Maoni yetu
Kama hodari wa kuhojiTuhoji pia
Tume ya Majeshi ya Vita
Na kile chama cha Wanajeshi wa Kikiristo Je!
VIBAKA wamekuwa ni kero kubwa katika miji mingi nchini kwetu. Linaloshangaza
ni kuwa pamoja na kushuhudia wenzao ama wakipondwa vichwa kwa matofali au
kuvishwa matairi na kupigwa kiberiti, vibaka hawajifunzi.
Badala ya kutia vichwa vyao maji baada ya kuona wenzao wakinyolewa, hubuni
mbinu mpya ya kuendeleza uporaji wao. Upo mtindo ulioibuka Jijini Dar es Salaam,
hivi sasa ambapo kibaka akikurupushwa hutimua mbio huku naye akipiga kelele za
"Mwizi huyo" "Mwizi huyoo". Au akamgeukia aliyempora na kumwita Mwizi. Katika
hali hiyo wenye usongo na kibaka wasipochukua tahadhari humpita mkuku kibaka
halisi wakaenda kumshughulikia mtu asiye na hatia au yule yule aliyeporwa.
Na vibaka sio wa kupora mikufu na saa pekee. Wapo pia vibaka wa haki za
wengine katika jamii na siasa. Watusi watawakandamiza na kuwaonea Wahutu,
wakihoji wataambiwa waasi na magaidi!
Majahudi wanawapora Wapalestina haki zao wakisimama kujitetea wataambiwa
siasa kali, magaidi n.k.
Waislamu watavamiwa na polisi msikitini kwao wakijitetea wataambiwa "wameleta
vurugu", "wahuni" na "wanahatarisha amani!" Ni yale yale; kibaka kakwapua
anampigia kelele za mwizi mtu aliye mbele yake ili yeye asalimike kuvishwa tairi
na kupigwa kiberiti.
Watu na vyombo rasmi vinahoji. Vipi "Islamic Club"! Kwanini "Islamic".
Kwanini Mawaziri na Maafisa waandamizi Serikalini wajihusishe na "Islamic
Club"!.
Octoba 15, 1997 wanajeshi Wakristo wapatao 150 walikutana katika hoteli ya
Sheraton mjini Kampala, Mada Kuu (Theme) ya mkutano wao ikiwa "Serving to lead _
The Christian in the Armed Forces."
Mkutano huo haukuwa wa siri, kwani ulifunguliwa rasmi na Mhe. Rebecca Kadaga,
ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda na kutangazwa na vyombo vya habari.
Wanajeshi kama Watanzania wengine wana haki ya ama kuwa Waislamu au Wakristo.
Ila jeshi halina dini. Na kule Uganda wanajeshi wetu Wakristo hawakwenda kama
watu binafsi, bali walikwenda kama wanachama wa "Association of Military
Christian Fellowships for East and North-East Africa. Kule wakakutana na
wanajeshi Wakristo wenzao wa Ghana, Congo (Kinshasa), Ethiopia, Kenya, Rwanda,
Eritria na Uganda. Kama si mbinu ya kibaka mzoefu, vipi mtu ahoji "Islamic Club"
ya kunywa chai asihoji wale maafisa wanajeshi walio Wakristo waliwakilisha jeshi
gani katika mkutano wa wanajeshi Wakristo!
Amani ya nchi itahatarishwa na "Club" ya kula mishikaki na kunywa soda au
Tume ya Majeshi ya Vita! Taarifa rasmi zimewasilishwa serikalini kuhoji vipi
baadhi ya madhehebu ya dini yawe na Tume za Majeshi ya Vita (Armed Forces).
Serikali ipo kimya na wanaohoji kwa nini "Islamic Club" nao wapo kimya!
La kushangaza kama kawaida yake, akikohoa "paroko" lazima serikali igwaye;
haraka haraka Wizara ya Mambo ya Ndani ikatoa ufafanuzi kuwatoa hofu wanaohoji
kwanini "Islamic Club". Uhodari huu wa kuharakia kuwatoa wananchi wasiwasi mbona
hawautumii katika hili la Tume ya Majeshi ya Vita! Hawa wenye kuharakia kuwatoa
wananchi wasiwasi, mbona hatuwaoni wakiwatoa wasiwasi wananchi juu ya ule
mkutano wa Maafisa wa jeshi Wakristo waliokutana Kampala!
Katika wanaohoji kwa nini "Islamic Club" wapo waliotupa mpaka orodha ya
washiriki wa hafla ya kuzindua "Islamic Club". Pengine wangetupa pia orodha ya
wajumbe wa Tume ya Majeshi ya Vita (Armed Forces) ya Kanisa Katoliki;
halikadhalika ile orodha ya wanajeshi Wakristo kutoka Jeshi la Tanzania (JWTZ)
waliokutana Kampala Oktoba 15, 1997.
Meja Generali (Mej. Gen) Elly Tumwine ndiye Mwenyekiti wa wanachama wa chama
cha Wanajeshi Wakristo huko Uganda. Hawa wanaotupa orodha ya washiriki wa hafla
ya uzinduzi wa "Club" ya kunywa chai watuambie jina pamoja na cheo cha
Mwenyekiti wa Wanachama wa Chama cha Wanajeshi Wakristo wa Tanzania. Lakini
wangetueleza pia upo uhusiano gani kati ya Chama hiki na hii Tume ya Majeshi ya
Vita ya Kanisa Katoliki! Kule Uganda wale Wanajeshi Wakristo walitumwa na nani,
walizungumzia agenda gani na walimwakilisha nani! Kuna "Crusade" (Vita vya
Msalaba) gani inakuja?
Baada ya "Islamic Club", baadhi ya watu na vyombo vya habari vinampa
changamoto Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere naye aanzishe "Tanzanian Christian
Club". Wale wanaanzisha Islamic Club ili kutafuta sehemu za kunywa chai na
kutafuna mishikaki bila kuathiriwa na mazingira ya wale ambao hawakubahatika
kuachiwa urithi wowote na babu zao ila "tembo" la kuzikoroga bongo zao. Sasa
Christian Club ya nini wakati hata kwenye duka la sembe, urithi wao upo!
"Christian Club" leo Mwalimu aanzishe ya nini wakati Watanzania wote
wanadhaniwa ni wanachama wa COBA! Ndiyo maana tuna Ubalozi wa Vatican, lakini
OIC ni haramu! Wanaosema Yesu si Mungu wanasota rumande, wakati waliosema Mtume
Muhammad (s.a.w.) kafa kwa ukimwi wapo nje wanatamba!
"Christian Club" ya nini wakati Paroko akikohoa polisi hutumwa Msikitini
wakavunja msikiti na kuua na bado walioua wakaendelea na nyadhifa zao!
Christian Club ya nini wakati Serikali ishatoa makamanda ambao
huthubutu kuwadungua Waislamu risasi na wakapongezwa!
Christian Club ya nini wakati hata Masheikh wanabakia na majoho tu.
Vijana wao wanalengwa shabaha kwa risasi; mabinti, wake zao na mama zao
wanavuliwa nguo wao ndio kwanza wanavaa kanzu safi na kujitia manukato tasbih
mkononi wanakwenda kwenye shughuli!
Christian Club ya nini wakati hata Waheshimiwa Wabunge wakitaka Tume
iundwe kuchunguza mauaji ya Waislamu yaliyofanywa na polisi, Spika wa Bunge
hupinga!
Jumuiya na Taasisi za dini huanzishwa ili ama kupigania haki na maslahi ya
waumini wao au kujiletea maendeleo.
Sasa Tanzania Christian Club (T.C.C.) ya nini wakati masista
wakipinga, ujenzi wa msikiti serikali hutekeleza matakwa yao! T.C.C. ya nini
wakati washapewa 'hati miliki' ya kuhodhi sehemu zote nyeti nchini mpaka
"Parole"! T.C.C. ya nini wakati hospitali za serikali hukosa hata aspirin,
lakini Serikali hiyo hiyo hutoa mabilioni ya fedha kuendeshea hospitali za
Kanisa! T.C.C. ya nini wakati Mwenyekiti Reinhard Bonnke mhadhara wake wa wiki
nzima wa kusema Yesu ni Mungu hupewa heshima kubwa na Serikali huku Magezi
Shaaban akisota rumande kwa Kusema Yesu si Mungu!
Mwalimu Nyerere aunde Christian Club kupigania nini wakati kutokana na
kazi ya COBA na "Marian Spirit" Dk. Sivalon anatuambia "matendo, msimamo na
uamuzi wa viongozi wa serikali unafanana mara kwa mara kwa namna moja au
nyingine na mafundisho na mwelekeo wa Kanisa!"
Lakini pengine hawa wanaohoji juu ya Islamic Club wangetueleza nini COBA
(Catholic Old Boys Association); ilianza lini yapi yalikuwa madhumuni yake na
watupe majina ya viongozi wa serikali (kama walivyotupa yale ya I.C.) ambao ni
wanachama wa COBA au waliwahi kuwa wanachama na viongozi wa COBA.
Ule ujinga wa kumfukuza aliyeibiwa na kumwacha kibaka, Alhamdulillah
umewatoka Waislamu na wazalendo wa nchi hii.
Na.154 Safar 1419, Juni 19-25,
1998.
Kila mwananchi anabaki sawa na mwingine katika masuala ya imani, siasa na
jamii kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Kama tunahoji Islamic Club, tuhoji
pia Tume ya Majeshi ya Vita na Association of Military Christian
Fellowships.
Chanzo: Annur
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !