeiacha njia ya
sheria ifanye kazi yake -ingeutaka uongozi wa kanisa katoliki kufungua
mashitaka/malalamiko yao mbele ya hakimu kama inavyoagizwa na CPA; waranti za
kukamatia kutolewa na watuhumiwa kukamatwa; na kuwaacha watuhumiwa kesi zao
ziendeshwe na zisikilizwe mahakamani.
Lazima isisitizwe kuwa kiini cha tatizo hili kimo katika tafsiri
ya nini ndilo kosa la kusema maneno kwa dhamiri ya kuumiza hisia za dini au
kashfa. Jambo linaloleta utata ni kutokukabaliana kati ya viongozi wa kanisa
katoliki na waisilamu kuhusu nini ni kashfa. Ni mvutano unaohusu suala la
sheria. Hili ni sula la sheria la kuamuliwa na mahakama. Ni jukumu la mahakama;
ambazo ndizo watumishi na walinzi wa sheria. Si kazi ya seirkali kuamua nini
ni kashfa, na nini si kashfa.
Lakini, na kuua maana yake, seirkali ya CCM haikuuacha utaratibu
wa sheria kufanya kazi yake sawa sawa. Kwa kweli, serikali ya CCM haikuzijali
sheria wala katiba iliyokabidhiwa na wanachi kuzilinda. Serikali ya CCM
imesahau kuwa mamlaka yake hayaendi zaidi ya mipaka ya uwezo wake wa kikatiba
na kwamba imejiingiza kinyume cha sheria kwenye maeneo ya mahakama. Katika
haraka zake za kuwaridhisha Viongozi wa kanisa katoliki, serikali ya CCM,
huku ikisahau kuwa kuna tofauti ya maneno na mkazo kati ya madai ya viongozi
wa kansia katoliki na waisilamu, umeonyesha kuwa haiyaelewi kabisa maadili ya
kikatiba na ya kisheria. Sidhani ni lazima kurudia kulieleza kila tendo na
kila tamshi la serikali ya CCM wakati ilipokuwa inalishughulikia suala hili.
Matamshi ya viongozi wa serikali ya CCM tangu hapo yalikuwa yanarudiwa rudiwa
yale yale kiasi cha kuchafua roho. Lakini suala lote linaweza kupatikana
kutokana na taarifa za magazeti na za polisi (kama "haizikusanfiwa").
I sitoshe tu kusema kuwa bada ya "tangazo la vita" dhidi ya
mihadhara ya waisilamu tarehe 4 Januari 1998 kule Tabora, mambo yakaanza
kwenda haraka haraka. Inawezekana kuwa jukumu la kupambana na wahubiri wa
kiisilamu walikabidhiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Mkoa, Dar es
salaam, Mkuu wa Polisi na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam; Makamu wa
Rais na Waziri Mkuu wakiwa wanajipenyeza penyeza hapa na pale. Baadhi ya
magazeti nchini yalishiriki kama vile yalipangiwa kazi ya kuchochea hisia za
uhasama dhidi ya waisilamu.
Tukio lote hili linakumbusha mwaka 1968 pale TANU ilipoamua
kuchukua hatua za kudhibiti WAISILAMU kwa mbinu za kugawa na kutawala kwa
kuipiga marufuku East Africa Muslim Welfare Society, iliyokuwa inapendwa na
kuwafanyia kazi safi waisilamu na kuweka badala yake chombo cha BAKWATA.
Wakati ule (kama ilivyo sasa) walitumiwa viongozi wa serikali waisilamu
wapenda madaraka kuongoza kampeni ile; gazeti la serikali, "The
Nationalist" likapewa kazi kuchochea hisia na hamasa za kutwanga
uisilamu. Lilikuwa suala la wachezaji wa zamani ndani ya jezi mpya. Kwa kweli
hii ni mojawapo ya sababu zinazowafanya waisilamu waone kuwa yanayotokea sasa
ni marudio tu ya yale yaliyotokea mwaka 1968. Tofauti pekee mara hii ni kuwa
wakati huu limekuwa ni jambo zito likihusu haki ya waisilamu kutangaza dini,
na watu wameuawa na kutendewa kinyama na kama wanyama.
Kimsingi, matokeo ya kampeni ya serikali ya CCM ya safari hii
yamekuwa kuwatendea waisilamu mambo ya kinyama kuwaua na kuumiza waisilamu,
kuwaghasi waisilamu, kukamata kamata waisilamu bila sheria, kuwanyima
waisilamu haki ya kisheria kwa kuwanyima dhamana , vitisho vya kuzifungia
jumuiya na taasisi za kiisilamu usajili wao, jambo lisilopata kutokea la
kufungia na kulinda misikiti, kupiga marufuku mikutano ya amani ya waisilamu,
kuwadhalilisha kijinsia wanawake wa kiisilamu wakiwa mkononi mwa polisi na
mwisho , bali kwa uzito huo huo vitisho kwa waisilamu.
Njia bora zaidi ya kuielezea hatua ya seirkali ya CCM dhidi ya
mihadhara ya Waisilamu ni kuwa ilikiuka katiba, ilivunja sheria na ilikuwa ya
udini. Serikali ya CCM imetumia utaratibu wa kuendesha mashitaka
kuwanyamazisha waisilamu kwa sababu tu kuwa wasilamu wamekuwa wakitumia haki
yao ya kikatiba kutangaza dini yao. Hatua iliyochukuliwa na serikali ya CCM
imekuwa ya matumzi mabaya ya nguvu za serikali. Kuhoji wenye kufanya uhalifu,
serikali ya CCM ikiwa haijali ile kanuni ya msingi kuwa haki iliyopo ya uhuru
wa nafsi kujiamulia, na dini, inaizuia serikali kuwalazimisha waisilamu
kujizuia kutekeleza wajibu wao wa kuwazindua wakristo juu ya hicho
kinachoitwa kweli ya ukristo.
Aidha, serikali ya CCM, kwa kuchukua hatua za haraka haraka na
bila ya kupima mambo, imeingilia haki ya waisilamu kuhubiri dini yao.
Kulazimisha huku kulikofanywa na serikali ya CCM juu ya waisilamu wasiweze
kuhoji itikadi za kanisa kunamaanisha kuwa serikali ya CCM inaulinda
ukatolki. Kulinda dini moja kwenye taifa ambalo halina dini kumejenga
mazingira ya ugawanyiko ambao matokeo yake ni kuingilia uhuru wa dini unaowekwa
na katiba.
Haipingiki kuwa kukubali kuwa serikali ya CCM ina haki ya
kuwalazimisha waisilamu wasihoji ukristo ni jambo ambalo halikubaliani na
kweli ya kuhifadhi na kutimiza uhuru wa kuabudu au urithi wa Watanzania wa
kuwa Taifa la watu wenye mchanganyiko wa dini mbalimbali. Kweli yenyewe ni
kwamba waisilamu wa Tanzania lazima watambue kuwa serkali ya CCM
imewakumbusha wao wako tofauti na hawamo kwenye utamaduni wa kikristo
unaotumika kuendeshea nchi.
Lakini lazima isisitizwe kuwa si halali kwa serikali ya Tanzania
kulazimisha kuwa wote lazima wakubaliane na vile viongozi wa kanisa katoliki
wanavyotaka. Tanzania ni nchi ya kisekula na viongozi wa serikali ya CCM siku
zote wanatukumbusha kuwa "serikali haina dini." Nchi hiyo kikatiba,
serikali ya CCM hina uwezo wa kutumia nguvu za sheria zilizopo kufikia lengo
la kidini, yaani kufuata itikadi za kikatoliki kwa kuupendelea ukristo dhidi
ya masilahi ya uisilamu.
Pamoja na kutenda kinyume cha katiba na sheria, sirkali ya CCM
vile vile imetudhihirishia utovu wa kuvumiliana usioeleweka na majivuno kwa
vile walivyoyakataa maombi ya waisilamu kufanyiwa haki na kwa uwajibikaji.
Kama vile serikali ya CCM ilivyolikataa mara moja ombi la waisilamu la
kuwekwa tume huru ya uchunguzi juu ya mauaji na kutia waisilamu vilema
waliyofanyiwa na polisi tarehe 13 Februari 1998. Kama vile Waziri wa Mambo ya
Ndani Ali Ameir Mohammed, alivyosema tarehe 4 Machi 1998, "serikali
inayoendeshwa kwa misingi ya utawala wa sheria (?!) haitashinikizwa na mtu yeyote
au kundi lolote kufanya vile wakatavyo wao."
Hii si chochote bali majivuno, hasa pale inapotoka kwa Waziri wa
shughuli za polisi ambao ndio wanaolalamikiwa malalamiko halali. Bila ya
shaka yoyote waziri hajali kuwa yeye anawajibika kwa wananchi kwa matendo ya
polisi wake.
Bwana Ali Ameir, kwa majivuno au kutojua, hajali kuwa utawala
mzuri na haki vinataka kuwa ni muhimu kwa serikali kufanya uchunguzi wa wazi
juu ya mwenendo wa kinyama unaofanywa na polisi kuonyesha kama kuna haja, au
hakuna ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa wa polisi wanaoonekana
kutumia nguvu za polisi zaidi ya vile ilivyo lazima.
Lakini hata kama kusingekuwako na maombi kutoka kwa waisilamu wa
kuweka Tume ya uchunguzi hata hapo, kwa matakwa ya haki na sheria, serikali
ya CCM, ikidai kuwa inajiendesha kwa utawala wa sheria kwa wananchi
inawajibika yenyewe kuteua Tume huru ya uchunguzi.
Lazima ikumbukwe kuwa mauaji na utiaji vilema haviwezi
kutenganishwa na suala la uhuru wa kuabudu. Kwa hiyo, kutokana na kweli kuwa
mauaji yale, bila ya shaka ni suala lenye umuhimu mkubwa kwa uma, serikali ya
CCM inawajibika kuweka chombo kitakachotafuta kweli kuisaidia kuamua juu ya
hatua zinazostahili kuchukuliwa kusahihisha mambo kwa kuyaondoa mabaya
yatakayogundulika, na kufanya yale mema ambayo serikali inayafikiria, kwa
mfano, polisi iliyotayarishwa na kupewa vifaa bora zaidi na vile vile fidia
kwa wale waliofikiwa na misiba.
Uchunguzi utagundua chanzo cha mauaji na kutia watu vilema na
kuturudishia imani za watu. Kama uchunguzi wa maana hautafanywa, hisia za
kudhulumiwa na kubaguliawa zitaongezeka. Na wasiwasi, na kuhisi kutokuwapo
amani malengo ambayo serikali ya CCM hujitia kuyalingania pale watakapo
kuhalalisha mambo.
Kama nilivyosema kenye utangulizi katika juhudi zake za
kuhalalisha mabavu aliyoyatumia, serikali ya CCM imeleta madai kuwa
ililazimika kuchukulia mihadhara ya kiisilamu hatua zile kwa sababu ya
"tishio kwa amani na usalama" wa Tanzania. Viongozi wa serikali ya
CCM wameripotiwa kusema kuwa mihadhara ya Waislamu ilikuwa inaendeshwa na
"wakorofi wachache wenye siasa kali na kwamba kama siasa kali hizi
zikiruhusiwa kuenea zitatishia amani ya nchi na kutumbukiza kwenye umwagaji
damu kama ilivyotokea Algeria.
Ni dhahiri hakuna mantiki kwenye madai haya. Kuhifadhi amani kwa
matendo ya kibabe na matumizi ya mabavu. Kinyume chake, hali huchafuka zaidi
kwa matumizi ya hatua haramu na za kinyama, kuwalazimisha wale wanaotakiwa
kudhibitiwa kufikia pahali ambapo lazima wajihami. Watu wanaofikishwa ukutani
ni rahisi zaidi kujihami kwa nguvu hasa pale wanapoona kuwa wameonewa.
Historia imejaa mifano ya naman hii.
Na kama serikali ya CCM kweli ilikua na lengo la kulinda amani
basi ingejitahidi kutafuta na kutumia njia zote za kupata ufumbuzi wa mivutano
iliyotokana na mihadhara ya waisilamu kwa mazungumzo na kushauriana. Serikali
ya CCM iliikataa njia hii. Na hata kama mazungumzo yasingefaa kulikuwa hakuna
uhalali wa kutumia njia zinazokwenda kinyume na katiba na haramu badala ya
kuiacha sheria ifanye kazi yake.
Hata hivyo, hakuna hata chembe ya ushahidi, hakuna hata mtu
mmoja hai anayeweza kuthibitisha kuwa mihadhara ya waisilamu inahatarisha
amani na utulivu nchini Tanzania kinyume chake kuna ushahidi uliohifadhiwa
kwenye kaseti za video za mihadhara mbalimbali inayoonyesha kuwa mikutano ile
imekuwa ya amani kabisa na ya furaha. Na lililo la kuzingatia sana ni kuwa
mihadhara hii imekuwa ikisilimisha wakristo hadharani (wakati mmoja idadi yao
ilifikia ishirini kwenye mhadhara mmoja).
Watu ambao sasa hivi imani yao imekuwa "ikitukanwa",
kama maaskofu wa kikatoliki na mapadri wao wanavyotutaka tuamini, hawabadili
dini na kusilimu, wajiunge na watu wale wale waliokuwa
"wanawatukana." Ni jambo rahisi hata mtoto wa miaka kumi anaweza
kuliona hili!
Kuhusu madai ya kuwapo kwa tishio la "Waisilamu wenye siasa
kali Tanzania" mimi nasema kuwa na hili nalo ni dai la kipuuzi na la
hovyo linalotokana na ushuku na Ishara za CNN" ("CNN
Syndrome") - kutazama na kusikiliza sana vipindi vya televisheni ya CNN
ambamo jambo lolote linalohusiana na harakati za Waisilamu wenye siasa
kali." Siasa kali si chochote bali ni mtindo wa kidini unaofuatwa na
muhafidhina wa kiprotestanti wa marekani ulioazishwa kwenye miaka ya 1920
ambamo wanadai kuwa kila neno la Biblia ni neo la Mungu na kwa hiyo ni kweli.
Hakuna "Uisilamu wenye siasa kali" au "Waisilamu wenye siasa
kali". Kwa mujibu wa Uisilamu, kuna waisilamu kweli na Waisilamu
wanafiki.
Vile vile si sahihi na kukosa mizani kwa viongozi wa serikali ya
CCM kutumia hali iliyopo Algeria kama mfano unaoelekeana na hali ya Tanzania.
Algeria ni moja kwa moja suala la kuingilia kwa jeshi kuwanyang'aya mamlaka
Islamic Salvation Front (FIS) ambao walikuwa wanashinda katika uchaguzi wa
kidemokrasia. Ilikuwa lazima kwa FIS kupinga mapinduzi haya ya jeshi la
kipinga maendeleo.
Kinachoendelea Algeia leo ni vita chafu inayoendeshwa na jeshi
la Algeria wakishirikiana na "serikali" na mgambo wanaodhibitiwa na
serikali, kwa madhumuni ya kuipakazia FIS. Katika vita hii maelfu na maelfu
ya Waisilamu wanaowaunga mkono FIS, au wanoashukiwa kuunga mkono wameuawa au
kutiwa vilema na jeshi la mgambo. "Kukamatwa bandia "kwa viongozi
wa mgambo wa kiraia kulikofanywa hivi juzi juzi baada ya shinikizo kutoka
Tume ya uchunguzi iliyopelekwa na jumuiya ya kimataifa -
kulinithibitishia hili. Kinyume chake, mamia ya mihadhara ya waisilamu
hayajaleta, kama nilivyoonyesha hata tukio moja la fujo. Na tena, mazingira
ni tofauti. Nchini Algeria suala ni juu ya nani ana haki ya kutawala baada ya
ushindi halali kwenye uchaguzi halali wa kidemokrasia. Na Tanzania, suala ni
juu ya nani ana haki ya kutafasiri sheria ya "kashfa" ni mahakama
au viongozi wa kanisa na serikali. Hakuna kufanana hata kidogo.
Ikumbukwe kuwa dhana hii liyozagaa dunia nzima kuwa kuna tishio
la wausemao kuwa ni Uisilamu wenye siasa kali ni uzushi wa watayarishaji wa
sera za nchi za nje wa serikali ya Marekani. Vita vya Baridi vilipokwisha,
watayarishaji wa sera za nchi za nje wa serikali ya Marekani waliamua kuwa
"aina kali" za Uisilamu zingejaza nafasi zilizoachwa wazi na
kuporomoka kwa Soviet Union na Ukomunist. "Uisilamu wenye siasa
kali" kwa hiyo ukaonekana kuwa ni tishio kwa masilahi ya Marekeni dunia
nzima na utawala wa Bush ukaamua kuwa "kuenea kwa Uisilamu wenye siasa
kali ndio jambo moja linalowasumbua watayarishaji sera." kwa hiyo sera
za kupinga ukomunisti, kudhibiti na kuizuia Urusi ya Soviet za serikali ya
Marekani wakati wa vita baridi mahali pake sasa pakajazwa na mtindo mwingine
dada wa kupinga Uisilamu uliokazia hasa kwenye makundi ya "siasa
kali" ya Mashariki ya kati na Africa ya Kaskazini, kwa mujibu wa P.J.
Schraeder kwenye kitabu chake "US Foregin Policy Toward Africa"
(Cambridge Univ. Press, 1994) jinsi serikali ya Marekani ilivyoyashughulikia
masuala ya Algeria ni mfano dhahiri wa sera hii - kwamba kuudhibiti na
kuuzuia Uisilamu kumechukua nafasi ya kudhibiti na kuzuia Ukomunisti kama
lengo katika masuala ya usalama linachukua nafasi ya juu mbele ya demokrasia:
"Kinyume kabisa na vile serikali ya Marekani inavyolaani
serikali za kidikteta katika sehemu nyingine za Afrika, watayarishaji wa sera
yake, kwa kushangaza walibaki kimya kabisa pale jeshi la Algeria lilipofuta
matokeo ya uchaguzi wa kidemokrasia wa kwanza na ukachukua uendeshaji wa nchi
kwa mapinduzi ya kijeshi. Kimya cha Marekani hakikusababishwa na imani yao
kwa majenerali kama walinzi wa demokrasia bali kilitokana na sababu kwamba
chama cha Kiisilamu "chenye siasa kali" - Islamic Salvation Front
(FIS) ambacho kiliahidi, pamoja na nyinginezo kampeni, kuiendesha nchi kwa
sharia, kilikuwa karibu kichukue mamlaka ya nchi kupitia uchaguzi wa
kidemokrasia" (uk.258).
Ni jambo la kuzingatia pia kuwa serikali ya CCM vile vile
ilijaribu kuhalalisha mauaji na kuwatia vilema Waisilamu kwa madai kuwa
polisi na polisi wa kuzuia fujo walikuwa na haki ya kujihami nafsi zao. Huku
ni kujipurukusha na kuukataa wajibu inapotokea kwa watu wanaoendesha serikali
ambao wajibu wao ni kulinda na kuhifadhi maisha ya raia wao. Kwa kweli ni
jambo linaloshangaza na lisilokubalika kupendekeza, wacha kudhani, kuwa
ilikuwa halali kwa polisi kutumia sub-machine guns" na risasi moto
kuwafyeka raia wenzi wao, pamoja na watoto wa shule kwa kisingizio kwamba
walikuwa wanatupiwa mawe. Kulikuwa hakuna mashambulizi yaliyotishia maisha au
kuumia vibaya kwa polisi ambao walisimama mbali na watupa mawe.
Hakuna polisi aliyeumizwa au aliyepigwa na jiwe kabla ya kuanza
kwa mashambuli ya risasi. Matumizi ya risasi yalianza bila ya matangazo
yoyote kwa jina la Rais ya kuwaamuru watu waliohusika kutawanyika, wazi wazi
vilikiukwa vifungu 27 na 28 vya Penal Code. Ile kanuni ya kutumia nguvu
isiyopelekea kuua; kidogo au inapostahiki dhidi ya mashambulizi
yaliyohatarisha maisha inayosisitizwa kila mara kwenye mafunzo ya kudhibiti
makundi na vurugu ilikuwa wapi? tukichukulia kuwa mafunzo hayo bado yapo!
Vipi kinga za ngao na kofia za polisi? Hizi hazikutosha
kuwalinda polisi dhidi ya mawe walipokuwa wanatupiwa? Na nini yalikuwa
madhumuni ya mabonu ya kutoa machozi yaliyotumiwa kama si kuwafadhaisha na
kupunguza nguvu za watupa mawe? Wazi wazi ushahidi ulioonekana unaonyesha
kuwa matumizi ya risasi moto yalianza muda mrefu kabla ya vikosi vya kuzuia
fujo kufika na kabla ya tangazo la kuwataka watu kutawanyika kutolewa.
Ni kutokana na sababu hizi mtu anapopata nguvu kuamini kuwa
kadinali Pengo katika mazungumzo yake kwenye kipindi cha "Hamza Kassongo
Hour" kilichotolewa na DTV tarehe 12 Aprili, 1998, angeweza pia kutoa
madai ya haki ya polisi ya kujihami wenyewe, kwa kutumia simulizi za Daudi na
Goliathi kuhalalishia madai hayo. Nani alikuwa Daudi na nani alikuwa Goliathi
katika mapambano ya Mwembechai ambapo watu walikuwa wanaonyesha upinzani wao
dhidi ya kuingiliwa kwa haki yao ya kuhubiri neno la Mungu?
Yaliyotangulia, Mh. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa jumla ni
waraka wangu kwako kuhusu jinsi serikali ya CCM ilivyolishughulikia suala la
mihadhara ya Waisilamu. Ni waraka mrefu, na kutokana na uchache wa elimu
yangu, unaweza hata kuhesabiwa kuwa ni kujikweza. Lakini unatokana na imani
yangu kuwa si mengi ya kutosha yanayojulikana kuhusu mihandara ya Waisilamu
na misimamo ya viongozi wa kanisa katoliki juu ya uhuru wa dini. Siwezi
kujidai kuwa nimefanikiwa kikamilifu katika lengo hili kwani najua upungufu
wangu kwenye elimu inayohusu maswali yaliyozungumzwa. Lakini kama
ningefanikiwa kukushawishi uende ndani zaidi kwenye suala hili hapo juhudi
zangu zitakuwa zimezaa matunda.
Naharakisha kuongeza, hata hivyo kuwa nimelazimika kukuletea
waraka huu kwa sababu hakuna ushahidi kuwa serikali ya CCM na washauri wake
wa mambo ya sheria na siasa, wana dhamiri yoyote ya kujaribu kufikia kwenye
mzizi wa tatizo hili. Kwa kweli kwa kushangaza, kumekuwako na njama za kuweka
ukinifu miongoni mwa waendesha mambo ya kiserikali na kisheria. Ni dhahiri,
kwa vile sina nafasi ya kufikia na kupata taarifa kama serikali ya CCM
hufanya kazi yake kutokana na ushauri inaoupata kutoka kwa washauri wake wa
kisheia, sipo katika nafasi ya kusema kwa hakika ya dhati kabisa kama ushauri
wa kisheria ulitolewa na halikutolewa na kama ushauri huo ulikubaliwa au
ulikataliwa.
Iwe iwavyo kweli inabaki pale pale kuwa serikali ya CCM
haikufanya juhusi zozote za kulishughulikia suala hili kwa haki ili kugundua
sababu zake ni jinsi ya kupata ufumbuzi wake. Kinyume chake kumekuwako na
majivuno tu pamoja na matumizi mabaya ya nguvu za dola bila ya kujali kabisa
matokeo mabaya ya kujiingiza kwenye uhasama na Waislamu kuhusiana na hili,
nadhani ni muhimu kuwa serikali isikubali kuhadika na kushiriki na kuungwa
mkono na baadhi ya viongozi wa kiisilamu na watendaji kunakoonekana. Serikali
itafanya vizuri ikikumbuka kuwa siku zote kuna waisilamu wachumia tumbo kama
vile siku zote kuna wajipendekezaji kwenye siasa na shughuli za umma.
Katika kipindi chote cha "mapambano", serikali ya CCM
imekuwa si wazi na ilikuwa ikitumia ubabe ubabe ikionyesha kutokujali kwake
utaratibu wa kuendesha nchi kwa sheria na ikionekana kuwa dhamiri yake
ilikuwa kukandamiza uhuru wa Waisilamu wa kueneza dini yao. La muhimu zaidi,
vile jinsi wakati serikali ya CCM ilipokuwa inatekeleza jukumu lake
halikuwaonyesha kuwa ilikuwa inajali uhuru wa kuabudu au hata kuma ilikuwa
inajali juu ya hisia za mamilioni ya Waisilamu wa Tanzania.
Juhudi zangu kwa hiyo zimelenga kwenye kufikia haki na kweli, na
kwenye ufumbuzi wa matatizo yaliyosababishwa na utendaji mbaya wa serikali ya
CCM. Wewe, Mh. Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mlinzi wa sheria za
Tanzania, na mshauri mkuu wa serikali kwenye mambo ya sheria, una wajibu wa
kudumu na jukumu la lazima kuhakikisha kuwa mtindo wa kutumia utaratibu wa
kuendesha kesi za jinai kunyamazishia Waisilamu na Watanzania wengine
unaachwa mara moja. Aidha, una wajibu na jukumu la kusikiliza kilio cha
Waisilamu kutaka watendewe haki na kuheshimiwa kwa haki zao za kikatiba za
kueneza dini yao.
Mh. Mwanasheria Mkuu mwanzo wa waraka wangu nilisema kuwa hakuna
mtu anayehoji haki ya kikatiba na kisheria ya serikali kutumia vikosi vyake
vya polisi wa kuzuia fujo siku ya Ijumaa tarehe 13 kwa madhumuni ya kulinda
amani na usalama baada ya mambo kuharibika. Nilihoji, hata hivyo, kukamatwa
kiholela na kibabe-babe tu kwa wahubiri wa Kiisilamu na kwa polisi kuingia
kwa kunajisi msikiti wa Mwembechai kulikotokea Alkhamisi ya tarehe 12.
Nilihoji pia matumizi ya mabavu na nguvu za kinyama mara zote
mbili. Nilionyesha kuwa matendo yale hayakuwa chochote bali uingiliaji wa
kibabe wa uhuru wa Waisilamu wa kuabudu na kueneza dini yao. Pahali pengine
nilionyesha kuwa hakuna ushahidi kabisa wa kuthibitisha madai ya serikali ya
CCM kuwa hatua walizochukua zilikuwa lazima kwa sababu kulikuwa na haja ya
kulinda amani iliyokuwa inatishiwa na mihadhara ya Waisilamu.
Wakati wote, msimamo wangu umekuwa kwamba kuna jambo jingine.
Kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa hakijajitokeza. Na linalohusika ni uhuru wa
kuabudu wa mamilioni ya Waisilamu wa Tanzania. Huoni kuwa inashangaza kuwa
mpaka kufikia tarehe 4 Januari 1998 kulikuwa hakujatokea hata tukio moja la
fujo au magomvi ambayo yangeweza kuhusishwa na mihadhara ya Waisilamu?
Kwa nini basi maaskofu wa kanisa katoliki na viongozi wa
serikali walikuwa wamekaa na madai kwamba mihadhara ya Waisilamu ilikuwa
inahatarisha amani ya Tanzania? Na kama kweli itasemwa kina nani hasa kwa
hatari kweli kweli walikuwa wanakazana kuichimba amani ya Tanzania? hawakuwa
viongozi wa kanisa katoliki na wa serikali ya CCM kwa kuchochea hisia za
chuki kushitua watu na hasira za watanzania kwa kuwajengea "picha ya
hatari ijayo ya kuvamiwa na Mujahidina" bila ya uhalali wala ushahidi
wowote?
Wahubiri wa Kiisilamu bado mpaka leo hawajui sheria gani ya
Tanzania wanadaiwa kuivunja au kosa gani wamelifanya. Qur'an inawaambia kuwa
Yesu (AS) si mwana wa Mungu. ushahidi wa Biblia unathibitisha imani yao.
Sheria ya Tanzania inakubali kuwa kwa Muisilamu kusema kuwa yesu si mwana wa
Mungu bali ni Mtume wa Mungu si kosa chini ya kifungu 129 cha `penal Code'
kwa sababu ni imani ya kiisilamu. Katiba ya Tanzania imeweka uhuru wa
waisilamu kutangaza imani hii na imani zao nyingine.
Na hata hivyo waisilamu bado wanasumbuliwa, wanazimwa vinywa na
wanashitakiwa kwa kosa ambalo halitambuliwi na Mungu, katiba na sheia za
Tanzania. Waisilamu wataona nini katika haya? Waamini sasa kuwa Tanzania ni
nchi ya utawala wa dini ya kikatoliki; kwamba kosa chini ya kifungu 129 cha
`Penal Code' maana yake ni kuwa kusema yesu si mwana wa Mungu ni kuutukana
ukristo; na kwamba Waislamu hawana haki ya kutangaza dini yao? Hili ndilo
linalotakiwa na uongozi wa kanisa katoliki na wa serikali ya CCM?
Linalotakiwa na uongozi wa kanisa katoliki na wa serikali ya CCM
ndilo linalotakiwa na katiba ya kisekula ya Tanzania na sheria za Tanzania?
Sidhani . Nadhani kuwa muundo wa mchanganyiko wa tamaduni za jumuiya ya
Tanzania unataka zaidi ya hivyo Tanzania inajumuisha watu wa dini nyingi na
tamaduni nyingi ambao, kwa mujibu wa katiba ya kisekula wote wanahitaji
kuheshimiwa haki na uhuru wao, kutobaguliwa, kuvumiliana na amani kwa wa
wote.
Rais, mkatoliki na kwa hiyo anatazamiwa kufuata amri na
mafundisho ya kanisa katoliki, akizungumza ex cathedra kwenye mkutano wa
viongozi wa makanisa, anaahidi kutumia uwezo aliopewa na katiba ya kisekula,
kuzima kabisa inapoonekana na kanisa katoliki kuwa inatukana ukristo, hawezi,
kwa kweli kuambiwa kuwa hakuwa anapendelea. Kwa kweli hawezi kuambiwa kuwa
hakuwa anafanya hivyo kinyume cha katiba. Kwa dhati kabisa nafikiri kuwa Rais
atafanya jambo jema kama ataiga mfano wa marehemu Rais Kennedy wa Marekani
ambaye, miaka arobaini iliyopita, katika kampeni zake za kugombea Urais,
akiwa anakabiliwa na mashitaka ya halali ya kutaka kuuvunja ukuta
unaotenganisha kanisa na serikali; alisema:
"Ninaamini kwenye Amerika ambamo kanisa na serikali
vinatenganishwa kabisa - ambamo hakuna kiongozi wa wakatoliki atamuamuru Rais
jambo la kufanya na hakuna mchungaji atakayewaamuru waumini wake nani
wampigie kura... Amerika ambayo rasmi si ya kikatoliki, kiprotestanti, wala
ya kiyahudi - ambamo hakuna mtumishi wa umma anayeomba au kukubali maagizo
kuhusu sera kutoka ... viongozi wowote wa dini... ambamo hamna kura ya
wakatoliki; hakuna kura ya kundi ya aina yoyote... na ambamo uhuru wa dini...
haugawanyiki.. mimi si mgombea Urais wa Wakatoliki, mimi ni mgombea urasi wa
Chama cha Democrat ambaye ni mkatoliki. Sisemi kanisa langu kwenye mambo ya
umma na kanisa langu halinisemi" (K.207-208, "Vicars of
Christ").
Kwa kauli hizi za kumalizia ningependa kupendekeza hatua chache
ambazo zitatusaidia kurudisha imani na turudie kwenye fahamu kamili. Najua
naweza kusemwa kuwa najivisha majoho ya wenyewe kwa kutoa baadhi ya
mapendekezo haya.
Siombi radhi. Hili, tangia hapo, si jambo binafsi la wachache
bali la umma lenye maana kubwa sana kuhusu uhuru wa mamilioni ya watanzania
na kuhusu amani na utulivu wa jumuiya yetu:
· marufuku yaliyopo hivi sasa juu ya mihadhara ya waisilamu
yaondolewa mara moja. Marufuku haya hayakubaliani na kifungu 19 cha katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia ambayo imeweka haki ya msingi ya dhana ya
kuabudu pamoja na uhuru wa kutangaza dini.
· tume ya uchunguzi huru na isiyo ya upande wowote iundwe na
serikali ipate kuchunguza, inter alia':
(a) polisi kuingia kwa kunajisi msikiti wa Mwembechai tarehe 12
Februari 1998;
(b) mambo yaliyopelekea mlipuko wa tarehe 13 Februari 1998;
(c) Kupigwa risasi na kuuawa/kuumizwa kwa waisilamu watano
kulikofanywa na polisi tarehe 13 February 1998;
(d) Kuumiza na kutiwa vilema waisilamu na wengine ulikofanywa na
polisi tarehe 13 Februari 1998;
(e) Kudhalilishwa kijinsia kwa wanawake wa kisilamu wakiwa
mikononi mwa polisi pamoja na kukamatwa kwao hapo mwanzo;
(f) kukamatwa na kuteswa kwa Waislimau wakiwa mikononi mwa
polisi;
(g) kukamtwa kwa waisilamu kwa kuwa nazo nakala na tafasiri za
aya za Qur'an zilizoonekana na polisi kuwa ni za kiadui kwa ukristo;
(h) kama kufungwa na kulindwa kwa msikiti wa Mwembechai
kunakubaliana na katiba na sheria zinazohusika;
(i) kama polisi na vikosi vya kuzuia fujo walifanya kazi zao kwa
mujibu wa taratibu za kudhibiti fujo na makundi ya watu zilizomo kwenye
vifungu 77 na 78 vya Penal Code,' `Police Force Ordinance' na `Police Force
General Orders';
(j) kama mwenendo wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Polisi
(Taifa) na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kabla, wakati na baada ya
matukio ya Mwembechai ulikuwa unakubaliana na matakwa ya katiba, na sheria
nyingine zinazohusika, za Tanzania; na
(k) hasa hasa kama tofauti na kutokukubaliana kuliopo kati ya
wakatoliki na waisilamu juu ya mambo yanayohubiriwa na waisilamu kwenye
mihadhara yao zilishughulikiwa na serikali kwa kufuata katiba ya Jamhuri za
Muungano wa Tanzania na sheria nyingine za Tanzania zinazohusika.
· Tume ya uchunguzi iongozwe na Jaji wa Mahakama ya Rufaa na wa
mahakama kuu ya Tanzania na wajumbe wake wakiwa mmoja mmoja kutoka kanisa
katoliki Tanzania, Kanisa la Kilutheri la Tanzania, AL MALID, BAKWATA, BARAZA
KUU, Baraza Kuu la Shia Ithnaashari Tanzania, Tanganika Law Society, TAWLA,
Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu, Dar es Salaam, Idara ya Political Science ya
Kitivo cha Arts na Sayansi za Kijamii Chuo Kikuu, Dar es Salaam na Taasisi ya
masomo ya Maendeleo ya Kijamii Chuo Kikuu, Dar es Salaam
· tume itoe mapendekezo itakayoamua yanastahiki ya kurekebisha
uovu wote utakaoonekana na juu ya hatua zitakazofaa kurudisha mshikamano wa
kiserkali.
· Mwendesha mashitaka Mkuu azipitie upya kesi zote za tuhuma za
"kashfa" dhidi ya Waisilamu kuona kama taratibu za kisheria
zilifuatwa na kufuta mashitaka yote yatakapoonekana kuwa si sahihi.c
· Mwendesha mashitaka Mkuu (DPP) awaagize waendesha mashiaka kuacha
kuwazuilia dhamana washitakiwa waisilamu bila ya sababu na kwa hoja za
kipuuzi. Dhamana ni haki si tunzo.
· Viongozi wa serikali washauriwe kuwa wanakwenda kwenye nyumba
za ibada kwenye nafasi zao kama watu binafsi kuswali na kufanya ibada kama
raia wengine wa kawaida. Kwa hiyo waache mara moja tabia ya kuzigeuza nyumba
za ibada kuwa majukwaa ya kutoa matamshi au kauli zinazohusu mambo ya
kisekula na/au kisiasa na wakatae mialiko ya kuhudhuria shughuli za kidini
katika nafasi zao za kiserikali. Vile vile waache tabia ya kugeuza nyumba za
ibada kuwa ngome zenye ulinzi mkali na barabara zote zinazoelekea huko
kufungwa na polisi wa trafiki kila waendapo kuswali na kufanya ibada (bila ya
shaka wana askari kanzu wa kutosha kuwalinda kutokana na matishio yoyote,
halisi au yanayofikiriwa yanaweza kutokea kwa ajili ya usalama wao).
· Viongozi wa serikali, hasa makamu wa Rais, washauriwe kuwa
sawa na kanuni za serikali ya kisekula serikali haiitambui rasmi BAKWATA
mbele au badala ya taasisi nyingine za kiisilamu zote ziko sawa mbele ya
sheria. Kadhalika serikali iache tabia yake ya kuingilia shughuli za
kuendesha taasisi za kiisilamu au misikiti au kuwalazimisha wasilamu lini na
wapi wanaweza kutekeleza shughuli yoyote ya kiisilamu.
· Serikali ishauriwe kutoa maagizo kwa idara zake zote mashirika
yake na mashirika yake ya umma yote kuheshimu usekula wa katiba ya nchi
katika shughuli zao zote, pesa za umma zisitumike katika kugharamia shughuli
yoyote ya dini.
· Matumizi ya "machine-guns" yanayofanywa na polisi yaachwe
mara moja. Ni silaha ya vita inayotumiwa na wanajeshi dhidi ya adui mwenye
silaha kama hizo na hazikukusudiwa kutumiwa dhidi ya raia wasio na silaha.
Mh. Mwanasheria Mkuu, niruhusu nimalizie kwa maoni yafuatayo.
Jambo la kwanza, ni dhahiri, ni kwamba uhuru wa kuabudu ni kanuni ya msingi
inayobeba ndani yake thamani kubwa. Serikali za kidemokrasia zinaweza
kuvunja, na huvunja, haki za raia. Kwenye jumuiya ya kisekula ambayo ni ya
mchanganyiko wa dini na tamaduni mbalimbali kama yetu taratibu za kuendeshea
nchi zenye nguvu zinahitajika kuhakikisha kuwa thamani kubwa hii haiingiliwi.
Watanzania tukiungana, na kujitolea wote kikamilifu kulinda kweli na haki na
tukiamua kushika uzi ule ule, tutakuwa na hakika kuwa thamani hii, na
nyingine hazitaingiliwa na matendo ya kibabe babe ya kisiasa, au nguvu za
dola, au matashi na mawazo ya sehemu fulani ya jumuiya yetu. Kupingana na
kusikilizana kati ya makundi au masilahi yanayogongana yashughulikiwe kwa
mujibu wa sheria na kushauriana. Serikali na vyombo vyake watekeleze shughuli
zao kwa mujibu wa wajibu wao kisheria. Ni hapo tu ndipo tutakapokuwa na
maendeleo katika hali ya utulivu. Badala yake ni maisha ya samaki na uonevu.
Mapambano dhidi ya mihadhara ya waisilamu, ingawa yalichochewa
na viongozi wa kanisa katoliki, yanaonekana kuongezewa nguvu na kutujua,
udini na mawazo potofu juu ya Uisilamu. Uisilamu ni dini inayoeleweka vibaya
sana. Mawazo yaliyopo ya watu wengi ni kwamba Uisilamu ni mila ya kidini ya
ajabu ajabu ya kiarabu na waisilamu ni watu wa madadi na magaidi. Kwa kweli
Uisilamu umekuwa ukieleweka vibaya mno na kuelezewa vingine mno kiasi kwamba
watu wengi wanaufikiria kuwa ni adui wa aina yoyote ya utulivu, amani na
maendeleo; hawauamini, wanauogopa na wanauona kama tishio kubwa bila ya kuwa
kawaida, kujua chochoe juu yake isipokuwa yale yanayoandikwa na magazeti juu
yake ambayo karibuni mara zote, huwa wamekosea sana ngano za kubuni na
makosa; zaidi kuliko taarifa za kweli. Lakini Uisilamu ni jumuiya ya kidini
ya pili kwa ukubwa duniani leo, ya kwanza ni ukristo. Ni imani inayofuatwa na
karibu watu bilioni moja wanaoishi kwenye kila sehemu ya dunia. Vile vile ni
dini inayoijuwa kwa haraka zaidi kuliko zote duniani. Wamarekani na Wazungu
wanaacha ukristo kuingia Uisilamu.
Tunaishi kwenye zana za misukosuko mikubwa na kutokuwapo kwa
hakika ya maisha. Watu dunia nzima wanapapasa papasa kwa wasiwasi mkubwa
kutafuta cha kumnusuru mwanadamu aliyepoteza dira. Ni kweli, inaweza kuwa
kweli, kuwa leo tunaishi kwenye zama za kofia ya maendeleo na ustaarabu wa
nyenzo za maisha duniani, bali katika maeneo ya thamani na maadili mwanadamu
yako karibu na kufilisika. Kwa mujibu wa Uisilamu matatizo haya ni matokeo ya
mwanadamu kupoteza kule kutambua yeye ni nani mintaarafu ya yeye mwenyewe,
wanadamu wengine na zaidi ya wote, Mwenyezi Mungu ambaye kutoka kweake, kuwa
kwenyewe, na mahusiano ya wanadamu yote, ndiko chanzo. Na mpaka pale
atakapoweza kupata majibu sahihi na yenye maana kwa maswali kiini kwa majibu
wa matatizo yake majibu yanayopatikana na kushikana na hali halisi za msingi
katika maisha yake, na dhati yake halisi ya maumbile, maisha yake yatabaki
hivyo hivyo yananing'inia na kupeperuka bila ya kuwa na pakushikia na bila ya
dira; dhati yake itapotoka na kutawanyika; utu wake ukidhalilika kwa kuruhusu
unyama wake kushika hatamu; na kaumu zake zikiinamiwa na matatizo.
Uisilamu unadai kuwa unatoa, majibu na ufumbuzi, majibu ambayo
yanaafikiana na kupatana na akili, mantiki, hali halisi ya ulimwengu wa
maada, na dhati ya maumbile ya mwanadamu yenyewe. kwa sababu Uisilamu, zaidi
ya yote, ni taswira ya kuwa kwenyewe kamili, ikibeba, taswira hii, kuwapo
kwa, na sifa za Muumba, uhusiano wa mwanadamu naye, nafasi na jukumu lake
humu duniani, na uhusiano baina ya maisha ya sasa na maisha ya Akhera, ambao
unaweka kila kilichopo katika nafasi yake muafaka na unaweka mizani na dira
kwenye maisha ya wanadamu na kaumu zao.
Kwa hiyo ni muhimu kwa Watanzania wale wanaotaka kuelimika na
kujua mambo, kujivua na taarifa za mawazo ya uongo waliyonayo juu ya Uisilamu
ili wauelewe kihalisi, kama ulivyo na kwa taarifa za kweli. Watanzania wengi
wameanza kuyafanya haya. Watu dunia nzima, zaidi na zaidi, wanapata taarifa
sahihi juu ya Uisilamu. Nchini Marekani kuna idadi kubwa inayoongezeka ya
wana taaluma; madaktari, wauguzi, maprofesa, wahandisi wanasheria, walimu,
wafanyabiashara - pamoja na wafanyakazi za mezani na wanafunzi, wanaorejea
(wanaoingia) kwenye Uisilamu. `Prince Charles' wa Uingereza, kama
alivyoripotiwa na `Daily Nation' (Nairobi) la tarehe 29 Octoba 1993, pia
ameona kuwa hukumu juu ya Uisilamu "imepotoshwa kweli kweli kwa
kuyachukulia yale ya ukali zaidi kuwa ndiyo ya kawaida." Katika hotuba
yake mbele ya wasomi 500, viongozi wa jumuiya za kiisilamu, watu wa kanisa na
mabalozi iliyotolewa kwenye shedonian Theatre, Oxford, tarehe 28 Octoba 1993,
waandalizi wakiwa "Islamic Society of Oxford University" Prince
Charles alisema kuwa: "Dunia ya Uisilamu na ya watu wa Magharibi
haziwezi tena kuendelea kuwa mbali mbali. Lazima tushirikiane kwenye ujuzi,
tujieleze kila mmoja kwa mwenzake. Uisilamu unaweza kufundisha leo njia ya
kuelewa mambo na kuishi duniani ambayo Ukristo wenyewe hainayo, umeingia
umasiki kwayo, kwa sababu umeipoteza."
Mwisho, kwa sababu suala la kuingiliwa kwa uhuru wa kuabudu
kibabe kibabe linahusu mamilioni ya Watanzania na dunia ya wapenda uhuru,
napeleka nakala za waraka huu kwa watu fulani fulani, balozi, vyama vya
siasa, vyombo vya habari na kwa watu na taasisi zote zinazohusika.
Abu Aziz
Muisilamu
15 May 1998
|
|
Written By Msamaa on Thursday, May 2, 2013 | 6:09 AM
Labels:
makala
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !